Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 55

Safari ya Vicky na mdogo
wake Winnie ilikuwa ya kimya
kimya na njia nzima Winnie
alikuwa anadondosha machozi
"Nyamaza kulia
Winnie"akasema Vicky
"Vicky naomba usinisemeshe
kabisa.Sitaki kuisikia sauti yako!
akasema Winnie kwa ukali
"Nafahamu umekasirika sana
Winnie kwa mambo yaliyotokea
usiku wa leo lakini nakuahidi
tukifika nyumbani nitakueleza kila
kitu"
"Sitaki kusikia chochote
kutoka kwako.What kind of sister
are you?Unawezaje kuwaacha wale jamaa wanitese namna ile
kwa kunichoma na umeme huku
ukiangalia? Vicky akameza
mate,alionekana kuumizwa sana
na kauli ile ya Winnie
"Winnie I'm sorry !!akasema
na kwa mbali akalengwa na
machozi
"Sorry?! akauliza Winnie.
"Winnie hatuwezi
kuzungumza suala hili
barabarani.Tutazungumza
tukifika nyumbani ni suala pana
sana ila kitu kimoja tu ambacho
nataka ukifahamu ni kwamba I
love you so much and I wont let
anybody hurt you" akasema Vicky
na safari ikaendelea

***************
Saa kumi na mbili na dakika
nane za asubuhi Patricia akaamka
na kitu cha kwanza alichokifanya
ni kuwasha simu yake na jumbe
nyingi zikaingia toka kwa watu
mbali mbali.Hakujishughulisha
nazo akazitafuta namba za Doren
akampigia na kumjulia hali halafu
akamuuliza endapo anazo namba
za Meshack Jumbo
"Meshack Jumbo?!! Doreen
akashangaa
"Ndiyo.Yule bosi wake na
Elvis tuliyekuwa naye msibani"
"Kuna tatizo gani Patricia?
akauliza Doreen kwa wasi wasi
"Ninahitaji kuonana naye ni
suala binafsi" akasema Patricia na Doreen akampatia namba za
Meshack Jumbo
"Ahsante Doreen
tutawasiliana
baadae.Nitakuelekeza mahala
nilipo ili uje tuwe wote kwa
sababu na hapa pia wana msiba
wamefiwa na baba yao" akasema
Patricia wakaagana.Patricia
hakupoteza muda akampigia
Meshack
"Hallow" ikasema sauti ya
upande wa pili
"Shikamoo mzee" akasema
Patricia
"Marahaba.Nani mwenzangu?
"Ni mimi Patricia mke wa
Elvis"
"oh Patricia.Habari yako? Vipi
maendeleo yako?"Ninaendelea vizuri
mzee.Nakushukuru sana kwa
msaada wako mkubwa kwa
wakati wote wa msiba wa Elvis"
akasema Patricia na kuhisi
analengwa na machozi
"Usijali Patricia.Elvis alikuwa
kijana wangu niliyempenda sana."
"Mzee samahani
nimekusumbua asubuhi
hii.Ninahitaji kukuona baadae
kidogo nina shida ya muhimu sana
na ni wewe tu unayeweza
kunisaidia kuitatua shida hiyo"
akasema Patricia
"Usijali Patricia muda
wowote utakaokuwa na shida
nitakuwa tayari
kukusaidia.Unataka tuonane saa
ngapi na wapi? Nataka tuonane asubuhi hii
mahala utanielekeza mwenyewe"
akasema Patricia na kisha mzee
Jumbo akamuelekeza mahala
mbako alitaka wakutane halafu
wakaagana
"Lazima nimsaidie Juliana ili
aweze kuwapata wale waliomuua
mdogo wake Godson.Mimi na yeye
sote tuko katika jahazi moja la
kufiwa na wapendwa
wetu.Ninataka waliomuulia
mpenzi na mdogo wake
wakamatwe kwa sababu
ninafahamu machunguya kufiwa
na umpendaye.Japo ni muda sasa
umepita lakini machungu ya
kufiwa huwa hayasahauliki na
hayazoelezi.Ni kidonda
kisichopona.Mimi pia ninataka waliomuua mume wangu nao pia
wakamatwe na wafikishwe mbele
ya sheria" akawaza Patricia na
kusikia sauti za watu
wakizungumza akafungua pazia
akaona mafundi wakiwa katika
harakati za kujenga hema kwa ajili
ya waombolezaji watakaoanza
kufika mapema asubuhi
"Patricia anahitaji nini hadi
akataka tuonane asubuhi hii? au
kuna fununu tayari amekwisha
zipata kuhusiana na kifo cha Elvis?
akawaza Meshack Jumbo halafu
akachukua simu yake na
kuzitafuta namba mpya za Elvis
akampigia
"Mzee shikamoo"akasema
Elvis baada ya kupokea simu Marahaba Elvis.Habari za
asubuhi? Vipi maendeleo yenu
hapo?
"Tunaendelea vyema
mzee.Usiku ulikuwa mrefu sana
lakini kuna mafanikio
tumeyapata,tutazungumza
utakapofika huku baadae"
"Vizuri sana.Nitafka huko
lakini kuna jambo lililonifanya
nikupigie asubuhi hii.Patricia
kanipigia simu muda si mrefu na
amenitaka tuonane asubuhi ya leo
tuzungumze"
"Patricia?! Ana tatizo
gani?akauliza Elvis ambaye kila
akisikia jina patricia likitajwa
hustuka sana
"Hajanieleza ni tatizo gani ila
amesema kwamba ana tatizo na mimi ndiye mwenye uwezo wa
kumsaidia tatizo lake" akasema
Meshack.Elvis akavuta pumzi
ndefu
"Sawa mzee.Utanijulisha
mara utakapoonana naye"
"Sawa Elvis.Nikitoka kuonana
naye nitakuja huko" akasema
Meshack na kukata simu


******************

Tayari kujua kimeanza
kuchomoza na tayari mafundi
walikwisha wasili nyumbani kwa
Elizabeth na kuanza kufanya
maandalizi ya kujenga mahema
kwa ajili ya waombolezaji
watakaofika msibani.Elizabethakiwa amezama katika maongezi
na mtu kwenye simu kengele ya
mlangoni ikalia akaenda
kuufungua mlango akakutana na
msaidizi wake Rosemary na
ikamlazimu Elizabeth kumuomba
mtu aliyekuwa anazungumza naye
kumsubiri kidogo
"Rose karibu"
"Ahsante madam.Samahani
sikujua kama uko simuni."
"It's ok.Nilikuwa nazungumza
na watu walioko Uingereza kwa
ajili ya taratibu za kusafirisha
mwili.Huko nje kila kitu
kinakwenda sawa?maandalizi
yamekwisha anza?
"Ndiyo madam.Kila kitu
tayari kinakwenda vizuri.Viti vimewasili na hata mpambaji
tayari amekwisha anza kazi"
"Good"
"Madam kuna mtu amekuja
anahitaji kukuona"
"Ni nani? Hujamueleza
kwamba huwa sionani na watu
asubuhi namna hii?
"Walinzi walimueleza hivyo
lakini akasisitiza kwamba ni
muhimu akaonana nawe ndipo
waliponiita nikaongea naye na
akasema kwamba anahitaji sana
kuonana nawe asubuhi ya leo"
"Ni nani huyo anayesisitiza
kutaka kuonana nami asubuhi
namna hii?
"Ni Brigedia Frank"
Elizabeth akafikiri kwa muda
na kusema Ok.let him in" akasema
Elizabeth na kuingia chumbani
kwake kujiandaa kwani alikuwa
katika vazi la kulalia.Akatoka
chumbani na kuelekea seuleni
akakutana na Frank ambaye
alisimama kwa adabu alipomuona
Elizabeh akamsalimia
"Madam Elizabeth" akasema
Frank
"Frank.Karibu sana"
"Ahsante madam" akasema
Frank
"Vipi mbona asubuhi namna
hii? Kwema huko
utokako?akauliza Elizabeth
"Huko kwema madam lakini
si kwema sana.Kwanza kabisa
utanisamehe kwa kukusumbua
asubuhi namna hii.Nafahamu huu si utaratibu wako lakini
imenilazimu kuja mida hii kwani
nisingeweza kupata nafasi ya
kuonana nawe baadae
tukazungumza kutokanana
kutingwa sana na shughuli za
msiba.Kabla sijaeleza
kilkichonileta hapa,niruhusu
nikupe pole nyingi sana kwa
msiba uliokupata.Nilistuka sana
uliponiambia kwamba Sir Deus
amefariki dunia.Sikuwa na taarifa
hizo na nikashangaa kwa nimi
madam ulinitenga hukunijulisha
kuwa bosi wangu amefariki
dunia"akasema Frank
"Wengi bado hawafahamu
kama Frank amefariki
dunia.Tumewajulisha watu
wachache tu kuhusiana na kifo hiki.Nimefanya hivi kwa sababu
maalum kwa hiyo
usihofu.Kuondoka kwa Deus
hakutaathiri chochote,kila kitu
kitaendelea kama kawaida kwa
sababu mimi nipo.Mimi ndiye
mkuu kwa sasa"
"Nimekuelewa madam"
"Tuachane na hayo.Nini
kimekusibu asubuhi yote
hii?Sikuwa nimepanga kuonana
nawe leo hadi pale nitakapomaliza
msiba ndipo ningekutana nawe na
kufanya mazungumzo ya kina
kuhusu mambo mbali mbali"
"Madam utanisamehe kwa
kuvuruga ratiba zako lakini
nimeshindwa kabisa kupata
usingizi hivyo ikanilazimu kuja
kukuona ana kwa ana" Nini kimekukosesha
usingizi? akauliza Elizabeth
"Kwanza ni taarifa za kifo cha
Deus na pili ni jambo lililotokea
jana usiku"
"Frank nilikupigia simu na
kukujulisha kuwa usifanye
chochote kuhusiana na kifo cha
Pascal ambaye ameuawa kwa
sababu maalum na mimi ndiye
niliyeagiza jambo hilo lifanyike
kwa hiyo sitaki maswali kuhusu
jambo hilo"akasema Elizabeth
"Madam Elizabeth
ninakuhesimu sana na sitaki
kukukosea adabu lakini ninahitaji
kueleweshwa japo kidogo nini
hasa kilichopelekea Pascal
akauawa?Alifanya jambo gani
baya?Ninamfahamu Pascal nimekuwa naye katika biashara
yetu kwa muda mrefu na
amekuwa msaidizi wangu
mzuri.Toka nilipomfahamu hadi
sasa sijaona tatizo lake.Utendaji
kazi wake ni mzuri na zaidi ya
yote amekuwa ni chanzo kizuri
sana cha taarifa kwetu na mara
nyingi nimekuwa nikikueleza
kuhusiana na kazi nzuri
anayoifanya.Mambo haya ndiyo
yanayonisukuma kutaka kujua ni
kwa nini ameuawa?tafadhafali
madam"akasema Frank
"Frank unanifahamu vyema
mimi huwa sipendi
ubishani.Nimekwisha kupa
maelekezo kwamba suala la Pascal
ni suala langu mwenyewe na
uachane nalo.Tafadhali nakuomba usiendelee na hili suala!! akasema
Elizabeth akionekna kuwa mkali
kidogo
"Sawa madam nimekusikia
lakini ninaomba nikupe maelezo
kidogo kama utaniruhusu"
"Go ahead" akasema
Elizabeth
"Nilikueleza kuhusiana na
Elvis kufahamu biashara yetu na
kuanza kutuchunguza.Alifahamu
pia kuhusu Victoria kwamba
tulimtumia kumuua Norman na
akaanza kumchunguza.Ulitoa
maelekezo kwamba niusafishe
uchafu huo na kuwaua wote
wawili Elvis na Vicky.Elvis tayari
amekwisha fariki na amezikwa ila
Vicky bado sijamuua
ninamtengenezea mazingira na muda wowote nitamkata
pumzi.Jana usiku nilimpigia simu
Pascal na kumtaka afike nyumbani
kwangu kwa ajili ya mazungumzo
muhimu na akaniambia kwamba
yuko njiani anakuja.Wakati
nikimsubiri akanipigia simu na
kunijulisha kuwa amepigiwa simu
na mtu fulani na kumtaka
waonane hivyo akanieleza kuwa
atachelewa kufika kwangu ili
akaonane na huyo mtu.Baaae
nikapigiwa simu na David
akanijulisha kuwa Pascal
amefariki dunia.Amepigwa
risasi.Nilikwenda eneo la tukio na
kujiridhisha kuwa ni kweli
amefariki dunia"
"Frank mbona unaanza
kunihutubia?Nina mambo mengi sana siku ya leo hivyo nakuomba
kama huna cha maana cha
kunieleza usubiri hadi siku yako
nitakapokuita kwa mazungumzo
rasmi"akasema Elizabeth
"Madam naomba unipe
dakika mbili tu nimalizie
nilichotaka kukisema"
"Be quick!! akasema
Elizabeth
"Thank you.Kabla hujanizuia
kufanya chochote kuhusiana na
kifo cha Pascal nilifanya
uchunguzi mdogo nikagundua
kwamba mtu wa mwisho
kuwasiliana na Pascal alikuwa ni
Vicky ambaye naamini ndiye
aliyemtaka waonane pale
hotelini.Nataka nifahamu je
ulimtumia Vicky katika kumuua Pascal? akauliza Pascal na
Elizabeth akastuka
"Vicky?
"Ndiyo.Ulimtuma amuue
Pascal?
Swali lile likambabaisha
Elizabeth.Akafikiri kidogo kisha
akasema
"Ndiyo nilimtumia"
"Inanishangaza kidogo
madam kwa nini umtumie mtu
ambaye umekwisha toa
maelekezo auawe?Umebatilisha
kauli yako na Vicky hauawi
tena?Halafu mbona hujanijulisha
kuwa kwa sasa umeamua
kumtumia Vicky ili nisiendelee na
mipango yangu niliyoipanga ya
kumuua? Frank kuna mambo mengi
yua kuzungumza mimi na wewe
lakini ni hapo baadae
nitakapokamilisha mazishi ya
mume wangu.Kwa sasa nakuomba
nenda kaendelee na masuala
mengine kuhusiana na operesheni
mapinduzi.Bado sijasikia tamko la
wanasiasa.Nini wanasubiri?
"Leo Dr Makwa Tusangira na
viongozi wenzake wa vyama vya
upinzani wanakutana na
waandishi wa habari na
kuwatangazia wanachama wao
wakutane kesho katika viwanja
jamhuri kwa ajili ya mkutano wa
hadhara.Bado hawajapewa kibali
cha kufanya mkutano lakini
watakaidi amri hiyo ili kupata
chanzo cha vurugu.Tayari maandalizi ya awali yamefanyika
na leo hii ninawafanyia mpango
wa fedha ili wapate kiasi cha
kuanzia.Mambo mengine yote
yanakwenda vizuri.Kila kitu
kinategemea vurugu
zitakazoanzishwa na wanasiasa
hapo kesho.Wanajeshi wote wako
tayari na leo hii nitafanya kazi ya
kushughukia malipo yao na
watakachobaki wanasubiri ni
wakati ufike waweze kuchukua
nchi"
"Good.Kazi inakwenda vyema
lakini bado naona kuna mianya ya
uzembe katika baadhi ya
sehemu.Nitakapokutana nawe
tutarekebishana kwani sitaki
uzembe wa aina yoyote utokee
katika operesheni hii muhimu sana.Uzembe wowote hata mdogo
unaweza ukasababisha mipango
yetu ikashindwa kufanikiwa"
akasema Elizabeth
Wakati Elizabeth na Frank
wakiendelea na mazungumzo
yao,Juliana na Patricia walikuwa
wanajiandaa kwa ajili ya kwenda
kuonana na Meshack Jumbo.
"Juliana are you sure you
want to do this? akauliza Patricia
kabla hawajatoka chumbani
"Patricia hakuna haja ya
kurudia rudia kujibu swali
hilo.Umeniuliza jana na
nilikujibu.Twende tuondoke
tukaonane na huyo mzee"
akasema Juliana wakatoka na
walipopita sebuleni wakawakuta Frank na Elizabeth katika
mazungumzo.Wakasalimiana
"Mama ninatoka kidogo na
Patricia kuna sehemu tunakwenda
ila hatutakawia sana"akasema
Juliana
"Mnakwenda wapi?
"Kuna mahala
tunakwenda.Tutazungumza
baadae" akasema Juliana na
kumshika mkono Patricia
wakaondoka hakutaka maneno
mengi na mama yake.Mara tu
walipotoka,Elizabeth naye
akamuomba Frank amsubiri
akaelekea chumbani kwake na
kuchukua simu akazitafuta namba
fulani akapiga
"Duma,kuna kazi nataka
uifanye ya haraka.Juliana na mwenzake wanaingia garini
wanaondoka kuna mahala
wanakwenda.Follow them.Fuatilia
wamekwenda wapi na kuonana na
nani.Nataka picha za mtu
wanayekwenda kuonana naye"
akasema Elizabeth halafu akarejea
sebuleni alikomuacha Frank
"Umemuona yule mwanamke
aliyeongozana na Juliana?
"Ndiyo nimemuona"akajibu
Frank
"Anaitwa Patricia ni mke wa
Elvis"
"Ni huyu? akauliza Frank kwa
mshangao
"Ndiyo"
"Amefikaje hapa? Ni rafiki na Juliana na ndiye
aliyemchukua akamleta hapa ili
aweze kupumzika"
"madam kukaa na mtu kama
huyu ndani ni hatari kubwa.What
are you going to do with her?
"Hutakiwi kunifundisha kazi
Frank mimi ninajua zaidi yako
hivyo nafahamu nini
nifanye.Nadhani tumemaliza .Una
lingine?akauliza Elizabeth
"Hapana sina
madam.Yalikuwa ni hayo
tu"akasema Frank
"Mazishi ni wiki ijayo.Jiandae
baada ya mazishi tutakuwa na
kikao kizito mimi na wewe"
akasema Elizabeth wakaagana na
Frank akaondoka Bado hainiingii kabisa akilini
eti madam Elizabeth amemtumia
Vicky katika mauaji ya Pascal.Cha
kushangaza nilipomueleza
kwamba Vicky ndiye mtu wa
mwisho kuzungumza na Frank
simuni na ndiye aliyemtaka
waonane pale hotelini,Elizabeth
alistuka na akababaika kujibu na
baadae akasema kwamba yeye
ndiye aliyemtuma.Hili nalikataa
kabisa kwa sababu alikwisha toa
maelekezo kwamba Vicky auawe
sasa iweje aamue kushirikiana na
adui yake?Mimi ni mwerevu na
hawezi kunidaganya
chochote.Hapa lazima kuna kitu
kinaendelea.Kwanza sina hakika
kama kweli madam Elizabeth
anahusika katika kifo ca Pascal.Hamfahamu Pascal japo
ninashirikiana naye katika
biashara ya silaha sasa iweje
amuue mtu ambaye hamjui.Kwa
kosa lipi? Taa nyekundu
inaniwakia hapa lazima kuna kitu
kinaendelea na siwezi kufumba
macho hadi nifahamu nini hasa
sababu na nani waliomuua Pascal?
Nisipofahamu chanzo cha mauaji
ya Pascal hata mimi naweza kuwa
niko hatarini bila kujifahamu
kwani Pascal alikuwa ni mtu
wangu wa karibu
sana.Nitachunguza kwa siri na
lazima nifahamu waliofanya
mauaji haya.Mtu pekee ambaye
anaweza akaniongoza katika
kuutafuta ukweli ni Vicky.Huyu
alikuwa mtu wa mwisho kuzungumza na Pascal na lazima
kuna kitu anakifahamu kuhusiana
na kifo hiki.Akipatikana akiteswa
ataeleza kila kitu" akawaza Frank
na kutoa simu yake akazitafuta
namba za Vicky akapiga,simu
ikaita na baada ya muda
ikapokelewa
"Hallo Frank"akasema Vicky
baada ya kupokea simu
"Habari yako
Vicky.Usingepokea simu yako au
ingekuwa haipatikani ningejua
tayari nawe umapatwa na
matatizo.Are you ok? akauliza
Frank
"Yes I'm ok. Vipi kuhusu
wewe uko salama?
"Niko salama.Nimekutafuta
sana kuanzia jana usiku lakini hukuwa ukipatikana,uko
wapi?Umekwisha pata taarifa za
jambo lililotokea jana usiku?
akauliza Frank
"Ndiyo nimesoma katika
mitandao ya kijamii kuwa Pascal
ameuawa.Nimesikitika sana.Nani
hasa waliomuua na kwa nini?
"Mpaka sasa hakuna
anayefahamu nini hasa
kilichotokea na kupeleka kifo
chake ila hali si nzuri hata
kidogo.Uko wapi mida hii?
"Niko nyumbani"
"Ok sawa nitakuomba
tuonane baadae mchana ili tuweze
kuzungumza kuhusu suala hili
kwani linatuhusu sote.Sisi
tulikuwa ni washirika wakubwa
wa Pascal na yawezekana na sisi tukawa hatarini pia.Tukutane
tujadili kwa kina suala hili na
tutafute namna ya kujilinda"
"Kwa mchana wa leo
sintaweza kupata nafasi nitakuwa
na mteja wangu wa muhimu sana
labda kesho ninaweza kupata
nafasi.Nitaomba unijulishe
taratibu za msiba na
mazishi.Ukinikosa hewani nitumie
ujumbe mfupi nitakapowasha
simu nitaupata"
"Vicky samahani si kwamba
ninaingilia ratiba zako lakini
Pascal alikuwa ni mtu wetu sote
na hata ulipopatwa na tatizo la
kufuatwa na yule jamaa
aliyetangulia mbele za haki
tulisimama wote kuhakikisha
unakuwa salama,huwezi ukaahirisha japo kwa siku moja tu
ratiba zako ili tuweze kujadili
suala hili muhimu na vile vile
kuhudhuria msibani?Tunapaswa
kuchukua hatua za haraka
kujilinda kwani hatujui bado ni
nani aliyemuua Pascal na kwa
nini?Tafadhali nakuomba"
"Frank kwa leo
haitawezekana.Mimi ninakwenda
kwa ratiba na kwa mujibu wa
ratiba yangu ya leo sintapata
nafasi hadi kesho.Usijali
nitakapopata wakati tutaonana na
kujadili.Nijuze tafadhali kila
kitakachoendelea kujiri" akasema
Vicky na kukata simu kabla Frank
hajatamka neno lolote
"bastard !!! akasema kwa
hasira na kuitupa simu pembeni Anafahamu alichokifanya na
ndiyo maana hataki kuonana
nami.Nitampata tu kahaba
mkubwa yule.Lazima nimuweke
katika himaya yangu na atajuta
kwa nini ulikuja duniani.Ni heri
angezaliwa mti kuliko kuzaliwa
mwanadamu.Nitamtesa na
utaeleza kila kitu" akawaza Frank
na kupekua simu yake akatafuta
jina limeandikwa Obi akapiga
"Heshima yako Afande"
ikasema sauti ya upande wa pili
"Obi habari yako?
"Nzuri kabisa mkuu"
"Obi uko wapi sasa hivi?
"Ninajiandaa kulala
afande.Nimefika nyumbani muda
si mrefu nimekuwa na kazi usiku
kuchaUsilale Obi.Kuna kazi nataka
kukupa.Nitakulipa vizuri"
"Mkuu kwa leo nimechoka
sana labda kesho"
"Hapana Obi,kazi hiyo
haiwezi kusubiri.Nataka leo hii hii
tena ifanyike kuanzia asubuhi ya
leo" akasema Frank
"Uko wapi mkuu? Obi
akauliza
"Niko njiani ninakuja hapo
kwako naomba unisubiri
tafadhali" akasema Frank
"Sawa ninakusubiri" akasema
Obi na kukata simu
Baada ya Frank kuondoka
Elizabeh akampigia simu David
ambaye bado alikuwa
kitandani.Alipoona jina la Elizabeth katika kioo cha simu
akakurupuka na kutoka chumbani
"Habari za asubuhi madam
Elizabeth? akasema David
"David we have problem"
"A problem?!
"Ndiyo.Frank ametoka hapa
muda si mrefu"
"Frank?
"Ndiyo.Amekuja asubuhi sana
na nilikuwa na mazungumzo naye
marefu kidogo.Anadai kwamba
kabla sijamzuia asifanye chochote
kuhusu kifo cha Pascal tayari
alikwisha anza kufanya uchunguzi
wake na aligundua kwamba yule
kahaba Vicky anahusika na kifo
cha Pascal kwani ndiye
aliyempigia simu na kumtaka
waonane hotelini ambako Pascal alikwenda kuuawa.Imenilazimu
kukubali kwamba mimi ndiye
niliyemtuma Vicky afanye mauaji
yale ya Pascal.Frank bado
hajaridhika na lazima atafanya
uchunguzi kwa siri na anaweza
akabaini kwamba unahusika
katika kifo cha rafiki yake na hii
inaweza kusababisha mipango
yetu ikashindwa kufanikiwa.Kwa
sasa naamini kitu pakee
anachokilenga ni kumpata
Vicky.Atatumia kila mbinu
kumpata na akifanikiwa atamtesa
hadi aufahamu ukweli.Atagundua
kwamba mimi sikumtuma Vicky
na hapa mimi na yeye tutaingia
katika mgogoro kitu ambacho
sitaki kitokee hasa kwa wakati
huu.Ningeweza kumuondoa Frank lakini bado ninahitaji kumtumia
katika mambo yangu hivyo mtu
pekee ambaye tunapaswa
kumuondoa hapa tena kwa haraka
ni Vicky.Akitoweka huyu kahaba
Frank hataweza kupata taarifa
anazozihitaji hivyo fanya kila
uwezalo,tumia kila mbinu huyu
mwanamke leo hii atoweke.Lakini
nina swali moja kwako"
"Uliza madam"
"Wewe si ndiye uliyefanya
mipango ya kumuua Pascal?
"Ndiyo madam"
"Vicky ulimshirikisha katika
mauaji hayo?
"Hapana madam.Mimi
niliomba msaada kutoka kwa
mwenzangu ambaye ana rasilimali
watu wa kuweza kuifanya hiyo kazi na sikufahamu chochote
kuhusu Vicky.Kwanza simfahamu
huyo mwanamke na wala sijawahi
kumuona.Hata mimi nimeshangaa
kwa taarifa kwamba anahusika
katika kifo cha Pascal"akasema
David
"Naweza kumfahamu ni nani
huyo uliyeshirikiana naye katika
kumuondoa Pascal?akauliza
Elizabeth
"Madam naomba ibaki kuwa
siri yangu"
"David jana tu nilikupa somo
kuhusu utii.Mimi ni kiongozi wako
na unapaswa unijibu kila
ninachokuuliza.Mbona mimi
nilikueleza siri yangu kuwa
nilifanya mipango ya kumuua
mume wangu?Naomba unieleza tafadhali ni nani huyo
mnashirikiana naye?akauliza
Elizabeth na David akasita kidogo
halafu akasema
"Ni makamu wa rais.Madam
naomba ufahamu kuwa makamu
wa rais Dr Shafi nayeni mwenzetu
katika operesheni
mapinduzi.Kuna mipango ambayo
tumeipanga mara tu nitakapoingia
ikulu na ndiyo maana akakubali
kushirikiana nasi"
"Good.Unajua sana kupanga
safu yako ya
ushindi.Ningeshangaa sana kama
katika mapinduzi haya
usingemshirikisha kiongozi
yeyote mkubwa.Hata hivyo bado
nina swali.Kama uliomba msaada
kutoka kwa makamu wa rais ili Pascal auawe kimya kimya Vicky
ameingiaje katika sakata hili?
"Madam,sina hakika kama
kweli Vicky anahusika katika
kumuua Pascal.Yawezekana
Pascal na Vicky walikuwa na
mahusiano yao na wakapanga
wakutane hapo hotelini na kwa
bahati mbaya Pascal akauawa"
akasema David
"David naomba
unisikilize.Mimi nimekuwa katika
magenge ya kimafia toka nikiwa
msichana nilipokuwa na
mahusiano na Deus hadi leo
hii.Ninafahamu mambo mengi
kuhusu wapelelezi,ninafahamu
mbinu zao na ninafahamu namna
ya kuwakwepa.Sina hakika bado
lakini kuna kitu kinaniambia kwamba yawezekana huyu Vicky
akawa ni miongoni mwao"
"Una maanisha Vicky ni
mpelelezi?! Akauliza David
"Ndiyo.Uwezekano huo
upo.Wapelelezi wanazo mbinu
nyingi za kupata taarifa kutoka
kwa watu mbali mbali"
"Hapana madam,sina hakika
kama inaweza kuwa kweli.Vicky
hawezi kuwa mpelelezi"
"Hiyo nimekupa kama
tahadhari tu ila fanya kila lililo
ndani ya uwezo wako na Vicky
apatikane.Asiuawe kwanza ili
apelekwe mahala akahojiwe na
tumfahamu ni nani.Nataka hadi
kufikia jioni ya leo nipate taarifa
kwamba suala hili limetekelezwa
kikamilifu na tayari tunamfahamu huyu Vicky ni nani" akasema
Elizabeth
"Sawa madam nitalitekeleza
hilo kama ulivyoagiza" akasema
David na simu ikakatwa
"Mambo haya mbona
yanaanza kunichanganya kichwa
changu?Huyu Vicky ameingiaje
tena katika sakata hili la
Pascal?Lakini naamini hizi ni hisia
tu za Frank na Vicky hahusiki na
chochote katika kifo hicho cha
Pascal.Waliotekeleza kifo hicho ni
watu wa usalama wa taifa.Hata
hivyo ngoja nifanye kama
alivyonielekeza.Lakini mambo
haya ya kuua ua watu yataendelea
hadi lini?Nilianza na Elvis
akafuata Pascal na sasa anafuata
Vicky.Natakiwa kuwa makini sana pale ninapotakiwa kutekeleza
mauaji haya" akawaza na
kuzitafuta namba za makamu wa
rais akampigia
"habari za asubuhi Dr
Shafi?akasema David baada ya Dr
Shafi kupokea simu
"Habari nzuri.Umeamkaje?
"Nimeamka salama
kabisa.Samahani sana kwa
usumbufu asubuhi hii"
"Bila samahani David"
"Ahsante sana.Nimekupigia
tena Dr Safi kuomba msaada
wako.Nina shida
nyingine.Tafadhali naomba
usinichoke"
"Usihofu David,tatizo lolote
ulilonalo nimekwisa kuahidi kukutatulia.Unahitaji nikusaidie
nini safari ii?
"Kuna mambo yamejitokeza
kwa yule mtu niliyekuomba
msaada wa kumlaza usingizi jana
ambayo yanahitaji kushugulikiwa
haraka sana.Imegundulika
kwamba Pascal alipigiwa simu na
mwanamke mmoja kahaba
anaitwa Vicky na kumtaka
wakutane hotelini na huko ndiko
alikokwenda kuuawa.Huyu
kahaba tayari anaanza kuhisiwa
kuhusika na mauaji hayo na kuna
hatari anaweza akakamatwa na
kutoa siri"
"Hilo lisikuogopeshe
David.Hakuna uchunguzi wowote
utakaofanyika kuhusiana na kifo
kile na tayari nimekwisha toa maelekzo kwa jeshi la polisi
wasifanye uchunguzi wowote
waachie suala hilo idara ya
usalama wa taifa hivyo hakuna
yeyote atakayekwenda kinyume
na maagizo hayo niliyoyatoa"
"Ahsante sana kwa hilo Dr
Shafi lakini wanaofuatilia suala
hili si polisi bali ni rafiki wa karibu
na Pascal na kwa hivi sasa
wanamuwinda wampate Vicky"
"Watu hao ni akina ani?
Tunapaswa kuwaondoa haraka
sana."
"Tutalazimika kuwaondoa
endapo wataendelea na kihere
here chao lakini kabla ya yote
nataka kufahamu kuhusu huyu
Vicky je ni mpelelezi? Anafanya kazi idara ya usalama wa
taifa?akauliza David
"Idara ya usalama wa taifa iko
chini ya ofisi yangu lakini si
wafanyakazi wote wa idara hii
ninawafahamu.Ninaowajua ni
viongozi wao.Unapoomba msaada
wa kumuondoa mtu fulani mimi
huwa nina mkabidhi jukumu hilo
mkuu wa idara ya ujasusi anaitwa
Meshack Jumbo na yeye hutoa
maelekezo kwa vijana wake na
mambo yakikamilika
hunijulisha.Siwezi kufahamu
kama huyo Vicky naye ni mmoja
wa watu wake au vipi hadi hapo
nitakapomuuliza"
"Ahsante sana Dr Shafi.Basi
ninamuhitaji huyo Vicky.Awe ni
usalama wa taifa au siyo ila ninamuhitaji kwa ajili ya
kumfanyia mahojiano.Huyu naye
nataka aondoke lakini kabla ya
kuondoka kuna mambo napaswa
kuyafamu kutoka kwake hivyo
natakiwa kumpata akiwa hai na
baada ya kumuhoji nitamkabidhi
kwa wahusika ili waweze
kumuondoa"
"Sawa David.Nitatoa
maelekezo jambo hilo lifanyiwe
kazi.Vipi kuhusu mambo yetu
yanakwendaje?
"Kila kitu kinakwenda
vyema.Maandalizi yanaendelea na
baadae leo wakuu wa vyama vya
siasa vya upinzani watakutana na
waandishi wa habari na
watatangaza kufanyika kwa
mkutano wao kesho na hapo ndipo tunapopatafuta.Safari yetu
ya kuelekea ikulu itaanzia hapo"
akasema David
"Sawa David usiache
kunijulisha kila kinachoendelea na
hata kama kuna yeyote unayeona
ni kikwazo katika kukwamisha
jambo hili nieleze tu na mimi
nitamkata kauli haraka
sana.Nitawasiliana nawe baadae
mara tu jambo hili
litakapokamilika" akasema Dr
Shafi na kuagana na
David.Hakupoteza muda
akampigia simu Meshack
"Dr Shafi habari za asubuhi?
akasema Meshack Jumbo baada ya
kupokea simu
"Meshack Jumbo,habari ni
nzuri sana.Vipi umeamka salama? Nimeamka salama kabisa"
"Nafurahi kusikia hivyo.Mzigo
wako niliokuahidi utawasili saa
sita mchana wa leo"
"ahsante sana Dr Shafi"
"Hata hivyo kuna kazi nataka
ifanyike leo.kwanza kabla ya kazi
naomba nikuulize unamfahamu
Vicky?
"Vicky?
"Ndiyo"
"Vicky yupi Dr Shafi?
"Una Vicky wangapi katika
idara yako?
"Sina mtu yeyote anayeitwa
Vicky katika idara yangu"
"Are you sure?
"yes I'm sure"
"Nani waliotekeleza mpango
wa jana wa kumuondoa Pascal? Nina vijana fulani ambao
huwa ninawatumia kwa shughuli
kama hizo ndio waliotekeleza huo
mpango"
"Kwa taarifa nilizonazo kuna
mwanamke mmoja anaitwa Vicky
ambaye anafanya biashara ya
ukahaba anadaiwa kushiriki
katika mauaji hayo.Inasemekana
kuwa ndiye aliyempigia simu
Pascal na kumtaka wakutane
hotelini na huko hotelini Pascal
akaenda kuuawa.Una taarifa
zozote kuhusu huyo mwanamke?
"Sina taarifa zozote Dr
Shaf.Mimi hutoa kazi kwa vijana
wangu na ninachohitaji ni kupewa
taarifa kwamba kazi imetekelezwa
na kumalizika bila kuhoji ni kwa
namna gani wametekeleza.Tulitaka Pasal afe
na ameariki.Yawezekana labda
vijana wangu waliona njia nyepesi
ya kumpata Pascal ni kwa
kumumia huyo Vicky"
"Hata mimi ninahisi hivyo
lakini kwa kuwa tayari amekwisha
anza kuhisiwa kuhusika katika
mauaji hayo huyo mwanamke
ayari ni hatari kweu hivyo
anapasswa aondolewe haraka
sana lakini kabla ya kuondolewa
anapaswa ahojiwe.Kuna mtu
anataka kumuhoji hivyo naaka
akamatwe na awekwe sehemu
fulani kwa ajiliya kuhojiwa kisha
nitaarifiwe.Nataka jambo hili
lifanyike leo hii"
"sawa Dr Shafi
nimekuelewa.Nitafanya hivyo na nitakujulisha pindi tukimpata
huyo mwanamke"
"Ahante sana Meshack.Uwe
na siku njema"
"Ahsante Dr Shafi" akasema
Meshack na kukata simu
"Sarakasi zimeanza.Tayari
Vicky amekwisha fahamika kuwa
alishiriki katika mauaji ya
Pascal.Ngoja nimjulishe Elvis
kuhusu jambo hili haraka"
akawaza Meshack na kumpigia
simu Elvis
"Mzee tayari umeonana na
Patricia ? akauliza Elvis baada ya
kupokea simu
"Nilikuwa najiandaa
niondoke lakini nikapokea simu
kutoka kwa makamu wa rais Dr
Shafi" Anataka nini Dr Shafi?
"Wanamtafuta Vicky
wanataka akamatwe akahojiwe
kuhusiana na kifo cha Pascal na
baadae auliwe.Bado uko naye
hapo nyumbani?
"Hapana amekwisha
ondoka.Mzee kuhusu Vicky
ninataka tuzungumze mara
utakapokuja huku lakini nadhani
nikupe maelezo kidogo.Jana
tumemfanyia mahojiano kwa
usiku mzima na tumegundua
kwamba Vicky ni mpelelezi
anayejificha chini ya mwamvuli
wa ukahaba.Anatumia njia hii kwa
ajili ya kupata taarifa muhimu
kutoka kwa watu mbali mbali
hususan viongozi wa
serikali.Anafanya kazi za siri za rais na kwa sasa amepewa kazi ya
kuchunguza kuhusiana na
mtandao wa biashara haramu ya
silaha.Rais pia amekwisha pata
tetesi kuhusu uwepo wa biashara
hii na anamtumia Vicky
kuchunguza.Imekuwa ni jambo
jema sana kwetu kumpata kwani
sote tuna lengo moja na tayari
tumeungana tumekuwa timu
moja."
"Real?!! akauliza Meshack
"Ndiyo mzee"
"Dah ! sikulitegemea kabisa
hili.Yuko wapi hivi sasa? bado
yuko hapo nyumbani kwako?
"Hapana hayuko hapa
amerejea nyumbani
kwake.Atakuja hapa baadae" Elvis call her right now.She's
in danger.Anatakiwa awepo
sehemu salama na kwa sasa
sehemu salama ni hapo kwako"
"sawa mzee ngoja nimjulishe"
"Mimi nitakuja huko baada ya
kukutana na Patricia na
nitakujuza kilichojiri" akasema
Meshack na kukata simu.Elvis
hakupoteza muda akampigia
Vicky lakini simu ya Vicky
haikuwa ikipatikana.Akapiga tena
haikupatikana.Akarudia zaidi ya
mara tano lakini simu ilikuwa
imezimwa
"C'mon Vicky kwa nini
unazima simu? akajisemea na
kuwaza kwa sekunde kadhaa
halafu akaenda chumbani kwa
Steve akaufungua mlango bila kubisha hodi na kwa kasi ya iana
yake Steve akakurupuka na
kuchukua bastora iliyokuwa
pembeni
"It's me Elvis don't shoot!!
ikamlazimu Elvis ajitambulishe
haraka
"Next time knock the door.!!
akasema Steve huku akiirudisha
bastora yake chini ya mto
"Sorry brother nilidhani
umelala ndiyo maana nikaingia
wangu wangu bila hodi"
"Kuna tatizo lolote? akauliza
Steve
"Ndiyo kuna tatizo.Muda
mfupi uliopita nimetoka
kuzungumza na
mkurugenzi.Amesema kwamba
amepigiwa simu na makamu wa rais asubuhi hii na akamueleza
kwamba tayari Vicky amekwisha
julikana kuwa anahusika katika
kifo cha Pascal hivyo anatafutwa"
"Oh my god! akasema Steve
"Mkurugenzi amepewa
maagizo ya kuhakikisha kwamba
Vicky anakamatwa na kuweka
sehemu salama kwa ajili ya
kuhojiwa kisha auawe.We have to
save her.Nimempigia simu yake
haipatikani inaonekana amezima
simu"
"Kwa hiyo tunafanyaje?
"Kwa kuwa nyumbani kwake
unapafahamu,unatakiwa kwenda
kumchukua yeye na mdogo
wake.Wote watakuja kuishi hapa
ambako watakuwa salama"
"Are you sure? akauliza Steve Steve hatuna namna
nyingine ya kufanya.We must save
them.Tunamuhtaji sana Vicky na
tukizembea wanaweza
wakamuua.Jiandae uende huko
haraka sana ukamchukue"
akasema Elvis na Steve akainuka
akaingia bafuni kujimwagia maji
****************

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kulubuleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ujageeeeeeeee bathiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii hali tete bin teteleeeeeeeeeeeeee
 
Sasa nafikiri twende nae mwendo flani wa ling'ang'a kulubule peke yako nyumaaaa geuka haya angalia tunavyo kutazama wewe tu ukikosea tu watu aghhhhaaaa kulubule kakosea basi fanya usikosee hiyo paredi poti wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom