RIWAYA KIJIJINI : KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.
SEHEMU YA TANO.
______________
ILIPOISHIA
______________
Kwa kuwa Omary alikaa kwenye kochi,
yeye
ndio akawa wa kwanza kutupia
macho chini ya kitanda, aliona
Stellah na Tausi wakiwa chini ya
kitanda, ila hakuamini alichokiona,
ilibidi asogee mpaka ilipo miili ya
wakina Stellah na kuhakikisha
mwenyewe kwa macho yake kuwa
wale wanawake wawili tayari ni
marehemu.
"Mungu wangu, umeua kweli" Omary
aliuliza huku akiwa anasimama,
Kayoza kuona hivyo nae allisimama
na kwenda alipokuwa Omary na
kumkaba shingo....
____________
ENDELEA...
____________
Denis akanyanyuka haraka mithili
ya gari inayowaisha mgonjwa
mahututi hospitalini, lakini kayoza
alikua na kasi mara mbili, akawai
mlangoni.."please Denis na Ommy, nawaomba
mtulie rafiki zangu, nahitaji msahada
wenu" kayoza aliongea kwa upole,
Denis ikabidi arudi na kufunua godoro na
kuziangalia zile maiti, huku akionekana ni mtu mwenye maswali
mengi kichwani, baada ya muda
kidogo akagutuka,
"imekuaje kaka?" Denis
akauliza huku akiwa bado anaziangalia zile maiti,
"Kwanza kubalini kuwa upande wangu, alafu nitawaambia ukweli" Kayoza aliongea huku akiwatazama wenzake kwa zamu,
"Tuambie kwanza nini tatizo?" Omary aliongea huku akijishika shingo kutokana na kabali alipigwa na Kayoza muda mchache uliopita,
"Mimi niko upande wako, na nitakuwa upande wako" Denis aliongea huku akimuangalia Kayoza aliyeonekana kuchanganyikiwa,
"Hata mimi niko upande wako, haya tuambie ilikuwaje?" Omary aliuliza,
"jamani nitawaambia tu,
cha muhimu tuondoke eneo hili haraka iwezekanavyo" Kayoza
akaongea kwa kuwasisitizia wenzake,
"Ok, fasta basi" Omari
akawaharakisha wenzake huku akionekana mwenye wasiwasi.
Wakavaa haraka, na wakawa wanaelekea nje. Wakanyoosha moja kwa moja mpaka mapokezi,
"Mbona Mpo peke yenu, wenzenu wako wapi?" Dada wa mapokezi aliwatania,
"Bado wanajipodoa, si unajua tena mambo ya wanawake?" Omary alijibu huku akicheka,
"Haya, nawasikiliza" Dada wa mapokezi aliongea,
"Tumekuja kulipia chumba" Omary aliongea huku akimkabidhi pesa Mhudumu,
"Sasa mbona ya chumba kimoja?" Dada wa mapokezi aliuliza baada ya kuzihesabu zile pesa,
"Hicho kingine watalipia wadada" Denis alijibu,
"Na wakikataa?" Dada wa mapokezi aliuliza ila kwa utani,
"Wakikataa itabidi muwazuie na wawasaidie kufua mashuka" Omary nae alitania huku wakianza kuondoka na kumuacha yule dada wa mapokezi akicheka.
Njiani kila mmoja
alikua anafikiria lake,
"Tunaenda wapi sasa?" Kayoza aliuliza huku akiwa hana muelekeo,
"Itabidi turudi kwanza chuo" Denis alitoa jibu lililomfanya Kayoza asimame ghafla,
"Hamuoni hatari iliyopo mbele yetu? Sasa tukirudi chuo si naweza kukamatwa?" Kayoza aliuliza huku akiwa bado amesimama,
"Acha ujinga wewe, hakuna hata mmoja atayetuhisi sisi tunahusika na vifo vile" Denis alimwambia Kayoza,
"Kwa hiyo?" Kayoza aliuliza,
"Kwa hiyo turudi chuo, alafu tuangalie upepo unaendaje na tukiona mambo yanaweza kuharibika basi ndio tutaangalia namna ya kupambana" Denis alimueleza Kayoza,
"Alafu hili suala ni letu sote, sio lako peke yako" Omary nae akaongezea maneno yalimpa nguvu kidogo Kayoza na kukubali kurudi kwanza chuo.
Walienda mpaka jamatini ambapo ndipo zilikuwa coaster za kuwapeleka chuo, wakatafuta usafiri ambao ulikuwa upo tayari kuondoka na wakaingia, baada ya muda mchache gari iliondoka.
Walipofika eneo la chuo wakaingia kwenye chumba chao, Denis na Omari wakaingia kuoga,
Kayoza akajitupa kitandani ila sio kwamba alitaka kulala, hapana, mawazo ndio yaliutawala ubongo wake muda wote.
Ilipofika mida ya saa 10 jioni, habari zikaenea
chuo chote kuwa kuna wanafunzi
wawili wa kike wamekutwa wamekufa
Katika nyumba ya kulala wageni, kwa denis na Omari hiyo habari kwao
haikuwa ngeni ila hofu waliyokuwa nayo mwanzo sasa iliwazidia kupita kiasi.
Usiku wa siku hiyo, Kayoza hakulala kabisa kila dakika
alikua anazunguka chumbani tu huku tukio la kumuua Tausi likimrudia kichwani mara kwa mara pamoja na sura ya Stellah, wakina Omary pia hawakulala ni
kutokana na uoga, walikua
wanaogopa kulala wakijua kuwa
kayoza anaweza kuwaua pia.
********
Kesho yake asubuhi wanafunzi
wakatangaziwa waende wakaage miili
ya wenzao, na utaratibu mzima
utakuwa katika hospitali kuu ya mkoa
wa dodoma inayoitwa jenero hospital(general).
"Jamani mimi nitaenda kuaga pia, maana ni watu ninaowafahamu" Omary aliwaambia wenzake baada ya kupata ratiba kamili ya kuiaga miili ya Tausi na Stellah,
"Kayoza na sisi itabidi tuende, haina haja ya kuogopa kitu ambacho hatujahisiwa nacho" Denis alimshawishi Kayoza,
"Hapana, nyie nendeni tu, mimi siendi" Kayoza aliwaambia wenzake,
"Ilo futa kichwani kwako, watu wote wanajua ulishawahi kuwa na uhusiano na Stellah, sasa usipoenda watu watakuchuliaje?" Denis alimwambia Kayoza,
"Hivi nyie hamuoni hatari iliyo mbele yetu?" Kayoza aliuliza huku akisikitika,
" hakuna hatari yoyote kwa sababu hakuna atayejua ni nani amewaua wakina Stellah" Denis alizidi kumueleza Kayoza,
"Na pia usipoenda haitakuwa picha nzuri kwa watu wanakufahamu" Omary alichangia na mwisho Kayoza alikubali kuambatana na wenzie ifikapo saa kumi jioni.
___________________
SAA KUMI JIONI
___________________.
Wanafunzi wengi walijitokeza eneo la hospitali, pia Kayoza na
wenzake walifika kuaga miili ya wenzao. Eneo lote lilitawaliwa na vilio vya wasichana wa chuo pamoja na walimu wao wachache walioguswa na vile vifo.
* * * * * * * *
Baada ya wahudumu kukaa mda mrefu bila
kuona wakina stellah wakitoka, walipata wasiwasi kidogo na waliitana wenyewe kwa wenyewe na kuulizana bila kupata jibu la uhakika, na mwisho walipanga kwenda kuwaogongea, ila
walitaka kutumia njia ya kutaka kufanya usafi ndio iwe kigezo, wakanteua mwenzao mmoja akawagongee mlango.
Mhudumu alipofika mlangoni akagonga,
hakusikia jibu, akagonga tena kwa nguvu kidogo pia hakusikia jibu,
akarudi nyuma kidogo alafu akachungulia korido, hakuona mtu,
akaenda upande wa vyoo na bafu pia
hakuna mtu, akakata shauri ya kurudi kufungua mlango ambao ndani alikuwepo Stellah na Tausi, akanyonga
kitasa akazama ndani, akakuta hamna mtu,
"khaa! wametutapeli!" Mhudumu akashangaa moyoni mwake huku akiwa amejishika kiuno, wakati akiendelea kuwaza na kuwazua, mbele akaona suruali ya
kike iko chini pamoja na pochi, ndio akapata faraja kidogo,
"Hodi wadada" Mhudumu aligonga hodi ilihali ameshaingia ndani, lengo lake alitaka kujua wakina Stellah wapo upande gani, alijaribu kuita tena na tena bila mafanikio,
"Ebu Ngoja niwaokotee pochi yao" Mhudumu aliongea huku akiinama chini kuokota pochi, wakati anaokota ndio
akaona mkono wa mtu chini ya
kitanda, akashtuka, akasimama
akalinyanyua godoro kidogo, alichokiona kilipekea kupiga kelele
hadi akapoteza fahamu.
Alipopata fahamu alijikuta yupo hospital huku pembeni yake yuko polisi,
"habari
yako dada, unajisikiaje?" Polisi alimsalimia yule
mhudumu,
"nzuri" Mhudumu akajibu huku akishangaa mazingira yaliyomzunguka,
"unajisikiaje sasa, una nguvu
kidogo?" Polisi aliendelea kuuliza.
"najiskia vizuri" Mhudumu alijibu,
Polisi akatoa simu akapiga, baada ya
dakika mbili, akaja daktari na askari
mwingne, daktari akamuuliza
maswali mawili matatu mhudumu
kuhusu hali yake, kisha akampima
pima, alafu akamruhusu.
Akapelekwa kituoni kwa ajili ya mahojiano. Pale kituoni walimkuta askari mmoja kijana mdogo mdogo, mweupe ila alikuwa amevaa nguo za kiraia, kilichomtambulisa kuwa ni Askari ni saluti kadhaa alizokuwa anapewa na askari wengine. huyu polisi kijana jina lake ni Joel Minja, ila jina ambalo hutumiwa na wengi kumuita ni Sajenti Minja.
"Mkuu, binti mwenyewe ni huyu hapa" Askari aliyeongozana na Mhudumu wa bar alimuongelesha Sajenti Minja,
"Oooh vizuri, mpeleke kule katika chumba cha mahojiano, mimi nakuja" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia yule Mhudumu, kisha akaelekea nje ambapo alienda mpaka katika moja iliyokuwa imeegeshwa hapo nje na kuchukua simu, kisha akaelekea katika chumba cha mahojiano na kumkuta yule dada Mhudumu akiwa amekaa anamsubili.
"unaitwa nani mrembo?" sajenti joel Minja alimuuliza mhudumu.
"Sania" Mhudumu ndivyo alivyojibu,
"huna baba au ubini?
Jitambulishe majina yako yote matatu" Sajenti Minja akatia msisitizo,
"Sania Juma Baruti" Mhudumu akajibu,
"unakumbuka tukio lililosababisha
ukapelekwa hospitali?" Sajent Minja
akauliza tena.
Mhudumu akaelezea
mwanzo hadi mwisho.
"je unawakumbuka vijana waliongia
na hao mabinti?" Sajenti Minja akauliza,
"nikiwaona nitawajua" Mhudumu
akajibu kwa ufasaha kabisa. Baada ya mahojiano yule Mhudumu alipelekwa selo kwa ajili ya usalama wake.
Kesho yake mishale ya saa kumi jioni, Sajenti Minja akiwa na Askari wengine, wakamchukua Mhudumu na kwenda nae hospitali ili
akahakishe kama wale maiti ni wateja aliowapokea au sio wao
* * * * * * *
Baada ya wakina Kayoza kutoka kuaga
maiti, Omari akaaga anaenda msalani
kukojoa na kuwaacha kayoza na Denis wakitangulia kutoka na kwenda nje ya eneo la hospitali.
Omari alipotoka msalani akawa anaelekea nje kuwafuata wenzake, ndipo mbele yake akawaona Askari wapatao watano wakiwa wanaelekea upande aliopo huku wameongozana na msichana ambae hakuweza kumtambua kutokana na umbali ulikuwa kati yao, ila kadri walivyozidi kusogeleana ndipo sura ya yule msichana ilivyozidi kumjia, zilipofika hatua mbili kabla hawajapishana ndipo Omary alipopata mshtuko baada ya kugundua kuwa yule msichana ni Mhudumu wa ile bar ambayo Kayoza alifanya mauaji.
Omary aliuficha mshtuko wake ila sasa yule Mhudumu akawa anamuangalia sana Omary, Omary akatamani hata apotee ghafla kama upepo ila ilishindikana na akaamua aendelee tú kwenda mbele kiume.
Wale Askari na mhudumu walipomfikia Omary wakampita na kufanya Omary ashukuru Mungu baada ya kupishana nao.
Yule Mhudumu alipompita Omary, alihisi hiyo sura siyo ngeni kwake, alitembea hatua mbili kisha akasimama, ikabidi Askari wote nao wasimame, kisha Mhudumu akageuka na kumtupia jicho Omary ambaye nae aliwageukia na sura yake ikaonekana vizuri na Mhudumu na kumfanya Mhudumu atoe mguno wa mshtuko..
******ITAENDELEA******
Je dada Mhudumu wa bar amemtambua Omary?
Na kama amemtambua atamchoma?
Nini hatma ya kayoza baada ya mauaji aliyoyafanya?
the Legend☆