Riwaya: Mfalme Anataka Kuniua

Mkuu nimekuelewa kwa uzuri sana fanya Yale yapo ndani ya uwezo wako!! Ahsante kwa burudani mungu akulipe zaidi
 
Mfalme Anataka Kuniua

Sehemu ya 13


Habari ya kuuawa kwa mbwa wa polisi katika Pango la Kifo zilitapakaa nchi nzima ya Kanakantale. Kama ilivyo desturi, ilitakiwa kutolewa sadaka ya kuteketezwa mnyama pembezoni mwa pango ili kuyatuliza mashetani hayo yasilete balaa zaidi.

Ilikuwa asubuhi jua likichomoza taratibu. Ndege walipokezana kuimba kwa umaridadi waliojaaliwa. Mbele ya mlango wa kuingilia Pango la Kifo, alisimama mfalme wa Kanakantale aliyefuatiwa na wananchi wengi wa Kanakantale waliojaaliwa kufika siku hiyo. Mfalme aliongoza ibada ya kutoa sadaka ya ng’ombe aliyenona ili kuyatuliza mashetani yale yasilete mabalaa katika nchi yao.

“Enyi mashetani muishio katika Pango la Kifo, tafadhali tunaomba msituletee mabalaa, hatutaki ungomvi nanyi, askari wetu wakiwa katika msako wa mtu mhalifu, walishindwa kumdhibiti mbwa mmoja ambaye aliingia ndani ya pango na kuwasababishia usumbufu. Chukueni sadaka ya ng’ombe huyu kama ishara ya uwepo wa amani baina yetu na nyinyi. Ishini katika pango, hatutawaingilia, nasi tunaishi nje ya pango, tunaomba msituingilie,” alisema mfalme kwa sauti kubwa iliyokwenda moja kwa moja mpaka pangoni.

Ng’ombe alichomwa akawiva vizuri, chini wakaweka kiroba cha chumvi. Baada ya kumaliza, mfalme alisema na watu wake kuashiria kuwa kazi ile ilikwisha, nao wakaanza kuondoka kuelekea katika majumba yao.

Wakati haya yote yanatokea, Mako aliyaona akiwa ndani ya Pango. Alimtazama ng’ombe mnono aliyechomwa, akaachia tabasamu jembamba.

Kigiza kilianza kuingia kuashiria mwanzo wa usiku. Mako alitoka katika pango, akakokota nyama ya ng’ombe na kuiingiza pangoni. Baada ya muda alionekana akitoka tena na kuchukua kiroba cha chumvi. Kilitanda kimya kifupi, lakini akatoka tena, safari hii akiwa ameshika karatasi ambayo aliifunga katika mti mfupi uliokuwa karibu na lango. Aliporejea ndani, kikaratasi kilibaki kikipepea kama bendera.

Mako hakulala, usiku kucha alifanya kazi ya kuitengeneza ile nyama, aliitengeneza kwa urefu kama mkanda kisha akaipaka chumvi ili isiharibike. Aliitengeneza kwa wingi akaiweka mahali pakavu pa juu. Hakufahamu angeishi pangoni kwa muda gani, lakini aliamini nyama ile ingemsaidia kupata kitoweo kwa muda mrefu. Alifurahi zaidi alipotazama mbele, aligundua uwepo wa kisima cha maji safi, hata hivyo, hakuelewa ni kwa namna gani kisima kilichimbwa katika pango lile gumu. Mbali na kisima, kingine kilichomstaajabisha ni taa zilizokuwa pangoni mule. Kila baada ya hatua kumi na tano, palikuwa na taa katika ukuta, pembezoni mwa kila taa paliwekwa kiberiti, aliziwasha taa hizo kwa wingi wake kadri alivyoweza na hakuwa na mpango wa kuzizima.

Asubuhi walionekana askari weusi warefu wakielekea Pango la Kifo. Walitembea kwa mwendo wa kunyakua, japo ilikuwa asubuhi, miili yao ilitapakaa jasho. Hawa walitumwa kwenda kukagua kama mashetani yalikubali sadaka.

Walitoa ukelele wa furaha baada ya kukuta ng’ombe hayupo. Waliruka wakishangilia mpaka macho yao yalipotua katika karatasi nyeupe iliyopepea kama bendera. Walisogea kusoma ujumbe ulioandikwa.

“SADAKA IMEKUBALIWA, NYUMBA ILIYOCHOMWA MOTO NA ASKARI IJENGWE.”

Askari walirudi wenye nyuso za furaha na ule ujumbe walioukuta. Taarifa zilipokelewa kwa furaha na wana Kanakantale nayo nyumba ya Oma ilijengwa tena. Basi watu wote wakawa wenye furaha isipokuwa familia ya Bwana Mako.
 
Hahahaaa mako bhana eti SADAKA IMEPOKELEWA NYUMBA ILIYOCHOMWA NA ASKARI IJENGWE mbona shetani hajasema mtu mnaemuwinda sio muhalifu? Shukrani Sana mkuu
 
Kumbe mashetni yanajua kuandika hahahah! Story tamu sana hii. Mako ni kichwa
 
Asanteeee
 
Mfalme Anataka Kuniua

Sehemu ya 15


Mako aliamua kulichunguza pango lote. Kila alipozidi kusonga mbele giza lilitanda hivyo alizidi kuziwasha zile taa zilizosimama juu ya kuta. Alitembea mwendo wa kilomita nne, akakutana na njia mbili. Akapiga hesabu na kuamua kuifuata iliyoelekea kushoto, ile ya kulia angeichunguza siku nyingine.

Aliendelea kutembea kama umbali wa kilomita tatu hivi, urefu wa pango ukazidi kupungua hata akawa akinyoosha mkono wake, anagusa juu na hapo ndipo akauona mwisho wa njia ile na ndiyo ulikuwa mwisho wa pango. Alisogea akaushika ukuta mgumu wa jiwe akistaajabu. Alipotazama juu ya ukingo wa mwisho, aliona pedali ndogo iliyotosha kushikwa kwa mkono. Aliikamata pedali ile, akaizungusha taratibu, upande wa juu wa pango ukaanza kufunguka na kumfanya Mako awe kama anayefungua mlango wa handaki. Aliendelea kuzungusha pedali mpaka upande wa juu ukafunguka katika duara iliyolingana na mdomo wa pipa.

Akitumia mikono, alijivuta nje. Akawa nusunusu, kichwa na kifua viko nje, tumbo na miguu vimo pangoni. Macho yake madogo yakawaona wafungwa wa gereza la Kanakantale wakioga kwa furaha. Haraka akarudi pangoni na kunyonga ile pedali, mlango wa juu ukajifunga.

Sasa alibaini kuwa, mwisho wa pango lile kwa kufuata njia ya kushoto ulikuwa mlango wa kuingia gereza la Kanakantale! Alijipumzisha kidogo kisha akarudi katika sehemu yake, kule alikoweka mikanda ya nyama, kule ambako aliweza kuchungulia na kuwaona askari wakirandaranda kumtafuta.

Siku iliyofuata aliamua kuichunguza njia iliyoelekea kulia. Aliifuata kwa mwendo wa kilomita nne, ukawa mwisho wa pango katika mazingira yanayofanana na ule mwisho wa njia ya kushoto. Kama kawaida, huko nako kulikuwa na pedali ndogo iliyotosha kuenea mkononi, aliizungusha, pango likafunguka upande wa juu. Alichungulia, akauona uwanja mkubwa katika ikulu ya Kanakantale, ni katika uwanja huu, mfalme hufanya mikutano na askari wake.

Akiendelea kutazama mpaka macho yake madogo yalipogongana na macho makubwa ya askari. Haraka kama sisimizi, akarudisha kichwa pangoni na kuanza kuzungusha ile pedali. Askari aliyeshtuka, alisogea sehemu ile, kadri alivyozidi kusogea, aliona ardhi ikijifunga na mwisho hapakuwa na yule mtu aliyechungulia wala shimo. Askari mtiifu alikaa mahali pale mwenye mawazo. Alitafakari kama alichokiona kilikuwa kweli au uongo. Mwisho aliamua kuamini kuwa, zilikuwa ndoto za mchana. Hakuondoka mahali pale, aliendelea kuzungukazunguka kwa muda mrefu mpaka alipojiridhisha hakukuwa na kitu.

Mako alizama pangoni mwenye hofu juu ya kuonekana kwake. Alihofia nini kingetokea kama wangeamua kuchimba, mwisho aliamua kuendelea na shughuli zake. Mwenye hofu, lakini anayejiamini.

Basi alibaini kuwa, ile njia ya kushoto inaelekea gerezani, na ile ya kulia inaelekea kwa mfalme.

***​

Kivuli cheusi kilionekana kikitoka katika shimo usiku wa manane. Kivuli hicho kilitambaa kama nyoka mpaka kandokando ya ukuta, kisha kwa mwendo wa kuficha umbo, kilijisogeza taratibu kikiwapita walinzi ambao hata hivyo walisinzia.

“Sipe… Sipe… Sipe…” kivuli kiliita kwa kunong’ona. Sipe mwenye hofu, alilala peke yake katika chumba kile cha jela, wenzake Sasi na Athu, walinyongwa siku tatu zilizopita.

“Nani wewe?” alihoji Sipe akiwa katikati ya usingizi na kuamka.

“Mimi Mako, sogea tuzungumze.”

“Mako…!” alijibu Sipe akisogea karibu, “Kulikoni ndugu yangu, ni ndoto au kweli?”

“Usiwe na hofu, utafahamu mengi ukiwa na subira. Pokea ujumbe wangu, kesho wakati wa kuoga, kaa pembeni upande wa kulia bila kukaribiana sana na watu, utasikia sauti ikikuita mara tatu, ukisikia hivyo, tazama upande wa kulia, utaniona nachungulia kichwa na mwili mwingine ukiwa shimoni, haraka sogea na ingia katika shimo.”

Baada ya kumaliza mazungumzo, Mako alitambaa kuelekea alikotoka, aliufikia mdomo wa shimo na kuingia ndani kama mchwa. Kisha akanyonga pedali kuifunga himaya yake.

Mwisho wa Sehemu ya Bure ya Riwaya Hii, Endapo unahitaji kununua riwaya yote Gusa Hapa.
 
Wish ziwe zinakuja 10
 


Najaribu sana kutafakari setting ya hii hadithi,

mazingira yake ni ya kizamani enzi za utawala wa kifalme au ya kisasa enzi hizi za bitcoin?

[emoji848]
 
Leo fupiiiiiii hila saaafi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…