Riwaya: I died to save my President

Mkuu Kulubule njoo useme neon tyu na hiz nafsi zenye mihangaiko zitulie
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 50

Brigedia Frank kwaju akiwa
katika chumba chake cha kusomea
akipitia nyaraka zake mbali mbali
mara simu yake ikaita na mpigaji
alikuwa ni David,akaipokea
haraka haraka
"Mheshimia rais" akasema
Frank kwa utani
"Frank kuna taarifa yoyote
umeipata kuhusu Pascal?
"Pascal? Frank akauliza kwa
mshangao
"Ndiyo.Una taarifa zozote juu
yake? Pascal nimewasiliana naye
usiku huu na kumtaka afike
nyumbani kwangu.Akiwa njiani
kuja huku akaniambia kwamba
atachelewa kidogo amepata
dharura kuna mtu amempigia
simu anahitaji kuonana naye.Niko
hapa nyumbani nikimsubiri.Kuna
taarifa gani kuhusu Pascal?
akauliza Frank kwa wasi wasi
"Nimepokea taarifa muda si
mrefu kwamba Pasal ameuawa"
Frank akakaa kimya kwa
zaidi ya sekunde thalathini halafu
akasema
“David mimi nawe ni watu
tunaoheshimiana mno na hatuna
utani wa aina yoyote.Tafadhali
usiingize utani katika suala kama
hili" Huu si utani Frank.Ni kweli
Pascal ameuawa usiku huu
hotelini Samawati beach hotel"
"Samawati beach hotel?!!
Alikwenda kutafuta nini huko?
"Hakuna anayefahamu
alikuwa anafanya nini huko."
"Ahsante kwa taarifa
David.Ninaelekea huko sasa hivi
nitakupigia simu baadae" akasema
Frank na kukata simu.Alihisi
miguu yake imeisha nguvu
akavuta pumzi ndefu na kuketi
kitini
"Pascal is dead?!! akasema
kwa sauti na kutikisa kichwa
"Thats not true.Ngoja niende
huko nikahakikishe kama taarifa
hizi ni za kweli" akawaza Frank na
kutoka kwa haraka sana akaingia garini akaondoka kwa kasi
kuelekea Samawati beach hotel.
"Nahisi taarifa hizi zinataka
kunipa uchizi.Ni vipi endapo ni
taarifa za kweli na Pascal akawa
kweli amefariki? akajiuliza akiwa
garini
"Pascal nimezungumza naye
usiku huu kweli anaweza kuwa
amefariki dunia? kama kweli
amekufa nani kamuua? akajiuliza
Frank na kuchukua simu yake
akazitafuta namba za simu za
Pascal akampigia lakini simu yake
haikuwa ikipatikana.
"Simu yake haipatikani.Wasi
wasi unazidi kunijaa yawezekana
kweli akawa ameuawa.lakini ni
nani ambaye amefanya kitendo
kama hiki?Naomba jambo hili lisiwe kweli .Naomba walau awe
amejeruhiwa ila awe mzima
kwani ni mtu muhimu sana
kwangu.Ni rafiki yangu mkubwa
na ninamtegemea katika mambo
mengi.Kama kweli amekufa
litakuwa ni pigo kubwa mno
kwangu" Kichwa cha Frank kilijaa
mawazo mengi.Alijaribu tena na
tena kupiga namba za simu za
Pascal bila mafanikio.
Aliwasili Samawati beach
hotel na kukuta kundi kubwa la
watu nje ya hoteli.Mapigo ya moyo
yakaanza kwenda haraka
haraka.Akasimamisha gari
akashuka na kutembea haraka
haraka akajiunga na kundi lile la
watu waliokua nje ya hoteli.Kulikuwa na gari nne za
askari polisi.
"Ndugu kuna nini kimetokea
hapa? Frank akamuuliza mtu
mmoja aliyekaa pembeni yake
"Kuna tukio la mauaji
limetokea hapa hotelini.Nasikia
kuna mtu ameuawa hapa ndani
usiku huu"
"Maiti yake imekwisha tolewa
?
"Bado polisi wanaendelea na
uchunguzi wao huko chumbani na
watakapomaliza wataondoka na
mwili wa marehemu.Binadamu
wamekuwa katili sana siku
hizi.Yaani mtu anathubutu kutoa
uhai mapema namna hii?akasema
yule jamaa Wauaji wenyewe
wamekamatwa? akauliza
"Sifahamu chochote,sisi
tumekuja hapa kwa ajili ya kupata
chakula na ndipo tukaona polisi
wakiingia hapa kwa kasi na baada
ya muda tukajulishwa kuwa kuna
mauaji yamefanyika" akasema
yule jamaa na kuzidi kummaliza
nguvu Frank
"David hawezi
kunidanganya.lazima itakuwa
kweli Pascal ameuawa.lakini nani
amemuua na kwa nini? Hakuwahi
kunieleza kama ana adui yeyote
anayemuwinda amtoe uhai.Hata
hivyo inaonekana tukio hili ni
mpango uliondaliwa kitaalamu
sana bila Pascal kufahamu
.Alikuwa njini kuja kwangu lakini akanipigia simu na kuniambia
kwamba atachelewa kidogo kuna
mahala anakwenda kuna mtu
anakwenda kumuona kwa
dharura.Huyo mtu aliyempigia
simu na kumtaka aje hapa hotelini
waonane naamini ndiye
aliyemuua au anahusika katika
mpango wa mauaji" Frank
akatolewa mawazoni baada ya
polisi kutoka katika mlango
mkubwa wakiwa wamebeba
mwili wa mtu katika machela
ukiwa umefunikwa shuka
wakaupakia katika gari lao na
kuondoka haraka eneo lile.Pamoja
na ujasiri wake lakini Frank
akajikuta akibubujikwa na
machozi na kwa haraka
akaondoka eneo lile akaenda katika gari lake na kuegemea
usukani akilia.
"Who ever did this must
pay!!.Nitamsaka kila kona ya
dunia hii lazima nimpate na alipe
kwa kitendo hiki cha
kikatili.Pascal alikuwa mtu
muhimu mno kwangu na
aliyemuua ameniondolea kiungo
muhimu. Nani huyo amethubutu
kufanya jambo hili ? Nitamsaka
mtu huyo hadi nihakikishe
nimempata na nitamondoa kiungo
kimoja baada ya kingine.”Frank
akazama katika mawazo mazito.
"Kuna namna moja ya
kumpata muuaji wa
Pascal.Natakiwa kumfahamu mtu
aliyempigia simu na kumtaka
waonane hapa hotelini ni nani.Nikimfahamu huyo nitakuwa
nimempata muuaji wa
Pascal.Lazima nifanye haraka sana
kumfahamu mtu huyo ili nijue
sababu za kumuua." akawaza
Frank na kuchukua simu yake.
"Kuna wazo linanijia
yawezekana labda ni wale
wanasiasa akina Makwa ndio
waliofanya hivi baada ya kuona
anaanza kuwafuatilia.Lakini
nitapata jibu muda mfupi ujao."
akawaza huku akizitafuta namba
fulani na kupiga,simu ikapokelewa
"hallow Imelda habari yako.?
akasema Frank
"habari nzuri Frank
umenisusa sana siku hizi.hata
salamu hakunaSijakususa mrembo ni
kutingwa na mambo mengi ndiyo
maana nimeshindwa hata
kuwasiliana nawe.Vipi maendeleo
yako?
"Ninaendelea vyema Frank"
"Nafurahi kusikia hivyo.Vipi
ile nyumba yako umekwisha
maliza?
“Nimefanikiwa kuezeka kwa
sasa nahangaika na milango na
madirisha"
"Basi usihofu Imelda
nitakusaidia kiasi cha pesa uweze
kuipata hiyo milango na
madirisha umalizie nyumba
yako.Unahitaji shilingi ngapi?
"ninataji kama milioni tano
hivi"
"Nitakutumia fedha hizo" "Real?!
"Kweli kabisa.Sijawahi
kukudanganya Imelda"
"Nakuamini Frank .Ahadi
zako ni za kweli kabisa.
Nashukuru umetokea kwa wakati
muafaka ambao nilikuwa nahitaji
sana msaada"
"Hili si tatizo kubwa kwangu
ningekwisha kutatulia muda
mrefu shida yako hutaki
kututafuta watu kama sisi na
unakimbilia kwa hawa vijana
wasio na chochote.Tuachane na
hayo kuna kitu naomba
unisaidie.Uko kazini mida hii?
"Ndiyo niko zamu ya
usiku.Kitu gani unahitaji Frank?
akauliza Imelda Nitakutumia namba fulani
ambayo nataka unisaidie
kutazama simu ya mwisho
iliyompigia na kama kuna
uwezekano nipate hata
mazungumzo yao"
"Mhh..!! akasema Imelda
"Tafadhali Imelda ni muhimu
sana kwangu.Nisaidie tafadhali"
"Hilo ni suala gumu kidogo
kwangu kwani nimehamishwa
kitengo kwa hivi sasa lakini ngoja
nione kama ninaweza kufanikiwa"
akasema Imelda
"Nashukuru sana Imelda ."
akasema Frank na kukata simu
halafu haraka haraka akamtumia
Imelda kiasi che pesa alichokuwa
anakihitaji na milimi moja ya
ziada.Baada ya sekunde kadhaa toka atume pesa ile Imelda
akampigia simu
"Oh Frank sijui nikushukuruje
kwa msaada huu mkubwa "
“Usijali Imelda mambo hayo
ni madogo sana kwetu.Ukiwa na
shida yoyote tafadhali usisite
kunitafuta nitakusaidia"
"Ahsante sana Frank.Nitumie
hiyo namba ili niifanyie kazi mara
moja" akasema Imelda na kukata
simu
"Siku zote ukitaka mambo
yaende haraka haraka penyeza
rupia.Pesa haijawahi kushindwa
sehemu yoyote ile" akawaza huku
akiziandika namba za Pascal
katika meseji na kumtumia Imelda
halafu akawasha gari akaondoka
kwa mwendo wa taratibu.Akachukua simu na
kumpigia David
"David ni kweli Pascal
amefariki.Nimetoka eneo la tukio"
"Nani lakini aliyefanya
unyama huo?David akauliza
"Bado haijulikani lakini huu
ni mpango maalum uliopangwa
kitaalamu.Uliponieleza kile
alichokifanya kwa Dr Makwa
nilimpigia simu na kumtaka
tuonane ili nimkanye asirudie
tena.Akiwa njiani kuja kwangu
akapigiwa simu na mtu na
kumtaka waonane akanipigia na
kunijulisha kwamba atachelewa
kidogo kuna mtu anakwenda
kuonana naye na nilikuwa
naendelea kumsubiri hadi
uliponipigia simu na kunijulishakuwa ameuawa.Mtu huyo
aliyemuita waonane naamini
ndiye aliyemuua na tayari
nimekwisha anza jitihada za
kuhakikisha ninamfahamu haraka
sana" akasema Frank
"Frank jitahidi umfahamu
mtu huyo ili tujue sababu ya
kumuua Pascal.Lazima mtu huyo
au kikundi hicho cha watu
watakuwa na sababu fulani ya
kumuua" akasema David na
ukapita muda kidogo halafu Frank
akauliza
"David I want you to be
honnest with me." akasema na
kunyamaza
"Honnest with you? David
akashangaaKama unahusika katika kifo
hiki cha Pascal tafadhali naomba
unieleze mapema ili tuyamalize na
nisiendelee na uchunguzi wangu"
"Frank kitu gani kimekuingia
kichwani hadi ukafikiria jambo
kama hilo?Kwa nini unahisi
naweza kuhusika katika kifo cha
Pascal?
"Nakumbuka jana katika
maongezi yetu uliweka wazi
chukio zako kwake na kutaka
nimuondoe katika timu.Kwa
maneno yale ya jana kuhusu
Pascal yeyote angeweza kuhisi
kuwa unahusika katika kifo chake
cha ghafla"
"Frank mimi na wewe
tumefahamiana kwa muda mrefu
na unafahamu kabisa kwamba siwezi kufanya jambo kama
hilo.Ni kweli sikupendezwa na
tabia ya Pascal na nikakuomba
tumuondoe katika timu lakini
ukagoma ukadai utazungumza
naye.Sikuwa na tatizo tena baada
ya kuniahidi kwamba
utazungumza naye na
kumuelewesha namna mambo
yanavyokwenda.I wanted him out
of the team but not to kill
him.Kama ningehitaji kumuua
ningefanya hivyo kimya kimya
bila kukueleza.Nakuomba ndugu
yangu ondoa hofu kabisa mimi
siwezi kushiriki katika jambo la
namna hiyo.Tunachotakiwa
kufanya kwa sasa ni kufanya
uchunguzi na kubaini ni nani hasa
aliyemuua?Mimi nitashirikiana nawe bega kwa bega hadi
tumbaini muuaji" akasema David
"Ahsante David na samahani
kwa kukuhisi vibaya.Kwa sasa
akili yangu naona haifanyi kazi
vyema ila nitaendelea na
uchunguzi wangu na nitakutaarifu
itakachokibaini"
"Ahsante sana.Nijulishe
tafadhali kila hatua
unayoichukua"akasema David na
kukata simu
"Sijui ninawaza wapi hadi
nikamuhusisha David na kifo hiki
cha Pascal.Yawezekana ni maneno
ya jana aliyoyazungumza ndiyo
yaliyonifanya niwe na hisia
kwamba anaweza kuwa anahusika
katika kifo hiki.Ngoja nisubiri
taarifa kutoka kwa Imelda halafu nitajua wapi pa kuanzia.Mabalaa
yanazidi kuniandama.Likitoka hili
linakuja hili.Wakati ambao tuko
karibu na mafanikio ndipo
linaponikumba jambo baya kama
hili.Dah ! imeniumiza
sana.Aliyemuua Pascal ameniweza
kweli kweli" akawaza Frank akiwa
katika mwendo mkali na mara
simu yake ikaita akatazama
mpigaji alikuwa ni Imelda
ikamlazimu kusimamisha gari
pembeni ili aweze kuzungumza
naye.
"Imelda kuna lolote
umefanikiwa kulipata? akauliza
Frank
“Ndiyo Frank.namba ile ya
simu uliyonipa imesajiliwa kwa
jina la Pascal Evarist Situmwa.Namba ya mwisho
kumpigia ni namba iliyosajiliwa
kwa jina la Victoria Boaz Tamile."
Frank akashusha pumzi na
baada ya sekunde chache akauliza
"Imelda are you sure?
"Ndiyo Frank nina uhakika
.Nimepata hiyo kutoka katika
kumbu kumbu zetu"
"Ahsante sana."akasema
Frank na kukata simu.Mapigo ya
moyo wake yalianza kumuenda
mbio
"Vicky?!! Akajiuliza huku
akitikisa kichwa
"Namba ya Vicky ndiyo ya
mwisho kumpigia Pascal kwa
usiku huu.Kama ndivyo basi Vicky
ndiye aliyemtaka Pascal waonane
hotelini? Kwa nini alitakawakaonane hotelini?Kwa nini
Pascal hakunieleza kama
anakwenda kuonan ana Vicky
hotelini? Frank akajiuliza maswali
mengi haraka haraka na kuhisi
kichwa kinagonga kwa nguvu.
"Ninaanza kuhisi yawezekana
Vicky akawa ameshiriki katika
mpango wa kumuua Pascal japo
wazo hili silipi uzito mkubwa
.Kama ni hivyo kwa nini?
akajiuliza na kuchukua simu
akazitafuta namba za simu za
Vicky akapiga lakini simu haikuwa
ikipatikana.Akawasha gari na
kuondoka
"Mbona hili jambo linazidi
kunichanganya? Ni kweli Vicky
anaweza kushiriki katika mauaji
ya Pascal?Kwa nini afanye hivyo wakati yeye pia ni mtu wetu wa
karibu?Bado inaniwia ugumu
kuamini kama kweli Vicky naye
anashiriki katika mauaji
haya.Ngoja niende hotelini kwake
nitamsaka kila mahal usiku wa leo
hadi nimpate.Vile vile kuna
ulazima wa kuchunguza pia kule
hotelini kama Vicky alionekana
pale.Kama alikuwa pale basi
hakutakuwa na shaka yeye ndiye
aliyemuua au alishiriki katika
mpango wa mauaji" akawaza
Frank
David alikuwa kama mtu
aliyemwagiwa maji baada ya
kuzungumza na Frank
simuni.Aliingiwa na woga.
"Hili suala naona litachukua
sura mpya kwani huyu Frank akifanya uchunguzi wake anaweza
akagundua kwamba ninahusika na
kifo cha Pascal na mimi na yeye
tutaingia katika uadui
mkubwa.Tukifikia hatua hiyo kila
kitu kitaharibika na tutakosa kila
kitu.Sitaki hilo litokee kabla
hatujachota yale matrilioni.I must
do something" akawaza David na
kuchukua simu akazitafuta namba
za simu za Elizabetha na
kumpigia.Simu iliita na kukatika
bila kupokelewa,akapiga tena
safari hii ikapokelewa
"Unasemaje David usiku huu?
akauliza Elizabeth
"Madam Elizabeth samahani
sana kwa kukusumbua usiku huu
ambao naamini utakuwa
umepumzikaNiko kwenye kikao kujadili
mazishi ya mume wangu"
"Madam ninahitaji msaada
wako ndiyo maana nimekupigia"
"Sema unahitaji msaada gani?
"Kuna rafiki yake Frank
anaitwa Pascal ambaye pia yupo
katika timu ya peresheni
mapinduzi.Kijana huyu anafanya
kazi idara ya usalama wa taifa"
"Ninamfahamu Pascal japo
sijawahi kuonana naye ana kwa
ana"
"Huyo Pascal tulikuwa naye
katika timu inayoandaa
mapinduzi .Nilimuona ni kikwazo
katika kufanikisha mipango yetu
kwani haniamini na amekuwa
anahoji kila jambo
ninaloliwasilisha na asubuhi ya leo alimfata mmoja wa wanasiasa
ambao tunawategemea sana
katika kuanzisha vurugu na
kumuhoji maswali.Sikufurahishwa
na jambo hilo ikanilazimu nifanye
mipango ya kumuondoa haraka
sana.Usiku huu ameuawa lakini
tayari Frank amekwisha anza
kuwa na wasi wasi kwamba
ninahusika na ameanza
uchunguzi"
"Unahitaji mimi nifanye nini?
akauliza Elizabeth
"You are the only one who
can stop him.Mzuie asiendelee na
uchunguzi wake"
"Sawa nitafanya hivyo lakini
nitahitaji maelezo ya kina kwa
nini umefikia maamuzi ya kumuua
huyo kijana ambaye alikuwa anamsaidia sana Frank katika
biashara ya silaha”
“I beg you madam Elizabeth
do anything to stop him”akasema
David
“I’ll stop him”
"Ahsante sana madam kwa
msaada huo"
"David wakati mwingine
usikurupuke kumuua mtu bila
kuwa na utafiti wa kutosha kama
kifo chake hakina madhara
baadae.Unadhani Frak akijua
umehusika katika kifo cha rafiki
yake atakuacha salama? Fikiri
mara mbili mbili kabla hujafanya
jambo"
"Nimekuelewa madam"
akasema David na simu ikakatwa Nilidhani kumshirikisha
David katika mpango huu wa
mapinduzi kungekuwa na
manufaa makubwa kwetu lakini
imekuwa ni mzigo mzito kuubeba"
akawaza Elizabeth na kuzitafuta
namba za simu za Frank
akampigia.
"Madam Elizabeth!! akasema
Frank kwa mshangao.Hakuamini
kuziona namba za Elizabeth.
"Frank habari yako"
"Habari nzuri madam.Mbona
umekuja kimya kimya?Hakuna
aliyeniambia kama unakuja
Tanzania”
"Nimekuja kwa dharura kwa
ajili ya mazishi ya Deus"
"Deus amefariki?!! akauliza
Frank kwa mshangao Ndiyo"
"Amefariki lini?mbona
sijataarifiwa?
"Hujataarifiwa kwa sababu ni
masuala ya kifamilia zaidi na si
lazima ujulishwe ila tuko katika
maandalizi ya mazishi atazikwa
hapa Tanzania"
"Madam uko wapi mida hii
nije nikuone ?Msiba uko wapi?
"Kwa sasa kinachoendelea ni
vikao vya maandalizi na
utajulishwa kila kitu pindi
taratibu zitakapokuwa tayari ila
kwa usiku huu nimekupigia simu
kukuelekeza jambo moja la
muhimu"
"Nakusikiliza madam"
akasema Frank kwa adabu Usifanye uchunguzi wowote
kuhusiana na kifo cha Pascal"
"What?!!!
"Umenisikia vyema.Usifanye
uchunguzi wowote kuhusiana na
kifo cha Pascal.Umenielewa?
"Madam umenichanganya
kidogo.Umefahamuje kuhusu
jambo hili?Kwa nini nisifanye
uchunguzi?
"Frank toka lini umeanza
kumuhoji mkuu wako?If I say stop
I mean it.Sitaki maswali
yoyote.Achana na uchunguzi
wowote kuhusiana na kifo cha
Pascal.!!
"madam I'm sorry to ask
this.are you behind this?
"You want to know? Yes I'm
behind this.I'm watching you Frank so dont try to desobey me!!
akasema Elizabeth na kukata
simu.Frank aliyekuwa njiani
kuelekea hotelini kwa Vicky
akabaki amepigwa na butwaa
asijue la kufanya
"Whats going on? Mambo
gani haya yanaendelea?Madam
Elizabeth yupo hapa nchini toka
lini?Deus is dead? How come I
wasn’t informed? Frank akajiuliza
maswali mfululizo akakosa majibu
"I'm confused right
now.Ngoja nikapumzishe kichwa
changu kwani naona kila muda
unavyozidi kwenda ndivyo
ninazidi kuchanganyikiwa na akili
kushindwa kufanya kazi
yake"akawaza Frank na kuwasha gari akaondoka kuelekea
nyumbani kwake.

*********

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…