Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Tupo tupo tayari kitu kinazidi kupagawisha ila hako ka winnie naona kama ni nuksi kwa nini kameiiba no ya Frank kwenye simu ya dadake ngoja tusubiri poti ila pamenogaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumosa mambo? tusaidie kumuita Kulubule, kuna watu wanataka kumpa shikamoo yake huku.
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 60

Saa kumi na mbili na dakika
sita iliwakuta akina Elvis nje ya
uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere wakiwa wamefika
kumpokea Omola anayetokea
nchini Afrika kusini.Ndani ya gari
alikuwemo Steve,Vicky na Elvis
ambaye kwa jioni hii alitumia ule
mtindo wake wa kujibadili
mwonekano kwa kuongeza ndevu
bandia na kuvaa kofia ya
mzunguko na miwani.Haikuwa
rahisi kumtambua kama ni
Elvis.Steve na Vicky wakashuka
garini na kwenda katika sehemu ya kusubiri abiria wanaowasili
Elvis akabaki garini
Ndege ya shirika la ndege la
Tanzania ambayo hufanya safari
zake kutoka Dar es salaam na
Johanesburg ilitua na abiria
wakashuka miongoni mwao
akiwemo Omola.Alikamilisha
taratibu za uhamiaji na
kuruhusiwa kuingia nchini.Vicky
ambaye ndiye aliyekuwa
akimfahamu alielekeza macho
yake katika mlango wanakotokea
abiria na mara akamuona Omola
akiwa amevaa suti nyeusi
akamfuata
"Mhh!! akaguna Steve baada
ya kumuona Vicky akisalimiana na
Omola Operesheni hii mbona
inanikutanisha na visura namna
hii.Nilidhani Vicky ni mzuri kupita
wote lakini huyu Omola ni
kiboko.Ana uzuri wa aina yake"
akawaza Steve
"Omola huyu ni mwenzangu
anaitwa Steve na vile vile kuna
mwingine yupo garini
utamfahamu anaitwa Elvis" Vicky
akafanya utambulisho
"Karibu sana Tanzania
Omola" akasema Steve
"Ahsante sana
Steve.Nashukuru kukufahamu"
akasema Omola kwa sauti laini
iliyopenya masikioni mwa Steve
kama kinanda.Steve akakokota
mabegi mawili ya Omola hadi katika gari akamfungulia mlango
na Omola akaingia garini
"Omola huyu ndiye Elvis
niliyekuambia kwamba utamkuta
garini.Huyu ndiye kiongozi wetu
mimi na Steve.Elvis huyu ndiye
Omola Otola"
"Omola nafurahi kukutana
nawe.karibu sana Tanzania"
akasema Elvis
"Ahsante sana nimekwisha
karibia" akasema Omola na Vicky
aliyekuwa katika usukani
akaondoa gari.Tayari kiza
kilikwisha ingia na moja kwa moja
wakaelekea Maasai 5 star hoteli . *************

Graca na Winnie walibaki
nyumbani peke yao baada ya
akina Elvis kuondoka kwenda
kumpokea Omola.
"Siamini kama ile ndoto
yangu leo imetimia.Elvis
amekubali kuwa mpenzi wangu!!
akawaza Graca akiwa jikoni
akiandaa chakula cha usiku
"Ninajiona mwenye furaha
kuliko wanawake wote wa dunia
hii.Kumpata mwanaume kama
Elvis si jambo dogo.Ni mwanaume
mwenye kila aina ya sifa nzuri.Ni
mzuri wa sura,ana roho
nzuri,anajali na zaidi sana
kitandani amehitimu shahada ya
uzamivu.Mchaka mchaka alionikimbiza leo sijawahi
kuuona.Siwezi kukubali Elvis
anitoke mikononi mwangu.Leo
amenionjesha asali lazima
nichonge mzinga.Lazima
nihakikishe baada ya operesheni
hii kumalizika mimi na yeye
tunakuwa pamoja.Lazima awe
wangu milel........." Graca
akaondolewa mawazoni na sauti
ya Winnie aliyemuita
" Unasemaje Winne?
"Graca mimi ninaondoka
siwezi kuendelea kukaa ndani ya
jengo hili kama mtumwa.Watu
hawa ni wabaya sana na siwezi
kuwaamini hata kidogo"
"Unaondoka?!!Graca
akashangaa
"Ndiyo ninaondoka zangu" Hapana usifanye hivyo
Winnie.Subiri hadi dada yako
atakaporudi ndipo ufanye
maamuzi ya kuondoka"
"Siwezi kumsubri kwani dada
hawezi kuniruhusu kuondoka
hapa.Hii ni nafasi nimepata lazima
niitumie vyema.Nisipoondoka
sasa siwezi kuondoka tena.Siwezi
kukaa humu nikifugwa kama kuku
nikizuiwa hata kutumia simu
yangu.Siyawezi maisha ya namna
hii.Kuishi ndani ya nyumba hii ni
zaidi ya kuishi gerezani"
"Winnie sikushauri uondoke
kwani huko nje si salama
kwenu.Dada yako amekubali mje
kuishi hapa kwa sababu za
kiusalama hivyo utakapotoka
hapa utahatarisha maisha yako mwenyewe.Tafadhali subiri hadi
watakaporejea na kama kuna
tatizo lolote uwaeleze watakusikia
na kukusaidia kuliko kuchukua
maamuzi ya kuondoka"
"I don’t care.Litakalonipata na
linipate ila nikiwa nje ya nyumba
hii.Kwanza dada amenificha siku
zote kuhusu kazi anazofanya na
jana tu ameua mtu.Sitaki kuwa
karibu naye nitakwenda kutafuta
maisha yangu mwenyewe.Graca
tafadhali naomba ukanifungulie
geti niende zangu" akasema
Winnie.Graca hakumjibu kitu
akabaki akimtazama
"Graca naomba ukanifungulie
geti niende zangu"
"Hapana Winnie siwezi
kukufungulia na kukuacha uondoke.Ni hatari huko nje si
salama kwako"akasema Graca na
winnie akatoa kisu akakunja sura
"Nenda kanifungulie geti
Graca ama sivyo
nitakumaliza.Tuepushe
shari.Nifungulie geti niende
zangu" akasema Winnie huku
akimsogelea Graca.Kwa nguvu
Graca akamsukuma Winnie
akaanguka chini halafu akatoka
mbio akaenda chumbani kwake
akajifungia.Winnie akainuka
akachukua sanduku lake na
kutoka akaelekea getini akapanda
juu ya pipa kuu kuu akalirusha
begi lake nje akapanda geti na
kuanza kushuka taratibu
akajiachia na kuanguka kama
furushi.Alichubuka mguuni,hakujali akasimama na
kuchukua begi lake akaondoka
"Kamwe siwezi kukaa
nyumba moja na hawa
mashetani.Huu ni wakati wa
kulipiza kisasi kwa ukatili
walionifanyia.Walinichoma na
umeme wakati sijawakosea
chochote.Kama haitoshi
walitakakuanza kunibandua
kucha zangu.Hawa jamaa ni
makatili mno na dada hapaswi
kabisa kuwaamini.They are
monsters!! akawaza Winnie akiwa
na hasira kali

****************

Vicky aliegesha gari nje ya
Maasai 5 star hoteli.Steve ndiye aliyetangulia kushuka akahakiki
usalama halafu wengine wote
wakashuka na kuelekea
ndani.Tayari chumba cha Omola
kilikwisha andaliwa na hivyo
akapelekwa moja kwa moja katika
chumba chake.Kilikuwa ni
chumba kikubwa chenye
kujitosheleza.Kulikuwa na sebule
kwa ajili ya maongezi na
kupumzika vile vile kukawa na
chumba cha chakula bila kusahau
bafu na choo.Kwa kuwa wote
hawakuwa wamepata chakula cha
usiku ikawalazimu kuagiza
chakula na kutokana na umahiri
wa wapishi wa hoteli hii ndani ya
muda mfupi chakula kikawa tayari
na kuandaliwa wakaanza
kula.Kulikuwa na maongezi na utani wa hapa na pale na Steve
ndiye aliyekuwa mzungumzaji
mkubwa sana pale
mezani.Alikuwa anataka
kumsoma Omola ni mtu wa aina
gani.
"Ninajaribu kumuingiza
katika darubini yangu lakini
haingii.Sikati tamaa nitamuingiza
tu katika kumi na nane
zangu"akawaza steve
Kisha kula wakaenda
sebuleni kwa ajili ya
mazungumzo.
"Omola kwa niaba ya
wenzangu napenda kuchukua
nafasi hii kukushukuru sana kwa
kukubali ombi langu la kuja
Tanzania.Hili halikuwa ombi langu
peke yangu bali letu sote unaotuona hapa tukiongozwa na
Elvis"Vicky akaanzisha maongezi
na kumpa ishara Elvis aendelee
"Kama alivyosema
Vicky,wazo la kukuomba uje
Tanzania ni la kwetu sote na
imetulazmu kufanya hivyo
kutokana na operesheni nzito
inayotukabili.Mimi na mwenzangu
Steve tunafanya kazi katika
shirika la ujasusi
Tanzania.Tumegundua uwepo wa
mtandao unaojishughulisha na
biashara haramu ya silaha na
waasi wanaopigana na serikali ya
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.Huu ni mtandao mkubwa
na unaohusisha watu wakubwa
waliomo katika serikali za
Tanzania na Congo.Tumeanza uchunguzi wa kuwabaini watu
waliomo katika mtandano huo na
tayari kuna watu tunawafahamu
lakini tunataka kuuchimba
mtandao huu hadi mzizi wake na
kisha kuwahakikisha wale wote
wanaofanya biashara hii haramu
wanafikishwa mbele ya
sheria.Miongoni mwa watu ambao
tumekwisha wafahamu kuwa
wanahusika na biashara hii ni ni
mtu mmoja anaitwa brigedia
Frank huyu ni mwanajeshi na
mwingine anaitwa Pascal ambaye
ameuawa jana.Kuna mwingine
ambaye tunahisi anaweza kuwa
na mahusiano na mtandao huu
lakini bado hatuna uhakika naye
na huyo ndiye tunayetaka
kumchunguza.Huyu ni makamu wa rais wa Tanzania"Elvis
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
"Kazi ambayo tunataka
utusaidie kuifanya ni
kumchunguza makamu wa
rais.Tunataka tufahamu kama ana
muunganiko na mtandao
unaofanya biashara ya silaha na
waasi wa Congo.Tayari mipango
imekwisha andaliwa ya wewe
kumchunguza.Utajifanya ni
mwandishi wa habari za
mazingira kutoka nje ya
nchi.Utatafuta chombo chochote
cha habari kikubwa cha nje ya
nchi kinachofahamika
tutatengeneza kitambulisho
kikionyesha unatoka katika
chombo hicho.Kila kitu kimekwisha andaliwa na kesho
asubuhi utaianza kazi yako kwa
kukutanishwa na makamu wa
rais” akasema Elvis
“Tunafahamu hili si jambo
jepesi lakini tumekwisha chukua
kila aina ya tahadhari kuhakikisha
kwamba unakuwa salama.Wewe
ni mzoefu katika hizi kazi na tuna
uhakika utafanya kila uwezalo
kuhakikisha kwamba unapata kile
tunachokihitaji kutoka kwa
makamu wa rais” akasema Elvis
“Nimekusikia Elvis lakini
nataka nifahamu mmefahamu vipi
kama makamu wa rais anaweza
kuwa na mahusiano na mtandao
huo wa kuuza silaha?Kuna kitu
chochote kilichowafanya muhisi
hivyo? Ndiyo.Kuna mambo ambayo
yanatufanya tuhisi makamu wa
rais anahusiana na mtandao huu
wa kuuza silaha.Kwanza kwa
kumtumia mkurugenzi wetu
aliagiza mimi niuawe kwa
kisingizio kwamba nimeingia
mahala ambako siruhusiwi
kufika.Alidai nimevuka mipaka
yangu.Hilo lilitokea baada ya
kugundua kuhusu uwepo wa
mtandao unaojihusisha na
biashara ya silaha.Ili niweze
kufanya uchunguzi wangu vizuri
ilinilazimu kughushi kifo changu
na mpaka hivi sasa wanaamini
tayari nimekufa.Haikuishia hapo
makamu wa rais akamtaka tena
mkurugenzi wetu ahakikishe
Pascal ambaye ni mmoja wa vinara wa biashara hiyo ya silaha
anauawa.Hakutoa sababu yoyote
kwa nini auawe na jana huyo
jamaa akauawa.Vicky alishiriki
katika tukio hilo na akafahamika
kwamba alishiriki na makamu wa
rais akamtaka mkurugenzi
ahakikishe Vicky anauawa.Kwa
bahati nzuri mkurugenzi wetu
yuko upande wetu na kila
linapotokea suala kama hilo
anatushirikisha na tulipopata
taarifa hizo tukawahi nyumbani
kwa Vicky na kumuokoa kutoka
kwa mtu ambaye alitumwa
kwenda kumteka.Matukio hayo
yanatufanya tuamini kuwa
makamu wa rais anajihusisha na
mtandao huu mkubwa wa uuzaji
silaha.Tunaamini kuna watu wakubwa katika mtandao huu na
makamu wa rais anaweza kuwa
mmoja wao hivyo tunataka tupate
uhakika.” Akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Kuna mtu moja ambaye naye
tunamtafuta ambaye anaonekana
ni kiongozi wa mtandao huu
anaitwa Deusdedith MM.Katika
nyaraka tulizozipata huyu
amekuwa akiwasiliana na
Brigedia Frank na kumpa
maelekezo.Vicky amewahi
kumchunguza mtu huyu lakini
hakufanikiwa.Ni mtu anayejua
sana kujificha na tukifanikiwa
kumpata huyu tutakuwa
tumefanikiwa sana katika
operesheni hii.Huyu anaishi nje ya
nchi na anaonekana ndiye anayeongoza mtandao huu akiwa
nje ya nchi.Tunataka kuchunguza
kama huyu Deus ana mawasiliano
pia na makamu wa rais” akasema
Elvis
“Elvis ahsante kwa maelezo
yako ambayo yamenifumbua
macho kuhusiana na kile
mlichoniitia hapa.Kabla ya yote
napenda kuwashukuru kwa
mapokezi mazuri na ninapenda
kuwahakikishia kwamba
nimekubali kwa moyo mmoja kuja
kuungana nanyi na kuwasaidia
katika kazi yenu.Aliponipigia simu
Vicky nilikuwa katika operesheni
fulani na nikashindwa kukataa
kuja kumsaidia kwani mimi na
yeye ni marafiki wakubwa sana na
tumekuwa tukisaidiana katika mambo mbali mbali.Kazi hizi ni za
kusaidiana huwezi kufanya peke
yako na hata mimi siku moja
nitakuja kuwaomba msaada wenu
na nina hakika hamtanitupa”
akasema Omola
“Uko sahihi kabisa
Omola.Tunashukuru sana kwa
kuacha shughuli zako na kuja
kutusaidia.Huu ni mwanzo mpya
wa mashirikiano makubwa baina
yetu na muda wowote
utakapohitaji msaada sisi tuko
tayari kukusaidia” akasema Elvis
“Ahsante sana.Nina waahidi
kwamba nitafanya kazi
mtakayonitaka niifanye kwa
weledi mkubwa na nitafanikiwa
kupata kile mnachokihitaji.Kwa
pamoja tutahakikisha tunaufagiamtandao huu wa kuuza silaha
ambao kupitia kwao mamia ya
watu wasio na hatia wamepoteza
maisha.Katika maelezo yako Elvis
nimekiona kitu fulani na
ninaomba mniruhusu nitoe
mawazo yangu kama itafaa”
“Karibu” akasema Elvis
“Nionavyo mimi inawezekana
makamu wa rais hana uhusika wa
moja kwa moja katika biashara hii
ya silaha lakini kuna watu
wanamtumia katika kufankisha
mambo yao hasa hili la kuua watu
ambao wanaonekana ni kikwazo
kwao kwa sababu yeye ana
nguvu.Wanatumia ofisi yake
kufanikisha mambo yao.Kuna
huyu mtu umemtaja hapa ambaye
ni kinara wa biashara hii ya silaha anaitwa Frank nadhani tungeanza
kwanza kuchunguza mahusiano
yake na makamu wa rais na kama
tukigundua kwamba kuna
mahusiano yoyote kati yake na
makamu wa rais itatusaidia sana
katika uchunguzi wetu.Huyu
Frank ni mtu wa kuchunguzwa
sana kwa kila kitu na kwa kupitia
yeye tutaweza kuufahamu
mtandao wake wote.Kuna
mipango yoyote mmeiweka ya
kumchunguza huyu mtu? Akauliza
Omola
“Mipango ipo na hata usiku
wa leo baada ya kutoka hapa
tunakwenda mahala ambako
tutapata mambo ambayo
yatatusaidia kumfahamu zaidi
Frank na mtandao wake.Tunaye mtoto wake ambaye ndiye
anayetusaidia katika kupata
taarifa za baba yake.Usiku wa leo
atatupeleka mahala ambako
tutaweza kupata mambo mengi
zaidi kuhusiana na Frank na
mt………………” Elvis akanyamaza
baada ya simu yake kuita.Alikuwa
ni Meshack Jumbo
“Mkurugenzi anapiga”
akasema na kuipokea
“Hallo mzee”
“Elvis habari za jioni?Vipi
maendeleo yenu?
“Tunaendelea vyema
mzee.Tuko na Omola tayari
amewasili na tuko hapa katika
hoteli aliyofikia tunapanga
mikakati” Good.Nimeshindwa kuja
jioni hii nimebanwa sana na
majukumu mengine.Utanijulisha
kila kitu
kinavyokwenda.Ulinipigia na
kuniomba nikusaidie kuhakiki
kuhusiana na kifo cha Joseph
Mballa mpenzi wa
Juliana.Nimefuatilia polisi na
wanasema kwamba jalada la
mauaji hayo lilifunguliwa lakini
hakuna anayejua liliko ama
uchunguzi huo uliishia wapi.Kwa
ufupi ni kwamba hakukuwa na
uchunguzi wowote kuhusiana na
kifo hicho”
“Inashangaza sana.Kwa nini
mauaji ya kinyama namna hii
yafanyike bila kufanyika
uchunguzi? Akauliza Hii inatuonyesha kwamba
kuna kitu hakiko sawa katika
mauaji yale.Naamini kwa jibu hili
kuna kitu mtakipata ambacho
kitawasaidia katika uchunguzi
wenu.Kama kuna kitu chochote
kile mnahitaji msaada wangu
nijulisheni mara moja"
"Ahsante sana
mzee.Tutawasiliana baaade
nitakujulisha mahala tulikofikia
kwani usiku huu kuna sehemu
tunakwenda ambako tunaweza
kupata mambo mengi kuhusiana
na Frank na mtandao wake"
akasema Elvis na kuagana na
Meshack.Elvis akamgeukia Steve
ambaye kwa muda mrefu
amekuwa kimya Mkurugenzi anadai kwamba
hakuna uchunguzi wowote
uliowahi kufanyika kuhusiana na
kifo cha Joseph.Hata jalada la
uchunguzi lililofunguliwa
halijulikani lilipo,limepotea"
akasema Elvis
"Joseph ni nani? akauliza
Vicky
"Kuna mtu wetu wa karibu
sana anaitwa Juliana ambaye
ametuomba tumsaidie kufanya
uchunguzi kuhusiana na mauaji ya
mpenzi wake pia mdogo wake
ambao waliuawa kikatili lakini
mpaka sasa hakuna muuaji yeyote
aliyepatikana.Taarifa za kutoka
polisi hazionyeshi kama kuna
uchunguzi wowote uliowahi
kufanyika kuhusiana na mauaji hayo.Haya yanaonekana ni mauaji
ya kulipiza kisasi.Kitu
tunachoweza kukifanya kwa sasa
ni kumchuguza mama yake Juliana
ili tufahamu anajihusisha na
biashara gani haramu na watu
gani anaohusiana nao katika
biashara hizo na vile vile
tuchunguze mahusiano kati yake
na wazazi wa Joseph.Tuchunguze
pia familia ya Joseph ni familia ya
aina gani?Wanajishughulisha na
mambo yapi?Tukipata majibu ya
maswali haya tutapata picha au
kufafahamu nani waliofanya
mauaji hayo.Steve ulisema mama
yake Juliana anaitwa nani?
akauliza Elvis
"Anaitwa Elizabeth Mlabwa
Mwakyusa" akajibu Steve Omola kwa taarifa alizotupa
Vicky ni kwamba wewe ni
mdukuaji hatari sana.Naomba
utusaidie kumtafuta huyu
mwanamama anaitwa Elizabeth
Mlilo Mwakyusa.Mwanae
ametuambia kwamba huyu mama
anajihusisha na biashara haramu
lakini hana uhakika ni biashara
gani hivyo tunataka tumfanyie
uchunguzi.Tunahisi chanzo cha
mauaji hayo ni huyu mama au
biashara nazoshughulika
nazo"akasema Elvis
"Anahusiana kwa namna
yoyote na mtandao wa kuuza
silaha? akauliza Vicky
"Hatuna uhakika bado ila
tunataka kumfahamu vyema ili
tutakapomaliza suala hili la silahabasi tumsaidie Juliana kuwatafuta
waliomuua mpenzi wake na
mdogo wake." akajibu Elvis
Omola akaenda katika
chumba cha kulala akafungua
moja ya sanduku lake na kutoa
kompyuta akarejea sebuleni
akaiwasha kisha akaanza kazi ya
kumtafuta Elizabeth.Wote
walikuwa kimya wakimsubiri
amalize shughuli yake ambayo
ilimchukua zaidi ya dakika tano
"Nimeshindwa kumpata huyo
Elizabeth labda ningeweza
kuipata picha yake ingeweza
kutusadia.Inaonekana huyu mama
anatumia jina lingine tofauti na
hilo.Watu wa namna hii ambao
hutumia majina tofauti tofauti
mara nyingi si watu wazuri.Kuna mambo mengi
wanayaficha"akasema Omola.
"Steve mpigie simu Juliana
mwambie akutumie picha ya
mama yake" akasema Elvis na
Steve akawasiliana na Juliana na
bila kuchelewa akamtumia picha
ya Elizabeth.Omola akaiingiza
katika programu yake na kuanza
kuifanyia kazi baada ya dakika
nne zikatokea picha nne
zinazofanana na Elizabeth
"Nimeingia katika kompyuta
za shirika la ujasusi la Uingereza
ambako mmesema kwamba huyu
mama anaishi na nimemtafuta
kwa kutumia picha hii
tuliyotumiwa.Majibu yanaonyesha
kuwa huyu mama anahisiwa
kujihusisha na magenge ya Mafia yanayojishughulisha na biashara
haramu japo mpaka sasa bado
hakuna ushahidi wowote wa
kuweza kumtia hatiani kwa
tuhuma hizo.Inasemekana
anamiliki makasino makubwa
katika nchi za Afrika
kusini,Uingereza,Italia na Urusi.Ni
katika makasino hayo magenge
hayo ya mafia hufanyia shughuli
zao"
"Juliana yuko sahihi kabisa
kuhisi kuwa mama yake
anajihusisha na biashara haramu
na hata mawazo yetu kuwa mauaji
ya mwanae Godson yametokana
na biashara haramu anazofanya ni
sahihi.Magenge ya kimafia hii
ndiyo aina yake ya mauaji.Kama
tayari Uingereza wamekwisha mtilia shaka huyu mama basi ni
mtu hatari na hili si suala dogo
wala la kufanyia mzaha hata
kidogo.Ni suala zito.Tusubiri
kwanza hadi tutakapomaliza suala
hilila mtandao wa silaha halafu
tutaanza kulishughulikia hilo
suala.Ahsante Omola kwa msaada
huo mkubwa" akasema
Elvis.Waliendelea na majadiliano
na ilipofika saa nne kasorobo Elvis
akawataka waondoke
wakaendelee na mambo mengine
wamuache Omola apumzike kwa
ajili ya kuanza shughuli yake
kesho
"Elvis nimekuja hapa kikazi
hivyo ninaomba kuongozana
nanyi huko mnakoenda" akaomba
OmolaOmola umechoka kwa safari
ndefu na kesho utakuwa na kazi
nyingine hivyo endelea
kupumzika na sisi tutaimaliza kazi
hii tunayokwenda kuifanya"
"Tafadhali naomba na mimi
niongozane nanyi huko
mnakoenda.Nitaboreka sana
nikibaki hapa peke yangu wakati
wenzangu wanakwenda
kupambana.Niruhusuni
niongozane nanyi tafadhali"
akazidi kuomba Omola
"Ok fine.Jiandae twende"
akasema Elvis na wote wakaingia
garini wakaondoka

******************* Winnie alitembea haraka
haraka na kwa tahadhari kubwa
huku akiangaza kila upande kuona
kama kuna mtu
anamfuatilia.Hakuna aliyemjali
kwani kila mmoja alikuwa na
mambo yake.Baada ya mwendo
wa dakika kumi na tano akatokea
katika baa kulikokuwa na taksi
zimeegeshwa.Akamfuata dereva
taksi mmoja na kumuelekeza
ampeleke nyumbani kwao
"Leo ni mwisho wa wale
mashetani.Dada pia lazima
aachane na kazi hizi za hatari.Ana
pesa nyingi sana kwa nini
aendelee kufanya kazi kama
hizi?Kwa nini ameingia katika
uuaji? Sikutegemea kabisa kama
dada Vicky anaweza kujihusisha na mambo kama haya.Kama
aliamua kujiingiza katika masuala
haya wakati hana fedha hivi sasa
tayari ni tajiri anapaswa aachane
na kazi hizi.Haipendezi hata
kidogo pamoja na utajiri wake
wote lakini hivi sasa anaishi kama
ndege.Hana amani na kila wakati
anahisi anatafutwa kuuawa.Mimi
pia nimeingizwa katika maisha
hayo ya kukimbia kimbia.Siwezi
kukubali kuishi maisha kama ya
kunguru.Nitafanya kile niwezalo
kwanza kumsaidia dada na pili
kulipiza kisasi kwa wale jamaa
walionitesa hasa yule
aliyenichoma na umeme bila
huruma.Kitendo kile kila
nikikumbuka kinaniumiza
mno.Sikuwa nimewafanyia jambo lolote baya hadi wanitese kiasi
kile.Huu utakuwa mwisho wao na
mwisho wa dada kufanya kazi
zake hizi za hatari" akawaza
Winnie akiwa garini na
kumkumbuka Graca
"Namshangaa sana yule Graca
kwa kukubali kukaa mle ndani
kama mateka.Anaishi kama
mfungwa hatoki nje anajifungua
tu ndani.Amenieleza historia ya
maisha yake inasikitisha amepitia
mambo mengi magumu lakini
hawa jamaa wanazidisha ugumu
zaidi katika maisha
yake.Wanamtumia tu na
hawatamsaidia kwa lolote.Halafu
nimegundua kitu,Graca na yule
jamaa Elvis wana mahusiano ya
kimapenzi kwani mchana wa leo wameitana na kujifungua
chumbani kwa takribani saa
nzima na Graca aliporejea alikuwa
amechoka akaoga na kulala.Yule
jamaa ana tabia chafu sana.Lazima
nimuokoe Graca naye atoke katika
mikono ya wale jamaa ambao
hawatamsaidia lolote zaidi ya
kumuharibia maisha yake.Wale
jamaa ni wanyama sana
ninawachukia mno na leo
utakuwa mwisho wao"
akaendelea kuwaza Winnie
Alifikishwa nyumbani kwao
akamlipa dereva na kuingia ndani
ambako mtumishi wao wa ndani
alifurahi sana kumuona.Winnie
hakutaka maongezi naye akaenda
chumbani kwake akajifungia
halafu akawasha simu yake na kuziandika namba za simu za
Frank alizozitoa katika simu ya
dada yake akapiga simu ikaita na
kupokewa na sauti nzito
"Hallow" ikasema sauti nzito
ya mwanaume
"Hallow nazungumza na nani
tafadhali?akauliza Winnie
"Wewe umempigia nani?
akauliza mtu yule kwa sauti kali
kidogo
"Ninataka kuzungumza na
brigedia Frank."
"Ndiye mimi.Wewe ni nani?
"Naitwa Winnie.Ni mdogo
wake Vicky nadhani
unamfahamu"
"Ndiyo ninamfahamu.Unataka
nini Winnie?
"Nahitaji kukuona mzee" kuniona?!! Frank akashangaa
'Ndiyo mzee nahitaji
kukuona"
"Kuna nini? Nani kakutuma
unitafute,Vicky?
"Hakuna aliyenituma bali
nimelazimika mimi mwenyewe
kukutafuta.Nina jambo kubwa
ambalo nahitaji kukueleza wewe
mwenyewe ana kwa ana"
"Jambo gani hilo?Huwezi
kunieleza katika simu hadi
tuonane?
"Ni kuhusiana na dada yangu
vile vile mwanao Graca"
"Graca?!! Frank akastuka
"Ndiyo"
"Umemfahamuje
Graca?Umejuaje kama ni
mwanangu?Nimeonana naye na
ninafahamu mahala alipo"
akasema Winnie na kupitia spika
ya simu Frank akasikika akivuta
pumzi ndefu
"Uko wapi sasa hivi? akauliza
"Niko nyumbani kwetu"
"Mimi niko msibani sasa
hivi.Ninakuja hapo nyumbani
kwenu muda si mrefu.Vicky yuko
hapo?
"Hapana usije hapa nyumbani
ni hatari hapafai kwani ninaamini
hivi sasa watakuwa wananitafuta
na sehemu ya kwanza kuja
watakuja hapa
nyumbani.Nielekeze nikufuate
wapi?
"Toka hapo nyumbani nenda
hadi Ashanti Club halafu subiri hapo nitakupa maelekezo"
akasema Frank na kukata simu
"Wale mashetani lazima
walipe uovu wao.Walinitesa sana
na kitendo kile hakiwezi kuachwa
hivi hivi.They must pay !! akawaza
Winnie huku akitoka chumbani
kwake akaenda chumbani kwa
dada yake akachukua funguo ya
moja wapo ya magari akatoka
kuelekea Ashanti Club kama
alivyoelekezwa na Frank
"Dada atanilaumu sana kwa
hiki ninachokifanya lakini ni kwa
faida yake mwenyewe.Wale jamaa
anaoshirikiana nao si watu wazuri
hata kidogo.Anapaswa kuachana
nao kabisa na aachane na shughuli
hizi za kipelelezi.Ninataka pia
kumsaidia Graca aweze kutoka ndani ya nyumba ile
anamofungwa na kugeuzwa
mtumwa wa ngono.Wale jamaa
watamuharibia maisha yake"
akawaza Winnie akionekana kuwa
na uso uliojaa hasira kali
Alifika Ashanti Club moja
wapo ya kumbi kubwa za
burudani na usiku huu kulikuwa
na onyesho la bendi,akaelekea
maegesho halafu akampigia simu
Frank.
"Tayari nimefika hapa
Ashanti"
"Good.Washa na kuzima taa
kubwa mara tatu" akaelekeza
Frank na Winnie akafanya kama
alivyoelekezwa
"Good.Usitoke garini hadi
nitakapokupa maelekezo" akasema Frank na kukata
simu.Baada ya dakika nane hivi
akampiga simu
"Kuna mtu atakuja kugonga
kioo cha gari,shuka
mfuate.Usimuulize chochote"
Hazikupita dakika mbili
akatokea mtu akagonga kioo cha
gari na kugeuka,Winnie akafungua
mlango wa gari na kutoka
akamfuata hadi katika gari aina ya
Prado lenye rangi nyeusi
wakaingia na ndipo Winnie
akastuka baada ya kuitambua sura
ya yule mtu.
"You ?!!! akauliza kwa
mshangao.Yule mtu alikuwa ni Obi
yule aliyewavamia mchana
nyumbani kwao No questions please !!
akasema yule jamaa kwa sauti kali
"Huyu jamaa ndiye yule
aliyetuvamia mchana wa leo.Ana
mahusiano na Frank? Au ndiye
Frank mwenyewe? akajiuliza
akiwa na woga mkubwa
"Unanipeleka wapi? akauliza
"Nimekwisha kwambia
kwamba sitaki maswali!! akasema
Obi
Walifika Tarakea
Supermarket akakata kona
wakaingia hapo
"Usitoke ndani ya
gari.Unahitaji nikuletee nini?
"Nothing" akajibu Winnie na
Obi akashuka garini akaingia
ndani.Alikaa humo ndani kwa
dakika kumi na Winnie akastuka baada ya mlango kufunguliwa
ghafla Obi akaingia garini
akamrushia pakiti ya chokolate
akawasha gari na
kuondoka.Hawakusimama kokote
hadi walipofika katika jumba moja
kubwa wakafunguliwa geti
wakaingia.Obi akamtaka Winnie
ashuke wakaingia ndani
"Wewe ndiye Frank? akauliza
winnie
"Hii ni mara ya mwisho
ninakuonya kwamba sitaki
maswali" akasema Obi na
kuchukua simu yake akamjulisha
Frank kuwa tayari
wamefika.Baada ya dakika kumi
Frank akawasili

*******************

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 61

Akina Elvis waliwasili katika
makazi yao wakiwa
wameongozana na Omola.Steve
akashuka na kwenda kubonyeza
kengele ya getini na zikapita
dakika tatu bila mtu kujitokeza
kuja kufungua geti.Akabonyeza
tena wakasubiri kwa muda bila
mtu yeyote kutokea.
"Yawezekana Graca amelala
kiasi cha kutokusikia kengele
ikilia? akauliza Steve
"Si kawaida ya Graca
kupitiwa na usingizi kiasi hiki
hasa tusipokuwepo.Mara nyingi
huwa macho hadi pale turudipo"
akasema Elvis na kumtaka Steve
apande ukuta aingie ndani
akafungue geti.Haraka haraka Steve akapanda kama paka na
kurukia ndani akafungua geti
wakaingia ndani.Kulikua na
ukimya mkubwa mle ndani na
walipojaribu kufungua mlango wa
sebuleni ulikuwa
umefungwa.Elvis akagonga
mlango lakini hakukusikika hata
nyayo za mtu akitembea ndani
"Huu si usingizi wa
kawaida.Graca hana kawaida ya
kulala namna hii" akasema Elvis
na kutoa vitu fulani mithili ya
funguo akaufungua mlango ule wa
sebuleni wakaingia ndani.
"Graca ! akaita Elvis lakini
hakujibiwa
"Graca ! akaita tena lakini
bado kukawa kimya Steve akatoa
bastora yake kwani walihisi hatari.Kwa tahadhari kubwa
wakaelekea katika mlango wa
chumba cha Graca ambacho
kilikuwa kimezimwa taa
"Graca ! akaita Elvis na
taratibu kukasikika sauti ya
funguo ikichomekwa katika kitasa
na mlango ukafunguliwa
"Uuuph ! Elvis akashusha
pumzi baada ya kumuona Graca
"Umetupa wasi wasi sana
Graca tayari tulikwisha anza
kuhisi hatari.Imekuaje leo
umepitiwa na usingizi kiasi hicho?
akauliza Elvis
"Sikuwa nimelala,nilikuwa
nimejificha nikiogopa"
"Kuogopa?Unaogopa nini
wakati nimekwisha kuhakikishia
kwamba nyumba hii ni salama? Nimeogopa labda Winnie
anaweza akawaeleza watu
kuhusiana na sisi kuwepo hapa"
"Winnie?akauliza Vicky
"Ndiyo Winnie ameondoka"
Watu wote
wakatazamana.Walipatwa na
mshangao
"Ameondokaje?
"Mlipoondoka tu naye
akasema anaondoka hawezi
kuendelea kukaa humu ndani
kama mfungwa"
"Kwa nini ukamuacha
akaondoka Graca? akauliza Vicky
"Alinitishia kunichoma kisu ili
nimfungulie geti lakini sikuwa
tayari nikamsukuma akaanguka
na mmi nikakimbia hadi
chumbani nikajifungia.Nilipotoka baadae hakuwepo.Inawezekana
alipanda ukuta akaruka nje kwani
geti halikufunguliwa"
"Jamani mdogo wangu !!
akasema Vicky kwa wasi wasi
"Tulia Vicky
usihofu.Tutafanya kila tuwezalo
kumpata Winnie" akasema Elvis
"Elvis watu wanaonitafuta
wakimpata Winnie watamtumia
kama fimbo ya kunichapia kwani
watanilazimisha nifanye kile
wakitakacho.Tafadhali Elvis
nisaidieni nimpate mdogo wangu"
"Nini kimetokea hapa?
akauliza Omola ambaye hafahamu
kiswahili sawa sawa.Elvis
akamsimulia kile kilikuwa
kimetokeaHilo si tatizo tunaweza
kufuatilia na kujua mahala
alipo.Naomba namba zake za
simu" akasema Omola na
kuiwasha kompyuta yake
akafungua programu fulani na
baada ya muda ukaonekana
mduara mwekundu
"Nimempata ! akasema Omola
huku akitabasamu na wote
wakamsogelea
"Hapa ndipo alipo kwa sasa"
akasema Omola na kubonyeza
bonyeza zaidi na kompyuta
ikamuelekeza mahala alipo
Winnie
"Ahsante sana Omola.Endelea
kumfuatilia Winnie na baada ya
kutoka huko mahala tunakotaka
kwenda usiku huu tutamfuata huko aliko na kumchukua"
akasema Elvis akaelekea
chumbani kwake na kurejea akiwa
na sanduku la silaha aliloletewa
na Meshack Jumbo akaliweka
mezani na kuwaacha wenzake
wakichagua silaha yeye akamtaka
Graca wakazungumze pembeni
"Graca muda ndio huu wa
kutimiza ile ahadi yako.Usihofu
utakuwa salama.Sote tumejiweka
tayari kukulinda wewe pekee
hivyo ndoa hofu na endapo
tukipata jambo lolote la
kutusaidia katika uchunguzi wetu
tutakuwa tumerahisisha sana kazi
na utakuwa huru muda si mrefu"
akasema Elvis
"Elvis mimi sina tatizo
nitawapeleka mahala ambako mtafahamu mambo mengi kuhusu
baba na mambo yake
anayoyafanya lakini naomba
uniahidi tena kwamba ile ahadi
yako ya kuwa na mimi utaitimiza"
"Usiogope Graca nimekwisha
kuahidi kukupa kila
unachokihitaji.Nimekudhihirishia
hilo mchana wa leo na tutaendelea
kufurahi kila siku kila pale
utakapohitaji" akasema Elvis
"Ahsante sana
Elvis.Ninakupenda mno zaidi ya
ninavyoweza kukueleza.Naomba
usiuvunje moyo wangu" akasema
Graca na kumbusu Elvis
"It's time.Jiandae tuondoke"
akasema Elvis
Dakika tano baadae wote
walikuwa tayari na safari ikaanza.Ni Graca pekee
aliyefahamu mahala walikokuwa
wanaelekea
WINNIE NDUGU MDOGO
WAKE VICKY ANAKUTANA NA
BRIGEDIA FRANK,ANATAKA
KUMUELEZA NINI?WAKATI HUO
HUO GRACA ANAWAPELEKA
AKINA ELVIS MAHALA
ANAKOPAFAHAMU YEYE ILI
KUPATA MAMBO MUHIMU
YANAYOHUSIANA NA BABA YAKE
JE WATAFANIKIWA KUPATA
WANACHOKITAFUTA?
MCHAKATO WA MAPINDUZI
UNASHIKA KASI WANASIASA
TAYARI WAMETANGAZA
KUFANYIKA KWA MKUTANO WA
HADHARA BILA KIBALI KWA LENGO LA KUANZISHA VURUGU
KUBWA JE WATAFANIKIWA
LENGO LAO?
JULIANA ANAAMUA LIWALO
NA LIWE LAZIMA WAUAJI WA
MPENZI WAKE NA MDOGO WAKE
WAJULIKANE,JE WATAFANIKIWA
KUWAPATA?MAMA YAKE
ATAGUNDUA?
MAJIBU YA MASWALI HAYA
NA MENGINE MENGI USIKOSE
SEHEMU YA MWISHO YA
SIMULIZI HII

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom