TUENDELEE
8
Saa kumi na mbili tulikurupuka kutoka usingizini, tulikuwa tumelala kwenye gari tulilopaki karibu na kabisa la sabato kirumba. Tuliogopa kurudi mahotelini kwetu kutokana na msako wa Patrick, hasa kwangu mimi ambaye tayari nilishapekuliwa kule chumbani kwangu Hotelini. Tuliegesha pale gari baada ya kuwa tumetoka kumpeleka Kikakika zahanati usiku ule.
Wakati sisi tumetoka kumuokoa Kikakika, haikupita mda mrefu mara Patrick akafika nyumbani kwake na watu wake wakitoka kwenye msako wa kunisaka.
Patrick alishituka mara tu alipokata kona ya kuelekea kwenye nyumba yake na kuona geti likiwa wazi. Alikamyaga breki ghafla na kuwaambia wenzake wateremke haraka na kuondoa gari huku wenzie wakija kwa mguu kwa kujificha ili waweze kumuokoa iwapo kutakuwa na mushkeri. Aliuliza na kusimama karibu na nyumba ndogo ambapo aligungua mlango wa gari na kujirusha huku akijiviringisha hewani mpaka kwenye ukuta wa nyumba karibu na mlango uliokuwa umerudishiwa tu. Alichomoa bastola na kuupiga mlango teke ukakubali, alichokiona ndani hakuamini alijikuta akisema peke yake "watajua mwiso P ni nani." Alisogea akasimama katikati ya chumba alafu kama aliyekumbuka kitu akatoka akikimbia mpaka kwenye nyumba kubwa. Kabla ya kuingia akakutana na maiti ya Ebby mlangoni akashikwa na bumbuwazi! Wakati huo Gilly Moddy na Zuberi na kumuangalia. Alitikisa kichwa na kuwaambia wamsubiri hapo nje kwanza. Aliingia ndani kwa tahadhari kubwa huku kashikilia bastola mkononi. Aliingia chumba kimoja baada ya kingine na alipogika chumba cha mawasiliano aliguna huku bastola ikimdondoka. Hakuwa na hamu mwili wote ulimuishia nguvu alipoona uhalibifu wa humo ndani.
"Gilly" alisikika akiita kwa sauti baadae.
Gilly aliingia baada ya kusikia akiitwa, aliongozana na wenzake na kukuta Patrick akiwa na sura ya huzuni.
"Hawa wa washenzi wametuganyia vibaya sana, kwanza wameua wenzetu alafu wameharibu mitambo yetu ya mamilioni ya fedha. Sasa nipeni mpangilio mzima wa haya mambo, maana mimi akili haifanyi kazi kwa sasa" alisema Patrick huku akimwangalia Gilly kwa macho ya mategemeo.
Gilly alikohoa kidogo na kuanza kueleza mawazo yake; "Mimi nafikiri boss Mwiso P tuchukue suala moja la maana ambalo litakuwa ni kuwaua tu pindi tukiwapatia nafasi, kwani suala la kuwahoji waeleze wapi ilipo mali ni gumu sana. Kulingana na mateso aliyopata yule mtu jana, sikutegemea kuwa asingesema chochote" alieleza Gilly.
Baada ya maelezo hayo ya Gilly akili ya Patrick ilishakaa sawa kutoka kwenye bumbuwazi,
"Sawa nimekuelewa kwa hiyo kuanzia Sasa inabidi tubadili mpango kazi, tukiwatia machoni tu ni kuwamaliza, potelea mbali hata iyo mali tukiikosa lakini lazima wakawasiliane na kuzimu" alisema Patrick kwa uchungu.
"Sasa boss tutawapataje iwapo watakuwa wameamua kuondoka usiku huu?" Aliuliza Moddy kwa uchungu.
"Najua haitakuwa rahisi kwao kuondoka kwa wakati huu kutokana na jinsi mwenzao alivyo itabidi apate matibabu kwanza. Vinginevyo mauti itamkuta." Alieleza Patrick na kuendelea; " kwanza kwa sasa tukusanye hizi maiti na kuziweka panapostahili. Baada ya hiyo kauli wote walitawnyika na punde kidogo kila mtu alirudi na maiti na kuziweka kwenye jokofu kubwa. Zilikuwa maiti nne na moja ilikuwepo ndani hivyo jokofu lilibeba maiti tano. Baada ya kuziweka zote vizuri walifunga jokofu na kurudi sebuleni.
"Hawa washenzi wametutia hasara isiyo kifani" aliongea Patrick huku akiwa kasimama. Kuanzia sasa hivi tunatakiwa macho yetu tuyaweke kwenye hospital ili tuweze kugundua alipowekwa yule mtu wetu. Nina Imani atakuwa anapata matibabu, tutakapo jua alipo kitakachofuata ni kumsafiriaha ahera bila mjadara. Ameishatupotezea wenzie wetu watano hivyo kwa yeyote atakayempatia nafasi ya kumuua ni rukhusa." Alieleza Patrick.
Mara simu ililia, Patrick akakatisha maongezi na kuchukua simu tayari kwa maongezi.
"Hallo, Patrick hapa." Alisema kwenye simu.
"Wanna See anaongea hapa" ilisikika sauti upande wa pili alafu aliyejibu akaendelea kuongea. "Nimewatafuta kwa mawasiliano yetu ya kawaida sikuwapata, vipi Kuna nini huko?" Alimaliza kwa swali.
Patrick alimueleza yote yaliyotokea kwa mafumbo ambayo wanaelewa wao tu. Baada ya Wanna See kusikiliza maelezo yote alisikika akisonya alafu akaanza kuongea;
"Inaonekana huko unafanya biashara uchwara, yaani unashidwa kuidhibiti hiyo bidhaa mpaka inatapakaa madukani. Sasa mimi nakuja huko pamoja na faili za mikataba mingine miwili. Nitegemee kufika kesho saa tano na ndege ya Air Tanzania inayotoka Nairobi. Nategemea kuondoka hapa muda mchache ujao kwa ndege inayokwenda Kenya. Mengi tutaongea huko nikifika" Alimaliza kuongea Mr Wanna See na kukata simu bila kusikiliza zaidi kutoka kwa Patrick. Alikuwa ni mwenye hasira Kali kutokana na kushindwa kwa Patrick. Hapo alikuwa Pretoria Afrika Kusini, aliondoka na vijana wake wawili wa kazi kuja Tanzania kutokana na uzito wa suala lililojitokeza. Licha ya kuzidiwa akili katika wizi wa dhahabu bado kulikuwa na jipya lililojitokeza kuhusu Pheady.
Baada ya simu kuwa imekatwa ghafla vile. Patrick alirudisha mkono wa simu na kutoa sigara akawasha na kurudi katika maongezi na vijana wake wa kazi; " Nilikuwa naongea na Wanna See, inaonekana kakasirishwa sana na mambo yalivyo amedai atafika hapa kesho saa tano." Alisema Patrick baada ya kuwasha sigara na kuvuta kama mikupuo miwili hivi alafu aliendelea: "Kwa hiyo lililopo sasa hivi tuchukue mait za wenzetu tukazidumbukize ziwani kwani hatutakuwa na nafasi tena baada ya Wanna See kufika. Mambo yanaweza yakabadilika maana amesema anakuja na watu wawili zaidi.
"Sasa boss Patrick hatuwaziki kwa heshima zao?" Aliuliza Zuberi.
"Tungefanya hivyo lakini kutokana na ujio wa Wanna See huenda kukawa na pilikpilika nyingi kiasi cha muda kuwa mfinyu hivyo tukaendelea kukaa na maiti ndani ambalo ni Jambo la hatari." Alijibu Patrick.
"Okey, naona la muhimu ni kupata usafiri wa kumpeleka hizi maiti katika kina kieefu cha maji." Alisema Moddy ambaye muda mwingi alikuwa kimya.
Baada ya kutoa kauli hiyo Patrick aliingia ndani ya chumba kimoja na kutoka na furushi la box baada ya kulifungua alitoa kitu kama tube ya gari lakini kubwa zaidi. Aliongozana na wenzie mpaka nje kwenye gari akachukua mrija furani na kuchomeka sehemu fulani ya hiyo tube alafu akapanda ndani ya gari na kuliwasha huku akipiga less kama mtu anayepasha injini motoi vile. Baada ya mda kidogo lile tube lilijaa upepo na kuwa mtumbwi mkubwa tu wa kuweza kuwekwa injini nyuma.
Walitaka kuweka injini lakini walighairi ili kuhepuka kukamatwa na askari wa doria ziwani iwapo wangesikia muungurumo wa injini. Hivyo wakaamua kutumia kasia ambazo Patrick alizifuata ndani. Zilikuwa kasia za plastiki. Walichukua maiti na kupanda watu watatu Patrick alibaki, walichukua na mawe ya kuzifunga zile maiti zisije zikaelea juu ya maji. Baada ya hapo waliondoka na kwenda kutupa zile maiti ziwa Victoria.
Baada ya kuwa wamerudi kutoka kutupa maiti walikubaliana walikubariana walale palepale wote kwani muda wa mapambazuko ulibaki mchache. Nao wakafanya hivyo huku wakiwa na mkakati wa kufanya uchunguzi kwenye hospitals kesho asubuhi kabla ya saa tano ili atakapo kuja boss wao kutoka Afrika Kusini Ndugu Wanna See, wawe na la kumueleza.
Baada ya kuwa tumetoka kwenye maegesho yetu kule tulipolala karibu na kanisa la Sabato kirumba, tulielekea kwa dada yangu nilikotunza zile mali. Tulipofika nilimuambia kuwa ndio narudi kutoka Bukoba, alitundalia kifungua kinywa wakati tunaoga. Tulipokuwa tumemaliza kuoga tulipata chai nzito huku tukiendelea na mazungumzo ya kawaida. Wakati huo ilikuwa inakaribia saa mbili na nusu, baada ya kupata chai nilimuambia dada tunahitaji kupumzika kidogo kutokana na uchovu wa safari. Alituelekeza chumba cha kwenda kupumzika, chumbani kulikuwa na vitanda viwili simu ya mezani pamoja na kabati la nguo lenye kioo cha kujiangalia. Baada ya kutuonyesha yeye aliendelea na hamsini zake.
Tulipokuwa ndani ya chumba tayari tushafunga mlango, nilinyanyua kiwiko cha simu na kuzungusha namba za zahanati tuliyompeleka Kikakika. Niliposikia upande wa pili unanyanyuliwa nikaitoa;
"Hallo"
"Hallo nani mwenzangu?" Sauti kutoka upande wa pili ilisikika.
"Pheady hapa, nataka kuongea na daktari mkuu." Niliongea.
"Subiri kidogo" ilisikika tena hiyo sauti kwenye simu. Baada ya sekunde kadhaa ilisikika sauti nzito ya daktari. " Hallo daktari hapa unasemaje ndugu?"
"Mimi naitwa Pheady nilileta mgonjwa toka kwa mzee Magesa jana usiku hivyo nataka kujua khaki ya mgonjwa. Nilieleza. Magesa ndie boss wa ofisi zetu hapa Mwanza.
"Ohoo! Ni wewe kijana, Khali ya mgonjwa inaendelea vizuri, ameishazinduka ila ana maumivu hawezi kutembea. Imebidi tumshone kidogo sehemu za mgongoni" daktari alieleza.
"Je uwezekano wa kuongea naye upo?" Nilimuuliza.
"Hakuna wasiwasi we njoo wakati wowote nitakuwepo, isipokuwa kuanzia saa saba mpaka saa Tisa." Alijibu.
"Sawa daktari, nitakuja kumuona muda utakaponiruhusu"
"Okay, kwa heri"
"Sawa"
Nilirudisha mkono wa simu baada ya kumaliza maongezi na daktari, nilimueleza Sonno maelezo niliyoyapata kwa daktari naye alifurahi kusikia Kikakika ameishazinduka. Tulijipumzisha mpaka ilipofika saa sita hivi ndio tukawa tumeamka na kwenda kuoga tena. Baada ya kumaliza kuoga tuliandaliwa chakula na kula. Baada ya hapo tulikaa sebuleni na dada tukiongea mazungumzo ya kawaida huku tukiangalia runinga. Ilipofika saa nane na nusu dada aliondoka kwenda kwenye biashara zake akatuacha na mfangakazi pamoja na watoto waliokuwa wamefika kutoka shule. Sie tukiendelea kuangalia vipindi vya runinga ambapo wakati huu tukiangalia ngumi za kimataifa zilizokuwa zikionyeshwa na stesheni moja ya Kenya.
Ilipotimia saa Tisa na nusu tuliondoka kwenda kumuona Kikakika kule zahanati, tulipofika tulimkuta daktari msaidizi akiwa mapokezi na wagonjwa. Tulimsalimia na kumuuliza iwapo daktari mkuu tumemkuta. Alisema yuko chumba cha tatu katika vyumba vilivyojipanga pembeni ya korido. Tulielekea tulikoelekezwa na kukuta akiwa anapekuwa mafaili.
"Habari za saa hizi daktari?" Tulimsalimia kwa pamoja
"Salama tu, na nyie habari za toka jana?"alijibu na kuuliza.
"Nzuri, tumekuja kumuona mgonjwa wetu" nilimjibu na kueleza.
"Sawa, twende mkamuangalie" daktari alijibu na kusimama akatuongoza kwenye korido mpaka chumba cha pili toka mlangoni. Aligungua mlango tukaingia ndani na kukuta kukiwa na wauguzi wawili pamoja na vitanda kama sita hivi kwa akili ya wagonjwa. Kati ya hivyo vitanda ni vinne vilivyokiwa na watu. Tuliwasalimia wale wauguzi wa kike alafu tukaenda kwenye kitanda alichokuwa amesimama daktari. Kikakika alikuwa amelala usingizini, daktari akamuamsha. Aliposhtuka usingizini na kutuona alitabasamu na kunyanyuka polepole akakaa kwenye kitanda.
"Pole sana Mr Kikakika" alisema Sonno, wakati huo daktari alishaondoka.
"Asanteni sana rafiki zangu" alijibu Kikakika.
""Vipi unajisikiaje?" Nilimuuliza.
"Sasa hivi najisikia vizuri kiasi sio kama asubuhi." Alijibu.
"Je unaweza kutembea kidogo?" Aliuliza Sonno.
"Ndio, lakini kwa shida maana vidonda nilivyoshonwa bado vibichi..
"Ilikuwaje mpaka yakawa yametokea yote hayo?" Nilimuuliza.
"Daa!! Ilikuwa hatari sana, sikutegemea kama ningekuwa salama hata Sasa. Wale watu washenzi sana na nikipona lazima watanitambua hata kama itachukua mwaka mbele lazima wayaone machungu ya maisha." Aliongea Kikakika kwa uchungu alafu akakatisha na kuomba maji ya kunywa, alikunywa kama birauli mbili hivi alafu akaendelea kuongea: baada ya kuachana na wewe pale benki, mimi nilienda kwenye duka moja pale stendi ya taxi kulikuwa na kitu nahitaji. Nilipofika kwenye hilo duka linaloitwa Bamboo shop nilifanya manunuzi yangu yaliyo nipereka pale. Wakati natoka nilielekea barabara ya mtaa wa Makoroboi na kabla sijafika Jafaries Hotel nikashtukia gari inapaki pembeni yangu nilipogeuka kuangalia nikajikuta naangaliana na midomo mitatu ya bastola huku mlango wa mbele ukifinguliwa na kuamlishwa niingie ndani ya gari. Sikuwa na ujanja kwani kwa vuovyote vile wangenitia risasi kama ningeleta maskhara. Nikatii na kuingia kwenye gari, kwanza nilifikiri ni askari kanzu. Lakini baada ya kufikishwa kwao na kuanza kuhojiwa ndio nikajua ni wamoja na yule niliyemuua kule Nyakato. Walinitesa sana ili niwaambie Ilipo dhahabu. Niliposhindwa kuwaambia zilipo ndopo wakanibadilishia somo na kuhoji ulipo wewe Pheady. Kutokana na kushindwa kuvumilia mateso waliyonipa ikabidi nitaje hotel uliyofikia. Wakatoka kwenda kukutafuta."
"Baadae wakarudi na kuendeleza mateso yao ili niwaeleze unaweza kuwa wapi kwa wakati huo. Nilikuwa nakumbuka ahadi yetu ya kukutana kule Magnum Club lakini sikuweza kuwaambia nikihofia kuvuruga kila kitu. Inavyoonekana wale jamaa wanakufahamu sana maana wamenionyesha na picha zako ukiwa na ile pikipiki pamoja na jina lako ila wanajua tupo wawili tu katika hili suala, Wala Sonno haeleweki. Katika maelezo yao inaoneka walikufahamu wewe kwanza ila mimi nimekuja kujulikana baada ya kuonekana nikiongozana na wewe kwani inaonekana walituona kabla ya kuingia banki. Baada ya hapo wakaona itakuwa rahisi kunipata mimi kutokana na kutoka kwa mguu na kuanza kutembea. Pamoja na mateso waliyonipa vilevile walinipiga sindano ya usingizi kwa kuhofia ninachoweza kufanya ikiwa nitakuwa na fahamu zangu. Nilishangaa sana nilipozinduka na kujikuta hapa, nilipomuuliza daktari ndipo aliniambia nileletwa na Pheady, hapo nilishangaa maana sikutegemea kama mngeweza kugundua kirahisi nilipo na kuja kuniokoa. Hebu na nyie nielezeni ilivyokuwa mpaka kunipata." Alimaliza Kikakika na kutoa hoja.
Nilimueleza Alfa mpaka Omega kuhusu tulivyofanikiwa kumpata naye akafurahi kwa roho ya upendo tuliyomuonesha. Tulikuwa tumeongea vya kutosha ndipo nilipobadili maongezi; " Naona ukipata nafuu tu tuondoke mji huu maana naona unanuka mauti. Mali zetu tutaziacha mpaka pale mambo yatakapotulia, maana askari nao wapo chonjo sana. Tumesikiliza taarifa ya habari ya saa saba inasema kuwa katika msako unaoendelea hapa, wameishakamatwa majambazi kama tisa hivi. Kwa hiyo tutakapoondoka hapa Kuna haja ya kuacha siraha zetu. Kwani katika njia zote zitokazo Mwanza wakikuhisi vibaya tu, unakaguliwa maana kuna vizuizi vya askari barabarani." Nilieleza.
Sonno naye aliongezea: " Hata Mimi nilikuwa na mawazo kama hayo kwani kuendelea kukaa hapa ni kuwapa nafasi akina Patrick kutufanya wanavyotaka. Kitu ambacho sitaki kitokee wakati watu tumeishashinda ushindi uzuri kilichobaki ni matumizi tu" aliongea Sonno.
"Sawa mie sina nyongeza, ngoja tuangalie Khali itakavyokuwa kesho na keshokutwa maana hata mimi sitaki vuramai wakati nikiwa na hali kama hii. Ila nitakapopona nitarudi kuja kuwaadabisha hawa washenzi. Ni lazima waupate uchungu wa maisha kana Mimi" Alisema Kikakika akiwa ameukunja uso mfano wa mtu anayenusa harufu mbaya.
Ilikuwa kwenye saa kumi na moja kasoro hivi tulipoaga hapo zahanati na kuondoka huku tukipanga kuja tena kesho kumjulia hali mwenzetu. Tulipanda kwenye gari letu na Sonno akashika usukani naikamuambia aongoze kwa dada. Sikutaka kuzurura mtaani isije ikawa taflani baadae.
Wakati sisi tunaendelea na mambo yetu, huko kwa Patrick mambo yalikuwa hekaheka, ukuzingatia kuwa ifikapo saa tano boss wao kutoka Afrika Kusini atakuwa amewasili kuja kushughurikia masuala yanayowasumbua.
Patrick alikuwa yu mwenye wasiwasi na majonzi kutokana na upungufu wa vijana wake wa kazi. Alishindwa kutoa mpangilio mzuri wa namna ya kupata habari za Pheady. Alikuwa na vijana kumi lakini watano wameisha punguzwa tayari na amebaki na watano tu ambao ni: Gilly, Moddy, Zuberi, Punzu, Herbert na yeye mwenyewe. Baada ya majadiliano marefu na wenzake ikaamuliwa Gilly, Moddy na Zuberi washughulikie upatikanaji wa habari kutoka sehemu zote zinazotoa matibabu katika mji wa Mwanza. Hii itawezesha kubaini alipo mateka wao aliyetoroshwa usiku. Herbert na Punzu wao wafanye patrol za sehemu muhimu kama za usafiri na starehe, Patrick mwenyewe atashughurika na ugeni unaokuja.
"Sasa kwa kuwa hatuna mawasiliano ya moja kwa moja kama ilivyokuwa hapo awali, inabidi kuwa makini sana kwani zile screen za kwenye magari hazifanyi kazi tena maana mitambo yake ndio iliyoharibiwa na washenzi wale." Alisikika akisema Patrick baada ya kuwa wamemaliza mipango yao.