RIWAYA: Mume Gaidi

RIWAYA: Mume Gaidi

SEHEMU YA 39

Walipogeukiana na kuonana ana kwa ana, kila mmoja alikuwa na ghadhabu na mwenzie.
Patrick akaanza kurudi akimfata Maiko akiwa amejiaminisha kabisa, Maiko akajua hapo si mahala pema kwani aliweza kuiona vizuri hasira ya Patrick.
Ndipo Maiko alipoanza kukimbia, ila hakufika mbali akawa amepigwa mtama na Patrick, Maiko akaanguka chini.
Patrick akamnyanyua Maiko kwa nyuma na kumgeuza huku akimpiga ngumi usoni, Maiko akaona kuwa ataonekana mzembe asipo pambana na Patrick, alichofanya ni kumpiga teke Patrick. Hasira ikamzidi Patrick, akainuka na kumrukia Maiko akampiga teke ambalo Maiko alikwepa, nae akarusha ngumi ambayo Patrick aliikwepa.
Pambano likaanza sasa, walipigana sana na kuumizana ila Maiko ndiye aliyeumia zaidi, alikuwa chini na Patrick juu huku akishambuliwa kwa ngumi, akabahatika kumpiga Patrick teke sehemu za siri, hapo ndipo akapata upenyo wa kukimbilia gari lake na kuondoka.
Patrick alionekana kuwa na hasira sana hadi mishipa ya sura ilimsimama.
Mashaka akaingia kwenye kile chumba alichowekwa Tina, akamkuta Tina akiwa amelala.
Akamfata karibu na kuanza kumpapasa, Tina akashtuka na kuanza kuogopa huku akitoa mikono ya Mashaka ila hakuacha, aliendelea kumpapasa papasa Tina.
Akataka kumuingilia, Tina akawa anakataa na purukushani kati yao zikafatia, ikawa kama mtafutano wa jogoo na kuku jike.
Mashaka akaona asisumbuliwe sana na huyu binti, akaamua kutumia nguvu sasa. Naye akampiga na kumbaka.
Alipomaliza akamuangalia Tina na kumwambia "asante kwa huduma ingawa nimetumia nguvu kuipata" halafu akatoka nje.
Tina akalia sana, akajiuliza maswali mengi "yani ofa ya bia mbili ndio nafanyiwa hivi! Jamani mimi! Maskini Tina mie. Mungu nisaidie nitoke humu."
Tina akawa analia tu bila msaada wowote.
Maiko aliondoka moja kwa moja hadi kwa wenzie walipo.
Mashaka akamshangaa Maiko kuwa na damu na alama za kupigwa mwilini.
MASHAKA: Vipi tena Maiko?
MAIKO: Hivi tumekuja huku Mwanza kumtafuta Patrick au Patrick kututafuta sisi?
MASHAKA: Kivipi Maiko?
MAIKO: Nimekutana na Patrick na ndiye aliyenifanya hivi, alikuwa na hasira sana hata nashangaa kwanini amekuwa vile.
MASHAKA: Dah! Yani Patrick ndo kakufanya hivi!! Hako ka Patrick nikikapata nakanyonga kabisa, yani yeye ndo mwenye makosa halafu anatuletea hasira sisi!
MAIKO: Umeona hapo! Hata mi namshangaa, angekuwa mwingine angekimbia kuniona eti yeye ndo akanikimbilia na kuanza kupigana nami.
MASHAKA: Madai yake imemuuma sana hiyo ya Tusa, ngoja sasa tutamchinja huyo Tusa mbele ya macho yake. Nimechukizwa sana kwakweli.
Maiko alishindwa kumuelewa kabisa Patrick kuwa ana matatizo gani hadi kumvamia yeye kiasi kile.
Deborah bado aliendelea kumtafakari Patrick.
DEBORAH: Nashindwa kumuelewa mwenzenu, kaondoka kimya kimya hadi leo hajarudi.
PAMELA: Ninachowaza mimi ni kuwa, kama Adamu amefika Mwanza basi itakuwa tabu kwamaana hanipati kwenye ile simu yako.
DEBORAH: Haya majanga mbona mmh! Sijui hata tufanyaje! Au labda niende mjini kununua line.
PAMELA: Nadhani hilo litakuwa jambo la busara sana.
DEBORAH: Basi hakuna tatizo nitaenda hata leo au kesho.
Deborah akajipanga kwenda kununua namba nyingine ili aweze kuwasiliana.
Patrick akaenda alipomuacha Yuda.
PATRICK: Nimekutana na Maiko leo, bora hukuwa pamoja nami.
YUDA: Bora tena!! Wakati ndio tungesaidiana kulipa kisasi!
PATRICK: Sitaki ajue mapema hivi kama tunafahamiana, kwasasa wewe unatakiwa ufanye kazi moja.
YUDA: Kazi gani hiyo?
PATRICK: Uwasiliane na wakina Maiko ili ujue walipo, halafu uwafuate. Hapo ndio tutacheza mchezo mzuri bila ya wao kujua. Si wamejileta wenyewe kwenye mji wetu bhana.
YUDA: Na je vipi haturudi nyumbani?
PATRICK: Hakuna kurudi hadi tukamilishe hili swala kwanza.
Yuda akaanza kutambua jinsi gani Patrick anawajua wakina Maiko na kundi lake.
Mashaka akapanga mkakati na Maiko.
MASHAKA: Hakuna kubweteka Maiko, hapa tumtafute Tusa kwa gharama yoyote ile kwanza tutafaidika na pili tutamkomesha Patrick.
MAIKO: Kwahiyo tuanze na msako wa Tusa kwanza?
MASHAKA: Ndio, tuanze na Tusa.
MAIKO: Vipi kale karembo ndani kapo!
MASHAKA: Kapo ndio, kale ndio katakuwa kutuburudisha baada ya kazi.
MAIKO: Yani na wewe unakatumia!
MASHAKA: Ndio kwani kuna ubaya gani?
MAIKO: Tafuta wako bhana, hapa Mwanza wamejaa kibao. Yule mrembo niachie mimi. Tafadhari sana sitaki tuingiliane kwa warembo, nawe tafuta wako bhana.
MASHAKA: Tujadili ya maana hapa, tukianza kujadili kuhusu hao wanawake tunaweza kugombana bure mwanangu. Hebu achana nao kwanza tuwaze ya muhimu hapa.
MAIKO: Hata na yao ni muhimu, sawa bhana. Tujadili sasa namna ya kumpata Tusa.
Wakaanza kupanga mipango ya kuweza kumpata Tusa.
Adamu alishakata tamaa kabisa.
ADAMU: Hivi tutakaa hapa Mwanza hadi lini jamani?
FAUSTA: Hata sielewi, Tina ametuletea mambo jamani.
ADAMU: Yani huyo Tina angekuwepo tungesharudi Dar. Ametuchanganya kweli huyo Tina.
FAUSTA: Mdogo wangu Pamela nae ni magumashi tu, tangu tuingie Mwanza kile kinamba chake hakipatikani wala namba aliyokupigia haipatikani hata sijui anafikiria nini.
ADAMU: Kwakweli wananichanganya sana hawa watu, alianza Tusa, akaja mama yake na sasa ni Tina. Wote namba zao hazipatikani tunabaki kukadilia tu kuwa ni wazima, ila haya ni mateso kwakweli.
FAUSTA: Sasa kaka itakuwaje?
ADAMU: Kama hadi kesho mambo hayaeleweki basi turudi tu Dar tukatafute njia ya kuwapata. Hapa Mwanza hatuna makazi wala nini, kwa kifupi hapatufai, asije akapotea na mwingine bure.
Adamu akatoka tena kwenda kujaribu kuwatafuta hawa watu wa tatu kama atapata taarifa zao zozote.
Adamu akiwa mjini anashangaa kumuona mtu ambaye hakumtarajia kabisa.
 
SEHEMU YA 40

Adamu akiwa mjini anashangaa kumuona mtu ambaye hakumtarajia kabisa.
Akajaribu kumtazama vizuri, akaona ni yeye na wala hata hajamfananisha. Akaona ni vyema kujificha kwani hakupanga kukutana na mtu huyo kwa muda huo.
Alikuwa ni Deborah akikazana kununua laini ya simu na kuijaribisha kwa kuiweka hewani, Adamu alijificha kabisa hadi pale Deborah alipoondoka eneo lile.
Adamu akaona hajielewi kwasasa, akaamua kurudi alipowaacha wakina Fausta.
Deborah akarudi nyumbani kwake na kumuita Pamela.
DEBORAH: Nishanunua line na nimeshaweka na vocha, unaweza kumpigia sasa huyo mumeo.
PAMELA: Kwakweli Deborah unanifanyia mambo mengi sana hadi naona aibu kwakweli.
DEBORAH: Huna sababu ya kuona aibu sasa Pamela, kama aibu ungeona kipindi kile wakati mimi nakulalamikia kuwa nahisi naibiwa mume na mwizi mwenyewe ukiwa makini kunisikiliza huku ukionyesha kusikitishwa na kilio changu.
PAMELA: Nisamehe Deborah, ilikuwa akili ya kitoto ikinisumbua.
DEBORAH: Akili ya kitoto!! Sawa sawa Pamela, ila mimi ndio nilikuwa na akili ya kikubwa na kukueleza matatizo yangu wewe mtoto Pamela.
PAMELA: Sina maana hiyo Deborah, ila mapenzi ni kama shetani anavyompitia binadamu maana unajikuta unafanya kitu ambacho hukukitarajia.
DEBORAH: Mapenzi eeh!! Mapenzi ya kupendana na mume wa mtu! Tena ni mume wa rafiki yako wa damu!! Ama kweli ni mapenzi, nadhani wewe ni mke sahihi kwa Jumanne na pia hamtojutia kamwe kitendo cha kuichanganya akili yangu. Nakubali nilifanya tukio la kusikitisha yote sababu ya mapenzi, mapenzi kwa mume na mtoto wangu. Sawa, yaliyopita si ndwele tugange yajayo mpigie mumeo ili ajue mlipo, ajue kuwa mwanamke yule mwenye roho mbaya ndiye aliyewapokea, nataka anione hapa kwa macho yake kuwa sikufa sababu nina ushuhuda mkubwa wa kuishuhudia dunia.
PAMELA: Maneno makali sana hayo Deborah mmh!!
Akachukua simu na kuanza kupiga akashangaa kuona haipatikani kumbe alikosea namba moja.
Patrick aliendelea kupanga mipango yake na Yuda.
Kama alivyopanga nae Yuda, ikabidi ampigie simu Maiko ili ajue walipo na aweze kwenda.
Yuda akafanikiwa kuongea na Maiko, halafu Maiko akamuelekeza Yuda mahali walipo huku akifurahi kuongezeka kwa jeshi lao hapo Mwanza.
YUDA: Kila kitu safi kabisa kaka, ndio nataka nianze safari ya kuwafata.
PATRICK: Ukifika huko usiwaeleze kabisa kama unanifahamu, jifanye hujui chochote. Nataka maelezo yote wakupe wao, sawa!
YUDA: Hakuna tatizo kaka, we niaminie tu. Mi nitahakikisha mambo yao yote yanakuwa wazi.
PATRICK: Wewe nenda huko halafu na mimi niandae mambo mengine hapa.
Yuda akaianza safari ya kwenda kwenye himaya ya kina Maiko.
Adamu alirudi pale hotelini akiwa na mawazo sana.
ADAMU: Huwezi amini Fausta, nimemuona Deborah akiwa mjini leo.
FAUSTA: Deborah!! Sasa ikawaje?
ADAMU: Nikajificha, sikuwa tayari kuzungumza nae kwakweli.
FAUSTA: kwanini? Au bado unamuogopa kwa alivyomtenda Vero?
ADAMU: Hapana si hivyo ila sidhani kama Deborah anaweza kuongea vizuri na mimi.
FAUSTA: Ila kumbuka alikuwa mkeo yule Adamu!
REHEMA: Na bora angebaki na huyo, si kwamba simtaki Pamela hapana ila wewe hukustahili kuishi na Pamela kama mke na mume, nyie ni kama ndugu na unaweza hata kujitafutia laana bure.
ADAMU: Lakini mama, mimi na Pamela si ndugu kivile, yeye ana wazazi wake na mimi nina wangu.
REHEMA: Ni vigumu kunielewa Adamu, ila kwa maelezo niliyopewa ni kwamba mzee Ayubu alimchukulia Pamela kama mwanae pia, halafu wewe ndo umemfanya mkeo mmh! Ila hata hivyo maji yakimwagika hayazoleki, vilevile sijaona sababu ya wewe kumkimbia huyo mkeo wa kwanza.
ADAMU: Mama, sikujiandaa kukutana nae. Yule ni mshtakiwa anaetembea huru halafu pia namuonea aibu mama yangu, jaribu kunielewa.
FAUSTA: Ila kesi yake si ilishaisha?
ADAMU: Ni kweli iliisha, muda mrefu sana umepita. Kipindi hicho alikuwa binti mdogo sana, ila sasa ni mmama kabisaa.
FAUSTA: Miaka inakwenda na watu hubadilika Adamu.
Mara simu ya Adamu ikaanza kuita, alikuwa ni Pamela baada ya kupatia namba ya simu sasa.
Adamu alifurahi sana kuongea na Pamela, halafu Pamela akawaelekeza mahali pa kwenda.
ADAMU: Mmh! Afadhari maana nishauchoka mji huu.
FAUSTA: Na mwanangu je itakuwaje?
ADAMU: Twendeni tukaonane kwanza na hawa watu wawili halafu ndio tuanze na harakati za kumtafuta Tina.
FAUSTA: Mmh! Mwanangu, sijui amekumbwa na janga gani jamani.
Sele alikuwa na mawazo mengi sana juu ya Tusa, akaamua tena kwenda kwa mamake mdogo.
SELE: Mamdogo, unajua Tusa anakuficha mambo ya Patrick, mwambie akwambie ukweli kuwa Patrick ni nani.
DEBORAH: Ukweli gani tena jamani? Eti Tusa, hebu niambie.
TUSA: Mmh! Sele! Hakuna ukweli wowote mama, mi sijui chochote.
SELE: Acha uongo Tusa, mwambie ukweli mamdogo. Mwambie kazi anayofanya Patrick.
DEBORAH: Mbona mnanichanganya sasa! Mnaniweka njia panda mjue! Eti Tusa!
TUSA: Hapana mama, mi sijui kazi ya Patrick.
DEBORAH: Utashindwa vipi kujua kazi anayofanya mumeo Tusa? Patrick ni mume wako na umeishi nae sana huko Arusha, kwanini usijue kazi yake.
TUSA: Kweli mama, sijui chochote.
SELE: Tusa sema ukweli, sema ukweli kama Patrick ni jambazi.
DEBORAH: Patrick ni nani?
SELE: Patrick ni jambazi mamdogo.
DEBORAH: Mungu wangu! Yani Patrick ni.... Hapana, hapana haiwezekani kabisa. Mwanangu Patrick hawezi kuwa jambazi.
Deborah akainuka pale na kwenda chumbani, hawakuelewa ameenda kufanya nini.
TUSA: Umeona Sele, unasababisha makubwa bure.
SELE: Tatizo ni wewe Tusa hupendi kuongea ukweli. Unaposema ukweli unakuwa huru, na ukweli huo utakuponya toka mikononi mwa Patrick.
TUSA: Sasa hapa umeponya au umeongeza tatizo Sele?
Wakawa wanatupiana mpira wa lawama tu. Sele alifanya hayo ili kumponya Tusa toka mikono ya Patrick.
Yuda aliingia kwenye himaya ya wakina Maiko, alimkuta Mashaka na kuzungumza nae mawili matatu, halafu akamuulizia Maiko alipo.
Mashaka akamuelekeza Yuda ambaye alienda moja kwa moja karibia na kichumba alichoelekezwa.
Akawaona vijana wawili wakiwa nje, alipokaribia alisikia sauti ya mwanamke ikilia toka kwenye chumba alichoambiwa kuwa Maiko yupo ndani.
Alipoisiliza kwa makini sauti hiyo akajikuta akipatwa na jazba kubwa sana na kuanza kwenda kwa kasi kwenye kile chumba.
 
SEHEMU YA 41

Alipoisikiliza kwa makini sauti hiyo, akajikuta akipatwa na jazba kubwa sana na kuanza kwenda kwa kasi kwenye kile chumba. Simu yake ya mikononi ikawa inaita ndani ya mfuko wa suruali, akaipokea na kuirudisha tena mfukoni kwani kadri alivyozidi kusogea ndivyo ile sauti ilivyozidi kupasua mawazo yake, akapatwa na hasira zaidi.
Alipofika mlangoni akataka kuingia wale vijana wakamzuia, akawasukuma pembeni na kuwafanya waanguke kwani alitumia nguvu nyingi kufanya hivyo, halafu akasukuma mlango kwa nguvu, akamkuta Maiko juu ya kifua cha Tina. Kwa gadhabu aliyokuwa nayo Yuda, akainama na kumnyanyua Maiko aliyekuwa kwenye ulimwengu mwingine uliyomfanya asijari zile kelele zilizopigwa na Tina.
Yuda alimnyanyua Maiko juu juu, na kumpiga ngumi moja ya haja iliyomfanya aanguke chini, halafu Yuda akainama chini na kumnyanyua yule binti.
Alipomtazama vizuri akashtuka na kumwambia "Tina!!"
Tina alikuwa analia tu.
Kabla Yuda hajafanya kitu kingine, wale vijana wawili aliowatupia pembeni nao wakaja mule ndani na kumkamata Yuda kwa nyuma.
Yuda alikukuruka na kuanza kupambana na wale vijana, wakaja na wengine wawili na kuweza kumdhibiti Yuda.
Tina nae akaona ule ndo upenyo wake kutoroka, wakati anakimbia akadakwa na Mashaka.
MASHAKA: Huna pa kwenda binti, hapa ndio umefika.
Tina akahisi kizunguzungu na kuanguka.
Pamela alienda kuwapokea wakina Adamu na kuweza kwenda nao kwa Deborah.
Adamu alifurahi sana kumuona mkewe, ila Pamela alishangaa kumuona dada yake na mkwewe nao wakiwa mahali hapo, akawasalimia na kuwakumbatia.
REHEMA: Usishangae Pamela, hata sisi tuna uchungu na wewe.
PAMELA: Yani mmenifanyia surprise kwakweli, sikutarajia kabisa.
FAUSTA: Tusa je yuko wapi?
PAMELA: Nimemuacha tulipofikia, nimeamua kumfanyia surpise na yeye hata hajui kama baba yake anakuja leo, mmh atafurahije.
REHEMA: Atafurahi na kuniona bibi yake ambaye hajawahi kuniona?
PAMELA: Atafurahi sana mama, unajua Tusa hakujui kabisa na kila siku anatamani kumjua bibi yake, nadhani leo itakuwa ni siku ya furaha kwake.
FAUSTA: Kama ulivyofurahi wewe kumuona mumeo.
PAMELA: Aaaah dada, mi nimewafurahia wote jamani.
Wote wakawa wanacheka na kufurahi, huku safari ikiendelea bila ya Pamela kuwaambia kuwa wanaenda kwa Deborah.
Deborah hakutoka ndani, alikuwa amejifungia tu hofu ikawatanda Sele na Tusa.
SELE: Tutafanyaje sasa?
TUSA: Ngoja nikamuangalie tena.
Tusa akaenda tena mlangoni kwa Deborah ila Deborah hakufungua mlango, akaenda dirishani kumchungulia ila hakuweza kumuona kumbe Deborah alikuwa amelala chini pembezoni mwa kitanda akilia kwa uchungu.
Tusa akarudi tena alipo Sele.
TUSA: Hali ni mbaya, hata haonekani humo chumbani.
SELE: Tusa, tuondoke hapa.
TUSA: Tuondoke! Twende wapi? Na hapa tutamuacha na nani?
SELE: Hali ni mbaya hapa Tusa, hivi unamjua Patrick vizuri? Akirudi hapa na kumkuta mama yake yupo hivyo eti sababu ni sisi, hali itakuwa mbaya ukizingatia hata hatujui alipo huyo Patrick.
TUSA: Sasa tutamuacha na nani huyo mama humo ndani? Maana hata mama yangu nae hayupo, ametoka.
SELE: Sikia Tusa, twende kwanza nyumbani kwetu nikamshtue mama yangu aje hapa au kwa mamdogo Anna nadhani kidogo atawaelewa hao, halafu na sie tutokomee huko huko.
TUSA: Na mama yangu je?
SELE: Atatukutia Dar, nataka nikakukabidhi kwa baba yako Tusa. Utakaa utumwani hivi hadi lini? Unatakiwa kuwa huru Tusa.
TUSA: Sawa, au hata atanikuta Morogoro kwa babu. Najua kule Patrick hawezi kufika.
Tusa na Sele wakaondoka mahali hapo.
Patrick ndiye aliyempigia simu Yuda muda ule wakati Yuda anaenda kwenye kile chumba, kwahiyo alisikia baadhi ya maneno na purukushani, akahisi kuwa lazima Yuda atakuwa ameenda kufanya fujo tu.
Kwavile Yuda alishamtajia mahali penyewe ikabidi na yeye ajiandae kwenda.
Akabeba silaha zake vizuri na kujiandaa kwenda eneo la tukio.
"labda kuna jambo limetokea kule, itabidi niwe makini sana. Safari hii nikiwapata ni kuwafyeka tu wale sio watu kabisa"
Patrick akaondoka kwa ghadhabu huku akiwa amejiandaa vya kutosha.
Pamela na wageni wake wakafika salama nyumbani kwa Deborah ila palikuwa kimya sana kama vile hakuna watu.
Pamela akawakaribisha ndani, hata wao walishangazwa na ukimya ule.
Pamela alijaribu kumuita Tusa ila hakuitikiwa, akaamua kwenda chumbani kwa Deborah ambako alikuta mlango umefungwa, akabaki akishangaa pale mlangoni.
Wakati Pamela akishangb pale kwenye chumba cha Deborah, huku sebleni aliingia Anna akiwa na wasiwasi mwingi, hakuweza hata kuwasalimia wale wageni aliowakuta, alichofanya ni kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha Deborah ambapo alimkuta Pamela mlangoni.
ANNA: Kuna nini hapa? Kuna nini?
PAMELA: Hata sielewi.
ANNA: Huelewi kivipi?
PAMELA: Na mimi ndio kwanza nimekuja muda huu kwahiyo hata sielewi kitu.
Ana akaanza kugonga huku akiita "Deborah, Deborah"
Ila ikawa kimya, hofu zaidi ikamtawala Anna. Nae akazunguka dirishani kuchungulia ila hakuona chochote.
Ndipo Pamela alipoenda pale sebleni na kuwaeleza wote ukweli kuwa pale ni kwa Deborah, na hadi muda huo hawajui kilichompata na huku Anna akidai kuwa Deborah yupo chumbani.
Adamu na wote wakashangaa sana kusikia hivyo kwani hakutarajia kama hapo pangekuwa kwa Deborah.
Ikabidi Adamu atumie uanaume wake kwenda kukorokochoa ule mlango na kujaribu kuvunja kitasa.
Walifanya hilo zoezi kwa muda, hata wakina Tusa wakasahaulika kabisa kama nao hawapo.
Walipofanikiwa kuufungua, wakamkuta Deborah akiwa kalala chini, alikuwa amezimia.
Mashaka alipompatia Tina huduma ya kumwagia maji, Tina akazinduka.
MASHAKA: Usijaribu tena kutoroka hapa binti, utakufa unajiona wewe.
Tina akatokwa na machozi baada ya kukumbuka kilichomtokea kabla.
Akabahatika kuinuka huku akiwa ameshikiliwa na Mashaka, gafla Tina akapatwa na nguvu za ajabu na kuinua mguu halafu akampiga teke sehemu za siri Mashaka, kitu hicho kilimfanya Mashaka amuachie Tina na kuanza kuugulia lile Teke.
Tina akatumia muda huo kujaribu tena kutoroka, akakimbia sana na kuona Mashaka akimkimbiza, akafika mahali na kujificha.
Alipokuwa amejificha, mara gafla akatokea mtu nyuma yake na kumziba Tina mdomo.
 
SEHEMU YA 42

Alipokuwa amejificha, mara gafla akatokea mtu nyuma yake na kumziba Tina mdomo.
Tina aliogopa na kutetemeka hadi mkojo ukamtoka safari hii kwani alijua kuwa yupo mikononi mwa adui na lazima atauwawa tu, kwahiyo Tina alikuwa akimwaga machozi huku akiombea muujiza utokee.
Mara Mashaka akafika eneo lile na kuanza kuangalia uelekeo wa Tina, yule mtu aliyemziba Tina mdomo akamuachia na kumrukia Mashaka kwa nyuma kisha akamkaba, Mashaka akakukuruka na kufanikiwa kumuangalia mtu huyo na kugundua kuwa ni Patrick, kabla Mashaka hajafanya chochote alishtukia Patrick akiruka hewani na kumpiga mateke mawili ya juu kwa juu, mateke hayo yalimfanya Mashaka aanguke chini, Patrick akamuinua pale chini na kumpiga teke moja matata lililomfanya Mashaka aanguke mbele zaidi kama mzigo, Mashaka akiwa hoi pale chini akamuona Patrick akimfata, akaamua kuinuka na kukimbia.
Patrick akaacha kumfatilia Mashaka na kurudi kwa Tina aliyekuwa anakimbia huku anachechemea, alipomfikia Tina akamnyanyua na kumuweka begani kisha akaifata bodaboda yake na kumpakia hadi barabarani ambako alisimamisha gari ya kukodi na kumpakiza Tina humo kisha akampa dereva maelekezo ya mahali pa kumpeleka Tina.
PATRICK: Ukifika waambie umeelekezwa na Patrick.
Tina akaitikia kwa kichwa huku akizidi kulia, na dereva akaondoka gari halafu Patrick akarudi eneo la tukio.
Kufika pale akawakuta vijana wa Mashaka wamejipanga tayari kwaajili ya kupambana nae, Patrick aliyekuwa na hasira, aliwafata na kuwavuruga vuruga, aliwapiga bila kujali sehemu.
Mashaka na Maiko kuona vile wakatoka kwenye chumba walichokuwemo na kukimbilia gari yao, wakapanda na kuondoka.
Patrick nae kuona vile hakutaka kupoteza muda na wale vijana, akaenda kuchukua bodaboda yake na kupanda ili awafate wakina Maiko.
Kabla ya kuondoka mara akasikia sauti nyuma yake,
"Patrick, nisaidie"
Alipogeuka nyuma, alimuona Yuda aliyekuwa anajikongoja huku anavuja damu, ikabidi Patrick aende kumchukua na kumpakia kwenye pikipiki yake na kuanza safari ya kwenda hospitali.
Deborah alipozinduka alikuwa anashangaa tu kwani hakujua chochote kilichoendelea, ikabidi wengine wapungue chumbani na kurudi sebleni ili Deborah apate muda wa kupumzisha mawazo.
DEBORAH: Patrick wangu yuko wapi?
ANNA: Hajarudi bado.
DEBORAH: Sele na Tusa je?
ANNA: Nao hawapo.
Debora akatingisha kichwa kama ishara ya kukataa au kusikitika.
ANNA: Tukuletee nini?
DEBORAH: Maji tu yatatosha.
Pamela akaenda jikoni na kumletea maji ambayo aliyanywa kidogo na kuyaacha.
Baada ya maongezi mawili matatu, Deborah alionekana kurudi katika hali ya kawaida na kuamua kwenda sebleni kukaribisha wageni.
DEBORAH: Karibuni sana, na pia naomba radhi kwa yote.
FAUSTA: Usijari Deborah, tunaelewa.
DEBORAH: Kumbe unanikumbuka?
FAUSTA: Ndio nakukumbuka, siwezi kukusahau Deborah.
DEBORAH: (Akacheka sana) sisahauliki kwasababu ya lile tukio nililofanya nini.
Wakamshangaa Deborah kuona anacheka kwa tukio la kusikitisha, hadi wakahisi kuwa huenda akili yake haipo sawa.
Mashaka na Maiko wakiwa wamechoka kwa tukio ambalo limewatukia siku hiyo.
Maiko ndio aliyemchoma kisu cha ubavu Yuda baada ya kugundua kuwa Yuda ni mshirika wa Patrick.
MASHAKA: Hapa Mwanza kishanuka, bora turudi Arusha tukaongezee jeshi.
MAIKO: Umeona mziki wa Patrick eeh!! Yule dogo hafai.
MASHAKA: Dah! Hafai kweli yule, anapiga kama anatwanga mmh!!
MAIKO: Si ulisema hakubabaishi wewe?
MASHAKA: Aaah wewe! Yule Patrick si mtu bhana, ana nguvu za ajabu. Ameharibu haribu vijana wetu wote wanne. Turudi tu Arusha.
MAIKO: Kabla ya kurudi Arusha, nina wazo kidogo.
MASHAKA: Wazo gani? Je litaweza kutusaidia?
MAIKO: Sikia, tumtafute kwanza Deborah yule mama wa Patrick hapo ndio itakuwa rahisi kumpata Patrick.
MASHAKA: Sasa huyo Deborah tutampataje?
MAIKO: Hiyo niachie mimi, ila itabidi tufanye kimya kimya na kwa umakini sana.
Mashaka na Maiko wakaanza kupanga mipango ya kumpata Debora sasa.
Tusa na Sele waliishia Singida ambapo pesa ya Sele iliishia hapo kwani nyingine aliibiwa njiani, ikabidi waende kufikia kwa rafiki wa Sele ambaye aliishi hapo Singida, huyu aliitwa Mwita.
Mwita aliwapokea na kuwakaribisha vizuri sana.
TUSA: Kwakweli haya ndio mambo nisiyoyapenda, yani safari ya Morogoro tu hapo hadi tuchukue mwezi!
SELE: Usijari Tusa, huyu Mwita ni rafiki yangu sana. Atanikopesha tu hiyo pesa na tutafika huko Morogoro.
TUSA: Aaaargh!!
SELE: Usichukie bhana Tusa, si unajua kuwa nimeibiwa pesa nyingine! Tutafika tu.
TUSA: Ila tusikae hapa sana.
SELE: Hakuna tatizo mama, usiwe na shaka.
MWITA: Karibuni sana na muwe huru.
Mwita nae alionekana kuvutiwa sana na Tusa.
Patrick akampeleka Yuda hospitali, ambako daktari alikataa kumuhudumia.
DAKTARI: Siwezi kumuhudumia bila PF3.
PATRICK: Tafadhari daktari, nakuomba utuhurumie.
Daktari akakataa kabisa, Patrick akajaribu kumuhonga napo akakataa. Ikabidi Patrick atumie nguvu, akamtolea silaha daktari.
PATRICK: Utamuhudumia au umuhudumii?
Daktari kuona silaha akaanza kutetemeka na kuamua kumuhudumia Yuda.
PATRICK: Na ole wako umlipue lipue, utaipata hii.
Daktari akamziba Yuda jereha, ila hakuumia sana sababu kisu hakikuingia chote, alipommaliza Patrick akatoka na mgonjwa wake na kuondoka bila ya kulipia gharama za matibabu.
Tina alifika mahali ambapo alielekezwa, akagonga mlango na akatoka mama wa makamo kumfungulia. Yule mama alimuangalia kwa makini sana Tina, kisha akamuuliza
"wee Tina, nini kimekupata? Mbona umekuwa hivyo?"
Tina akabaki anamshangaa huyu mmama kwani yeye hakumjua.
 
SEHEMU YA 43

Tina akabaki anamshangaa huyu mmama kwani yeye hakumjua vizuri.
Yule mama akazidi kumkaribisha Tina ndani.
"karibu sana, na hata sijui umepatwa na nini jamani"
Tina alizidi kushangaa na kufanya huyu mama amuulize tena.
"mbona unashangaa! Kwani wewe sio Tina mtoto wa Fausta?"
Tina akaitikia kuwa ni yeye.
Huyu mama alikuwa ni Marium, mama yake na Sele. Patrick alimuelekeza huku kwavile alikuwa akipatana sana na mama zake hawa, pia hakutaka Tina aende kwao moja kwa moja kwa kuhofia kumpa presha mama yake kwa atakayoelezwa na Tina.
TINA: Mimi ni Tina ndio mtoto wa Fausta ila sijui umenijuaje?
MARIUM: Fausta ni rafiki yangu sana, kuna kipindi nilikuwa nafanya nae biashara ya kuchukua bidhaa Chini, yani wewe nakujua tangia....."
Kabla Marium hajamalizia kueleza, Tina alikuwa ameanguka chini na kuzimia, ikabidi Marium aombe msaada kwa majirani na kumpeleka hospitali.
Deborah akaamua kuongea kilichomchekesha.
DEBORAH: Msifikirie nacheka tukio nililofanya Dar, hapana. Bali namcheka Jumanne.
ADAMU: Unanicheka mimi? Kwani nimefanyaje?
DEBORAH: Hujui kituko ulichofanya mjini Jumanne?
PAMELA: Kituko gani tena?
DEBORAH: Kwakweli Jumanne umenipa sababu ya kucheka, hivi ni kitu gani kilichofanya ujifiche baada ya kuniona mjini?
ADAMU: Mmh! Inamaana uliniona?
DEBORAH: Umekua ila bado una fikra ndogo, nilikuona hadi mahali ulipojificha ila nikachuna sababu nilijua wapi pa kukupata tu. Haya sasa upo nyumbani kwangu, vipi wataka kujificha tena?
Deborah akawa anacheka, Adamu nae aliona aibu kwani hakujua kama alionekana wakati anajificha pale mjini.
Patrick alienda na Yuda kwenye hotel na kupumzika.
PATRICK: Tungerudi nyumbani, ila na alama hizo itakuwaje!! Tutawaelezaje?
YUDA: Dah!! Labda tuwaambie kuwa nilivamiwa na majambazi. Au unaonaje?
PATRICK: Basi sawa, hakuna tatizo.
YUDA: Au mama atamaindi? Basi tukae kama wiki ndo turudi nyumbani au vipi?
PATRICK: Vyovyote vile kwangu ni sawa.
YUDA: Dah! Samahani sijakuuliza, ulipokuwa unakuja pale kwenye himaya, je hujabahatika kumuona binti aliyekuwa anakimbia?
Patrick akamueleza ilivyokuwa kwa huyo binti.
PATRICK: Nadhani atakuwa kwenu sababu nilimuelekeza aende huko.
YUDA: Dah! Kama yupo nyumbani sina budi kurudi, nahitaji sana kuzungumza nae yule. Nashukuru sana Patrick kwa kumuokoa yule.
PATRICK: Kwani wewe umemfahamia wapi yule?
YUDA: Dah!! Yule binti ndo aliyefanya hadi mimi kuamua kufanya kazi za ajabu ili nipate mkwanja.
PATRICK: Sijakuelewa bado.
Ikabidi Yuda amueleze Patrick jinsi ilivyokuwa hadi yeye akafahamiana na Tina.
"Kuna kipindi mimi nilitoka Mwanza na kwenda Dar kumtembelea Sele, na ndio huko nikajua kama anatumia jina la Sele.
Nilipokuwa kwake, nikamfahamu msichana wake aliyeitwa Tusa. Mara nyingine Tusa akawa anakuja na huyu msichana aitwaye Tina kumtembelea Sele. Kwakweli nikatokea kumpenda sana Tina, ikabidi nimwambie ukweli ila akanikataa kwa kigezo kuwa sina pesa. Nakumbuka kitu alichoniambia Tina ni kuwa nikatafute pesa kwanza ndio niende kumtongoza tena. Nilirudi huku Mwanza na kutafakari sana maneno ya Tina, nikapata kazi Mombasa ila nikapitia tena Dar kumuona Tina, akaniambia kitu kilekile kuwa nitafute pesa kwanza kwani yeye hawezi kuwa na mwanaume mwenye pesa za mawazo.
Tina ni msichana mwenye maringo sana ila nampenda sana, sikutaka kumkosa, nikasema nitafanya kazi yoyote ile ili niweze kuwa naye. Ndio nikaenda Mombasa ila kazi ya kule ilikuwa hailipi kivile, katika pitapita ndio nikakutana na Mashaka, akaniomba nikafanye nae kazi akanitajia mshahara mnono sana. Sikuweza kukataa kwani pesa niliitaka, ndio huko nikakutana na yale maswahibu ya kuona kichwa cha baba"
PATRICK: Dah! Pole sana Yuda, kumbe yule ndio Tina aliyeutesa moyo wako! Pole sana.
YUDA: Kwakweli nilishindwa kujizuia baada ya kusikia sauti ya Tina ikilia toka kwenye kile chumba, na ndiomana nikafanya gafla bila makubaliano.
PATRICK: Ndio hivyo mdogo wangu, pesa kwanza mapenzi badae. Bila pesa huthaminiki.
YUDA: Ila mbona Tusa anampenda Sele bila ya pesa jamani!
PATRICK: Dah! Pole sana Yuda, nadhani huujui ukweli. Tusa ni mke wa mimi sasa, nae alidanganyika kwa kitu kidogo tu nacho ni Pesa. Unatakiwa uiheshimu pesa kwani ukiwa nayo chochote utakacho unapata.
Yuda akabaki anashangaa tu kwani hakujua chochote kuhusu Sele, Patrick na Tusa.
Tusa na Sele wakiwa nyumbani kwa Mwita, wakiwa hawajui hili wala lile.
Mwita akamwambia Sele kuwa aende nae mahali ambako atampa pesa za kumuwezesha kuendelea na safari yao, ikabidi Sele amuage Tusa.
SELE: Nadhani kesho ndio tutaenda Morogoro, sababu leo Mwita ananipeleka kuchukua pesa.
TUSA: Sawa, ila nakuomba uwe makini sana.
SELE: Usijari Tusa.
Sele na Mwita wakaondoka huku Sele akiwa hajui wazo alilonalo Mwita.
Mashaka na Maiko wakaendelea na mipango yao na kuona kuwa karibia wanafanikiwa.
MAIKO: Kuna mtu nimeongea nae, amesema atanitumia details zote za alipo Deborah.
MASHAKA: Hapo ni safi sana, nangoja majibu tu.
MAIKO: Itabidi niende mjini nikakutane nae.
MASHAKA: Hakuna tatizo, nenda tu.
Maiko akajiandaa na kuondoka.
Marium aliendelea kumshughulikia Tina hospitali, akasahau kila kitu.
MARIUM: Nakuomba daktari, muhurumie binti yangu.
Daktari huyu alikuwa kimya tu kwani alikuwa na hasira na wakina Patrick, ila Marium hakujua kama huyu Daktari ametoka kufanya kazi kinguvu kwa watoto wake.
Daktari alijawa na hasira iliyoambatana na uoga kwani alihudumia wagonjwa huku akihofia ujio wakina Patrick tena.
Maiko alipokuwa mjini kwaajili ya kuonana na mtu aliyepanga nae. Mara gafla akashtukia amepigwa mtama na kuanguka chini.
 
SEHEMU YA 44

Mara gafla akashtukia amepigwa mtama na kuanguka chini.
Maiko akashangaa sana, kabla hajajiweka sawa alijikuta akipigwa tena teke lilolomfanya aanguke tena, akaanza kufuatwa pale chini na Patrick,kwakweli Maiko akaona amepatikana kwasasa na hana ujanja tena.
Patrick alipomkutia pale chini na kumkunja . Halafu akakunja ngumi kwaajili ya kumshindilia nayo usoni, ndipo Maiko alipoanza kuongea,
MAIKO: Unatafuta kesi bure Patrick.
PATRICK: Unajua maana ya kesi wewe? Ungekuwa unajua ungeua watu hovyo.
MAIKO: Anaeua watu si mimi Patrick.
PATRICK: Najua, kazi yako si kutuagiza vijana tusio na hatia kutenda dhambi.
MAIKO: Hapana sio hivyo ni Mashaka ndiye anayetoa maagizo, hata mimi huwa naagizwa tu.
Patrick akamshindilia ile ngumi usoni
PATRICK: Hata kama, wewe ni muuaji tu Maiko huna cha kujificha. Haya huyo Mashaka wako yuko wapi?
Mara simu ya Patrick ikaanza kuita, mwanzoni akaipotezea ila ilipoanza kuita tena akaamua kuipokea na Maiko nae akatumia muda huo kukimbia kwani alichota mchanga pale chini alipokuwa na kumrushia Patrick usoni, kitendo kilichofanya Patrick amuachie Maiko na kuanza kupekecha macho.
Maiko akakimbilia gari yake na kuondoka.
Deborah na wote pale nyumbani wakaamua kufanya harakati.
DEBORAH: Kama hivyo unavyosema kuwa huyo Tina hajulikani alipo, itabidi tukatoe taarifa polisi.
PAMELA: Nadhani tufanye hivyo, ila vipi kuhusu Tusa?
DEBORAH: Tusa hajapotea ila wamejipoteza na Sele wake nadhani watarudi tu.
ADAMU: Ila huyo mtoto ndiye anayenipa presha jamani, sijui hata atakuwa wapi?
DEBORAH: Mmoja mmoja ndio mpango, anzeni na huyo Tina kwanza halafu wakina Tusa watafuata.
Ikabidi Adamu na Fausta wafanye safari ya kwenda polisi.
Maiko alirudi kwa Mashaka akiwa na alama za kudundwa usoni.
MASHAKA: Vipi tena?
MAIKO: Nimekutana na Patrick.
MASHAKA: Dah! Nilishakwambia mimi, hapafai huku bora turudi Arusha tukajipange upya bhana.
MAIKO: Kwakweli Patrick amenidhalilisha sana, wala sikufikiria kama angenifanya vile sehemu kama ile. Nakwambia sukubali hadi nimkomeshe, nitakapotoka tena hapa ni moja kwa moja hadi kumchukua mama yake, yani nimechukia sana.
MASHAKA: Sasa na huyo mama yake utampataje?
MAIKO: Nitampata tu, kwasasa sitaki kuwaagiza watu kukutana mjini, ila nitakutana nao hapahapa.
MASHAKA: Haya bhana, ila na mimi leo nitatoka kidogo. Kuna mahali naenda.
MAIKO: Kuwa makini sana huko uendako.
MASHAKA: Usijari chochote.
Mashaka nae akatoka kwenda alipopanga.
Patrick alirudi kwa Yuda akiwa na hasira sana.
PATRICK: Simu uliyonipigia imeniharibia kila kitu. Haya unataka nini?
YUDA: Samahani kaka, ila leo nilipowasha simu nimepigiwa na mama kuwa niende nyumbani kuna matatizo.
PATRICK: Sinilishakwambia kuwa huyo Tina nilimuelekeza aende huko! Sasa tatizo ni nini kuambiwa kuwa kuna matatizo?
YUDA: Hapana tatizo Patrick ila ningependa twende wote.
PATRICK: Aaah!! Wewe nenda tu kawachek, mimi nitakuja hata kesho.
YUDA: Kwahiyo umeniruhusu?
PATRICK: Ndio, nenda tu kawachek.
Yuda akaamua kwenda kwao ili kumuona Tina na mama yake.
Patrick nae akatoka kwaajili ya kuendelea kuwasaka wabaya wake, alitoka na bodaboda yake kama kawaida.
Tina alipopata unafuu akaruhusiwa na kurudi na Marium, kufika nyumbani kwake akafurahi kumuona mwanae Yuda. Na Yuda nae akafurahi kumuona Tina, akaenda kumkumbatia na kumpa pole.
Marium akawashangaa,
MARIUM: Kwani mnafahamiana?
YUDA: Usijari mama, nitakueleza tu.
Wakaingia ndani, na kuanza mazungumzo.
MARIUM: Nimekuita mwanangu kwavile nilishachanganyikiwa kabisa, Tina alikuwa na hali mbaya sana. Mbona hukuja moja kwa moja hospitali niliyokuelekeza?
YUDA: Aaah mama, niliona bora mje mnikutie nyumbani tu.
Yuda hakuweza kwenda kwenye hospitali aliyotajiwa kwakuwa ndio hospitali aliyofanya nayo majanga yeye na Patrick.
Tina nae akaamua kumuuliza Yuda.
TINA: Na yule aliyeniokoa na kunielekeza hapa, yule Patrick yuko wapi?
YUDA: Yupo nimemuacha mjini ila atakuja tu.
MARIUM: Mbona mnanichanganya, inamaana Yuda ulikuwa na Patrick? Siku zote ulipotoweka hapa ulikuwa na Patrick? Hivi unajua kama.... Aaargh!!
Marium akaingiwa na hofu kwani alishaambiwa na Sele kuwa Patrick ni jambazi na anapotoweka kwao basi huenda kufanya ujambazi, mwanzoni alishindwa kuamini ila imani ilimjia pale Sele alipopigwa na kuumizwa sana na Patrick.
Mwita alienda na Sele sehemu ya mbali sana, akamuacha hapo na kumwambia amsubirie ili arekebishe baadhi ya vitu.
Ila Sele alisubiri na kusubiri bila ya Mwita kutokezea. Ikabidi atafute utaratibu mwingine wa kuweza kurudi nyumbani kwa Mwita, na akaona kuwa Mwita hakuwa na lengo zuri, hivyo nia yake ilikuwa ni kurudi na kwenda kumchukua Tusa tu.
Mwita alirudi nyumbani kwake na kumkuta Tusa sebleni, akasalimiana nae na kwenda chumbani. Tusa akashangaa bila ya kumuona Sele, Tusa alipokuwa akitafakari mara Mwita akarudi tena sebleni ikabidi Tusa aulize.
TUSA: Kwani Sele yuko wapi?
MWITA: Yupo tu, unataka kujua alipo?
TUSA: Ndio, niambie ulipomuacha.
Mwita akainuka na kumwambia Tusa amfuate alipo Sele.
Tusa akainuka ila akasita kumfuata kwani aliona akielekea chumbani.
MWITA: Mbona umekwambia njiani? Twende ukamuone.
TUSA: Mbona huko ni chumbani?
MWITA: Hapana si chumbani ila kule kuna mlango mwingine, Sele ameamua kukusurprise.
Tusa akabaki akishangaa tu.
MWITA: Twende Tusa, usiwe na hofu. Mimi sio mtu mbaya.
Tusa akamfata, walipoingia tu, Mwita akafunga mlango na kuanza kumwambia Tusa.
MWITA: Binti mrembo kama wewe ni halali ya watu kama mimi wenye pesa na si mtu kama Sele, atakupa nini Yule eeh!
TUSA: (Huku akiogopa), mimi nampenda Sele sitaki mwingine.
MWITA: Kuwa mpole tu Tusa maana hapa hutaki utataka, unataka utapata.
TUSA: (Akaanza kutokwa na machozi), mimi sitaki, tafadhari usinifanye vibaya.
MWITA: Na mimi siwezi kumuacha mrembo kama wewe uende, hapa utanipa tu.
Mwita akaanza kumng'ang'aniza Tusa, ikawa purukushani. Tusa akampiga teke Mwita sehemu za siri ili apate kutoroka, ile anafika mlangoni tu Mwita akamkamata tena Tusa na safari hii akampiga hadi Tusa akazimia halafu akambaka wakati amezimia.
Watu wa namna hii wanaweza kubaka hata maiti kwa uchu wao.
Adamu na Fausta walipokuwa wanarudi toka kituo cha polisi, Adamu alimuomba Fausta amsubirie ili akatoe haja ndogo.
Fausta akawa amesimama akiwa hajui hili wala lile, mara akatokea mtu nyuma yake na kumziba mdomo kisha akampakia kwenye gari na kuondoka nae.
Tukio lile lilionwa na Patrick aliyekuwa kwenye bodaboda.
Patrick akaamua kuifatilia ile gari.
 
SEHEMU YA 45

Patrick akaamua kuifatilia ile gari.
Dereva wa ile gari alikuwa akiendesha kwa kasi sana ila Patrick nae alikuwa na kasi ya ajabu kwenye bodaboda yake kwasababu hakutaka ile gari impotee.
Kwenye ile gari alikuwemo Mashaka na akagundua kuwa kuna bodaboda inamfatilia ila hakujua ni nani kwavile mwendeshaji alivaa helementi, ila hofu ikamjia kuwa huenda akawa ni Patrick, maneno ya Maiko yakamrudia kichwani kuwa anatakiwa awe makini sana.
Kila akizidi kuongeza kasi ndipo na ile pikipiki ilivyoongeza kasi.
Mashaka akajua kuwa anafatiliwa sababu amemteka Fausta, kwahiyo akaamua kufanya uamuzi wa gafla, akafungua mlango wa gari wakati ipo kwenye kasi na kumsukumia Fausta nje. Ni hapohapo kikatokea kitendo cha gafla pia toka kwa Patrick, kwani alichukua bastola na kulenga tairi moja wapo la gari ya Mashaka, kitu kilichofanya gari kukosa muelekeo na kuseleleka hovyo na mwisho kusimama.
Mashaka alikuwa mashakani sasa, akaamua kufanya uamuzi mwingine wa kukimbia, akatoka ndani ya gari, kwa bahati alitokea mwendesha bodaboda na bodaboda yake, alichofanya Mashaka ni kumsukuma yule wa bodaboda kwa mti, kitu kilichofanya bodaboda iwe upande wake na mtu upande wake. Mashaka akaikimbilia ile bodaboda na kuondoka nayo. Ikawa bahati kwa Mashaka na mkosi kwa mwendesha bodaboda.
Patrick hakuweza kumkimbiza tena Mashaka kwani alimuhurumia mwanamke aliyetupa pembeni na Mashaka.
Patrick aliinama na kumuangalia mwanamke huyo aliyekuwa anavuja damu hasa sehemu ya kichwani kwani aliangukia kichwa.
Ikabidi amnyanyue na kusimamisha gari ya kukodi akampakiza na kwenda naye hospitali.
Adamu alipotoka kujisaidia, akashangaa bila ya kumuona Fausta, akamtafuta sana bila ya mafanikio yoyote, ikabidi arudi nyumbani kwa Deborah.
Wote wakashangaa kumuona Adamu amerudi peke yake, na kumuuliza alipo Fausta. Akawajibu anachojua yeye.
DEBORAH: Sasa atakuwa ameenda wapi jamani? Maana Mwanza yenyewe hata haijui.
REHEMA: Isije ikawa amepotea kama mwanae Tina!!
PAMELA: Mmh! Mama, hata hakuna skendo za ajabu hapa Mwanza. Sasa huko kupotea watakuwa wanapoteaje?
ADAMU: Kwakweli mimi ndio sielewi kabisa, tumeandikisha vizuri pale polisi. Ila kitendo cha mimi kwenda kujisaidia tu yeye katoweka.
PAMELA: Au kuna mahali kapita atarudi.
ADAMU: Sidhani kama Fausta anaweza kushika njia kwa siku moja, ubaya ni kuwa nikimpigia simu inaita tu bila ya kupokelewa.
DEBORAH: Mmh! Huo mtihani, yani mengine hayajaisha yanakuja mengine mweeeh!! Sasa itakuwaje?
REHEMA: Mimi nadhani wewe Adamu na Pamela muende pale ambapo ulimuacha huyo Fausta, anaweza akawa amerudi pale ila amekosa uelekeo.
ADAMU: Ngoja tukajaribu basi.
Ikabidi Adamu na Pamela waende kumuangalia Fausta pale alipoachwa mwanzo na Adamu.
Mashaka alirudi hotelini akiwa anahema juu juu.
MAIKO: Vipi tena?
MASHAKA: Si yule mpumbavu wako, dah amenidhalilisha sana yani hadi nimeacha gari yangu.
MAIKO: Ila si nilikwambia uwe makini? Patrick ni khatari.
MASHAKA: Yani leo nilimpata mbaya wangu niliyemtafuta kwa muda mrefu, halafu Patrick kanizingua dah!!
MAIKO: Pole sana, gari umeiacha kabisa?
MASHAKA: Nitaifata tu, ila nimechukia sana leo. Yani yule mtoto wa kike ningemtesa leo na kumchinjilia mbali, ana bahati sana.
MAIKO: Mtoto wa kike gani huyo?
MASHAKA: Fausta huyo.
Maiko akashtuka na kushangaa kuwa Fausta yupo Mwanza.
MAIKO: Bora Patrick alivyotokea, dah yani wewe sijui hata ukoje! Unataka kuua watu wasio hata na hatia.
MASHAKA: Mimi ndiye ninayeijua hatia ya Fausta, yani Patrick namuandalia kisasi cha kufa mtu si anajifanya yeye ni bingwa wa kutetea watu wa Mwanza! Ngoja nitamkomesha tu.
MAIKO: Huna jipya Mashaka, ngoja nitoke mie ila mwenzio niko makini sana kwanza sitoki hovyo kwenye gari.
MASHAKA: Haya bhana, kunya anye kuku akinya bata....malizia mwenyewe.
MAIKO: Methali mbele ya Patrick!! Mbona utazijua zote mwaka huu, mtoto mdogo anatujambisha.
Maiko akatoka kwenda sehemu nyingine kwaajili ya kukutana na watu wake.
Tina akawa amepata unafuu kiasi pale nyumbani kwa Marium.
Ikabidi Marium amtume mwanae Yuda kwenda kumtembelea Deborah.
MARIUM: Yuda, ufanye uende kwa mamako mdogo ukamuangalie maana nikimpigia simu hata hapatikani. Si unajua atakuwa mwenyewe pale.
YUDA: Sele je yuko wapi?
MARIUM: Nimesahau, Sele aliniambia anaenda Singida mara moja. Mamako mdogo nasema yuko mwenyewe sababu huyo Tusa mwenyewe pale kwake ni kama mgonjwa tu.
YUDA: Yupo na mama yake Tusa.
MARIUM: Nimekwambia uende ukamuangalie, porojo sitaki sijui yupo nani na nani sitaki. Nenda kamuangalie mdogo wangu anaendeleaje.
YUDA: Sawa basi, nitaenda kesho.
Halafu Marium akamfata Tina ili wamjaribishe mama yake ila simu iliita tu bila ya kupokelewa.
TINA: Labda atakuwa mbali na simu, ila akikuta kuwa amepigiwa basi atapiga tu hiyo simu.
MARIUM: Ila usiwe na mashaka sana Tina, jisikie huru.
TINA: Sawa mama, nashukuru.
Tina alijilaumu sana kwa tamaa ya pesa, kwani ndiyo iliyomponza.
Patrick alimpeleka Fausta hospitali ile ile aliyotibiwa Yuda.
Daktari hakutaka mabishano safari hii, alimuhudumia Fausta bila hata ya kuulizia karatasi namba tatu (PF3).
Alimuogopa sana Patrick, alifanya kazi kwa uoga mkubwa.
Baada ya kumfunga bandeji na kumpa baadhi ya dawa akaruhusiwa kuondoka, ikabidi Patrick amchukue hadi alipo yeye.
PATRICK: Je unapajua kwa ndugu zako?
FAUSTA: Kwakweli mimi ni mgeni hapa Mwanza, hata sijui panaitwaje pale tulipofikia.
Patrick akaona kuwa huu sasa ni mtihani, akawa anawaza je ampeleke kwa mama yake au kwa mama yao na wakina Sele.
Pamela na Adamu walipoenda kumsaka Fausta.
ADAMU: Hivi wewe Pamela, kwanini hukuniambia mapema kuwa upo kwa Deborah?
PAMELA: Vipi kwani?
ADAMU: Sikuwa tayari kukutana nae kwasasa.
PAMELA: Kwani bado wampenda?
ADAMU: Maswali gani hayo bhana!! Aaargh.
Wakajikuta wakibishana bila hata ya faida.
Walikuwa wanaendelea kubishana ndipo waliposikia tukio la mwendesha bodaboda.
Hata pale Mwita alipomaliza haja zake, Tusa alikuwa bado kazimia.
Mwita akawaza cha kufanya na yule binti.
"Hivi amezimia kweli au amekufa? Kama amekufa mbona itakuwa ni balaa hili mmh!!
Akimtazama mapigo ya moyo yalikuwa bado yanadunda, ila alikuwa mtu asiyejitambua kabisa.
Mwita alipokuwa anahangaika cha kufanya na Tusa, mara anasikia mtu anagonga hodi.
Kwenda kumchungulia dirishani alikuwa ni Sele.
 
SEHEMU YA 46


Mara anasikia mtu anagonga hodi.
Kwenda kumchungulia dirishani alikuwa ni Sele.
Mwita akaona sasa kazi anayo na atamweleza vipi Sele, ikabidi ajiandae namna ya kupanga maelezo halafu akamvuta Tusa pale sebkeni na kumfunika, ndipo alipoenda kufungua mlango.
SELE: Mbona uliniacha Mwita?
MWITA: Nilisahau kama tulienda wote ila nilitaka nikufate wewe.
SELE: Hizo ni porojo tu, haya Tusa yuko wapi?
Ikabidi Mwita amuonyeshe Tusa aliyekuwepo pale chini.
Sele akashtuka sana na kwenda kumfunua Tusa.
Sele aliinuka na kumkunja Mwita.
SELE: Niambie haraka umemfanya nini Tusa?
MWITA: Sijui, nimemkuta hivyo hivyo.
SELE: Muongo mkubwa wewe.
Sele akampiga Mwita ngumi ya tumbo,
SELE: Niambie ukweli Mwita.
MWITA: Unanionea tu ila sijui chochote.
Siku zote mkosaji mwenye hofu huishiwa na nguvu na ndivyo ilivyokuwa kwa Mwita.
Sele akampiga Mwita ngumi nyingine, ikabidi Mwita nae aanze kujitetea na kuanza kupigana, wakapigana sana.
Mara Mwita akachukua kisu kilichokuwa mezani ili kumtishia Sele.
Yuda alienda moja kwa moja hadi kwa Deborah.
YUDA: Nimekuja kukusalimia tu mamdogo na kuangalia unaendeleaje.
DEBORAH: Naendelea vizuri ila ukirudi nyumbani mwambie dada yangu kuwa namwitaji sana, nina matatizo hapo.
YUDA: Sawa, ila je yule bibi pale nje ni nani?
DEBORAH: Ni bibi yenu yule.
YUDA: Kivipi mamdogo?
DEBORAH: Hata nikikueleza hautanielewa, wewe ukienda mtaarifu tu dada yangu.
YUDA: Na huyo Tusa yuko wapi maana namsikia kwenye mabomba tu.
DEBORAH: Kamuulize kaka yako Sulemani, kwakweli hata sielewi mie jamani na hata sijui akija Patrick nitamuelezaje mwenzenu.
YUDA: Mmh! Khatari kama ndo hivyo.
Yuda ikabidi aage na kuendelea kupewa msisitizo wa kumwambia mama yake.
Adamu na Pamela ikabidi nao waende kwenye eneo la tukio ambako walikuta damu na gari ambayo iliachwa pale, watu walikuwa wanashangaa na kuondoka ila wao walikuwa wanashangaa na kuendelea kubishana kuhusu kupelekwa kwa Deborah.
Wakati wanaendelea kubishana, Adamu akawa amevutwa sana na maelezo ya mwenye bodaboda, akataka kumfata ili aweze kumsikiliza na kung'amua japo kitu kimoja, akamwambia Pamela kuwa wasogee pale kumsikiliza.
PAMELA: Tufate kilichotuleta, hayo maelezo ya huyo mtu hayawezi kutusaidia kitu.
ADAMU: Huwezi jua Pamela, pengine tutagundua kitu chochote hapo.
PAMELA: Babu wee, nenda mwenyewe.
Pamela alionekana kuchukizwa na zile lawama alizopewa na Adamu pia alihisi kuwa huenda Adamu akawa bado anampenda Deborah.
Adamu alijua ni hasira za muda mfupi tu zile, akaamua kwenda kumsikiliza yule wa boda boda.
ADAMU: Nikukute hapo hapo.
PAMELA: Utamkuta beberu.
Akawa amesema kwa kumtania mumewe humo humo.
Adamu alipokuwa anasikiliza maelezo ya yule kijana wa bodaboda ambapo baadhi ya wananchi walikuwa wakimsaidia, akaona yale maelezo yanaweza kuwa na kitu cha kuwasaidia, akarudi kwa Pamela ili amueleze na ikiwezekana wakasikilize wote. Ila Hakumkuta Pamela, akamtazama kila sehemu hakumuona. Akaanza kujiuliza, "inamaana aliposema kuwa nitamkuta beberu alikuwa anatania au alimaanisha? Kama alimaanisha je amekwenda wapi jamani?"
Adamu akamuangalia sana bila matumaini.
Ikabidi arudi nyumbani kwa Deborah ili kumuangalia kama amesharudi.
Yuda aliporudi kwao alimpa mama yake taarifa aliyopewa na Deborah.
MARIUM: Ana matatizo gani kwani?
YUDA: Sijui, ila ukienda atakueleza mwenyewe vizuri.
MARIUM: Mmh! Mnanitisha sana.
YUDA: Halafu mama, huyu kaka Sele huyu anatafuta matatizo.
MARIUM: kivipi tena?
YUDA: Nini kimemtuma kuondoka na Tusa? Nakwambia mama, Patrick akijua basi ujue Sele atakuwa hatiani.
MARIUM: Jamani jamani nyie watoto, mtaniua kabla ya siku zangu jamani. Mmh! Sele nae kwanini hakubali kushindwa? Hili ni tatizo sasa.
YUDA: Sijui hata itakuwaje kwakweli, hali ni mbaya mama.
Yuda nae alianza kumuhurumia Sele kwani kipigo cha Patrick kilimtisha sana.
Patrick aliendelea kumuhudumia yule mwanamke.
PATRICK: Ukipata nafuu kidogo nitakupeleka kwa mama yangu kama hutojali.
FAUSTA: Hakuna tatizo kijana, nitashukuru sana.
Fausta alikuwa hajielewi kwani mara nyingine kumbukumbu zake zinakuja na mara nyingine zinapotea.
Adamu akarudi bila ya Pamela, akaanza kuulizwa maswali juu ya Pamela na kusema kuwa haelewi alipo.
REHEMA: Una nini Adamu, kwanini kila ukiondoka na mtu unarudi peke yako?
ADAMU: Sielewi tatizo mama, yani sielewi kabisa.
REHEMA: Umempoteza Fausta, na sasa ni Pamela. Naomba uende mwenyewe kituo cha polisi ukaripoti kupotea kwao.
ADAMU: Yani mama hujui tu nilivyochanganyikiwa hapa.
DEBORAH: Kuchanganyikiwa hakutasaidia, fanya kama ulivyoambiwa na mama. Sijui kuna nini Mwanza hapa, mbona mambo ya ajabu haya. Kupotea kwa watu wazima mmh!
ADAMU: Sawa nitaenda basi.
REHEMA: Ila uwe makini maana naona hali ni mbaya kabisa.
ADAMU: Sawa, ila itabidi tungoje kwanza ili niende kesho.
Wakakubaliana kuwa aende kesho kutoa taarifa ili kwa siku hiyo wawe wanaangalia kwanza kama watarejea.
Sele alipoona Mwita amebeba kisu ikabidi auwahi mkono wa Mwita, katika purukushani kile kisu kikamuangukia Tusa ila wenyewe hawakugundua hilo na kuendelea kupigana, kumbe pale chini Tusa alizinduka.
Katika kupigana Mwita akafanikiwa kumuangusha Sele na kuanza kumkaba, ndipo Tusa alipoinuka na kile kisu na kumchoma nacho Mwita mgongoni.
Tusa alifanya kitendo hicho kwa gafla sana na kujikuta anatetemeka, damu zilijaa kwani Mwita alitokwa na damu nyingi sana. Sele aliinuka na kushangaa lile tukio la gafla lililofanya Mwita atapetape.
Wakati wanashangaa na hawajui cha kufanya, mara alisikika mtu akigonga mlango wa Mwita.
 
SEHEMU YA 47


Wakati wanashangaa na hawajui cha kufanya, mara alisikika mtu akigonga mlango wa Mwita.
Hofu ikawatanda Sele na Tusa.
SELE: Umeona sasa ulichofanya Tusa? Hii ni kesi tayari.
Tusa alikuwa akitetemeka tu kwani hakudhamiria kumchoma mtu kisu, ila alimchoma sababu ya maumivu aliyonayo moyoni juu ya kubakwa.
Yule mtu aliyekuwa anagonga aliendelea kugonga, ikabidi Sele aende kumchungulia, akamuona ni mwanajeshi akajua ni rafiki wa Mwita au anafanyakazi na Mwita kwani Mwita nae alikuwa mjeshi.
Sele akarudi kwa Tusa,
SELE: Hali mbaya Tusa, huyo anayegonga ni mwenzie na Mwita, nae ni mwanajeshi. Hata sijui itakuwaje.
Tusa hakujibu kitu, ila akajivika ujasiri na kwenda mlangoni, akawa anamuuliza bila kufungua mlango.
TUSA: Nani wewe?
MGENI: Mimi hapa Hamis, namtaka Mwita mara moja.
TUSA: Mwita ametoka na ameondoka na fungua, nadhani atarudi asubuhi.
MGENI: Mbona gari yake ipo?
TUSA: Kuna rafiki yake alikuja kumfata, sitaki maswali zaidi maana sina majibu yake.
Tusa alimjibu kwa ujasiri na kujiamini sana, ikabidi Hamis aondoke zake.
SELE: Mmh Tusa! Umekuwa mkavu kama hujafanya chochote vile, haya tuondoke hapa fasta kabla mambo hayajaharibika.
Wakachukua vitu vyao na pesa iliyopo ya Mwita halafu wakaondoka bila kujali kama Mwita yupo hai au amekufa.
Adamu akajiandaa kwaajili ya kwenda tena polisi.
REHEMA: Unatakiwa usimame kama baba, uitetee familia yako. Sasa ukikata tamaa unadhani itakufaidia nini?
DEBORAH: Mwambie ukweli mama, nadhani matendo uliyofanya nyuma unayajutia hata kama hayana madhara kwako. Ila uwe makini kwasasa usije ukajutia maisha yako yote.
ADAMU: Umakini gani unaousemea Deborah? Wewe ndo chanzo cha yote haya, tusingekuja Mwanza haya yasingetupata.
DEBORAH: Kunilaumu ni kawaida yako, kwahiyo sioni tatizo. Katika swala la ndoa, upendo ni kitu muhimu sana.
ADAMU: Sasa swala la ndoa na upendo vinahusika nini hapa? Deborah nadhani kuna kitu unahitaji toka kwangu wewe.
DEBORAH: Tena usitake kunikera mwanaume wewe, sina chochote ninachotaka toka kwako. Nikutake kwa lipi msaliti wewe!!
Ikabidi bi.Rehema aingilie kati.
REHEMA: Jamani jamani msije mkaanza kugombana bila sababu hapa, haya Adamu nenda polisi na utuache hapa.
Ikabidi Adamu atoke na kuondoka. Deborah akakaa chini huku machozi yakimlengalenga.
REHEMA: Tulia mama, hii ni changamoto ya maisha.
DEBORAH: Inaniuma sana kuona Jumanne anaona ni sawa tu hadi leo kitu alichonifanyia, ila mama Mungu ni mkubwa sana na anaendelea kunitetea ingawa ni mapito mengi niliyopitia.
REHEMA: Usijali mwanangu.
Rehema akaendelea kumpooza Deborah kwani alipandisha jazba sana.
Pamela alizinduka na kuanza kurudisha kumbukumbu, akakumbuka mara ya mwisho alikuwa anabishana na mumewe halafu mumewe akaenda kumsikiliza dereva wa bodaboda na kumuacha yeye amesimama, akakumbuka alisikia mikono ya baridi ikipita toka nyuma yake na kitambaa kilichomziba pua na kupoteza fahamu kabisa, ndio amezinduka sasa na yuko kwenye mikono ya adui ambaye ni Maiko.
MAIKO: Ulijiona umewin kwa kunikimbia na Patrick wako, haya sasa huyo Patrick wako alikupeleka wapi?
Pamela akawa anatetemeka bila ya kujibu chochote.
MAIKO: Nijibu bhana, Patrick alikupeleka wapi?
PAMELA: Kwa mama yake.
MAIKO: Unamaanisha Deborah eeh!
PAMELA: Ndio ni Deborah.
MAIKO: Haya sasa, pona yako ni kunielekeza mimi nyumbani kwa Deborah au tutaenda wote. Kwanza Patrick yuko wapi?
PAMELA: Hayupo kwao, nadhani wiki ya pili hii.
Maiko alifurahi kwa kupata kupajua nyumbani kwa Deborah kwa wepesi bila hata ya kutumia nguvu.
Tusa na Sele walienda kufikia kwenye hoteli moja wapo kwenye mji wa Dodoma kwani ilishindikana kusafiri zaidi kwa usiku ule.
SELE: Tusa, nadhani sasa umekuwa na tabia za Patrick.
TUSA: Kivipi?
SELE: Hivi Tusa wewe ni wa kuua mtu kweli? Mbona umefanya ukatili mkubwa sana.
TUSA: Yani mimi kukutetea wewe ndio unaniona kuwa nimekuwa katili? Yote haya umeyataka wewe Sele. Tungebaki Mwanza hata yasingetokea, vipi nikianza kutafutwa na polisi?
SELE: Tusa sina nia mbaya kukwambia kuwa umekuwa katili, nisamehe kwa hilo ila kumbuka yule Mwita ni mwanajeshi na sijui kama tutaweza kupambana na mtiti wa wajeshi.
TUSA: Tusitishane basi.
Kesho yake wakatoka kwaajili ya kuendelea na safari, walipokuwa stendi walimuona Hamis na baadhi ya wanajeshi wakikagua abiria wa pale stendi ikabidi waende kwenye choo cha pale stendi na kujificha kwani walikuwa hawajui wale wajeda wanatafuta nini.
Adamu alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, aliona mji wa Mwanza ukimchanganya sana.
Alipotoka polisi akaamua kwenda baa ili apate bia mbili tatu aweze kupunguza mawazo.
Huko baa akakutana na mtu mwenye kuitwa Mashaka na katika stori mbili tatu akaamua kumsimulia yanayomsibu.
Patrick aliona kuendelea kukaa na Fausta kutakwamisha mipango yake, kwahiyo akaamua kumchukua kama alivyopanga na kuanza safari ya kumpeleka kwa mama yake, pia alihitaji kumuona na kumsalimia mama yake. Alimkumbuka sana.
FAUSTA: Ndio unanipeleka kwa huyo mama yako?
PATRICK: Ndio, na kule utakuwa salama zaidi.
Hakutaka tena kumpelekea mzigo mamake mkubwa, aliona huyu ampeleke kwa mama yake tu.
Maiko aliondoka na Pamela hadi nyumbani kwa Deborah, Maiko alijiandaa vya kutosha na shida yake ilikuwa ni moja tu, nayo ni kumchukua na kumteka Deborah.
Walipofika pale, walimkuta bi.Rehema akiwa nje.
Wakati Maiko anaingia kwenye nyumba ya Deborah, macho yake yakagongana na macho ya bi.Rehema.
Maiko alimuangalia sana bi.Rehema bila ya kufanya chochote, alihisi kuwa sura ya mama huyo si ngeni machoni mwake.
Maiko aliendelea kuduwaa huku akimtazama bi.Rehema.
 
SEHEMU YA 48

Maiko aliendelea kuduwaa huku akimtazama bi.Rehema.
Alihisi kabisa kuwa anamjua mama huyo, Pamela nae akawa anamshangaa Maiko jinsi alivyozubaa kwa kumtazama bi.Rehema kwani hata yeye aliyekuwa ameshikiliwa kwanguvu kama mtuhumiwa aliachiliwa, ndipo alipouliza.
PAMELA: Mbona unamshangaa, kwani unamjua?
Maiko hakujibu chochote alikuwa ameganda tu.
Rehema nae alikuwa amepatwa na kitu kama mshtuko kwa kumuona Maiko, akamsogelea karibu, akamshika kichwa na kuanza kumkagua kagua mwilini, Maiko aliganda kama sanamu alikuwa kama mtu aliyepigwa bumbuwazi.
Rehema alimshika mkono Maiko na kumvutia ndani kwa Deborah.
Alipofika nae sebleni, Deborah nae alikuwa anatoka chumbani na kushangaa kumuona Maiko, akajikuta akisema kwa kustaajabu.
DEBORAH: Maiko!!!
Maiko alimtazama tu Deborah kamavile hakumfata yeye.
Deborah akamshangaa bi.Rehema kumkaribisha Maiko ndani.
DEBORAH: Mama tafadhari, simtaki huyo mtu ndani ya nyumba yangu.
MAIKO: (Akaongea kwa mshtuko) mama!!!
Maiko akaanguka chini na kupoteza fahamu, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Deborah kumuona Maiko akipoteza fahamu.
DEBORAH: Kheee!! Na mashetani huwa wanazimia?
PAMELA: Hata na mie nashangaa!
Rehema hakujibu kitu zaidi ya kutokwa na machozi tu.
Tusa na Sele walikuwa hatiani sasa na hawakujua ni jinsi gani watajinasua kutoka kwenye tukio la kumchoma kisu mwanajeshi.
SELE: Tusa, hii ni hatari sasa, naomba tufanye kitu.
TUSA: Kitu gani?
SELE: Tusiende tena Morogoro Tusa, machale yananicheza kuwa hatutakuwa salama huko.
TUSA: Sasa unataka twende wapi?
SELE: Twende Songea kwa bibi.
TUSA: Aaah! Mi Songea siendi.
SELE: Ubishi sio mzuri Tusa kumbuka kuwa tumeshaharibu, basi twende hata Mbeya.
TUSA: Mbeya ndo hunipeleki kabisaaa, sitaki kwenda kokote zaidi ya Morogoro. Nahitaji kumuona babu.
SELE: Tusa, tafadhari naomba unielewe. Twende Mbeya tutakuwa salama zaidi, Morogoro tutaenda mambo yakitulia.
TUSA: Sele, tafadhari usinichanganye. Huko Mbeya kuna tofauti gani ya Arusha na Mwanza? Kuchunwa ngozi hukohuko, kupiga nondo na matukio yote ya ajabu halafu unipeleke mimi Mbeya! Nishakwambia siendi popote zaidi ya Morogoro kwa babu.
SELE: Ubishi hauna faida Tusa, basi chagua mkoa unaoupenda zaidi ya Moro.
TUSA: Nishakwambia siendi popote zaidi ya Morogoro, kwanza wewe ndo chanzo. Usinichanganye sasa, unataka twende wote Moro hutaki baki Dom au uende hiyo mikoa yako ya ajabu.
Kwavile Sele alimpenda sana Tusa ikabidi akubaliane nae na hakutaka kumuona anaangamia.
Walipoona wale wanajeshi wameondoka wakaenda kupanda busi la kwenda Morogoro.
Marium akajiandaa kwaajili ya kwenda kumuona Deborah.
Akahitaji kwenda na Tina ili akamfahamu mdogo wake.
YUDA: Mmh! Mama, Tina muache achangamke kwanza halafu ndio utaenda nae.
MARIUM: Ila nilitaka akamfahamu mdogo wangu.
YUDA: Mama usijali, atamfahamu tu muda ukifika. Ila kwasasa muache hapa abaki na mimi.
MARIUM: Eti Tina, nikuache?
TINA: Usijali mama, nitaenda siku nyingine.
MARIUM: Sawa basi mbaki salama.
YUDA: Sawa mama, na wewe nenda salama.
Marium akaondoka kwaajili ya kwenda kwa Deborah.
Adamu alipokuwa anamuelezea Mashaka kuhusu matatizo yake, Mashaka akahisi moja kwa moja undugu uliopo kati ya Fausta na Adamu.
MASHAKA: Inamaana huyo Fausta ni ndugu yako?
ADAMU: Ndio, ni dada yangu kabisa.
MASHAKA: Halafu umesema kuwa Pamela ni mkeo?
ADAMU: Ndio ni mke wangu.
Mashaka akajikuta na maswali, kwani ajuavyo yeye ni kuwa Fausta na Pamela ni ndugu, sasa anamshangaa Adamu kusema kuwa mmoja na dada yake na mwingine ni mke wangu.
MASHAKA: Rafiki, pombe ulizokunywa zimekupeleka vibaya nini?
ADAMU: Kwanini?
MASHAKA: Yani ni kweli kabisa hayo maelezo uliyonipa?
ADAMU: Ndio ukweli mtupu huo.
Mashaka akahisi maelezo anayopewa na Adamu si sahihi, akafikiria labda watu anaowataja ni wengine.
MASHAKA: Itabidi ujiandae kurudi kwako.
ADAMU: Leo sirudi labda kesho, siwezi kulala nyumba ya mwanamke mimi.
MASHAKA: Hakuna tatizo basi, tushakuwa marafiki tayari. Utaenda kulala nilipofikia halafu kesho nitakusindikiza ulikofikia.
Mashaka aliamua kufanya hivyo ili apate kugundua ukweli wa maneno.
Patrick alifika karibia na kwao ila akasita kwenda kwani alijua wazi kuwa mama yake atamzuia kutoka wakati yeye bado alikuwa na mipango yake, na kikubwa alitaka kwenda kumjulia hali Tina, binti aliyemuokoa ili kujua maendeleo yake. Na ikiwezekana nae amlete kwao.
Akamwambia Fausta ashuke kwenye ile pikipiki na kumuelekeza.
PATRICK: Umeona ile nyumba yenye rangi ya maziwa?
FAUSTA: Ndio nimeiona.
PATRICK: Basi nenda pale waambie kuwa Patrick ndio ameniambia nije hapa, pale kuna mama yangu na mke wangu. Watakupokea vizuri tu hata usijali.
FAUSTA: Kwanini tusiende wote?
PATRICK: Usijali, mi nitakuja tu ngoja nikamalizie mambo flani kidogo halafu nitakuja.
Fausta akashuka na kutembea taratibu, kila alipokuwa anakwenda ndipo kumbukumbu zilipoanza kumrudia.
Deborah na Pamela walikuwa wakimshangaa bi.Rehema kutoa machozi kwaajili ya Maiko.
DEBORAH: Mama mbona hatukuelewi?
REHEMA: (Huku akilia), mwanangu huyu.
Wote wawili walisema kwa mshangao "mwanao!! Kivipi?"
REHEMA: Huyu ni mwanangu, huyu ni mtoto niliyemtafuta kwa kipindi kirefu sana.
Mara wakamuona Fausta akiingia mlangoni, Pamela alipomuona dada yake alifurahi sana na kuenda kumpokea ingawa alikuwa na bandeji kichwani.
DEBORAH: Jamani Fausta, imekuwaje?
Fausta aliwaangalia kwa sura ya huzuni huku akilia tu.
Ni muda huo huo Maiko nae akazinduka.
Tusa na Sele walipokaribia Morogoro ikambidi Sele ampigie simu Yuda ili tu kumpa taarifa kwani aliona usalama wao ni mdogo sana.
Wakati Sele anazungumza na Yuda ni muda huohuo ambao Patrick alikuwa nyumbani kwa wakina Yuda kwaajili ya kumuona Tina.
PATRICK: Vipi Yuda kuna nini?
YUDA: Mmh! Sele anasema anatatizo.
PATRICK: Kwani yuko wapi?
YUDA: Ameenda Morogoro.
PATRICK: Ameenda kufanya nini?
YUDA: Sijui.
PATRICK: Basi atajijua mwenyewe.
YUDA: Ila yupo na Tusa.
PATRICK: Nini?
Patrick akapandwa na hasira za ajabu.
Sele na Tusa wakati wanashuka kwenye basi wakakuta wanajeshi kama kumi wapo pale stendi
Ni Rehema tu ndiye aliyekuwa akishughulika na Maiko kwani Pamela na Deborah walikuwa makini kuongea na Fausta.
Mara dada yake na Deborah akawasili na kuingia ndani, mtu wa kwanza kumuangalia ni yule Maiko aliyekuwa amekaa chini.
Marium alijikuta akienda pale chini na kumkaba Maiko bila hata ya kuwasalimia aliowakuta ndani.
MARIUM: Shetani mkubwa wewe, na lazima nikuue na wewe.
Marium alionekana kuwa na hasira sana dhidi ya Maiko.
 
SEHEMU YA 49

Marium alionekana kuwa na hasira sana dhidi ya Maiko.
Aliendelea kumkaba Maiko huku Rehema akimtoa ile mikono, Deborah na Pamela walipoona lile tukio walistaajabu sana haswa Deborah, alishangaa dada yake amemjulia wapi Maiko.
Fausta nae alipotazama kinachoendelea akajikuta akimkumbuka vilivyo Maiko, naye akaenda kwa hasira alizo nazo na kuanza kumshambulia Maiko.
Rehema aliwasihi sana wasimshambulie vile, ikabidi yeye ajikinge juu ya Maiko.
DEBORAH: Hivi mama kwanini wamzuia huyo shetani asipigwe?
REHEMA: Jamani huyu si shetani, ni mwanangu jamani.
DEBORAH: Mungu wangu, na mashetani nayo huwa yanazaliwa na binadamu!!
Fausta na Marium walikuwa na hasira sana dhidi ya Maiko, Rehema nae alizidi kumzuia mwanae asipigwe.
MARIUM: Jamani mnaumzuia huyo mtu asipigwe? Ngoja niwaonyeshe sasa.
Marium akainuka na kwenda jikoni, alipotoka alitoka na panga. Maiko akaona hili sasa ni balaa, ikabidi atumie ujasusi wake kukimbia eneo hilo.
Hata wote mule ndani walishangaa amewaponyoka vipi.
MARIUM: Na ningemchoma nimkatekate na nyama, shetani mkubwa.
PAMELA: Mmh!! Kweli yule ni shetani jamani.
DEBORAH: Tena ni shetani mwenye mapembe.
Rehema alijiinamia akitoa machozi tu kwani kama mama ilimuuma sana kuona mwanae anaitwa majina ya ajabu kiasi kile.
Patrick akiwa pale kwakina Sele, akamuamuru Yuda awapigie simu wakina Sele ili wapete maelekezo ya kutosha.
YUDA: Mko wapi sasa?
SELE: Tupo hapa stendi ya Morogoro na tumezungukwa na wanajeshi nadhani tutakamatwa maana hatuna pa kukimbilia.
YUDA: Wawakamate kwa kosa lipi?
SELE: Siwezi kueleza ila wakitukamata nadhani watatupeleka Singida kuna tukio tumefanya kwa mjeda mmoja.
YUDA: Mbona nashindwa kukueleweni kaka?
SELE: Kuna mjeshi mmoja anaitwa Mwita tumeharibu kwake, sasa huyu rafiki yake Hamisi na wajeshi wengine ndio wanatufatilia yani hapa......
Kabla hajamaliza kusema anachosema alisikika Tusa akipiga kelele na gafla simu ikakatika.
Patrick alisikia yote kwani simu iliwekwa sauta kubwa, Patrick alichukia sana kusikia vile na kujikuta akisema "Tusa!!"
YUDA: Kaka haya majanga sasa.
PATRICK: Lazima nikamuokoe Tusa.
YUDA: Kwa wanajeshi kaka!! Utamuokoaje? Na utajuaje alipo?
Patrick alikaa kimya na kutafakari huku akili yake ikimcheza vizuri.
Maiko alikimbia na kwenda hotelini moja kwa moja, ilikuwa ni usiku ila hakujali alienda kwenye chumba cha Mashaka kwanza.
Alipofika jambo la kwanza ni kwenda kumkaba Mashaka bila ya kujali mgeni wake mule ndani.
MAIKO: Niambie ukweli Mashaka, mama yangu yupo hai au amekufa?
MASHAKA: Usinikabe basi, hayo si mambo ya kukabana bhana. Kwani vipi?
MAIKO: Sielewi, ila leo nimemuona mama yangu kwa macho yangu haya mawili.
MASHAKA: Kwani wewe mama yako unamjua?
MAIKO: Ndio namjua, mama yangu namjua vizuri sana. Ni mwanamke mpole, mcheshi na mkarimu.
MASHAKA: Mama yako ni nani?
MAIKO: Hilo sio jibu la swali langu, nijibu kwanza Mashaka.
MASHAKA: Mbona wanikosea adabu Maiko! Mimi ni nani yako?
MAIKO: Unataka kujua wewe ni nani yangu eeh!! Subiri nikuonyeshe.
Maiko akatoka chumbani kwa Mashaka na kwenda kwenye chumba chake.
Adamu alibakia kaduwaa na pombe pombe zake.
ADAMU: Kwani kuna nini?
MASHAKA: Usijali rafiki, wewe pumzika tu.
ADAMU: Maana mmenitisha.
MASHAKA: Usiwe na shaka bhana.
Adamu akaendelea kulala kwani akili ya pombe bado ilimtawala.
Wakina Deborah ilibidi wamuulize vizuri bi.Rehema kuhusu Maiko.
DEBORAH: Unajua mama hata hatujakuelewa, kwani Maiko ni mwanao kivipi?
REHEMA: Yule haitwi Maiko, ni mwanangu Juma yule. Mtoto anayenitoa machozi sikuzote nikimkumbuka.
PAMELA: Inamaana huyo ndio pacha wa Adamu?
REHEMA: Ndio, niliwazaa mapacha siku ya Jumanne. Ndipo mmoja nikamuita Juma na mwingine Jumanne. Hata nashangaa hilo jina la Maiko limetokea wapi!
DEBORAH: Ila tu hushangai jina la Adamu limetokea wapi!! Ama kweli ni mapacha mmh!!
PAMELA: Jamani Deborah, kwani tupo kwenye marumbano hapa?
DEBORAH: Na wala sijarumbana ila nimeongea ukweli, Juma amekuwa Maiko na Jumanne amekuwa Adamu. Mapacha wasiofanana hao.
Fausta alikuwa akilia tu, ndipo Marium alipogundua kuwa yule ni Fausta.
PAMELA: Fausta, mbona unalia tu kwani yule shetani alikufanyeje?
FAUSTA: Yule alikuwa mume wangu.
Wote mule ndani wakajikuta wakistaajabu na kusema kwa mshangao.
"mume wako!!!"
Fausta aliendelea kulia huku akikumbuka matukio aliyofanyiwa na Maiko.
DEBORAH: Mmh! Mbona haya majanga jamani!!
REHEMA: Mungu wangu, huu ni msiba wa familia sasa.
Rehema nae aliendelea kulia kwani hakujua ni jinsi gani atafanikiwa kutatua hilo tatizo.
Patrick aliondoka usiku uleule kwani kila walipompigia tena simu Sele alikuwa hapokei, simu iliita tu bila ya kupokelewa.
Patrick akarudi alipokuwa amehifadhi vitu vyake na akajiandaa na kuianza safari ya usiku kwa usiku ili kesho yake imkutie Singida na ajue jinsi gani ya kufanya atakapofika huko.
Yuda aliyekuwa na hofu juu ya Patrick, akaamua kumpigia simu.
YUDA: Kuwa makini sana kaka, na ukumbuke hao ni wanajeshi.
PATRICK: Usijali.
YUDA: Siwezi kukuzuia kwavile wewe ukiamua kitu umeamua ila umakini ni wa muhimu sana ndugu yangu.
Patrick alikuwa na nia moja tu nayo ni kumuokoa Tusa.
Alipokuwa anasafiri na gari yake usiku ule, akakutana na majambazi njiani waliozoea kupora na kuwaibia watu usiku, majambazi yale huwa yanangoja mabasi ya abiria barabarani ili wapore mali za abiria na magari ya kawaida ili wapore magari hayo. Ila Patrick alikuwa ni makini sana kwani kashapitia maovu mengi.
Akawaona njiani wakisimamisha gari yake, alichofanya ni kupunguza mwendo halafu akatoa bastola yake na kuwapiga majambazi wawili waliokuwa wanamsimamisha halafu akamwamuru yule jambazi aliyebaki kutoa mawe waliyoyapanga barabarani. Yule jambazi akaona kweli wamepatikana safari hii kwani walikutana na jambazi mwenzao, alipangua yale mawe na kumuacha apite.
Patrick aliporudi kwenye gari yake, akachukua bastola yake na kummalizia yule jambazi aliyebaki halafu akaendelea na safari.
Tusa na Sele walikuwa kwenye mikono ya wanajeshi, na yote ilitokana na kelele alizopiga Tusa kwani zilifanya wajulikane ni wapi wamesimama.
Sele alikuwepo kumtetea Tusa ila juhudi zake ziligonga mwamba na wote wawili kukamatwa kwani wanajeshi walikuwa kumi pale stendi.
Tusa aliendelea kupiga kelele baada ya kukamatwa, kitendo kilichomfanya apigwe vibao vingi na wale wanajeshi waliokuwa na hasira.
Wakawapakia kwenye gari yao na safari ilikuwa ni kuelekea Singida. Kwani muda ambao Sele na Tusa walitoroka, ni muda huo Hamisi alirudi tena kwa Mwita na kumuona akitapatapa na kuvuja damu nyingi, ikabidi amuwahishe hospitali ambapo alipopata nafuu kidogo akasema kuwa waliomfanyia hivyo ni Tusa na Sele, kwavile Hamisi alishawaona alikuwa ameshika sura zao vilivyo, na Mwita aliwaambia kuwa watu hao walikuwa na mpango wa kwenda Morogoro, kitendo hicho kiliwafanya wale wanajeshi kuzingira kila kituo cha basi Morogoro ili kukagua abiria wanaoshuka. Na kama wanajeshi walivyo na ushirikiano hiyo haikuwa kazi ngumu hata kidogo kwao, kwani walishapata maelekezo ya kutosha juu ya jinsi walivyo Sele na Tusa.
Hawakutaka kuchelewesha wakati, walisafiri nao jioni ile ile ili wawahi kufika nao Singida.
Ingawa Sele alikuwa amefungwa kamba vya kutosha ila nae alikuwa na mipango ya kumuokoa Tusa, alikuwa anaona bora yeye afe kuliko Tusa.
Maiko akarudi kwa Mashaka na picha ndogo mkononi yenye watoto wawili.
MAIKO: Haya mtambue mwanao hapo?
Mashaka alishika zile picha na kuziangalia kwa makini sana.
MASHAKA: Wewe ndio mwanangu Maiko.
MAIKO: Punguani kabisa wewe, hata mwanao humjui. Mimi sio mwanao Mashaka.
MASHAKA: Unasemaje Maiko?
MAIKO: (Akacheka sana), ulijiona mjanja eeh!
MASHAKA: Mbona sikuelewi Maiko?
MAIKO: Mwanao ulimuua kwa mikono yako mwenyewe bwege wewe, si ulisema kuwa alikuwa mzembe mzembe? Na uchizi wako toka milembe.
MASHAKA: Sikumuua mwanangu, niliyemuua ni Juma.
MAIKO: (Akacheka tena), kwa taarifa yako mimi ndio Juma. Huyo mwanao Maiko ulimuua mwenyewe. Mimi ndio mtoto niliyekuwa mjanja bhana.
Mashaka akampokonya ile picha Maiko, kumbukumbu zikamjia akapatwa na gadhabu kubwa sana, iliyopelekea yeye na Maiko kuanza kupambana mule ndani.
Patrick aliingia ndani ya Singida, alipomuona mwanajeshi akavutiwa nae na kupenda kufahamiana, mtu yeyote akikutana na Patrick hawezi kusita kuzungumza nae kwani alikuwa na kauli za kuvutia sana. Baada ya salamu na maneno mawili matatu, akaanza kujitambulisha.
PATRICK: Samahani kaka, naitwa Patrick sijui mwenzangu unaitwa nani?
MJESHI: Aah! Upo na Hamisi hapa ndugu yangu.
Patrick aliposikia hilo jina hakutaka kujua zaidi kama ndio Hamisi huyu au mwingine ila aliamua kushughulika na huyu kwanza.
 
SEHEMU YA 50

Patrick aliposikia hilo jina hakutaka kujua zaidi kama ni Hamisi huyu au mwingine ila aliamua kushughulika na huyu kwanza.
Alianza kumvuta vizuri Hamisi ili aweze kupata uelekeo.
PATRICK: Dah! Nina rafiki yangu mwingine naye ni mwanajeshi, yani nimemkumbuka balaa ila sijui anapoishi.
HAMISI: Anaitwa nani?
PATRICK: Anaitwa Mwita.
HAMISI: Dah! Namjua huyo ni rafiki yangu pia. Yupo anauguza kidonda alichochomwa kisu.
PATRICK: Kachomwa kisu!! Mungu wangu, hebu Hamisi nipeleke nikamuone.
Hamisi akaanza safari ya kumpeleka Patrick nyumbani kwa Mwita.
Adamu alikuwa akisikilizia ugomvi wa Maiko na Mashaka kwakweli maneno yao yakamchanganya na yeye.
MASHAKA: Haya, huyo mama yako unayejivunia ni nani?
MAIKO: Ni dada yako Rehema, kichwa hiki kina kumbukumbu zote wewe. Usinitanie hata kidogo.
Kwakweli Mashaka aliishiwa uelewa na alijuta kwenda Mwanza na Maiko.
MASHAKA: Mmh! Maiko basi yaishe mwanangu.
MAIKO: Achana na mimi kabisa, ngoja niangalie ustaarabu wa kumpata mama yangu tu hapa.
Maiko akaamua kutoka, ndipo Adamu nae alipoinuka na kumfata Maiko kwa nyuma kwani alishindwa kumuelewa.
Mashaka alikaa chini huku akitawaliwa na mawazo kwenye akili yake.
Tina alikuwa amebaki na Yuda nyumbani.
TINA: Yuda, mbona nilikuwa siwaelewi. Mlikuwa mnamtaja Tusa Tusa, huyo Tusa ndio Tusa yupi?
YUDA: Ni Tusa ndugu yako.
TINA: Kapatwa na nini? Na je hapa Mwanza alikuwa anaishi wapi?
YUDA: Ametoroka na Sele, kwa hapa Mwanza alikuwa anaishi kwa mamdogo alipoenda mama.
TINA: Tafadhari naomba unipeleke.
YUDA: Mama mwenyewe hajarudi hadi leo hata sijui kuna nini.
TINA: Nipeleke hivyo hivyo bhana.
Yuda akaamua kujiandaa na Tina ili kwenda nae nyumbani kwa Deborah.
Sele na Tusa walikuwa kwenye mateso ya wanajeshi, watu hawa hawakuwa na huruma hata kidogo. Waliwatesa kama vile si binadamu, kwakweli wanajeshi huwa wanafanya mambo ya kikatili sana.
Wakati wa yale mateso, Tusa akaanza kuugulia tumbo, aliwaambia ila hawakumsikiliza.
Tumbo lilimuuma sana Tusa, kwakweli Sele alimuonea huruma sana. Akamuita mjeshi mmoja ili kuzungumza nae.
SELE: Tafadhari nawaomba, adhabu zote za huyu mwanamke nipeni mimi. Nitafanya pamoja na adhabu zangu.
Yule mjeshi akacheka sana na kuwaita wenzie kisha akamwambia
"hebu sema tena"
SELE: Nipeni mimi adhabu zote, mwachieni Tusa. Tazama anavyoteseka, muoneeni huruma jamani.
MJESHI: Je, yeye aliona huruma kumchoma Mwita kisu?
SELE: Ile ilikuwa ni gafla ukizingatia alikuwa amezimia, tafadhari nawaomba mmuhurumie.
MJESHI: Ngoja nikwambie kitu rafiki, sisi wanajeshi kwetu huruni ni no tena big NO. Hakuna kumuhurumia mtu, ni adhabu kwenda mbele hadi muonje mauti. Nyie si mnajifanya wababe? Hapa huwa hatuwafungulii kesi watuhumiwa, hapa ni adhabu tu.
Sele alijitahidi kuwasihi lakini hawakukubali.
Tusa aliendelea kuumwa na tumbo huku damu nyingi zikilowanisha gauni lake.
Patrick na Hamisi walifika nyumbani kwa Mwita ila hawakumkuta.
HAMISI: Sijui kaenda wapi huyu mgonjwa? Au kaenda kuwatazama wale watuhumiwa!
PATRICK: Watuhumiwa! Inamaana waliomchoma kisu mnawajua?
HAMISI: Tumewakamata kabisa, unajua wanajeshi huwa tunauwezo mkubwa sana wa kucheza na akili za watu. Eti walikuwa wanakimbilia Morogoro, yani huko huko tukawatia mbaroni.
PATRICK: Mmh! Kwani ni wengi sana?
HAMISI: Wawili tu, ni mwanamke na mwanaume.
PATRICK: Sasa kati yao nani aliyemchoma kisu Mwita?
HAMISI: Ni mwanamke ndo kamchoma Mwita, ila wote wanapata adhabu kwakuwa wameshirikiana kutoroka.
PATRICK: Unaonaje tukiwafata huko eneo la tukio, ujue nimemkumbuka sana Mwita.
HAMISI: Aah! Tuwangoje bhana. Kule atakupeleka Mwita mwenyewe.
Patrick alikuwa anaichezesha akili yake jinsi ya kuwaingia iawa wajeda kwani alijua lazima watakuwa wengi tu.
Akajisemea kimoyomoyo.
"maisha ya Tusa yapo mikononi mwangu. Huyu ni mke wangu lazima nimkomboe. Mmh! Sele nae ni ndugu yangu, siwezi kumuacha na hawa bora nimtoe hapa nikamshughulikie mwenyewe"
Patrick aliwaza mengi huku akimngoja huyo Mwita kujua ni mtu wa aina gani na vile vile kujua jinsi gani ya kumuingia.
Akaona ni vyema amgeleshe yule Hamisi kwa kuondoka ila badae arudi mwenyewe na akutane yeye na Mwita tu.
PATRICK: Nimechoka kungoja hapa nje, ngoja nirudi kupumzika. Kwavile nishakujua nitarudi tena badae.
HAMISI: Basi ngoja tuondoke wote, maana na mimi nataka kwenda kwangu mara moja.
Patrick akaondoka na Hamisi kwa lengo la kumgelesha tu.
Fausta aliendelea kulia na kubembelezwa na wote.
DEBORAH: Nyamaza Fausta, yule Maiko ni shetani kila mmoja analijua hilo. Utaumia zaidi ukizingatia tayari una majeraha mengine ndugu yangu.
MARIUM: Hivi, mnajua kama yule ndio aliyemkata kichwa mume wangu?
PAMELA: Mungu wangu, nyie yule Maiko ni gaidi kweli. Yani alimkata kichwa?
MARIUM: (Akiongea huku machozi yakimbubujika), yani alimchinja huku na mimi nikishuhudia kwa macho yangu haya mawili, halafu akaondoka na kichwa chake na kuniachia mwili wake tu.
FAUSTA: Mimi je, alimkatakata mwanangu vipande vipande kama nyama buchani. Inaniuma sana tena sana, Maiko ni gaidi tena wa kishetani.
Walikuwa wakilia na kuomboleza huku Pamela akiwabembeleza kwani Deborah nae alikumbuka matukio aliyofanyiwa na Maiko na kujikuta akilia kwa uchungu.
Rehema nae aliomboleza sana baada ya kusikia matendo aliyoyafanya mwanae mwenyewe.
Yuda na Tina walipofika mlangoni mwa nyumba hiyo walishangaa kuona kilio kimetawala hadi wakapatwa na hofu kuwa huenda kuna msiba.
Maiko alipoingia chumbani mwake alimuona Adamu nae akimvamia bila hodi.
MAIKO: Unataka nini wewe?
ADAMU: Nahitaji kuzungumza na wewe.
MAIKO: Sina muda huo, nakuomba utoke humu ndani.
ADAMU: Tafadhari naomba unisikilize.
MAIKO: Toka kabla sijatenda dhambi tena.
ADAMU: Nisikilize kwanza basi.
MAIKO: (Akiongea kwa ukali) nishakwambia sina muda huo, nakuamuru utoke humu ndani.
ADAMU: Kutoka nitatoka ila naomba unisikilize kwanza.
MAIKO: Wewe ni mbishi eeh! Haya kwa mara ya mwisho toka. Nahesabu hadi tatu uwe umetoka. Moja... Mbili.... Tatu.... Hujatoka eeh ngoja sasa.
Adamu alikuwa kaganda pale pale akimshangaa huyu Maiko na matatizo yake.
Maiko akainama kwenye begi lake na kuchukua bastola kisha akamlengeshea Adamu.
Mwita aliporudi tu nyumbani kwake, Patrick nae alikuwa mitaa ile ile.
Akaenda kugonga mlango, Mwita akamfungulia bila hofu yoyote kwani alijua ni wenzie.
Ile kufungua tu, Patrick alikuwa tayari na bastola mkononi akamnyooshea Mwita, nae Mwita alipomtazama vizuri akamwambia.
MWITA: Aah! Patrick, tusifanyiane ubaya bhana.
PATRICK: Kumbe Mwita ndio wewe?
MWITA: Ndio mimi bhana Patrick.
Patrick alishangaa kuona kuwa Mwita ni mtu anayefahamiana nae.
 
Simulizi Zinazorushwa na BURE SERIES

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi

4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)

💥 💥 💥NEW 💥💥💥

8. RIWAYA: Mume Gaidi

Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Mume Gaidi

9. STORY: Sitaki Tena

Bonyeza hapa chini kusoma
STORY: Sitaki Tena

10. Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)

Bonyeza hapa chini kusoma
Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)
 
SEHEMU YA 51


Patrick alishangaa kuona kuwa Mwita ni mtu anayefahamiana nae.
Patrick akashusha bastola chini ili apate kuzungumza nae.
MWITA: Mbona hivyo ndugu yangu kunijia na bastola?
PATRICK: Unajua nini? Mimi nimekuzoea wewe kwa jina la Frank kumbe na Mwita ni jina lako?
MWITA: Ndio bhana, mi naitwa Frank M. Mwita na huku wamezoea kuniita jina la mwisho yani hili la Mwita.
PATRICK: Sawa sawa, kwanza nashukuru kuwa tunafahamiana. Nadhani kazi yangu itakuwa nyepesi.
MWITA: Kazi gani hiyo?
PATRICK: Kwanza niambie Tusa na Sele wamekufanya nini?
Mwita akaeleza ilivyokuwa jinsi Sele alivyorudi na kuanza kupambana nae hadi pale alipochomwa kisu na Tusa.
PATRICK: Unataka kuniambia Tusa alikuchoma kisu tu bila sababu?
MWITA: Si aliona nimemkaba Sele ndomana akanichoma.
PATRICK: Haya, mi nataka kitu kimoja tu hapa Frank.
MWITA: Kitu gani?
PATRICK: Namtaka huyo Tusa na Sele.
Mwita akashtuka na kuuliza,
MWITA: Sasa mimi nitawatoaje ilihali nishawaamuru wajeshi wenzangu wawafanye watakavyo?
PATRICK: Nadhani unanijua vyema Frank, sitaki kutumia nguvu tusije tukaumizana bure hapa. Ukinisaidia hilo jambo, nami nitakusaidia lile swala lako la baba yako.
MWITA: Kweli Patrick?
PATRICK: Huu ni ukweli, huwa sina ahadi za uongo mimi.
MWITA: Ngoja basi tutafanya kitu flani hivi. Kwani wewe ni nani zako hao?
PATRICK: Nitakwambia tu usiwe na shaka.
Ikabidi Mwita aamue kwenda na Patrick eneo la tukio, akapanga kwenda nae kesho yake kwani siku hiyo usiku ulishaingia.
Maiko aliendelea kumnyooshea bastola Adamu, na kuendelea kumuamuru atoke.
Ila Adamu hakutoka, aliendelea kung'ang'ania kuongea nae, Maiko akajaribu kufyatua risasi ili kumtishia, na ile risasi ikampata Adamu begani na kujikuta akianguka huku akisema,
"Umeniua Jumaaaa"
Maiko akajikuta akishtuka na kumfata Adamu pale chini ambapo alikuwa akitokwa na damu nyingi, ikabidi amchukue na kumpakiza kwenye gari na kumpeleka hospitali.
Kwakweli Maiko alikuwa hajielewi kabisa na alifanya vitu bila hata ya kufikiria.
Akawa anajiuliza kuwa yule mtu kwanini aseme umeniua Juma, au amesikia maongezi yake na Mashaka? Alijiuliza sana ila alikuwa anaombea apone tu ili aweze kumuuliza, alijilaumu sana kwa kitendo chake cha hasira na kukumbuka kuwa kweli hasira hasara.
Yuda na Tina waliingia ndani kwa Deborah ila hofu yao kubwa ni kuwa kuna msiba.
Walipoingia wakawaona hawa wanawake wa humu wote wakilia na kuomboleza. Yuda akaamua kuuliza,
"Kuna nini jamani?"
wakajikuta wakinyamaza na kuangalia watu walioingia ndani, ndipo walipomuona Tina na Yuda.
Tina kwanza hakuamini kuonana tena na familia yake, mama yake aliinuka na kumkumbatia mwanae kwa machozi.
FAUSTA: Jamani mwanangu, ulikuwa wapi siku zote?
Tina nae akaanza kulia.
TINA: Nilitekwa mama.
DEBORAH: Mmh! Jamani, naona hii Mwanza imeharibika sasa hadi nashikwa na hofu mwenzenu. Pamela alitekwa, Fausta alitekwa kumbe na huyo Tina nae alitekwa mmh!
REHEMA: (Akawa kama mtu aliyeshtuka usingizini), jamani Adamu!!
PAMELA: Kwani nae yuko wapi?
DEBORAH: Alienda kuripoti kupotea kwenu na ndio hajarudi hadi leo. Inamaana nae katekwa?
REHEMA: Mungu wangu, tutafanyaje sasa?
Yuda alikuwa akiwasikiliza tu huku nae akijiuliza anayefanya huo utekaji ni nani? Na kwanini atoke familia moja tu? Alikosa jibu kabisa kwani hakufikiria kama Maiko na Mashaka watakuwa wanahusika kwa wote.
Mashaka alijiona kuwa atakuwa amepoteza kila kitu asipofanya kitu.
"Yani Maiko amenidanganya mimi? Yani siku zote hizi amekuwa akicheza na akili yangu? Inamaana akili yangu imepoteaje hadi nimsahau mwanangu mwenyewe? Inamaana Rehema yuko hapa Mwanza au Maiko amemuonea wapi? Lazima nifanye kitu, lazima nifanye kabla ya Maiko. Ngoja nikanywe kwanza ili akili ikae sawa"
Mashaka akaenda kununua konyagi za kumtosha kulewa ili anywe hadi alale kabisa na akiamka afanye analotaka kufanya.
Tusa na Sele walikuwa katika wakati mgumu bado, Tusa aliendelea kumwaga damu iliyotoa harufu kama kitu kilichooza.
SELE: Pole Tusa ila ungenisikiliza yote haya yasingetupata.
Tusa hakuweza hata kuzungumza kwa maumivu ambayo alikuwa akiyapata.
Alishindwa kabisa kuendelea na adhabu, akawa ameanguka chini. Wanajeshi wasio na huruma walikuwa wakimburuta Tusa.
Wakati wanajeshi hao wawili wakiendelea kumburuta Tusa wakamuona mbele yao Mwita na mtu mwingine ambaye ndio Patrick.
Patrick alipowaona akawapigia makofi sana,
PATRICK: Vizuri sana, huo ndio uanajeshi kwakweli mnastahili pongezi.
Wale wanajeshi wakafurahi sana na kuendelea kumpiga mateke Tusa aliyekuwa ameshindwa hata kutoa tena sauti ya kilio, Sele aliangalia lile tukio na kuumizwa sana moyo wake.
MWITA: Umeona kazi yao eeh! Wengine wapo kwa yule kijana.
PATRICK: Ila mimi nimewapenda hawa, jamani muacheni huyo dada hapo chini. Nyie wawili jioni nitawapa ofa.
MJESHI 1: Dah! Hiyo sitakosa bhana, utushtue basi.
PATRICK: Ngoja tupeane mawasiliano basi.
Patrick akachukua namba za simu za wale wajeshi ambao walikuwa wakimtesa Tusa huku wakifurahia.
PATRICK: Mwacheni huyo dada basi.
MJESHI 2: Wa nini sasa huyu?
MWITA: Nataka nikadeal nae.
Wakamuacha pale chini ambapo Mwita alimuamuru mjeshi mwingine amchukue na kumpakiza kwenye gari, mjeshi huyo aliyeitwa Musa alimbeba Tusa na kumtupia kwenye gari.
PATRICK: Kwakweli nimependa sana kazi yako kaka, na wewe jioni uje kwenye ofa.
Naye alifurahi na kupeana mawasiliano na Patrick.
Wakabaki wengine wawili ambao hawakupata ofa, ikabidi waonyeshe ujuzi wao kwa Sele, wakawa wanampiga na kumpondaponda kila mahali. Mwita akawaamuru wamuache halafu nae akapakizwa kwenye gari.
Patrick akawageukia wale na kuwaambia nao kuwa jioni ofa, akachukua na mawasiliano yao.
Maiko aliendelea kushughulika na Adamu pale hospitali, kwavile alikuwa na pesa basi kila kitu kikaenda kama anavyotaka yeye. Nia yake kubwa ikawa ni kumuona Adamu akiwa mzima ili apate kuzungumza naye.
Adamu alipoanza kufumbua macho Maiko alifurahi sana, alihitaji majibu ya maswali yake. Hakutaka kumpoteza mtu huyu tena, ukizingatia alimkuta na Mashaka akajua lazima kuna mambo mengi anayoyajua kuhusu yeye.
Hali za Tusa na Sele zilikuwa mbaya sana hasa Tusa ambaye alipoteza fahamu kabisa, kitu cha kwanza alichofanya Patrick ni kuwakimbiza hospitali.
Akawaacha wakihudumiwa pale hospitalini na yeye akarudi kwa Mwita.
MWITA: Mbona umewapongeza wale wanajeshi halafu bado umeenda kutupa pesa ya matibabu kwa Tusa na Sele?
PATRICK: Nimewapongeza kwasababu wamefanya kazi nzuri sana, na wale nimewapeleka hospitali kwavile nao nawahitaji wakiwa hai.
Mwita hakuwa na wasiwasi wowote na Patrick kwani aliujua vizuri ukatili alionao Patrick kwahiyo alihisi amewapongeza kwa nia njema, na kweli jioni hiyo aliwaita wale wanajeshi na akawanywesha sana pombe huku wakifurahia siku yao kuwa poa, hakuna hata mmoja aliyejua Patrick ana lengo gani nao.
PATRICK: Kesho tena nitawapa ofa.
MUSA: Dah! Wee jamaa uko poa sana yani. Sisi ni makomando, vijitu kama vile huwa tunapiga hadi kufa.
PATRICK: Hapo ndio ninapowapendea wanajeshi, kazi nzuri sana. Nitakuwa nawapa ofa hadi nitakapoondoka Singida.
Wote wakafurahi sana kwa ofa walizopewa na Patrick.
Ikabidi Yuda nae aamue kufanya kitu kama mwanaume maana akaona kukaa tu na wanawake hakutamsaidia chochote.
Sasa aliamua kwenda kuzunguka mjini ili kujua kama kweli Maiko na Mashaka wameondoka au la.
Safari yake ilianzia moja kwa moja kwenye hoteli ambayo Tina alimuelekeza kuwa alifikia mwanzoni.
Kufika kule aliweza kugundua vitu baadhi kwani alipata kujua uwepo wa mtu aliyepigwa risasi ndani ya hoteli hiyo ila huyo mtu na aliyepigwa hawakujulikana walipo.
Wakati anasikiliza hayo maelezo mara akamuona Mashaka kwa mbali, akaamua kumfatilia.
Mashaka alishapanga vitu vyake kwenye akili yake, na kitu cha kwanza aligundua hospitali ambayo Maiko amempeleka Adamu, Mashaka aliamua kwenda kwani alijua kuwa lazima kuna kitu kilichofanya hadi Maiko ampeleke Adamu hospitali kwani Maiko hakuna na roho ya kumuhurumia mtu hata siku moja.
Mashaka akaingia chumba alicholazwa Adamu, kabla hajafanya chochote akamuona Yuda nae ameingia humo.
 
SEHEMU YA 52


Mashaka akaingia chumba alicholazwa Adamu, kabla hajafanya chochote akamuona Yuda nae ameingia humo.
Wakawa wanatazamana sasa, Mashaka hakuelewa kwanini Yuda amemfata kwenye mishe zake kama zile.
Ikabidi atoke nje na kumpita Yuda pale mlangoni, Yuda nae akamfata Mashaka nje.
MASHAKA: Kijana, nini unataka kutoka kwangu?
YUDA: Hakuna ninachotaka.
MASHAKA: Sasa mbona wanifatilia? Naomba kaa mbali na mimi, nitakupoteza.
YUDA: Siku yako inakuja ya wewe kupotezwa.
Mashaka akamtazama Yuda kwa jicho kali sana, akatamani hati ampige makofi ila akaona hawapo sehemu nzuri ya kufanya hivyo ukizingatia kuwa Yuda nae ni kijana mwenye fujo.
Yuda akamuangalia Mashaka anavyoondoka, ila akavutwa zaidi kwenda kumtazama yule mgonjwa aliyefatwa na Mashaka.
Alipoingia wodini safari hii akamkuta Maiko akiwa pale kwa mgonjwa. Kwakweli Yuda alishindwa kuelewa kabisa kuwa Mashaka na Maiko wana nini na huyo mgonjwa.
Nyumba ya Deborah ilikuwa kama vile nyumba ya wanawake wenye huzuni na waombolezaji.
REHEMA: Kwakweli nashindwa kuelewa jamani, hivi kwanini mwanangu Juma akajiita hilo jina la Maiko?
DEBORAH: Mama, usimlaumu sana huyo Maiko. Sote hapa tunajua kuwa huyo Maiko ni shetani. Swala linakuja kwa huyu mwanao mwadilifu Jumanne, kwanini alibadili jina na kujiita Adamu?
PAMELA: Debo, hapa tunamuongelea Maiko, sasa Adamu anaingiaje hapa?
DEBORAH: Pamela huelewi na huwezi kunielewa. Nimeishi na Jumanne akiwa anaitwa Jumanne, iweje akabadili jina kwako. Au mlitaka kuficha maovu yenu Pamela?
PAMELA: Najua shida yako ni kunikandamiza mimi, nilishakuomba msamaha ila hutaki kunielewa Deborah. Tuongee ya msingi tu hapa, tumuongelee huyo Maiko.
DEBORAH: Sikia Pamela, nimeishi na Jumanne na nimeishi na Maiko. Uchungu niupatao sasa moyoni mwangu huwezi kuudhania wewe.
REHEMA: Inamaana wote umeishi nao kama mke?
DEBORAH: Ndio ila kwa wakati tofauti.
REHEMA: Mungu wangu, mbona mimi sielewi kitu jamani. Mbona naona kizunguzungu?
DEBORAH: Mama sikiliza nikwambie, huu muda ni wa kutuliza akili ili ijulikane ni wapi palipokosewa. Yote haya chanzo chake ni kutokufahamiana. Mimi sikujua kama Maiko ni ndugu wa mume wangu wa kwanza. Maiko ni shetani mkuu halafu huyo Adamu atakuwa msaidizi wake.
FAUSTA: Mnajua hata mimi nimechanganyikiwa hapa, kama Maiko ni ndugu wa Adamu inamaana Maiko ni ndugu yangu pia, Deborah ni mke mwenzangu. Yani nilizaa na ndugu yangu? Hapana, kwanini huyo Juma asiwe mtu mwingine zaidi ya Maiko?
Fausta akawa analia.
PAMELA: Naona hapa kila mtu ana msiba wake, na kilio kikubwa ni Maiko mmh!
DEBORAH: Ndio, hapa kila mtu ana msiba wake kasoro wewe Pamela.
REHEMA: Mabishano si mazuri jamani, yote haya yataisha siku moja.
Maelewano ya Pamela na Deborah tangia ujio wa kina Adamu yalikuwa hafifu sana kwani walikuwa watu wa kutupiana maneno tu.
Patrick alienda kuwatizama Sele na Tusa hospitali ambapo Sele alikuwa akiendelea vizuri, ila Tusa hali yake haikuwa nzuri.
Daktari akamwambia Patrick kuwa Tusa alikuwa mjamzito ila mimba yake imetoka kutokana na misukosuko, Patrick roho ilimuuma sana kwani alijua wazi kuwa ile mimba ilikuwa yake. Upande mwingine alimlaumu Sele kwa kumchukua mkewe bila ruhusa ila aliwalaumu zaidi wale wanajeshi waliomtesa Tusa kwani alijua ndio wamesababisha yote yale.
Akamfata Sele ambaye alikuwa anaendelea vizuri na kuongea nae.
PATRICK: Hivi wewe ndugu yangu, kilichokutuma kutaka kuondoka na mke wangu ni nini?
SELE: Hatukuwa na nia mbaya Patrick ila Tusa aliitaji kumuona babu yake.
PATRICK: Kwanini msingesubiri mimi nirudi? Ngoja Tusa apate nafuu, nitawasafirisha wewe na yeye mrudi Mwanza. Sasa ole wako umtoroshe tena, nakuhakikishia kichwa chako nitakitenganisha na mwili. Watu husema mchawi mpe mtoto akulelee, sasa mimi nitakukabidhi Tusa urudi nae Mwanza. Sawa.
Sele aliitikia kwa kichwa huku moyoni akiumia kwani aliona akiteswa na mapenzi aliyonayo kwa Tusa.
Adamu nae alikuwa anaendelea vizuri na hiyo ikawa furaha kwa Maiko.
Maiko aliondoka pale hospitali na Adamu akaenda nae sehemu aliyofikia, Yuda sasa akaanza kufatilia nyendo zote za Maiko ili kujua anapojificha.
Maiko alimuomba msamaha Adamu aliyekuwa na bandeji kwasasa,
MAIKO: Hasira zilinifanya nifanye yale, nisamehe kwanza.
ADAMU: Hakuna tatizo ndugu yangu.
MAIKO: Eeh! Niambie, ulijuaje kuwa mimi naitwa Juma?
ADAMU: Sikia ndugu yangu, wakati unaongea na yule baba nilisikia vizuri maelezo yako kuwa mama yako anaitwa Rehema si ndio?
MAIKO: Ndio ni kweli?
ADAMU: Hata mimi mama yangu anaitwa Rehema, halafu mimi jina langu lingine ni Jumanne. Nilipokusikia nikahisi labda wewe ni pacha wangu ambaye mama aliniambia kuwa yupo Mombasa na anaitwa Juma.
MAIKO: Mmh!! Kwakweli sijui chochote, inawezekana ni kweli.
ADAMU: Kwani wewe mama yako ulimkutia wapi hapa Mwanza?
Maiko akamuelekeza Adamu nyumbani kwa Deborah.
ADAMU: Basi huyo huyo ndio mama yangu.
Maiko hakuamini wala kuelewa kwavile alichojua yeye ni kuwa hana ndugu kabisa. Ikabidi aongee na Adamu na wapenge jinsi atakavyomkutanisha tena na bi.Rehema.
Deborah aliamua kumuita Pamela pembeni ili apate kuzungumza nae.
DEBORAH: Pamela wewe ni rafiki yangu sana, kiukweli sipendi tunavyorumbana. Hebu tuongee ya maana sasa.
PAMELA: Nakusikiliza Debo.
DEBORAH: Hivi kwa mara ya kwanza kabisa Patrick alivyokuleta hapa, ulikuwa umetoka nae wapi?
Pamela akamsimulia Deborah jinsi alivyotekwa na wakina Maiko hadi kuja kuokolewa na Patrick.
PAMELA: Kwakweli Deborah, mtoto wako Patrick ni mtu mzuri sana.
DEBORAH: Inamaana Patrick anajuana na wakina Maiko?
PAMELA: Itakuwa maana walikuwa wakimtajataja sana.
DEBORAH: Mmh! Kazi ipo. Patrick atakuwa ameshaharibika tayari.
PAMELA: Kivipi Debo? Na hivi huyu Patrick ulizaa na nani?
DEBORAH: Mmh! Historia ndefu ila nitaisema Patrick akirejea. Kwanini umeniuliza hivyo?
PAMELA: Umempata mtoto shujaa sana Deborah, na mimi isingekuwa.....
Akaanza kulia, Deborah akambembeleza bila ya kujua anacholilia.
DEBORAH: Isingekuwa nini Pamela?
PAMELA: Mapenzi yaliniponza Debo, ingawa nimeolewa na Adamu ila kuna tukio ambalo kila nikifikiria halitaki kutoka kwenye akili yangu. Roho yangu inaniuma na kunisuta pia.
DEBORAH: Yote maisha na mapito, kuna wakati huwa tunafanya mambo bila kufikiri ila badae hugeuka na kuwa majuto, na ndio hapo kauli ya ningejua hutokea. Niambie nini tatizo ndugu yangu.
PAMELA: Nitakwambia Debo, inaniuma sana kwakweli.
Deborah alitulia kumsikilizia Pamela kitu ambacho anataka kusema.
Tusa alipopata nafuu kidogo, Patrick hakutaka kupoteza muda akafanya kama alivyopanga. Akawasafirisha Tusa na Sele warudi Mwanza ili Tusa akapate matibabu mengine kwenye mkoa wa Mwanza.
Patrick akaenda nyumbani kwa Mwita,
MWITA: Nilitaka nikutafute Patrick maana ahadi ni deni, nieleze basi kuhusu baba yangu.
PATRICK: Unamsema huyo baba yako Maiko?
MWITA: Ndio huyo huyo, kwakweli natamani kumfahamu.
PATRICK: Usijari utamfahamu.
MWITA: Anaishi wapi nimfate basi.
PATRICK: Anaishi Arusha ila nadhani kwasasa bado yuko Mwanza. Ukitaka tangulia Mwanza, nitakuja kuwakutanisha mfahamiane kabla sijafanya yangu.
MWITA: Yapi tena?
PATRICK: Ni siri ndomana nimesema yangu ingekuwa sio siri ningesema yetu.
MWITA: Sasa vipi huko Mwanza hatuendi wote?
PATRICK: Tangulia tu, mimi nataka nifike Manyoni mara moja halafu ndio nitaenda Mwanza moja kwa moja.
Mwita hakumuelewa Patrick anampango gani hapo Singida.
Sele aliposafiri na Tusa walienda vizuri ila walipokaribia kufika Tusa akazidiwa sana ikabidi ashuke na kumuwaisha hospitali, hali ya Tusa ilikuwa mbaya sana kiafya kwani alinyong'onyea na kunyorodoka zaidi.
Hawakuweza tena kufika nyumbani.
Matukio ya ajabu yakasikika Singida, wanajeshi wapatao wanne walikutwa wamechinjwa sehemu tofauti tofauti. Kila mtu alipatwa na mashaka, msako ukaanza kwa kumtafuta mtu anayefanya matukio ya kusikitisha kama yake.
Wakati kila mwananchi akiwa na hofu, Hamisi alienda kumtembelea Mwita kama kawaida yake. Leo hii aliingia ndani bila hata ya kugonga hodi kwaajili ya kumpa taarifa ya vifo vya wanajeshi hao.
Ile ameingia tu akamuona Patrick akiwa na kisu mkononi tena kisu kilicho kuwa damu nyingi.
 
SEHEMU YA 53


Ile anaingia tu mlangoni akamuona Patrick akiwa na kisu mkononi tena kisu kilichokuwa na damu nyingi.
Hamisi akapigwa na butwaa na kubakiwa na bumbuwazi,
HAMISI: Vipi tena Patrick?
PATRICK: Usishtuke Hamisi, njoo nikuonyeshe nilichokuwa nafanya.
HAMISI: Mwita yuko wapi?
PATRICK: Katoka kidogo kaenda kununua bidhaa, leo tumeamua kufanya mapishi hapa. Nilikuwa nachinja kuku.
HAMISI: Sasa ndio uchinjie ndani?
PATRICK: Sijachinjia ndani bhana, hiki ni kisu tu.
Hamisi alimtazama Patrick kwa macho ya wasiwasi na Patrick akaligundua hilo, akaamua kuweka kisu pembeni na kumkaribisha Hamisi ndani.
Hamisi hakutaka kuingia ndani kabisa ila kabla hajasogea kokote, Patrick alikuwa tayari yupo mlangoni. Hamisi akaogopa sana,
PATRICK: Wasi wasi wako ni nini Hamisi? Najua wewe ni mwadilifu na mwanajeshi imara katika kulitumikia taifa, sasa unaogopa nini kwa mtu kama mimi Hamisi?
HAMISI: Aaah..... Unajua..... Aaaah.....
Hamisi alishikwa na kigugumizi cha gafla.
PATRICK: Unawaza nini juu ya matukio ya vifo uliyoyasikia?
HAMISI: (Akashtuka kwanza), ndio nilikuja kumweleza bwana Mwita hapa ili nizungumze nae.
PATRICK: Na je iwapo unamjua mtu anayefanya hayo? Usiwe na shaka Hamisi, nataka kusaidia upelelezi.
HAMISI: Nikimjua nitachukua hatua ya kumripoti.
PATRICK: Je, hautapenda kupambana nae?
Hamisi akabaki kumuangalia tu Patrick huku akiwa hajui dhamira ya Patrick ni nini.
Mara akapigiwa simu kuwa mwanajeshi mwingine amekutwa amekufa. Baada ya simu kukatika, akajikuta akisema kwa hasira.
HAMISI: Hivi ni nani anayetenda haya?
PATRICK: Ni mimi Hamisi.
Halafu akaanza kucheka.
Adamu na Maiko kama walivyopanga, ikabidi Adamu afanye juhudi za kwenda kumchukua bi.Rehema ili Maiko apate kuzungumza nae.
MAIKO: Basi ukirudi njoo nae moja kwa moja huku.
ADAMU: Hakuna tatizo ila sielewi tu kwanini hutaki kwenda kule nilipokwambia.
MAIKO: Kuna muda utaelewa ila sio sasa, naomba tu nizungumze na mama kwasasa, niletee yeye tu ananitosha.
Adamu akaondoka na safari ya kwenda kwa Deborah ikaanza.
Deborah na Pamela walipatana sasa na kuendelea kufanya maongezi pamoja.
DEBORAH: Pamela rafiki yangu hata siku moja usikimbie tatizo ila kabiliana nalo na hapo utapata njia ya kuliondoa kabisa ila kulikimbia ni kujiongezea tatizo zaidi.
PAMELA: Nakubaliana nawe Deborah, sitapenda tuendelee kurumbana. Maji yakishamwagika hayazoleki tena. Ngoja nikueleze nilichofanya huko nyuma na kinachofanya nijute hadi leo.
Mara wakamuona Adamu amerudi, wakabaki wanamshangaa kwani alishindwa kuwapa hata salamu zaidi ya kumfata mama yake ndani.
DEBORAH: Hivi mumeo ameanza kuchanganyikiwa? Inamaana hajatuona hapa nje?
PAMELA: Sijui.
Wakamuona akitoka na mama yake na kuanza kuondoka, ndipo Pamela alipoinuka na kuuliza.
PAMELA: Wee Adamu, unafika bila salamu unamchukua mama bila ya kusema chochote halafu unataka kuondoka nae ndio nini hivyo? Ustaharabu gani huo?
ADAMU: Yani wewe ndio usiongee kabisa, ngoja nirudi unieleze ulipokuwa hadi mimi nahangaika mapolisi kukutafuta.
Adamu na mama yake wakaingia kwenye gari ya kukodi aliyoenda nayo Adamu mahali pale na kuondoka.
Rehema hakutaka sema chochote kwani alishanong'onezwa na Adamu kuwa wanaenda kwa nani, akajua kuwa angesema tu basi wale wanawake wote wenye hasira na huyo mtu wasingekubali.
Deborah na Pamela wakaendelea na mazungumzo yao hawakuwa na shaka sana kwani wanajua kuwa bi.Rehema ameondoka na mwanae.
Hamisi kumsikia Patrick kuwa ndiye aliyefanya mauaji yote yake, kwanza aliogopa pili alishangaa ni jambo lipi lilimpelekea Patrick kuua kiasi kile.
PATRICK: Unataka kujua nimewaua kwanini?
Hamisi aliitikia kwa kichwa tu.
PATRICK: Nimewaua kwasabu wana roho mbaya kushinda yangu, sasa wale wakiendelea kuwa jeshini watawatesa sana wananchi.
HAMISI: Ila umelitia jeshi hasara.
PATRICK: Hilo nalitambua.
Halafu akamfata tena Hamisi na kumkaba, ikabidi Hamisi ajitetee kwa kupigana na Patrick. Ila Hamis alishindwa na kujikuta akiwa chini.
Akachukua kamba na kumfunga mikono na miguu kisha na kumchinja kawa kuku. Huku akisema,
"Hivyo ndivyo nilivyowamaliza wenzio wote. Nilipambana nao kwanza na kuwafunga kamba, kisha nikawachinja taratibu kama kuku ili wayapate mateso waliyowatesea watu wote hadi kifo"
Akainuka juu na kumwambia tena,
"Sina sababu ya kukumaliza ila ushahidi wako umefanya nikumalize ili usije ukaniripoti kabla sijamaliza kazi yangu nyingine. Nayo ni Maiko tu."
Patrick hakupoteza muda zaidi mahali hapo na usiku huo huo akasafiri kurudi Mwanza.
Bi.Rehema alipelekwa hadi alipo Maiko, yote haya yalishuhudiwa na Yuda.
Bi.Rehema alifurahi sana kumuona tena mtoto wake huku akimuangalia kwa umakini mkubwa. Maiko nae alifurahi kumuona mama yake na kwa mara ya kwanza tangia kukua kwake aliweza kutoa machozi siku hii ya leo.
REHEMA: Niambie mwanangu, kwanini imekuwa hivi?
MAIKO: Ni ndugu yako Mashaka ndiye aliyesababisha haya, alinifanya niamini kuwa ulikufa kitambo sana na hatuna ndugu tena. Na kwavile alirudi kama kachanganyikiwa tukaamini kuwa ni kweli.
REHEMA: Mmh! Jamani mwanangu!! Na kwanini ulibadili jina?
Maiko akaamua kuwaelezea kilichotokea,
"Ilitokea tu mama, mimi ni Juma na mtoto wa Mashaka aliitwa Maiko. Kipindi tunaenda Mombasa alimpitia huyo Maiko tukaondoka nae. Tulivyofika kule yeye akarudi kwenu, ni kipindi hicho ambacho mimi na mwanae tulibadilishana majina.
Alikawia sana kurudi, alikaa kama miaka mitatu, sisi tulikuwa tukitumikishwa tu na yule mwenzie tuliyekuwa nae. Aliporudi alikuta tumeyazoea yale majina tuliyobadilishana na hakuweza kutambua kwavile wote tulikuwa rika moja, tukamuuliza kuhusu mama zetu akajibu kuwa walikufa, kwakweli nilishikwa na uchungu sana na machozi yakanitoka, yule mwenzangu alilia hadi kujigalagaza chini na hakukubaliana na maneno kuwa mama yake amekufa, wakati huo ukumbuke alikuwa hatujui vizuri kwahiyo alitutambua kwa majina tu, alikuwa akijua mimi ndio yule na yule ndio mimi.
Akamgeukia mwenzangu na kumwambia kuwa yeye ndio hata asijisumbue kulia kwani ameshapoteza ndugu wote, hana ndugu hata mmoja zaidi yake. Mwenzangu hakukubali aliendelea kulia kila panapokucha, Mashaka hakupendezewa na yale makelele ya kila siku.
Siku hiyo usiku alituita na kutukanya tena ila bado ilikuwa kazi bure kwa yule mwenzangu, nikamuona Mashaka akitoa kisu na kumchoma yule mtoto kifuani na kusema hataki watoto wazembe. Na huo ukawa ndio mwisho wa mwanae Maiko ila yeye alijua ni Juma.
Nikabaki mimi na yeye na akanifundisha kazi za kujipatia kipato huku akiamini kuwa mimi ni mwanae ndio hadi ukubwa huu nakuja kutambua uwepo wa mama na ndugu zangu"
ADAMU: Duh!! Huyo Mashaka hafai basi.
Rehema alikuwa akilia tu huku mwanae akielezea.
REHEMA: Mashaka sio mtu kabisa, ni ndugu yangu ila hafai. Tafadhari mwanangu Juma, nina swali moja tu nataka unijibu.
MAIKO: Uliza tu mama.
REHEMA: Hivi ni kweli umekuwa katili kama huyo Mashaka?
Maiko alibaki kumtazama tu kwasababu ni ukweli mtupu tena yeye ndio alipatwa na ukatili wa ajabu. Ila kabla hajajibu, Mashaka alikuwa ameshaingia ndani ya nyumba ile.
Hali ya Tusa haikuwa nzuri sana ila Sele akaona ni vyema aondoke nae hapo hospitali na aende nae Mwanza mjini ikiwezekana familia nayo ipate habari kwa mambo yaliyotukia.
Kwahiyo akaanza safari ya kuondoka na Tusa kwenda nae Mwanza mjini, wakiwa kwenye bus wanasikia habari ya vifo vya kusikitisha vya wanajeshi mkoani Singida, majina yao yanatajwa na kwaharaka haraka Sele anatambua kuwa ni wale wanajeshi waliowatesa.
Tusa nae aliposikia hivyo anahisi moja kwa moja kuwa aliyehusika ni Patrick tu. Hofu inawatawala wote wawili juu ya Patrick.
Patrick ameingia Mwanza na jambo la kwanza kufanya ni kumtafuta Sele ili aweze kujua ni wapi alipo Tusa.
Akaanza kumtafuta hewani, ila kabla hajapiga simu ya Sele inaingia simu ya Yuda kwake, ikimwambia aachane na shughuli zote ili waende kupambana na Maiko kwani ameshajua sehemu alipo.
Habari ile inamvutia Patrick kwani bado anahamu ya kuua watu wote wanaoharibu furaha yake.
Akiwa anatafakari la kufanya pale njiani kama akamuangalie Tusa kwanza au akashughulike na Maiko, mara akashikwa bega, kugeuka nyuma ni Mwita akiwa na wanajeshi wengine watatu.
 
Back
Top Bottom