Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESDANT


Sehemu 42

Muda ulizidi
kuyoyoma,Meshack Jumbo,Steven
na Dr Philip walikuwa sebuleni
wakipata mvinyo wakisubiri Elvis
arejewe na fahamu kamili.
“Unadhani itamchukua muda
gani Elvis kurejewa na fahamu
zake kamili? Akauliza Meshack
Jumbo kisha akapiga funda moja la
mvinyo.
“Kama nilivyosema inaweza
kumchukua saa moja au mbili kurejewa na fahamu zake kamili
toka azinduke.Dawa ile
niliyomchoma ukiamka lazima
uwe kama umechanganyikiwa
ndiyo maana mliona akizungumza
maneno ya ajabu ajabu.Ile ni hali
ya kawaida” akasema Dr Philip
“Elvis anampenda sana
Patricia na ndiyo maana kitu cha
kwanza kukitamka mara tu
alipozinduka lilikua ni jina
lake.Inasikitisha kwamba mapenzi
haya mazito yamefika
mwisho.Walikuwa na ndoto nyingi
sana kuhusu maisha yao na
matarajio ya kufika hadi uzee
lakini ndoto hizo zote zimeyeyula”
akasema Meshack Jumbo
“Usiseme hivyo mzee.kwa
ninavyomfahamu Elvis atafanya
lolote lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha kwamba anakuwa na
Patricia” akasema Steven
“Si kwamba ninapenda
watengane bali kwa hali halisi
ilivyo inabidi iwe
hivyo.Itakapogundulika kwamba
Elvis hakufa itatuweka sote katika
matatizo makubwa.Mara tu
atakapokamilisha operesheni hii
salama itamlazimu kuondoka
nchini na kwenda nje ya nchi
kuanza maisha mapya”
“Hilo ni wazo zuri endapo
atakubali,lakini endapo akikubali
kwenda kuanza maisha mapya nje
ya nchi itakuwa vyema kama
tutafanya mpango aweze
kuungana na kuanza ,maisha
mapya na mke wake Patricia”
akashauri Steven
“Hilo si wazo baya ila
tutaangalia kama litawezekana na endapo…..” Meshack akanyamaza
baada ya simu ya Steven
kuita.Akatoka nje ili kuipokea
“Hallo Summer baby”
akasema Steven baada ya
kuipokea simu
“Mpenzi wangu vipi hali
yako?Kutwa nzima ya leo sijaisikia
sauti yako.kwa nini unanifanyia
hivi Steven? Au bado umekasirika
kuhusu lile suala uliloniambia
jana?Naomba usikasirike mpenzi
nimekwisha kuahidi kwamba
nitalifanyia kazi ila si kwa haraka
kama unavyotaka.Naomba nipe
muda ili niweze kuachana na yule
mzee taratibu.Niamini mpenzi
wangu kwani hata mimi nina hamu
sana ya kuwa na wewe pekee”
Samira akalalamika simuni.Steven
akatoa tabasamu pana baada ya
kuisikia sauti ile tamu Samahani summer baby kwa
kutokupigia simu toka
nilipoondoka asubuhi.Nilikuwa
katika kazi moja kubwa.Usijali
kuhusu lile suala nimekwisha
kuelewa na ninaamini utalifanyia
kazi kama ulivyoahidi.Uko wapi
mida hii?
“Niko hapa chumbani
nimejilaza kitandani mtupu kama
nilivyozaliwa.Nawashwa sana leo”
akasema Samira kwa sauti
laini.Steven akahisi mwili
unamsisimka kwa maneno yale ya
Samira na akahisi ikulu kunaanza
kufukuta
“Umeanza uchokozi wako
Samira” akasema Steven
“Si uchokozi mpenzi wangu,ni
kweli ninawashwa sana leo na
ninahitaji kukunwa.Ningependa
sana kama ningekunwa na mtu mwenye pumzi na ujuzi kama
wewe.Kitandani naweza kukuita
Simba.Mambo yako ni makubwana
huchoki”
“Usijali malaika wangu
ninakuja hapo kukuhudumia mara
tu nikimaliza hii kazi ninayoifanya
hapa” akasema Steven huku mono
wake wa kushoto ukiwa maeneo ya
ikulu ambako kulipoteza utulivu
“Hapana usije leo Steven.Yule
mzee amenipigia simu kaniambia
atakuja baadae”
Uso wa Steven ukabadilika
baada ya kusikia maneno yale
“Haya ndiyo mambo
nisiyoyataka.Kwa sababu ya huyu
mzee ninashindwa kuwa huru
kujivinjari na mpenzi wangu
ninavyotaka.Tutaishi hivi hadi lini
Samira?akauliza Steven kwa sauti
ya ukali kidogo Vumilia mpenzi wangu na
nitayamaliza haya
mambo.Tutakuwa pamoja na
utanipata kila pale
utakaponihitaji”
“Samira jambo hili
halijanipendeza hata kidogo”
“Nafahamu Steven lakini
nakuomba uwe mvumilivu na
utafika wakati ambao dunia nzima
itafahamu kuhusu mimi na wewe”
akasema Samira lakini Steven
hakujibu kitu,tayari alikwisha
pandwa na hasira
“Steven ! akaita Samira
“Tafadhali naomba
usikasirike mpenzi
wangu.Nakuahidi tena kwamba
nitalishughulikia hili suala na
litamalizika”akasema
Samira,Steven akakata simu Aaaagghh !!! akasema kwa
hasira akiwa amekunja ngumi
“Hii ndiyo taabu ya kuchangia
mwanamke na hawa
vigogo.Nafahamu Samira
ananipenda lakini tamaa ya fedha
inamfanya akubali kuwa na
mahusiano na hawa vigogo
wanaompa pesa nyingi na
kumfanya kutonipa thamani
yoyote.Mimi ni kama chaguo lake
la pili.Safari hii sintakubali
kushindwa na kigogo au gogo
lolote.Nitapambana kuhakikisha
Samira anakuwa wangu.Nataka
awe wangu peke yangu na si
kuchangia na hawa wazee wenye
pesa.Safari hii niko tayari uhai
unitoke au nitoe uhai wa mtu
katika kumpigania Samira.Kama ni
maisha mazuri anayoyataka
nitampatia.Nitafanya kazi kwa juhudi kubwa na kuhakikisha
ninakuwa na maisha bora na
uwezo wa kumtunza lakini awali
ya yote lazima nihakikishe hakuna
kigogo yoyote atakayemsogelea
Samira.Nitaanza na huyu waziri
mkuu mstaafu na kuhakikisha
kwamba anakaa mbali kabisa na
Samira.” Akawaza akiwa amewaka
hasira
“Si jambo jepesi kuamua
kupambana na hawa vigogo hasa
mtu mkubwa kama huyu ambaye
amewahi kuwa waziri mkuu,ana
nguvu kubwa kifedha na ana
uwezo pia wa kuniondoa pumzi
yangu muda wowote akipenda
lakini nguvu yake hiyo haiwezi
kuiogopesha.Nikiwa mafunzoni
nilifundishwa kumuogopa Mungu
pekee aliyenipa pumzi ya uhai na
si mwanadamu anayevuta hewa sawa na mimi hivyo sipaswi
kumuogopa.Nitapambana naye.Hii
ni vita kama ile ya David na Goliath
ambayo David aliibuka
mshindi.Wakati wa kunyanyaswa
na hawa vigogo umepita”
Steven akatolewa mawazoni
baada ya Meshack kutoka nje naye
akizugumza na simu na kumlazimu
Steven aingie ndani akaendelea
kukata mvinyo akiwa na hasira
Zilipita saa mbili toka Elvis
alipozinduka,fahamu zake
zikarejea sawa sawa.Graca ambaye
alikuwa na Elvis chumbani aliwapa
taarifa akina Meshack kwamba
hali ya Elvis imeimarika na sasa
anaweza akatambua vitu.Wote
wakatoka pale sebuleni na kuingia
chumbani
“Elvis !!akaita Dr Philip.Elvis
akafumbua macho na kumtazama Mimi ni nani? Akauliza.Elvis
akamtazama kisha kwa sauti
dhaifu akajibu
“Dr Philip” akajibu Elvis na
nyuso za watu wote mle chumbani
zikachanua kwa tabasamu
“Huyu naye unaweza
ukamtambua? Akauliza Dr Philip
akimuelekezea kidole Meshack
Jumbo
“Huyo ni mkurugenzi Meshack
Jumbo”
“Na huyu je ? akamuonyeshea
Steven
“Steven Kinko”
“Huyu naye unamfahamu?
“Huyu ni Graca”
“Oh thank you Lord !!
akasema Meshack Jumbo na watu
wote wakakumbatiana kwa furaha
“We need champage in here to
celebrate ! akasema Steven ambaye hasira zake zote alizokuwa
nazo baada ya kuzungumza na
Samira zilipoteza
Dr Philip akamuagiza Graca
ampatie Elvis uji aliouandaa kisha
akaenda kuungana na Meshack
Jumbo na Steven waliokuwa
sebuleni wakifurahia kwa Elvs
kurejewa na fahamu zake.Chupa
tatu za mvinyo zilikuwa mezani
wakinywa kwa furaha huku
wakipongezana
“We sent the man to the moon
and brought him back !.Let”s drink
for that !! akasema Steven
aliyeonekana kufurahi kupita
wengine wote.
“We did it ! akasema Dr Philip
huku akigonganisha glasi na
wenzake
“Katika kipindi chote cha
maisha yangu hii ni mara yangu ya kwanza kughushi kifo cha mtu na
mpango ukafanikiwa.Siwafichi
vijana wangu nilikuwa na wasi
wasi ambao siwezi
kuuelezea.Nawashukuru mno kwa
kazi kubwa mliyoifanya.Hili ni
jambo zito lakini kwa uchache
wenu mmeweza kulifanikisha..”
Simu ya Meshack ikaita akainuka
na kutoka nje akaenda
kuipokea.Baada ya dakika kadhaa
akarejea ndani akamalizia mvinyo
uliokuwamo katika glasi na
kusema
“Vijana baada ya kuwa na
uhakika kwamba zoezi
limekwenda vizuri na kwa
mafanikio ni wakati wangu sasa
kwenda kupumzika.My wife needs
me.Hata ninyi pia mnahitaji
kupumzika.Siku hizi mbili
zimekuwa ni zenye changamoto kubwa sana kwangu na sijawahi
kuwa na siku ngumu kama hizi
katika maisha yangu.Tukutane
kesho kwa ajili ya mikakati mipya”
akasema Meshack Jumbo
“Mzee kuna jambo ulinieleza
kuhusiana na mtu wa
kumshughulikia.Mpango huo
umeahirishwa?Steven akauliza
huku naye akisimama
“Tutazungumza kesho.Mambo
yaliyofanyika leo yanatosha na
twendeni tukapumzishe vichwa
vyetu.Kesho tutakutana hapa na
tutazungumza” akasema Meshack
Jumbo kisha wote wakaelekea
chumbani kwa Mathew
“Mathew unajisikiaje sasa hivi
? Meshack akauliza
“Najisikia vizuri isipokuwa
kichwa kinauma sana” “Pole.Hicho ni kitu kidogo
kitapona.Dr Philip ataendelea
kufuatilia hali yako kwa
ukaribu.Mimi nimekuja kukuaga
ninakwenda
kupumzika.Tutaonana hapa
kesho.Natumai hadi hiyo kesho
hali yako itakuwa bora zaidi”
“Ahsante sana mzee.Vipi
kuhusu Patricia?
“Ameumia lakini atakuwa
sawa.She’s strong woman she’ll be
fine” akasema Meshcak Jumbo na
Elvis akafumba macho alihisi
uchungu mwingi.Meshack
akawaaga wote mle chumbani na
kuondoka.Steven akaenda
sebuleni akaendelea kunywa
mvinyo.
“Napatwa na hasira kali
nivutapo picha na kuona Samira
amekumbatiwa na yule mzee,wakibusiana na kupeana
maneno matamu ya mahaba,kisha
yule mzee anamvua Samira nguo
ya ndani na kumuacha mtupu na
kisha anaanza kumchezea
atakavyo.Aaaggghhh!!!!
Hasira zikazidi kumpanda
Steven baada ya mawazo yale
kumjia.
“Natamani niende sasa hivi
nikamtoe yule mzee kifuani kwa
Samira na kumuonya asimsogelee
tena lakini Samira
hatafurahi.Ngoja niendelee
kuvumilia kama alivyonitaka ili
nione kama atatimiza ahadi yake
ya kuachana na yule mzee.Endapo
atashindwa kuachana naye I swear
I’ll kill him.Samira is mine and will
always be mine !! akaendelea
kuwaza ******************
Mshale wa saa ulionyesha ni
saa tano na dakika nane za
usiku.Waziri mkuu David Sichoma
alikuwa katika jakuzi nyumbani
kwa Samira.Alifika hapo baada ya
kumaliza mazungumzo na
makamu wa rais Dr Shafi
Omar.Mke wake alikuwa safari nje
ya mkoa hivyo alikuwa na nafasi
na uhuru wa kufanya atakavyo
“Darling” akaita Samira kwa
sauti laini aliyoibana zaidi na
kuzidi kumpagawisha David
“Unasemaje Samira?
Samira akamsogelea karibu
zaidi na kwa kutumia mkono wake
akaanza kuchezea ikulu na David
akatoa mguno Unasemaje Samira? David
akauliza akiwa amefumba macho
yake kwa raha alizokuwa akihisi
pale Samira alipokuwa
anazichezea nyeti zake
“Unasemaje Samira? David
akauliza tena
“Ninaye binamu yangu
anahitaji msaada”
“Msaada gani anahitaji?
“Anahitaji mtaji wa
biashara.Alipatwa na matatizo
akafungwa gerezani na sasa tayari
amemaliza kifungo chake hivyo
anahitaji kuanza maisha mapya”
akasema Samira akiendelea
kufanya utundu wake ikulu kwa
David na kumfanya ahisi raha ya
ajabu
“Anataka kufanya biashara
gani? Anataka kuanzisha biashara
ya kuuza magari yaliyotumika
kutoka Japan”
“Oh No !Hiyo si biashara
nzuri.Kwa hivi sasa serikali iko
katika mchakato wa kupiga
marufuku uingizwaji wa magari
yaliyotumika hapa nchini.Labda
afungue duka kubwa la kuuza
pikipiki na vipuri vyake.Hii ni
biashara nzuri sana kwa sasa
kwani vijana wengi wamejiajri
katika boda boda.Baadae baada ya
mchakato wangu wa urais
kukamilika nitamuongezea mtaji
na atafungua duka la magari
mapya kabisa.Nataka ufurahi
Samira” akasema David na Samira
akamwagia mabusu mfululizo
“Ndiyo maana nakupenda
sana mpenzi wangu.Kila siku
unanifanyia mambo makubwa ambayo hakuna mwanaume
anaweza akanifanyia.Ahsante sana
David” akasema Samira na
kumuongezea mabusu
“Ni wajibu wangu
kukuhudumia kwa sababu ni wewe
pekee unayenifanya nijione kama
vile nina miaka ishirini kwa
mambo makubwa
unayonifanyia.Vile vile nataka
nikutimizie kila unachokihitaji ili
asitokee mtu mwingine
akakurubuni kwa kitu
chochote.Nimekwisha kupa ruhusa
endapo kuna kitu chochote
unakihitaji usisite kunieleza na
mimi nitakupatia ila sitaki kusikia
una mwanaume mwingine.Mimi
nina wivu mno na pindi
nikigundua kwamba una
mwanaume mwingine ninaapa
nitamuondoa haraka sana duniani.Wewe ni wangu peke
yangu na sitaki mtu mwingine
yeyote akusogelee.Najua wewe ni
mzuri na uzuri wako ni kama ua
lenye harufu nzuli linalowavutia
nyuki wengi kulifuata.Uzuri wako
unawavuta wanaume wengi hivyo
nakutahadharisha kwamba uwe
makini sana katika hilo
suala.Nitakufanyia mambo mengi
makubwa hata yale ambayo
hukuwahi kuyafikiria au hata
kuyaota.Nilikueleza kwamba niko
katika mchakato wa urais na pindi
nikifanikiwa nitakuweka katika
nafasi ya juu mno.Utaishi zaidi ya
anavyoishi mwana malkia.Utaishi
katika kasri kubwa utabadili
magari ya kila aina ,utavaa
dhahabu na kila aina ya vito katika
mwili wako.Itoshe kusema tu
kwamba nitakuweka katika nafasi ya juu mno ila nikigundua kwamba
una mwanaume mwingine haya
yote utayakosa” akasema
David.Samira akambusu na
kuendelea kumchezea nyeti
“Hivi ni mwanamke wa aina
gani atakayethubutu kuwa na
mwanaume wa pembeni wakati
akihudumiwa namna hii?Sijawahi
omba chochote kwako
nikakosa.Nikikuomba kumi
unanipa mia hivyo sina sababu
yoyote ya kunifanya niwe na
mwanaume mwingine.Wewe
pekee unanitosha hivyo nakuomba
usiwe na wasi wasi wowote na
mimi.Kuwa na amani moyoni
mwako.Siwezi katu
kuchepuka.Wewe ni wangu daima
na ningefurahi kama siku moja
tungefunga hata ndoa” akasema Samira na kumfanya David atoe
kicheko
“Mbona unanicheka David?
Nimeongea kitu kibaya?
“Hata mimi ningefurahi sana
kama ingekuwa hivyo lakini kwa
sisi wakristo,ndoa ni moja
tu.Kinachoweza kuwatenganisha
ni kifo pekee.Mke wangu
niliyefunga naye ndoa bado yuko
hai na tunapendana.Japokuwa kwa
sasa umri umekwenda na hawezi
mapigo kama yako lakini bado
namheshimu sana na katu siwezi
kumuacha.Yeye ana mchango
mkubwa kwa mimi kufika hapa
nilipofika.Tutaendelea na
mahusiano yetu ya siri na mimi
nitakutunza kama mke mdogo”
akasema David kisha wakatoka
majini wakahamia chumbani na
mtanange mkali ukaanza.Samira aliukamata usukani na kukaa
juu.Alifanya mambo ya kipekee
kabisa na kumfanya David licha ya
utu uzima wake kuongea maneno
asiyoyafahamu.Mtanange ukiwa
umeshika kasi simu ya David
ikaanza kuita.David akastuka na
kumtaka Samira ampatie simu
yake
“Achana na simu
mpenzi,utazungumza nao
tutakapomaliza starehe zetu”
“Hapana Samira,naomba
nipatie simu yangu ninategemea
simu ya muhimu sana” akasema
David na Samira akaichukua simu
ya David akatazama mpigaji jina
liliandika Elizabeth,kisha akampa
David simu yake.Mara tu David
alipotazama jina la mpigaji
akastuka sana akashindwa kuipokea na ikulu kukasinyaa
ghafla.
“Mbona hupokei simu?
Akauliza Samira .David hakujibu
kitu akainuka taratibu akajifunga
taulo na kutoka akaenda nje.
“What’s wrong with
him?Mbona amebadilika ghafla?
Samira akajiuliza.
David akazitafuta namba zile
za Elizabeth na kupiga
“hallo David” ikasema sauti ya
upande wa pili.David akavuta
pumzi ndefu na kusema
“Hallo madam Elizabeth”
akasema David na kwa mbali sauti
yake ilikuwa na kitetemeshi
“David,how’re you?
Hatujaonana siku nyingi”
“Naendelea vyema madam
Elizabeth” akajibu David “David relax my baby.Naisikia
sauti yako ikitetemeka”
“Madam Elizabeth lazima
niogope kwanza sikutegemea
kama uko hapa nchini pili kila
unapopiga simu lazima kuna
jambo”
“Usiogope David.Hatujaonana
muda mrefu nimeona
nikukaribishe nyumbani kwangu
kwa chakula cha mchana kesho”
“Ahsante madam Elizabeth
nitafika bila kukosa” akasema
David na simu ikakatwa.Hata
baada ya simu kukatwa bado
David aliendelea kusimama huku
jasho likimtiririka
“Nimestuka mno kwa
Elizabeth kunipigia simu hasa
muda kama huu.Kuna jambo gani
safari hii?nafahamu kabisa
kwamba mwaliko wa chakula cha mchana ni kigezo tu lazima kuna
jambo lingine.Huyu mama mbona
anataka kunichanganya akili
yangu hasa kwa muda huu ambao
kuna mambo mazito yananikabili”
akawaza David halafu akarejea
ndani.Samira akastuka kwa namna
David alivyoloa jasho
“Darling kuna tatizo gani?
Mbona umebadilika sana baada ya
kuzungumza na ile simu?Who is
Elizabeth? Akauliza Samira
“Samira I have to go! Akasema
David huku akianza kuvaa nguo na
kumshangaza Samira
“Elizabeth ni mke wako?
Akauliza Samira lakini David
hakujibu kitu akaendelea kuvaa
nguo
“Answer me David,who is she?
Is she your wife? Akauliza Samira
“She’s no one” akajibu David No one?!
“Samira tafadhali sihitaji
maswali” akasema David huku
akimalizia kufunga mkanda wa
suruali yake na kumbusu samira
kisha akaondoka.Usiku huu
hakuwa na dereva aliendesha gari
mwenyewe
“Huyu Elizabeth ni nani? Ni
mke wa David?Ninahisi ni mke
wake kwani alibadilika ghafla
baada ya kuliona jina lile katika
kioo cha simu na cha kushangaza
zaidi hata ikulu kukasinyaa ghafla
jambo ambalo halijawahi kutokea
hata mara moja.Inaonekana David
anamuogopa mno mke wake na
ndiyo maana akaogopa namna
ile.Kuna ulazima wa kufanya
uchunguzi na kufahamu kama
huyo Elizabeth ndiye mke wa
David ili niweze kujiepusha naye kwani anaonekana ni mwanamke
mkorofi sana na akigundua
kwamba ninamuibia mume wake
ninaweza kufanywa kitu kibaya
.Niliona woga wa David
aliposhindwa hata kupokea
simu.Siku zote ninapokuwa na
David huwa ananing’ang’ania
kama amepakwa gundi lakini leo
baada ya kuzungumza na Elizabeth
hakutaka tena kuendelea kukaa
hapa alinyong’onyea mno na
kuondoka.Nimeshangaa sana”
akawaza Samira na kuingia bafuni
akajimwagia maji na kujilaza
kitandani.
******************

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom