Riwaya: Jina langu ni Pheady

Riwaya: Jina langu ni Pheady

Kama naangalia muvi ila mkuu weka vipande ata kuanzia vitatu na kuendelea naona inazidi kupamba moto.
 
TWENDE KAZI


7
Nilipoingia ukumbi wa disk nilitafuta sehemu nzuri ya kukaa, viti vingi vilikuwa wazi watu walikuwa ukumbini wakicheza mziki. Nikakaa kwenye kona moja itakayo niwezesha kuona karibu sehemu nzima ya ikumbi wa disko, niliwasha sigara na kuanza kuvuta wakati naangalia watu wakicheza na baada ya muda akapita muhudumu ambaye nilimuita na kumuagiza aniletee chupa ndogo ya pombe aina ya Long John. Aliniletea nikaendelea kunywa huku nikiwaza na kuwazua, nilikuwa nimekaa karibu saa moja na kitu hivi walipoingia wasichana wawili warembo sana na wamevaa mavazi nadhifu. Walipoingia waliongoza moja kwa moja na kuja kukaa kwenye meza iliyokuwa karibu yangu, muda mfupi baadae muhudumu aliwaletea bia za kopo aina ya Stella, nilishangaa kidogo kuona wasichana wawili tu aniletewa katoni nzima kwa mpigo. Walianza kunywa huku wakiongea taratibu na kitambo kidogo walikuwa wameisha kunywa nusu ya katoni na hapo sauti zao zilianza kupanda kiasi cha kuwasikia maongezi yao. Baada ya muda mfupi kidogo waliniomba niwaangalizie bia zao wakacheze disko, kwa kuwa waliona mimi ndio nilikuwa meza ya jirani yao.
Ulikuwa ni muziki wa rhumba uliopigwa na Oliver Ngoma ndio ulikuwa unapigwa nao waliucheza vizuri sana na kwa maringo hasa punde uliunganisha muziki uitwao Azaraki nao wa Oliver. Vimwana waliendelea kucheza name niliwaangalia kwa chati, baada ya kwisha mziki wa Azaraki walirudi kukaa sehemu yao. Walipo rudi sehemu yao walinishukuru huku wakinikaribisha nijiunge nao nami nilishukuru na kuendelea kukaa nilipokuwa wao waliendelea na maongezi yao huku wakizitimba bia.
Ghafla mawazo yalirudi kwa Sonno na Kikakika, nikajihisi vibaya kwa kutokuwa nao wakati huo, nilipoangalia saa yangu ilikuwa ni saa mbili na dakika ishirini na tano na Sonno alikuwa bado hajarudi. Nilitupa macho kwa wale wasichana nikaona mmoja wao akiangalia saa yake alafu nikamsikia akimaka, “Unajua huyu Patrick mshenzi sana”alimueleza mwenzie. Roho ikanishituka kusikia jina, nikatega masikio kunasa sauti zao zaidi.
“Hata mimi huwa namchukia, sijui kwa nini Moddy anamuona wa maana kiasi cha kuniacha nikastare peke yangu na yeye kuongozana naye. Mwenzie alichangia katika maongezi ya rafiki yake.
“Basi mimi ndio usiseme maana namchukia ile mbaya, sasa fikiria kitendo cha kuja kumchuka Zuberi kwangu mchana wakati akisubiri mlo ni uungwana huo”. Aliongea Yule msichana wa kwanza.
“Mimi nashangaa sana kuhusu huyu Patrick, toka wiki hii ianze amekuwa akimfuatafuata sana Moddy, mara ampigie simu aende kwake, wakati mwingine amuijie na gari. Kwa mfano usiku wa jana kampigia simu jioni akaenda na hakurudi mpaka saa tisa usiku ndio anarudi. Nilipomuuliza akanambia alikuwa kwenye mambo ya biashara” aliongea Yule mwingine.
“Kama ni hivyo inashangaza kwani hata mimi Zuberi aliniaga kuwa anakwenda kwa Patrick na sikumuona tena mpaka asubuhi ya leo, tena anakuja ananiambia hata kuwa na nafasi ya kunutoa out leo kwa sababu ana masula nyeti na Patrick.
Nafikiri ndugu msomaji hata kama ni wewe ungekuwa muhusika wa hili suala langu la wizi na kusikia maongezi haya yanayoendelea baina ya hawa mabinti ungegundua kitu kama wewe sio mpungufu wa akili. Nilianza kufikiri haraka nini nifanye ili hawa wasichana wanieleze anakokaa huyo Patrick bila wao kuwa na mashaka na mimi. Hapo likaja wazo kuwa nimsuburi kwanza Sonno maana ilikuwa mapema mno kuchukua muelekeo mwingine, hivyo nilikaa nikiwachunga kwa macho ili wasije wakaondoka bila kufahamu.
Disko lilikuwa linaendelea na watu walizidi kumiminika katika ukumbi huu wa Magnum, ghafla wale wasichana walikuja kwenye meza yangu na vikopo vine vya Stella walivyokuwa wamebakiza na kuviweka mezani huku wakiniomba niwaangalizie wakati wao wakicheza mziki. Walifanya hivyo kutokana na ongezeko la watu, walijua sio rahisi kuziacha mezani kwao na mimi nimudu kuziangalia kwa mbali.
Walicheza kama miziki mitatu hivi alafu wakaja wameshikana mikono mpaka kwenye meza yangu, hawakurudi kwenye meza yao kwani walivuta viti na kukaa huku wakinisogezea kopo moja la Stella na kuniambia ninywe. Ilionekana wazi kuwa pombe zilishawapanda kichwani, niliwashukuru kasha nikawambia kuwa huwa situmii kwani nimezoea pombe kali, walisikitika kwa kukataa kinywaji chao alafu wakaanza mazungumzo yao. Niliwasikiliza huku nikijifanya sina habari nao huku nikiyakata makali polepole, walikuwa wakiongea maongezi ya kawaida tu na tulidumu katika hali hiyo kama dakika tano hivi ndipo nilipowachokoza kwa maneno.
“Akina dada naona tumekaa meza moja lakini hatufahamiani.” Nilitoa kauli ambayo ilikatisha maongezi yao na kuniangalia alafu mmoja wao akasema;
“Unajua kaka tuliona kana kwamba hupendi bugudha ndio maana tukaendelea na maongezi yetu.” Aliongea mmoja wao.
“Sawa dada nafikiri hiyo ilikuwa tafsiri ya kihisia tu” nilisema na kuendelea “sijui wewe unaitwa nani?”
“Naitwa Mtuli.” Alijibu na kunyamaza.
“Na wewe dada unitwa nani?” Nilimuuliza mwingine.
“ Mie naitwa Monica” alijibu.
“Nyie ni wanyeji hapa? Niliuliza.
“Ndio” walijibu kwa pamoja alafu Monica akaunganisha swali, kwani wewe ni mgeni?
“Ndio” nilijibu kwa kudanganya.
“Unatokea wapi?” aliuliza Mtuli.
“Mbeya” niliendelea kudanganya
“Karibu sana Mwanza” alisema Mtuli.
“Nimeishakaribia ila nitashukuru sana nikipata wenyeji kama ninyi” nilijibu na kutupa kijembe.
Sikujibiwa ila niliunganishiwa swali kutoka kwa Monika.
“Unaitwa nani?”
“Naitwa Lyampili Mabagala” nilijibu.
“Hapa Mwanza umekuja kutembea tu au kibiashara” nilitupiwa swali linguine.
“Nimepita tu naenda Ukerewe kumuona mdogo wangu ambaye anafanya kazi huko.”
“Kumbe unaenda Ukerewe, basi mimi ndio kwetu.” Alisema Mtuli.
“Kwenu ni sehemu gani pale ukerewe?” nilimuuliza.
“Wewe unafahamu sehemu gani huko Ukerewe?” Niliulizwa badala ya kujibiwa.
“Nafahamu Muriti, Nansio na Murutunguru.” Nilijibu.
Ahaa!! Hizo sehemu zote umewahi kufika na ukapakariri vizuri?” MTuli aliendelea kunimiminia maswali.
“Sio sana ila nazifahamu.” Nilijibu kwa mkato.
“Basi mie kwetu ni pale Muriti madukani.” Alisemsa na kuendelea. “Baba yangu ni maarufu kidogo pale Muriti kama ulikaa kidogo huenda ikawa ulimufahamu.
“Anaitwa nani?” nilimuuliza.
“Anaitwa Kazobha ndie mwenye bucha la kuchinja nguruwe pale.” Alijibu.
Kwa hakika nilikuwa namfahamu kwani kule Muriti kuna ndugu zangu hata baba yake alikuwa ananifahamu ila huyu binti sikumfahamu kabisa hata yeye hakuonyesha dalili za kunifahamu. Hapo nikavunga. “Huyo mzee niliwahi kumsikia wakati nilipotembelea pale.
Mara Sonno akaingia na kuangaza kwani alikuwa hajaniona, nikampungia mkono naye akaniona na kunihuata. Alifika na kuvuta kiti kimoja kilichosalia ili kuhitimisha mzunguko wa viti vine. Tulijuliana hali kasha akawasalimia waschana wale alionikuta nao;
“Habari zenu akina dada?” alisalimu.
“Nzuri tu, sijui wewe.” Waliongea kwa pamoja.
“ Mie poa kabisa.” Alijibu Sonno.
“Karibu.” Alisema Mtuli huku akumsogezea kopo la Stella.
Sonno alichukua na kukipachua tayari kwa kunywa, alikunywa kama funda tatu hivi na kurudisha kopo kwenye meza huku akiangaza macho ukumbini, alafu akamuita muhudumu na kumuajizia kopo sita za Stella na chupa moja ya Konyagi. Vinywaji vilipoletwa aliwapa wasichana yale makopo ya Stella na kuilaza chupa ya konyagi mezani, ikawa kama unywaji ndio umeanza. Baada ya kuwa nimewatambulisha wote na kufahamiana Sonno alinikonyeza na kutoka hapo tulipokaa, kitambo name niliwaaga hawa wasichana na kuwaambia kuwa naenda maliwatoni na hapo nilimfuata Sonno aliyekuwa ametoka nje ya jingo na kuegamia gari pale maegesho.
“Vipi?” Niliuliza punde nilipofika tu.
“Huyo mtu wako nimemkuta na amenieleza kila kitu ila nimemuachia uhai sijui nimefanya makosa.” Aliongea Sonno.
“Hapana.” Hebu nipe maelezo kwa kifupi.” Nilisema.
“nilipofika nilifanya kama nahitaji chumba hivyo nililipa na akaenda kunionyesha chumba, kulikuwa na watu wanazagaasehemu hizo. Baada ya kuonyeshwa chumba niliingia kuoga na nilipomaliza kuoga alikuwa amebaki peke yake hapo nilimuita kama vile ni shida ya dharura. Alikuja chumbani na alipoingia tu nikafunga mlango na kutoa bastola”
“Hapo nilimshinikiza kujibu maswali yangu huku nikimtishia kuwa akileta ubishi amekwisha na kwa mkwala niliachia risasi moja kwenye sakafu kuonyesha kuwa sitanii kwa kuwa bastola yangu ina kiwambo sauti haikusikika. Alibabaika na kuanza kutetemeka huku akisema. “Usiniue nitajibu.”
“Chumba namba ishirini na saba kinamilikiwa na nan?.” Nilimuhoji.
“Alikuwepo jamaa mmoja hivi ambaye katoka jioni.” Alijibu.
“Ni akina nani waliingia humo zaidi ya huyo jamaa? Alisita kidogo lakini aliponiangalia usoni akaendelea.
“walikuja watu wawili wakanipa pesa alafu wakaenda kukagua humo ndani, tulikuwa nao hawakuchukua kitu chochote.” Aliongea huyo muhudumu kwa uoga.
“Nimekuuliza ni wakina nani? Na je ndio utaratibu wenu kuruhusu wateja kukaguliwa?” niliuliza huku nikisogeza bastola sikioni kwake.
“Namfahamu mmoja tu, anaitwa Patrick Mwisongo anakaa Kigoto kwenye jumba lililo kando ya ziwa.” Alisema
“Hebu nieleze vizuri kabla sijachukia na kusambaza kichwa chako kwa risasi.” Nilizidi kumchimba mkwala.
“Ukivuka pale mwaloni soko la samaki unaendelea mbele baada ya kuacha nyumba za kawaida utakuta jumba la kifahari lenye ua wa michongoma ndio jumba la kwanza la kifahari na liko mbali nyumba nyingine upande wa kushoto kama unatokea mwaloni.” Baada ya hapo nilimwambia atulie asimwambie mtu yeyote juu ya jambo hilo alafu nikampatia sh. Elfu ishirini na kuagana naye bila tatizo. Alimalia kueleza Sonno.
Mzgo unazdi kunoga
 
TUENDELEE WAKUU


“Ok kama ni hivyo tusubiri mpaka saa zisogee alafu twende kwa huyo Patrick” Nilisema na kufunga mjadala wetu huku Sonno akipitia kwenye nyama choma mimi nikaongoza tulipokuwa tumekaa na kukuta wale wasichana wakiendeleza vinywaji.
Vipi Lyampili mbona umekawia sana? Mtuli alinidaka kwa swali.
Nilipita kwa mchoma nyama ambopo nimemuacha rafiki yangu akisubiri. Nilisema.
Tulifikiri labda ndio imetoka hiyo. Alisema Monika aliyeonekana pombe zishamkamata.
Siwezi ondoka kihuni namana hiyo. Nilisema.
Wakati tunaongea Sonno alikuja akiongozana na mtu aliyebeba sinia la nyama, alipofika alivuta kiti na kukaa na Yule muhudumu mwenye sinia aliweka mezani na kuondoka.
Tuendelee na nyama ili tupunguze ukali wa hizi pombe. Alisema Sonno.
Hapo tulianza kushambulia nyama baada ya kuwa tumenawishwa na muhudumu.
Halo Mtuli, ningefurahi kama ningepata nafasi ya kuongea na wewe tena kabla sijaondoka.” Nilimwambia Mtuli
Unaposema hivyo unamaanisha leo au kabla ya kuondoka hapa Mwanza. Alihoji Mtuli.
Nina maana kabla ya kuondoka hapa Mwanza. Nilisema
Kama ni vivyo tunaweza onana kesho. Alisema Mtuli.
Wapi na saa ngapi? Niliuliza baada ya kuwa nimejibiwa.
Tuonane River Side saa saba mchana. Alisema. Wakati sie tunaongea Sonno alimuomba Monika wakaenda kucheza disko.
Kwani wewe huna namba ya simu ninayoweza kukupata kirahisi? Nilimuuliza.
Ninayo ya kazini namba 333 na tunatoka saa tisa.
Unafanyia wapi kazi? Nilimuuliza.
Idara ya maji. Alijibu.
Kwa hiyo ina maana hiyo kesho saa saba utatoka kazini na kuja River side.
Ndiyo.
Kwa nini nisikupitie pale kazini tukaenda tukaenda kupata chakula la mchana sehemu nyingine.nilieleza.
Hapana haiwezekani, kuna mchumba wangu anayejulikana pale kazini kwa hiyo itakuwa rahisi yeye kupata habari kuwa nimetoka na mtu mwingine. Isitoshe yeye ana desturi ya kuja kunichukua. Alieleza.
Inamaana iwapo atakuja kukuchukua hiyo kesho hatutaonana. Nilisili.
Najua nitakavyofanya wewe usiwe na wasiwasi tutaonana tu muda huo niliokueleza. Alisema Mtuli.kwa sauti ya unyonge na aibu kidogo tofauti na alivyokuwa anaongea mwanzo. Nikajua ana uhakika na anachokisema.
Ilipofika saa sita na robo akina Mtuli waliaga kutaka kuondoka hapo Sonno aliwaambia awapeleke kwa gari lakini Monika alikataa, akasema wanayo gari huku akitoa funguo, tukapeana mikono ya kwa heri na wao kuondoka.
Tuliendelea kukaa pale huku tukiangalia watu wanaocheza disko, hatukutaka kuendelea na unywaji kwa kuwa tulikuwa tunasubiri muda wa kwenda kwenye mapambano. Nilimweleza Sonno kuhusu maongezi niliyoyasikia kutoka kwa Mtuli na Monika naye akaunga mkono huenda wakawa wapenzi wa wabaya wetu. Nilipomwambia kuwa nimeahidiana na Mtuli tuonane kesho alisema nimefanya jambo la maana sana.
Ilipofika saa saba na nusu usiku tulianza safari ya kwenda kwa Patrick na kuacha watu wakiendelea kusakata disko. Haukupita mda mrefu tukawa tumefika soko la mwaloni na tulipolipita eneo la soko tuliendelea mbele kidogo na kutafuta sehemu nzuri tukaegesha gari.
“ Inabidi tuitafute hiyo gari kwa mguu tokea hapa” Nilimweleza Sonno.
Tulifunga gari vizuri na kuanza mwendo wa miguu, baada ya mwendo wa dakika tano tukawa tumefika usawa wa jengo tuliloelezwa lilikuwa usawa wa mita kama mia mbili hivi kutoka barabara kuu. Tuliendelea mbele kama hakuna tulilolona, baada ya kupita eneo hilo mwendo wa hatua kama thelathini hivi tuliona kinjia kidogo kinachopitia kwenye nyasi kwenda ufukwe wa ziwa Victoria kwa upande huo. Nafikiri kilitumiwa na wavuvi au wanaoenda kuchota maji na kuoga ziwani.
Tulikata kona na kufuata hiyo njia na jengo tunaloliendea lilikuwa mkono wa kushoto, tulipotokeza kando ya ziwa tuliona miamba iliyoingia mpaka ndani ya maji hapo tulikata kushoto tukawa tunaelekea kwenye jingo kwa nyuma huku tukitemdea kwenye mchanga wa kando ya ziwa Victoria. Baada ya kwenda mbele kidogo tulikutana na mwamba uiokuwa umeingia mpaka ziwani.
Nilivua nguo na kumwabia sonno anisubiri hapo ili nizunguke nikaangalie upande wa pili, nilibaki na chupi tu nikachukua na bastola yangu moja maana nilikuwa nimebeba mbili. Niliyaingia maji na kuanza kutembea kuuzunguka ule mwamba, haukufika mbali sana, maji yalipofika usawa wa kitovu nilikuwa tayari mbele ya ule mwamba. Niliendelea kuzunguka huku nikiwa na tahadhari bastola mkononi, sio kwamba niliyaogopa maji ila nilichuka tahadhari ya ulinzi dhidi ya adui yeyote.
Nilifika upande wa pili bila matatizo na kujikuta karibu na ua wa michongoma uliokaribu kugusa maji ya ziwa, kwa upande mwingine ardhi ilikuwa imepanda juu na kukaribia kilele cha jabari. Nilisogelea ua kwa kuzama ndani ya maji huku kichwa na bastola tu ndio vikiwa nje, hapo niliweza kuona upande wa ndani ya ua kulikuwa na jumba la kifahari na nyumba nyigine ndogo pembeni ambayo nilihisi ilikwa stoo au nyumba ya wafanyakazi. Nikatambua hapo patakuwa kwa Patrick kutokana na maelezo niliyokuwa nayo. Nilirudi upande wa pili nikapanda jabari na kuchungilia upande wa pili nilipomuacha Sonno nikaona kivuri cha Sonno yeye hakuweza kuniona kutokana giza, nilimsogelea huku nikiwa juu ya jabari nilipofika karibu nilichuchumaa na na kumuita. Alinyanyua kichwa juu kuniangalia nikamwambia kwa sauti ya chini anirushie nguo naye akafanya hivyo nami nilivaa haraka haraka na baada ya kuvaa nililala juu ya mwamba na kumpa Sonno mkono lakini haikugusana ilikuwa imebakiza umbali wa futi moja na nusu hivi katikati. Hapo nilinyanyuka na kutoa mkanda wa suluari yangu nikamsogezea akaushika na kuanza kujivuta nao huku miguu yake ikiwa anakanyaga kwenye jabari.
Baada ya kuwa amefika juu tuliongozana mpaka kwenye ua wa nyumba tulisimama mwisho wa ua kwa upanda wa ziwani. Ile nyumba ilikuwa na mlango wa mbao ukiangalia ziwani na taa kubwa juu ya mlango nyumba ndogo iliyokuwa pembeni kidogo karibu na ua mlango wake ulitazama katikati ya ua, hatukuweza kuona mlangoni kwani tulikuwa kwa pembeni lakini tulijua kuna taa kwani mwanga ulikuwa unatokeza kwa mbele kwanye geti kutazama barabara kuu hatukuweza kuona kuna nini kutokana na nyumba kutukinga.
Kulionekana hakuna ulinzi wowote lakini lakini nilijua lazima kule mbele getini kutakuwa na ulinzi. Nilimwambia Sonno asimame hapo anilinde wakati mimi ninatembelea tumbo kuelekea nyuma ya ile nyumba ndogo. Nililala chini na kuanza kusota kwa tumbo huku nikiambaaambaa chini ya kivuli cha michongoma iliyokatwa kiustadi.
Nilifanikiwa kufika nyuma ya hiyo nyumba ndogo na kuona dirisha kwa upande niliopo, lilikuwa dirisha la vioo na nilijinyanyua polepole na kulisogelea dirisha ambalo lilikuwa limefungwa na ndani kulikuwa na pazia hivyo sikuweza kuona ndani ila taa ilikuwa inawaka. Niligeuka kumwangalia Sonno ambaye mda wote alikuwa makini na mimi, nilimpa ishara ya kumwabia anifuate naye akanifuata kwa njia niliyoitumia. Hapo nilianza kusogea pembeni ya ukuta ili nione sehemu ya mbele kwenye geti ndipo nilipoona kubanda kilichojengwa nusu ukuta na ndani yake kukiwa na meza na simu. Kwenye kiti alikaa mtu aliyeweka mikono juu ya meza na kulaza kichwa chake. Kwa upande huu ukuta wa nyumba kubwa ulikuwa na madilrisha mawili ya vioo kila karibu na pembe ya ukuta. Wakati wote huo Sonno alishafika na alikuwa nyuma yangu huku tumepeana migongo, nilimwambia anilinde nimfuate Yule mtu aliye kule getini. Kabla sijalala chini kuanza safari tukasikia muanguko wa kitu ndani ya nyumba tuliyokuwepo tukatulia. Wakati wote taa zote zilikuwa zinawaka nasi hatukupenda kukata umeme kwani tulihofia kuwashitua kabla hatujawa na uhakika na mpango wetu wa kumuokoa Kikakika.
Hakuna kilichoendelea humo ndani baada ya kuwa tumesikia muanguko wa kitu, Sonno alinyata na kusogelea dirisha aliangaza dirishani alafu akatega sikio. Baada ya muda kitambo alirejea nilipo na kuniambia kuwa amesikia minongono humo ndani, nani nilijisogeza pale dirishani wakati yeye alibaki pale nilipokuwa mwanzo. Nilisogeza sikio kwanye nyufa za dirisha nikasikia minong'ono ya chini chini ambayo haikuniwezesha kusikia maongezi ambayo yaliendelea. Nikirudi kwa Sonno na kuniambia awe making sana na hao watu kwani mimi naenda kwa yule mtu wa getini asije akawa kizingitii kwetu.
Nililala chini na kuanza kutembelea tumbo kuelekea kwa huyo mtu, niliendelea mbele bila matatizo, nilipofika usawa wa hicho kibanda nilielekea ubavuni mwa kibanda chini ya ukuta wa kibanda. Kutokana na mwanga uliokiwepo Sonno alikuwa akiniona vizuri, niligeuka kumwangalia akanionyesha ishara kuwa bado kalala. Nilijivuta nikachuchumaa alafu nikatembea kwa mtindo wa pekee kuelekea kwenye mlango wa kibanda huku nikiwa nimechuchumaa ili nisitokeze kwa juu ya ukuta.
Nilipofika mlangoni nilichungulia ki mtindo nikiwa katika hali ile ile ya kuchuchumaa, niliona bunduki aina ya sub machine gun ikiwa mapajani mwake. Nilisimama ghafla bastola mkononi tayari kwa lolote lakini alionekana kukolewa na usingizi kwani hakuonyesha dalili yoyote ya kushituka. Nilisogea mpaka alipokuwa nikaitoa mapajani mwake ile bunduki yeye hana habari. Niliishika ile bunduki mkono wa kushoto na bastola mkono wa kulia alafu nikamgongagonga na mdomo wa ile sub machine gun kichwani ili ashituke. Aliposhtuka na kugeuza shingo akakutana na midomo ya siraha mbili ikimuangalia. Jasho lilimtoka alitahayari sana kiasi cha kutoka kwenye kit na kuanza kurudi nyuma huku mikono akiwa amenyoosha juu bila kuambiwa.
"Simama hapo hapo" nilimuungurumia akasimama huku miguu ikimtetemeka kwa hofu.
"Unamlinda nani hapa" nilimuuliza kwa sauti nzito ya kukoroma isiyosikika mbali
"Patrick" alijibu kwa kuilopoka.
"Yuko wapi" nilimuuliza.
"Ametoka mda mrefu hajarudi" alijibu.
"Yule mtu waliyemteka yuko wapi?"
"Yupo nyumba ya nyuma na akina Sifongo?" Alijibu.
"Wako wangapi?" Nilimuuliza
"Wapo wawili na mateka wa tatu" alijibu
"Kwenye nymba kubwa Kuna nani?"
"Yupo Ebby kwenye chumba cha mawasiliano yote hayo alijibu akiwa kwenye mchanganyioko wa usingizi na hofu ya kuona siraha mbele yake. Mara alianza kubadilika sura nikajua usingizi na hofu vimeaanza kumtoka.
"Unaniuliza maswali hayo ukiwa kama nani?" Aliuliza.
"Usitake kujua lililopo ni kufuata amri yangu" nilimjibu kifedhuri.
"Toka nje ukiwa hivyo hivyo na uongoze kwenye nyumba ndogo ukifika gonga mlango nataka ufunguliwe, jeuri yoyote itakufikisha ahera." Alitoka akiwa mikono juu akaongoza njia kuelekea nilikotaka. Tulipofika katikati ya kibanda na nyumba kubwa ghafla bila kutegemea alijirusha hewani huku akijiviringisha kwa kurudi nyuma na kunitandika teke moja la kidevu, nilifumba na silaha zikaanguka pembeni, alirusha teke jingine nikaliona na kulipisha akainama kutaka kuchukua bastola, hapo nikamuwahi kwa teke la mbavuni akapepesuka na kuguna kidogo. Akawa amesimama kunikabiri nami vilevile, alitisha kama anapiga ngumi ya kulia alafu akarusha ngumi ya kushoto ambayo niliiona na kuinama chini kidogo ikapita juu na hapo nikiwa nimeinama niliachia ngumi mbili tatu za haraka kwenye makende yake akatoa mguno mkali na kuanguka chini.
Nilimsogelea kumuangalia na kukuta eshakata kamba. Nilimuangalia Sonno aliyekuwa wakati wote akituangalia toka mafichoni akanipa ishara nimufuate. Nilipofika akanionyesha niangalie kwenye mlango wa nyumba kubwa, kuangalia nikaona mtu kaanguka chini huku bunduki ikiwa pembeni yake. Akanieleza wakati tukiwa kwenye mapigano na yule bwana huyo mtu alitokeza mlangoni kwa tahadhari na kuanza kutembea kwa kunyata, alimuona na kumuwahi kwa risasi mbili za shingo. Nami nilimueleza maelezo ya yule marehemu na tukaamua kuingia ndani ya hicho kijumba.
Nilikwenda dirishani kusikiliza kama kuna dalili ya watu kuwemo ndani lakini nilikuta kimya. Nilirudi kwa Sonno tukaongoza mlangoni kwa kunyata huku bastola mkononi. Tulipofika mlangoni nilimwambia Sonno anilinde mimi naingia ndani.
Nilivuta pumzi na kuruka kwa kuupiga teke mlango na kuupasua mlango. Nilipotua ndani nilijiviringisha sakafuni na kumuona mtu mmoja aliyekuwa nyuma ya mlango akitahamaki na kunyanyua bunduki kunilenga, nilimuwahi kwa risasi tatu za kifua. Nilipogeuka katika mzunguko wangu wa hapo chini nikaona mtu mwingine ameegemea ukuta huku damu zikiwa zinamtoka tumboni. Nikajua kazi ya Sonno hiyo.
Sonno alikuwa amesimama mlangoni huku akitabasamu na bastola mbili mikononi. Aliniambia nimfungue Kikakika aliyekuwa amefungwa kwenye kiti huku amezirai huku yeye akiwa mlangoni kuangalia usalama.
Nilimsogelea Kikakika aliyekuwa uchi wa mnyama, nilipomuangalia vizuri wakati namfungua kamba niliona kachanwachanwa na nyembe mgongoni huku damu zikiwa zimegandamana. Nilimaliza kumfungua na kumbeba mpaka kwa Sonno. Sonno alipomuangalia alisisimka na kukunja uso alafu akasema "wamemtesa sana, hebu angalia hata sehemu za siri zimebabuka" kweli nilipoangalia nikaona nikaona sehemu ya kichwa cha uume imebabuka.
Sonno aliniambia nimuweke chini alafu nimlinde yeye akafanye upekuzi wa haraka kwenye ile nyumba kumbwa. Nilimuweka chini Kikakika aliyekuwa akihema kwa mbali na kumfuata Sonno. Tulifika kwenye nyumba kubwa Sonno alisukuma mlango akaingia ndani Mimi nikabaki mlangoni.
Aliingia chumba kimoja baada ya kingine na kitambo kidogo akatoka na mfuko wa khaki na bahasha alafu akaniambia Kuna chumba kimoja kina mitambo ya ajabu ya mawasiliano. Hapo nilimuambia akachukue gari alilete huku ndani tuondoke. Alipotoka kuendea gari mimi niliingia ndani ya ile nyumba, nilienda kwenye hicho chumba cha mitambo ya mawasiliano na kukisambaratisha kwa risasi kadha wa kadha. Mitambo yote iliharibiwa na risasi.
Gari ilifika, nikambeba Kikakika aliyekuwa bado kapoteza fahamu na kumuweka ndani ya gari. Nilimwambia Sonno aongoze Mwanza South kwa mkuu wa ofisi za hapa ili tupate msaada. Naye akafanya hivyo.
Ilikuwa saa nane na dakika ishirini wakati tulipofika kwa huyo mzee. Sonno alipiga honi na kwenye geti akajitokeza mlinzi, nikashuka kwenye gari na kumfuata.
"Habari za saa hizi?" Nilimsabahi.
"Nzuri" alijibu huku akiwa na wasiwasi. Nafikiri ni kutokana na kuwa usiku sana hivyo nilionelea nimtoe wasiwasi.
"Unanikumbuka?" Nilimuuliza.
"Nakufananisha lakini sikukumbuki." Alijibu.
Wakati wote tulikuwa tunaongea yeye yuko ndani ya geti mie nje.
"Nilikuja usiku wa kuamkia jana nikaacha hapa pikipiki" nilimueleza.
"Ahaa!" Sawa, sasa nimekumbuka alisema akionyesha uso wa kirafiki tofauti na mwanzo.
"Sasa mweleze mzee mimi nipo hapa nje nataka kumuona" nilimueleza.
"Lakini mzee huwa hataki kuamshwa usingizi I." Alisema yule mlinzi.
"Kwa masuala yangu nafikiri atafurahi ukimuambia" nikisema.
"Sawa ngoja nijaribu" alikubari kwa shingo upande huku akigeuka kwenda kwenye kibanda na kuchukua simu. Mie nilimsubiri hapo getini. Sonno alishazima taa za gari na injini akabaki garini kimya. Mlinzi alizungusha namba za simu na kusubiri kidogo. Baadae nilimuona akiongea alafu akarusha mkono wa simu na kugeuza kuja kwangu. Alipifika alinifungulia geti na kuniambia niende ndani, nilimuambia Sonno anisubiri kwa sauti alafu nikaongoza ndani. Kabla sijafika nyumba taa za sebuleni ziliwashwa nikajua mzee mwenye nyumba tayari yupo macho. Niliongoza mlangoni na kugonga, kitambo kidogo mlango ukafunguliwa na mzee mwenyewe huku akiwa amevaa pajama na makubazi chini. Nilimsalimia baada ya kuwa nimeingia ndani na kukaa. Baada ya hapo sikuwa na maelezo mengi zaidi ya kumueleza suala lililonileta.
"Kuna mwenzetu mmoja alikamatwa mchana na watu ambao nao walikuwa wanazitaka zile dhahabu lakini tumefanikiwa kumuokoa ila hali yake ni mbaya tunahitaji msaada wa matibabu kwani mpaka sasa kazimia ndani ya gali" nilimueleza.
"Nimekuelewa kijana, hebu subiri kidogo" aliongea huku akinyanyuka na kuiendea simu iliyokuwa mbali kidogo. Aliifikia na kuanza kuzungusha namba ilipopokelewa alianza kuzungumza na baada ya mazungumzo ya kwenye simu alirudisha simu sehemu yake na kurudi sehemu aliyokaa mwanzo.
"Sasa kijana nenda umpeleke huyo mgojwa katika zahanati iliyopo mtaa wa Nera iitwayo MAGAMBO, ipo kwenye barabara inayoteremka kutoka karibu na manispaa ya hapa. Utamkuta daktari akikusubiri nimeishaongea naye kila kitu. Nenda mkapate matibabu tu hamtadaiwa malipo yoyote." Alieleza yule mzee.
Tuliagana na kurudi mpaka kwa Sonno baada ya kumuaga mlinzi na kuingia ndani ya gari, tuliongoza moja kwa moja kwa zahanati
 
Kama naangalia muvi ila mkuu weka vipande ata kuanzia vitatu na kuendelea naona inazidi kupamba moto.
Polepole tutafika unajua mzigo huu up natoka jikoni na kutua hapa. Hivyo uwezekano wa kuweka vipande vingi ni mgumu .
 
TUENDELEE



8
Saa kumi na mbili tulikurupuka kutoka usingizini, tulikuwa tumelala kwenye gari tulilopaki karibu na kabisa la sabato kirumba. Tuliogopa kurudi mahotelini kwetu kutokana na msako wa Patrick, hasa kwangu mimi ambaye tayari nilishapekuliwa kule chumbani kwangu Hotelini. Tuliegesha pale gari baada ya kuwa tumetoka kumpeleka Kikakika zahanati usiku ule.
Wakati sisi tumetoka kumuokoa Kikakika, haikupita mda mrefu mara Patrick akafika nyumbani kwake na watu wake wakitoka kwenye msako wa kunisaka.
Patrick alishituka mara tu alipokata kona ya kuelekea kwenye nyumba yake na kuona geti likiwa wazi. Alikamyaga breki ghafla na kuwaambia wenzake wateremke haraka na kuondoa gari huku wenzie wakija kwa mguu kwa kujificha ili waweze kumuokoa iwapo kutakuwa na mushkeri. Aliuliza na kusimama karibu na nyumba ndogo ambapo aligungua mlango wa gari na kujirusha huku akijiviringisha hewani mpaka kwenye ukuta wa nyumba karibu na mlango uliokuwa umerudishiwa tu. Alichomoa bastola na kuupiga mlango teke ukakubali, alichokiona ndani hakuamini alijikuta akisema peke yake "watajua mwiso P ni nani." Alisogea akasimama katikati ya chumba alafu kama aliyekumbuka kitu akatoka akikimbia mpaka kwenye nyumba kubwa. Kabla ya kuingia akakutana na maiti ya Ebby mlangoni akashikwa na bumbuwazi! Wakati huo Gilly Moddy na Zuberi na kumuangalia. Alitikisa kichwa na kuwaambia wamsubiri hapo nje kwanza. Aliingia ndani kwa tahadhari kubwa huku kashikilia bastola mkononi. Aliingia chumba kimoja baada ya kingine na alipogika chumba cha mawasiliano aliguna huku bastola ikimdondoka. Hakuwa na hamu mwili wote ulimuishia nguvu alipoona uhalibifu wa humo ndani.
"Gilly" alisikika akiita kwa sauti baadae.
Gilly aliingia baada ya kusikia akiitwa, aliongozana na wenzake na kukuta Patrick akiwa na sura ya huzuni.
"Hawa wa washenzi wametuganyia vibaya sana, kwanza wameua wenzetu alafu wameharibu mitambo yetu ya mamilioni ya fedha. Sasa nipeni mpangilio mzima wa haya mambo, maana mimi akili haifanyi kazi kwa sasa" alisema Patrick huku akimwangalia Gilly kwa macho ya mategemeo.
Gilly alikohoa kidogo na kuanza kueleza mawazo yake; "Mimi nafikiri boss Mwiso P tuchukue suala moja la maana ambalo litakuwa ni kuwaua tu pindi tukiwapatia nafasi, kwani suala la kuwahoji waeleze wapi ilipo mali ni gumu sana. Kulingana na mateso aliyopata yule mtu jana, sikutegemea kuwa asingesema chochote" alieleza Gilly.
Baada ya maelezo hayo ya Gilly akili ya Patrick ilishakaa sawa kutoka kwenye bumbuwazi,
"Sawa nimekuelewa kwa hiyo kuanzia Sasa inabidi tubadili mpango kazi, tukiwatia machoni tu ni kuwamaliza, potelea mbali hata iyo mali tukiikosa lakini lazima wakawasiliane na kuzimu" alisema Patrick kwa uchungu.
"Sasa boss tutawapataje iwapo watakuwa wameamua kuondoka usiku huu?" Aliuliza Moddy kwa uchungu.
"Najua haitakuwa rahisi kwao kuondoka kwa wakati huu kutokana na jinsi mwenzao alivyo itabidi apate matibabu kwanza. Vinginevyo mauti itamkuta." Alieleza Patrick na kuendelea; " kwanza kwa sasa tukusanye hizi maiti na kuziweka panapostahili. Baada ya hiyo kauli wote walitawnyika na punde kidogo kila mtu alirudi na maiti na kuziweka kwenye jokofu kubwa. Zilikuwa maiti nne na moja ilikuwepo ndani hivyo jokofu lilibeba maiti tano. Baada ya kuziweka zote vizuri walifunga jokofu na kurudi sebuleni.
"Hawa washenzi wametutia hasara isiyo kifani" aliongea Patrick huku akiwa kasimama. Kuanzia sasa hivi tunatakiwa macho yetu tuyaweke kwenye hospital ili tuweze kugundua alipowekwa yule mtu wetu. Nina Imani atakuwa anapata matibabu, tutakapo jua alipo kitakachofuata ni kumsafiriaha ahera bila mjadara. Ameishatupotezea wenzie wetu watano hivyo kwa yeyote atakayempatia nafasi ya kumuua ni rukhusa." Alieleza Patrick.
Mara simu ililia, Patrick akakatisha maongezi na kuchukua simu tayari kwa maongezi.
"Hallo, Patrick hapa." Alisema kwenye simu.
"Wanna See anaongea hapa" ilisikika sauti upande wa pili alafu aliyejibu akaendelea kuongea. "Nimewatafuta kwa mawasiliano yetu ya kawaida sikuwapata, vipi Kuna nini huko?" Alimaliza kwa swali.
Patrick alimueleza yote yaliyotokea kwa mafumbo ambayo wanaelewa wao tu. Baada ya Wanna See kusikiliza maelezo yote alisikika akisonya alafu akaanza kuongea;
"Inaonekana huko unafanya biashara uchwara, yaani unashidwa kuidhibiti hiyo bidhaa mpaka inatapakaa madukani. Sasa mimi nakuja huko pamoja na faili za mikataba mingine miwili. Nitegemee kufika kesho saa tano na ndege ya Air Tanzania inayotoka Nairobi. Nategemea kuondoka hapa muda mchache ujao kwa ndege inayokwenda Kenya. Mengi tutaongea huko nikifika" Alimaliza kuongea Mr Wanna See na kukata simu bila kusikiliza zaidi kutoka kwa Patrick. Alikuwa ni mwenye hasira Kali kutokana na kushindwa kwa Patrick. Hapo alikuwa Pretoria Afrika Kusini, aliondoka na vijana wake wawili wa kazi kuja Tanzania kutokana na uzito wa suala lililojitokeza. Licha ya kuzidiwa akili katika wizi wa dhahabu bado kulikuwa na jipya lililojitokeza kuhusu Pheady.
Baada ya simu kuwa imekatwa ghafla vile. Patrick alirudisha mkono wa simu na kutoa sigara akawasha na kurudi katika maongezi na vijana wake wa kazi; " Nilikuwa naongea na Wanna See, inaonekana kakasirishwa sana na mambo yalivyo amedai atafika hapa kesho saa tano." Alisema Patrick baada ya kuwasha sigara na kuvuta kama mikupuo miwili hivi alafu aliendelea: "Kwa hiyo lililopo sasa hivi tuchukue mait za wenzetu tukazidumbukize ziwani kwani hatutakuwa na nafasi tena baada ya Wanna See kufika. Mambo yanaweza yakabadilika maana amesema anakuja na watu wawili zaidi.
"Sasa boss Patrick hatuwaziki kwa heshima zao?" Aliuliza Zuberi.
"Tungefanya hivyo lakini kutokana na ujio wa Wanna See huenda kukawa na pilikpilika nyingi kiasi cha muda kuwa mfinyu hivyo tukaendelea kukaa na maiti ndani ambalo ni Jambo la hatari." Alijibu Patrick.
"Okey, naona la muhimu ni kupata usafiri wa kumpeleka hizi maiti katika kina kieefu cha maji." Alisema Moddy ambaye muda mwingi alikuwa kimya.
Baada ya kutoa kauli hiyo Patrick aliingia ndani ya chumba kimoja na kutoka na furushi la box baada ya kulifungua alitoa kitu kama tube ya gari lakini kubwa zaidi. Aliongozana na wenzie mpaka nje kwenye gari akachukua mrija furani na kuchomeka sehemu fulani ya hiyo tube alafu akapanda ndani ya gari na kuliwasha huku akipiga less kama mtu anayepasha injini motoi vile. Baada ya mda kidogo lile tube lilijaa upepo na kuwa mtumbwi mkubwa tu wa kuweza kuwekwa injini nyuma.
Walitaka kuweka injini lakini walighairi ili kuhepuka kukamatwa na askari wa doria ziwani iwapo wangesikia muungurumo wa injini. Hivyo wakaamua kutumia kasia ambazo Patrick alizifuata ndani. Zilikuwa kasia za plastiki. Walichukua maiti na kupanda watu watatu Patrick alibaki, walichukua na mawe ya kuzifunga zile maiti zisije zikaelea juu ya maji. Baada ya hapo waliondoka na kwenda kutupa zile maiti ziwa Victoria.
Baada ya kuwa wamerudi kutoka kutupa maiti walikubaliana walikubariana walale palepale wote kwani muda wa mapambazuko ulibaki mchache. Nao wakafanya hivyo huku wakiwa na mkakati wa kufanya uchunguzi kwenye hospitals kesho asubuhi kabla ya saa tano ili atakapo kuja boss wao kutoka Afrika Kusini Ndugu Wanna See, wawe na la kumueleza.
Baada ya kuwa tumetoka kwenye maegesho yetu kule tulipolala karibu na kanisa la Sabato kirumba, tulielekea kwa dada yangu nilikotunza zile mali. Tulipofika nilimuambia kuwa ndio narudi kutoka Bukoba, alitundalia kifungua kinywa wakati tunaoga. Tulipokuwa tumemaliza kuoga tulipata chai nzito huku tukiendelea na mazungumzo ya kawaida. Wakati huo ilikuwa inakaribia saa mbili na nusu, baada ya kupata chai nilimuambia dada tunahitaji kupumzika kidogo kutokana na uchovu wa safari. Alituelekeza chumba cha kwenda kupumzika, chumbani kulikuwa na vitanda viwili simu ya mezani pamoja na kabati la nguo lenye kioo cha kujiangalia. Baada ya kutuonyesha yeye aliendelea na hamsini zake.
Tulipokuwa ndani ya chumba tayari tushafunga mlango, nilinyanyua kiwiko cha simu na kuzungusha namba za zahanati tuliyompeleka Kikakika. Niliposikia upande wa pili unanyanyuliwa nikaitoa;
"Hallo"
"Hallo nani mwenzangu?" Sauti kutoka upande wa pili ilisikika.
"Pheady hapa, nataka kuongea na daktari mkuu." Niliongea.
"Subiri kidogo" ilisikika tena hiyo sauti kwenye simu. Baada ya sekunde kadhaa ilisikika sauti nzito ya daktari. " Hallo daktari hapa unasemaje ndugu?"
"Mimi naitwa Pheady nilileta mgonjwa toka kwa mzee Magesa jana usiku hivyo nataka kujua khaki ya mgonjwa. Nilieleza. Magesa ndie boss wa ofisi zetu hapa Mwanza.
"Ohoo! Ni wewe kijana, Khali ya mgonjwa inaendelea vizuri, ameishazinduka ila ana maumivu hawezi kutembea. Imebidi tumshone kidogo sehemu za mgongoni" daktari alieleza.
"Je uwezekano wa kuongea naye upo?" Nilimuuliza.
"Hakuna wasiwasi we njoo wakati wowote nitakuwepo, isipokuwa kuanzia saa saba mpaka saa Tisa." Alijibu.
"Sawa daktari, nitakuja kumuona muda utakaponiruhusu"
"Okay, kwa heri"
"Sawa"
Nilirudisha mkono wa simu baada ya kumaliza maongezi na daktari, nilimueleza Sonno maelezo niliyoyapata kwa daktari naye alifurahi kusikia Kikakika ameishazinduka. Tulijipumzisha mpaka ilipofika saa sita hivi ndio tukawa tumeamka na kwenda kuoga tena. Baada ya kumaliza kuoga tuliandaliwa chakula na kula. Baada ya hapo tulikaa sebuleni na dada tukiongea mazungumzo ya kawaida huku tukiangalia runinga. Ilipofika saa nane na nusu dada aliondoka kwenda kwenye biashara zake akatuacha na mfangakazi pamoja na watoto waliokuwa wamefika kutoka shule. Sie tukiendelea kuangalia vipindi vya runinga ambapo wakati huu tukiangalia ngumi za kimataifa zilizokuwa zikionyeshwa na stesheni moja ya Kenya.
Ilipotimia saa Tisa na nusu tuliondoka kwenda kumuona Kikakika kule zahanati, tulipofika tulimkuta daktari msaidizi akiwa mapokezi na wagonjwa. Tulimsalimia na kumuuliza iwapo daktari mkuu tumemkuta. Alisema yuko chumba cha tatu katika vyumba vilivyojipanga pembeni ya korido. Tulielekea tulikoelekezwa na kukuta akiwa anapekuwa mafaili.
"Habari za saa hizi daktari?" Tulimsalimia kwa pamoja
"Salama tu, na nyie habari za toka jana?"alijibu na kuuliza.
"Nzuri, tumekuja kumuona mgonjwa wetu" nilimjibu na kueleza.
"Sawa, twende mkamuangalie" daktari alijibu na kusimama akatuongoza kwenye korido mpaka chumba cha pili toka mlangoni. Aligungua mlango tukaingia ndani na kukuta kukiwa na wauguzi wawili pamoja na vitanda kama sita hivi kwa akili ya wagonjwa. Kati ya hivyo vitanda ni vinne vilivyokiwa na watu. Tuliwasalimia wale wauguzi wa kike alafu tukaenda kwenye kitanda alichokuwa amesimama daktari. Kikakika alikuwa amelala usingizini, daktari akamuamsha. Aliposhtuka usingizini na kutuona alitabasamu na kunyanyuka polepole akakaa kwenye kitanda.
"Pole sana Mr Kikakika" alisema Sonno, wakati huo daktari alishaondoka.
"Asanteni sana rafiki zangu" alijibu Kikakika.
""Vipi unajisikiaje?" Nilimuuliza.
"Sasa hivi najisikia vizuri kiasi sio kama asubuhi." Alijibu.
"Je unaweza kutembea kidogo?" Aliuliza Sonno.
"Ndio, lakini kwa shida maana vidonda nilivyoshonwa bado vibichi..
"Ilikuwaje mpaka yakawa yametokea yote hayo?" Nilimuuliza.
"Daa!! Ilikuwa hatari sana, sikutegemea kama ningekuwa salama hata Sasa. Wale watu washenzi sana na nikipona lazima watanitambua hata kama itachukua mwaka mbele lazima wayaone machungu ya maisha." Aliongea Kikakika kwa uchungu alafu akakatisha na kuomba maji ya kunywa, alikunywa kama birauli mbili hivi alafu akaendelea kuongea: baada ya kuachana na wewe pale benki, mimi nilienda kwenye duka moja pale stendi ya taxi kulikuwa na kitu nahitaji. Nilipofika kwenye hilo duka linaloitwa Bamboo shop nilifanya manunuzi yangu yaliyo nipereka pale. Wakati natoka nilielekea barabara ya mtaa wa Makoroboi na kabla sijafika Jafaries Hotel nikashtukia gari inapaki pembeni yangu nilipogeuka kuangalia nikajikuta naangaliana na midomo mitatu ya bastola huku mlango wa mbele ukifinguliwa na kuamlishwa niingie ndani ya gari. Sikuwa na ujanja kwani kwa vuovyote vile wangenitia risasi kama ningeleta maskhara. Nikatii na kuingia kwenye gari, kwanza nilifikiri ni askari kanzu. Lakini baada ya kufikishwa kwao na kuanza kuhojiwa ndio nikajua ni wamoja na yule niliyemuua kule Nyakato. Walinitesa sana ili niwaambie Ilipo dhahabu. Niliposhindwa kuwaambia zilipo ndopo wakanibadilishia somo na kuhoji ulipo wewe Pheady. Kutokana na kushindwa kuvumilia mateso waliyonipa ikabidi nitaje hotel uliyofikia. Wakatoka kwenda kukutafuta."
"Baadae wakarudi na kuendeleza mateso yao ili niwaeleze unaweza kuwa wapi kwa wakati huo. Nilikuwa nakumbuka ahadi yetu ya kukutana kule Magnum Club lakini sikuweza kuwaambia nikihofia kuvuruga kila kitu. Inavyoonekana wale jamaa wanakufahamu sana maana wamenionyesha na picha zako ukiwa na ile pikipiki pamoja na jina lako ila wanajua tupo wawili tu katika hili suala, Wala Sonno haeleweki. Katika maelezo yao inaoneka walikufahamu wewe kwanza ila mimi nimekuja kujulikana baada ya kuonekana nikiongozana na wewe kwani inaonekana walituona kabla ya kuingia banki. Baada ya hapo wakaona itakuwa rahisi kunipata mimi kutokana na kutoka kwa mguu na kuanza kutembea. Pamoja na mateso waliyonipa vilevile walinipiga sindano ya usingizi kwa kuhofia ninachoweza kufanya ikiwa nitakuwa na fahamu zangu. Nilishangaa sana nilipozinduka na kujikuta hapa, nilipomuuliza daktari ndipo aliniambia nileletwa na Pheady, hapo nilishangaa maana sikutegemea kama mngeweza kugundua kirahisi nilipo na kuja kuniokoa. Hebu na nyie nielezeni ilivyokuwa mpaka kunipata." Alimaliza Kikakika na kutoa hoja.
Nilimueleza Alfa mpaka Omega kuhusu tulivyofanikiwa kumpata naye akafurahi kwa roho ya upendo tuliyomuonesha. Tulikuwa tumeongea vya kutosha ndipo nilipobadili maongezi; " Naona ukipata nafuu tu tuondoke mji huu maana naona unanuka mauti. Mali zetu tutaziacha mpaka pale mambo yatakapotulia, maana askari nao wapo chonjo sana. Tumesikiliza taarifa ya habari ya saa saba inasema kuwa katika msako unaoendelea hapa, wameishakamatwa majambazi kama tisa hivi. Kwa hiyo tutakapoondoka hapa Kuna haja ya kuacha siraha zetu. Kwani katika njia zote zitokazo Mwanza wakikuhisi vibaya tu, unakaguliwa maana kuna vizuizi vya askari barabarani." Nilieleza.
Sonno naye aliongezea: " Hata Mimi nilikuwa na mawazo kama hayo kwani kuendelea kukaa hapa ni kuwapa nafasi akina Patrick kutufanya wanavyotaka. Kitu ambacho sitaki kitokee wakati watu tumeishashinda ushindi uzuri kilichobaki ni matumizi tu" aliongea Sonno.
"Sawa mie sina nyongeza, ngoja tuangalie Khali itakavyokuwa kesho na keshokutwa maana hata mimi sitaki vuramai wakati nikiwa na hali kama hii. Ila nitakapopona nitarudi kuja kuwaadabisha hawa washenzi. Ni lazima waupate uchungu wa maisha kana Mimi" Alisema Kikakika akiwa ameukunja uso mfano wa mtu anayenusa harufu mbaya.
Ilikuwa kwenye saa kumi na moja kasoro hivi tulipoaga hapo zahanati na kuondoka huku tukipanga kuja tena kesho kumjulia hali mwenzetu. Tulipanda kwenye gari letu na Sonno akashika usukani naikamuambia aongoze kwa dada. Sikutaka kuzurura mtaani isije ikawa taflani baadae.
Wakati sisi tunaendelea na mambo yetu, huko kwa Patrick mambo yalikuwa hekaheka, ukuzingatia kuwa ifikapo saa tano boss wao kutoka Afrika Kusini atakuwa amewasili kuja kushughurikia masuala yanayowasumbua.
Patrick alikuwa yu mwenye wasiwasi na majonzi kutokana na upungufu wa vijana wake wa kazi. Alishindwa kutoa mpangilio mzuri wa namna ya kupata habari za Pheady. Alikuwa na vijana kumi lakini watano wameisha punguzwa tayari na amebaki na watano tu ambao ni: Gilly, Moddy, Zuberi, Punzu, Herbert na yeye mwenyewe. Baada ya majadiliano marefu na wenzake ikaamuliwa Gilly, Moddy na Zuberi washughulikie upatikanaji wa habari kutoka sehemu zote zinazotoa matibabu katika mji wa Mwanza. Hii itawezesha kubaini alipo mateka wao aliyetoroshwa usiku. Herbert na Punzu wao wafanye patrol za sehemu muhimu kama za usafiri na starehe, Patrick mwenyewe atashughurika na ugeni unaokuja.
"Sasa kwa kuwa hatuna mawasiliano ya moja kwa moja kama ilivyokuwa hapo awali, inabidi kuwa makini sana kwani zile screen za kwenye magari hazifanyi kazi tena maana mitambo yake ndio iliyoharibiwa na washenzi wale." Alisikika akisema Patrick baada ya kuwa wamemaliza mipango yao.
 
Sio patupu nimetupia kidogo hapo. Kwani nilibanwa na majukumu ya kutafuta mkate.
 
Back
Top Bottom