Chachasteven
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 1,941
- 2,044
- Thread starter
- #181
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
Walipofika ghorofa ya nne, Reacher aliongea. "Haya fungua."
Mlango wa nyumba ya Jodie ulikuwa na rangi nyeusi. Jodie alitumia funguo zake kuufungua na wakaingia ndani. Reacher aliifunga cheni ya mlango kutokuruhusu anayetoka nje kuingia kirahisi. Jodie alibofya swichi fulani ukutani na taa zikapata uhai. Reacher alimpa ishara asimame halafu yeye akaanza kuizunguka nyumba. Korido, sebule, jiko, chumba cha kulala, bafu na choo na kabati ya nguo. Hakukuwa na dalili ya mtu. Alirudi sebuleni na kuvua koti lake na kulitupa kwenye kiti na kumuangalia Jodie kwa uso wa amani. Lakini Jodie alionekana kukosa amani. Alikiwa na hofu kubwa na alibaki amesimama bila kukaa.
"Upo sawa," Reacher aliuliza.
"Nadhani niingie kuoga kwanza," Jodie alisema.
"Siku mbaya sana hii, sio?" Reacher aliuliza.
"Mbaya sana kiasi kwamba siamini. Nahitaji kulala pia."
Jodie alimaliza kuongea na kuanza kwenda chumbani. Alimtazama Reacher kwa jicho la aibu kidogo.
"Kesho saa ngapi?" Reacher aliuliza.
"Saa moja na nusu asubuhi."
"Sawa," Reacher alijibu na kuongeza. "Usiku mwema, Jodie."
Jodie alitikisa kichwa kukubali na kuelekea chumbani. Reacher alisikia mlango wa chumbani ukifunguliwa na kisha kufungwa. Reacher alibaki tu ametulia usingizi ukiwa mbali. Alianza kutathmini ile nyumba. Ilikuwa ni jengo la muda kidogo likiwa na muonekano mzuri. Kuta za ndani zilikuwa zimepakwa rangi za kuvutia nyeupe isipokuwa sakafu ilikuwa ni rangi ya malumalu tofauti. Kulikuwa kuna urembo pia wa picha za ukutani. Kulikuwa hakuna dalili ya kama kuna mtu mwingine tofauti na Jodie aliwahi kuishi hapo.
Kwa sababu hakukuwa na ladha ya mawazo ya watu wawili kwenye mpangilio wa vitu. Masofa meupe, viti vyeupe, kabati za vitabu nyeupe na karibu kila kitu rangi yake ilikuwa nyeupe.
Kitu pekee ambacho kilikuwa cha tofauti kwa rangi ni mchoro mmoja tu ambao ulikuwa ni mchanganyiko wa rangi ya bluu ,njano na nyekundu. Ni mchoro uliochorwa na mchoraji maarufu Mondrian mwaka 1930. Na nakala yake halisi Reacher aliwahi kuiona Zurich, Switzerland.
Kulikuwa na kabati ndogo pia. Ilikuwa imebeba Tv na vifaa vinavyoifanya Tv ioneshe. Kulikuwa na mkusanyiko wa CD pia. Nyingi zilikuwa ni za mziki aina ya Jazz.
Alinyanyuka na kuelekea lilipo dirisha lililoonesha upande wa nje. Kulikuwa na watu wanapitapita, lakini hakuna aliyempa mashaka.
Alienda jikoni. Huko nako karibu makabati na vyote vilivyokuwepo rangi yake ilikuwa ni nyeupe. Kulikuwa na kila aina ya kitu. Alijicheka mwenyewe kwa sababu kuna wakati aliwahi kuishi kwenye vyumba vidogo kuliko hata jokofu lililokuwemo mule jikoni. Aliifungua jokofu na kuangalia vilivyokuwemo. Aliona aina ya maji aliyokuwa anayapendelea kama alipokuwa Keys. Alichukua moja na kulifungua na kuelekea chumba cha wageni kulala.
Chumbani kila kitu kilikuwa cha rangi nyeupe kama sehemu zingine zote. Aliweka maji yake juu ya meza na kuingia bafuni. Alivua nguo zake mpya na kuingia kuoga. Alipomaliza alirudi na kupanda kitandani akaanza kuwaza.
Mawazo na uhalisia. Miaka tisa ilikuwa ni nini? Ni mingi, alijiambia. Kipindi hicho Jodie alikuwa na miaka kumi na tano na yeye alikuwa na miaka ishirini na nne, lakini sasa hivi? Yeye Reacher alikuwa na thelathini na nane, na Jodie alikuwa ama na miaka ishirini na tisa au thelathini. Kwani shida ipo wapi? Kwanini sifanyi kitu chochote? Au shida ni umri. Au labda kwa sababu alikuwa ni mtoto Garber. Ilimpa mawazo kuwa Jodie ni kati ya dada yake au mpwa. Hiyo ilimpa wasiwasi, lakini yalikuwa mawazo tu, sio?
Uhalisia ni kwamba, Jodie alikuwa ni mtoto wa rafiki yake tu. Rafiki ambaye sasa hivi alikuwa ni marehemu. Sasa mbona alikuwa anajihisi vibaya kumkumbatia wakiwa utupu. Kwanini asifanye hivo? Kwanini alikuwa amelala peke yake kwenye hiki chumba wakati walitakiwa wawe pamoja.
Jodie alikuwa upande wa pili wa chumba na hakuna kitu Reacher angefanya. Hakuna kitu. Na isingewahi kutokea wakafanya jambo lolote. Alijua hilo jambo litamchanganya akili akaamua kubadilisha mawazo yake. Vitu ambavyo vilikuwa na uhalisia. Wale jamaa wawili, lazima wangekuwa wameshajua mahali Jodie anapokuwa anakaa. Labda wangekuwa nje ya nyumba sasa hivi. Alianza kuikagua nyumba kichwani mwake. Milango yote ilikuwa imefungwa. Kwahivyo usiku huo kila kitu kilikuwa salama. Lakini kesho asubuhi ingekuwa hatari. Alianza kuwaza namna atakavyoshughulika na wale wanaume wawili. Gari lao, suti zao, miili yao na nyuso zao.
Lakini kwa muda huo, ni mwanaume mmoja tu aliyekuwa na uso kati ya wale wawili aliokuwa anawawaza Reacher. Wanaume hao walikuwa wamepanda boti moja kwenda hadi katikati kidogo ya maji yalioko ufukwe wa New York. Huko walishirikiana kuutupa mwili wa yule sekretari ndani ya mdomo mpana wa bahari ya Atlantic. Halafu jamaa mmoja alimgeuka mwenzake na kumpiga shaba usoni kwa kutumia Beretta iliyokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti. Risasi tatu alizopigwa zilimvuruga kabisa sura yake. Uso wake ulikuwa ni vurugu kwenye giza la ule usiku. Halafu yule bwana akaukata mkono mmoja wa yule mwanaume mwenzake na kuuweka kwenye mfuko wa plastiki kabla ya kuutupia mwili wake kwenye maji kama walivyokuwa wameutupa ule mwili wa yule katibu muhtasi.
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE