Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
- Thread starter
- #21
PASPOTI YA GAIDI.
MTUNZI, Richard MWAMBE
SEHEMU ya 13
Hayuko peke yake, wako kama wane hivi, wote lazima washughulikiwe,” Briston akiajbu huku akifungua mlango kutoka. Nje ya hoteli hiyo kila mmoja alichukua gari yake na kuondoka. Lakini Kubrah aliitazama sana gari ya Amata na akaiona ikiwa palepale, ina maana huyu mshenzi bado yupo humu ndani? Akajiuliza. Na taratibu akaondosha gari yake pale hotelini huku akimwagiza mmoja wa vijana wake kuiangalia ile gari mpaka itakapoondoka.
Ile gari aliyopanda Amata iliingia ndani ya majengo yasiyokwisha ambayo bado yalikuwa yakiendelea na ujenzi, ikaingia na kufika mahali ndani ya kitu kama chumba hivi. Ikasimama na milango ikafunguliwa huku wale jamaa wakiteremka hai hai.
“Vipi huko?” mtu mmoja aliyeonekan kama mlinzi aliuliza.
“Jamaa kauawa bwana na tunayemsaka inaonekana katoroka eneo lile,” akajibu mmoja wa walioshuka kwenye ile gari.
“Kwa hiyo tunafanyaje?”
“Mpango ni uleule, kesho asubuhi, tunaondoka na Malkia na kuelekea kisiwani kwani mpango mwingine unatakiwa kuchukua nafasi, weka kila kitu sawa kama mpango ulivyo,” akatoa maagizo ambayo Amata alikuwa akiyasikia vyema. Kwa kutumia simu yake akatuma ujumbe mfupi kumpa Madam S juu ya hayo anayoyasikia. Kisha akatulia palepale kusubiri watu hao watoke eneo hilo ili naye aweze kujitokeza na kufanya yake.
IKULU
USIKU UOHUO
SIMU YA RAIS iliita kwa fujo, mheshimiwa bado alikuwa hajalala na wala hakuwa hata na lepe la usingizi, alipoitazama akajua ni ile simu nyeti ambayo huweza kukaa zaidi ya siku tatu bila kuita isipokuwa kwa jmabo muhimi na la kiusalama tu, akaitazama na kuona kwenye kioo TSA, akaiweka sikioni mara moja.
“Taarifa kutoka TSA juu ya usalama wa taifa usiku huu, naomba kikao cha dharula kama inawezekana,” upande wa pili ukasubiri jibu. Bila kusita Mheshimiwa Rais akakubali kikao hicho usiku huo akakata simu na kutoa taarifa kwa wanausalama wachache juu ya ujio wa Selina ndani ya jingo hilo jeupe.
Saa tisa usiku, mwanamama huyo aliwasili Ikulu na kupokelewa na mtu alioyeandaliwa na moja kwa moja alifikishwa kwenye ofisi ya Rais kwa mazungumzo.
“Kwanza samahani kukukatisha usingizi,” akaanza kwa kusema hivyo.
“Hapana Sellina, siwezi kupata usingizi kwa hali hii ambayo inanikabili, na najua ni wewe tu kwa sasa unaeweza kunipa jibu ambalo litanifariji, nipe maendeleo ya kazi niliyowapa,” Rais akamwambia kisha akatulia kitini.
“TSA tupo kwenye uchunguzi wa hali ya juu sana katika swala la uvamizi wa Ikulu uliofanyika hapa na tumeshagundua mambo mengi sana kuliko unavyotarajia kusikia…”
“Enhe…”
“Kwanza kabisa, mkuu umezungukwa na maadfua kila kona ndani ya idara zako na nchi yako kwa ujumla. Uvamizi wa Ikulu ulipangwa na watu walio chini yako kwenye idara nyeti za uslama…” akamweleza kila kitu lakini hakutaja wahusika wa tukio hilo. Mheshimiwa Rais alikuwa katika hali ya hasira na uchungu alipokuwa akipokea taarifa hiyo fupi lakini iliyojaa utaalam wa kikachero wa hali ya juu, moyoni mwake alimshukuru aliyekuwa na wazo la kuanzisha idara hii ambayo sasa anaielewa umuhimu wake.
“Sasa kuna watu ambao wapo chini ya jicho letu na tunahitaji kuwakamata mara moja ikiwezekana kwa amri yako usiku huu, hawa watatueleza vyema juu ya mpango mzima tangu mwanzo na nani anahusika,” Madam Sellina akaeleza na Rais akalipokea kwa kutikisa kichwa akiashiria kuwa amekubaliana naye. Lakini mpaka hapo hakuwa anajua ni nani na nani.
“Nani na nani?” akauliza.
“Wa kwanza ni Kepteni Benzilahagi…”
“Kepteni? Wa jeshi au wa meli?” akauliza kwa hamaki.
“Bora angekuwa wa meli, ni wa jeshi tena JW, tunamshuku kutokana na nyendo zake siku hizi, baadae nitakujulisha nyendo hizo lakini sio leo kwa sababu za kiusalama. Mbaya zaidi mtu huyu yupo kwenye kitengo nyeti sana ndani ya jeshi letu, nikiwa na maana kuwa anajua kila kitu, kila siri, kila mpango wa jeshi letu. Ni msaliti…”
“Akamatwe na ahojiwe mara moja!” Rais akatoa amri na kupiga ngumi juu ya meza baada ya kutajiwa kitengo cha mtu huyo.
“Na wa pili nani? Nataka kumjua!” akang’aka mheshimiwa.
“Wa pili ni afisa ubalozi wa Nduruta anaitwa Kimosa Kabalege, sasa kwa huyu tulisita kwa sababu za kidiplomasia,” Madam S akaeleza.
“Kamata, weka ndani ahojiwe. Sellina unataka kunambia hii ni njama kutoka Nduruta?” akauliza Mheshimiwa Rais huku akionekana wazi kuhamanika kwa mpango huo.
“Ndiyo Mheshimiwa, kumbuka umeamuru vikosi vyako vya JW kuvaa kofia ya UN na kwenda kuendesha operesheni dhidi ya waasi wa X65, waasi hawa kwa uchunguzi wetu ni watu wa Rais Sebutunva wa Nduruta na washirika wake ambao siku hizi umeona wakikutenga katika mambo mengi ya ki-kanda. Tumegundua kwamba wafadhili wakubwa wa waasi hawa ni vyama vyenye mlengo wa kushoto huko Ughaibuni, kwa biashara ya mabadilishano wa vitu wao hupeleka Almasi na kupewa silaha nzito na za kisasa. Hivyo basi kama kisasi kutoka kwa jirani yao Sebutunva ndiye aliyefanya mipango yote ya kutekwa kwa First Lady akishirikiana na watu ambao ni mapandikizi ambao kila siku unakula na kunywa nao…”
“Stop!!! Ishia hapohapo Sellina. Sasa nimeielewa TSA na kazi yake, mmefanya kazi kubwa sana na je habari zozote juu ya mke wangu?” akauliza kwa shauku.
“Ninavyoongea na wewe hapa tupo kazini, na kwa kuwa tulikwambia ni saa sabini na mbili tutakuwa na jibu, nakuhakikishia tuko mbioni kumpata First Lady katika saa zizi hizi,” Madam S alimhakikishia Sellina hayo asemayo. Baada ya dakika chache zilizofuata waliagana huku…
Oda ya kukamatwa Kepteni Benzilahagi ilifika makao makuu ya jeshi, Upanga. Usiku huohuo polisi wa jeshi, sita walikuwa ndani ya Nissan Patrol ya kijani wakielekea nyumbani kwa Kepteni huyo, walitumwa kazi moja tu, kumkamata Benzilahagi na kumpeleka walikoamriwa.
Scoba alisthuliwa na simu iliyokuwa ikifanya fujo mfukoni mwake alipoikwapua alikutana na TSA 2.
“Sema namba 2,” akaitikia.
“Kuna jamaa wanakuja hapo, waache wafanye kazi, kutoka ulipo hakikisha tu operesheni imekwenda sawa wala usitie nguvu yoyote,” Chiba akamaliza.
“Copy!”
Alipoishusha simu hiyo aliona taa za gari zilizowashwa full zikicheza na kuyumbayumba akajua moja kwa moja kuwa hiyo gari iko kasi sana kupita maelezo.
Kepteni Benzilahagi aliiweka vizuri bastola yake ikiwa full, akaipachika kiunoni mwake na kuvaa fulana yake pull neck pamija na jinzi yake nyeusi. Akaketi kitako akinywa pombe kali makusudi kusubiri kile anachokitarajia. Muungurumo wa gari ulimuondoa pale kitini, akasimama na kujiweka vizuri kitini huku simu yake iliyokuwa sikioni. Kengele ya mlango ikafuatia, akasimama na kuelekea mlangoni hapo, macho kwa macho akakutana na MP waliovalia kijeshi wakiwa kamili na barua yao mkononi ya kumkamata.
“Mmetumwa kunikamata mimi?” akawauliza huku akiwarudishia ile karatasi.
“Ndiyo, tunavyoongea hivi sasa unatakiwa kuondoka nasi,” wakamwambia.
“Kwa kosa gani hasa?”
“Kosa utalijua hukohuko ukifika,” wakamueleza.
“Sawa hakuna tabu, nipeni dakika moja tu nimuage mama watoto kisha nakuja,” akawaambia, nao wakamruhusu na kumsubiri palepale. Benzilahagi akatembea kwa mikogo huku akipiga mluzi kuelekea chumbani.
“Suzi! Suuuuzi! Mi naondoka Suzi naenda kazini…” akaongea huku akiingia chumbani na kuufunga mlango nyuma yake. Pumbavu sana, subirini hapohapo narudi, akasema kwa sauti ya kujisikia mwenyewe moyoni. Akavuta kabati kubwa na kulisukuma pembeni kisha akatoa funguo zake na na kufungua mlango uliokuwa nyuma ya kabati hilo, alipoingia ndani ya kijichumba hicho, akarudisha lile kabati palepale na kuufunga mlango kisha akateremka ngazi zinazokwenda chini kisha akapita kwenye kitu kama andaki na kutokea nje ya ukuta kulikokuwa na kitu kama chemba ya maji taka. Alipomaliza kuurudishia ule mfuniko wa chuma, akajipukuta vumbi na kutokomea katika majumba ya jirani.
“Asee huyu jamaa anaaga kwa maneno au kapanda kitandani kabisa?” MP mmoja akauliza.
“Ah kweli hebu tumfatilie hukohuko dakika kumi sasa,” mwingine aliyekuwa kiongozi wao akawaambia kisha akawaongoza kuingia ndani ya jumba lile, walipoufikia lango wa chumbani, wakagonga, kimya, hakuna jibu wakagonga tena na tena, kimya kilekile kikaendelea. Alipousukuma, ukafunguka, wakaingia chumbani, wakatanabahi hakuna mtu, kitanda tupu.
“Unataka kusema kaondoka hapa hapa?” mmoja akauliza huku akitupa godoro upande wa pili, hakuna mtu. Mwingine alikuwa akipekuwa makabati bila mafanikio.
“Jamaa katoroka, lakini kapitia wapi? Mbona hakuna mlango humu? Atakuwepo tu mumu humu. Dakika ishiririni ziliwachukua kupekua chumba hicho lakini hawakuona mtu wala nyau.
“Ni aibu, tumewezwa!” Yule kiongozi wao akaongea huku mikono ikiwa kichwani na wakati huo akitoka nje ya chumba kile, “Hebu zunguka nyumba muifanyie ukaguzi huko nje,” akaamuru na vijana wake wakafanya hivyo.
Scoba akiwa ndani ya gari yake ametulia tuli, aliona kitu kama kivuli kikipita nyuma ya ga ri hiyo, alipogeuka akamwona mtu, mwanaume anayeishia kizani. Machale yakamcheza, akainuka na kuufungua mlango taratibu kisha akafuata njia ile ambayo yule kijana aliingia. Kona ya kwanza nay a pili akasikia mlio wa injini ya gari iliyokuwa ikiwashwa na gari ile ikaondoka zake. Scoba akajikuta anashindwa la kufanya kwa wakati ule, akarudi haraka kwenye gari yake na alipoiwasha na kuigeuza akasimamishwa na wale MP.
“Teremka chini ukiwa mikono kichwani,” akaamuriwa. Scoba akateremka na kusimama akiwa mikono kichwani. Wakampekua harakaharaka na kumwacha pembeni.
“Unafanya nini hapa usiku huu?” mmoja akauliza.
“Kuna mtu namsubiri,” akajibu.
“Haujaona mtu kapita hapa sasa hivi?”
“Nimemwona, alitokea upande huu!” akajibu.
“Kaenda wapi?”
“Kapita hapa hivi kaingia upande wa pili,” akawaelekeza na wale MP wakalekea upande ule, alipohakikisha wamepotelea kizani akawasha gri na kuondoka kwa kasi kuelekea upande ule ambao Benzilahagi amekwenda na gari, akajaribu kuifuata bila mafanikio, Kepteni Benzilahagi alikuwa ametoweka.
Itaendelea.