Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 54

Mimi ni jasusi wa siri sana
ambaye ninafanya kazi maalum na
kuripoti moja kwa moja kwa
rais.Nilichukuliwa na rais na
kupelekwa katika mafunzo nchi
mbali mbali kwa siri na kuhitimu
halafu nikaja kuanza kufanya kazi
aliyotaka niifanye."


ENDELEA………………………………
"Tueleze kwa ufasaha
umefahamiana vipi na rais hadi
akakuchukua na kukupeleka
mafunzoni.Ni mafunzo gani
uliyapitia na kazi gani ambayo
unaifanya hivi sasa? akauliza Elvis Awali kabla ya kuingia katika
shughuli hizi nilikuwa na
kijisehemu kidogo ninauza
vinywaji.Baba moja namfahamu
kwa jina moja tu la Gidioni
alikuwa ni mteja wangu sana na
kila siku lazima afike kupata
kinywaji,alivutiwa nami na
tukaanza kutoka.Baadae akanipa
mtaji nikafungua baa kubwa
ambayo ilijipatia umaarufu na
wateja wengi na hapo ndipo
nilipoanza kujulikana.Siku moja
mzee Gidion alinieleza kwamba
kuna mtu mmoja mzito anahitaji
kuonana nami.Sikujua ni nani
huyo mtu,jioni akanipeleka katika jengo fulani la ghorofa tukaingia
ndani na kupanda hadi ghorofa ya
sita na nikagundua kwamba ile ni
klabu ya viongozi wakubwa na
watu wazito.Tuliingia katika
chumba fulani na nikastuka
kumuona rais wa Tanzania mle
ndani.Sikuwa nimetegemea kama
siku moja ningekutana na rais wa
nchi ana kwa ana.Rais Dastan
Mkobolwa akanikaribisha vizuri
na kwa upendo mkubwa na
alinisihi nisiogope.Alinieleza
kwamba kuna kazi anataka
kunipa.Baada ya uchunguzi wa
muda mrefu ameniona ninafaa
kuifanya kazi yake.Alinieleza kwamba kabla ya kuifanya kazi
hiyo lazima kwanza nikapate
mafunzo nje ya nchi na
nitakapokuwa tayari basi nitaanza
rasmi kuifanya kazi
hiyo.Alinielezea faida ambazo
nitazipata endapo nitakubali
kuifanya kazi yake na kwa sababu
nilikuwa na hamu na mafanikio
makubwa nikakubali bila kujua ni
kazi gani rais anataka kunipa"
Vicky akanyamaza kwa muda
halafu akaendelea
"Niliondoka nchini na
kwenda nchini Ujerumani nikiwa
sielewi ninakwenda kujifunza
nini.Nilipokewa katika uwanja wa ndege na mtu maalum na
kupelekwa katika chuo fulani cha
mafunzo ya ujasusi.Nilianza
mafunzo japo yalikuwa magumu
lakini kadiri muda ulivyosonga
ndivyo nilivyojikuta nikiyamudu
na kuyapenda mafunzo yale.Baada
ya kutoka Ujerumani nikaenda
nchini Ufaransa nikajifunza tena
kwa muda wa mwaka mzima na
halafu nikaenda nchini Uingereza
kujifunza tena kwa miezi
sita.Baada ya hapo nikarejea
nyumbani na ndipo rais akanipa
kazi” akanyamza tena kidogo na
baada ya muda akaendelea Mara tu alipochaguliwa,rais
Dastan na wakuu wenzake wa
nchi za Afrika Mashariki kwa
pamoja walikutana na wakuu wa
umoja wa ulaya na kujadili kwa
kina kuhusiana na biashara
iliyoanza kushika kasi barani
afrika ya kuuza binadamu kama
watumwa.Kila nchi ilitakiwa
kuunda kikosi maalum chenye
watu waliopata mafunzo
makubwa ya namna ya kubaini na
kukabiliana na mtandao wa watu
wanaofanya biashara hii haramu
ya kusafirisha na kuuza binadamu
kikosi ambacho kitafadhiliwa na
umoja wa ulaya.Hapa Tanzania kiliteuliwa kikosi cha watu sita
kwa ajili ya kuendesha zoezi la
kubaini mtandao wa watu
wanaojishuhusisha na biashara ya
binadamu.Watatu kati yetu tayari
wamekwisha fariki dunia na
tumebaki watu watatu.Ofisi yetu
iliunganishwa na ofisi nyingine
kama hizi katika nchi nyingine za
bara la Afrika kwa lengo la
kupeana taarifa lakini baada ya
wenzetu watatu kufariki dunia
ikabainika kwamba kuna viongozi
katika baadhi ya nchi wanafanya
hujuma ili kikosi hiki kishindwe
kufanya kazi zake na baadhi yetu
kuuawa kwani wana mahusiano na watu wanaofanya biashara hii
na kuna faida wanazipata hivyo
mtandao wa kikosi hiki
ukavunjika na kila nchi ikaanza
kujitegemea yenyewe.Baada ya
hilo kutokea wenzangu wawili
wakapelekwa katika idara ya
usalama wa taifa na mimi
nikapewa kazi nyingine.Rais
alinitaka nifanye uchunguzi
kuhusiana na mtandao unaofanya
biashara ya kuuza silaha.Alipata
tetesi kwamba waasi
wanaopambana na serikali ya
jamhuri ya kidemokrasia ya watu
wa Congo wanapata silaha zao
kutokea Tanzania.Alitaka kujiridhisha na tetesi hizi kama ni
za kweli na kama ni kweli
niwabaini watu hao ni akina nani"
akanyamaza.Elvis na Steve
wakatazamana na halafu Elvis
akampa ishara Steven ya
kumfungua pingu Vicky.
“Thank you” akasema Vicky
baada ya kufunguliwa
"Endelea" akasema
Elvis.Vicky akaomba maji
akanywa kulainisha koo halafu
akaendelea
"Nilianza kufanya uchunguzi
wangu kuubaini mtandao huu
unaojishughulisha na biashara ya
silaha lakini mpaka sasa bado sijafanikiwa kuubaini.Watu hawa
ni makini sana na wanafahamu
kuwa biashara wanaoifanya ni
haramu hivyo wanachukua kila
tahadhari ya kuhakikisha
hawafahamiki na mpaka leo bado
sijafanikiwa kuwafahamu.Wakati
nikiendelea na uchunguzi huo
nimekuwa pia nikifanya kazi
mbali mbali anazonipa
rais.Naweza kusema kwamba
nimekuwa mpelelezi maalum wa
rais.Ili kufanikisha baadhi ya kazi
ambazo nimekuwa nikipewa na
rais imenilazimu kujigeuza
kahaba.Kupitia kazi yangu ya
ukahaba nimekuwa nikitembea na watu mbali mbali hasa viongozi
wa serikali ninaotakiwa
kuwachunguza.Nimekuwa
nikipata taarifa mbali mbali toka
kwao na kumpatia rais.Kwa kifupi
hiyo ndiyo kazi ninayoifanya
pembeni ya biashara zangu.Vipi
kuhusu ninyi,who are
you?akauliza Vicky
"Ahsante Vicky kwa
kujitambulisha.Tumefurahi
kukufahamu kwani utakuwa na
msaada mkubwa kwetu zaidi ya
tulivyotarajia"akasema Elvis na
kunyamaza kidogo halafu
akaendelea Mimi naitwa Elvis tarimo na
yule mwenzangu anaitwa Steve
Kinke sote tunafanya kazi katika
idara ya ujasusi"
"Good to hear .But Elvis you
are supposed to be dead"
"I'm not dead”
"Ilitokeaje hadi ukafanikiwa
kumuaminisha kila mtu kuwa
umefariki?akauliza Vicky
"Tusipoteze muda tafadhali
katika hilo,tujielekeze katika
mambo ya msingi.Labda nianze na
maelezo mafupi ili tuelewane
vizuri" akasema Elvis
"Kuna msichana mmoja
anaitwa Graca ambaye ni mtoto wa mtu mmoja anaitwa brigedia
Frank Kwaju.Huyu msichana
alikuwa katika hospitali ya
magonjwa ya akili nchini Afrika
kusini na nilimtorosha nikamleta
hapa Tanzania kutokana na kuwa
na taarifa nyeti sana kuhusiana na
baba yake. Graca aliwahi kupewa
kompyuta na mama yake ambayo
aliiba kutoka katika ofisi ya
nyumbani ya Frank na kumtaka
akaifiche sehemu
salama.Kompyuta hiyo ilileta
mtafaruku mkubwa sana baina ya
wazazi wake na siku chache
baadae mama yake akafariki
katika ajali tata.Kilichoendelea hapo ni mtafaruku baina ya Frank
na mwanae Graca.Frank alimpa
vitisho vingi sana akimtaka
arejeshe kompyuta hiyo.Pamoja
na masahibu mengi yaliyomkuta
lakini Graca hakuwahi kuirejesha
kompyuta ile kwa Frank bali
aliificha sehemu
salama.Nimefanikiwa kuipata
kompyuta hiyo yenye siri nyingi
za Frank.Baada ya kupitia mafaili
yaliyomo katika kompyuta hiyo
nimegundua kwamba Frank
akishirikiana na Pascal Situmwa
wanashiriki katika biashara
haramu ya silaha.Wanawauzia
silaha waasi wanaopambana na serikali ya jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo"
"Real?! akauliza Vicky kwa
mshangao mkubwa
"Nilipopekua mawasiliano
yake nikakuta kuna maelekezo
amekuwa akipokea kutoka kwa
mtu anayejiita Deusdedith
MM.Huyu amekuwa akimpa
maelekezo mengi na inaonekana
ni mtu mwenye sauti katika
mtandao huu.Katika moja ya
mawasiliano yao Deusdedith MM
amemuelekeza Frank kwamba
akutumie wewe katika kumuua
kanali Norman.Hii inakufanya
uwe mtu muhimu sana kwetu kwani tayari unashirikiana na
watu tunaowachunguza.Nataka
tuanzie hapo.Deusdedith MM ni
nani? akauliza Elvis.Vicky akavuta
pumzi ndefu na kusema
"Nilipoanza uchunguzi
kuhusiana na mtandao wa
biashara ya silaha ilinichukua
muda mrefu hadi kubaini kwamba
kuna mtu anaitwa Deusdedith MM
ambaye anahusika na mtandao
huu.Huyu ni mfanya biashara
mkubwa na tajiri mwenye makazi
yake nchini Uingereza na vile vile
ana makazi afrika ya
kusini.Ilinilazimu kuanza
kumfuatilia ili kuubaini ukweli.Niligundua huyu jamaa
anapenda sana kwenda katika
makasino na ikanilazimu kuishi
Afrika kusini kwa muda
nikimuwinda.Nilijifanya kahaba
katika moja ya kasino
analolimiliki na nikafanikiwa
kumuweka karibu.Alinipenda
zaidi alipogundua kwamba
ninatokea Tanzania.Mimi na yeye
tukawa na mahusiano ya siri huku
nikiendelea kumchunguza"
"Uligundua nini katika
uchunguzi wako?akauliza Elvis
"Deus ni mtu makini sana na
anafahamu kujificha.Katika
uchunguzi wangu wote sikuwahi kubaini chochote kuhusiana na
yeye kuhusika katika biashara ya
silaha.Nilizifahamu biashara zake
za halali kama vile maduka
makubwa ya kuuza magari ya
kifahari Dubai.Nchini uingereza
ana duka la bidhaa za asili za
Afrika na kasino.Anazo biashara
nyingine pia nchini Afrika
kusini,Urusi na Italia.Vile vile
anazo biashara za siri lakini
anajua mno kuzificha na sikuwahi
kufanikiwa kuzifahamu"
"Stupid" akawaza Elvis
"Deus alininitaka nirejee
Tanzania kuna kazi anataka
kunipa ambayo nikiikamilisha atanilipa feda nyingi
sana.Nilikubali kurejea Tanzania
kuifanya kazi yake na baada ya
miezi miwili toka nirejee Tanzania
alinifuata Frank na kunieleza
kwamba amepewa maelekezo na
Deus aje anione anipe
kazi.Alinieleza kwamba kuna mtu
anahitajika kuuawa ambaye ni
kanali Norman.Sikuweza kukataa
kwani nilitaka bado kuendelea
kuwa karibu na Deus.Nilianza
ukaribu na Norman na muda
ulipofika ikanilazimu
kumuua.Nilipoikamilisha shughuli
hiyo Deus alinilipa fedha nyingi
sana na kunitaka nisiendelee tena na kazi ya ukahaba na wala
nisirejee tena Afrika kusini bali
nianzishe biashara hapa hapa
Tanzania na ndipo nikaamua
kujenga ile hoteli.Huo ndio
ulikuwa mwisho wa mawasiliano
yangu na Deus kwani
hakupatikana tena katika namba
za simu wala katika barua
pepe.Aliuza biashara zake zote
nchini Afrika kusini.Deus ni mtu
mmoja makini sana na anajua
kujificha.Baada ya kumpoteza
Deus ilinilazimu kuanza kujenga
mahusiano na akina Frank ili
niwachunguze kwani niliamini
lazima watakuwa na mahusianona Deus lakini kila nilipojitahidi
kujiweka karibu nao walinikwepa
kabisa lakini sikukata tamaa
nikaendelea kuwachuguza hadi
pale ulipojitokeza na kuanza
kunichunguza ukijiita
Robin.Niliwaeleza kwamba kuna
mtu ananichunguza ili kujiweka
karibu zaidi nao, wakanipeleka
mafichoni katika shamba la Frank
nikaishi huko kwa siku chache
hadi nilipoambiwa kwamba
umekufa"
"Nini umekigundua kutoka
kwa akina Frank? Elvis akauliza
"Sijagundua chochote bado
japo ninafamu kuna mambo wanayafanya kwa siri na wana
mahusiano na Deus"
"Wewe ni mpelelezi wa aina
gani uliyeshindwa hata
kuwachuguza panya wadogo
kama Frank na
mwenzake?akauliza Steve kwa
ukali
"Taratibu Steve" akasema
Elvis
"It's not easy like you
think.These peole are very
smart.Wanajihami kwa kila
namna wawezavyo hivyo ni
ngumu kuwapata kirahisi"
"Umefanya kazi nzuri Vicky
japo hujaweza kufika mwisho
lakini hapa ulipofika ni pakubwa.Kuna jambo nataka
kulifahamu.Kwa nini ulimuua
Pascal? akauliza Elvis
"Kama nilivyosema kwamba
ulipoanza kunichunguza
niliwaeleza akina Frank na
wakanieleza kwamba wewe ni
mtu wa usalama na wakanipeleka
mafichoni katika shamba la
Frank.Nikiwa kule nilisikia
mazungumzo yao Pascal
akimshinikiza Frank waniue
kwani tayati nimekwisha kuwa
hatari kwao lakini Frank alikataa
kwa vile alikuwa ananihitaji
kingono.Mlipotaka nimuite Pascal
pale hotelini nilijua mtampeleka
kumuhoji na kwa vile mtandao
wao ni mrefu angeweza kuachiwa
na kama angeachiwa huru basi lazima angeniua ndiyo maana
nikamuua"akasema Vicky
"Maelezo yako bado
hayajajibu swali kwa nini ulimuua
Pascal?Sababu ulizotoa
hazijitoshelezi kabisa.Tushawishi
tukuamini kwamba yale yote
uliyotueleza ni ya kweli" akasema
Elvis
"Yote niliyowaeleza ni ya
kweli kabisa.Pascal alikuwa ni
mtu anayeniwinda aniue na ile
ilikuwa ni nafasi yangu nzuri ya
kumuwahi"
"Hukufikiri kwamba kitendo
kile kinaweza kukuweka hatarini
na hata kukuharibia kabisa
maisha yako?
"Hilo haliwezi kutokea kwa
sababu nina ngao kubwa.Rais asingeweza kukubali niingie
katika matatizo ndiyo maana
sikusita kumuua
Pascal.Nisingefanya hivyo
angeniwahi kwani alikuwa na
mpango huo" akasema Vicky
"Ulifanya kosa kubwa sana
kumuua Pascal kwani alikuwa ni
mtu muhimu sana kwetu na
angeweza kutupa taarifa nyingi za
kutusaidia katika uchunguzi
wetu.Hata hivyo umezungumzia
kuhusu akina Pascal kuwa na
mtandao mkubwa,unataarifa
zozote kuhusiana na mtandao
wao?
"Ninafahamu wanao mtandao
mrefu lakini bado sijafanikiwa
kuubaini" What kind of agent are
you?Mbona kila kitu
hujafanikiwa? akauliza Steve kwa
ukali
"Steve taratibu,usiwe na
hasira"akasema Elvis na kumtaka
Steve watoke nje ya kile chumba
wazungumze
"Elvis this woman il lying to
us" akasema Steve
"Nisikilize Steve"
"Tumeianza operesheni yetu
na huyu Vicky anazo taarifa
zinazoweza kutusaidia hivyo
tumsikilize na kuna mambo
tunaweza kuyapata toka kwake
ambayo yanaweza yakatusaidia"
"I don't believe her.Kwa nini
kila kitu hafanikiwi?Do you
believe her? Yes I do believe her.She's
telling te truth" akajibu Elvis
"Nakuomba tumuhoji taratibu
ili atueleze kila kitu
anachokifahamu.Niachie mimi
nitazungumza naye" akasema
Elvis kisha wakarejea ndani
"Vicky nieleze tena kuhusu
huyu Deusdedith MM namna
unavyomfahamu.Ni mtu wa aina
gani? Ana familia?Anapendelea
vitu gani?
"Kama nilivyokueleza awali
kwamba Deus ni mtu anayejua
sana kujificha.Tabia zake haziweki
wazi hivyo ni vigumu sana
kumfahamu ni mtu wa namna
gani.Ninachoweza kusema ni mtu
anayebadilika badilika kama
kinyonga.Unaweza ukadhani havuti sigara lakini ukamkuta
anavuta,naweza kusema ni mtu
mwenye kubadilika kila
mara.Kuhusu familia anayo
familia lakini sikubahatika
kuifahamu wala mke wake
sijawahi kumuona.Ni watu
wanaojificha sana.Nimewapa
maelezo mengi kuhusu mimi ni
zamu yenu sasa kunijibu na mimi
kwa nini mlikuwa mnamtaka
Pascal? akauliza Vicky
"Tulimhitaji Pascal kwa
mambo mawili.Kwanza kumuokoa
na pili kupata taarifa za muhimu
kutoka kwake zitakazotusaidia
kuubaini mtandao
unaojishughulisha na uuzaji wa
silaha "
"Mlitaka kumuokoa? Ndiyo.Pascal alikuwa
anatakiwa kuuawa"
"Nani walitaka kumuua?
"Bado hatuna taarifa za
kutosha ni nani walitaka kumuua
na tulikuwa katika kuwatafuta
watu hao ila tunahisi ni watu
anaofanya nao biashara" akasema
Elvis
"Mshirika wake mkubwa ni
Frank kama ni wenzake wanataka
kumuua basi lazima Frank
atakuwa analifahamu jambo hilo"
akasema Vick
"Vicky limekuwa jambo zuri
tumekutana wote tukiwa na lengo
moja.Sote tunautafuta mtandao
wa kuuza silaha.Ninakuomba
uungane nasi katika kuusaka mtandao huu na kuufutilia mbali"
akasema Elvis
"Hata mimi nimefurahi
kukutana nanyi na nina uhakika
mkubwa kwamba kama
tukishirikiana na kuunganisha
nguvu tutafanikiwa
kuusambaratisha mtandao huu
ambao peke yangu nimejitahidi
kuutafuta bila mafanikio.Ninyi
wenzangu mnaonekana mnao
uzoefu mkubwa sana katika
masuala haya tofauti na
mimi.Naamini nitapata fursa nzuri
ya kujifunza kutoka kwenu"
"Usemayo ni ya kweli
Vicky,mtandao kama huu hauwezi
ukapambana nao mtu
mmoja,mnapaswa kunganisha
nguvu.Utakuwa ni msaada mkubwa sana kwetu.Karibu
kwenye timu" akasema Elvis
"Ahsante sana Elvis"
"Naamini utatusamehe
kuhusu mdogo wako Winnie
lakini hatukuwa na namna ya
kukufanya ufunguke zaidi ya
kumtumia yeye.Ni kwa sababu
yake tumeweza kugundua
kwamba nawe ni mwenzetu lakini
bila kufanya vile usingeweza
kufunguka na tungeendelea
kutesana hadi asbuhi"akasema
Elvis
"Kabla hatujaendelea mbele
naomba niwaweke wazi jambo
moja.Mimi ninayo timu yangu
ambayo wananifuatlia kila mahala
ninapokwenda kwa kutumia vifaa
maalum.Hata sasa wanajua kuwa niko hapa na kwa mujibu wa
taratibu zetu kila baada ya saa sita
natakiwa kubonyeza namba fulani
katika simu yangu kuwataarifu
wenzagu kuwa niko salama na
nikichelewa kufanya hivyo basi
wataamni niko katika hatari na
watavamia.Sitaki wavamie hapa
hivyo naomba simu yangu
niwasiliane nao kwa sababu saa
inanionyesha kuwa muda wangu
wa kubonyeza namba umekaribia"
akasema Vicky.Elvis akamfanyia
ishara Steve ailete simu ya Vicky
ili aweze kubonyeza namba
"Ahsante Elvis .Wewe
unaonekana ni mtu mwenye
kuelewa haraka sana tofauti na
huyu mwenzako Steve.Mpaka sasa anaonekana bado hajanikubali na
haniamini kabisa"
"Binadamu tuko tofauti sana
na Steve ndivyo alivyo huwa
hamuamini mtu haraka
haraka.Mvumilie kwa maneno na
maswali yake lakini atakuelewa
tu"
"What about you.Do you
believe me? Do you trust
me?Vicky akauliza,Elvis
akamtazama akatabasamu kwa
mbali na kusema
"Sina sababu ya
kutokukuamini wakati macho
yako yananionyesha kwamba
unasema ukweli,ila nikigundua
kwamba kuna udanganyifu
wowote nakuhakikishia utajuta kunifahamu.Mimi ni mtu mbaya
sana ninapodanganywa"
"I can see both angel and
devil in your eyes.Kuna nyakati
unakuwa malaika lakini kuna
nyakati unakuwa shetani.Hata
hivyo you are not a bad person"
akasema Vicky na mlango
ukafunguliwa akaingia Steve
akiwa na simu ya Vicky akampatia
kisha akaziandika namba fulani
katika simu yake na kuiweka
pembeni
"Sasa tunaweza
kuendelea"akasema
"Lengo letu kuu bado ni lile
lile kuutafuta na kuusambaratisha
mtandao wote wa watu
wanaofanya biashara ya kuuza
silaha kwa waasi wa Congo.Mtandao huu ni mkubwa
na unawahusisha watu walioko
hapa Tanzania,Congo na hata nje
ya nchi.Tunaanza kwanza na hawa
waliopo Tanzania kwa sababu
silaha zote zinapitia
hapa.Tutawasambaratisha wote
na hakuna jiwe litasalia juu ya
jiwe.Hakuna anaeshiba kwa fedha
za mauzo ya silaha atabaki
salama.Wote lazima wakutane na
mkono wa sheria.Hii ni ahadi
yangu na ni lengo letu sote hivyo
tuhakikishe tunalitimiza.Vicky
wewe tutakutumia sana katika
kupata taarifa mbali
mbali.Unatakiwa kumuweka
Frank katika himaya yako na kisha
upate taarifa za muhimu kutoka
kwake.Naamini hili utalitekeleza vyema kwani liko ndani ya uwezo
wako.Frank ndiye kinara wa
biashara hii ambaye
tunamfahamu hadi sasa na kupitia
huyo tutaufahamu mtandao wote
unaohusika na biashara hii hivyo
unapaswa kuwa karibu naye
sana"akasema Elvis
"Frank ni dhaifu sana kwangu
na ninao uwezo wa kumfanya
chochote" akasema Vicky
"Good.Utautumia udhaifu huo
ili kuweza kutusaidia kupata
taarifa za muhimu kuhusu watu
anaoshirikiana nao katika
biashara hiyo ya silaha.Hakikisha
umekutana naye kesho na ufanye
kila uwezalo uipate simu yake na
ndani ya muda mfupi utaingiza
namba fulani nitakazokupatia katika simu yake ambazo
zitatuwezesha kupata
mawasiliano yake yote.Tutajua
anawasiliana na nani na
wanaongea kuhusu nini.Tunaweza
kufanikiwa kunasa jambo kupitia
mawasiliano yake"
"Hilo ni wazo zuri lakini watu
hawa ni makini sana na wanajua
kuficha mambo yao hata hivyo
nitafanya kama ulivyoniagiza"
"Jambo lingine tunataka
kumchunguza pia makamu wa
rais Dr Shafi ambaye tunahisi
anaweza kuwa anahusiana na
mtandao huu.Makamu wa rais
ndiye aliyetoa amri mimi niuawe
na ndiye aliyetoa maelekezo
Pascal auawe pia."akasema Elvis Makamu wa rais?!! Vicky
akashangaa
'Ndiyo.Mimi sifahamiani naye
hata kidogo lakini alitoa
maelekezo niuawe.Lazima kuna
jambo kwani hawezi akatoa
maelekezo kama yale kama
hakuna sababu ya msingi .Lazima
kuna mahala nimemgusa na ndiyo
maana akaamua kutumia nguvu
yake ili kuniondoa.Nina hisi
lazima atakuwa na mashirikiano
na akina Frank japo kwa siri
sana.Huyu naye anapaswa
kuchunguzwa pia" akasema Elvis
"Nimestuka sana kusikia
kuwa ni makamu wa rais ndiye
aliyetoa maelekezo ya kuuawa
wewe na Pascal.Kama
unavyosema lazima kuna sababu kubwa.Sina mahusiano yoyote na
makamu wa rais lakini tunaweza
kutafuta namna ya kumchunguza"
akasema Vicky na kuinamisha
kichwa akafikiri kwa muda na
kusema
"Ofisi ya makamu wa rais
ndiyo inayojishughulisha na
masuala yote ya
mazingira.Tumtafute mwanamke
mmoja mrembo sana ambaye
atajifanya ni mwandishi wa habari
za mazingira kutoka nje ya nchi na
ambaye mipango itafanyika ili
aweze kukutanishwa na makamu
wa rais.Nitazungumza na rais na
kumtaka amuunganishe huyo
mwanamke na makamu wa rais na
tutamtumia katika
kumchunguza.Ninaye rafiki yangu ambaye tunaweza kumtumia
katika shughuli hiyo ambaye
tulikuwa naye mafunzoni anaitwa
Omola Otola.She's pretty like me
but she's a professional
hacker.Hakuna mtandao asioweza
kuudukua.Kwa sasa anafanya kazi
zake nchini Afrika kusini akiwa na
kampuni fulani ya uchunguzi
akichunguza mtandao wa
biashara ya pembe za
ndovu.Nitamuomba aje atusaidie
katika shughuli hii kama
mtaridhia lakini atahitaji malipo
makubwa.Atalipiwa tiketi ya
ndege ya kuja na kurudi mara
atakapomaliza kazi yake,hoteli
nzuri atakakofikia kwa muda wote
atakaokuwa hapa nchini na
malipo yake ya kufanya kazi.Japo malipo yake ni makubwa lakini ni
mtu sahihi tunayeweza kumtumia
katika kuifanikisha kazi
yetu.Kupitia kwake tunaweza
kupata taarifa zote tunazozihiaji
kuhusu makamu wa rais" akasema
Vicky
"Una mawazo mazuri kama
ilivyo sura yako" akasema Steve
na kutabasamu
"Ni wazo zuri sana hilo
Vicky.Kuhusu gharama usihofu
tutamlipa kiasi chochote
atakachokihitaji,pesa si
tatizo.Tena itakuwa vyema
kuongeza mtu mwingine katika
timu yetu kwani tunahitaji sana
mtaalamu wa teknolojia.Sote
tunaweza kucheza na kompyuta
lakini tukimpata mtaalamu zaidi ambaye ana ufundi wa hali ya juu
wa kucheza na mitandao itakuwa
vyema zaidi."
"So can I call her right now?
akauliza Vicky
"Ndiyo" akajibu Elvis na Vicky
akachukua simu yake akazitafuta
namba fulani
akapiga.Akazungumnza kwa
takribani dakika ishirini halafu
akakata simu
"Omola ana kazi nzito sasa
hivi lakini nimemuomba sana aje
anisaidie.Ni rafiki yangu mkubwa
na amesema atanipa jibu kabla ya
saa tatu kesho asubuhi kama
atakuwa na uwezo wa kuja au
vipi.Tuombe akubali"
"Ok good.Tutasubiri hadi
muda huo na kama akishindwa kuja basi tutatafuta namna
nyingine"akasema Elvis na
wakaendelea na kupanga mikakati
mingine namna ya kufanikisha
jukumu lile hadi mshale wa saa
ulipoonyesha ni saa kumi na moja
na dakika nane.
"Umekuwa ni usiku mrefu
sana.Kwa sasa baada ya kuwa kitu
kimoja mnaweza mkaturuhusu
mimi na Winnie tukapumzike
nyumbani ili niweze kujiandaa
kwa kazi kubwa inayotukabili?
akauliza Vicky
"Hakuna shaka mnaweza
kwenda kupumzika.Mtatumia
mojawapo ya magari tuliyonayo
hapa ila tukutane saa nne za
asubuhi kwa mipango zaidi.Halafu
kuna kitu kimoja ambacho unapaswa kukizingatia ni kwamba
usithubutu kumueleza rais
kwamba kuna watu unashirikiana
nao au hata kutaja jina langu
kwani mke wangu ni daktari wa
mke wa rais na wanafahamu kuwa
nimekufa.Wakijua niko hai
inaweza kuvuruga mambo
yote.Kwa taarifa yako hata mke
wangu hajui kama niko
hai"akasema Elvis
"Mkeo hajui kama uko hai?!
akashangaa Vicky
"Ndiyo hafahamu chochote
kama niko hai"
"Dah huu ni uongo mkubwa
sana lakini katika kazi hizi kuna
nyakati inabidi kutumia mbinu
kama hizi ili kufanikisha mambo
muhimu" akasema Vicky na mlango ukafunguliwa akaingia
Steve akiwa amemshika mkono
Winnie ambaye alikuwa analia
"Tafadhali usilie Winnie"
akasema Elvis
"Mnataka kunitesa tena?
akauliza Winnie
"Hapana Winnie.Yale mambo
yamekwisha na hautateswa tena"
akasema Vicky
"Winnie I'm sorry for what
happned.Halikuwa lengo letu
kukuumiza lakini ilitulazimu
kufanya vile ili kumfanya dada
yako atupe taarifa fulani
muhimu.Kwa sasa tumekwisha
elewana na tumekuwa kitu
kimoja" akasema Elvis
"You are all monsters!!
akasema Winnie kwa hasira Nataka kwenda nyumbani!!
akasema Winnie
" Guys we have to go
now.Tutaonana hiyo baadae"
akasema Vicky kisha
wakaelekezwa gari la kutumia
wakaondoka.
"Imekuaje ukamuamini yule
kahaba haraka namna hii hata
ukamjumuisha katika timu?
akauliza Steve baada ya akina
Vicky kuondoka
"Macho yake yananionyesha
kuwa anachokiongea ni cha kweli
na halafu atakuwa na msaada
mkubwa kwetu.Ni mwanamke
mwenye kufikiri haraka haraka
sana na anazo mbinu nyingi za
kufanikisha mambo.Katika
operesheni kama hii mwanamke kama Vicky ni muhimu mno kuwa
naye"
"Elvis wewe ni kiongozi
wangu na sikupingi katika
maamuzi yako ila suala la ka Vicky
katika mpango huu bado linanipa
mashaka sana.Ni mapema mno
kumuamini"akasema Steve
"It's not a mistake
Steve.Haikuwa rahisi hata kwangu
kumuamini lakini moyo wangu
umenituma nimuamini na
ninakuomba nawe
umshirikishumuamini.Atatusaidia
sana katika mambo
mengi.Tupumzike kidogo kwani
usiku umekuwa mrefu sana lakini
wenye mafanikio"akasema Elvis
na kila mmoja akaenda chumbani
kwake kupumzika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom