Riwaya: Senyenge

How soon is soon?
Bruv, writing something stellar is not as easy as you imagine. It takes time, research and reading and editing and reading and editing again. Not a soft work considering I have other issues to focus on. I don't just get from bed and voila!.. I have something to post. No, it doesn't work out like that.

Truth is siwezi kupandisha kitu ilimradi nimepandisha tu. Ninapandisha pale ambapo nakuwa nimeridhika kimekaa sawa - I promised, yes, but unfortunately things got into the way! You can't understand that? Really?

RN, I have no option but to cancel. And for the benefit of all of us [I & My beloved readers] I won't be posting anymore. Perhaps until June or July. Thank you.
 
RN, I have no option but to cancel. And for the benefit of all of us [I & My beloved readers] I won't be posting anymore. Perhaps until June or July. Thank you.

I personally saw this coming.

BTW, I appreciate for what you gave us.

All the best bruv, I hope once you start posting you will be for real.
 
Hii story naifananisha na movie moja amecheza Tom Cruise
 
Huu uzi umekufa na kuzikwa rasmi kwenye makaburi ya sahau.Pamoja na yote hongera BWANA Chacha!
 
Duhhh ndio hivyo mimi ndio story zangu nazipenda za mithili hii sio za mbususu,papuchi nyingii,heko mkuu ukijaaliwa pandisha.regards.
 
Hii kitu tuliambiwa mwezi wa 6, sasa ni mwezi wa 7 yan
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

Jodie ndiye aliendesha gari. Reacher alikuwa anageuka huku na huku kuona kama wanafuatwa. Hakukuwa na dalili za kufuatwa. Ilikuwa ni siku nyingine tulivu tu ya mwezi tano.

Jodie alisimamisha gari kwenye duka kubwa la mahemezi - mall. Lilikuwa ni jengo kubwa lililosimama kifahari hapo katikati. Waliposhuka Jodie alimuongoza Reacher hadi mlango wa kuingilia.

"Haya," Jodie alisema. "Tuanzie wapi sasa?"

Reacher aliinua mabega tu. Hakuwa anajua jambo lolote kuhusu mahemezi. Ni kweli alikuwa amenunua nguo nyingi mpya ndani ya miaka miwili iliyopita, lakini ilikuwa ni kwa sababu alikuwa hana tabia ya kufua zile za zamani. Ilikuwa ni tabia ya kujiwekea kinga fulani. Ilimkinga na kubeba mizigo mikubwa endapo angetaka kwenda mahali fulani. Lakini pia ilimkinga na suala la kufua. Kwahivyo njia sahihi ya yeye kufanya ilikuwa ni kununua nguo kila mara hapa na pale. Kwahivyo alikuwa amenunua nguo nyingi sana, lakini sehemu alizonunua ilikuwa ni ngumu kwake kuzikumbuka.

Kwa ufupi angeona tu nguo kwenye dirisha la duka fulani na kwenda kununua tu.

"Kuna duka moja niliwahi kuingia," Reacher alianza kuongea. "Kitu kama lilikuwa linaitwa The Gap."

Jodie alicheka. Akamshika mkono Reacher na kumwambia, "Humu wana tawi lao. Twende."

Waliyapita maduka kadhaa ya vipodozi na maduka mengine ya vitu tofauti. Kulikuwa na migahawa pia ndani ya jengo hilo. Na ni kitu ambacho kiliinasa pua ya Reacher ni harufu ya kahawa.

"Tunywe kahawa," Reacher alisema.

Jodie alicheka, "Hapana. Tunahemea nguo kwanza, ndiyo tunahamia kwenye kahawa.

Jodie alimuongoza Reacher hadi wakapanda ngazi za juu lilipokuwa duka la The Gap. Reacher alitabasamu. Alikuwa amehisi namna ambavyo Jodie alikuwa anajisikia. Yeye pia aliwahi kujisikia hivyo miaka kumi na tano iliyopita.

"Unaonaje tukiingia humu?" Jodie aliuliza.

Halikuwa ni duka la The Gap. Ilikuwa ni duka fulani tu la nguo. Jodie alimshika mkono Reacher. Mkono wake ulikuwa laini na wenye joto. Alimuongoza kuingia hadi ndani ya duka na kuanza kuangaza macho kwenye nguo zilizokuwa mule ndani. Alichukua shati, suruali na koti fulani na kumuonesha Reacher.

"Unaonaje hii?"

Alikuwa amemchagulia suruali ya kijivu, shati la kijani. Na koti la udhurungi.

"Ni nzuri tu mbona." Reacher alijibu.

Bei za nguo zilikuwa zimeandikwa kwenye kitikiti. Reacher aligeuza kukiangalia.

"Mungu wangu," Reacher alisema. "Achana nazo hizo mbona zina bei sana?"

Shati peke yake tu lilikuwa linagharimu mara mbili ya kila alichokuwa amevaa.

"Nitalipia mimi," Jodie alisema. "Unakumbuka ile cheni?"

Reacher alitikisa kichwa kukubali. Alikuwa anaikumbuka vyema. Jodie aliipenda enzi hizo, ila baba yake, mzee Garber alikuwa na aina fulani ya ukoloni hivyo hakumnunulia. Ila Reacher alimnunulia, sio kwaajili ya birthday yake au sherehe yeyote. Alimnunulia tu kwa sababu alikuwa anampenda.

"Nilifurahi sana uliponinunulia," Jodie alisema. "Mpaka leo ninayo na huwa ninaivaa. Kwahivyo acha na mimi nilipe fadhila kidogo."

Reacher alitikisa kichwa kukubali. "Sawa."

Hata hivyo angeweza kumudu kulipia. Jodie alikuwa ni mwanasheria na alikuwa anatengeneza pesa nyingi tu.

"Sawa." Reacher alijibu. "Unahitaji na socks pia."

Walichagua soksi na Reacher aliingia chumba cha kubadilishia nguo. Alipotoka Jodie alimwambia amependeza.

"Haya tukanywe kahawa." Reacher alisema.

"Hapana, Duka la dawa kwanza halafu Pharmacy."

Walipotoka pharmacy walielekea kwenye mgahawa wa karibu na kuagiza chakula. Bili alilipia Reacher.

"Sawa, tunaenda nyumbani," Reacher alisema. "Na kuanzia hapa tunatakiwa kuwa makini sana."

Reacher alianza kukagua usalama kuanzia eneo la maegesho ya gari. Hakukuwa na tatizo lolote. Akamruhusu Jodie apande gari waondoke.

"Mara nyingi huwa unatumia njia ipi?"

" Kutokea hapa huwa napitia FDR Drive."

"Sawa. Sasa leo pitia LaGuardia, halafu tutaingia Brooklyn tupite daraja la Brooklyn."

Jodie alimwangalia Reacher kwa jicho la mshangao. " Umekuwa mtalii? Tunaweza kupita njia zingine uone vivutio vizuri kuliko Brooklyn."

"Lengo sio vivutio." Reacher alianza kuelezea. "Mtu akiweza kukutabiri ni hatari sana. Kama kuna njia huwa unapita kila siki, leo tutapita njia tofauti."

"Unamaanisha unachokisema?"

"Unaweza ukaweka uhai wako dhamana. Nimewahi kutoa huduma ya ulinzi kwa watu wakubwa serikalini."

Lisaa limoja baadae, giza lilikuwa limeingia na walikuwa wapo daraja la Brooklyn. Muda kidogo walikaribia nyumbani kwa Jodie.

"Pitiliza nyumba kadhaa halafu tutarudi tena."

Reacher aliangalia kwa mbele kuona usalama.

"Nivuke nyumba tatu." Jodie alisema.

"Kwani huwa unaegesha gari wapi?"

"Gereji."

"Sawa, endelea kwenda." Reacher alisema. "Utanishusha mimi halafu nitaendelea kukagua wewe utaendelea na gari mbele. Baada ya dakika tatu rudi utanikuta na kama utanikuta sipo, nenda moja kwa moja kituo cha polisi."

Jodie alisimamisha gari Reacher akashuka na kuelekea ilipo nyumba ya Jodie. Ilikuwa ni nyumba kubwa, nzuri na ya kuvutia. Kulikuwa na watu wanapita hapa na pale, lakini Reacher aligundua hakuna yeyote aliyejali kuhusu uwepo wao.

Aliendelea kukagua hapa na pale kwenye nyumba, lakini hakuona dalili ya mtu yeyote kujificha sehemu yeyote. Alirudi barabarani na kwenda hadi pale walipoachana na Jodie, ambaye pia ndiyo alikuwa anafika.

"Kila kitu kipo sawa." Reacher alisema.

Jodie alienda kuliegesha gari na kulizima na kuzima taa.

"Huwa unapandaje ghorofani huko?"

"Tunapita mlangoni hadi kwenye korido."

Waliingia ndani hadi koridoni na Reacher alikagua, lakini hakuona mtu.

"Mimi nipo ghorofa ya nne."

Reacher alibofya kitufe cha ghorofa ya tano.

"Tunaenda huko halafu tutashuka kwa ngazi hadi ghorofa ya nne."

Walipofika ghorofa ya tano wakaanza kushuka chini kwa ngazi kwenda ghorofa ya Jodie.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…