HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
- Thread starter
-
- #141
I DIED TO SAVE MY PRESDENT
Sehemu 23
wapi ilipo kompyuta yake.Elvis
naomba usiniache hapa.take me
anywhere safe.Ni mara yanguya
kwanza kukuona lakini I feel safe
around.macho yako yananifanya
nikuamini” akasema Graca huku
macho yake yakilengwa na
machozi
“ Nitakusaidia
Graca.Nitakuondoa hapa na
kukupeleka sehemu salama
kabisa ambako si baba yako wala
yeyote anayekutafuta
atakupata.Lakini kabla ya kufanya
hivyo kuna jambo nataka
kulifahamu toka kwako.Nataka
kufahamu ndani ya hilo begi
kulikuwa na kitu gani cha
muhimu kiasi cha kupelekea
baba yako kufanya haya yote
aliyoyafanya?Kompyuta hiyo uliyoichukua ilikuwa na jambo
gani na iko wapi kwa sasa?
Graca akamtazama Elvis na
kusema
“Siwezi kukueleza chochote
kwa sasa hivi hadi hapo
nitakapohakikisha kwamba niko
sehemu salama.Take me
somewhere safe and I will tell you
everythingI know na nitakueleza
kompyuta hiyo iko wapi” akasema
Graca
“ Graca ninaelewa hofu yako
lakini naomba uniamini na
uniambie kuhusiana na
ulichokigunuda kwa baba
yako.Tafadhali naomba
ushirikiane nani.Usiniogope mimi
si mtu mbaya” akasema Elvis
“ Elvis najua umefunga safari
ndefu kuja huku kuonana na mimi kwa nia njema kabisa na
kama nilivyokueleza awali kwamba
ninakuamini na niko tayari
kukueleza kila kitu lakini kwa
sasa siwezi kukueleza jambo lolote
ninalolifahamu hadi hapo
nitakapohakikisha kwamba niko
salama.Mkoba ule na kilichomo
ndani yake ndiyo kinga yangu kwa
sasa kwa hiyo fanya
nilivyokuelekeza na nitakueleza
kila unachokitaka” akasema Graca
“ Graca !!... Elvis akataka
kusema kitu lakini Graca
akamzuia
“ Elvis hakuna chochote
utakachoniambia kitakachoweza
kuubadili msimamo wangu.Ninazo
taarifa nyeti sana ambazo
ninaamini zitakuwa ni za msaada
mkubwa sana kwako lakini siwezi kukueleza hadi hapo
nitakapohakikisha kwamba niko
salama” akasemaGraca.Elvis
akamtazama kwa makini usoni na
kuamini kile alichokisema Graca
“ She’s telling the
truth.hawezi kunieleza chochote
bila kufanya anavyotaka” akawaza
Elvis na kusema
“Nimekuelewa
Graca.Naomba unipe muda
kidogo niangalie namna ya
kufanya.I promise you I’ll get
you out of here.”akasema
Elvis.Bila kusema chochote
Graca akainuka na kutembea
taratibu kuelekea ndani.Elvis
akamtazama namna
alivyokuwa akitembea kwa
unyonge akamuonea huruma
sana lazima nimsaidie.Siwezi
kumuacha hapa akiendelea
kuteseka.Akawaza Elvis
halafu akaelekea katika meza
waliyokuwa wamekaa Bongan
na Dr Susan
“ Tayari mmekwisha
ongea? Umefanikiwa kupata
ulichokuwa unakihitaji? Akauliza
Bongani
“ Bongani mambo si rahisi
kama nilivyitegemea" akasema
Elvis
“ Nini kimetokea Elvis,Graca
hajakupa ushirikiano? ” akauliza
Bongani.Elvis akamvuta pembeni
kidogo ili waongee.Akamweleza
kila kitu alichoongea na Graca
“kwa hiyo mambo yako
namna hiyo Bongani.Graca kuna
jambo kubwa analifahamu kuhusiana na baba yake lakini
hayuko tayari kuliweka wazi bila
kwanza kuwa na uhakika wa
usalama wa maisha yake”
akasemaElvis
“ kwa hiyo tutafanya nini
Elvis ili tuweze kuzipata taarifa
hizo toka kwa Graca?akauliza
Bongani
“hakuna njia nyingine ya
kufanya zaidi ya kufanya vile
anavyotaka yaani kumpeleka
sehemu salama.Bongani naomba
unisaidie katika hili ili niweze
kumuondoa Graca hapa
hospitali.Pamoja na kuwa na kitu
cha muhimu ninachokihitaji lakini
nimeguswa sana na mateso ya
binti huyu,ameteseka kiasi cha
kutosha na siko tayari kumuacha akiendelea kuteseka
hapa.Tafadhali naomba unisaidie”
Bongani akafikiri kwa muda
na kusema
“ Hata mimi nimeguswa sana
na histora ya huyu binti na
nitakusaidia ili tuweze kumtoa
hapa.Ninachotaka kufahamu ni
kuhusu usalama wa maisha yake
endapo tutafanikiwa kumuondoa
hapa.Una hakika atakuwa
salama?akauliza Bongani.Elvis
akawaza kidogo na kusema
“Bongani suala la usalama wa
Graca lina changamoto nyingi
lakini hilo ni jukumu langu
ambalo sina budi kulibeba na
nitahakikisha kwamba anakuwa
salama.Nitamlinda dhidi ya yeyote
mwenye nia ya kumdhuru” “Bongani akainama akafikri
kidogo na kusema
“ sawa Elvis
.Nitakusaidia,naomba unipe muda
wa dakika kama kumi nikaongee
na Dr Susan nione kama anaweza
akatusaidia”
“ una hakika atatusaidia?
Akauliza Elvis
“ Nina uhakika lakini hatuna
budi kujaribu.Nina mahusiano
naye mazuri.Tuliwahi kuwa katika
mahusiano ya kimapenzi wakati
tukiwa chuo kikuu na mpaka sasa
bado tuna mahusiano mazuri”
akasema Bongani na kuelekea
katika ofisi ya Dr Susan
“Nahisi kuna suala zito sana
ambalo liko nyuma ya pazia kiasi
kwamba Frank alikuwa tayari hata
kutaka kumuua mwanae kwa ajili ya kulificha.Lazima nilifahamu
suala hilo .Nitamsaidia Graca kwa
namna yoyote ile nitakayoweza na
nitamuondoa hapa.Nitamlinda
dhidi ya yeyote yule anayetishia
maisha yake.”akawaza Elvis
Bongani alitumia zaidi ya
dakika kumi na tano kuongea na
Dr Susan kumuelezea kuhusiana
na tatizo la Graca.Hadi anamaliza
kumueleza Dr Susan alikuwa
anahisi baridi.Alionekana kuzama
katika mawazo mengi
“ Siku zote nilijua lazima
kuna jambo haliko sawa kwa
Graca.Sikutaka kuharakisha
kumuuliza nini kilichokuwa
kinamsumbua na ndiyo maana
nikajenga ukaribu mkubwa kati
yangu naye ili siku moja aweze
kunieleza tatizo lake.Namuoenea huruma sana binti huyu kwa
mateso makubwa aliyonayo.Huu
ni mtihani mkubwa kwangu lakini
lazim animsaidie” Dr Susan akiwa
katika mawazo mengi mara
akastuliwa na Bongani
“ Dr Susan !!...
Akainua kichwa na kumtazama
Bongani
“Unasemaje Bongan? Akauliza
“ natumani umenisikia na
kunielewa.Nini mawazo yako?
Akaulizia Bongani .Dr Susan
akavuta pumzi ndefu na kusema
“Bongani nashindwa niseme
nini lakini naomba nikiri kwamba
nimegswa mno na historia nzima
ya Graca.Siku zote nilikuwa
nikifahamu kwamba Graca ana
tatizo kubwa linalomsumbua
tofauti na ugonjwa wa akili lakini sikuweza kumshawishi anieleze
tatizo lake.Maelezo uliyonipa
yamenistua mno”akasema Dr
Susan
“ Dr Susna sote tumeguswa
na tatizo la Graca na ndiyo maana
tunatafuta namna ya kumsaidia
na mtu pekee ambaye
tunamtegemea kwa sasa ni wewe”
akasema Bongani .Dr Susan
akaonekana kuzama mawazoni
halafu akakohoa kidogo na
kusema
“ Una hakika kwamba Elvis
ana nia ya dhati kumsaidia Graca
na si mmoja wa watu wa baba
yake ambaye anataka kumchukua
na kwenda kumdhuru?
Bongani akatabasamu na
kusemaElvis anafanya kazi kama
ninayofanya mimi na lengo lake ni
kumsaidia Graca hivyo nakuomba
usiwe na hofu naye hata kdogo”
akasema Bongani.Dr Susan
akaegemea kti chake akatazama
juu kwa sekunde kadhaa na
kusema
“ Nitamsaidia.Ninakuamini
sana na nina hakika baada ya
kutoka hapa Graca atakuwa
katika mikono salama”
“ Ahsante sana Dr Susan
.Ahsante sana kwa msaada wako”
akasema Bongani kwa furaha.
“Tutafanya hivi.Graca
nitaondoka naye mimi katika gari
langu.Hataondoka na kitu
chochote hapa kila kitu chake
atakiacha hapa ili kutoleta udadisi
pindi itakapobainika kwambaametoweka.Baada ya kama dakika
kumi nitakapoondoka ninyi
mtafuata kwa nyuma.Nitawasubiri
pale kwa Pamela
Thambo”akasemaDr Susna
naBongani akatoka mle ofisini kwa
Dr Susan akamfuata Elvis
“ What happened? amekubali
kutusuaidia?akauliza Elvis kwa
wai wasi mara tu alipomuona
Bongani
“ Ndiyo! Amekubali
kutusaidia” akasema Bongani
“ Thank you Lord! Akasema
Elvis huku akiinua mikono
kumshukuru Mungu.Bongani
akamueleza Elvis namna mpango
utakavyokuwa kisha wakaelekea
katika kantini ya hospitali hapo
wakaagiza vinywaji baridi.Wakati
wakiendelea na vinwyaji mara ikapita gari ya Dr Susan
ikafunguliwa geti na kutoka bila
kukaguliwa . Dakika kumi baada
ya Dr Susan kutoka Bongani na
Elvis nao wakaelekea lilipo gari
lao,wakaingia na kuondoka.Katika
lango kuu walikaguliwa na
kuruhusiwa kupita wakaondoka.
******************
Katika nyumba kubwa
iliyokuwa na utulivu
mkubwa,Bongani ,Elvis na Graca
walikuwa wamekaa wakijaribu
kuangalia ni kwa namna gani
Elvis na Graca watakavyoweza
kurejea Tanzania salama.Graca
alionekana mchovu sana hali
iliyomlazimu alale sofani na kuwaacha Bongani na Elvis
wakiendelea kujadiliana
“ Kuna njia nyingi za kuweza
kuwaondoa hapa na kuwarudisha
Tanzania lakini tunahitaji kupata
usafiri wa haraka wa kuweza
kuwaondoa hapa leo hii
.Hamtakiwi kulala hapa leo”
akasema Bongani
“ Hilo ni jambo la msingi sana
.Kwa hali ilivyo hatutakiwi kulala
hapa leo.Tutawezaje basi kupata
usafiri wa haraka wa kutuondoa
hapa? “ akauliza Elvis .Bongani
akainama akafikiri kidogo na
kusema
“ Usihofu kuhusu suala hilo
Elvis.Ni jukumu langu
kuhakikisha kwamba unapata
usafiri na unaondoka hapa
salama.Ngoja kwanza niwasiliane na washirika wangu kadhaa nione
namna watakavyoweza kunisaidia”
akasema Bongani kisha akainuka
na kuelekea chumbani .Elvis
akamtazama Graca aliyekuwa
amelala sofani .Graca akageuza
shingo na kugonganisha macho na
Elvis ,akatabasamu kidogo na kwa
sauti ndogo akauliza
“ Mbona unanitazama hivyo?
Elvis akainuka na kwenda kukaa
katika sofa lililokuwa pembeni ya
Graca
“ Unajisikiaje Graca?
Akauliza
“ Ninajisikia vizuri tu.Ni yale
madawa waliyokuwa wakinichoma
ndiyo yanayonifanya nionekane
naumwa sana lakini mimi siumwi”
akasema Pole sana Graca.Kuna kitu
chochote unahitaji kwa sasa?
“Elvis Kwa sasa Ninachohitaji
ni kwenda sehemu salama”
“ Usihofu Graca.Nimeibeba
dhamana hiyo ya usalama wako
na nitahakikisha unakuwa salama
na hakuna atakayekudhuru”
“ Nitashukuru sana kwa hilo
Elvis….” Akasema Graca na mara
Bongani akaingia pale sebuleni
“ Vipi kuna mafanikio yoyote ?
akauliza Elvis
“ Ndiyo.Kunaweza kuwa na
uwezekano.Nimewasiliana na
mmoja wa rafiki zangu
amenidokeza kwamba kuna ndege
ya jeshi inaondoka usiku wa leo
kuelekea Zambia.Nimewasiliana
na mmoja wa makamanda wa
jeshi amenitaka nionane naye sasa hivi.Ngoja nikaonane naye
nimsikilize ni mtu ambaye nina
hakika anaweza akanisaidia”
akasema Bongani
“ Ahsante sana Bongani kwa
msaada wako huu
mkubwa.Ninaomba Mungu
ufanikiwe ili tuweze kuondoka
hapa” akasema Elvis
“ Usihofu Elvis.Ngoja
nikaonane na huyu mkuu
nitarejea baada ya muda mfupi”
akasema Bongani na kutoka.
“ Huyu rafiki yako ana roho
nzuri sana.Ni nadra sana katika
dunia ya sasa kumpata mtu
ambaye anaweza akakuhangaikia
kama huyu.” Akasema Graca
baada ya Bongani kuondoka.Elvis
akatabasamu na kusema Anaitwa Bongani.Naye
anafanya kazi kama ninayoifanya
mimi na vile vile ni rafiki yangu
sana.Ni jadi yetu kusaidiana
tunapokuwa na matatizo na hata
yeye akija Tanzania na akiwa na
tatizo ni jukumu langu
kuhakiksha kwamba nimemsaidia
kwa kila namna.Hivyo ndivyo
tunavyofanya kazi” akasema Elvis
“ Natamani na mimi siku
moja ningefanya kazi kama yako”
akasema Graca
“ Unaipenda kazi hii?
Akauliza Elvis
“ Ndiyo nimetokea kuipenda
sana” akasema Graca
“ Kwa nini unaipenda kazi
hii?
“ Mambo yaliyonikuta ndiyo
yananifanya niipende na na nitake kufanya kazi kama yako.Nataka
nipambane na watu makatili wasio
na hata chembe ya huruma kwa
binadamu wenzao.Vile vile nataka
nilipe kisasi kwa baba yangu
pamoja na washirika wake kwa
kusababisha maisha yangu yawe
namna hii.Unawezaje kunisaidia ili
niweze kuifanya kazi hii? akauliza
Graca
Elvis akavuta pumzi ndefu
akamtazama Graca ambaye
hakuonyesha kama alikua
akitania
“ Graca naomba unisikilize
mdogo wangu .Kwanza kabisa
naomba ufahamu kwamba kuna
maisha mazuri zaidi
yanayokusubiri pale utakapokuwa
huru na unastahili maisha
mazuri.Umri wako bado unaruhusu wewe kuendelea na
masomo na baadae ukaishi
maisha yale ambayo umekuwa
ukiyaota kwa siku nyingi hivyo
naomba uondoe kabisa kichwani
mwako wazo la kutaka kufanya
kazi kama hii.Kazi hii ni ngumu
mno na ina mambo mazito ndani
yake .Inahitaji mtu mwenye roho
ngumu kama ya paka.Mara tu
uingiapo katika kazi hii hutakuwa
na maisha ya kawaida tena kwani
muda wote unakuwa
umezungukwa na maadui ambao
dhamira zao si njema hata kidogo
na walio tayari kuua muda wowote
.Kazi hii inakuweka katika hatari
muda wote.Wengi wetu tumeingia
katika kazi hii bila kufahamu
tunakwenda kukutana na mambo
gani na kwa sasa tumekwisha zoea na kuiona ni ya kawaida lakini
naomba nikuhakikishie kwamba
hii si kazi rahisi kuifanya na wala
usiitamani.Niko tayati kukusaidia
kwa kila namna niwezavyo
kuyajenga maisha yao lakini si
kukusaidia ili uingie katika kazi
hii.Umenielewa Graca? Akaulizia
Elvis
“ Nimekuelewa Elvis japokuwa
bado moyo wangu unataka sana
kuifanya kazi hii ili niweze
kuufutilia mbali mtandao wote wa
baba” akasema Graca na kuzidi
kumvutia zaidi Elvis
“ Mtandao upi Graca? Baba
yako ana mtandao
unaoshughulika na nini? Akauliza
Elvis
“ Usiwe na haraka
Elvis.Utafahamu kila kitu ila naomba ufuate makubaliano yetu
.Nipeleke sehemu salama na
nitakueleza kila kitu
ninachokifahamu” akasema Graca
“ Sawa nitahakikisha
unakuwa salama.Ninahitaji sana
taarifa zako”
“ Usijali Elvis,nitakueleza kila
kitu,” akasema Graca halafu
ghafla akaonekana kama kuna
kitu anakiwaza
“ Elvis kuna kitu ambacho
nilisahau kukwambia”
“ Kitu gani Graca?
“ Kuna watu wawili pale
hospitali wamekuwa
wakinichunguza.Kuna mpishi
mmoja pamoja na mlinzi.Watu
hawa wamekuwa wakinifuatilia
sana na nina hakika watakuwa
wanalipwa na baba ili wanichunguze nyendo
zangu.Japokuwa sina hakika sana
lakini kwa namna walivyokuwa
wakinifuatilia nina hisi lazima
watakuwa wamepewa kazi ya
kunichunguza” akasema Graca
“ Usijali kuhusu hao
watu.Hata kama wamewekwa na
baba yako kukuchunguza hawana
uwezo wa kupambana na
mimi.Usihofu kitu ukiwa na mimi”
akasema Elvis
“ Ahsante sana Elvis”
akasema Graca na kimya kifupi
kikapita
Ilipita saa moja na dakika ishirini
Bongani akarejea
“ Hallow Elvis.Mko salama
wote?
“ Tuko salama.Mambo
yamekwendaje huko? Mambo yamekwenda vizuri
sana .Kuna ndege ya jeshi
inayowapeleka wanajeshi kwenye
mazoezi nchini Zambia na tayari
nimekwisha ongea na kiongozi wa
kikosi hicho na amenikubalia
kuwachukua na ninyi.Hakukuwa
na ugumu wowote kwani wakuu
wengi wa jeshi ni marafiki
zangu.Pale Lusaka nimekwisha
wasiliana na mtu mmoja anaitwa
Stanley Chiteta.Huyu ni rafiki
yangu mkubwa na ni mfanyakazi
wa idara ya usalama wa taifa ya
Zambia.Yeye ndiye
atakayewapeleka hadi katika
mpaka wa Tanzania na Zambia
katika mji wa Tunduma na tokea
pale hamtakuwa na wasi wasi tena
mtakuwa mmekwisha ingia nchini
kwenu na mtatafuta usafiri wa kuelekea Dar es salaam.Stanley ni
mzoefu na nina hakika atakuwa ni
msaada mkubwa kwenu” akasema
Bongani
“ Bongani sina namna ya
kukushukuru kwa msaada wako
huu mkubwa uliotusaidia.”
Akasema Elvis .Bongani
akatabasamu na kusema
“ Usijali Elvis ni jukumu
langu kukusaidia na nimefanya
kile ninachopaswa kukifanya .Kwa
kuwa hatuna muda wa kutosha ni
wakati sasa wa kujiandaa kwa
safari.” Akasema Bongani na
kumpatia Graca mfuko uliokuwa
na nguo na vitu vingine mbali
mbali alivyomnunulia.Graca
akaingia chumbani kujiandaa na
baada ya kuwa tayari safari ya kuelekea uwaja wa ndege wa jeshi
ikaanza
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Ni saa moja za jioni ,kiza
tayari kimetanda angani,Patricia
na Doreen rafiki yake wamekaa
katika kibaraza nyumbani kwa
Doreen wakiongea.Walionekana
kuzama katika maongezi mazito
“ Kwa hiyo Doreen maisha
yangu yanazidi kuwa magumu
siku hadi siku.Umeona wewe
mwenyewe ujumbe ninaotumiwa
katika simu na ndugu za
Elvis.Wanayafanya maisha yangu
yawe magumu sana.Hakuna mtu
anayejali upendo mkubwa uliopo
kati yangu na Elvis.Wao
wanachotaka ni mtoto tu” akasema Patricia kwa
uchungu.Doreen akamtazama
akamuonea huruma rafiki yake
“ Pole sana Patricia
.Ninafahamu ni kiasi gani
unaumizwa na suala hili na kama
nilivyokueleza toka awali kwamba
niko tayari kukusaidia katika
jambo hili.Sipendi kukuona
ukiumia namna hii” Akasema
Doreen
“ Doreen nashukuru sana
kwa kukubali kunisaidia ingawa
najua haikuwa rahisi kukubali
kufanya jambo kama hili lakini
tutafanya nini tena wakati mpango
wetu ulishindikana? Akasema
Patricia .Kimya kikatanda kila
mmoja alikuwa anawaza lake.Ni
Doreen ndiye aliyeuvunja ukimya Patricia naomba usikate
tamaa ndugu yangu. Ni kweli
tulijaribu ikashindikana lakini
hatupaswi kukata tamaa
.Tunapaswa kufikiri namna
nyingine tutakayoweza kufanya ili
kumfanya Elvis akubaliane na
wazo letu” akasema Doreen
“ Doreen unionavyo hapa
tayari nimekwisha fikiri sana na
ninatumai akili yangu imefikia
kiwango chake cha mwisho cha
kufikiri na bado sijapata jibu”
akasema kwa uchungu
Patricia.Doreen akamshika bega
na kumwambia
“ Patricia its too early to give
up.Nina hakika lazima tutapata
njia ya kufanya .Kitu cha msingi
ni kujaribu kutuliza akili na kuja na mpango mpya.Nina hakika
tutafanikiwa “ akasema Doreen
“ Doreen sina shaka nawe
hata kidogo najua uko tayari
kunisadia lakini tatizo liko kwa
Elvis.Ananipenda kupindukia na
hayuko tayari kufanya jambo
kama hili tunalolipanga.Suala la
kumuomba azae na mwanamke
mwingine kwake yeye ni sawa na
usaliti kwangu kwa hiyo hataki
kabisa
kulisikia.Nimechanganyikiwa
Doreen na sijui tutafanya nini na
ndugu za Elvis ndo hao wanadai
mtoto kila leo” akasema Patricia
“ Unaonaje endapo tutakaa
naye na kuongea naye kwa pamoja
kuhusiana na suala hili pengine
anaweza akatuelewa” Akasema
Doreen Elvis ni mtu mwenye
msimamo mkali sana na akisema
hapana katika jambo Fulani basi
huwa ni vigumu sana
kumbadili.Sina hakika kama hata
tukimueleza ukweli anaweza
akatuelewa.Mpango ule
ulioshindikana ulikuwa mzuri
sana” akasema Patricia
“ Pamoja na hayo Patricia ni
mapema mno kukata tamaa.Bado
kuna njia nyingi tu tunaweza
kufanya ili kumfanya Elvis
akubaliane nasi” Akasema Doreen
Patricia akamtazama na
kuonyesha wasi wasi
“ Unazungumzia njia gani
Doreen? Kama unazungumzia
masuala ya waganga mimi siko
tayari kwa hilo.Ni bora niendelee kuteseka kuliko kwenda kwa
waganga”
Doreen akacheka na kusema
“ Hapana Patricia.Mimi si
muumini wa masuala hayo na
tangu utoto wangu siamini kabisa
katika mambo hayo ya
waganga.Nilikuwa namaanisha
kutafuta njia nyingine za kuweza
kulifanikisha jambo hili hata kama
Elvis hataki kuliko kukata tamaa”
akasema Doreen
“ Hilo ndilo jambo la msingi
ambao tunapaswa kulifanya kwa
sasa.Ngoja kwanza niende
nikapumzishe kichwa ili nije na
wazo jipya.” Akasema Patricia
huku akinyanyua mkoba wake na
kupiga hatua kuelekea lilipo gari
lake Sikuwahi kuota kama siku
moja nitakuwa na wakati mgumu
kama nilionao hivi sasa. Kuna
wakati ninajuta hata kuolewa
.Ningekuwa peke yangu haya yote
yasingenitokea.Anyaway
ninampenda Elvis na nitalipigania
penzi letu kwa gharama zozote
zile” akawaza Patricia
********************
Ni shamba lenye ekari zaidi ya
kumi lililoko njekidogo ya jiji la dar
es salaam.Ndani ya shamba hilo
lililosheheni mazao mbalimbali
kulikuwa pia na mifugo kama vile
kuku,ng’ombe n.k.Kati kati ya
shamba lile kuwa kulikuwa na
jumba kubwa la kifahari la ghorofa
tatu.Hili ni shamba linalomilikiwa na Brigedia jenerali Frank
kwaju.Jioni hii ukimya mzito
ulitawala kulizunguka jumba
hili.Ni milio ya mifugo tu ndiyo
iliyokuwa ikisikika .Hakukuwa na
zile pita pita za kila siku za
wafanyakazi
Saa mbili na dakika tatu za
usiku,gari tatu zikawasili katika
geti la kuingilia shambani
hapo.Geti kubwa likafunguliwa na
walinzi na kisha gari zile
zikaikamata barabara iliyokuwa
inaelekea moja kwa moja katikati
ya shamba liliko jumba lile kubwa
lililozungukwa na ukuta mkubwa
na nyaya za umeme juu yake.Geti
likafunguliwa na gari zikaingia
Watu kumi wakashuka toka
katika zile gari wakiongozwa na
Brigedia jenereli Frank halafu wakalekea ndani katika ukumhi
wa siri wa mikutano ulioko ndani
ya jumba lile.Ukumbi tayari
ulikwisha andaliwa maalum kwa
ajili ya kikao hiki kizito
kinachotaratiwa kufanyika usiku
huu.Baada ya kama dakika
ishirini toka akina Frank wawasili
pale numbani,zikawasili gari mbili
na akashuka waziri mkuu mstaafu
Daud Sichoma akiwa
ameongozana na watu wengine
watano wakapokelewa na Brigedia
Frank na kupelekwa katika
ukumbi wa mikutano ambako
wajumbe wote waliokuwa
wakitakiwa katika kikao kile
walikwisha wasili na aliyekuwa
akisubiriwa ni Mheshimiwa Daudi
Sichoma na ujumbe wake.Mara tu
walipoingia katika chumba cha mikutano,watu wote wakasimama
kuonyesha heshima kwa wgeni
waliowasili.Daudi na ujumbe wake
wakaonyeshwa viti wakaketi na
bila kupoteza wakati mwenyekiti
wa kikao kile brigedia Frank
akafungua kikao.Kwanza alianza
kwa kufanya utambulisho.Baada
ya wajumbe kufahamiana kwa
majina na sehemu watokako
Frank akaendelea
“ Ndugu wajumbe nadhani ni
wakati sasa wa kuwatambulisha
wageni wetu wakuu waliotufanya
tukusanyike hapa usiki
huu.Wageni wetu watasimama na
kujitambulisha wao ni akina nani
na kisha tutaendelea na kile
kilichotuleta” akasema Frank na
kuwaomba wageni wale wawili wasimame mmoja mmoja na
kujitambulisha
“ naitwa Mustapha Al
jamal”akaanza kujitambulisha
mgeni wa kwanza
“ Mimi ni raia wa Iran na ni
mmiliki wa wa kampuni moja
kubwa ya mafuta katika
mashariki ya kati.Kwa sababu za
kiusalaam naomba nisiitaje
kampuni yangu hadi hapo
mbeleni” akamaliza
kujitambulisha ndugu Mustapha
na kumpa nafasi mwenzake
aliyeambatana naye
“ Mimi naitwa Alhafidh
Sadiq.Na mimi kama mwenzangu
aliyetangulia ni mmiliki wa
kampuni kadhaa kubwa za mafuta
katika eneo la mashariki ya
kati.Vile vile kama alivyofanya mwenzangu nisingependa na mimi
kuziweka wazi kampuni zangu”
akasema Alhafidh
“ Ahsanteni sana wageni wetu
kwa kujitambulisha.Sisi ni
wenzenu na tumefurahi sana
kuwa nanyi hapa kwa usiku
huu”akasema Frank akameza
mate na kuendelea
“ Ndugu wajumbe baada ya
kuwafahamu wagheni wetu
naomba sasa tuendelee na kikao
chetu.” Akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“ Wageni wetu hawa
wamekuja na jambo zito sana
ambalo utekelezaji wake
unatuhitaji sana sisi.Endapo
jambo hili likifanikiwa basi sisi
sote pamoja wao tutafaidika
sana.Kwa hiyo basi sitaki kuchukua muda mwingi kwani
muongeaji mkuu yupo na ndiye
atakayetueleza kila kitu.Karibu
ndugu Alhafidh ili uweze kutueleza
nini hasa kilichowaleta hapa
Tanzania” akasema Frank.Alhafidh
akaweka sawa koo lake akafungua
faili lililokuwa mbele yake
akaisoma karatasi ya kwanza kana
kwamba kuna mambo
anajikumbusha halafu akasema
“ Ndugu zangu ni furaha
kubwa kwetu kukutana nanyi
usiku huu.Kwa niaba ya
mwenzangu napenda kuchukua
nafasi hii kuwashukuru nyote kwa
kuacha shughuli zenu na kuja
kutusikiliza.Napenda
kuwahakikishia kwamba
hamtajutia kufika kwenu hapa
usiku huu kwani suala tulilowaitia hapa ni lenye manufaa makubwa
kwenu na kwetu pia.Brigedia
jeneral Frank ni rafiki yangu sana
wa muda mrefu.Tumefahamiana
katika shughuli zetu za kibiashara
na ninyi nyote aliowachagua
kuhuddhuria kikao hiki nina
imani ni watu makini na
anaowaakini hivyo natumaini
mazungumzo yetu yatakwenda
vizuri” Alhafidh akanyamza kidogo
akameza mate na kuendelea
“ Nadhani ninyi nyote hapa
mnafahamu hali halisi ya eneo
zima la masharaiki ya kati
inavyoendelea hivi sasa.Katika kila
taarifa ya habari inayotangazwa
duniani hakukosekani taarifa
kuhusiana na mashariki ya
kati.Lakini nini hasa kiini cha
machafuko yote katika eneo hili la mashariki ya kati?.Chanzo chote
cha machafuko ni nchi za
Marekani na washirika wake.Nchi
hizi za magharibi zimekuwa
zikiendesha chochoko dhidi ya
serikali za mashariki ya kati na
hivyo kusababisha machafuko
kusambaa katika eneo zima la
masharikiya kati.Lakini naomba
nyote mjiulize kwa nini mashariki
ya kati? Kwa nini nchi za
magharibi zinachochea migogoro
na mifarakano mashariki ya kati?
Jibu hapa ni jepesi sana.Ni kwa
sababu ya utajiri mkubwa wa
mafuta ulioko katika eneo
hili.Migogoro hii inapotokea
wanaofaidika ni Marekani na
washirika wake kwani hujitokeza
na kuingilia kati huku wakibeba
na kujiwekea akiba kubwa ya mafuta katika nchi zao huku
wakiwaacha maelfu ya watu wasio
na hatia wakiuana.Suala hili
limeamsha hasira na chuki kubwa
dhidi ya marekani na washirika
wake na ndiyo maana mnasikia
kila mara vinaibuka vikundi
mbalimbali vya kigaidi ambavo
vingi adui yake mkubwa ni
Marekani na washirika wake.Hii ni
sababu kubwa iliyopeleka
Marekani kuanza kujitoa taratibu
katika siasa za mashariki ya kati
na kuanza kupunguza utegemezi
wa mafuta toka mashariki ya kati
.Kwa hivi sasa marekani
imeongeza juhudi katika kuzalisha
mafuta ya ndani ikiwemo mafuta
yatokanayo na mimea
.Wamewekeza katika teknolojia
mpya ili watengeneze magari na mitambo visivyohitaji mafuta
mengi.” Alhafidh akanyamaza
kidogo halafu akaendelea.
“ Baada ya utafiti wa miaka
mingi kuhusiana na uwepo wa
mafuta na gesi katika bahari kuu
nchini Tanzania na kulitolewa
taarifa iliyoushangaza
ulimwengu.Kumegunduliwa kiasi
kikubwa cha mafuta nchini
Tanzania ambacho kinasemekena
ni kikubwa kuliko hata
kilekinachoweza kupatikaana eneo
zima la mashariki ya kati.Huu ni
ugunduzi mkubwa sana kuwahi
kufanyika katika miaka ya hivi
karibuni.Ugunduzi huu unaifanya
Tanzania kuingia katika
ulimwengu mpya kwani mataifa
yote makubwa hivi sasa
yameelekeza macho yao nchini Tanzania.Uchumi wa Tanzania
utapaa kwa kasi kubwa na ndani
ya muda mfupi ujao nchi yenu
itaingia katika nchi tajiri duniani”
Alhafidh akatulia na kuwatazama
wajumbe ambao wote walikuwa
wakitabasamu kutokana na taarifa
ile
“ Rais wa marekani
amemaliza ziara ya siku nne
nchini Tanzania ikiwa ni ziara
ndefu kuwahi kufanywa na rais
wa marekani katika taifa moja
husan haya ya bara la
Afrika.Ninathubutu kusema
kwamba hii imekua ni ziara yenye
mafanikio makubwa sana kwa
marekani.Mambomengi mazuri
yamefanyika katika ziara hiyo
ikiwa ni pamoja na kuzindua
miradi mikubwa ya nishati ,reli na maji,Pamoja na mambo hayo
makubwa huku watanzania walio
wengi wanaamni ni neema kubwa
wameipata lakini nataka mjiulize
kwa nini iwe sasa? Kwanini rais
wa marekani aitembelee Tanzania
sasa tena ikiwa ni ziara ndefu
kuwahi kufanywa na kiongozi
yoyote wa taifa la marekani katika
nchi yoyote ya afrika? Jibu hapa
ni rahisi tu.Nikwa sababu ya
neema kubwa ya mafuta na gesi
iliyogunduliwa Tanzania..Sababu
ya pili ni kujiimarisha kijeshi kwa
kujenga kambi yake hapa
Tanzania ili kuendeleza
mapambano dhidi ya wale wote
wenye kupambana na taifa hili
bila kuchoka na hasa vikundo vya
kigaidi kama vile
Alqaeda,alshabaab,Boko haram, n.k ambavyo vimekuwa
vikijimarisha sana kwa siku za
karibuni” Alhafish akanyamaza
kidogo na kuwatazama wajumbe
wa kikao kile ambao wote
walikuwa kimya kabisa
wakimsikiliza kisha akaendelea
“ Kama nilivyowafahamisha
kwamba ziara hii ya rais wa
Marekani nchini Tanzania ilikuwa
ni kwa sababu maalum zenye
manufaa kwa taifa hilo.Ukiacha
sababu za kiusalama ,kubwa
lililomleta hapa ni suala la mafuta
na gesi.Mtakumbuka awali
niliwaeleza kwamba kwa sasa
Marekani wanapunguza utegemezi
wa mafuta ya mashariki ya kati na
na kuifanya itegemee mafuta yake
ya ndani.Ugunduzi huu wa
kiwango kikubwa cha mafuta na gesi nchini Tanzania umeifanya
Marekani ianze kitolea macho
tanzania nchi ambayo imekuwa
ikipokea misaada mingi toka
Marekani.Katika ziara hii ya rais
wa Marekani kumesainiwa
mikataba kadhaa mikubwa baina
ya serikali ya tanzania na
wawekezaji wakubwa wa mafuta
na gesi toka Marekani.Katika
mikataba hiyo Serikali ya
Tanzania imeyaruhusu
makampuni makubwa ya
marekani kufanya uwekezaji
mkubwa katka sekta ya mafuta
na gesi Tanzania.Hii ina maana
moja kubwa kwamba makampuni
ya kimarekani ndiyo
yatakayoliongoza soko la mafuta
duniani .Marekani haitakuwa tena
na tatizo la mafuta na haitahitaji tena mafuta toka mashariki ya
kati.Washirika wa Marekani pia au
nchi zile kubwa zinazoongoza kwa
viwanda duniani hazitakuwwa
tena na wasi wasi kuhusiana na
suala la mafuta na gesi
,watahamia katika mafuta
yatokayo Tanzania.Bei ya mafuta
duniani itaporomoka na hali hii
itayalazimisha makampuni ya
mafuta ya mashariki ya kati
kupunguza bei ya mafuta ili
kuendana na bei itakayokuwepo
katika soko la dunia.Kushuka kwa
bei ya mafuta kwa nchi za
mashariki ya kati inamaanisha
kwamba hata uchumi wa nchi hizi
lazima utaporomoka kwa sababu
uchumi wao unategemea sana
biashara ya mafuta.Lengo kuu la
Marekani ni kuhakikisha kwamba uchumi wa nchi za mashariki ya
kati unazorota kutokana na
kudorora kwa biashara ya mafuta”
akanyamaza akanywa maji kidogo
kisha akaendelea.
“Nadhani hadi hivi sasa kuna
picha ambayo tayari mmekwisha
ipata kuhusiana na ziara ya rais
wa Mareani” akasema Alhafidhi na
wajumbe wote wakatikisa vichwa
ishara kwamba wanakubaliana
naye.Akatabasamu halafu
akaendelea
“ Suala hili limekuwa
likiumiza vichwa sana
makampuni makubwa ya mafuta
ya masharki ya Kati na hata
serikali zao kwa ujumla.Ni suala
linalohusu maslahi mapana ya
mataifa haya ambayo uchumi
wake unategemea mafuta.Hatutaki makampuni yetu yatetereke
kutokana na kuyumba kwa bei ya
mafuta katika soko la
dunia.Hatutaki uchumi wa
mataifa yetu uzorote kutokana na
kuyumba kwa bei ya mafuta .Vita
vya wenyewe kwa wenyewe katika
eneo zima la mashariki ya kati
vimesababisha chumi za mataifa
haya zilizokuwa zikikua kwa kasi
kuzozorota .Endapo litaatokea
tena baa hilo la kuporomoka kwa
bei ya mafuta mataifa haya
yatakuwa yakichungulia katika
lindi kubwa la umasikini kwani
chumi zao hazitaweza kustawi
kamwe.Ni kutokana na hali hiyo
kumekuwa na mazungumzo ya
kina kati ya serikali za mashariki
ya kati na makampuni makubwa
ya mafuta ya wazawa wa mashiriki ya kati.katika mazungumzo hayo
yote suala la Marekani kuendesha
sekta ya mafuta ya Tanzania
limepingwa vikali.Hatuko tayati na
hatutakuwa tayari kuiacha
Marekani itawale sekta hii nyeti
sana ambayo ndiyo hasa uchumi
wetu sisi watu wa mashariki ya
kati.Narudia tena kwamba hatuko
tayari na wala hatuwakuwa tayari
kuiacha Marekani itawale sekta ya
mafuta ya dunia.Kwa maana hiyo
basi tumefikia uamuzi wa
kuusimamisha na kuuzima kabisa
mpango wa marekani wa
kuidhibiti sekta ya mafuta
duniani.” Alhafidh akatoa
kitambaa na kujifuta jasho halafu
akanywa maji kidogona kuendelea.
“ Serikali ya Tanzania tayari
imekwisha sainiana mikataba mikubwa na makampuni ya
kimarekani na hivyoo suala hilo
kwa sasa lipo kisheria .Hakuna
namna tunayoweza kufanya ili
kutengua mikataba hiyo mikubwa
sana.Kuna njia moja tu ambayo
tunaweza kuifanya ili kulimaliza
suala hili” Alhafidh akanyamaza
na kuziangalia nyuso za wajumbe
waliokuwa kimya
wakimsikiliza.Akanyanyua glasi ya
maji na kupiga funda moja
akaiweka chini akatoa kitambaa
na kujifuta jasho lililokuwa
likimtoka usoni licha ya ukumbi
ule mdogo kuwa na kiyoyozi.Hii
ilitokaa na uzito wa suala
walilokuwa wakiliongelea
“ Ndugu wajumbe njia pekee
ya kuweza kulipatia ufumbuzi suala hili ni kwa kuiangusha
serikali iliyoko madarakani”
Kimya kizito kikatanda mle
ndani.Sura za wajumbe
zilionyesha mabadiliko ya
ghafla.Minong’ono ya chini kwa
chini ikasikika.Mara Daudi
Sichoma akasimama na
kumuelekezea macho Brigedia
Frank huku midomo yake
ikitetemeka
“ What is this Frank? Hiki
ndicho kitu cha muhimu
ulichoniitia? I cant believe this
!!!....akasema Daudi kwa ukali
.wajumbe wengine wanne
wakasimama wakionyesha
kustushwa na kauli ile.Hali
ilibadikika mle chumbani
ikamlazimu Brigedia Frank
asimame. Please calm down
guys.Nawaombeni mtulie na
tusikilizane.Mr David tafadhali
naomba ukae chini na
tusikilizane”akasema Frank na
wale wajumbe waliokuwa
wamesimama wakiongozwa na
Daudi Sichoma wakaketi na
ukimya ukatawala mle ndani
.Frank alipohakikisha wajumbe
wote wametulia kaendelea
“ Ninauona mstuko mkubwa
katika nyuso zenu.Nilitegemea
kitu kama hiki kutokea.Hii si
taarifa nyepesi hata kidogo.Ni
taarifa nzito na yenye kustusha
lakini nyote niliowachagua
kuhudhuria kikao hiki
ninauhakika mkubwa kwamba
hizi ni taarifa njema sana
kwenu.Naomba msiwe na jazba na twende taratibu tutaelewana”
akasema Frank
“Frank kuiangusha serikali si
suala rahisi hata kidogo kama
unavyodhani” akasema David
Sichoma .Frak akatabasamu na
kusema
“ Ninafahamu
unachokimaanisha David lakini
nina uhakika mkubwa hakuna
kitakacho
shindikana.Nime………”kabla
Frank hajaendelea zaidi Daudi
Sichoma akamkatisha
“Frank you know nothing
.Suala ulilolileta ni suala
lisilowezekana kabisa” akasema
Daudi
“ Unaweza kuwa sahihi David
kwamba sijawahi kuwa katika
serikali lakini ninafahamu kila kinachoendelea
serikalini.Ninawafahamu viongozi
wakubwa serikalini.Ninaifahamu
seriali nje na ndani.Daudi
Sichoma ninakufahamu vyema
umewahi kushika nyadhifa
mbalimbali za uongozi serikalini
na hatimaye ukafanikiwa kwa
waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania.Nafahamu
ndoto yako kubwa ilikuwa ni kuwa
rais wa Tanzania lakini kwa bahati
mbaya ndoto yako hiyo
haikuwezekana kutimia kwa
sababu watu ndani ya serikali
waliligundua hilo na hawakuwa
tayari kukuona ukishika nafasi ya
urais na ndiyo maana walianza
kukuandama kwa mambo mengi
na hatimaye kukuzushia kashfa
kubwa na ukaondolewa katika nafasi yako ya uwaziri
mkuu.Ninafahamu madai yale
yaliyotolewa dhidi yako kuhusiana
na kashfa ile hayakuwa ya kweli
na zilikuwa ni njama za kisisasa
na kuhakikisha unapotea kabisa
katika ulingo wa siasa.Lengo lao
limefanikiwa kwani wamefanikiwa
kabisa kukuondoa katika ulingo
wa siasa.Hausikiki tena viywani
mwa watu.Umekwisha sahaulika
kabisa na ndoto yako ya urais
imepotea.Najua unajitahidi sana
kutaka kujirudisha katika medani
za siasa lakini wabaya wako
hawataki kukupa tena
nafasi.Vikwazo vimekuwa vingi na
wamepambana hadi kuhakikisha
kwamba umaarufu wako
unapotea.This is your last chacne
to make your dream come true.Ni wakati wako wa kuitengeneza njia
ya kuingia katika lile jumba
jeupe.” Frank akanyamaza
akamtazama Daudi Sichoma
aliyekuwa kimya akimsikiliza
halafu akawageukia wajumbe
wengine
“Nyote niliowaita hapa
nafahamu ni wenye kuhitaji sana
nafasi za uongozi na mpango huu
wa kuiangusha serikali ndio
mpango pekee utakaowawezesha
na kuwahakikishia nafasi za
uongozi.Kuiangusha serikali
iliyoko madarakani ni jambo zito
ambalo haliwezi kufanywa na sisi
pekee yetuliomo humu chumbani
.Huu ni mchakato mrefu na
jumuishi nikimaanisha kwamba ni
mchakato unaohusisha watu
wengi lakini wenye lengo na nia moja.Sisi sote tulioko hapa ndio
tutakaoratibu mchakato mzima wa
mapinduzi haya.Naombeni ndugu
zangu msikate tamaa.Tunaweza
kulifanya jambo hili.Mkumbuke
pia tunayo sapoti ya kutosha toka
kwa washirika wetu katika suala
hili.Tayari zimekwisha tengwa
shilingi Trilioni sita kwa ajili tu ya
kufanikisha jambo hili.Pamoja na
fedha lakini washirika wetu
watatusaidia pia katika ila kitu
tunachokihitaji”akasema Frank na
kunyamaza tena akawatazama
wajumbe wale.daudi sichoma
akakohoa kidogo na kusema
“ Kidogo sasa ninaanza
kukuelewa Frank.Mpango huu si
mbaya kama nilivyokuwa
ninaufukiria isipokuwa ni mpango
mzito wenye kuhitaji mikakati mizito pia .Lazima tuvihusishe
vyombo vya ulinzi na usalama
hususani jeshi na idara ya
usalama wa taifa,wanasiasa na
wadau wengine watakaoonekana
kuhitajika.Mimi niko tayari
kushirikiana nanyi katika mpango
huu lakini kwa makubaliano
maalum” akasema Daudi Sichoma
“ Ahsante sana Daud kwa
maamuzi yako .Kwa kuwa bado
tuna mchakato mrefu mbele yetu
nina imani kwamba tutafikia
makubaliano unayohitaji”
akasema Frank na kuwageukia
wajumbe wengine
“ Ndugu zangu kati yenu
kuna yeyote mwenye mawazo
tofauti? Kuna yeyote mwenye
duku duku au maoni yoyote
kuhusiana na mpango huu? Akauliza Frank.Kabla mtu yeyote
hajajibu,simu ya Frank
ikaita,akastuka baada ya kuona
watu wote wanamtazama
“ Samahani ndugu zangu
kwa kutoizima simu yangu katika
kikao kizito kama hiki” akasema
Frank huku akitoa simu yake kwa
lengo la kuizima lakini mara tu
alipotazama jina la mpigaji
akastuka.Jina lilisomeka kama
hospitali Graca
“ Samahani jamani naomba
niipokee simu hii ni muhimu
sana” akasema Frank na kutoka
nje ya kile chumba
“Hallow” akasema Frank
“ Hallow Frank habari za Dar
es salaam? Ikasema sauti ya
upande wa pili
Sehemu 23
wapi ilipo kompyuta yake.Elvis
naomba usiniache hapa.take me
anywhere safe.Ni mara yanguya
kwanza kukuona lakini I feel safe
around.macho yako yananifanya
nikuamini” akasema Graca huku
macho yake yakilengwa na
machozi
“ Nitakusaidia
Graca.Nitakuondoa hapa na
kukupeleka sehemu salama
kabisa ambako si baba yako wala
yeyote anayekutafuta
atakupata.Lakini kabla ya kufanya
hivyo kuna jambo nataka
kulifahamu toka kwako.Nataka
kufahamu ndani ya hilo begi
kulikuwa na kitu gani cha
muhimu kiasi cha kupelekea
baba yako kufanya haya yote
aliyoyafanya?Kompyuta hiyo uliyoichukua ilikuwa na jambo
gani na iko wapi kwa sasa?
Graca akamtazama Elvis na
kusema
“Siwezi kukueleza chochote
kwa sasa hivi hadi hapo
nitakapohakikisha kwamba niko
sehemu salama.Take me
somewhere safe and I will tell you
everythingI know na nitakueleza
kompyuta hiyo iko wapi” akasema
Graca
“ Graca ninaelewa hofu yako
lakini naomba uniamini na
uniambie kuhusiana na
ulichokigunuda kwa baba
yako.Tafadhali naomba
ushirikiane nani.Usiniogope mimi
si mtu mbaya” akasema Elvis
“ Elvis najua umefunga safari
ndefu kuja huku kuonana na mimi kwa nia njema kabisa na
kama nilivyokueleza awali kwamba
ninakuamini na niko tayari
kukueleza kila kitu lakini kwa
sasa siwezi kukueleza jambo lolote
ninalolifahamu hadi hapo
nitakapohakikisha kwamba niko
salama.Mkoba ule na kilichomo
ndani yake ndiyo kinga yangu kwa
sasa kwa hiyo fanya
nilivyokuelekeza na nitakueleza
kila unachokitaka” akasema Graca
“ Graca !!... Elvis akataka
kusema kitu lakini Graca
akamzuia
“ Elvis hakuna chochote
utakachoniambia kitakachoweza
kuubadili msimamo wangu.Ninazo
taarifa nyeti sana ambazo
ninaamini zitakuwa ni za msaada
mkubwa sana kwako lakini siwezi kukueleza hadi hapo
nitakapohakikisha kwamba niko
salama” akasemaGraca.Elvis
akamtazama kwa makini usoni na
kuamini kile alichokisema Graca
“ She’s telling the
truth.hawezi kunieleza chochote
bila kufanya anavyotaka” akawaza
Elvis na kusema
“Nimekuelewa
Graca.Naomba unipe muda
kidogo niangalie namna ya
kufanya.I promise you I’ll get
you out of here.”akasema
Elvis.Bila kusema chochote
Graca akainuka na kutembea
taratibu kuelekea ndani.Elvis
akamtazama namna
alivyokuwa akitembea kwa
unyonge akamuonea huruma
sana lazima nimsaidie.Siwezi
kumuacha hapa akiendelea
kuteseka.Akawaza Elvis
halafu akaelekea katika meza
waliyokuwa wamekaa Bongan
na Dr Susan
“ Tayari mmekwisha
ongea? Umefanikiwa kupata
ulichokuwa unakihitaji? Akauliza
Bongani
“ Bongani mambo si rahisi
kama nilivyitegemea" akasema
Elvis
“ Nini kimetokea Elvis,Graca
hajakupa ushirikiano? ” akauliza
Bongani.Elvis akamvuta pembeni
kidogo ili waongee.Akamweleza
kila kitu alichoongea na Graca
“kwa hiyo mambo yako
namna hiyo Bongani.Graca kuna
jambo kubwa analifahamu kuhusiana na baba yake lakini
hayuko tayari kuliweka wazi bila
kwanza kuwa na uhakika wa
usalama wa maisha yake”
akasemaElvis
“ kwa hiyo tutafanya nini
Elvis ili tuweze kuzipata taarifa
hizo toka kwa Graca?akauliza
Bongani
“hakuna njia nyingine ya
kufanya zaidi ya kufanya vile
anavyotaka yaani kumpeleka
sehemu salama.Bongani naomba
unisaidie katika hili ili niweze
kumuondoa Graca hapa
hospitali.Pamoja na kuwa na kitu
cha muhimu ninachokihitaji lakini
nimeguswa sana na mateso ya
binti huyu,ameteseka kiasi cha
kutosha na siko tayari kumuacha akiendelea kuteseka
hapa.Tafadhali naomba unisaidie”
Bongani akafikiri kwa muda
na kusema
“ Hata mimi nimeguswa sana
na histora ya huyu binti na
nitakusaidia ili tuweze kumtoa
hapa.Ninachotaka kufahamu ni
kuhusu usalama wa maisha yake
endapo tutafanikiwa kumuondoa
hapa.Una hakika atakuwa
salama?akauliza Bongani.Elvis
akawaza kidogo na kusema
“Bongani suala la usalama wa
Graca lina changamoto nyingi
lakini hilo ni jukumu langu
ambalo sina budi kulibeba na
nitahakikisha kwamba anakuwa
salama.Nitamlinda dhidi ya yeyote
mwenye nia ya kumdhuru” “Bongani akainama akafikri
kidogo na kusema
“ sawa Elvis
.Nitakusaidia,naomba unipe muda
wa dakika kama kumi nikaongee
na Dr Susan nione kama anaweza
akatusaidia”
“ una hakika atatusaidia?
Akauliza Elvis
“ Nina uhakika lakini hatuna
budi kujaribu.Nina mahusiano
naye mazuri.Tuliwahi kuwa katika
mahusiano ya kimapenzi wakati
tukiwa chuo kikuu na mpaka sasa
bado tuna mahusiano mazuri”
akasema Bongani na kuelekea
katika ofisi ya Dr Susan
“Nahisi kuna suala zito sana
ambalo liko nyuma ya pazia kiasi
kwamba Frank alikuwa tayari hata
kutaka kumuua mwanae kwa ajili ya kulificha.Lazima nilifahamu
suala hilo .Nitamsaidia Graca kwa
namna yoyote ile nitakayoweza na
nitamuondoa hapa.Nitamlinda
dhidi ya yeyote yule anayetishia
maisha yake.”akawaza Elvis
Bongani alitumia zaidi ya
dakika kumi na tano kuongea na
Dr Susan kumuelezea kuhusiana
na tatizo la Graca.Hadi anamaliza
kumueleza Dr Susan alikuwa
anahisi baridi.Alionekana kuzama
katika mawazo mengi
“ Siku zote nilijua lazima
kuna jambo haliko sawa kwa
Graca.Sikutaka kuharakisha
kumuuliza nini kilichokuwa
kinamsumbua na ndiyo maana
nikajenga ukaribu mkubwa kati
yangu naye ili siku moja aweze
kunieleza tatizo lake.Namuoenea huruma sana binti huyu kwa
mateso makubwa aliyonayo.Huu
ni mtihani mkubwa kwangu lakini
lazim animsaidie” Dr Susan akiwa
katika mawazo mengi mara
akastuliwa na Bongani
“ Dr Susan !!...
Akainua kichwa na kumtazama
Bongani
“Unasemaje Bongan? Akauliza
“ natumani umenisikia na
kunielewa.Nini mawazo yako?
Akaulizia Bongani .Dr Susan
akavuta pumzi ndefu na kusema
“Bongani nashindwa niseme
nini lakini naomba nikiri kwamba
nimegswa mno na historia nzima
ya Graca.Siku zote nilikuwa
nikifahamu kwamba Graca ana
tatizo kubwa linalomsumbua
tofauti na ugonjwa wa akili lakini sikuweza kumshawishi anieleze
tatizo lake.Maelezo uliyonipa
yamenistua mno”akasema Dr
Susan
“ Dr Susna sote tumeguswa
na tatizo la Graca na ndiyo maana
tunatafuta namna ya kumsaidia
na mtu pekee ambaye
tunamtegemea kwa sasa ni wewe”
akasema Bongani .Dr Susan
akaonekana kuzama mawazoni
halafu akakohoa kidogo na
kusema
“ Una hakika kwamba Elvis
ana nia ya dhati kumsaidia Graca
na si mmoja wa watu wa baba
yake ambaye anataka kumchukua
na kwenda kumdhuru?
Bongani akatabasamu na
kusemaElvis anafanya kazi kama
ninayofanya mimi na lengo lake ni
kumsaidia Graca hivyo nakuomba
usiwe na hofu naye hata kdogo”
akasema Bongani.Dr Susan
akaegemea kti chake akatazama
juu kwa sekunde kadhaa na
kusema
“ Nitamsaidia.Ninakuamini
sana na nina hakika baada ya
kutoka hapa Graca atakuwa
katika mikono salama”
“ Ahsante sana Dr Susan
.Ahsante sana kwa msaada wako”
akasema Bongani kwa furaha.
“Tutafanya hivi.Graca
nitaondoka naye mimi katika gari
langu.Hataondoka na kitu
chochote hapa kila kitu chake
atakiacha hapa ili kutoleta udadisi
pindi itakapobainika kwambaametoweka.Baada ya kama dakika
kumi nitakapoondoka ninyi
mtafuata kwa nyuma.Nitawasubiri
pale kwa Pamela
Thambo”akasemaDr Susna
naBongani akatoka mle ofisini kwa
Dr Susan akamfuata Elvis
“ What happened? amekubali
kutusuaidia?akauliza Elvis kwa
wai wasi mara tu alipomuona
Bongani
“ Ndiyo! Amekubali
kutusaidia” akasema Bongani
“ Thank you Lord! Akasema
Elvis huku akiinua mikono
kumshukuru Mungu.Bongani
akamueleza Elvis namna mpango
utakavyokuwa kisha wakaelekea
katika kantini ya hospitali hapo
wakaagiza vinywaji baridi.Wakati
wakiendelea na vinwyaji mara ikapita gari ya Dr Susan
ikafunguliwa geti na kutoka bila
kukaguliwa . Dakika kumi baada
ya Dr Susan kutoka Bongani na
Elvis nao wakaelekea lilipo gari
lao,wakaingia na kuondoka.Katika
lango kuu walikaguliwa na
kuruhusiwa kupita wakaondoka.
******************
Katika nyumba kubwa
iliyokuwa na utulivu
mkubwa,Bongani ,Elvis na Graca
walikuwa wamekaa wakijaribu
kuangalia ni kwa namna gani
Elvis na Graca watakavyoweza
kurejea Tanzania salama.Graca
alionekana mchovu sana hali
iliyomlazimu alale sofani na kuwaacha Bongani na Elvis
wakiendelea kujadiliana
“ Kuna njia nyingi za kuweza
kuwaondoa hapa na kuwarudisha
Tanzania lakini tunahitaji kupata
usafiri wa haraka wa kuweza
kuwaondoa hapa leo hii
.Hamtakiwi kulala hapa leo”
akasema Bongani
“ Hilo ni jambo la msingi sana
.Kwa hali ilivyo hatutakiwi kulala
hapa leo.Tutawezaje basi kupata
usafiri wa haraka wa kutuondoa
hapa? “ akauliza Elvis .Bongani
akainama akafikiri kidogo na
kusema
“ Usihofu kuhusu suala hilo
Elvis.Ni jukumu langu
kuhakikisha kwamba unapata
usafiri na unaondoka hapa
salama.Ngoja kwanza niwasiliane na washirika wangu kadhaa nione
namna watakavyoweza kunisaidia”
akasema Bongani kisha akainuka
na kuelekea chumbani .Elvis
akamtazama Graca aliyekuwa
amelala sofani .Graca akageuza
shingo na kugonganisha macho na
Elvis ,akatabasamu kidogo na kwa
sauti ndogo akauliza
“ Mbona unanitazama hivyo?
Elvis akainuka na kwenda kukaa
katika sofa lililokuwa pembeni ya
Graca
“ Unajisikiaje Graca?
Akauliza
“ Ninajisikia vizuri tu.Ni yale
madawa waliyokuwa wakinichoma
ndiyo yanayonifanya nionekane
naumwa sana lakini mimi siumwi”
akasema Pole sana Graca.Kuna kitu
chochote unahitaji kwa sasa?
“Elvis Kwa sasa Ninachohitaji
ni kwenda sehemu salama”
“ Usihofu Graca.Nimeibeba
dhamana hiyo ya usalama wako
na nitahakikisha unakuwa salama
na hakuna atakayekudhuru”
“ Nitashukuru sana kwa hilo
Elvis….” Akasema Graca na mara
Bongani akaingia pale sebuleni
“ Vipi kuna mafanikio yoyote ?
akauliza Elvis
“ Ndiyo.Kunaweza kuwa na
uwezekano.Nimewasiliana na
mmoja wa rafiki zangu
amenidokeza kwamba kuna ndege
ya jeshi inaondoka usiku wa leo
kuelekea Zambia.Nimewasiliana
na mmoja wa makamanda wa
jeshi amenitaka nionane naye sasa hivi.Ngoja nikaonane naye
nimsikilize ni mtu ambaye nina
hakika anaweza akanisaidia”
akasema Bongani
“ Ahsante sana Bongani kwa
msaada wako huu
mkubwa.Ninaomba Mungu
ufanikiwe ili tuweze kuondoka
hapa” akasema Elvis
“ Usihofu Elvis.Ngoja
nikaonane na huyu mkuu
nitarejea baada ya muda mfupi”
akasema Bongani na kutoka.
“ Huyu rafiki yako ana roho
nzuri sana.Ni nadra sana katika
dunia ya sasa kumpata mtu
ambaye anaweza akakuhangaikia
kama huyu.” Akasema Graca
baada ya Bongani kuondoka.Elvis
akatabasamu na kusema Anaitwa Bongani.Naye
anafanya kazi kama ninayoifanya
mimi na vile vile ni rafiki yangu
sana.Ni jadi yetu kusaidiana
tunapokuwa na matatizo na hata
yeye akija Tanzania na akiwa na
tatizo ni jukumu langu
kuhakiksha kwamba nimemsaidia
kwa kila namna.Hivyo ndivyo
tunavyofanya kazi” akasema Elvis
“ Natamani na mimi siku
moja ningefanya kazi kama yako”
akasema Graca
“ Unaipenda kazi hii?
Akauliza Elvis
“ Ndiyo nimetokea kuipenda
sana” akasema Graca
“ Kwa nini unaipenda kazi
hii?
“ Mambo yaliyonikuta ndiyo
yananifanya niipende na na nitake kufanya kazi kama yako.Nataka
nipambane na watu makatili wasio
na hata chembe ya huruma kwa
binadamu wenzao.Vile vile nataka
nilipe kisasi kwa baba yangu
pamoja na washirika wake kwa
kusababisha maisha yangu yawe
namna hii.Unawezaje kunisaidia ili
niweze kuifanya kazi hii? akauliza
Graca
Elvis akavuta pumzi ndefu
akamtazama Graca ambaye
hakuonyesha kama alikua
akitania
“ Graca naomba unisikilize
mdogo wangu .Kwanza kabisa
naomba ufahamu kwamba kuna
maisha mazuri zaidi
yanayokusubiri pale utakapokuwa
huru na unastahili maisha
mazuri.Umri wako bado unaruhusu wewe kuendelea na
masomo na baadae ukaishi
maisha yale ambayo umekuwa
ukiyaota kwa siku nyingi hivyo
naomba uondoe kabisa kichwani
mwako wazo la kutaka kufanya
kazi kama hii.Kazi hii ni ngumu
mno na ina mambo mazito ndani
yake .Inahitaji mtu mwenye roho
ngumu kama ya paka.Mara tu
uingiapo katika kazi hii hutakuwa
na maisha ya kawaida tena kwani
muda wote unakuwa
umezungukwa na maadui ambao
dhamira zao si njema hata kidogo
na walio tayari kuua muda wowote
.Kazi hii inakuweka katika hatari
muda wote.Wengi wetu tumeingia
katika kazi hii bila kufahamu
tunakwenda kukutana na mambo
gani na kwa sasa tumekwisha zoea na kuiona ni ya kawaida lakini
naomba nikuhakikishie kwamba
hii si kazi rahisi kuifanya na wala
usiitamani.Niko tayati kukusaidia
kwa kila namna niwezavyo
kuyajenga maisha yao lakini si
kukusaidia ili uingie katika kazi
hii.Umenielewa Graca? Akaulizia
Elvis
“ Nimekuelewa Elvis japokuwa
bado moyo wangu unataka sana
kuifanya kazi hii ili niweze
kuufutilia mbali mtandao wote wa
baba” akasema Graca na kuzidi
kumvutia zaidi Elvis
“ Mtandao upi Graca? Baba
yako ana mtandao
unaoshughulika na nini? Akauliza
Elvis
“ Usiwe na haraka
Elvis.Utafahamu kila kitu ila naomba ufuate makubaliano yetu
.Nipeleke sehemu salama na
nitakueleza kila kitu
ninachokifahamu” akasema Graca
“ Sawa nitahakikisha
unakuwa salama.Ninahitaji sana
taarifa zako”
“ Usijali Elvis,nitakueleza kila
kitu,” akasema Graca halafu
ghafla akaonekana kama kuna
kitu anakiwaza
“ Elvis kuna kitu ambacho
nilisahau kukwambia”
“ Kitu gani Graca?
“ Kuna watu wawili pale
hospitali wamekuwa
wakinichunguza.Kuna mpishi
mmoja pamoja na mlinzi.Watu
hawa wamekuwa wakinifuatilia
sana na nina hakika watakuwa
wanalipwa na baba ili wanichunguze nyendo
zangu.Japokuwa sina hakika sana
lakini kwa namna walivyokuwa
wakinifuatilia nina hisi lazima
watakuwa wamepewa kazi ya
kunichunguza” akasema Graca
“ Usijali kuhusu hao
watu.Hata kama wamewekwa na
baba yako kukuchunguza hawana
uwezo wa kupambana na
mimi.Usihofu kitu ukiwa na mimi”
akasema Elvis
“ Ahsante sana Elvis”
akasema Graca na kimya kifupi
kikapita
Ilipita saa moja na dakika ishirini
Bongani akarejea
“ Hallow Elvis.Mko salama
wote?
“ Tuko salama.Mambo
yamekwendaje huko? Mambo yamekwenda vizuri
sana .Kuna ndege ya jeshi
inayowapeleka wanajeshi kwenye
mazoezi nchini Zambia na tayari
nimekwisha ongea na kiongozi wa
kikosi hicho na amenikubalia
kuwachukua na ninyi.Hakukuwa
na ugumu wowote kwani wakuu
wengi wa jeshi ni marafiki
zangu.Pale Lusaka nimekwisha
wasiliana na mtu mmoja anaitwa
Stanley Chiteta.Huyu ni rafiki
yangu mkubwa na ni mfanyakazi
wa idara ya usalama wa taifa ya
Zambia.Yeye ndiye
atakayewapeleka hadi katika
mpaka wa Tanzania na Zambia
katika mji wa Tunduma na tokea
pale hamtakuwa na wasi wasi tena
mtakuwa mmekwisha ingia nchini
kwenu na mtatafuta usafiri wa kuelekea Dar es salaam.Stanley ni
mzoefu na nina hakika atakuwa ni
msaada mkubwa kwenu” akasema
Bongani
“ Bongani sina namna ya
kukushukuru kwa msaada wako
huu mkubwa uliotusaidia.”
Akasema Elvis .Bongani
akatabasamu na kusema
“ Usijali Elvis ni jukumu
langu kukusaidia na nimefanya
kile ninachopaswa kukifanya .Kwa
kuwa hatuna muda wa kutosha ni
wakati sasa wa kujiandaa kwa
safari.” Akasema Bongani na
kumpatia Graca mfuko uliokuwa
na nguo na vitu vingine mbali
mbali alivyomnunulia.Graca
akaingia chumbani kujiandaa na
baada ya kuwa tayari safari ya kuelekea uwaja wa ndege wa jeshi
ikaanza
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Ni saa moja za jioni ,kiza
tayari kimetanda angani,Patricia
na Doreen rafiki yake wamekaa
katika kibaraza nyumbani kwa
Doreen wakiongea.Walionekana
kuzama katika maongezi mazito
“ Kwa hiyo Doreen maisha
yangu yanazidi kuwa magumu
siku hadi siku.Umeona wewe
mwenyewe ujumbe ninaotumiwa
katika simu na ndugu za
Elvis.Wanayafanya maisha yangu
yawe magumu sana.Hakuna mtu
anayejali upendo mkubwa uliopo
kati yangu na Elvis.Wao
wanachotaka ni mtoto tu” akasema Patricia kwa
uchungu.Doreen akamtazama
akamuonea huruma rafiki yake
“ Pole sana Patricia
.Ninafahamu ni kiasi gani
unaumizwa na suala hili na kama
nilivyokueleza toka awali kwamba
niko tayari kukusaidia katika
jambo hili.Sipendi kukuona
ukiumia namna hii” Akasema
Doreen
“ Doreen nashukuru sana
kwa kukubali kunisaidia ingawa
najua haikuwa rahisi kukubali
kufanya jambo kama hili lakini
tutafanya nini tena wakati mpango
wetu ulishindikana? Akasema
Patricia .Kimya kikatanda kila
mmoja alikuwa anawaza lake.Ni
Doreen ndiye aliyeuvunja ukimya Patricia naomba usikate
tamaa ndugu yangu. Ni kweli
tulijaribu ikashindikana lakini
hatupaswi kukata tamaa
.Tunapaswa kufikiri namna
nyingine tutakayoweza kufanya ili
kumfanya Elvis akubaliane na
wazo letu” akasema Doreen
“ Doreen unionavyo hapa
tayari nimekwisha fikiri sana na
ninatumai akili yangu imefikia
kiwango chake cha mwisho cha
kufikiri na bado sijapata jibu”
akasema kwa uchungu
Patricia.Doreen akamshika bega
na kumwambia
“ Patricia its too early to give
up.Nina hakika lazima tutapata
njia ya kufanya .Kitu cha msingi
ni kujaribu kutuliza akili na kuja na mpango mpya.Nina hakika
tutafanikiwa “ akasema Doreen
“ Doreen sina shaka nawe
hata kidogo najua uko tayari
kunisadia lakini tatizo liko kwa
Elvis.Ananipenda kupindukia na
hayuko tayari kufanya jambo
kama hili tunalolipanga.Suala la
kumuomba azae na mwanamke
mwingine kwake yeye ni sawa na
usaliti kwangu kwa hiyo hataki
kabisa
kulisikia.Nimechanganyikiwa
Doreen na sijui tutafanya nini na
ndugu za Elvis ndo hao wanadai
mtoto kila leo” akasema Patricia
“ Unaonaje endapo tutakaa
naye na kuongea naye kwa pamoja
kuhusiana na suala hili pengine
anaweza akatuelewa” Akasema
Doreen Elvis ni mtu mwenye
msimamo mkali sana na akisema
hapana katika jambo Fulani basi
huwa ni vigumu sana
kumbadili.Sina hakika kama hata
tukimueleza ukweli anaweza
akatuelewa.Mpango ule
ulioshindikana ulikuwa mzuri
sana” akasema Patricia
“ Pamoja na hayo Patricia ni
mapema mno kukata tamaa.Bado
kuna njia nyingi tu tunaweza
kufanya ili kumfanya Elvis
akubaliane nasi” Akasema Doreen
Patricia akamtazama na
kuonyesha wasi wasi
“ Unazungumzia njia gani
Doreen? Kama unazungumzia
masuala ya waganga mimi siko
tayari kwa hilo.Ni bora niendelee kuteseka kuliko kwenda kwa
waganga”
Doreen akacheka na kusema
“ Hapana Patricia.Mimi si
muumini wa masuala hayo na
tangu utoto wangu siamini kabisa
katika mambo hayo ya
waganga.Nilikuwa namaanisha
kutafuta njia nyingine za kuweza
kulifanikisha jambo hili hata kama
Elvis hataki kuliko kukata tamaa”
akasema Doreen
“ Hilo ndilo jambo la msingi
ambao tunapaswa kulifanya kwa
sasa.Ngoja kwanza niende
nikapumzishe kichwa ili nije na
wazo jipya.” Akasema Patricia
huku akinyanyua mkoba wake na
kupiga hatua kuelekea lilipo gari
lake Sikuwahi kuota kama siku
moja nitakuwa na wakati mgumu
kama nilionao hivi sasa. Kuna
wakati ninajuta hata kuolewa
.Ningekuwa peke yangu haya yote
yasingenitokea.Anyaway
ninampenda Elvis na nitalipigania
penzi letu kwa gharama zozote
zile” akawaza Patricia
********************
Ni shamba lenye ekari zaidi ya
kumi lililoko njekidogo ya jiji la dar
es salaam.Ndani ya shamba hilo
lililosheheni mazao mbalimbali
kulikuwa pia na mifugo kama vile
kuku,ng’ombe n.k.Kati kati ya
shamba lile kuwa kulikuwa na
jumba kubwa la kifahari la ghorofa
tatu.Hili ni shamba linalomilikiwa na Brigedia jenerali Frank
kwaju.Jioni hii ukimya mzito
ulitawala kulizunguka jumba
hili.Ni milio ya mifugo tu ndiyo
iliyokuwa ikisikika .Hakukuwa na
zile pita pita za kila siku za
wafanyakazi
Saa mbili na dakika tatu za
usiku,gari tatu zikawasili katika
geti la kuingilia shambani
hapo.Geti kubwa likafunguliwa na
walinzi na kisha gari zile
zikaikamata barabara iliyokuwa
inaelekea moja kwa moja katikati
ya shamba liliko jumba lile kubwa
lililozungukwa na ukuta mkubwa
na nyaya za umeme juu yake.Geti
likafunguliwa na gari zikaingia
Watu kumi wakashuka toka
katika zile gari wakiongozwa na
Brigedia jenereli Frank halafu wakalekea ndani katika ukumhi
wa siri wa mikutano ulioko ndani
ya jumba lile.Ukumbi tayari
ulikwisha andaliwa maalum kwa
ajili ya kikao hiki kizito
kinachotaratiwa kufanyika usiku
huu.Baada ya kama dakika
ishirini toka akina Frank wawasili
pale numbani,zikawasili gari mbili
na akashuka waziri mkuu mstaafu
Daud Sichoma akiwa
ameongozana na watu wengine
watano wakapokelewa na Brigedia
Frank na kupelekwa katika
ukumbi wa mikutano ambako
wajumbe wote waliokuwa
wakitakiwa katika kikao kile
walikwisha wasili na aliyekuwa
akisubiriwa ni Mheshimiwa Daudi
Sichoma na ujumbe wake.Mara tu
walipoingia katika chumba cha mikutano,watu wote wakasimama
kuonyesha heshima kwa wgeni
waliowasili.Daudi na ujumbe wake
wakaonyeshwa viti wakaketi na
bila kupoteza wakati mwenyekiti
wa kikao kile brigedia Frank
akafungua kikao.Kwanza alianza
kwa kufanya utambulisho.Baada
ya wajumbe kufahamiana kwa
majina na sehemu watokako
Frank akaendelea
“ Ndugu wajumbe nadhani ni
wakati sasa wa kuwatambulisha
wageni wetu wakuu waliotufanya
tukusanyike hapa usiki
huu.Wageni wetu watasimama na
kujitambulisha wao ni akina nani
na kisha tutaendelea na kile
kilichotuleta” akasema Frank na
kuwaomba wageni wale wawili wasimame mmoja mmoja na
kujitambulisha
“ naitwa Mustapha Al
jamal”akaanza kujitambulisha
mgeni wa kwanza
“ Mimi ni raia wa Iran na ni
mmiliki wa wa kampuni moja
kubwa ya mafuta katika
mashariki ya kati.Kwa sababu za
kiusalaam naomba nisiitaje
kampuni yangu hadi hapo
mbeleni” akamaliza
kujitambulisha ndugu Mustapha
na kumpa nafasi mwenzake
aliyeambatana naye
“ Mimi naitwa Alhafidh
Sadiq.Na mimi kama mwenzangu
aliyetangulia ni mmiliki wa
kampuni kadhaa kubwa za mafuta
katika eneo la mashariki ya
kati.Vile vile kama alivyofanya mwenzangu nisingependa na mimi
kuziweka wazi kampuni zangu”
akasema Alhafidh
“ Ahsanteni sana wageni wetu
kwa kujitambulisha.Sisi ni
wenzenu na tumefurahi sana
kuwa nanyi hapa kwa usiku
huu”akasema Frank akameza
mate na kuendelea
“ Ndugu wajumbe baada ya
kuwafahamu wagheni wetu
naomba sasa tuendelee na kikao
chetu.” Akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“ Wageni wetu hawa
wamekuja na jambo zito sana
ambalo utekelezaji wake
unatuhitaji sana sisi.Endapo
jambo hili likifanikiwa basi sisi
sote pamoja wao tutafaidika
sana.Kwa hiyo basi sitaki kuchukua muda mwingi kwani
muongeaji mkuu yupo na ndiye
atakayetueleza kila kitu.Karibu
ndugu Alhafidh ili uweze kutueleza
nini hasa kilichowaleta hapa
Tanzania” akasema Frank.Alhafidh
akaweka sawa koo lake akafungua
faili lililokuwa mbele yake
akaisoma karatasi ya kwanza kana
kwamba kuna mambo
anajikumbusha halafu akasema
“ Ndugu zangu ni furaha
kubwa kwetu kukutana nanyi
usiku huu.Kwa niaba ya
mwenzangu napenda kuchukua
nafasi hii kuwashukuru nyote kwa
kuacha shughuli zenu na kuja
kutusikiliza.Napenda
kuwahakikishia kwamba
hamtajutia kufika kwenu hapa
usiku huu kwani suala tulilowaitia hapa ni lenye manufaa makubwa
kwenu na kwetu pia.Brigedia
jeneral Frank ni rafiki yangu sana
wa muda mrefu.Tumefahamiana
katika shughuli zetu za kibiashara
na ninyi nyote aliowachagua
kuhuddhuria kikao hiki nina
imani ni watu makini na
anaowaakini hivyo natumaini
mazungumzo yetu yatakwenda
vizuri” Alhafidh akanyamza kidogo
akameza mate na kuendelea
“ Nadhani ninyi nyote hapa
mnafahamu hali halisi ya eneo
zima la masharaiki ya kati
inavyoendelea hivi sasa.Katika kila
taarifa ya habari inayotangazwa
duniani hakukosekani taarifa
kuhusiana na mashariki ya
kati.Lakini nini hasa kiini cha
machafuko yote katika eneo hili la mashariki ya kati?.Chanzo chote
cha machafuko ni nchi za
Marekani na washirika wake.Nchi
hizi za magharibi zimekuwa
zikiendesha chochoko dhidi ya
serikali za mashariki ya kati na
hivyo kusababisha machafuko
kusambaa katika eneo zima la
masharikiya kati.Lakini naomba
nyote mjiulize kwa nini mashariki
ya kati? Kwa nini nchi za
magharibi zinachochea migogoro
na mifarakano mashariki ya kati?
Jibu hapa ni jepesi sana.Ni kwa
sababu ya utajiri mkubwa wa
mafuta ulioko katika eneo
hili.Migogoro hii inapotokea
wanaofaidika ni Marekani na
washirika wake kwani hujitokeza
na kuingilia kati huku wakibeba
na kujiwekea akiba kubwa ya mafuta katika nchi zao huku
wakiwaacha maelfu ya watu wasio
na hatia wakiuana.Suala hili
limeamsha hasira na chuki kubwa
dhidi ya marekani na washirika
wake na ndiyo maana mnasikia
kila mara vinaibuka vikundi
mbalimbali vya kigaidi ambavo
vingi adui yake mkubwa ni
Marekani na washirika wake.Hii ni
sababu kubwa iliyopeleka
Marekani kuanza kujitoa taratibu
katika siasa za mashariki ya kati
na kuanza kupunguza utegemezi
wa mafuta toka mashariki ya kati
.Kwa hivi sasa marekani
imeongeza juhudi katika kuzalisha
mafuta ya ndani ikiwemo mafuta
yatokanayo na mimea
.Wamewekeza katika teknolojia
mpya ili watengeneze magari na mitambo visivyohitaji mafuta
mengi.” Alhafidh akanyamaza
kidogo halafu akaendelea.
“ Baada ya utafiti wa miaka
mingi kuhusiana na uwepo wa
mafuta na gesi katika bahari kuu
nchini Tanzania na kulitolewa
taarifa iliyoushangaza
ulimwengu.Kumegunduliwa kiasi
kikubwa cha mafuta nchini
Tanzania ambacho kinasemekena
ni kikubwa kuliko hata
kilekinachoweza kupatikaana eneo
zima la mashariki ya kati.Huu ni
ugunduzi mkubwa sana kuwahi
kufanyika katika miaka ya hivi
karibuni.Ugunduzi huu unaifanya
Tanzania kuingia katika
ulimwengu mpya kwani mataifa
yote makubwa hivi sasa
yameelekeza macho yao nchini Tanzania.Uchumi wa Tanzania
utapaa kwa kasi kubwa na ndani
ya muda mfupi ujao nchi yenu
itaingia katika nchi tajiri duniani”
Alhafidh akatulia na kuwatazama
wajumbe ambao wote walikuwa
wakitabasamu kutokana na taarifa
ile
“ Rais wa marekani
amemaliza ziara ya siku nne
nchini Tanzania ikiwa ni ziara
ndefu kuwahi kufanywa na rais
wa marekani katika taifa moja
husan haya ya bara la
Afrika.Ninathubutu kusema
kwamba hii imekua ni ziara yenye
mafanikio makubwa sana kwa
marekani.Mambomengi mazuri
yamefanyika katika ziara hiyo
ikiwa ni pamoja na kuzindua
miradi mikubwa ya nishati ,reli na maji,Pamoja na mambo hayo
makubwa huku watanzania walio
wengi wanaamni ni neema kubwa
wameipata lakini nataka mjiulize
kwa nini iwe sasa? Kwanini rais
wa marekani aitembelee Tanzania
sasa tena ikiwa ni ziara ndefu
kuwahi kufanywa na kiongozi
yoyote wa taifa la marekani katika
nchi yoyote ya afrika? Jibu hapa
ni rahisi tu.Nikwa sababu ya
neema kubwa ya mafuta na gesi
iliyogunduliwa Tanzania..Sababu
ya pili ni kujiimarisha kijeshi kwa
kujenga kambi yake hapa
Tanzania ili kuendeleza
mapambano dhidi ya wale wote
wenye kupambana na taifa hili
bila kuchoka na hasa vikundo vya
kigaidi kama vile
Alqaeda,alshabaab,Boko haram, n.k ambavyo vimekuwa
vikijimarisha sana kwa siku za
karibuni” Alhafish akanyamaza
kidogo na kuwatazama wajumbe
wa kikao kile ambao wote
walikuwa kimya kabisa
wakimsikiliza kisha akaendelea
“ Kama nilivyowafahamisha
kwamba ziara hii ya rais wa
Marekani nchini Tanzania ilikuwa
ni kwa sababu maalum zenye
manufaa kwa taifa hilo.Ukiacha
sababu za kiusalama ,kubwa
lililomleta hapa ni suala la mafuta
na gesi.Mtakumbuka awali
niliwaeleza kwamba kwa sasa
Marekani wanapunguza utegemezi
wa mafuta ya mashariki ya kati na
na kuifanya itegemee mafuta yake
ya ndani.Ugunduzi huu wa
kiwango kikubwa cha mafuta na gesi nchini Tanzania umeifanya
Marekani ianze kitolea macho
tanzania nchi ambayo imekuwa
ikipokea misaada mingi toka
Marekani.Katika ziara hii ya rais
wa Marekani kumesainiwa
mikataba kadhaa mikubwa baina
ya serikali ya tanzania na
wawekezaji wakubwa wa mafuta
na gesi toka Marekani.Katika
mikataba hiyo Serikali ya
Tanzania imeyaruhusu
makampuni makubwa ya
marekani kufanya uwekezaji
mkubwa katka sekta ya mafuta
na gesi Tanzania.Hii ina maana
moja kubwa kwamba makampuni
ya kimarekani ndiyo
yatakayoliongoza soko la mafuta
duniani .Marekani haitakuwa tena
na tatizo la mafuta na haitahitaji tena mafuta toka mashariki ya
kati.Washirika wa Marekani pia au
nchi zile kubwa zinazoongoza kwa
viwanda duniani hazitakuwwa
tena na wasi wasi kuhusiana na
suala la mafuta na gesi
,watahamia katika mafuta
yatokayo Tanzania.Bei ya mafuta
duniani itaporomoka na hali hii
itayalazimisha makampuni ya
mafuta ya mashariki ya kati
kupunguza bei ya mafuta ili
kuendana na bei itakayokuwepo
katika soko la dunia.Kushuka kwa
bei ya mafuta kwa nchi za
mashariki ya kati inamaanisha
kwamba hata uchumi wa nchi hizi
lazima utaporomoka kwa sababu
uchumi wao unategemea sana
biashara ya mafuta.Lengo kuu la
Marekani ni kuhakikisha kwamba uchumi wa nchi za mashariki ya
kati unazorota kutokana na
kudorora kwa biashara ya mafuta”
akanyamaza akanywa maji kidogo
kisha akaendelea.
“Nadhani hadi hivi sasa kuna
picha ambayo tayari mmekwisha
ipata kuhusiana na ziara ya rais
wa Mareani” akasema Alhafidhi na
wajumbe wote wakatikisa vichwa
ishara kwamba wanakubaliana
naye.Akatabasamu halafu
akaendelea
“ Suala hili limekuwa
likiumiza vichwa sana
makampuni makubwa ya mafuta
ya masharki ya Kati na hata
serikali zao kwa ujumla.Ni suala
linalohusu maslahi mapana ya
mataifa haya ambayo uchumi
wake unategemea mafuta.Hatutaki makampuni yetu yatetereke
kutokana na kuyumba kwa bei ya
mafuta katika soko la
dunia.Hatutaki uchumi wa
mataifa yetu uzorote kutokana na
kuyumba kwa bei ya mafuta .Vita
vya wenyewe kwa wenyewe katika
eneo zima la mashariki ya kati
vimesababisha chumi za mataifa
haya zilizokuwa zikikua kwa kasi
kuzozorota .Endapo litaatokea
tena baa hilo la kuporomoka kwa
bei ya mafuta mataifa haya
yatakuwa yakichungulia katika
lindi kubwa la umasikini kwani
chumi zao hazitaweza kustawi
kamwe.Ni kutokana na hali hiyo
kumekuwa na mazungumzo ya
kina kati ya serikali za mashariki
ya kati na makampuni makubwa
ya mafuta ya wazawa wa mashiriki ya kati.katika mazungumzo hayo
yote suala la Marekani kuendesha
sekta ya mafuta ya Tanzania
limepingwa vikali.Hatuko tayati na
hatutakuwa tayari kuiacha
Marekani itawale sekta hii nyeti
sana ambayo ndiyo hasa uchumi
wetu sisi watu wa mashariki ya
kati.Narudia tena kwamba hatuko
tayari na wala hatuwakuwa tayari
kuiacha Marekani itawale sekta ya
mafuta ya dunia.Kwa maana hiyo
basi tumefikia uamuzi wa
kuusimamisha na kuuzima kabisa
mpango wa marekani wa
kuidhibiti sekta ya mafuta
duniani.” Alhafidh akatoa
kitambaa na kujifuta jasho halafu
akanywa maji kidogona kuendelea.
“ Serikali ya Tanzania tayari
imekwisha sainiana mikataba mikubwa na makampuni ya
kimarekani na hivyoo suala hilo
kwa sasa lipo kisheria .Hakuna
namna tunayoweza kufanya ili
kutengua mikataba hiyo mikubwa
sana.Kuna njia moja tu ambayo
tunaweza kuifanya ili kulimaliza
suala hili” Alhafidh akanyamaza
na kuziangalia nyuso za wajumbe
waliokuwa kimya
wakimsikiliza.Akanyanyua glasi ya
maji na kupiga funda moja
akaiweka chini akatoa kitambaa
na kujifuta jasho lililokuwa
likimtoka usoni licha ya ukumbi
ule mdogo kuwa na kiyoyozi.Hii
ilitokaa na uzito wa suala
walilokuwa wakiliongelea
“ Ndugu wajumbe njia pekee
ya kuweza kulipatia ufumbuzi suala hili ni kwa kuiangusha
serikali iliyoko madarakani”
Kimya kizito kikatanda mle
ndani.Sura za wajumbe
zilionyesha mabadiliko ya
ghafla.Minong’ono ya chini kwa
chini ikasikika.Mara Daudi
Sichoma akasimama na
kumuelekezea macho Brigedia
Frank huku midomo yake
ikitetemeka
“ What is this Frank? Hiki
ndicho kitu cha muhimu
ulichoniitia? I cant believe this
!!!....akasema Daudi kwa ukali
.wajumbe wengine wanne
wakasimama wakionyesha
kustushwa na kauli ile.Hali
ilibadikika mle chumbani
ikamlazimu Brigedia Frank
asimame. Please calm down
guys.Nawaombeni mtulie na
tusikilizane.Mr David tafadhali
naomba ukae chini na
tusikilizane”akasema Frank na
wale wajumbe waliokuwa
wamesimama wakiongozwa na
Daudi Sichoma wakaketi na
ukimya ukatawala mle ndani
.Frank alipohakikisha wajumbe
wote wametulia kaendelea
“ Ninauona mstuko mkubwa
katika nyuso zenu.Nilitegemea
kitu kama hiki kutokea.Hii si
taarifa nyepesi hata kidogo.Ni
taarifa nzito na yenye kustusha
lakini nyote niliowachagua
kuhudhuria kikao hiki
ninauhakika mkubwa kwamba
hizi ni taarifa njema sana
kwenu.Naomba msiwe na jazba na twende taratibu tutaelewana”
akasema Frank
“Frank kuiangusha serikali si
suala rahisi hata kidogo kama
unavyodhani” akasema David
Sichoma .Frak akatabasamu na
kusema
“ Ninafahamu
unachokimaanisha David lakini
nina uhakika mkubwa hakuna
kitakacho
shindikana.Nime………”kabla
Frank hajaendelea zaidi Daudi
Sichoma akamkatisha
“Frank you know nothing
.Suala ulilolileta ni suala
lisilowezekana kabisa” akasema
Daudi
“ Unaweza kuwa sahihi David
kwamba sijawahi kuwa katika
serikali lakini ninafahamu kila kinachoendelea
serikalini.Ninawafahamu viongozi
wakubwa serikalini.Ninaifahamu
seriali nje na ndani.Daudi
Sichoma ninakufahamu vyema
umewahi kushika nyadhifa
mbalimbali za uongozi serikalini
na hatimaye ukafanikiwa kwa
waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania.Nafahamu
ndoto yako kubwa ilikuwa ni kuwa
rais wa Tanzania lakini kwa bahati
mbaya ndoto yako hiyo
haikuwezekana kutimia kwa
sababu watu ndani ya serikali
waliligundua hilo na hawakuwa
tayari kukuona ukishika nafasi ya
urais na ndiyo maana walianza
kukuandama kwa mambo mengi
na hatimaye kukuzushia kashfa
kubwa na ukaondolewa katika nafasi yako ya uwaziri
mkuu.Ninafahamu madai yale
yaliyotolewa dhidi yako kuhusiana
na kashfa ile hayakuwa ya kweli
na zilikuwa ni njama za kisisasa
na kuhakikisha unapotea kabisa
katika ulingo wa siasa.Lengo lao
limefanikiwa kwani wamefanikiwa
kabisa kukuondoa katika ulingo
wa siasa.Hausikiki tena viywani
mwa watu.Umekwisha sahaulika
kabisa na ndoto yako ya urais
imepotea.Najua unajitahidi sana
kutaka kujirudisha katika medani
za siasa lakini wabaya wako
hawataki kukupa tena
nafasi.Vikwazo vimekuwa vingi na
wamepambana hadi kuhakikisha
kwamba umaarufu wako
unapotea.This is your last chacne
to make your dream come true.Ni wakati wako wa kuitengeneza njia
ya kuingia katika lile jumba
jeupe.” Frank akanyamaza
akamtazama Daudi Sichoma
aliyekuwa kimya akimsikiliza
halafu akawageukia wajumbe
wengine
“Nyote niliowaita hapa
nafahamu ni wenye kuhitaji sana
nafasi za uongozi na mpango huu
wa kuiangusha serikali ndio
mpango pekee utakaowawezesha
na kuwahakikishia nafasi za
uongozi.Kuiangusha serikali
iliyoko madarakani ni jambo zito
ambalo haliwezi kufanywa na sisi
pekee yetuliomo humu chumbani
.Huu ni mchakato mrefu na
jumuishi nikimaanisha kwamba ni
mchakato unaohusisha watu
wengi lakini wenye lengo na nia moja.Sisi sote tulioko hapa ndio
tutakaoratibu mchakato mzima wa
mapinduzi haya.Naombeni ndugu
zangu msikate tamaa.Tunaweza
kulifanya jambo hili.Mkumbuke
pia tunayo sapoti ya kutosha toka
kwa washirika wetu katika suala
hili.Tayari zimekwisha tengwa
shilingi Trilioni sita kwa ajili tu ya
kufanikisha jambo hili.Pamoja na
fedha lakini washirika wetu
watatusaidia pia katika ila kitu
tunachokihitaji”akasema Frank na
kunyamaza tena akawatazama
wajumbe wale.daudi sichoma
akakohoa kidogo na kusema
“ Kidogo sasa ninaanza
kukuelewa Frank.Mpango huu si
mbaya kama nilivyokuwa
ninaufukiria isipokuwa ni mpango
mzito wenye kuhitaji mikakati mizito pia .Lazima tuvihusishe
vyombo vya ulinzi na usalama
hususani jeshi na idara ya
usalama wa taifa,wanasiasa na
wadau wengine watakaoonekana
kuhitajika.Mimi niko tayari
kushirikiana nanyi katika mpango
huu lakini kwa makubaliano
maalum” akasema Daudi Sichoma
“ Ahsante sana Daud kwa
maamuzi yako .Kwa kuwa bado
tuna mchakato mrefu mbele yetu
nina imani kwamba tutafikia
makubaliano unayohitaji”
akasema Frank na kuwageukia
wajumbe wengine
“ Ndugu zangu kati yenu
kuna yeyote mwenye mawazo
tofauti? Kuna yeyote mwenye
duku duku au maoni yoyote
kuhusiana na mpango huu? Akauliza Frank.Kabla mtu yeyote
hajajibu,simu ya Frank
ikaita,akastuka baada ya kuona
watu wote wanamtazama
“ Samahani ndugu zangu
kwa kutoizima simu yangu katika
kikao kizito kama hiki” akasema
Frank huku akitoa simu yake kwa
lengo la kuizima lakini mara tu
alipotazama jina la mpigaji
akastuka.Jina lilisomeka kama
hospitali Graca
“ Samahani jamani naomba
niipokee simu hii ni muhimu
sana” akasema Frank na kutoka
nje ya kile chumba
“Hallow” akasema Frank
“ Hallow Frank habari za Dar
es salaam? Ikasema sauti ya
upande wa pili