I DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 52
Dr Philip alipomaliza kazi
yake aliaga na kuondoka kwani
alikuwa na kazi nyingine ya
upasuaji kwa usiku ule katika hospitali ambako hufanyia kazi
kwa muda wa ziada.Meshack
Jumbo naye alikuwa amechoka
sana hivyo naye akaomba andoke
kwenda kupumzika
"Umefanya kazi nzuri sana leo
Steve" akasema Elvis
"Ahsante.Ni muda mrefu
nilikuwa nimezikosa kadhia kama
hizi lakini taratibu nitarejea katika
ubora wangu"
"Good.Hatuna muda wa
kulala, ni wakati wa kuanza
kumchunguza Vicky tufahamu
kwa nini alimuua Pascal.Baadae
atakapoamka tutamfanyia
mahojiano lakini kwa sasa
tuchunguze kila kitu
chake.Tuchunguze simu yake
anawasiliana na akina nani na tuchunguze kila alichonacho hata
kama ni kidogo kiasi gani
kitatusaidia kuweza kumfahamu
vizuri" akasema Elvis.Steve
akaufungua mkoba wa Vicky na
kumwaga mezani kila
kilichokuwemo katika mkoba wa
Vicky na kukuta kuna vitu
vichache kama kadi za
benki,heleni mikufu na vitu
vingine vidogo vidogo vya
urembo.
"Hakuna chochote cha maana
hapa" akasema Steve
"Hizi kadi za benki
tutazichunguza pia na kufahamu
kuna kiasi gani katika akaunti
yake na kujua fedha hizo
anapokea kutoka wapi.Zinaweza
kutusaidia kuufahamu mtandao wake.Kwa sasa tuichunguze simu
yake ili tuone kama kuna kitu
tunaweza kukipata" akasema Elvis
na simu yake ikaingizwa katika
kifaa fulani ambacho
kiliunganishwa na kompyuta
kisha wakaanza
kuchunguza.Baada ya dakika
kadhaa za uchunguzi Elvis
akasema
"Hakuna kitu kikubwa cha
kutuwezesha kumfahamu Vicky
kwani inaonekana simu hii
anaitumia sana kibiashara.Kuna
kitu kimoja ambacho kinaweza
kutusadia kumfungua na akatupa
taarifa zozote tuzitakazo.Ni kwa
kuitumia familia yake.Tuchunguze
tujue kama ana watoto au ndugu
au hata wazazi wake na tukimpatammoja wao basi atakuwa tayari
kutueleza kila kile tunachokihitaji.
Kuna picha fulani nimeziona
humu katika simu ambazo
zinamuonyesha Vicky akiwa na
msichana fulani wamefanana
sana.Fungua faili la picha"
akasema Elvis na Steve
akalifungua faili la picha na ndani
ya faili hilo kulikuwa na faili
lingine limeandikwa
W.Bday.Wakalifungua faili hilo
ambalo lilikuwa na picha zaidi ya
mia moja.Walipitia picha hizo
kisha Elvis akasema
"Keki ina maandishi
yanasomeka Happy birthday
Winnie ikimaanisha msichana
huyu ambaye alikuwa
anasherehekea siku yake ya kuzaliwa anaitwaWinnie.Picha
nyingi zinaonyesha Winnie akiwa
na Vicky.Wawili hawa wana
ukaribu mkubwa.Inawezekana ni
mtu na mdogo wake au ni ndugu"
"Nakubaliana nawe Elvis
kuna uwezekano wawili hawa
wakawa ni ndugu kwani hata sura
zao zinafanana japo Vicky
amekuwa mweupe sana."akasema
Steve.Elvis akaichukua picha moja
ya Winnie akaikata kiufundi na
kubakisha sehemu ya kichwa
pekee halafu akaiweka picha ile
katika programu ya kufananisha
picha.Picha zilipita haraka haraka
sana na baada ya nusu dakika
programu ikasimama na
kuonyesha majibu.Ilitoa picha
mbali mbali za Winnie ambazoalikuwa ameziweka katika
mitandao
"Wasichana hawa huwa
wanaweka taarifa zao nyingi
katika mitandao na wakati
mwingine hata namba zao za
simu." akasema Elvis na
kuufungua ukurasa wa facebook
wa Winnie na kuanza kupitia
taarifa zake.Jina lake katika
ukurasa huu liliandikwa queen
Winnie.Aliweka picha nyingi na
katika taarifa zake aliweka pia
namba zake za simu na mwaka
aliozaliwa.Alikuwa na miaka
ishirini na nne.
"Kama watakuwa na
mahusiano basi lazima huyu
atakuwa ni mdogo wake kwani
kwa umri wa Vicky huyu Winnie hawezi kuwa mwanae." akasema
Steve
"Tunachotakiwa kukifanya ni
kufahamu mahala alipo na
kumpata usiku huu huu na
kumuweka tayari ili Vicky
atakapoleta ukaidi au ugumu wa
kutupa taarifa basi tumtumie
huyu Winnie.Mpigie simu kwa
kutumia simu ya Vicky na jifanye
wewe ni daktari.Mdanganye kuwa
Vicky amepata ajali na anataka
kumuona halafu muulize mahala
aliko ili umfuate.Ataamini kuwa ni
kweli na tutamfuata kwenda
kumchukua" akasema Elvis na bila
kupoteza muda akaziandika
namba za simu za Winnie
walizozitoa mtandaoni na baada
ya kupiga likatokea jina Winnie.Simu ikaita na kukatika
bila kupokelewa akapiga tena na
safari hii ikapokelewa
"hallow dada samahani kwa
kuchelewa kupokea simu nilikuwa
usingizini"
"Hallow Winie"akasema Steve
"Wewe ni nani? akauliza
Winnie kwa mstuko mkubwa
"Naitwa Dr Bakari kutoka
hospitali ya
Samaria.Nimeelekezwa na dada
yako anaitwa Vicky kuwa
nikupigie simu.Amepata ajali
ndogo ya gari na amelazwa hapa
hospitalini kwetu"
"Amepata ajali?! Winnie
akastuka
"Ndiyo amalazwa hapa
hospitaliOh my God ! anaendeleaje?
"Ni mzima kabisa amepata
majeraha kidogo na tumemlaza
kwa muda hapa hospitali "
"Thank you God! akasema
Winnie na kushusha pumzi
"Vicky amenituma kuwa
anahitaji kukuona kuna mambo
anataka akuelekeze ya muhimu
sana.Uko wapi mida hii?
"Niko nyumbani"
"Nielekeze nyumba yenu ilipo
ili nikufuate hapo mara moja"
akasema Steve na Winnie
akamuelekeza kila kitu
"Vizuri Winnie ninakuja hapo
sasa hivi kukuchukua ili uje
umtazame dada yako.Kingine
anachosisitiza ni kwamba usimweleze mtu yeyote kuwa
amepata ajali hadi mtakapoonana”
"Dr Bakari una hakika dada
yangu ni mzima?
"Vick ni mzima kabisa
usihofu.Amepata majeraha
madogo madogo kama
nilivyokueleza.Jiandae ninakuja
hapo kukuchukua sasa hivi"
akasema Steve na kukata simu
"Umefanya vizuri.Sasa wewe
nenda kamchukue Winnie mimi
nitabaki hapa nataka nianze
kumuhoji Vicky ili hadi
utakaporejea kama hajasema
chochote basi tujue namna ya
kufanya"akasema Elvis na bila
kupoteza muda Steve akaondoka
kwenda kumchukua Winnie.Elvis
akaelekea katika chumba alimoVicky akaufungua mlango na
kumkuta Vcky amekaa
kitandani.Elvis akavuta kiti karibu
yake na kuketi wakatazamana
halafu akasema
"Unajisikiaje Vicky? akauliza
lakini Vicky hakumjibu kitu
"Unaendelaje Vicky? akauliza
tena
"Unataka niendelee vipi?
Vicky akauliza kwa ukali
"Usiwe na hasira Vicky.Kuwa
mtulivu na kila kitu kitakwenda
vizuri.We're not bad people.I'm
sorry for what happened
hatukuwa na lengo la kukuumiza
kwani wewe si yule tuliyekuwa
tunakuhitaji lakini nililazimika
kukupiga risasi ya mkono kufuatia
kitendo ulichokifanya ambacho hakuna kati yetu aliyetegemea
kama ungekifanya" akasema Elvis
na kutulia kidogo akamtazama
Vicky aliyekuwa anamtazama kwa
macho yaliyojaa hasira
"Kufuatia kiendo kile
ulichokifanya nina maswali
machache ambayo ninataka
unijibu kwa ufasaha
mkubwa.Endapo utanijibu vizuri
utanishawishi nikuachie huru
uende zako lakini endapo
utakuwa kiburi na kukataa
kunijibu maswaliyangu utanipa
hasira na utakuwa ni mwisho
wako wa kuliona jua
.Nitakupeleka kuishi mahala
penye giza hadi kifo
chako.Utauona mwanga mara tatu
tu kwa siku na utafungwa miguu na mikono kwa minyororo.Sitaki
nikufanyie hivyo mrembo kama
wewe hivyo nakuomba unijibu
maswali yangu"
Vicky akabetua midomo na
kusonya kwa dharau
"Wewe kama nani wa
kunitaka mimi nikujibu maswali
yako? Hunijui na bado unataka
nikujibu maswali.Save your time
you idiot mimi siwezi kukujibu
mtu kama wewe! akasema Vicky
kwa dharau
"Huyu mwanamke ni mtu
mjanja sana na anajibu hivi kwa
ajili ya kunipandisha hasira kwani
anajua mtu ukiwa na hasira
huwezi kufikiri sawa sawa na
anaweza akapata upenyo wa
kutoroka" akawaza Elvis Kwa nini ulimuua Pascal?
Elvis akauliza.
"Sina muda mchafu wa
kukujibu chawa kama
wewe.Wewe ndiye unayetakiwa
unijibu kwa nini unamuhitaji
Pascal? akauliza Vicky na
kumfanya Elvis ainuke kitini
akamsogelea Vicky
"Nisikilze vizuri Vicky kwa
sasa wewe hauna uwezo wowote
wa kuniuliza maswali.Nakuomba
usiendelee kupoteza muda wangu
nijibu maswali yangu
ninayokuuliza ama sivyo
utanilazimisha nitumie nguvu
jambo ambalo silitaki" akasema
Elvis
"Nimekwisha kueleza
kwamba sina muda wa kujibu swali la taka taka kama
wewe.Huna uwezo wa kunihoji
mimi na kitendo hiki
ulichokifanya cha kunishikilia na
kuniweka mimi hapa utakijutia
kwa maisha yako yote hadi siku
unaingia kaburini" akasema Vicky
kwa kujiamini sana.Hakuonekana
kuwa na wasi wasi hata chembe.
"Vicky narudia tena
kukusisitiza kwamba sitaki
kutumia nguvu kukulazimisha
unijibu mawali yangu.Naomba
unijibu bila jeuri na tutakwenda
sawa lakini endapo utakuwa
kiburi utanibadilisha na nitakuwa
mtu mwingine kabisa.Tafadhali
nakuomba usinilazimishe
nikabadilika utaomba ugeuke
hewa upotee.Jibu swali langu tafadhali"akasema Elvis na Vicky
akatoa kicheko kidogo cha dharau
na kusema
" Sikiliza handsome boy mimi
sitishiki na hayo maneno
yako.Sikulazimishi unifungue
lakini utajutia kilichokufanya
ukanileta hapa."
"Soon that handsome will be
a monster please dont push me to
change into a monster" akasema
Elvis
"I'm a monster too.Monsters
dont hurt each other"akasema
Vicky huku akicheka
"Please dont try me Vicky"
akasema Elvis
"Go to hell handsome"
akasema Vicky na Elvis
akamtazama kwa hasira. Umeniudhi sana Vicky kwa
kiburi chako.Endelea kupumzika
nitarudi tena baadae kidogo na
nina hakika wakati huo
tutaelewana" akasema Elvis na
kutoka mle chumbani akiwa
amefura kwa hasira
"Who is this woman?Kwa nini
anajiamini namna hii? Vicky huyu
ni tofauti na yule Vicky
kahaba.Kuna mambo mengi ya
kufahamu kutoka kwa huyu
mwanamke.Kabla ya jogoo kuwika
alfajiri lazima tutakuwa
tumekwishamfahamu ni
nani.Ngoja nimsubri Steve arejee
na mdogo wake na ndipo
atakapotufahamu sisi ni akina
nani" akawaza Elvis na kuingia chumbani kwake na kuanza
kuandaa zana zake za kutesea
***************
Steve aliwasili katika nyumba
aliyoelekezwa na Winnie.Lilikuwa
ni jumba kubwa la
ghorofa.Alipokaribia getini
akamulikwa na tochi yenye
mwanga mkali na mlinzi
,akapunguza mwendo na
kusimamisha gari.Mlinzi yule
aliyekuwa amevaa sare za
kampuni ya ulinzi na aliyekuwa na
bunduki mkononi akalisogelea
gari la Steve ambaye alishusha
kioo na kumsabahi yule mlinzi
kwa adabu. Steve akajitambulisha
kwamba ni mgeni wa Winnie na ili kumthibitishia mlinzi yule
analolisema ni la kweli akachukua
simu yake na kumpigia Winnie
akamjulisha kuwa tayari
amekwisha fika yuko pale
nje.Mlinzi yule hakuamini alikuwa
amesimama imara ameshika
bunduki yake hadi aliposikia geti
likifunguliwa na Winnie akatoka.
"Aunt huyu ni mgeni
wako?akauliza
"Ndiyo" akajibu Winnie na
Steve aliyekuwa amevalia nadhifu
akashuka akamfungulia Winnie
mlango wa gari akaingia kisha
wakaondoka
"Nimestuka sana kwa taarifa
ulizonipa kuhusu dada
Vicky.Anaendeleaje?Kama nilivyokueleza simuni
kwamba hali yake ni nzuri
anaendelea vyema
kabisa.Amepata majeraha
madogomadogo"
"Alikuwa amelewa?
"Hapana hakuwa
amelewa.Kwa mujibu wa maelezo
yake ni kwamba yeye ndiye
aliyegongwa na gari
lingine.Usihofu Winnie hali ya
dada yako ni nzuri na kesho
asubuhi ataruhusiwa kutoka
hospitali" akasema Steve na
ukimya ukatanda garini
"Vicky ni nani kwako?
Akauliza Steve
"Vicky ni dada yangu.Wazazi
wetu wamekwisha fariki na yeye ndiye baba na mama
yangu.Tumezaliwa wawili tu"
"Oh nilihisi hivyo kwani
amenisisitiza sana akitaka
nikupeleke akuone ili aweze
kukutoa hofu kwani alihisi
ungestuka sana kama ungezipata
taarifa kutoka kwa watu wengine"
akasema Steve na safari
ikaendelea kimya
kimya.Barabarani magari
hayakuwa mengi sana usiku huu
"Unafanya kazi gani Winnie?
"Mimi bado
mwanafunzi.Ninasomea udaktari
niko mwaka wa tatu"
"Hongera sana" akasema
Steve na hakutaka tena
mazungumzo akihofu pengine
Winnie angeweza kumuuliza maswali ambayo angeshindwa
kuyajibu
"Winnie tunapitia sehemu
fulani kuna dawa nataka
kuzichukua ili twende nazo
hospitali" akasema Steve
"hakuna tatizo" akajibu
Winnie.Steve akaliongoza gari
kuelekea katika makazi yao
"She's very pretty.Hapa
ametoka kuamka na anaonekana
mremo hivi je akijiremba si
atakuwa malaika.Ana uzuri wa
kipekee sana lakini uzuri wote
huu unakwenda kuharibika
.Mpaka kesho asubuhi hatakuwa
anatazamika labda dada yake
aamue kutueleza ukweli.Wakati
mwingine inaumiza kuwaumiza
watu wasio na hatia yoyote lakini hakuna namna lazima tutumie kila
aina ya mbinu hadi Vicky
afunguke." akawaza Steve na
kuanza kukumbuka mambo
aliyoyafanya na Vicky usiku ule
kule hotelini
"Vicky tayari alikwisha
ukubali mziki wangu.Nilimfanyia
mambo makubwa ndani ya kipindi
kifupi na akachanganyikiwa hadi
kukiri kwamba hajakutana na
mwanaume ninayejua mapenzi
kama mimi.Hakujua kama
nilikuwa kazini.Aliamini kweli
mimi ni bilionea kutoka nje ya
nchi.Shukrani za kipekee
zimwendee Samira ambaye
aliandaa mpango huu hadi
nikafanikiwa kukutana na Vicky
japo nimevunja ahadi niliyompa kwamba sintafanya mapenzi na
Vicky.Ningewezaje kumuacha
malaika yule hivi hivi? "akawaza
Steve na kwa mbali akatabasamu
"Pamoja na uzuri wake lakini
mwanamke yule ni hatari
sana.Kitendo alichokifanya cha
kumuua Pascal kwa haraka namna
ile kinanifanya niamini yule si
mwanamke wa kawaida.Ni
jambazi? Kwa nini anatembea na
bastora?Nilifanya makosa sana
kutomchunguza kwanza kabla ya
kukimbilia kufanya ngono.Lakini
sipaswi kujilaumu kwani sote
tulijua yule ni kahaba tu.Baada ya
kuishika bastora na kumuua ndipo
sote tukapata akili kuwa Vicky ni
zaidi ya kahaba.Kabla ya
mapambazuko lazima tumfahamu yeye ni nani na kwa nini akamuua
Pascal” akaendelea kuwaza Steve
huku akiendesha gari kwa kasi
kwa sabau maeneo haya
hakukuwa na magari mengi usiku
huu.
Walifika katika makazi yao
akabonyeza kengele ya geti na
Elvis akatoka akawafungulia
mlango wakaingia ndani
"Winnie kama hutajali
naomba uingie ndani upate walau
maji wakati ninapakia mzigo"
akasema Steve na kumfungulia
Winnie mlango wakaeleka
sebuleni.Mara tu walipoingia
sebuleni sura ya Winnie ikapatwa
na mstuko mkubwa alipoiona
bastoa ikiwa mezani,akataka
kugeuka ili akimbie lakini nyuma yake alikuwepo Steve akamshika
mkono na kumuamuru akae kitini
kisha akaichukua simu ya Winnie
akaizima kabisa
"Tafadhali jamani naomba
msiniue!! akasema Winnie huku
akitetemeka kwa woga.
"Relax Winnie.We're not bad
people and we're not going to hurt
you" akasema Elvis
"Mnataka nini kwangu
?Msiniue jamani dada yangu ana
pesa na atawapa kiasi chochote
mnachokihitaji.Tafadhali msinuie"
akasema Winnie huku macho yake
yamejaa machozi
"Winnie nimekuleta kuja
kumuona dada yako na muda si
mrefu utakwenda kuonana naye
na mtazungumza.Usiwe na wasi wasi wowote.Baada tu ya kuonana
naye nitakurejesha nyumbani
kwenu" akasema Steve halafu
yeye na Elvis wakasogea pembeni
"Kuna chochote umekipata
toka kwa Vicky?Steve akauliza
"Hapana sikufanikiwa kupata
chochote.Yule mwanamke ni jeuri
sana.Steve ninahisi huyu
mwanamke ni tofauti sana na
tunavyomchukulia kama
kahaba.Kuna kitu zaidi ya
ukahaba na kuna mambo mengi
anayafahamu ambayo lazima
tuyajue kwa kumtumia mdogo
wake.Endelea kumchunga Winnie
mimi ninarejea tena chumbani
kabla ya kumuingiza Winnie"
akasema Elvis na kurejea
chumbani alimo Vicky ambaye alikuwa amejilaza
kitandani.Mlango ulipofunguliwa
akainuka na kukaa
"Umekuja kunifungua?
akauliza
"Hapana hautafunguliwa
Vicky hadi kiburi chako
kitakapokwisha.Sikiliza Vicky
awali nilipokuja nilikuuliza
kirafiki sana na kutaka unieleze
wewe ni nani na kwa nini ulimuua
Pascal lakini ukawa kiburi
ukagoma kujibu swali langu.Kwa
kitendo kile uliniudhi na
kunilazimisha nitumie nguvu
kupata kile ninachokihitaji"
"Are you going to hurt me?
akauliza Vicky huku akitoa
kicheko cha dharau
"No" akajibu Elvis I'm not gong to hurt you but
your sister Winnie "
Sura ya Vicky ikabadilika
akapandwa na hasira
zilizochanganyika na
mstuko,akamtazama Elvis kwa
macho yaliyojaa hasira
"Umesema nini wewe
ng'ombe?akauliza Vicky
"Nadhani umenisikia
vizuri.Mmi sina shida ya
kukuumiza wewe.Nitaanza na
mdo wako Winnie.Tayari yuko
hapa ndani "
"You are kiddng.This is a
joke" akasema Vicky kwa ukali
"Its not a joke.Winnie tunaye
hapa ndani na utashuhudia namna
nitakavyomtesa .Utashuhudia
machugu atakayoyapata.She's so young and pretty.Kwa nini uache
ateseke? Kwa nini umuumize? Just
tell me what I want and we'l let
her go.Hata mimi sipendi
kumuumiza mtoto mzuri kama
yule lakini ukinilazimisha
nitamuingiza katika mateso
makali na atakuchukia kwa
kushindwa kumsaidia.Ni wewe
pekee ambaye unaweza
kumuokoa kutika katika dhaama
inayomkabili.Nakupa dakika moja
kuamua hatima ya mdogo wako"
akasema Elvis na kuanza
kuhesabu sekunde katika saa yake
hadi ilipotimia dakika moja
"Tayari dakika moja.Naamini
umekwisha fanya maamuzi
kuhusu mdogo wako" "Go to hell! Sina ndugu
anaiwa Winnie.Kama ulidhani
kwa kufanya ujinga huo unaweza
kunipata umekosea sana.Wewe
bado ni chawa tu.Nakupa ,saa
mbili uweze kunifungua niende
zangu" akasema Vicky
"Nakupa nafasi ya mwisho
Vicky.Tafadhali naomba msaidie
mdogo wako.She dont deserve
this" akasema Elvis.
Kwa nini una kichwa kigumu
kuelewa wewe
kobe?Nimekwambia sina ndugu
mwenye jina hilo na kama
ulidhani kwa kutumia njia hiyo
unaweza ukanipata umekosea
sana.Narudia tena kukusisitiza
kwamba muda unakwenda na
usiponiachia yatakufika makubwa sana.Bado saa moja na dakika
arobaini za mimi kukaa humu
ndani.Naomba ulizingatie hilo"
akasema Vicky.Elvis akamtazama
halafu akatoka
"I have no
choice.Amenilazimisha nifanye
jambo ambalo sikuwa nimetaka
kulifanya.Huyu mwanamke ni
jeuri sana lakini leo amekutana na
jeuri zaidi yake na atasema tu kila
kitu" akawaza Elvis na kuingia
chumbani kwake akachukua vifaa
vyake vya kutesea na kuvipeleka
chumbani alimo Vicky akaviweka
mezani na bila kusema chochote
akatoka na kuelekea sebuleni
"Steve it’s time."
akamwambia Steve. Winnie inuka twende
ukamuone dada yako"akasema
Steve
"Mnanipeleka wapi?
Tafadhali nawaomba msiniue
jamani,dada yangu atawapa kiasi
chochote cha pesa
mtakachokihitaji" akasema
Winnie huku akilia na kumlazimu
Steve kumtolea bastora
"Kaa kimya na ufuate kila
utakachoamriwa
kukifanya.Umenisikia Winnie?
akasema Steve kisha akamshika
Winnie mkono wakaelekea
chumbani alimo Vicky.Elvis ndiye
aliyekuwa wa kwanza kuingia
halafu akafuata Winnie na nyuma
yake alikuwepo Steve Winnie ?!!! akasema Vicky
kwa mshangao
"Dada !! Winnie naye
akashangaa na kutaka
kumkimbilia dada yake lakini
Steve akamzuia
"Dada yangu amefanya nini?
akauliza Winnie huku akilia baada
ya kumuona dada yake akiwa
amefungwa mkono na mguu kwa
pingu.Elvis akamfanyia ishara
Steve amruhusu Winnie
akasalimiane na dada yake
akamuachia wakakumbatiana
huku wote machozi yakiwatoka
"Wamekuumiza kokote?
akauliza Vicky
"Hapana hawajaniumiza"
"Wamewezaje kukupata
Winnie? Wamenipigia simu kwa
kutmia simu yako na kunieleza
kwamba umepata ajali huko
hospitali na unataka kunioa hivyo
nikawaelekeza nyumbani wakaja
kunichukua.Who are these
people?Kwa nini wamekufunga?
akauliza Winnie na Vicky akafuta
machozi.Elvis akashika Winnie na
kumvuta pembeni
"Vicky nadhani sasa
umeamini kwamba mimi sisemi
uongo.Nataka uniambie huyu ni
nani?Ulisema kwamba hauna
ndugu yako anaitwa
Winnie.Nataka utamke mbele
yake ni kweli hauna ndugu yako
anaitwa Winnie? akauliza Elvis
"Nawaonya msijaribu
kumgusa mdogo wangu!!Ninaapa nitawafanyia kitu kibaya sana
endapo mtamfanya chochote
mdogo wangu.Shida yenu ni mimi
kwa hiyo mdogo wangu hahusiki
na chochote.Muacheni haraka
sana aende zake" akasema
"Ahsante sana Vicky kwa
kukiri kuwa Winnie ni mdogo
wako.Ninakupa nafasi ya mwisho
Vicky ya kumsaidia mdogo
wako.Una dakika tano za
kutafakari na kufanya maamuzi"
akasema Elvis na kisha akamtoa
Winnie mle chumbani
"Nini kinaendelea hapa? Dada
yangu amefanya nini?Naombeni
mumfungue tafadhali.Kama ni
fedha mnahitaji atawapa anazo za
kutosha" akalia Winnie, Winnie tunafahamu kuwa
unampenda sana dada yako na
ninaomba nikuhakikishie tena
kuwa sisi si watu wabaya na
tutamuachia dada yako ila kuna
mambo tunahitaji
kuyafahamu.Unaweza kutusaidia
kutuambia dada yako
anajishughulisha na nini? akauliza
Elvis
"Dada ni mfanya bashara "
"Anafanya biashara gani?
Steve akauliza
"Anafanya biashara ya hoteli
na ana maduka ya nguo na
urembo"
"Hakuna mambo mengine
anayafanya kwa siri nyuma ya
hizo biashara? Kama unafahamu
tueleze tafadhali kwani utakuwa umemsaidia sana dada yako
kipenzi"
"Ninachokifahamu ni
kwamba amekuwa akitoka na
wanaume mbali mbali kiasi cha
watu kumuita kahaba"
"Una hakika hakuna jambo
lingne unalolifahamu kuhusu dada
yako?
"Ukiacha hayo
niliyowaelezeni hakuna kingine
ninachokifahamu" akajibu Winnie
"Are you sure?Steve akauliza
"yes I'm sure" akajibu Winnie
"Kwa ufupi tu ni kwamba
dada yako yuko hapa kwa sababu
amefanya jambo kubwa usiku
huu.Amempiga risasi na kumuua
mtu ambaye ni hatari kwa
taifa.Tumemleta hapa ili kumhoji na kufahamu sababu za kumuua
mtu yule ambaye tulitegemea
kupata taarifa nyeti sana kutoka
kwake?Dada yako amekuwa
mgumu sana kutupa ushirikiano
na ndiyo maana tumelazimika
kukuleta hapa ili utusadie
kumshawishi afunguke na atupe
sababu za kumuua yule
mtu"akasema Elvis
"Dada yangu ameua mtu?
akauliza Wnnie kwa mshangao
"Ndyo.Umewahi kumuona
akiwa na bastora?
"Ndiyo nafahamu kuwa anayo
bastora lakini aliniambia ni kwa
ajili ya kujilinda"
"Ukiiona bastora hiyo
unaweza kuifahamu?
Sent using
Jamii Forums mobile app