Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 58

Nyumbani kwa Elizabeth
hakukuwa na watu wengi kwani
msiba wa mumewe Deus
ulihusisha ndugu na watu
wengine wachache wa karibu na
familia hasa wafanya biashara
wakubwa. Elizabeth akiwa
amekaa na baadhi ya wafanya
biashara waliokuja kumfariji,simu
yake ikaita akatazama mpigaji alikuwa ni Duma kijana
aliyemtuma kuwafuatilia Juliana
na Patricia ,akaomba samahani
kisha akaelekea ndani na
kumpigia Duma
"Nipe ripoti" akasema
Elizabeth
"Madam nimewafuata Juliana
na mwenzake kama
ulivyonitaka.Walipotoka hapo
walielekea moja kwa moja
Mawenzi Complex na pale
wakaingia Kibo Restaurant na na
baada ya muda akatokea mzee
mmoja hivi ambaye nahisi ndiye
waliyekuwa
wakimsubiri.Sikuweza kunasa
mazungumzo yao ila kuna picha
nimezichukua nitakutumia"
akasema Duma Nini kiliendelea baada ya
kukutana na huyo mzee?
"Kwa namna walivyokuwa
wakiiongea inaonekana walikuwa
na mazungumzo nyeti sana na
walipomaliza yule mzee
akaondoka zake na akina Juliana
wakaenda makaburini.Sifahamu
walikwenda kutafuta nini kule na
baada ya kutoka makaburini
wakaelekea saloon ambako wako
hadi sasa ninaendelea
kuwafuatilia"
"Good Job.Nitumie hizo picha
sasa hivi" akasema Elizabeth na
Duma akamtumia picha
alizowapiga akina
Juliana.Akazifungua na picha ya
kwanza ikamstua sana Meshack jumbo!!! akasema
Elizabeth kwa suti ndogo akiwa
katika mshangao
"Namfahamu Meshack Jumbo
ni mkuu wa idara ya
ujasusi.Wamefahamiana vipi na
Juliana?Mambo gani walikuwa
wanaongea? akajiuliza halafu
akatabasamu
"Nimepata jibu.Huyu alikuwa
ni mkuu wa kazi wa Elvis mume
wa Patricia na nina hakika hapa
alikuwa na mazungumzo na
Patricia na si Juliana.Hata hivyo
Juliana hapaswi kuwa na ukaribu
na watu kama hawa ambao ni
hatari kwetu.Lazima nitafute
namna ya kumuweka mbali na
Patricia kwani kama wakiendelea
kuwa karibu basi atakuwa akikutana mara kwa mara na
hawa wapelelezi ambao wako
karibu na Patricia.Suluhu pekee ni
Patricia aondoke hapa nyumbani
haraka sana.Sitaki aendelee tena
kuwa na ukaribu na Juliana kwa
sababu anafahamiana na
wapelelezi wengi na iko siku huyu
Meshack au mpelelezi mwingine
yeyote anaweza kuja hapa
nyumbani kumsalimu Patricia na
akaanza kuchunguza mambo
yasiyomuhusu”akawaza Elizabeth.
"Dah ! Tayari nilikwisha anza
kupatwa na wasi wasi mkubwa
kumuona Juliana na Meshack
Jumbo" akawaza Elizabeth na
kutoka chumbani na kuelekea
waliko waombolezaji ******************

Ukumbi wa mikutano katika
hoteli ya Sahare ulijaa waandishi
wa habari walioitika wito wa
viongozi wa vyama vya siasa
waliowataka waandishi wa habari
kufika katika hoteli hiyo kwa ajili
ya mkutano maalum.Saa tano
kasoro dakika mbili Dr Makwa
Tusangira na wenyeviti wenzake
wa vyama vya upinzani
wakawasili katika chumba cha
mikutano na ukumbi ukawa kimya
.Dr Makwa ambaye ndiye kiongozi
wa jopo lile la viongozi wa vyama
vya siasa akasimama na
kuwasalimu waandishi wa habari
"Habari za asubuhi ndugu
waandishi wa habari.Kwa niaba ya wenzangu wote walioko hapa
mbele ninapenda nitoe shukrani
zangu nyingi kwenu kwa kuitika
wito wetu na kufika kwa wingi
sana.Hatukutegemea kama
mngeitika kwa wingi namna
hii"akanyamaza halafu akafungua
kitabu chake alichoandika yale
ambayo alitaka kuwaeleza
waandishi,akasoma kidogo na
kusema
"Ndugu zangu waandishi wa
habari,walioko mbele yenu
pamoja nami ni wenyeviti wa
vyama vya siasa vyenye usajili wa
kudumu na uwakilishi
bungeni.Karibu vyama vyote vya
siasa vilivyo na usajili wa kudmu
hapa nchini kiongozi au
mwakilishi wake yuko hapa.Huu ni muunganiko mkubwa wa
vyama vya siasa na tumeamua
kuwa kitu kimoja ili tuwe na
nguvu moja katika kupigania zile
hoja zetu za msingi kwa
maendeleo ya nchi yetu Tanzania"
akanyamaza akasoma kidogo
halafu akaendelea
"Ndugu waandishi wa
habari,tumewaiteni hapa siku hii
ya leo ili kupitia kwenu wafuasi
wetu wa vyama vya upinzani na
watanzania wote hasa wale
wapenda maendeleo waweze
kupata kile ambacho tumekusudia
kiwafikie.Kikubwa tulichowaitia
hapa ni kuwafahamisha wafuasi
wetu kuhusiana na mkutano
mkubwa tuliowatangazia kuwa
utafanyia siku yakesho.Tumewasilisha taarifa
mapema kwa jeshi la polisi
kuwaomba waturuhusu tufanye
mkutano wetu wa hadhara siku ya
kesho lakini bila sababu za msingi
jeshi la polisi wametukatalia
tusifanye kufanya
hivyo.Tumetuma wawakilishi
kwenda kwa viongozi wa juu wa
jeshi la polisi kuomba tufanye
mkutano wetu wa hadhara lakini
bado tumenyimwa na hakuna
sababu yoyote kubwa ya msingi
iliyotolewa kwa nini tunazuiwa
kufanya mkutano wetu kwa
amani.Huu ni ukandamizaji
mkubwa wa demokrasia
unaoendelea hapa nchini
kwetu"akanyamaza kidogo halafu
akaendelea Kupitia kwenu ndugu
waandishi wa habari tunapenda
kuwataarifu wafuasi wetu kuwa
licha ya jeshi la polisi kutuzuia
tusifanye mkutano wa hadhara
lakini siku ya kesho wafike kwa
wingi sana katika viwanja vya
jamhuri ambako tutafanya
mkutano wetu mkubwa wa
hadhara na viongozi wote wa
vyama vya siasa hapa nchini
watahudhuria.Katika mkutano
huo tutaeleza dhumuni letu la
kuunda umoja huu wa vyama vya
siasa vya upinzani na nini hasa
shabaha yetu.Njooni siku ya kesho
mje msikilize namna nchi yenu
inavyouzwa,namna rasilimali
zenu zinavyofilisiwa na wajanja
wachache ambao wanatumia kila aina ya nguvu waliyonayo
kuhakikisha kwamba wananchi
hawafahamishwi kuhusu mambo
maovu wanayoyafanya.Wakati
umefika sasa wa kuweka wazi
mambo yote tunayofanyiwa
watanzania.Wakati umefika wa
kukomesha unyoyaji huu
mkubwa wa rasilimali zetu.
Nawasihi msiogope tujitokezeni
kwa wingi sana katika mkutano
wa kesho ambapo mambo
makubwa ya kitaifa
yatajadiliwa"akanyamaza na
kuwatazama waandishi wa habari
na kuendelea
"Nawasihi tena wafuasi wetu
na wale wote wenye mapenzi
mema na nchi hii msiache kuja
kesho tuanze pamoja safari ya ukombozi wa nchi
yetu.Hatutaogopa mabomu au
risasi za polisi.Hatutafanya fujo
bali tutafanya mkutano wetu kwa
amani na utulivu
mkubwa.Nawaomba vyombo vya
dola wasiwazuie wananchi
kuhudhuria mkutano wetu kwani
tutahakikisha hawafanyi vurugu
bali wanakaa kwa amani
wakiwasikiliza viongozi wao"
“Ndugu zangu waandishi wa
habari kwa leo ni hayo tu
machache niliyowaitia hapa
naamini nyote tutakutana kesho
katika viwanja vya
jamhuri.Naomba mfike kwa wingi
sana kuna mambo mengi
mtayasikia siku ya kesho ili
muweze kuwahabarisha wananchi.Kwa kuwa muda mfupi
ujao tutakuwa na kikao na hawa
wakuu hakutakuwa na maswali
kutoka kwenu bali tutapanga tena
mkutano mwingine ambako
mtapata fursa ya kuuliza mawali
yenu ila kwa leo mtatuwia radhi
kwani muda si rafiki
kwetu.Ahsanteni sana kwa kuja na
ninawatakia kila la heri katika
shughuli zenu za kila siku.Mungu
awabariki sana" akamaliza Dr
Makwa na wenzake wote
wakasimama wakatokea mlango
wa nyuma na kuwaacha
waandihsi wa habari waliokuwa
na kiu kubwa ya kutaka kuuliza
maswali
Mara tu baada ya kumaliza
mkutano ule na waandishi wa habari Dr Makwa akampigia simu
David
"David kila kitu kimekwenda
vizuri.Tumemaliza kikao na
waandishi wa habari na sasa
tunaingia katika kikao cha
ndani.Ninakukumbusha kuhusu
zile fedha ziwe tayari leo hii kwani
mambo yameanza kupamba
moto.Tayari tumekwisha tangaza
mgogoro na serikali"
"Kazi nzuri Dr Makwa.Usijali
kuhusu fedha.Suala hilo
linashughulikiwa na mpaka badae
kila kitu kitakuwa tayari" akasema
David ambaye naye baada ya
kukata simu akampigia Dr Shafi
"Dr Shafi kila kitu
kinakwenda vizuri.Muda mfupi
uliopita Dr Makwa ametangaza mkutano wa hadhara kesho licha
ya polisi kupiga marufuku
mkutano huo na hapo ndipo safari
yetu itakapoanzia.Nimeona
nikujulishe namna mambo
yanavyokwenda"
"Ahsante sana kwa taarifa
David.Nina imani kila kitu
kitakwenda kama
tunavyotarajia.Endelea
kunihabarisha kila hatua
inapopigwa"akasema Dr Shafi
wakaendelea na mazungumzo
mengine

****************

Steve aliwasili katika makazi
yao akiwa ameongozana na Vickyna mdogo wake
Winnie.Akawakaribisha ndani
"Dada siwezi kukaa hapa"
akasema Winnie baada ya Steve
kutoka kwenda kumuita Elvis
"Winnie tafadhali hii
ni....."kabla hajamaliza sentensi
yake Elvis akatokea
"Karibuni sana" akasema
Elvis
"Dada sitaki kukaa
hapa.Sitaki kumuona huyu jamaa
ambaye jana amenichoma na
umeme !! I dont want to be near
this monster!! akasema Winnie
kwa ukali
"Steve mpeleke Winnie kwa
Graca" akasema Elvis na Steve
akamchukua Winnie akampeleka chumbani kwa Graca halafu
akarejea sebuleni
"Nilikupigia simu lakini
ikakatwa na haikupatikana
tena.What happened? akauliza
Elvis.Steve akamuelezea kila kitu
kilichotokea
"Ninashukuru sana kwa Steve
kufika kwa wakati kwani bila yeye
sijui yule jamaa angetufanya nini
kwani tayari sikuwa na ujanja wa
kujinasua"akasema Vicky
"Huyo jamaa
unamfahamu?Umewahi
kumuona?
"Hapana simfahamu na ni
mara yangu ya kwanza kumuona"
"Nini hasa alichokuwa
anakitafuta? Swali pekee aliloniuliza ni
akina nani ninashirikiana
nao?Kabla sijamjibu chochote
akatokea Steve ambaye aliweza
kupambana naye akatuokoa lakini
kwa bahati mbaya akafanikiwa
kumjeruhi Steve kwa risasi begani
na akakimbia"akasema Vicky
"That man was a
professional" akasema Steve huku
akivua shati lake na Elvis
akalikagua jeraha alilojeruhiwa na
Obi
"kwa bahati nzuri risasi
haikuweza kuingia ndani
ilikwaruza kwa nje.Pole sana"
akasema Elvis
"Ilikuaje hadi huyo jamaa
akafanikiwa kuingia ndani na
kuwawekeni chini ya ulinzi?Hakuna walinzi nyumbani
kwako?
"Kama alivyosema Steve huyo
jamaa ni mzoefu sana kwani
akiwa na mwenzake mmoja
walifanikiwa kumdhibiti mlinzi
mmoja aliyekuwepo getini halafu
wakaingia ndani wakamdhibiti
msichana wa kazi na kumfuata
Winnie chumbani kwake kwani
kwa muda huo sote tulikuwa
tumelala kutokana na uchovu wa
jana usiku,wakamtumia msichana
wa kazi kugonga mlango wangu
na akaniita hivyo sikuwa na wasi
wasi na nilipofungua tu nikajikuta
nikitazamana na bastora
wakanikamata wakanifunga
mikono na sote tukawekwa
sebuleni na yule jamaa akaanza kunihoji ,kwa habati nzuri
akatokea Steve na
kutuokoa.Mlifahamuje kama tuko
katika hatari?akauliza Vicky
"Nilipigiwa simu na
mkurugenzi wetu akaniambia
kwamba amepewa maelekezo na
makamu wa rais ukamatwe
ukahojiwe kisha uuawe.Tayari
wanazo taarifa kwamba
umeshiriki katika mauaji ya Pascal
.Wewe ni mmoja wa watu
unaoshirikiana nao na
walipogundua kwamba
umeshiriki katika mauaji ya Pascal
wamestuka na wanataka kujua
kwa nini umeshiriki katika tukio
lile na ndiyo maana maelekezo ya
makamu wa rais ni kukuteka
wakuhoji na uwataje wale wote ulioshirikiana nao katika kifo cha
Pascal halafu wakuue.Baada ya
kupokea maelekezo hayo kutoka
kwa mkurugenzi wetu nikapiga
simu yako ili nikutahadharise
lakini haikuwa ikipatikana ndipo
nilipomtuma Steve haraka sana
akufuate.Nilipatwa na wasi wasi
baada ya kumpigia simu ya Steve
ikaita na kukatika halafu
haikupatikana tena"
"Kuna simu ilipigwa wakati
nikiwa nje nikimvizia kijana
aliyekuwa na yule jamaa na
nikaizima haraka na sikukumbuka
kuiwasha tena" akasema Steve
"Imekuwa vyema kuwa Steve
alifika kwa wakati na kuzima
jaribio hilo la hao
wavamizi.Lazima mfahamu kuwa hivi sasa mnawindwa ila
ninawahakikishia kuwa hapa
mtakuwa salama.Tuliweke
kwanza hilo
pembeni.Umewasiliana na Omola?
"Bado sijawasiliana naye
nilikuwa nimezima simu"
akasema Vicky na kuwasha simu
yake akazitafuta namba za Omola
na kupiga
"Vicky nimekutafuta simuni
lakini hukuwa ukipatikana”
akasema Omola
“Nilikuwa katika kazi
iliyonilazimu nizime simu.Vipi
umeamua nini?
“Nimeweka vizuri ratiba
yangu na nitakuja Tanzania ila
kwa wiki moja tu.Kama kazi
unayotaka nikusaidie itachukuazaidi ya wiki moja utanisamehe
sintaweza"
"Asante sana Omola.Kazi
yenyewe haitazidi wiki
moja.Nashukuru sana kwa siku
hizo chache ulizojitolea kuja
kunisaida.Lini unategemea kuja
Tanzania?
"Nitaondoka saa tisa alasiri
na saa kumi na mbili za jioni
nitawasili Dar es
salaam.Nitakujulisha
nitakapoanza safari"
"Ahsante sana
Omola.Nikutakie safari
njema"akasema Vicky
"Omola amekubali kuja
Tanzania kutusadia japo ametoa
sharti kwamba ana nafasi ya wiki
moja tu" Hata siku hizo saba
zinatosha sana.Atakuwa
ametusaidia mambo mengi ndani
ya siku hizo chache.Anatakiwa
kuandaliwa hoteli nzuri
atakayokaa kwa muda wa siku
hizo zote atakazokuwa hapa
nchini.Aandaliwe gari zuri na kila
chochote kitakachomfaa"
"Sawa nitalishughulikia hilo
suala" akasema Vicky.Baada ya
ukimya mfupi akauliza
" Kwa sasa nini
kinachoendelea?
"Kitu ambacho unatakiwa
ukifanye kwa sasa ni kuonana na
rais kuanza maandalizi ya
kumuunganisha Omola na
makamu wa rais.Rais anapaswa
afahamu kuhusu mpango wa kumtumia Omola kumchunguza
Dr Shafi na yeye ndiye aandae
mazingira ya Omola na Dr Shafi
kukutana.Sisi tunaendelea
kuandaa mikakati ya
kumchunguza Frank.Unadhani
rais anaweza kukubali kuonana
nawe?
“Rais hawezi kukataa
kuonana nami.Nitamjulisha kuwa
ninahitaji kumuona.Hata hivyo
nina wazo moja Elvis,kama tayari
mnafahamu na mnao ushahidi
usio na shaka kuwa Frank
anajihusiaha na biashara hii ya
silaha kwa nini basi asikamatwe
ateswe na ataje wote
anaoshirikiana nao?
"Kweli hatuna shaka kuhusu
Frank kujihusisha na biashara hii ya silaha lakini hatuwezi kufanya
hivyo, kumkamata na kumtesa ili
atuonyeshe mtandao wake.Hata
kama tukimkamata tukamtesa
hataweza kutueleza kuhusu
mtandao wake kwani watu kama
hawa wamekula yamini ya
kutokusema siri zao na yuko radhi
afe kuliko kutoa siri hivyo
hataweza kutusaidia kwa lolote
hata kama tukimpa mateso ya
aina gani.Alikuwa tayari kumuua
mtoto wake ili kuilinda siri hii
hivyo hataweza kabisa kutamka
chochote hata
akiteswa.Tunachotakiwa kufanya
ni kumchunguza na hatimaye
kuubaini mtandao wake wote na
tuung'oe hadi mizizi yake.Usihofu
Vicky tutawapata tu japo inaweza kuchukua muda kidogo lakini
lazima tutawapata"
"Sawa Elvis mimi ngoja
niwasiliane na rais niombe
kuonana naye" akasema Vicky
"Vicky kumbuka
unapozungumza na rais
usimueleze chochote kuhusu
kushirikiana nasi.Mueleze
kwamba mpango huu unaufanya
wewe peke yako na haushirikiani
na yeyote"
"Nimekuelewa Elvis nitafanya
hivyo.Ni wapi chumba changu?
Steve akampeleka Vicky
katika chumba atakachokitumia
halafu akarejea sebuleni
"Elvis kama tusingewahi
tungeweza kumpoteza Vicky
kwani yule jamaa aliyetumwa kumteka ni mtaalamu
sana.Anaweza kucheza na silaha
na hata karate pia.Kama
nisingekuwa makini angeweza
kuniua"akasema Steve
"Pole Steve.Tuliweke kwanza
pembeni suala hilo la Vicky kwani
tayari tumekwisha muondoa
katika hatari.Mkurugenzi
alikuwepo hapa na kuna jambo
alikuja kunieleza"
"Jambo gani Elvis?
"Ameonana na Patricia
asubuhi hii wakazungumza lakini
Patricia hakuwa na tatizo lolote
bali rafiki yake anaitwa
Juliana.Huyu Juliana ni
mwanamitindo maarufu sana
hapa nchini lakini kwa muda
mrefu amekuwa akiishi nje ya nchi na sasa amerejea
nchini.Juliana ana tatizo na
anahitaji msaada" akasema Elvis
na kisha akamsimulia Steve tatizo
la Juliana
"Elvis kwa maelezo hayo
uliyonipa ninapata picha kwamba
haya ni mauaji ya visasi.Kuna kila
sababu ya kuamini kuwa
wanaofanya mauaji yale aidha
wana kisasi na Juliana au wana
kisasi na familia yao"
"Hata mimi nilimweleza hivyo
mkurugenzi.Pamoja na kwamba
tuna shughuli kubwa mbele yetu
lakini lazima tumsaidia pia
Juliana.Tumuhoji na atueleze kwa
kina zaidi na tutaweza kubaini
namna ya kumsaidia"
"Juliana tutampataje? Mkurugenzi atatuunganisha
naye.Kwa mchana huu wakati
tunamsubiri Omola,Vicky
anafanya mpango wa kuonana na
rais hivyo nawe itumie nafasi hii
kuzungumza na Juliana.Mimi
nitazungumza na Graca na
kumuhoji zaidi ili nione kama
ataweza kutusaidia namna
nyingine ya kumchunguza zaidi
baba yake" akasema Elvis halafu
akampigia simu Meshack Jumbo
akamjulisha kuwa Steve anataka
kwenda kuonana na Juliana na
Meshack akawaomba wasubiri ili
awasiliane na Juliana.Vicky
akarejea sebuleni
"Nimezungumza na rais na
amekubali kuonana nami ila
amesema niwahi kabla ya saa saba kwani kwa muda huo anategemea
kuwa na wageni muhimu hivyo
natakiwa kuwahi"
"Sawa Vicky,jiandae uende
ikulu kuonana na rais.Utatumia
moja wapo ya gari hapo nje.Steve
kuna kazi anaenda kuifanya
angeweza kukusindikiza na
kuhakikisha unakuwa salama"
"Usihofu Elvis nitakuwa
salama.Ninaweza kujilinda.Ni kwa
bahati mbaya tu yule jamaa
aliniwahi lakini asingeniweza hata
kidogo.Ngoja nikajiandae nielekee
ikulu kuonana na rais" akasema
Vicky na kwenda chumbani kwake
kujiandaa.Baada ya dakika nne
Meshack Jumbo akapiga simu
"Nimewasiliana na Juliana
ameniambia kwamba kwa sasa yuko saluni lakini ameelekeza
sehemu ya kukutana na Steve"
akasema Meshack na
kumuelekeza Steve mahala
ambako atakutana na Juliana
akamtumia pia namba zake za
simu ili akifika sehemu hiyo
awasiliane naye
Steve na Vicky baada ya
kujiandaa kila mmoja akaondoka
kwenda kushughulkikia jukumu
alilopewa na pale nyumbani
wakabaki Elvis Graca na Winnie
"Nadhani ni muda muafaka
wa kuongea na Graca.Anaweza
kutusaidia kupata namna ya
kumchunguza zaidi baba
yake.Yeye anamfahamu vizuri
zaidi kuliko mtu yeyote" akawaza
Elvis na kuelekea chumbani kwa Graca akabisha hodi,Graca
akaufungua mlango
"Elvis karibu ndani" akasema
Graca na Elvis akaingia mle
chumbani,Winnie alipomuona
akajifunika na mto.
“Winnie" akaita Elvis lakini
Winnie hakujibu kitu
"Elvis kwa sasa Winnie
hayuko tayari kuzungumza nawe
lolote.Mpe muda muache
apumzike na atakapokuwa tayari
mtazungumza" akasema Graca
"Sawa Graca ila lengo langu ni
kutaka kumuelewesha tu hali
halisi ilivyo.Hata hivyo
nitazingatia ushauri wako na
nitasubiri hadi hapo atakapokuwa
ametulia ili nizungumze naye"
"Sawa Elvis"Graca tunaweza
kuzungumza kidogo? akasema
Elvis
"Hakuna tatizo" akasema
Graca kisha wakatoka wakaenda
kukaa katika viti vya kupumzikia
pembeni ya bwawa la kuogelea.
"Mambo yanakwendaje
Elvis?Huyu Winnie na mama yake
ni akina nani na kwa nini wako
hapa? akauliza Graca
"Samahani kwa
kutokufahamisha Graca ila hawa
ni wenzetu tutaishi nao hapa
nyumbani kwa muda wakati
tukiendelea na operesheni
yetu.Vicky mama yake Winnie ni
mpelelezi na ameungana nasi ili
kutusaidia katika kazi yetu na kwa
kuwa hivi sasa wako katika hatari tumeona itakuwa vyema endapo
watakaa nasi hapa nyumbani ili
kuhakikisha usalama wao hasa
Winnie"
"Nimefuarahi kusikia
hivyo.Vicky ni mwanamke
mrembo sana.Kumbe hata mimi
ninafaa kuwa mpelelezi.Kama
Vicky mwanamke mrembo namna
hii ameweza hata mimi nitaiweza"
akasema Graca
"Graca sikuzuii kuipenda hii
kazi lakini sikushauri utake
kuifanya.Ni kazi yenye hatari
nyingi.Ona maisha yangu yalivyo
hivi sasa.Kama ningekuwa katika
kazi nyingine nisingekuwa na
maisha haya hivi sasa.Ni kazi
nzuri lakini lazima ukubali
kwamba hautakuwa na maisha ya kawaida.Ukitaka kuifanya kazi hii
ujiandae kwa hilo" akasema Elvis
"Ninaipenda hii kazi japo
bado sijafikiria kuifanya ila
nitazingatia ushauri wako.Vipi
kuhusu uchunguzi unaendeleaje?
akauliza Graca
"Uchunguzi wa kuubaini
mtandao wa baba yako umeanza
japo hatujapiga hatua kubwa bado
lakini kuna mambo tayari
tumeyagundua.Kwanza naomba
ufahamu kuwa Pascal yule
mshirika mkubwa wa baba yako
amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo"
"Pascal !!
"Ndiyo.Yule alikuwa ni
mshirika mkubwa na mtu muhimu
sana katika uchunguzi wetu lakini amefariki jana kwa bahati mbaya
wakati tukiwa katika harakati za
kumpata ili tumuhoji.Hata hivyo
kifo chake hakiwezi kutuzuia
kuendelea mbele.Uchunguzi
unaendelea na hivi tuongeavyo
Steve na Vicky wote
wametawanyika katika majukumu
niliyowapa"
"Natamani kusikia baba
amekamatwa na kufikishwa
mbele ya vyombo vya sheria.Ni
mtu mkatili sana yule,mambo
aliyotufanyia mimi na mama ni
mabaya mno na mengine siwezi
kueleza.Itakuwa ni sherehe kubwa
kwangu siku nitakapomshuhudia
akiwa katika pingu" akasema
Graca akionekana kuwa na hasira
za wazi juu ya baba yake Hilo litafanyika Graca na
baba yako pamoja na wenzake
wote anaoshirikiana nao katika
biashara yake haramu
watakamatwa na kufikishwa
mbele ya sheria"
"Naingoja kwa hamu sana
siku hiyo.Nataka nimuone baba
yangu akiwa kizimbani akijibu
tuhuma zinazomkabili na mimi
nitasimama kama
shahidi.Nitaeleza uovu wake wote
alioufanya" akasema Graca
"Graca narudia tena
kukuhakikishia kwamba hilo
litafanyika lakini nahitaji msaada
wako zaidi”
"Sema Elvis unauhitaji
msaada gani?Niko tayari
kukusaidia kwa lolote ambalol iko ndani ya uwezo wangu”akasema
Graca
"Tunafahamu baba yako ni
kinara katika biashara hii ya
silaha lakini hatuwezi kumkamata
yeye peke yake bali lengo letu ni
kuuondoa kabisa mtandao wote
unaojishughulisha na biashara
hii.Ili tuufahamu mtandao wote
lazima tumfanyie baba yako
uchunguzi wa kina.Nataka
utusaidie ni kwa namna gani
tunaweza kumchunguza zaidi
baba yako?Kuna mahala unadhani
tunaweza kupata nyaraka au
ushahidi wowote wa kuweza
kutusadia?Kuna mtu yeyote
unayemfahamu ambaye unadhani
anaweza akatusaidia kupata
taarifa za uhakika kuhusu Frank na mtandao wake?Nafahamu
umetusaidia sana na hadi hapa
tulipofika ni kwa sababu yako
lakini bado nahitaji msaada wako
zaidi.Kama kuna lolote ambalo
unaona linaweza kutusaidia
kupata taarifa za kutosha kuhusu
baba yako na mtandao wake
nisaidie tafadhali" akasema
Elvis.Graca akatabasamu
"Nilifahamu iko siku utakuja
kuniomba kitu kama hicho na
nilikuwa naisubiri sana siku kama
hii.Ni wakati wangu wa kutimiza
kile nilichokuwa nakitaka"
akawaza Graca
"Unasemaje Graca kuhusu
ombi langu hilo?Unaweza
ukatusaidia?Elvis akauliza Elvis I'm not comfortable
here.Twende tukazungumzie
suala hili ndani.Twende chumbani
kwako" akasema Graca kisha
wakainuka wakaelekea chumbani
kwa Elvis
"Haya nieleze Graca
unachotaka kunieleza" akasema
Elvis
"Elvis ninaweza kukusaidia
kupata taarifa muhimu kuhusu
baba.Kuna sehemu anahifadhi
taarifa zake za siri.Nitakusaidia
kukupeleka mahala hapo ambako
nina imani utapata mambo mengi
yatakayokusaidia"
"Ahsante sana
Graca.Nakuhakikishia kuwa
nitakulinda kwa kila namna niwezavyo" akasema Elvis huku
naye akitabasamu
"Hata hivyo" akasema Graca
na Elvis akamtazama kwa makini
"I need something in
exchange.Kuna kitu nakihitaji
kutoka kwako na tafadhali
usiseme hapana kwani ni muhimu
mno kwangu" akasema Graca
"Graca nakuhakikishia kitu
chochote utakachokihitaji
utakipata hata kama sina
nitahakikisha unakipata" akasema
Elvis kwa kujiamini
"Are you sure?Graca akauliza
"Yes I'm sure"
"Good"akasema Graca halafu
akakaa kimya kama vile anaogopa
kusema kile anachokihitaji"
"Sema Graca unahitaji nini? Nimekuwa katika hospitali
ya magonjwa ya akili kwa muda
mrefu sasa na katika muda huo
wote sijawahi kuwa na
furaha.Ninataka sasa kuanza
kuishi kama wenzangu.Nataka
niwe na furaha nifurahi kama
wenzangu.Ili furaha yangu
ikamilike ninahitaji mtu wa
kunipa raha za dunia na kunifanya
niwe na furaha kila sekunde"
"Graca usihofu.Sisi tuko hapa
na tutakusadia kwa kila hali
kuhakikisha kwamba unakuwa na
furaha tele katika maisha
yako.Ahadi yangu kwako siku zote
ni kufanya uso wako uwe na
tabasamu"akasema Elvis
"Nalifahamu hilo na
ninawashukuru sana nyote kwa namna mlivyojitolea kunitunza na
kunilinda.Hata hivyo ninaposema
kwamba nahitaji mtu wa kunipa
raha za dunia namaanisha nahitaji
kuwa na mpenzi.Nahisi nataka
kuingia tena katika
mapenzi.Nahitaji mpenzi na hicho
tu ndicho ambacho ninakihitaji
kwa sasa"
"Graca siwezi kukuzuia jambo
hilo lakini nadhani huu si wakati
wake .Mambo yako yakishakaa
vizuri basi utakuwa na nafasi pana
zaidi ya kuchagua mpenzi
umtakaye.Ninakushauri kwa sasa
uliweke pembeni suala hilo.Sisi
tupo hapa tutahakiksha unakuwa
na maisha mazuri na hapo ndipo
utakapokuwa na uhuru wa kuchagua mwanaume umtakaye"
akasema Elvis
"Elvis sina haja ya kusubiri
kwa muda mrefu wakati tayari
nimekwisha zama mapenzini"
"Umezama mapenzini?
Mbona sikuelewi Graca? akauliza
Elvis
"Ndio Elvis.I'm in love with
you" akasema Graca na maneno
yale yakamstua sana Elvis
akamtazama Graca kwa
mshangao.Wakatazamana kwa
dakika moja Graca akasema
"Hukutegemea kusikia kitu
kama hiki kutoka kwangu Elvis
lakini huo ndio
ukweli.Ninakupenda sana na
wewe ndiye mwanaume pekee
ambaye nakuhitaji katika maisha yangu.Elvis naomba tafadhali
usinielwe vibaya,hata mimi
sikutegemea kabisa kitu kama hiki
kunitokea.Nimejikuta tu
nikikupenda bila sababu.Moyo
wangu umekuridhia wewe.Najua
kiumri hatulingani lakini hiyo si
hoja bado tunaweza kuwa
wapenzi.Naamini haitakuwa rahisi
kurejeana tena na mkeo Patricia
hivyo mimi niko hapa nitakupa
kila aina ya huduma unayoikosa
kutoka kwa mkeo Pat......"
"Graca please stop" akasema
Elvis na kujikuta ameshika kichwa
"Tafadhali naomba usirudie
tena kutamka maneno kama hayo"
"Elvis nafahamu ni vigumu
sana kwako kunikubalia ombi
langu lakini naomba ufahamu kwa ni kweli ninakupenda na
ninahitaji kuwa na
wewe.Ukilikubali hilo
nitakupeleka mahala ambako
utapata kila kitu
unachokihitaji.Fikiri kuhusu hilo
halafu utanijibu" akasema Graca
na kusimama ili aondoke
"Graca naomba ukae
tafadhali" akasema Elvis na Graca
akaketi
"Graca huu si wakati wa
utani.Tuko vitani tunapambana na
mtandao mkubwa wenye
nguvu.Watu hao ni makatili na
wasio na hata chembe ya
huruma.Nimejitoa mhanga
kupambana nao na kuhakikisha
ninaufutilia mbali mtandao wao
hivyo nahitaji msaada mkubwa kutoka kwenu.Unadhani ni jambo
rahisi kuamua kuwadanganya
watu ninaowapenda kuwa
nimekufa?Unadhani ninafurahi
mateso anayoyapata mke wangu
Patricia?Nimewaumiza watu
wengi sana lakini si makusudi bali
kwa ajili ya kupata nafasi nzuri ya
kuusafisha mtandao huu wote
ambao unauza silaha
zinazotumiwa na waasi kuua watu
huko mashariki ya Congo.Wewe
pia ni mmoja wa waathirika wa
mandao huu kwani baba yako
ambaye ni kinara wa biashra hii
ya kuuza silaha amekutesa sana
hadi kukupeleka katika hospitali
ile ya magonjwa ya
akili.Nimefanya haya wa ajili yenu
ninyi wote mnaomizwa na mtandao huu.Nataka niwakomboe
ili muwe huru hivyo nahitaji sana
ushirikiano mkubwa kutoka
kwenu.Jambo unalolihitaji ni
gumu kukutekelezea kwa sababu
kwanza mimi ni mume wa mtu na
ninampenda sana mke wangu
Patricia.Pili wewe ni kama mdogo
wangu hivyo siwezi kuwa na
mahusiano na mtu mwenye umri
wa mdogo wangu.Naomba
tusilifanye suala hili liwe gumu
Graca nieleze kile
unachokifahamu kuhusu baba
yako ili tuweze kuufutilia mbali
mtandao wake na hatimaye wewe
na wote mlioteseka kwa uwepo
wao muweze kupumua na hata
wewe uweze kuwa huru na
kufanya chochote ukitakachoikiwamo kumtafuta mpenzi
atakayekufaa.Tafadhali sana
Graca" akasema Elvis
"Elvs utanisamehe sana hata
mimi sikutaka kuyatamka maneno
haya ila nimeshindwa
kuvumilia.Moyo wangu unateseka
na kuumia kwa namna
ninavyokupenda.Siwezi kueleza ni
kwa namna gani umeweza kuingia
moyoni mwangu na kung'ang'ania
kiasi hiki.Nakupenda sana Elvis na
ndio maana niko tayari kufanya
lolote hata la hatari kwa ajili
yako.Nataka ufanikiwe katika
operesheni hii,nataka uuondoe
mtandao huu wote wa baba lakini
hata mimi ninataka mahitaji
yangu yatimie pia na hitaji langu
pekee ni kuwa nawe.Hata kama si kwa maisha yote basi kwa wakati
huu ambao tuko hapa naomba
tafadhali tuwe wote.Umri wetu
isiwe kigezo cha mimi na wewe
kutokuwa wapenzi.Nakubali
umenizidi umri lakini bado
tunaweza kuwa na mahusiano
yenye furaha.Elvis si rahisi
kwangu kukutamkia maneno
kama haya mtu kama wewe
ambaye umenisaidia kwa mengi
na bado nahitaji msaada wako ila
nimeshindwa kujizuia na kuamua
kukueleza kweli japo naamini
unaweza ukaniona kama mgonjwa
wa akili lakini mimi ni mzima wa
afya na sina tatizo lolote la
kiakili.Naliongea hili nikiwa na
akili zangu timamu" akasema
Graca halafu akainuka Elvis lifikirie saula hilo na
utakapokuwa tayari unijulishe"
akasema Graca na kuondoka
akimuacha Elvis haamini
alichokisikia kutoka kwa Graca
"Ama kweli haya ni maajabu
ya Musa.Graca!! akasema na
kuinuka akatikisa kichwa
" Sikutegemea kabisa kusikia
maneno kama yale kutoka kwa
Graca.Sura yake haifanani kabisa
na maneno aliyoyatamka.Eti
anataka mimi na yeye tuwe
wapenzi!! Nini kimemuingia Graca
hadi akatamka maneno kama
yale.Anawezaje kunipenda mtu
kama mimi ambaye kwanza
hatulingani kiumri,pili mimi nina
mke wangu ambaye siachi kueleza
namna ninavyompenda.Sikutegemea
kabisa jambo kama hili" akawaza
Elvis
" Nataka ufanikiwe katika
operesheni hii,nataka uuondoe
mtandao huu wote wa baba lakini
hata mimi ninataka mahitaji
yangu yatimie pia na hitaji langu
pekee ni kuwa nawe.Hata kama si
kwa maisha yote basi kwa wakati
huu ambao tuko hapa naomba
tafadhali tuwe wote.Umri wetu
isiwe kigezo cha mimi na wewe
kutokuwa wapenzi.Nakubali
umenizidi umri lakini bado
tunaweza kuwa na mahusiano
yenye furaha."maneno haya ya
Graca yakaendelea kujirudia
kichwani kwa Elvis Dah ! nahisi huyu Graca
bado atakuwa na matatizo ya
akili.Maneno kama haya hayawezi
kutoka kwa mtu mwenye akili
zake timamu.Lakini…....” akawaza
Elvis na kusita kidogo
“Graca hana matatizo ya akili
na nilipomtazama machoni
alionyesha wazi kumaanisha kile
alichokisema yaani ananitaka
kimapenzi.Oh my God nitafanya
nini?Nahitaji sana msaada wake
na yupo tayari kunisaidia ila
ametoa sharti kwamba ili nisaidie
lazima nimkubalie tuwe na
mahusiano ya
kimapenzi.Nitawezaje kuwa na
mahusiano na mtu mwenye umri
wa mdogo wangu?Kwa nini kila
wakati wanawake huniweka katika majaribu makubwa.Kwanza
alianza Doreen ambaye ni wazi
ananitaka na anafanya kila
awezalo kuhakikisha kuwa
ninakuwa na mahusiano naye japo
nimejaribu kumkwepa lakini bado
ni king’ang’anizi.Nimefanikiwa
kumuondoa hapa na kumuweka
mbali ila naamini atarejea tena na
kabla hilo sijalimaliza anaibu ka
tena Graca na jambo lake.Kwa nini
wananifanyia hivi hawa
wanawake? Akajiuliza Elvis
“Graca hakupaswa kunifanyia
hivi wakati anafahamu kabisa
kwamba jambo hili ninalolifanya
ni kwa faida yake mwenyewe.Kwa
mateso makubwa aliyoyapitia
kutoka kwa baba yake alipaswa
kunipa ushirikiano mkubwakuhakikisha kwamba ninaufyeka
mtandao wa baba yake asiye na
huruma hata chembe lakini
anaonekana amekwisha sahau
ukatili wote wa baba yake na sasa
anataka kutumia nafasi hii
kufanya mambo ambayo
hayatamletea faida yoyote”
Akaendelea kuwaza Elvis
“Nifanyaje kumshawishi
Graca anieleze mahala
ninakoweza kupata taarifa zaidi
kuhusu mtandao wa baba yake
bila kumkubalia ombi lake?
Akajiuliza Elvis na kutoka akaenda
kukaa nje
“Huwaogopi hawa jamaa?
Winnie akamuuliza Graca
aliporejea chumbani kwake Siwaogopi.Kwa nini wewe
unawaogopa?
“Ni watu makatili sana hawa
hasa huyu jamaa aliyekuja kukuita
muda mfupi uliopita”
“Elvis?
“Simfahamu jina lake lakini ni
mkatili sana yule.Alinichoma na
umeme kama mimi si binadamu
na sikuwa nimemfanyia kosa
lolote.Siwezi kusahau mateso
niliyoyapata kwa usiku wa jana”
akasema Winnie huku akionekana
kulengwa na machozi
“Sikiliza Winnie hawa jamaa
si watu wabaya hata kidogo.Ni
watu wema sana lakini
wanapokuwa kazini huwa
wanabadilika na ndiyo maana
wanaonekana wakatili” Who are they?
“Hawa ni wapelelezi”akajibu
Graca
“Vipi kuhusu wewe imekuaje
ukafika hapa?Umekutaka wapi na
hawa jamaa?Nawe pia ni
mpelelezi?Winnie akauliza
“Hapana mimi si mpelelezi”
akasema Graca na kumsimulia
Winnie kila kitu kuhusiana na
maisha yake historia
iliyomshangaza sana Winnie
“Sikujua kama umepitia
mambo mengi namna hiyo.Pole
sana Graca.Huyo baba yako
anaonekana ni mtu mkatili sana.Ni
mtu wa namna gani huyu
anayeweza kumfanyia ukatili huu
mtoto wake wa kumzaa
mwenyewe?akauliza Winnie na Graca akamuelekeza mahala
anapoishi baba yake
“kwa hiyo una mpango gani
na maisha yako ya mbele?
“Kwa sasa ninamsubiri Elvis
amalize operesheni yake na
atanisaidia kwenda kuishi nchi ya
mbali ambako nitakuwa salama na
hakuna ambaye atatishia tena
maisha yangu” akasema Graca
“Hilo ni wazo zuri lakini
unawaamini hawa jamaa kama
watakusaidia kuyaanza upya
maisha yako?
“Ninawaamini hawa jamaa
hasa Elvis.Amepitia mambo mengi
na mazito kwa ajili yangu na
hawezi kuniangusha hata kidogo”
akasema Graca na mlango ukagongwa akaufungua na
kukutana na Elvis
“Graca nakuomba
tuzungumze”akasema Elvis kisha
Graca akatoka wakaenda
chumbani kwa Elvis
“Graca nimetafakari kuhusu
lile suala uliloniambia lakini jibu
langu ni hapana.Siwezi kufanya au
kuwa na mahusiano nawe.Wewe
ni mdogo wangu na ninafanya
haya yote kwa sababu yako na
wengine wale wanaoteseka
kutokana na silaha zinazouzwa na
mtandao wa baba yako.Please
don’t make this hard for
me.Nahitaji sana msaada wako ili
niweze kuumaliza mtandao huu
na wewe uwe huru.Ukiwa huru
utaweza kumpata mwanaume wa hadhi yako ambaye utampenda
kuliko wote lakini mimi
haitawezekana”akasema Elvis
“Elvis nimekwisha weka wazi
kwako kwamba ninahitaji sana
uumalize mtandao huu tena
haraka iwezekanavyo lakini
nimepatwa na huu ugonjwa wa
kukupenda ambao hauna dawa
zaidi ya wewe kunikubalia kuwa
na mahusiano nami hata kwa
kipindi hiki ambacho tutakuwa
hapa wote.Elvis mwili wote
unawaka moto kila pale
ninapokuwaza.I need you darling.I
need you to hold me in your
strong arms.Please kiss me…”
akasema Graca na kufumba macho
na kumbusu Elvis.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…