Riwaya: Kijijini kwa Bibi

Riwaya: Kijijini kwa Bibi

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA NANE.

_______________
ILIPOISHIA...
_______________

"taxi hiyo imeingia sasa hivi, ongea
na dereva
akupeleke" mwenzake alimjibu huku
akinyooshea kidole gari waliomo
ndani
wakina kayoza,

"poa basi, tutakutana kesho ili tujue
ofisi itasema nini kuhusu hili tukio"
Sajenti Minja aliongea Kisha
akapeana mikono na mwenzake ikiwa
ni ishara ya kuagana.

Alafu akawa anaelekea kwenye gari
ambalo ndani wapo wakina Kayoza....

____________
ENDELEA...
_____________

Sajenti Minja aliendelea kuisogelea ile taxi waliyokuwamo wakina kayoza,

"Au mkuu..." Dereva wa kwenye ile gari ya Polisi aliita na kumfanya Sajenti Minja asimame,

"Unasemaje tena Timo?" Sajenti Minja aliuliza huku akisimama,

"Njoo nikukimbize mara moja, maana nahisi waliopo ndani hawatatoka sasa hivi" Dereva wa gari la polisi aliongea,

"Ni jambo la kheri, ila wakitoka alafu wakakukosa?" Sajenti Minja aliuliza,

"Wewe twende tu, hata usijali" Dereva wa Gari ya polisi alijibu na kumfanya Sajenti Minja aache kuifuata gari waliyokuwepo wakina Kayoza na kurudi kuipanda gari ya Polisi, kisha ikaondoka.

Wakina Omary walikuwa katika taxi walishuhudia kila hatua iliyokuwa inafanywa na Sajenti Minja, na kila mmoja tumbo lilikuwa na joto,

"Umeshakuwa mkosi huu, hamna ya kushuka, bora tuondoke tu" Omary aliongea huku akitetemeka,

"Na hivyo vidonda vyako vitapona vipi bila kutibiwa?" Denis alimuuliza Omary,

"Tutajua mbele ya safari" Omary alijibu,

"Usije ukaoza mgongo" Denis alimtahadharisha Omary,

"Dereva ebu tupeleke Lodge yoyote iliyo karibu na Stendi ya mabasi ya mikoani" Kayoza aliongea baada ya ukimya wa muda mrefu na kuwafanya wenzie wamuangalie,

"Vipi, unajisikiaje bab?" Omary alimuuliza kayoza huku akimshangaa,

"Tutaenda kuulizana mbele ya safari" Kayoza alijibu huku akijishangaa alivyochafuka kama alilala kwenye vumbi.

Dereva wa taxi aliindoa gari eneo la hospitali na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye eneo ambalo aliamini zinapatikana nyumba za wageni na pia ni jirani na stand ya mkoa wa Dodoma, na kuwashusha hapo,

"Shilingi ngapi unatudai?" Omary alimuuliza Dereva baada ya kushusha mabegi yao,

"Kwa mizunguko tuliyofanya, uwa nafanya shilingi elfu kumi na tano, kwa kuwa nyinyi Mi washkaji, nitawafanyia elfu kumi" Dereva taxi aliongea huku akitabasamu,

"Punguza bwana, sisi tuna elfu saba" Omary aliongea kwa kulalamika,

"Suka shika pesa yako" Kayoza aliongea huku akimpa noti ya shilingi elfu Dereva taxi,

"Ungesubiri kwanza nimsaundishe" Omary aliongea huku akimlaumu Kayoza,

"Hakuna kusaundishana hapa, unapoteza muda tu" Denis aliongea huku akibeba begi lake na kuingia ndani, Kayoza akamfatia.

"Niachie namba yako, kesho asubuhi tunaweza kukupigia utufuate ili utupeleke stand" Omary alimwambia Dereva taxi,

"Stand si hapo nyuma tu, mnaweza kwenda hata kwa mguu" Dereva taxi alimjibu Omary,

"Wewe nipe tu hizo namba, unakuwa kama sio mfanyabiashara bwana" Omary aliongea na kumfanya Dereva taxi ampe namba zake za simu na kisha wakaagana.

Omary akachukua begi lake na kuingia nalo ndani, kwa bahati nzuri aliwakuta wenzake wakimsubiri mapokezi,

"Jamaa unatuyeyusha sana" Denis alimwambia Omary huku wakielekea sehemu vyumba vilipo,

"Nawayeyusha na nini sasa?" Omary alihoji huku akiwafuata wenzake,

"Sasa muda wote ulikuwa unaongea nini na Dereva?" Kayoza alimuuliza Omary,

"Nilikuwa nachukua namba ya simu ya Dereva" Omary alimjibu kayoza,

"Sasa namba ya simu ya nini wakati stand ipo karibu?" Denis aliuliza,

"Hamuwezi jua, kama sio kesho anaweza kuwa msaada siku nyingine" Omary alijibu wakati Denis akiufungua mlango wa chumba walichotakiwa kulala,

"Alafu huo ujinga wako uachage. Kwanza jana ilikuwaje mpaka ukakamatwa?" Denis aliuliza wakati akikaa kitandani,

"Dah, ilikuwa kama movie yaani" Omary aliongea huku akicheka utadhani anasimulia jambo zuri,

"Hivi utakua lini wewe?" Kayoza aliuliza kwa hasira,

"Kwani nimefanyaje boy?" Omary aliuliza huku akimshangaa Kayoza,

"Wewe si umeulizwa ilikuwaje ukakamatwa jana? Badala ya kujibu unaleta utoto" Kayoza aliongea huku akivua suruali,

"Sasa si ndio nilikuwa naanza kujibu?" Omary aliongea,

"Jibu sasa, acheni kulumbana" Denis aliongea huku akimuangalia Omary.

Omary akaelezea mwanzo mpaka mwisho wa kukamatwa kwake na mpaka Mipango ilivyosukwa na Sajenti Minja ili kuwaingiza mtegoni Kayoza na Denis.

"Sajenti Minja ndiyo nani?" Denis aliuliza,

"Yule polisi aliyetaka kuja kwenye taxi tuliyokuwepo" Omary alimjibu Denis wakati huo Kayoza alikuwa ameingia bafuni kuoga,

"Alafu tumuulize Kayoza ni kwa nini alikuwa katika umbo la kutisha namna ile kule lodge?" Omary alimshauri Denis,

"Kweli aisee, ila tutaanzaje sasa? maana anaogopesha" Denis aliuliza kwa mashaka,

"Hawezi kutufanya kitu bwana, kama angekuwa na lengo la kutudhuru, angetudhuru toka zamani" Omary aliongea kwa kujiamini,

"Kama ni hivyo ni sawa, ila utamuuliza wewe" Denis alimwambia Omary,

"Sawa, mimi nitamuuliza" Omary alijibu kisha nae akavua suruali kwa lengo la kwenda kuoga Kayoza akitoka bafuni.

********

Baada ya saa moja, wote watatu walikuwa tayari wameshaoga na kila mmoja alikuwa akiwaza jambo lake,

"Jamani eeh, wote tumebeba mabegi lakini hatujahambiana kila mmoja wapi anaelekea" Denis aliuliza baada ya ukimya wa muda mrefu,

"Sasa si tulikuwa na matatizo, unadhani huo muda wa kuambiana ungepatikana vipi?" Kayoza nae aliuliza,

"Mimi naenda Tanga, hadi hapo tayari nimeshawajibu" Omary alijibu huku macho yakiwa kwenye simu yake,

"Tanga kufanya nini? Wewe kwenu si ni kondoa wewe?" Denis alimuuliza Omary huku akicheka,

"Kule kuna babu yangu, sijamuona siku nyingi na inabidi nikamuone kwanza kama wiki mbili hivi" Omary aliwaelezea wenzake,

"Na wewe Kayoza unaenda wapi?" Denis alimuuliza kayoza,

"Mimi nitaenda Bukoba" Kayoza alijibu,

"Mimi kama kawaida, Dar hiyo" Denis aliongea kwa furaha,

"Nadhani tutaondoka pamoja ingawa tutapanda mabasi tofauti" Omary aliwaambia wenzake,

"Wazo zuri sana hilo" Denis aliongea kukubaliana na Omary,

"Ila ndugu yetu, ebu tueleze nini tatizo?" Omary alimuuliza Kayoza,

"Tatizo lipi?" Kayoza nae akamuuliza Omary na kufanya washangaane,

"Hujui au?" Omary aliuliza kwa upole,

"Sio sijui, ebu liweke swali lako vizuri ili nijue nianzie kujibu wapi" Kayoza nae alijibu kwa upole,

"Sawa. Ilikuwaje ukawaua wakina Stellah kule Guest?" Omary aliuliza huku akiwa na wasiwasi kidogo,

"Dah, sijui nianzaje kujibu, ila kifupi Stellah naweza kusema sijamuua ila Tausi nilimuua bila kutegemea" Kayoza alijibu huku machozi yakimtoka kuonesha kujutia kile alichokifanya,

"Sasa kama hukumuua Stellah ni nani alimuua wakati mlikuwa peke yenu chumbani?" Denis aliuliza,

"Mimi sijui ndugu zangu, niliamka asubuhi nikamkuta katika hali ile na sijui nini kilitokea" Kayoza alijitetea,

"Na Kwanini ulimuua Tausi?" Omary aliendelea kuuliza,

"Tausi nilimuua bahati mbaya baada ya kumziba mdomo asipige kelele alipouona mwili wa stelah, Kumbe wakati namziba mdomo nilimziba na pua akajikuta anashindwa kupumua" Kayoza aliwaeleza wenzake,

"Hiyo hali ya kubadilika na kuwa kiumbe cha kutisha inatokana na nini?" Denis alimuuliza Kayoza,

"Mimi?" Kayoza aliuliza huku akijioneshea kidole,

"Sasa kwani naongea na nani?" Denis nae aliuliza huku amemtolea macho Kayoza,

"Mnanishangaza mjue, mimi sijaiona hiyo hali initokee" Kayoza alitoa jibu lililofanya wenzake waangaliane,

"Tulivyoingia kwenye chumba alichoruelekeza Omary tumfuate, ulifanya nini?" Denis alimkumbusha Kayoza,

"Si tuliwakuta polisi watatu, alafu sikumbuki kitu zaidi ya kujikuta nimelala barabarani" Kayoza alitoa jibu jingine lililowashangaza wenzake,

"Makubwa basi, Ngoja nilale mie" Omary aliongea kisha akajifunika shuka na kuwaacha wenzake wakiendelea kuongea.

Saa kumi na moja alfajili waliamka na kuanza kujitayarisha kwa ajili ya safari.

Ilipotimia saa kumi na mbili kila mtu alikuwa tayari na wakatoka mpaka mapokezi, wakakabidhi chumba na kuondoka kuelekea stand ya mabasi, walitembea kwa miguu tu kwa maana haikuwa mbali na lodge waliyoichukua.

Walipofika karibu na Stand walishangaa kuona Askari wakiwa wengi, wamejitawanya eneo lile la Stand ya mabasi,

"Nadhani wako Pale kwa ajili yetu" Kayoza aliongea huku akisimama na wenzake pia wakasimama,

"Dah, kweli imeshakuwa tabu" Denis aliongea kwa kukata tamaa,

"Tunafanyaje sasa?" kayoza aliuliza,

"Turudi tukajipange" Denis alijibu,

"Hapa hakuna kurudi, ngojeni kwanza" Omary aliongea huku akiitoa simu yake na kumpigia Dereva taxi,

"Kwa hiyo akishakuja ndio tunafanyaje?" Kayoza aliuliza,

"Anatupeleka mpaka nje ya mji, alafu uko mbele tutashuka kuyasubiri mabasi" Omary aliwaambia wenzake,

"Hapo umefanya vizuri" Denis alimpingeza mwenzake kisha wakasubiri dakika kadhaa na taxi ikaja kuwachukua,

"Mpaka nzuguni utadai shilingi ngapi?" Omary alimuuliza dereva taxi,

"Elfu kumi na tano tu bosi wangu" Dereva taxi alijibu kwa unyenyekevu,

"Twendeni wanangu" Omary akawaambia wenzake ambao waliingia ndani ya gari.

Safari ikaanza, ubaya ilikuwa ni lazima upite karibu na Stand, wakati wanapita eneo hilo kulikuwa na gari ya polisi imeegeshwa pembeni huku likiwa na Askari wamekaa pembeni yake.

Gari waliyopanda wakina kayoza ikasimamishwa na wale Askari,

"Usisimame wewe" Omary alimsisitizia Dereva taxi ambaye alikuwa anataka kusimama,

"Kwanini nisisimame? Au nyie waarifu?" Dereva taxi alijibu huku akisimama,

"Acha upumbavu wewe" Denis aliyekaa kiti cha mbele aliongea huku akimsukumia Dereva nje na yeye akakaa kwenye kiti cha Dereva na kuiondoa gari kwa kasi.

Polisi kuona hivyo nao wakawasha gari yao na kuanza kuifukuza ile gari waliyokuwemo wakina Kayoza.

"Umefanya jambo la maana sana. Kumbe nawe ni jasiri hivyo?" Omary aliongea kumpongeza Denis kutokana na tukio alilolifanya,

"Ilikuwa haina namna" Denis aliongea huku macho yakiwa mbele,

"Lakini umeona wako nyuma wanatufuata?" Kayoza aliongea huku macho yake yakiwa nyuma,

"Nimeshawaona, hapa tuombe tu gari iwe na mafuta ya kutosha, vinginevyo hawatupati" Denis aliongea huku akizidisha mwendo wa gari,

"Kuwa makini lakini, usije ukatumwaga" Omary aliongea huku akitetemeka.

Gari zilifukuzana kwa mwendo wa dakika thelathini mpaka kwenye barabara moja nyembamba iliyo juu juu na chini kulikuwa na mabonde.

Kufika eneo lile, Denis akapunguza mwendo kwa kuwa barabara ni mbaya.

Gari ya polisi ikaongeza mwendo na kuwafikia kisha ikaigonga kwa nyuma gari waliyokuwemo wakina Denis na ile gari ikapoteza muelekeo na kupinduka kuelekea kwenye korongo huku ikibiringita zaidi ya mara kumi na kusimama ikiwa haitamaniki kwa jinsi ilivyopondeka baada ya ile ajali.

Gari ya polisi baada ya kuigonga gari waliyokuwamo wakina kayoza, nayo ilipoteza muelekeo na kuanza kubiringita kuelekea kwenye korongo na mwisho ikaenda kuokita ile gari waliyopanda wakina Denis na baada ya hapo ni damu tu zilitawala eneo lile......

+++++ITAENDELEA+++++

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA TISA.

______________
ILIPOISHIA..
_______________

Gari ya polisi ikaongeza mwendo na
kuwafikia kisha ikaigonga kwa nyuma
gari waliyokuwemo wakina Denis na
ile gari ikapoteza muelekeo na
kupinduka kuelekea kwenye korongo
huku ikibiringita zaidi ya mara kumi
na kusimama ikiwa haitamaniki kwa
jinsi ilivyopondeka baada ya ile ajali.

Gari ya polisi baada ya kuigonga gari
waliyokuwamo wakina kayoza, nayo
ilipoteza muelekeo na kuanza
kubiringita kuelekea kwenye korongo
na mwisho ikaenda kuokita ile gari
waliyopanda wakina Denis na baada
ya hapo ni damu tu zilitawala eneo
lile......

____________
ENDELEA..
____________

kilikua ni kishindo kikubwa sana,
na kwa kuwa eneo lile kulikuwa na
vimilima vidogo vidogo, zile gari
zikaanza kujibiringisha kuelekea
chini, zilijibingirisha kwa muda wa
dakika mbili, ya kwanza kusimama
ilikuwa ya polisi, alafu ya wakina
denis ikaja kujiegemeza kwa
pembeni yake, askari nane walikuwa
wamepoteza maisha na wengine
watatu walikuwa hawana fahamu.

Upande wa gari waliyopanda wakina Kayoza. Denis ambae ndo alikaimu nafasi
ya udereva alikufa pale pale, usukani
ulimbana sehemu za kifua na
kupelekea Denis kutokwa na damu
puani, masikioni na mdomoni, Omari
na Kayoza nao pia walipoteza
fahamu, tena kayoza alitupwa umbali
mrefu sana kutoka yale magari
yaliposimama, eneo lote kulikuwa na
harufu ya damu.

Baada ya robo saa, katika gari ya Polisi alionekana
askari mmoja akifumbua macho, ila
alikuwa hana nguvu za kutosha,
akajaribu kuinuka, ila akashindwa,
akasubiri mda kama dakika kumi, ndio
akapata nguvu kidogo za kujikongoja.

Akafungua mlango wa land cruiser ya polisi kisha akatoka nje.

Baada ya kutoka nje akaiangalia gari yao jinsi
ilivyo, kiukweli hakuamini kama amepona.

Akazunguka upande wa nyuma ya gari na kwa bahati nzuri gari yao ilikuwa imesimama, kwa hiyo aliweza kuwaona wenzie wakiwa wamelala kwenye bodi ila hawakuwa na fahamu.

Akaanza Kutoa msaada.
akawa anamtoa mtu mmoja mmoja,
paka wakakamilika kumi na yeye wa
kumi na moja, akaenda katika mlango wa pili wa pili wa gari kumtoa Askari aliyekuwepo kakaa kiti cha mbele ambaye alikuwa Sajenti Minja kisha akakitoa kidumu cha lita 5 ambacho kilikuwa na maji, akawa
anawamwagia kidogo kidogo, ila ni
wawili tu ndo walikua wamezinduka,
kati yao alikuwepo Sajenti Minja,
ambae alikuwa hana majeraha mengi
sana usoni.

Sajenti Minja alipopata
nguvu, akaenda moja kwa moja hadi
kwenye gari ambalo walikuwemo wakina Kayoza,

"shit" Sajent Minja alisema maneno hayo
baada ya kuhisi watuhumiwa wote
wamekufa,

Akawatoa ndani ya gari,
akawalaza nje, lakini aliwakuta wawili tu, Omary na Denis ambaye alikuwa ameshakufa muda mrefu na Omary ambaye alikuwa hana fahamu.

"hivi hapa ni wapi?,
maana hata sioni dalili ya kuwepo
mtu eneo hili?" Sajent Minja alihoji wenzake,

"duh! Hata mi sipajui" mwenzake
alijibu huku akitupa macho yake kule na huku.

Baada ya muda kidogo. Omary alianza kuijgeuza geuza ikiwa ni ishara ya kurejewa na fahamu,

"ah, ebu mmwagieni maji huyo" Sajenti Minja
akatoa amri huku akimnyooshea kidole Omary.

Wakammwagia Omary maji na akakurupuka huku akijishangaa huku akiwa na maswali mengi kichwani mwake, ila
alionekana ana maumivu sehemu ya
mguu wa kushoto, hasa kwenye goti,

"nyie mbwa mmetusumbua sana, na
hamna haki ya kuendelea kuishi"
Sajenti Minja aliongea maneno hayo
huku akichomoa bastola yake kutoka
katika maeneo ya kiuno, kisha
akaikoki, alafu mdomo wa bastola
akauelekeza kwa
omari.

*****************

Baada ya muda mrefu wa kulala, Kayoza akakurupuka, akawa anahisi
maumivu eneo lote la kichwa,
akajaribu kuvuta kumbukumbu,
akakumbuka yote yaliyosababisha
kuwepo pale.

Ila alishangaa mbona haoni magari aliyopata nayo ajali na pia lile eneo alijikuta yupo peke na swali jingine akajiuliza wenzake wako wapi?

Akajiinua na kuanza kuranda randa lile eneo, na mwisho akawa anasikia sauti za watu wakibishana kwa mbali sana.

Akaamua aanze kuifuatilia zile sauti.

Alitembea mwendo wa dakika tano, akaanza kuhisi arufu ya damu puani ni kutokana na damu zilizomwagika eneo la ajali zilikuwa zinatoa harufu.

Akaanza kuhisi kizungu zungu na mwisho akaanguka chini na kuanza kugalagala huku mwili wake ukianza kubadilika taratibu na kuwa katika umbo la kutisha. Ilimchukua dakika chache za mabadiliko na alipokamilika, alisimama na kuanza kukimbia kuifuata harufu ya damu aliyokuwa anaisikia.

Baada ya dakika kadhaa aliweza kuyaona yale magari waliyopata nayo ajali yakiwa yameegemeana. Pia aliweza kumuona Omary yuko mbele ya watu
watatu ambao ni Askari, huku akinyooshewa bastola.

Pembeni ya Omary kulikuwa na maiti
ambae alikuwa katapakaa damu
mwili mzima, huyu ndiye aliyemvutia zaidi Kayoza.

Sajenti Minja akiwa na wenzake huku bastola yake akiielekeza kwa Omary, walisikia kichaka kikipiga kelele kama kuna mtu au mnyama ndani yake,

"Mh..nini hicho?" Askari mmoja aliwauliza wenzake,

"Simba nini?" Askari mwingine aliuliza baada ya ule mtikisiko kuwa mkubwa,

"Simba hawezi kuishi katika kakichaka kama haka" Sajenti Minja alijibu huku macho yake pia yakiwa yanaangalia sehemu zinapotokea hizo kelele,

"Usidharau mkuu, Simba anaishi mahali popote penye chakula" Askari mwingine aliongea.

Wakiwa bado wako katika sintofahamu, Kayoza alichomoza kama mshale na akawa anaelekea eneo
walilopo, wakina Sajenti Minja. Nao
walimuona pia, mmoja akakimbilia
ndani ya gari, akatoka na bunduki,

"usimpige" Sajenti Minja,
akamwambia yule askari mwenye
bunduki.

"sasa mkuu huoni anakuja
upande wetu" Askari akajaribu kujitetea huku akiwa bado na bunduki yake mikononi

"ngoja kwanza, labda hawezi kuwa na madhara" Sajenti
Minja akajibu huku wote Wakiwa hawajui kile ni kiumbe cha aina gani?.

Kayoza aliendelea kuwasogelea na alipofika
pale, akaenda karibu ya Omary, akamuangalia kwa dakika kadhaa,
Omary alikuwa anatetemeka mpaka
mkojo ukamtoka.

Kisha Kayoza
akaikota maiti ya pembeni ya Omary, ambayo ilikuwa ni maiti ya Denis.

Akailamba damu iliyopo katika ile
maiti kisha akaitupa ile maiti.

Kipindi chote hicho Askari walikuwa wanaangalia kinachoendelea.

Kayoza akawa
anaelekea upande waliopo wale
Polisi, wale askari kuona vile, yule
mwenye bunduki akampiga risasi Kayoza,
Kayoza akasimama, kisha akaangalia
eneo ambalo risasi ilipita, akaingiza
kucha akaitoa, kisha kwa kasi ya hatari alikimbia kumuelekea yule Askari aliyempiga risasi na akamrukia, akatua shingoni akaanza kumfyonza damu,
wale wengine kuona vile wakaanza
kukimbia, ila walichelewa, mmoja
alishikwa akapigwa kucha ya tumbo,
kayoza alipovuta kucha zake, zikatoka
na utumbo wote, mwingne
akanyonywa damu kama mwenzake.

Sajenti Minja
akaona njia sahihi ya kujiokoa ni
kuingia chini ya uvungu wa gari, akaingia,
Kayoza hakumuona.

kayoza alipomaliza kumnyonya yule askari,
akamuona Omari kashika bastola
anachungulia chini ya gari, Kayoza
kama mshale, akalisogelea lile gari,
kisha akalibeba juu, akalitupa
umbali mrefu. Alikuwa na nguvu kwelikweli, kama mashine au mnyama mkubwa.

Baada ya kurirusha gari, akawa anamsogelea
Sajenti Minja aliyekuwa amelala chini huku akiwa amekata tamaa.

Kayoza alipomfikia,
akamkamata Majenti Minja mabega na kumnyanyua juu, Sajenti Minja akawa kama ametundikwa.

Kayoza akamvuta karibu na kumkumbatia kisha akawa anaupeleka mdomo wake
shingoni kwa Sajenti Minja kwa huku meno yakiwa tayari kumng'ata Sajenti Minja.

Sajenti Minja akafumba macho huku akiwa tayari amekubaliana na matokeo..

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO..

SEHEMU YA KUMI.

______________
ILIPOISHIA
______________.

Sajenti Minja akaona njia sahihi ya kujiokoa ni
kuingia chini ya uvungu wa gari, akaingia,
Kayoza hakumuona.

kayoza alipomaliza kumnyonya yule
askari, akamuona Omari kashika bastola
anachungulia chini ya gari, Kayoza kama mshale, akalisogelea lile gari,
kisha akalibeba juu, akalitupa umbali mrefu.

Alikuwa na nguvu
kwelikweli, kama mashine au
mnyama mkubwa.
Baada ya kurirusha gari, akawa anamsogelea
Sajenti Minja aliyekuwa amelala chini huku akiwa amekata tamaa.

Kayoza alipomfikia,
akamkamata Sajenti Minja mabega
na kumnyanyua juu, Sajenti Minja akawa kama ametundikwa.

Kayoza akamvuta karibu na kumkumbatia kisha akawa anaupeleka mdomo wake
shingoni kwa Sajenti Minja huku
meno ya Kayoza yakiwa tayari kumng'ata Sajenti Minja.

Sajenti Minja akafumba macho huku akiwa tayari amekubaliana na matokeo

____________
ENDELEA..
____________
Kayoza akaingiza meno kwenye
shingo ya Sajenti Minja na kuanza kumnyonya damu, ghafla
akamuachia huku akiwa anamuangalia kwa
mshangao.

Kayoza akamuangalia
Sajenti Minja kwa dakika kadhaa. Akamfuata tena na kumshika kichwani Sajenti Minja huku akimgeuza geuza kichwa kumuangalia kama mtu anayemjua, kisha akamuachia na kugeuka nyuma huku akianza kuondoka jirani na Sajenti Minja.

Alipopiga hatua mbili tú ghafla akaanguka chini akapoteza
fahamu.

Sajenti Minja aliendelea kuganda tu,
huku yanayomtokea akihisi labda
huenda ni ndoto. Baada ya kumuona Kayoza ameanguka, sasa akawa kama
kagutuka, akatoka mbio kuelekea
eneo ambalo litakua ni salama kwake, na njia aliyokua anaelekea ni ile iliyokuwa inaelekea barabarani.

Alikimbia huku kila dakika akigeuza
shingo kuangalia kama Kayoza anamfuata
kwa nyuma, huku jeraha lake la
shingoni kalifunika na kiganja cha
mkono.

Alipowapoteza kabisa
machoni kwake, akagutuka, kisha
akaingiza mkono mfukoni, akatoa
simu, akatafuta namba anayoijua
yeye, alafu akapiga, akaonekana
kukunja sura

"hili eneo gani, hata
network hakuna?" Sajenti Minja aliongea peke yake kisha akairudisha simu
mfukoni, akakimbia kama dakika saba hivi,
ndio akaiona barabara kwa mbali.

Akajitahidi kuongeza mwendo hadi akaifikia.

Alipifika alikuwa anahema haraka haraka huku kila muda akiangalia njia aliyotokea.

Magari mawili ya mwanzo alipoyasimamisha
yalimpita, ni kutokana na hali
aliyokuwa nayo, vidonda, damu
ilimtapakaa karibia eneo lote la
mwili wake na pia eneo alilokuwepo lilikuwa linatisha na kingine cha ziada ni kwamba hakuvaa sare za polisi,

"mh....hapa nisipotumia
akili naweza kulala huku huku" Sajenti Minja alijisemea peke yake.

Gari la tatu
lilikuwa Toyota prado, na
ayelikuwa anaendesha ni mwanamama na
siti ya pembeni yake alikaa
msichana ambaye nadhani alikuwa ni mwanaye.

Sajent Minja akaichomoa
bastola yake kiunoni, kisha akawa
ameilenga ile gari na akitoa amri
isimame, yule mama akaisimamisha
huku akionekana ana hofu,

"mnaelekea wapi?" Sajenti Minja
akawauliza.

"singida mwanangu"
yule mama akajibu huku akitetemeka.

Sajenti Minja akawaonyesha kitambulisho chake,
ndipo hofu ikawatoka, kisha
akawaomba msaada, wakamkubalia,
akajipakia katika gari na kisha wakaishia

*****************

Baada ya Sajenti Minja kuondoka eneo la tukio,
ilichukua mda kama wa dakika tano
kayoza kupata fahamu.

Alishtuka akamkuta Omary yuko pembeni yake,

"mapolisi wameenda wapi?" Kayoza ndio
lilikuwa swali lake la kwanza kumuuliza
Omary,

"umewaua" Omary akajibu na kumfanya Kayoza ashangae,

"Mimi nimewaua?" Kayaza aliuliza kwa mshangao,

"Ndio, si hapo wamelala" Omary alijibu huku akiwaonyeshea kidole Askari waliikuwa wamekufa,

"na Denis nae kaenda wapi?" Kayoza akauliza
tena.
Hapo wote wakashtuka,
wakaenda kuingalia gari waliyokuwa
nayo lakini hawajamkuta, ndipo Omary akakumbuka kuwa aliporejewa na fahamu pembeni yake kulikuwa na mtu, ndipo alipohisi huyo mtu atakuwa Denis.

Wakarudi mpaka eneo la mwanzo, masikini ya mungu, walimkuta
Denis Paul Simiwe, akiwa amelala
huku damu zikiwa zimeganda kwenye
pua na midomo yake.
wote wakajikuta machozi yanawatililika mashavuni.

"Tuondoke, hili eneo sio salama" Omary alimtahadhalisha Kayoza,

Wakachukua kitambulisho cha Denis
kama kumbukumbu ya jamaa yao,
kisha wakabeba mabegi yao, wakawa
wanaelekea barabani.

walipofika barabarani
walikaa kama nusu saa, wakaiona
gari ndogo inakuja na aliyekuwa anaendesha ni mzee mmoja wa makamo.
Omary alisimama katikati ya barabara na kuipungia
mkono ile gari, ikasimama,

"shikamoo mzee"
wakamsalimia kwa pamoja,

"marhaba waheshimiwa" Mzee makamo aliwaitikia.
"mzee tunaomba
Lifti" Omary akasema katika sauti
tulivu,

"mnaelekea wapi?" Mzee wa makamo akawauliza,

"tulikuwa tunaenda
tanga, ila hata ukitufukisha eneo
lenye usafiri tutakushukuru" Omary akajibu,

"vizuri, hata mi naelekea
Tanga, mbona mko katika hali hiyo?"
yule Mzee wa makamo akauliza baada ya kuwaona wana damu katika baadhi ya sehemu mwilini,

"tumepata
ajali"Omary akajibu huku akijifuta damu shavuni,

"poleni sana,
ingieni twendeni" Mzee
akaongea.

Wakaingia, safari ikawa
inaendelea, mwendo kama wa nusu
saa hivi, yule mzee kupitia kioo cha
juu mbele, alishuudia kitu,
kinachoendelea kwenye siti ya
nyuma, ambayo walikaa wakina
kayoza, akapata mshtuko,
akapunguza mwendo wa gari, kisha akageuka ili kuhakikisha kama ni kweli au kioo kinamdanganya?..

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
Hahaha iko ki vampire kiaina..the walking dead... Tuko pamoja kamarade!
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA KUMI NA MOJA.

_______________
ILIPOISHIA..
_______________

Wakaingia, safari ikawa
inaendelea, mwendo kama wa nusu
saa hivi, yule mzee kupitia kioo cha
juu mbele, alishuudia kitu,
kinachoendelea kwenye siti ya
nyuma, ambayo walikaa wakina
kayoza, akapata mshtuko,
akapunguza mwendo wa gari, kisha
akageuka ili kuhakikisha kama ni
kweli au kioo kinamdanganya?..

____________
ENDELEA..
____________
"mbona unalia kijana?" yule mzee alimuuliza
kayoza,

"ni maumivu tu, mzee
wangu" Kayoza akadanganya huku akijifuta machozi, ila
kilichokuwa kinamliza, ni mambo ya ajabu ambayo yanayomtokea, na kikubwa
haswa ni kumpoteza rafiki yake,
denis. Mzee akairudisha gari barabarani baada ya kuridhika na majibu ya Kayoza.

Gari ikaenda hadi morogoro
mjini, yule mzee akaipaki gari nje ya
hoteli moja maarufu pale Morogoro.

"twendeni tukale waheshimiwa" Yule mzee
aliwaambia wakina Kayoza huku
akiuchomoa ufunguo wa gari kutoka
mahali pake, wakina kayoza
wakashuka, huku kila mmoja akiwa
kabeba suruali na fulana ili wakazivae mariwatoni, kwa hali
waliyokuwa nayo, watu wengi
waliwashangaa kutokana na nguo zao kuchanika na kuchafuka kutokana na ajali waliyoipata.

Wakaingia hadi ndani, kisha Omary akaomba
kuelekezwa choo kilipo,
alipoonyeshwa, wakaenda kisha
wakabadili nguo, alafu wakarudi
kujumuika na yule mzee pale
mezani.

Baada ya kumaliza kula,
wakajipakia kwenye gari, kisha safari
ikaendelea.

"mnaenda Tanga katika
eneo gani?" Mzee yule aliwauliza wakati
gari ikianza kushika kasi.

"Chumbageni" Omary akajibu huku safari ikiendelea.

Tanga mjini waliingia saa nne usiku. Yule mzee
akawashusha, wakamshukuru sana,
kisha yule mzee akaendelea na safari
zake, hakuna aliyejua yule mzee alikuwa
anaelekea wapi?, ila walichoshukuru
ni kufika salama.

"kwa muda huu
hatuwezi kupata usafiri, itabidi tutafute guest ya kulala, kesho
tutaamka na hiyo safari yachumbageni" Omary alimwambia
Kayoza hayo maneno,

"mi nakusikiliza wewe" Kayoza ndivyo
alivyomjibu. Wakatafuta nyumba ya wageni, wakaipata.

wakaweka mizigo yao,
kisha wakaenda kutafuta chakula, waliporudi wakalala.

Waliamka saa
nne za hasubui, wakaoga, kisha
wakaenda kupata chai, alafu
wakarudi kuchukua mabegi yao,
safari ya kwenda Chumbageni
ikaanza, wakaulizia sehemu
yanapopaki magari ya Chumbageni,
wakaonyeshwa, wakatafuta gari
iliyokuwa karibu kuondoka,
wakajipakia.

**************

Sajenti Minja alifikia moja kwa moja kituo
kikuu cha polisi, akatoa ile taharifa
ya mauaji, ikatayarishwa gari,
ikambeba yeye pamoja na askari
wengine watatu, wakaondoka, huku
nyuma wakifuatiliwa kwa karibu na
gari la wahandishi wa habari,
wakaenda hadi eneo la tukio,
likapigwa picha pamoja na maiti
zote, kisha miili ya marehemu
ikawekwa ndani ya gari, safari ya
kurudishwa Dodoma mjini ikaanza,
walipofika, maiti zote zikaenda
kuifadhiwa katika monchwari ya
hospitali ya mkoa, kisha polisi
wakafanya kikao na waandishi wa
habari, kuhusu ule mlolongo wa
matukio ya kutisha, ila kwa bahati
nzuri, Sajenti Minja alikuwa na
kitambulisho cha Omari Said Mkwiji,
kwa hiyo akawapa nafasi waandishi
wa habari waipige picha, huku
Sajenti Minja akiwaambia ile picha ni
ya mmoja kati ya wale watuhumiwa
watatu wa mauaji na akaongeza
kuwa mtuhumiwa mwingine (Denis)
amekufa katika ajali iliyotokea wakati
wanakimbizana na polisi.

Kesho yake asubuhi, magazeti yote yalitoka na
habari hizo za mauaji, na pembeni
ya hizo habari kulikuwa na picha
kubwa ya Omari, akitajwa kama
mmoja wa wahusika wa mauaji ya unyonyaji damu.

*******************

Wakina kayoza walipoingia ndani ya basi, walikaa
siti ya nyuma kabisa, siti ya mbele
yao walikaa wakina mama wawili
ambao walikuwa wanazungumzia juu
ya mauaji ya kutisha yaliyotokea kati
ya Dodoma na Morogoro.

"na tena hadi picha ya muuaji imetolewa"
mama mmoja wapo. ambae alikuwa
kabeba mtoto katika miguu yake
alikuwa akimsimulia mwenzie,

"imetolewa na gazeti gani?" yule
mama mwingine wa makamo
akamuuliza yule mama mwenye
mtoto.

"magazeti yote unayoyajua
wewe wametoa hiyo habari" mama
mwenye mtoto akajibu.

"chumbageni
si hapo tu tunakaribia, nitanunua
gazeti ili na mimi nione" yule mama wa makamo
akajibu.

Kipindi chote wakati
wanaingia, hadi safari ilipoanza,
wakina Omary walikuwa
wanawasikiliza tu, ila habari
iliyowashtua ni kuchapishwa kwa
picha ya Omary kwenye magazeti.

"Bab hii ishu imeshakuwa kubwa kupita kiasi" Kayoza alimwambia mwenzake wakati wale wakina mamá wanaongea,

"Maji tumeshayavulia nguo, kuyaoga haina budi" Omary aliongea kwa sauti ndogo,

"Maisha ya kukimbia kimbia tutaishi mpaka lini sasa?" Kayoza aliuliza kwa masikitiko,

"Kila lenye mwanzo halikosi mwisho" Omary alijibu kifupi.

Walipofika karibu na
chumbageni, ile gari ikasimama kwa
dharura, kulikuwa na mushkeli katika
upande wa injini, wale wakina mama
wakanunua gazeti, wakawa wanasoma
ile habari

"mimi nikimuona, yaani
haraka nawajulisha polisi" yule
mama mwenye mtoto aliongea.

"hata mimi, mwenzangu milioni kumi
nyingi" yule mama wa makamo
akajibu baada ya kusoma habari
kuwa atayemkamata au atakayefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa atapewa kiasi
hicho cha pesa, kipindi chote hicho wakina Kayoza walikaa tu kwenye siti za nyuma ya gari, hawakuthubutu kushuka.

Gari lilipotengemaa likaendelea na
safari. Kipindi chote Omari alikuwa
kaielekeza sura yake sanjari na
dirisha ili kukwepa sura yake isionekane na abiria wengine kwa maana alishapatwa na wasiwasi.

Gari ikafika mwisho wa safari,
watu wakaanza kutelemka, wale
wakina mama kwa ajili ya kuwa na
mtoto, ikabidi wasubiri ili watu wote watoke na wao watoke wa
mwisho, sasa wakati wakina kayoza
wanawapita, Omary akamkanyaga yule
mama mwenye mtoto kwa bahati
mbaya,

"samahani mama" Omary
akamtaka radhi yule mama huku akimwangalia
usoni, yule mama akapata mshtuko,

"ah!, si ndo
huyu?" Yule mama alisema kwa kupayuka..

*****ITAENDELEA*******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO..

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

_______________
ILIPOISHIA..
_______________

Gari ikafika mwisho wa safari,
watu wakaanza kutelemka, wale
wakina mama kwa ajili ya kuwa na
mtoto, ikabidi wasubiri ili watu wote
watoke na wao ndio watoke wawe wa
mwisho, sasa wakati wakina kayoza
wanawapita, Omary akamkanyaga
yule
mama mwenye mtoto kwa bahati
mbaya,

"samahani mama" Omary
akamtaka radhi yule mama huku
akimwangalia
usoni, yule mama akapata mshtuko,

"ah!, si ndo
huyu?" Yule mama alisema kwa
kupayuka..

____________
ENDELEA...
_____________

"sio mimi" Omary aliongea bila kutarajia huku akijinasua kutoka kwenye mkono wa yule mwanamke, kisha wakatoka haraka ndani
ya ile gari na kukimbilia nje.

Yule mama akachukua
gazeti kutoka kwa mwenzake, kisha
akaiangalia ile picha ya Omary iliyokuwepo katika gazeti

"mh!, haswaa
ndiye yeye" Yule mama akajisemea moyoni, kisha
akatoka kwa lengo la kuwatazama
walipoelekea wakina Omari, ila
alichelewa, akakuta peupe.
akaangaza tena, hakuona mtu,
akaishia kusonya.

Baada ya wakina
kayoza kufanikiwa kushuka kwenye
gari, wakakimbilia nyuma ya ile gari,
wakawa wanamchunguza yule mama,
paka alivyotoka ndani ya gari na kuanza kuangaza
walikuwa wanamuangalia, mpaka ule
msonyo uliotolewa na yule mama pia waliusikia, wakasubiri mpaka yule mama alipoondoka, nao
ndio wakaondoka ila kwa kujificha ficha sana nyuma ya magari mengine yaliyokuwepo pale.

"Yaani tayari habari zimeshasambazwa katika vyombo vya habari?" Omary alimuuliza mwenzake wakiwa tayari wameshatoka katika kituo cha mabasi,

"Tena wamechelewa kweli, ilitakiwa watoe taharifa jana" Kayoza alijibu huku akikagua mandhari ya mji wa Tanga,

"Ebu twende pale tukasome some magazeti" Omary aliongea huku akielekea sehemu ambapo kulikuwa na magazeti yametandazwa juu ya meza,

"Acha ujinga wewe" Kayoza aliongea huku akiwa anamzuia Omary,

"Kwanini?" Omary aliuliza huku akimshangaa Kayoza,

"Unajua kuwa sisi tunatafutwa na mbaya zaidi picha yako ndiyo imeonekana kwenye magazeti, kwa hiyo wewe huoni kwenda eneo kama lile ni rahisi sana kukamatwa?" Kayoza aliuliza baada ya maelezo marefu,

"Ila kweli, basi nenda wewe kaangalie, alafu uje unijulishe" Omary alimwambia Kayoza,

"Mimi naenda, ila sio kuangalia. Naenda kununua gazeti tutaenda kusoma mbele Safari" Kayoza aliongea huku akielekea pale walipotandaza magazeti mezani. Alifika na kununua magazeti mawili ya kisiasa na jamii na kisha akarudi mahali Omary alipo na kumpa gazeti moja, nae akabaki na moja,

"Alafu ujue umenishangaza sana" Omary alimwambia Kayoza,

"Kwanini?" Kayoza aliuliza,

"Kwanini yule Askari mweupe haujamuua?" Kayoza aliuliza huku akimaanisha Sajenti Minja,

"Mimi?" kayoza aliuliza tena,

"Ndio, ni wewe" Omary alikazia swali lake,

"Sasa mimi nitajuaje wakati unajua kabisa mimi nikiwa katika hali ile uwa sijitambui?" Kayoza nae alijibu kwa mtindo wa kuuliza,

"Hicho kitu kimenishangaza sana" Omary aliongea huku akiendelea kushangaa,

"Wewe mwenyewe uwa sikudhuru na Kwanini hushangai?" Kayoza alimuuliza Omary,

"Dah, tuachane na hayo, maana tukiulizana sana hatutapata majibu ila tutaongeza maswali" Omary aliamua kupotezea huo mjadala,

"Na mbona hawajaandika habari za Denis katika haya magazeti?" Kayoza alimuuliza Omary,

"Hata mimi sijaelewa, au labda kuna sababu waliyofanya wafiche kifo chake?" Omary aliongea ila wote walilijadili jambo hilo huku wakiwa na huzuni,

"Muda bado upo, Ngoja tusubiri habari za kesho, labda wanaweza kuja na habari zake" Kayoza aliongea na baada ya hapo ukimya ukafuata.

*******************

Sajenti Minja hakuwa na raha kabisa siku hiyo, maana ndani ya siku chache alishuhudia vifo vya ajabu sana na pia na yeye aliponea chupuchupu kufa na akaachwa na alama ya meno kwenye shingo,

"Kiongozi bora uende hospitali ukaangaliwe kama ayo meno yanaweza kukuletea madhara" Askari mmoja alimshauri Sajenti Minja,

"Nina mpango huo, ila mkuu amesema anataka kuongea na mimi muda huu, so nasubiri nimalize nae maongezi ndio niende hospitali" Sajenti Minja alimjibu yule Askari na muda huo huo kuna Askari mwingine akaja kumwambia Sajenti Minja kuwa anahitajika na mkuu.

Sajenti Minja akanyanyuka na kwenda moja kwa moja ofisini kwa mkuu wake.

"Poleni kwanza kwa matukio mabaya" Mkuu wa polisi aliongea baada ya salamu,

"Tumeshapoa" Sajenti Minja alijibu kwa unyonge,

"Nini maoni yako kuhusu hii kesi?" Mkuu wa Polisi alimuuliza Sajenti Minja,

"Naomba mnitoe kwenye hii kesi, naona kama nimeishindwa" Sajenti Minja aliongea kwa heshima mbele ya mkuu wake,

"Kwanini?" Mkuu aliuliza,

"Nafikiri hiyo ndio njia pekee ya kuweka maisha yangu salama, maana wale tunaowafuatilia sio watu wa kawaida" Sajenti Minja alimueleza mkuu wake,

"Wewe unadhani kufanya hivyo ni sahihi?" Mkuu aliuliza,

"Nadhani inaweza kuwa sahihi" Sajenti Minja alijibu,

"Sawa, nakupa muda wa kwenda kujiuliza tena kuhusu hili, alafu kesho uje tena kuzungumza kuhusu jambo hili hili" Mkuu aliongea na kumruhusu Sajenti Minja aondoke.

Sajenti Minja akatoka na akili yake yote akaielekeza hospitali kwa nia ya kwenda kuangalia kama jeraha aliloachiwa na Kayoza lina madhara gani.

********?******

Kayoza na Omary baada ya mwendo mrefu kutoka kituo cha mabasi, Wakatafuta
baiskeli za kuwafikisha kijijini, bahati
nzuri wakaipata. Walitumia muda wa
dakika ishirini kufika kijiji husika,
wakawalipa madereva ujira wao,
kisha wakaanza kutembea kwa
miguu, walitembea hadi wakafika
sehemu moja, ambayo kulikuwa na
kajumba kadogo kamejitenga kidogo
na nyumba nyingine,

"sijui ndio hapa, ebu ngoja tujaribu" Omari
aliongea bila ya uhakika,
wakiisogelea ile nyumba, kisha wakagonga mlango,

"karibu" sauti
ikajibu kutoka ndani, wakasubiri
mwenyeji hatoke, lakini hakuna
aliyetoka, wakarudia tena kugonga

"shabashi, pita ndani" ile sauti ikajibu kwa ghadhabu kidogo, Omari
akausukuma mlango kisha akaingia,
akamkuta mzee mmoja mfupi mweupe, kavaa baraghashia,

"shikamoo babu" 0mari akamsalimia
kwa furaha.

"marhaba, karibu" yule
mzee aliitikia huku sura yake
ikionesha anajaribu kuvuta
kumbukumbu fulani.

"asante" 0mari
akajibu huku akitambua alichokuwa
anakifikiria babu yake,

"Karibuni mkae" Yule mzee aliongea huku akiendelea kuvuta kumbukumbu,

"babu mimi
mjukuu wako 0mari" Omari akasema huku akitabasamu,

"omari, omari, Omary wa wapi? " Babu aliuliza akiwa bado
anafikiria huku akijaribu kuvuta
kumbukumbu.

"omari mkwiji mtoto wa mwanao wa Dodoma" Omari akamsaidia babu yake kumuelewesha.

"ooh, karibu babu, vipi
mbona umekuja bila taharifa" Babu
akauliza huku akimpa mkono Omary na Kayoza.

"ni matatizo babu,
nitakusimulia tu babu" 0mari akamwambia babu yake huku akifurahi babu yake kumtambua,

"Naona umekuja na mwenzako?" Babu akamuuliza Omary,

"ndio babu" 0mari akajibu,

"karibu kijana" Babu akamwambia Kayoza huku
akimpa mkono, ila kitu cha ajabu,
babu aliung'ang'ania mkono wa
kayoza kwa dakika mbili nzima huku akiwa amemkazia macho,

"kijana una mzigo mzito sana wa matatizo" Babu alimwambia Kayoza huku machozi yakimtoka....

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO..

SEHEMU YA KUMI NA TATU.

______________
ILIPOISHIA..
______________

"ooh, karibu babu, vipi
mbona umekuja bila taharifa" Babu
akauliza huku akimpa mkono Omary
na Kayoza.

"ni matatizo babu,
nitakusimulia tu babu" 0mari akamwambia babu yake huku
akifurahi babu yake kumtambua,

"Naona umekuja na mwenzako?"
Babu akamuuliza Omary,

"ndio babu" 0mari akajibu,

"karibu kijana" Babu akamwambia
Kayoza huku
akimpa mkono, ila kitu cha ajabu,
babu aliung'ang'ania mkono wa
kayoza kwa dakika mbili nzima huku
akiwa amemkazia macho,

"kijana una mzigo mzito sana wa matatizo" Babu alimwambia Kayoza
huku machozi yakimtoka..

_____________
ENDELEA....
_____________

kayoza akashtuka,

"hapana babu, mimi
niko sawa tu" Kayoza akamjibu babu
huku akijilazimisha kutabasamu,

"kijana jaribu kuwa mkweli,
vinginevyo utapata matatizo zaidi ya hayo
yaliyokukuta" Babu akamsisitiza
Kayoza,

"babu tutakusimulia baadae" Omary akaingilia kati baada ya kuona Kayoza hawezi kukubali.

Babu yake na Omary
anaitwa Mzee Salum Said Omari
Shekindile Mkwiji, ila jina maarufu
lililozoeleka kwa watu wa pale
kijijini, wanamuita Mzee Mkwiji,
huyu mzee katika maisha yake ya
ujana alioa wanawake saba na
kuwazalisha watoto zaidi ya hamsini,
na ana wajukuu wasio na idadi, ila
kitu ambacho kilichokuwa
kinawachanganya watoto wake, ni
kuwa huyu mzee hakuitaji kabisa
msaada wao, wakimpelekea pesa,
anawarudishia.

Kuna kipindi watoto wake walijipanga
wamjengee nyumba nzuri, akakataa,
ila watoto wake hawakujua sababu
ya yote hayo, ila sababu aliijua
mwenyewe mzee Mkwiji, na sababu
yenyewe ni kuwa na mizimu ya
kiganga aliyorithishwa na baba yake,
ambayo yenyewe inataka anayeimiliki
awe anatoa tu misaada, na asiwe
anapokea, anaishi peke yake, wake
zake watano walishafariki, na wawili
aliwapa talaka.

Ni mganga
anayependwa sana katika eneo
analoishi.

Baada ya kupata chai na
mihogo, Omary na Kayoza walimsaidia
kazi ndogo ndogo babu yao, baada
ya shughuli za hapa na pale kuisha,
wakatindika mkeka nyuma ya
nyumba, wakaanza kumsimulia Mzee
Mkwiji, kuanzia mwanzo hadi
mwisho, Mzee Mkwiji aliwasikiliza
kwa makini, kisha akaingia ndani
kwake akatoka na kibuyu kidogo,
alafu akamwambia Kayoza ateme
mate chini, Kayoza akatema, Mzee
Mkwiji akamimina dawa kidogo
kutoka kwenye kibuyu alafu
akaichanganya na mate ya kayoza,
ukatokea moshi mweusi, ukawa
unapanda juu kuelekea mashariki,

"mh, kazi ipo" Mzee Mkwiji
akajisemea huku akitingisha kichwa kwa masikitiko, kisha akarudia tena
kufanya kama mwanzo, sasa hivi ule
moshi ulipotoka, ukaingia puani kwa
mzee Mkwiji, kisha akapiga chafya,
akawa kama kasinzia, alikuwa katika
hali hiyo kwa muda ya dakika tatu, kisha
akafungua macho na kusema,

"pole
sana kijana, ningekusaidia ila
mizimu yangu imeingiwa na uoga
kupambana na mzimu ulionao" Mzee Mkwiji aliongea huku akimuangalia Kayoza kwa jicho la huruma,
Kayoza akapoteza matumaini, ila
babu akaendelea kumwambia,

"mama yako ndio anaweza kuwa
msaada mkubwa kwako" Mzee Mkwiji alitoa kauli ilijenga swali kwa Kayoza,

"Samahani babu, umesema nina mzimu?" Kayoza aliuliza kanakwamba hakumsikia Mzee Mkwiji,

"Tena wa hatari sana" Mzee Mkwiji alijibu,

"Sasa unaposema mama yangu ndio anaeweza kuwa msaada kwangu hapo unanivuruga kidogo, kwa maana mama yangu sio mganga, kwa hiyo ni vipi atakuwa msaada kwangu?" Kayoza alimuuliza Mzee Mkwiji,

"Kwa kweli hilo swali nitashindwa kukujibu, ila mizimu yangu ndio imeniambia hivyo" Mzee Mkwiji alijibu huku akimwaga yale maji yake aliyofanyia uganga,

"Ila naweza kupona, si ndio?" Kayoza alimuuliza tena Mzee Mkwiji,

"Kama mizimu imesema msaada upo, basi unaweza kupona" Mzee Mkwiji alitoa jibu lililompa matumaini Kayoza,

"Sasa inabidi kesho tu nisafiri, niende kwa mama" Kayoza aliongea huku akimuangalia Omary,

"Ungepumzika kwanza mjukuu wangu, yaani jana umekuja alafu uondoke kesho? Shinyanga ni mbali kutoka hapa" Mzee Mkwiji aliongea na kumfanya Kayoza ashtuke,

"Umejuaje Nataka niende shinyanga?" Kayoza aliuliza huku akishangaa,

"Si ndio mama yako yupo uko?" Mzee Mkwiji nae aliuliza badala ya kujibu,

"Ndio, sasa umejuaje yupo uko?" Kayoza aliuliza tena huku akistahajabu maono ya Mzee Mkwiji,

"Sina uganga wa kubahatisha, mizimu yangu uwa inaniambia ukweli" Mzee Mkwiji alijibu huku akitabasamu,

"Aisee wewe mzee ni kiboko" Omary aliongea huku akicheka,

"Kama nilivyosema hawali, kesho naondoka" Kayoza alirudia Kutoa taharifa,

"Itabidi twende wote" Omary aliongea,

"Wewe baki tu ndugu yangu, msaada ulionipa ni mkubwa sana. Nakushukuru sana" Kayoza alimwambia Omary,

"Hapana siwezi kubaki, kama kutafutwa ni mimi ninayetafutwa kwa maana picha yangu ndio ipo katika vyombo vya habari, kwa hiyo ni bora niwe na wewe popote niendapo kwa maana wewe pekee ndiye unaweza kuniokoa mikononi kwa polisi" Omary aliongea kwa huzuni,

"Omary unafuata kifo uko" Mzee Mkwiji alimwambia mjukuu wake,

"Kivipi babu?" Omary aliuliza,

"Mnapoenda mtapata utatuzi wa tatizo lenu, ila kurudi salama ni kazi sana" Mzee Mkwiji aliwaambia na kufanya vijana waogope,

"Kwa hiyo tukienda uko shinyanga tunakufa?" Omary aliuliza kwa taharuki,

"Shinyanga hamtokufa, ila kazi isipofanikiwa shinyanga, basi mtakuwa na safari nyingine itakayoambatana na kifo" Mzee Mkwiji alizidi Kutoa taharifa mbaya kwa vijana,

"Kwa hiyo tusiende au?" Kayoza aliuliza,

"Usipoenda itakuwa umeridhika na Maisha ya kuua, cha muhimu ni uende, ila kuweni makini na maamuzi yenu uko muendako" Mzee Mkwiji aliongea huku akijinyanyua mkekani,

"Mbona umakini tunao tu babu" Kayoza alijibu wakati babu akiingia ndani,

"Pamoja na umakini wako, kifo chako kitakuwa cha kujiua mwenyewe" Babu aliongea kwa utani huku akipotelea ndani,

"Babu mzinguaji kweli, kaongea vya maana wee, ameona amalizie na utani" Kayoza aliongea huku akicheka,

"Ndivyo alivyo huyo, akiona maswali yanakuwa mengi uwa anayapotezea kwa utani" Omary aliongea huku wakikunja mkeka kwa lengo la kuingia ndani.

**********

Sajenti Minja alienda hospitali na kufanyiwa vipimo katika jeraha lake na hakukutwa na tatizo lolote,

"Daktari rudia kunipima, haiwezekani nikutwe sina kitu" Sajenti Minja aliongea na pia akishangaa majibu ya vipimo,

"Ridhika na majibu, au kama hutuamini nenda kajaribu kucheki kwenye hospitali nyingine, labda jibu linaweza kuwa tofauti" Daktari alimjibu kistaharabu Sajenti Minja,

"Sio kama nadharau huduma zenu, kinachotisha ni kiumbe kilichoniachia hizo alama, kiko kama zombi, nahisi na mimi naweza kubadilika na kuwa kama hicho kiumbe" Sajenti Minja aliongea kwa upole huku akishika eneo la jeraha lililokuwa na bandeji,

"Acha kuamini movie au masimulizi ya kizombi, zile uwa ni habari tu za kusadikika zisizo na ukweli wowote" Daktari alijibu huku akicheka,

"Hayajakukuta wewe na ndio maana unasema hivyo" Sajenti Minja aliongea huku akinyanyuka katika kiti,

"Usiondoke, bado hatujamaliza" Daktari alitoa kauli iliyomrudisha Minja kwenye kiti,

"Bado nini?" Sajenti Minja aliuliza,

"Kuna dawa unatakiwa ukanunue kwa ajili ya kukausha jeraha lako" Daktari aliongea huku akimpatia Sajenti Minja kikaratasi chenye maandishi yaliyoandikwa kwa mkono, Sajenti Minja akapokea na kuondoka.

***************

Baada ya Kayoza na Omary kumaliza mambo yao madogo madogo, ilipofika jioni Kayoza akachukua
simu ya Omari akampigia mama yake,
baada ya salamu,

"mama keshokutwa
nitakuja huko" Kayoza akamwambia
mama yake.

"chuo mmeshafunga?"
mama yake akauliza.

"Sio mda mrefu
sana toka tufunge, mama" kayoza akamjibu,

"uko wapi, au kwa shangazi yako?" mama yake akamuuliza.

"nipo Tanga kwa rafiki yangu" Kayoza
akajibu.

"Kuna nini uko Tanga, au matembezi tu?" Mama Kayoza aliuliza,

"Ni safari tu ya bahati mbaya mama" Kayoza alijibu,

"Kwanini iwe ya bahati mbaya?" Mama Kayoza akauliza kwa shahuku,

"Ngoja nije, tutaongea vizuri mama" Kayoza alimwambia mama yake,

"Lakini wema upo au?" Mama Kayoza alimuuliza mwanaye,

"Nikija tutaongea mama" Kayoza alijibu,

"Sasa si inabidi kwanza nijue kama kuna wema au lah?" Mama Kayoza alitilia mkazo msimamo wake,

"Wema upo" Kayoza alijibu ili kumridhisha mama yake, kwa maana anamjua jinsi alivyo na maswali mengi,

"haya, karibu mwanangu"
Mama yake akamwambia, kayoza akaitikia kisha akakata simu.

********

Hiyo siku ya Safari ilipofika ikabidi waondoke
pamoja na Omari kama walivyokubaliana. Mzee Mkwiji akawafanyia tambiko dogo kwa ajili ya usalama wao, kisha
wakaagana nae kwa ahadi ya kurudi
tena baada ya kutoka uko waendako.

Wakaenda mpaka mjini, wakaingia
kwenye mashine ya kutolea pesa (ATM), wakachukua
pesa ya kuwatosha wao, wakatafuta
mabasi ya Shinyanga wakapanda, safari ya kuelekea shinyanga ikaanza..

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO..

SEHEMU YA KUMI NA NNE.

________________
ILIPOISHIA..
________________

Hiyo siku ya Safari ilipofika ikabidi
waondoke
pamoja na Omari kama
walivyokubaliana.
Mzee Mkwiji
akawafanyia tambiko dogo kwa ajili
ya usalama wao, kisha
wakaagana nae kwa ahadi ya kurudi
tena baada ya kutoka uko waendako.

Wakaenda mpaka mjini, wakaingia
kwenye mashine ya kutolea pesa
(ATM), wakachukua
pesa ya kuwatosha wao, wakatafuta mabasi ya Shinyanga wakapanda, safari ya kuelekea shinyanga ikaanza..

____________
ENDELEA..
_____________
...Muda wote safarini Omari
aliutumia kujificha na gazeti ambalo
alikuwa analisoma, na hata
aliposinzia, alilitumia gazeti hilo
kujifunika nalo usoni.

Shinyanga
mjini waliingia saa tano usiku,
walipokelewa na mama yake Kayoza,
ila aliwashangaa kwa jinsi
walivyokuwa na majeraha,
"vipi jamani, mbona mna mavidonda hivyo
usoni" mama yake Kayoza akauliza.

"tulipata ajali mama" Kayoza akajibu
kwa kudeka.

"na hii gari, au?" mama
Kayoza akaongeza swali lingine huku kidole chake akikielekeza katika basi walilokuja nalo wakina Kayoza.

"sio hili mama, wakati tunaenda Tanga
ndio tulipata ajali" Kayoza akajibu.

"aah, haya twendeni wanangu"
mama kayoza akaridhika na majibu
ya mwanae.

Wakabeba mizigo yao,
wakaenda kwa dada yake mama
Kayoza kwa kuwa nyumbani kwa mama Kayoza kulikuwa nje ya mji, iliwabidi walale hapo mpaka siku inayofuata ndio waende kwa Mama Kayoza.

**********

Sajenti Minja alishaanza kuiogopa ile kesi, maana tayari alishaona ile kesi ina mambo kama ya kishirikina na ukingatia si polisi wala serikali inayoamini kitu hicho, na swali alilojiuliza ni kwamba, akisema ahache kaifuatilia hiyo kesi, je kwenye ripoti yake ataandika sababu gani iloyopelekea kuacha hiyo kesi?

Kipindi anawaza hayo yote, alikuwa ndani ya gari akirejea ofisini kwao ili akamshawishi tena mkuu wake ili aone kama atamuelewa katika jambo hilo la kuacha kwake kazi.

Alifika na kumkuta mkuu wake akitoka,

"Nina maongezi na wewe mkuu" Sajenti Minja aliongea kikakamavu huku amepiga saluti,

"Ingia kwenye gari twende" Mkuu wake alijibu na Sajenti Minja hakutaka kuuliza wanaenda wapi, cha muhimu alichokiona ni kuongea na mkuu wake tu.

"Nini tatizo?" Mkuu wake alimuuliza wakati akiiondoa gari,

"Kama nilivyokwambia hawali, naomba hii kesi muiamishie kwa mtu mwingine" Sajenti Minja aliongea,

"Sababu ni ipi?" Mkuu wake aliuliza,

"Sababu ni ile ile, nahisi yule sio kiumbe wa kawaida" Sajenti Minja alijibu,

"Je nikikuambia uniletee barua ya kutaka kuacha hii kesi utaandika sababu ni ipi?" Mkuu wake alimuuliza,

"Hicho ndicho kinachonitatiza" Sajenti Minja alijibu,

"Basi nenda katafute jibu, na ukilipata uje na barua yenye maombi yako" Mkuu wake alimwambia wakati akiliegesha gari nje ya mgahawa,

"Dah, mbona ni mtihani" Sajenti Minja aliongea,

"Huo sio mtihani, mtihani ni kushindwa kujielewa wewe kama askari una jukumu gani katika taifa?" Mkuu aliongea huku akiwa ndani ya gari,

"Unamaanisha nini?" Sajenti Minja aliuliza,

"Kama unashindwa kuelewa hata nilichomaanisha, basi napata wasiwasi kuhusu hata uwanajeshi wako" Mkuu aliongea huku akitelemka katika gari, Sajenti Minja nae akafuata huku akihisi kudharauliwa kwa ile kauli ya mkuu wa Polisi,

"Lakini mkuu hiyo kauli inahusiana vipi na maongezi yetu?" Sajenti Minja aliuliza kwa upole,

"Nadhani haihusiani, kwa maana uwanajeshi na akili ni vitu tofauti" Mkuu alijibu kwa kejeli huku akikaa juu ya kiti, na Sajenti Minja nae akakaa,

"Tuachane na hayo mkuu, naomba tu unisaidie kunivua ile kesi" Sajenti Minja aliamua kupuuza kauli za mkuu,

"Numeshakwambia nenda kaandike barua na ulete ofisini kwangu, ila iwe na sababu tofauti na hiyo" Mkuu aliongea kisha akaagiza chakula,

"Na wewe kaka nikuletee chakula gani?" Mhudumu wa mgahawa alimuuliza Sajenti Minja aliyekuwa na mawazo,

"Naomba wali, wali nyama. Atalipa bosi hapa" Sajenti Minja aliongea huku akimaanisha kuwa atakayemlipia chakula ni mkuu wa polisi,

"Mimi na wewe biashara imekwisha, nyanyuka uondoke" Mkuu aliongea kwa amri na kwa kuwa uaskari ni utiifu, Sajenti Minja aliinuka kwa unyonge na kutoka zake nje ya mgahawa.

*************

kesho yake hasubui
wakapanda gari ambayo iliwapeleka
katika kijiji anachokaa Mama yake
kayoza, iliwachukua mwendo wa nusu saa na daladala kufika mpaka eneo ambalo alikuwa anaishi Mama Kayoza, wakatelemka na kisha wakatembea mwendo wa dakika kumi mpaka kuifikia nyumba ya mama Kayoza.

"karibuni, hapa ndio
nyumbani" Mama Kayoza aliongea huku akifungua mlango,

"asante mama" wakajibu
kwa pamoja.

Wakavua viatu, kisha
wakapita ndani,

"ehe, za chuo
mwanangu" Mama Kayoza alimuuliza mwanae baada ya kukaa,

"Za uko ni nzuri, sijui za hapa" Kayoza akajibu,

" na huyu ni nani?",
Mama kayoza akamuuliza mwanae
huku akimwangalia Omari.

"huyu ni ndugu yangu mama" Kayoza akajibu
kwa kifupi.

"ndugu yako?, mtoto wa
shangazi zako au?" Mama kayoza
akauliza tena.

"ni rafiki yangu, ila
kwa matatizo yalinitokea, alisimama kama ndugu yangu" Kayoza akamjibu
mama yake.

"Matatizo? matatizo gani
yaliyokukuta uko dodoma?" Mama
kayoza akamtupia swali jingine
mwanae.

"ni makubwa mama, na
huyu mwenzangu hadi polisi aliwekwa kwa ajili yangu" Kayoza
akamrejeshea jibu mama yake, huku
akijilaza juu ya kochi la sofa ambalo
awali alikuwa kalikalia.

"sasa si ungenitaharifu nimwambie mjomba
ako yuko pale ni polisi pia" Mama
kayoza akaongea huku sura yake
ikiwa na huzuni.

"mama bwana, sasa
we si ungenitaharifu kwanza kwamba
una ndugu dodoma" Kayoza alisema
maneno hayo kwa kudeka mbele ya mama yake.

"mimi nina mambo
mengi mwanangu" Mama kayoza akajitetea.

"ulisema ni polisi eeh?,
anaitwa nani?" kayoza akamuuliza
mama yake.

"ndio ni polisi, tena ana
cheo cheo, anaitwa Joel Minja, ila wenzake wamezoea kumuita sajenti Minja" Mama kayoza akajibu.

"mh, Sajenti Minja!!!!?" Omari akajikuta
anauliza bila kutarajia...

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
Back
Top Bottom