Riwaya: Senyenge

Riwaya: Senyenge

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

Walipofika ghorofa ya nne, Reacher aliongea. "Haya fungua."

Mlango wa nyumba ya Jodie ulikuwa na rangi nyeusi. Jodie alitumia funguo zake kuufungua na wakaingia ndani. Reacher aliifunga cheni ya mlango kutokuruhusu anayetoka nje kuingia kirahisi. Jodie alibofya swichi fulani ukutani na taa zikapata uhai. Reacher alimpa ishara asimame halafu yeye akaanza kuizunguka nyumba. Korido, sebule, jiko, chumba cha kulala, bafu na choo na kabati ya nguo. Hakukuwa na dalili ya mtu. Alirudi sebuleni na kuvua koti lake na kulitupa kwenye kiti na kumuangalia Jodie kwa uso wa amani. Lakini Jodie alionekana kukosa amani. Alikiwa na hofu kubwa na alibaki amesimama bila kukaa.

"Upo sawa," Reacher aliuliza.

"Nadhani niingie kuoga kwanza," Jodie alisema.

"Siku mbaya sana hii, sio?" Reacher aliuliza.

"Mbaya sana kiasi kwamba siamini. Nahitaji kulala pia."

Jodie alimaliza kuongea na kuanza kwenda chumbani. Alimtazama Reacher kwa jicho la aibu kidogo.

"Kesho saa ngapi?" Reacher aliuliza.

"Saa moja na nusu asubuhi."

"Sawa," Reacher alijibu na kuongeza. "Usiku mwema, Jodie."

Jodie alitikisa kichwa kukubali na kuelekea chumbani. Reacher alisikia mlango wa chumbani ukifunguliwa na kisha kufungwa. Reacher alibaki tu ametulia usingizi ukiwa mbali. Alianza kutathmini ile nyumba. Ilikuwa ni jengo la muda kidogo likiwa na muonekano mzuri. Kuta za ndani zilikuwa zimepakwa rangi za kuvutia nyeupe isipokuwa sakafu ilikuwa ni rangi ya malumalu tofauti. Kulikuwa kuna urembo pia wa picha za ukutani. Kulikuwa hakuna dalili ya kama kuna mtu mwingine tofauti na Jodie aliwahi kuishi hapo.

Kwa sababu hakukuwa na ladha ya mawazo ya watu wawili kwenye mpangilio wa vitu. Masofa meupe, viti vyeupe, kabati za vitabu nyeupe na karibu kila kitu rangi yake ilikuwa nyeupe.

Kitu pekee ambacho kilikuwa cha tofauti kwa rangi ni mchoro mmoja tu ambao ulikuwa ni mchanganyiko wa rangi ya bluu ,njano na nyekundu. Ni mchoro uliochorwa na mchoraji maarufu Mondrian mwaka 1930. Na nakala yake halisi Reacher aliwahi kuiona Zurich, Switzerland.

Kulikuwa na kabati ndogo pia. Ilikuwa imebeba Tv na vifaa vinavyoifanya Tv ioneshe. Kulikuwa na mkusanyiko wa CD pia. Nyingi zilikuwa ni za mziki aina ya Jazz.

Alinyanyuka na kuelekea lilipo dirisha lililoonesha upande wa nje. Kulikuwa na watu wanapitapita, lakini hakuna aliyempa mashaka.

Alienda jikoni. Huko nako karibu makabati na vyote vilivyokuwepo rangi yake ilikuwa ni nyeupe. Kulikuwa na kila aina ya kitu. Alijicheka mwenyewe kwa sababu kuna wakati aliwahi kuishi kwenye vyumba vidogo kuliko hata jokofu lililokuwemo mule jikoni. Aliifungua jokofu na kuangalia vilivyokuwemo. Aliona aina ya maji aliyokuwa anayapendelea kama alipokuwa Keys. Alichukua moja na kulifungua na kuelekea chumba cha wageni kulala.

Chumbani kila kitu kilikuwa cha rangi nyeupe kama sehemu zingine zote. Aliweka maji yake juu ya meza na kuingia bafuni. Alivua nguo zake mpya na kuingia kuoga. Alipomaliza alirudi na kupanda kitandani akaanza kuwaza.

Mawazo na uhalisia. Miaka tisa ilikuwa ni nini? Ni mingi, alijiambia. Kipindi hicho Jodie alikuwa na miaka kumi na tano na yeye alikuwa na miaka ishirini na nne, lakini sasa hivi? Yeye Reacher alikuwa na thelathini na nane, na Jodie alikuwa ama na miaka ishirini na tisa au thelathini. Kwani shida ipo wapi? Kwanini sifanyi kitu chochote? Au shida ni umri. Au labda kwa sababu alikuwa ni mtoto Garber. Ilimpa mawazo kuwa Jodie ni kati ya dada yake au mpwa. Hiyo ilimpa wasiwasi, lakini yalikuwa mawazo tu, sio?

Uhalisia ni kwamba, Jodie alikuwa ni mtoto wa rafiki yake tu. Rafiki ambaye sasa hivi alikuwa ni marehemu. Sasa mbona alikuwa anajihisi vibaya kumkumbatia wakiwa utupu. Kwanini asifanye hivo? Kwanini alikuwa amelala peke yake kwenye hiki chumba wakati walitakiwa wawe pamoja.

Jodie alikuwa upande wa pili wa chumba na hakuna kitu Reacher angefanya. Hakuna kitu. Na isingewahi kutokea wakafanya jambo lolote. Alijua hilo jambo litamchanganya akili akaamua kubadilisha mawazo yake. Vitu ambavyo vilikuwa na uhalisia. Wale jamaa wawili, lazima wangekuwa wameshajua mahali Jodie anapokuwa anakaa. Labda wangekuwa nje ya nyumba sasa hivi. Alianza kuikagua nyumba kichwani mwake. Milango yote ilikuwa imefungwa. Kwahivyo usiku huo kila kitu kilikuwa salama. Lakini kesho asubuhi ingekuwa hatari. Alianza kuwaza namna atakavyoshughulika na wale wanaume wawili. Gari lao, suti zao, miili yao na nyuso zao.

Lakini kwa muda huo, ni mwanaume mmoja tu aliyekuwa na uso kati ya wale wawili aliokuwa anawawaza Reacher. Wanaume hao walikuwa wamepanda boti moja kwenda hadi katikati kidogo ya maji yalioko ufukwe wa New York. Huko walishirikiana kuutupa mwili wa yule sekretari ndani ya mdomo mpana wa bahari ya Atlantic. Halafu jamaa mmoja alimgeuka mwenzake na kumpiga shaba usoni kwa kutumia Beretta iliyokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti. Risasi tatu alizopigwa zilimvuruga kabisa sura yake. Uso wake ulikuwa ni vurugu kwenye giza la ule usiku. Halafu yule bwana akaukata mkono mmoja wa yule mwanaume mwenzake na kuuweka kwenye mfuko wa plastiki kabla ya kuutupia mwili wake kwenye maji kama walivyokuwa wameutupa ule mwili wa yule katibu muhtasi.

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
 
I feel you, bruv. Ila siachi kwa maksudi. Nadhani unaelewa majukumu na uandishi tunafanya for fun! Sio kazi ambayo itakupa chakula mezani. Samahani lakini kama nimewahi kukukera.
Tunaelewa kaka, huyo jamaa pia muelewe, hii kitu ni tamu na inaleta uraibu, ikikawia inaumiza[emoji23][emoji23]
 
Tunaelewa kaka, huyo jamaa pia muelewe, hii kitu ni tamu na inaleta uraibu, ikikawia inaumiza[emoji23][emoji23]
Nimekuelewa, mkuu. Ila ingependeza kama mngekuwa pia mnamjali mwandishi 😂😔. Apate hata za maji ya kunywa na data...
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

Jodie aliamka mapema ilipofika asubuhi, jambo ambalo halikuwa kawaida yake. Kwa kawaida angelala akikoroma hadi hapo alarm yake itakapomwamsha, lakini asubuhi ya leo aliamka lisaa limoja kabla ya muda aliopaswa awe ameamka. Alikuwa akihema taratibu na mapigo ya moyo wake yakiwa kasi.

Kuta za chumba chake zilikuwa zimepakwa rangi nyeupe kama nyumba yake yote ilivyokuwa. Chumba cha wageni kilikuwa kimepakana na cha kwake na kwa namna kitanda chake kilivyokuwa kimewekwa, ilimaanisha kichwa chake na cha Reacher wakati wa kulala vilikuwa vimetenganishwa na ukuta tu.

Nyumba hii aliikarabati mwenyewe kwa kiwango kikubwa kwa sababu aliinunua ikiwa haijaisha kabisa. Kwahivyo wazo la nini kiwekwe wapi ilikuwa ni wazo lake kabisa. Na kuta alizochagua zilikuwa ni kuta za mbao - hivyo usiku wa jana kilichowatenganisha na Reacher ilikuwa ni inchi chache tu za mbao.

Na kama kuna jambo Jodie alikuwa na uhakika nalo, basi ni kwamba alikuwa anampenda Reacher. Hakuna ubishi. Alikuwa anampenda tangu zamani. Lakini je ilikuwa ni sahihi kuwa na hisia za mapenzi kwa Reacher? Hilo lilikuwa ni swali alilojiuliza kila mara miaka nenda miaka rudi. Lile daraja la miaka tisa kati yao lilikuwa ni kikwazo. Msichana wa miaka kumi na tano asingepaswa kuwa na hisia za hivyo kwa mtu mkubwa zaidi yake. Yule alikuwa ni kama mjomba wake. Kanuni za jeshi zilikuwa zimeweka hilo wazi kabisa. Lakini moyo ulikuwa umemzimia Reacher. Hakuna shaka kabisa.

Walikuwa wapo pamoja mara nyingi. Wakiongea kila walivyoweza na wakishikana kila walipohitaji. Alikuwa na picha moja iliyomuonesha akiwa kashika kiuno cha Reacher miaka ya nyuma huko. Ni picha aliyoihifadhi vyema na kuiangalia kila wakati. Kwa miaka mingi alikuwa bado anakumbuka alivyojihisi kugusana naye, na harufu yake. Alijitahidi kuziondoa hizo hisia, lakini hazikuwahi kuondoka. Alihisi labda ilikuwa ni suala la ujana tu. Balehe. Lakini hapana. Hizo hisia zilikuwa naye. Reacher alikuwa amepotea, na yeye alikuwa amekwishakuwa mkubwa lakini hisia zilikuwa palepale.

Hazikuwahi kufutika, lakini zilibaki naye kwenye maisha yake. Jana ilitakiwa kuwa siku mbaya sana kwake. Alikuwa amemaliza kumzika baba yake, ndugu yake pekee duniani. Jana pia alikuwa amekaribia kuuliwa. Angetakiwa kuwa na huzuni. Lakini hakuwa na huzuni. Baadala yake jana ilikuwa imekuwa siku yake ya furaha. Reacher alikuwa amekuja. Alitokea kama zawadi tu ghafla pale msibani. Moyo wa Jodie ulirukaruka na zile hisia za miaka yote zikarudi upya kama dawa iingiavyo kwenye mishipa.

Lakini yote hayo ilikuwa ni kupoteza muda. Alikuwa na uhakika na hilo. Reacher alikuwa anamchukulia kama dada tu. Kama vile utofauti wa miaka tisa kati yao ulikuwa na maana yeyote bado. Mtoto wa miaka kumi na tano kuwa na mapenzi na mtu waka ishirini na nne lingekuwa tatizo. Lakini miaka thelathini kwa thelathini na tisa ilikuwa poa kabisa. Kuna watu wako kwenye mahusiano na utofauti kati ya umri zao ni kubwa sana. Na hakuna anayehoji.

Miaka ya nyuma, walikuwa wameishi kama kaka na dada. Ingewezekana vipi wawe na uhusiano wa mapenzi? Ni kweli walifurahi pamoja na kusaidiana. Si zaidi ya hapo.

Alijinyoosha mwili wake na kukaa kitandani. Akajifariji angalau Reacher alikuwepo nyumbani kwake.



YULE MWANAUME ALIKUWA NA masaa matatu kabla ya kuwasilisha mzigo, hivyo alipiga kasia boti yake na kupita nyumbani kulala kabla ya kuamka saa kumi na mbili alfajiri. Alioga haraka na kubadilisha nguo bila ya kunywa hata chai. Mkono aliokuwa ameukata kutoka kwa mwezake, ulikuwa umehifadhiwa vyema kwenye mfuko wa plastiki.

Alitumia Tahoe nyeusi na kuendesha kwa kasi kuliko hata watu wa delivery za asubuhi. Aliliegesha gari na kuanza kupanda hadi ilipokuwa ghorofa namba themanini na nane. Tony ndiye alikuwa yupo nyuma ya dawati la mapokezi. Yule mwanaume alijua hakukuwa na mtu mwingine kutokana na mazingira yalivyokuwa. Aliinua furushi la mfuko wake juu kama medani ya ushindi.

"Nina mzigo wa Hook," alisema.

"Hook hajafika leo," Tony alimjibu. "Uweke kwenye jokofu huo."

Kulikuwa na jiko dogo upande wa nyuma. Lilikuwa na muonekano wa hovyo kama majiko mengi ya ofisini yanavyoonekana. Yule mwanaume alifungua jokofu na kuweka ule mkono kwenye sehemu uliyokuwa haina kitu.

"Malengo ya leo ni Mrs. Jacob," Tony alisema. Alikuwa amesimama kwenye mlango wa jikoni. "Tumekwishafahamu anapoishi. Majirani wake wanasema huwa anaondoka saa moja nusu kwenda kazini na anatembea kwa miguu. Nyumba yake ni kama nyumba nane kutokea hapa."

"Ni wapi haswa?"

"Wall Street." Tony alisema na kuongeza, "Mimi nitaendesha, wewe kazi yako ni kumnasa tu. Sawa?"

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

Chester Stone aliendesha kwenda nyumbani kwa muda uleule kama anavyofanya kila siku na hakuongea neno lolote na Marilyn. Hakukuwa na kitu chochote cha kusema. Mambo yaliyomtokea yalikuwa yamefanyika kwa kasi ya ajabu kiasi cha kumpa ganzi ya akili. Ulimwengu wake wote ulikuwa umegeuka juu chini ndani ya kipindi cha masaa ishirini na nne tu. Ilikuwa ni jambo gumu kustahimili. Alipanga kulipuuza hadi pakuche ndipo aende kuonana na Hobie ajaribu kuongea naye. Ingawa akili yake ilikuwa imeganda, moyoni mwake aliamini kulikuwa bado kuna nafasi ya yeye kujiokoa.

Ile kampuni ilikuwa ina umri wa miaka sitini. Karibu vizazi vitatu vya Chester Stone. Kulikuwa na kumbukumbu nyingi ambazo ingekuwa ni ngumu kuzisahau kwa usiku mmoja tu. Kwahivyo hakusema neno lolote kwa Marilyn.

Marilyn pia hakusema neno lolote kwa Chester. Ilikuwa bado ni mapema kumwambia amechukua maamuzi. Kwahivyo Marilyn aliendelea na kazi zake za jioni kama kawaida. Halafu walipopanda kitandani Marilyn alisinzia huku Chester akiwa bado anakodolea macho dali.


JODIE ALIPOWEKA MKONO wake kwenye ukuta uliowatenganisha na Reacher, Reacher alikuwa bafuni anaoga. Alikuwa ana machaguzi matatu ya namna ya kuoga na kila asubuhi alijiuliza atumie chaguzi lipi. Namna ya kwanza ilikuwa ni kuoga tu. Hakuna kitu cha ziada. Hii mara nyingi ilimchukua dakika kumi na moja. Namna ya pili ilikuwa ni kunyoa halafu kuoga. Hii ilimchukua dakika ishirini na mbili. Ya tatu ilikuwa na ugumu kiasi na aliitumia mara chache sana. Hii ilitakiwa aanze kuoga, halafu anyoe na arudi tena kuoga. Ilitumia zaidi ya nusu saa bafuni. Lakini faida yake ni kwamba unyevu wakati wa kunyoa ulisaidia sana.

Na leo Reacher alikuwa anatumia namna ya tatu. Oga, nyoa, oga tena. Na alijihisi vizuri. Alijimwagia maji, akanyoa ndevu zake, halafu akajimwagia tena maji. Alipomaliza kuoga alihamia kusukutua.

Alitumia dakika tano kwenye meno yake. Aliporidhika alivaa suruali yake bila shati na kuelekea jikoni kwaajili ya kifungua kinywa.

Jodie alikuwepo jikoni. Yeye pia alikuwa amemaliza kuoga. Nywele zake zilikuwa na viashiria vya maji. Alikuwa amevaa tisheti kubwa iliyomfunika hadi juu kidogo ya magoti. Shati lenyewe lilikuwa jepesi. Miguu yake ilikuwa ni ya kuvutia. Alikuwa mwembaba isipokuwa mahali ambapo hakutakiwa kuwa mwembaba. Reacher alibaki amesimama tu.

"Za asubuhi, Reacher," Jodie alisema.

"Safi tu, Jodie," Reacher alijibu.

Jodie alikuwa anamuangalia. Macho yake yalikuwa yanatalii mwili wa Reacher.

"Hilo jeraha," Jodie alianza kuongea. "Linatisha."

Reacher alijiangalia. Jeraha lilikuwa jekundu na bichi bado.

"Umepaka dawa?"

Reacher alitikisa kichwa kukataa. "Hapana. Nilisahau."

"Kalete hembu." Jodie alisema.

Reacher alirudi hadi bafuni na kuichukuwa dawa. Alirudi nayo hadi sebuleni. Jodie alichukua kutoka kwenye mikono yake na kufungua mfuniko. Alidumbukiza kidole chake cha shahada na kuibuka nayo kidogo. Alikuwa makini huku akiwa kaung'ata ulimi wake. Alianza kuipaka dawa kwenye lile jeraha. Reacher alibaki amezubaa tu. Jodie alikuwa karibu naye kimwili. Tena akiwa kavaa tisheti tu bila kitu chochote kwa ndani. Huku akimshikashika kifuani. Alitamani amkumbatie. Alitamani ambusu kuanzia kwenye shingo yake. Alitamani amwambie ainue uso wake ili ambusu midomo yake. Reacher alijikuta anamshika mkono Jodie.

"Ninakuumiza?" Jodie aliuliza.

"Unasema?"

"Nilikuwa nakuumiza?"

"Kidogo." Reacher alijibu.

Jodie alitikisa kichwa kukubali. "Pole ni dawa chungu, ila mgonjwa anaihitaji."

"Upo sahihi." Reacher alisema.

Halafu ikaishia hapo. Jodie alifunga kopo la ile dawa na kuinuka hadi ilipokuwa jokofu. Hakuna anahitaji kitu kwenye jokofu. Alienda alimradi tu. Aliifungua na kutoa ndizi na kuiweka mezani. Sio kwamba alikuwa anaihitaji, ila alijikuta tu.

"Ninaenda kuvaa," Jodie alisema. "Inatakiwa tuanze kuondoka."

"Ok, Mimi pia acha nijiandae."

Jodie aliondoka kuelekea chumbani. Reacher alichukua ile ndizi na kuila. Alipomaliza alirudi chumbani ambako alivaa shati lake. Na kulichomekea na juu akavaa tena mkoti wake. Halafu akatoka tena kurudi sebuleni kumsubiria Jodie.

Akiwa hapo akaliendea dirisha na kufungua kuona usalama kwa nje. Jua ndio kwanza lilikuwa linatokea. Kulikuwa na watu pia wanatembea kuwahi maofisini. Magari yalikuwa yanapishana hapa na pale.

Jengo lenyewe lilikuwa lipo mashariki mwa Broadway. Magari yalikuwa yanapita kwa njia moja tu. Kwa hivyo ili Jodie atembee kufika kazini ingempasa atumie upande wa kulia wa barabara. Halafu angetembea kuzivuka jengo kadhaa kabla hajafika ofisini kwake.

Kwahivyo wale watu wangetaka kumteka watatumia njia gani? Fikiria kama adui yako. Fikiria kama wale wanaume wawili. Ni kweli wale wanaume walikuwa na mionekano ya kazi, lakini bado uwezo wao ulikuwa ni kiwango cha kawaida. Hakuna ubishi njia ambayo wangeitumia ilikuwa wazi tu. Watakuwa na gari la milango minne litakaloegeshwa mtaani hapo. Labda nyumba ya tatu kutokea hapo kwa Jodie. Lazima watakuwa wamekaa siti za mbele kwenye gari lao wanasubiria. Watategemea Jodie atokee usawa wao halafu asimame kidogo baada ya kusikia honi. Halafu dereva atasogeza gari na kuliegesha pembeni yake. Mwanaume wa nyuma atafungua mlango na kumvuta Jodie kwa nguvu aingie kwenye gari.

Tukio moja la akili nyingi kidogo. Akili nyingi, lakini halina ugumu wowote. Hakuna ugumu kabisa. Likiwa na asilimia nyingi za kufaulu, kutegemea na mlengwa. Reacher alikuwa amefanya tukio kama hilo, mara nyingi sana, kwa walengwa tofauti wenye nguvu na uelewa kuliko Jodie. Kuna mara moja aliwahi kulifanya hilo tukio huku Leon mwenyewe akiwa ndiye dereva. Kwahivyo alikuwa anafahamu namna inavyofanyika.

"Nipo tayari. Tunaweza kwenda." Jodie alimshtua.


MUDA HUOHUO TONY na yule mwanamume walikuwa wanashuka kutoka ghorofa namba themanini na nane kushika yalipokuwa maegesho ya gari.

"Inatakiwa tutumie hiyo gari kubwa." Yule mwanamume alimwambia Tony.

"Sawa," Tony alisema. Alilifungua gari na kuingia upande wa dereva. Yule mwanaume alifuata kwa nyuma na kukaa kiti cha upande wa abiria. Tony aliwasha gari na kuanza kuungia mtaa.

"Kwahivyo tunatekelezaje huu mpango?" Tony aliuliza.

Yule mwanaume alitabasamu kwa kujiamini.

"Ni rahisi sana. Lazima atakuwa anatembea barabarani upande wa watembea kwa miguu. Sisi tutaegesha gari kwenye kona moja wapo ili anapotokea tu tunasimamisha na kumchukua. Hivyo."

"Umekosea," Tony alisema. "Tutatumia njia tofauti."

"Kwanini?" Yule bwana aliuliza huku ametoa jicho la mshangao.

"Kwasababu hauna akili," Tony alimwambia. "Kama hivyo ndivyo ambavyo wewe unapanga ungefanya basi lazima kuna njia bora zaidi. Ulizingua kule Garrison basi utazingua na hapa. Nina uhakika huyu binti yupo na huyo Reacher na kama walikupiga kule na hapa atakupiga pia. Kwahivyo mawazo yako siwezi kuyatumia hata kidogo."

"Kwahivyo tutafanya nini?" Yule mwanaume aliuliza.

"Naomba utege masikio vizuri," Tony alianza kuongea. "Nitakueleza kwa utaratibu kwa hivyo unisikilize vizuri sana."

ITAENDELEA...
 
Nimekuelewa, mkuu. Ila ingependeza kama mngekuwa pia mnamjali mwandishi [emoji23][emoji17]. Apate hata za maji ya kunywa na data...
Nadhan hili ni muhimu sana, kuandika si mchezo, uwaze, usome, uandike, uhariri, si kazi rahis kabisa
 
  • Thanks
Reactions: ADK
Nadhan hili ni muhimu sana, kuandika si mchezo, uwaze, usome, uandike, uhariri, si kazi rahis kabisa
Haha! Ukitaka namba ya kufanyia muamala DM. Ni kwa hiari lakini. 😂
 
Wakuu, nina ombi kidogo. Riwaya inaendelea. Lakini kwa yeyote ambaye anaona umuhimu wa kutoa kifuta jasho kwa mwandishi anakaribishwa. Kiasi chochote kinatosha.

Namba ya halopesa: 0621391581.

Jina: Chacha Steven.
Umesikika ila hii no c rafiki kwa wengi embu km una tg pesa, airtel money ama m pesa tuwekee na mkono wa Bwn utakugusa[emoji120]
 
Hivi hii hadithi ndio ilishakomeaga hapa? Naikumbuka hii stori kwenye movie ya Jack Reacher
 
Back
Top Bottom