Brodre
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 2,585
- 1,771
- Thread starter
-
- #361
SIN 159
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
Akachukua begi lake na kutoa baibui lake, akachomoa bastola yake aliyo iweka chini ya siti ya gari lake ambapo sio rahisi kwa mtu kuweza kuiona. Akalivua baibui hilo na kujifunika uso wake na kitambaa cha baibui hilo. Akafunga kiwambo cha kuzuia sauti kwenye bastola yake kisha akaichomeka kiunoni. Alipo hakikisha kwamba amejikamilisha kwa kila kitu. Akashuka kwenye gari lake na kuanza kutembea kwenye mtaa huo ulio tulia na hauna hata watu wanao katika katiza. Akafika katika geti la Magreth na kulitazama kwa sekunde kadhaa kisha akarudi nyuma kwa sekunde kadhaa kisha kwa kasi ya ajabu akakimbia na kuupanda ukuta huo kwa kasi hiyo ambayo, kwa uwezo wake wa mazoezi haikuwa kazi ngumu kuuruka ukuta huo na kutua ndani ya nyuma ya Magreth.
ENDELEA
Jackline akaanza kunyata kwa umakini huku bastola yake akiwa ameishika kwa umakini mkubwa sana. Akalisogela dirisha hilo la kioo, taratibu akalisogeza, kitendo cha kufunua pasia. Magreth akastuka na kutazmaa dirishani hapo kwani alihisi kama kuna mtu ameingia katika nyumba yake ila alihisi ni ndoto. Jackline hakutaka kufanya makosa akaanza kufyatua risasi zilizo mfanya Magreth kujirusha upande wa pili wa sofa na risasi hizo kwa bahati nzuri hazikuweza kumpata. Magreth akajikagua kiononi mwake na kukuta hana bastola yake, akakumbuka kwama bastola yake hiyo ameiacha ndani ya gari lake lililopo nje hapo alipo adui. Jackline akatulia kwa sekunde kadhaa huku akisikilizia kama risasi hizo alizo zifyatua kama zita kuwa zime zaa matunda. Mapigo ya moyo ya Magreth yakazidi kumuenda kasi kwani kama mtu amemfwata hadi nyumbani kwake kwa ajili ya kumuua basi mtu huyo ana jiamini sana. Simu ya Magreth iliyopo mezani ikaanza kuita na kumstua Jackline ambaye bado amejibanza dirishani. Jackline akafyatua risasi mbili ambazo moja iliipiga simu hiyo na ikapasuka hapo hapa huku risasi nyingine ikipasua meza hiyo ya kioo na ikachanguka vipande vipande.
Magreth akashusha pumzi yake kwa sekunde kadhaa kuhakikisha kwamba ana punguza wasiwasi na kufikiria nini cha kufanya ili kupambana na adui yake huyo.
‘Nina bastola ndani’
Magreth alijisema kimoyo moyo. Akaiona rimoti ya redio ikiwa karibu naye, akaivuta kwa umakini kisha akawasha redio hiyo na kuweka mziki mkubwa jambo lililo mchanganya Jackline ambaye kitendo cha kuitazama redio hiyo, ikampa nafasi Magreth kunyanyuka kwa kasi na kukimblia ndani kwake. Akafungua droo ya dreasing table na kutoa bastola yake pamoja na magazine. Akaichomeka magazine hiyo iliyo jaa risasi. Akafungua kabati lake na kutoa nguo zake za kufanyia kazi na uzuri wa nguo hizo haziingii risasi kwa maana zime tengenezwa kwa utaalamu mkubwa unao weza kumlinda mtu anaye zivaa. Magreth akatoka sebleni kwa kujiamini, Jackline akanza kufyatua risasi mfululizo ambazo zote zilimpiga magreth kifuani mwake, jambo lililo muacha mdomo wazi Jackline ni jinsi risasi hizo zinavyo dunda na kuanguka chini. Magreth akaanza kufyatua risasi zilizo toka na milio mikubwa kwa maana bastola yake hajaifunga kiwambo cha kuzuia risasi. Jackline alipo ona mambo yama muwia ugumu akaona isiwe shida. Akaanza kukimbilia getini kwa uharaka akafungua na kuanza kukimbia kwa kasi kuelekea kwenye gari lake. Magreth akaanza kuitafuta fungua yake na kuikuta ikiwa katika sehemu alipo angukia, akaichukua na kufungua mlango wa mbele na kukimbilia nje. Akamuona mtu huyo aliye valia baibui akiwa ana ingia kwenye gari nyeusi. Magreth akarudi ndani na kuchukua funguo ya pikipiki yake, akatoka nje na kupanda pikipiki hiyo, akaigeuza kwa utaalamu wa hali ya juu na kutoka nje. Akalishuhudia gari hilo lilikunja kona ya kushoto inayo ingia mtaani kwao. Akavuta mafuta ya kutosha huku akiwa ameihimili vizuri pikipiki hiyo. Akaliona gari hilo likiwa lina endeshwa kwa mwendo wa kasi saha na yeye akazidi kuendesha gari hilo kwa mwendo wa kasi.
Kwa kupitia kioo cha pembeni, Jackline akamuona Magreth akiwa katika pikipiki na akimfukuzia kwa kasi ya ajabu sana.
“Shitii”
Jackline alizungumza huku akizidi kukanyaga mafuta ya gari lake hili aina ya BMW SERIES 7 yenye speed 260 KM/H. Uwezo wa pikipiki ya Magreth nayo haitofautiani sana na gari hilo kwani kadri jinsi Jackline anavyo ongeza mwendo kasi wa gari hilo ndivyo jinsi Magreth anavyo zidi kumsogelea. Jackline akaichukua simu yake na kuitafuta namba ya nabii Sanga. Akampigia na simu ikapokelewa.
“Vipi?”
“Aisee huyu mtu wako ni jini?”
“Nani?”
“Huyu Magreth”
“Kwa nini?”
“Nimekwenda kumvamia nyumbani kwake, ila nikimpiga risasi hafi”
“Hafi ina kuwaje hafi?”
“Sijajua na hapa ninavyo kuambia ana nifukuzia kwa pikipiki?”
“Ohoo upo wapi kwani?”
“Kigamboni?”
“Ila si una mmudu?”
“Nita mmudu vipi mtu ambaye hata risasi haiingia mwilini mwake na amevalia zile nguo ambazo ulisema kwamba una nishonea”
“Duuu kwa hiyo itakuwaje?”
“Hapa cha msingi ni kutafuta namna ya kujiokoa tu”
“Fanya hivyo Jack nina kuaminia”
“Poa”
Jackliene akakata simu na kuiweka pembeni, mshale wa speed kwenye dashboard ina elekea kwenye namba 240. Speed iliyo sababisha gari hilo kuanza kutoa mlio wa kumuashiria dereva apunguze mwendo kwani akizidi kwenda kasi zaidi basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata ajali. Maandishi ya alama nyekundu yanayo onekana kwenye tv ndogo iliyopo ndani ya gari hilo, yana zidi kumsisitizia Jackline kupunguza mwendo. Magreth akachomo bastola yake kwenye eneo alipo ichomeka katika paja lake na kuanza kufyatua risasi kuelekea kwenye gari hilo. Wananchi walio isikia milio hiyo ya risasi na jinsi gari na pikipiki hiyo zinavyo pita kila mtu alijihami kwa kutafuta sehemu ya kuokoa maisha yake kwa maana ni wananchi wengi wana hofu kwani toka kutokee milipuko ya mabomu kila mmoja haamini usalama kabisa wa nchi yake.
***
“Mkuu njoo uone”
Mmoja wa vijana wa kitengo cha NSA, alimuambia bwana Msangi video inayo rekodiwa kutokea juu kwa kupitia sattelaite.
“Itume kwenye screan kubwa”
Bwana Msangi alizungumza huku akiyahamishia macho yake kwenye screan kubwa iliyopo ndani ya chumba hicho. Kila mmoja akashangaa kuona jinsi pikipiki inavyo ifukuzia gari hiyo.
“Ni Magreth”
Bwana Msangi alizungumza huku akitoa simu yake mfukoni na kuanza kumpigia simu Magreth, kwa bahati mbaya akakuta simu yake ikiwa haipatikani.
“Shitt hapatikani. Ana hitaji kupatiwa msaadaa. Timu D7 ondokeni na helicopter hakikisheni muna izuia hiyo gari”
Bwana Msangi alizungumza kwa kinasa sauti. Vijana watano walio valia nguo nyeusi, ambazo ndio sare kuu ya kitengo hicho cha NSA, pamoja na majaketi ya kuzuia risasi, yenye maandishi makubwa meupe mngononi na kifuani yanayo someka NSA. Wakaingia kwenye helicopter huku kila mmoja akiwa ameshika bundiki yake pamoja na kuvalia kinasa sauti. Rubani wa helicopter hiyo ya kitengo cha NSA. Akaanza kuipaisha juu taratibu na ikaanza kuelekea eneo wanapo elekea Magreth na mtu huyo ambaye hawamfahamu hadi sasa. Halikuwa jambo gumu helicopter hiyo kufika katika barabara hiyo wanayo fukuzana Magreth na Jackline.
“What’s fuc**”
Jackline alitukana mara baada ya kuoan helicopter ya kitengo cha NSA ikipita juu yake. Magreth akatabasamu kwa maana amepata msaada huo. Jackline akashusha kioo cha upande wake taratibu kidogo kisha akaanza kushambulia helicopter hiyo.
“Mkuu tumshambulie?”
Kijana mmoja alizungumza kwa kupitia kinasa sauti chake huku wakisubiria amri ya kulishambulia gari hilo kwa manaa sehemu walipo wana liona vizuri na hata dereva wana uwezo wa kumpiga risasi.
“Hapana ina bidi tumpate hai”
Bwana Msangi alizungumza na vijana hao walio jipanga vizuri ndani ya helicopter hiyo wana hakikisha wana mzuia mtu huyu pasipo madhara yoyote. Magreth akautazama mkono wa Jackline ambaye akili yake yote kwa sasa ina izingatia helicopter hiyo. Akafyatua risasi moja iliyo mpiga Jackline mkononi na kusababisha bastola yake kuanguka barabarani.
“Fuc**”
Jackline alilia kwa maumivu makali huku akiurudisha mkono wake huo wa kulia ndani ya gari. Damu zinazo mtoka kwa wingi zikamfanya ahisi kuchanganyikiwa. Amefanya kazi nyingi sana za ujasusi ila hakuwahi kupigwa sirasi hata siku moja na wala hayajui maumivu ya risasi.
“No siwezi kufa”
Jackline alilalama huku akiendelea kuongeza mwendo. Jackline macho yakaanza kumtoka mara baada ya gari lake kuanza kupungua mwendo taratibu huku alama zinazo muashiria kwamba gari hilo lime kwisha mafuta zikianza kuoenkana.
“Mother fuc*. Fuc* me”
Jackline alilalama huku akipiga piga mskani wa gari lake kwa kutumia mkono wa kulia. Taratibu gari hilo likasimama katikati ya barabara, Magreth akasimisha pikipiki yake mita chache kutoka sehemu lilipo gari la Jackline, akashuka kwenye pikipiki huku bastola yake ikiwa mkononi. Helicopter hiyo ya NSA, taratibu ikatua katikati ya barabara hiyo na askari wa kitengo cha NSA, wakashuka huku bunduki zao wakizielekezea kwenye gari hilo.
“No siwezi kufa”
Jackline alizungumza huku jasho likimwagika mwili mzima. Damu nazo hazikuacha kumwagika kwa maana risasi hiyo ime piga katika mshipa una safirishia damu na ime toboa na kutoke upande wa pili wa mkono. Simu yake ikaanza kuita, akaitazama na kukuta ni nabii Sanga. Akaichukua na kuiweka sikioni mwake.
“Vipi ume fikia wapi?”
“Nime zingirwa. NSA na yule malaya wame zingira gari langu. Bye”
Jackline mara baada ya kukata simu hiyo akaiweka pembeni na ndani ya sekunde kumi na tano simu hiyo ika jifunga kwa namba za siri ambazo ni yeye pekee tu ndio ana zifahamu na ubaya ni kwamba simu yake ni Iphone X ambazo zime tengenezwa katika ubora wa hali ya juu, zinazo muwezesha mtumiaji wa simu hiyo kuweka neno la siri ambalo hata watundu wa mambo ya I.T wajaribu kuifungua hawato weza, tofauti na simu nyingine ambazo ulinzi wake ni mdogo hata kama mtu ame ingiza neno la siri. Magreth akavunja kioo cha dereva kwa kutumia kitako cha bastola yake na kwa ishara akamuomba Jackline kushuka kwenye gari.
Jackline akawatazama askari wa kitengo cha NSA ambao wame simama mbele ya gari hilo huku banduki zoa wakimuelekezea yeye, akamtazama Magreth aliye mnyooshea bastola yake.
‘Sihitaji kufa’
Jackline alijisema kimoyo moyo huku akinyoosha mkono wa kushoto juu na kushuka kwenye gari hili akiashiria kwamba ame sarenda. Magreth akamvua kitambaa cha usoni mwake, macho yakamtoka mara baada ya kumkuta ni mtu ambaye wana mtafuta kwa udi na uvumba kuhakikisha kwamba wana mzuia katika kusitisha zaoezi la kumuua makamu wa raisi wa nchi ya Marekani.
***
Nabii Sanga akahisi kichwa kina mpasuka kwa maumivu. Akamtazama Julieth ambaye naye tumbo la woga lina mkata kisawa sawa.
“Baba tuna fanyaje sasa?”
“Yaani hata sijui na nina hisi ata kuwa amekamatwa”
“Akikutaja baba si familia nzima tuta chinjwa sisi?”
“Yaani sielewi mwanangu ita kuwaje”
Nabii Sanga alihahaa huku ajsho likimwagika mithili ya mtu aliye toka kuoga.
“Nenda ikulu”
“Wapi!!?”
Julieth aliuliza kwa mshangao mkubwa sana.
“Ikulu”
“Kufanya nini baba?”
“Nenda kahakikishe una jua wapi alipo pelekewa Jackline na tuta jua jinsi gani ya kutumia nguvu ya pesa katika kumuachia”
“Baba hivi una mjua vizuri yule mzee? Nimkali hana masihara na toka mke wake afe ame kuwa ni mtu asiye hitaji hutani hata kidogo na majambazi”
“Sasa una taka kukaa hapa ili iweje, tuje kukamatwa au?”
Nabii Sanga alizungumza kwa kufoka huku akimkazia macho Julieth aliye jikuta akikaa kimya.
“Usisahau ume kwenda ikulu kufanya kitu gani, nina hitaji uhakikishe una jua kila kinacho endelea juu ya huyo msichana”
“Sawa baba”
“Fanya hivyo sasa hivi”
Nabii Sanga alizungumza kwa kukoroma huku wasiwasi wake ukiwa ni kwenye simu zake alizo piga na kupigiwa na Jackline.
‘Siwezi kushikwa kirahisi namna hii’
Nabii Sanga alizungumza huku akijaribu kutafakari nini cha kukifanya. Akapata wazo, kwa haraka akaingia bafuni, akaoga kwa haraka na kurudi chumbani, akatafuta suti moja kali sana na kuiva. Akatoka nje na kumfwata msaidizi wake wa kanisani kwake.
“Nina omba uwatangazie waumini wetu kwamba tuna kongamano la kuiombea nchi litakalo anza leo saa kumi kanisani pale”
“Sawa nabii”
“Pia waambie watu wa dini zote wana karibishwa. Nime pewa maono sasa hivi na Mungu, ina bidi kuliombea taifa na kulitoa kwenye hali ya matatizo tunayo kabiliwa”
“Sawa sawa mtu wa Mungu”
Msaidizi wake huyo alizungumza kwa upole na unyenyekevu wa hali ya juu. Laiti kama engefahamu upande wa pili wa kiongozi wake huyo wala asinge thubutu kufungua kinywa chake na kumuita mtu wa Mungu.
“Baade tuta wasiliana”
Julieth alimuambia baba yake huku akipanda kwenye gari lake na wakaondoka nyumbani hapo na walinzi hao ikulu na kuianza safari ya kuelekea ikulu.
***
“Kazi nzuri sana Magreth”
Raisi Mtenzi alizungumza na Magreth kwa kupitia video call.
“Shukrani sana muheshimiwa”
“Nina kupa mamlaka ya kumuhoji huyo mtuhumiwa. Tumia kila aina ya uwezo na nguvu ulizo nazo kuhakikisha kwamba una muhoji na ana wataja walio muagiza”
“Sawa muheshimiwa. Tume ipata simu yake hapa nina imani kupitia hii simu tuna weza kujua ni nani ambaye alimtuma”
“Sasa chochote mutakacho kihitaji basi nipo tayari kuwapa ushirikiano wa asilimia mia moja”
“Nashukuru kwa hilo muheshimiwa”
Magreth akaka simu hiyo na raisi Mtenzi akamtazama Josephine aliye tawaliwa na tabasamu pana usoni mwake.
“Hakika Mungu aliyemo ndani yako ni Mungu wa kweli”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwa na furaha kubwa sana.
“Nina shukuru sana muheshimiwa. Nipo kwa ajili ya kuisaidia hii nchi, nina imani kwamba hapata kuwa na jambo lolote baya litakalo jitokea endapo nita kuwa hai”
“Mungu ni mwema ata kupa maisha marefu. Hata kipindi changu cha uongozi kitakapo kwisha basi nina imani hata huyo raisi ajaye uta shirikiana naye vizuri katia kuiongoza hii nchi iende katika mstari mzuri na unao faa”
“Amen”
“Basi nenda kaendelee na kazi na endapo kuta kuwa na jambo lolote utakalo lihitaji nina omba uni fahamishe”
“Sawa muheshimiwa”
Josephine akatoka ofisini hapo na kuaelekea ofisini kwake, kwenye kordo akakutana na Julieth anaye tembea kwa mwendo wa haraka huku akionekana ana wahi jambo fulani.
“Hei Julieth”
Josephine alizingumza huku akimsimamisha Julieth.
“Nini?”
Julieth alijibu kwa hasira kidogo huku akimpita Josephine ambaye hakuhitaji kujisumbua kuhisi chochote kwa maana alimshuhudia Jery akiingia ofisini kwa baba yake asubuhi hiyo akiwa katika hali ya hasira. Julieth akasimama kwenye mlango wa kuingia ofisini kwa raisi Mtenzi. Akavuta pumzi nyingi na akazishusha taratibu, akaingia ofisini hapo kwa mwendo wa taratibu huku usoni mwake akiwa na furaha hafifu ambayo moja kwa moja raisi Mtenzi alitambua ni kutokana na kukosana kwake na Jery.
***
Magreth akakabidhi bastola yake mapokezi na kuingia katika chumba cha mahojiano alipo wekwa Jackline ambaye tayari amesha patiwa matibabu ya mkono wake ulipo pigwa risasi. Magreth akavuta kiti na kukaa mbele ya Jackline aliye fungwa pingu mikononi na nyororo miguuni mwake. Katikati yao wame tenganishwa na meza ya chuma mbayo ime jengwa chini na haiwezi kusogea. Magretg akatazama kamera nne zilizo fungwa kwneye kila kona ya chumba hicho na zina rekodi kiloa kitu kinacho zungumzwa ndani hapo.
“Najua aliye kuagia uniue, sasa hivi ata kuwa ana pata tabu sana akiwaza ni kwa nini ume kamatwa”
Magreth alizungumza huku akiweka simu ya Jackline juu ya meza hiyo. Jackline hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kuendelea kumtazama Magreth ambaye amevua kofia ya juu ya nguo yake hiyo aliyo ivaa na kumfanya sura yake kuonekana vizuri sana.
“Mdada mzuri, mwenye kipaji chake kizuri, una hadaika na pesa kwa ajili ya kuhitaji kunia mimi na kumuua makamu wa raisi wa nchi ya Marekani. Hivi huyo aliye kutuma kwa nini usinge mueleza aifanye kazi hiyo peke yake kama kweli ana kupenda?”
Maneno ya Magreth yaka mstua sana Jackline kwa maana ana tambua kwamba dili hilo la nabii Sanga hakuna mtu mwengine anaye lifahamu zaidi yake.
“Jackline ume salitiwa na mtu aliye kupa hii kazi. Jiulieze, tulikujuaje kama upo Tanzanai, jiulize nime juaje kama una mpango wa kunia mimi na kumuua makamu wa raisi kesho kutwa. Huyo aliye kutuma ame kudanganya na hana mpango wa kukulipa hata kiasi hicho cha pesa mulicho kubaliana. Niambie ni nani huyo aliye kuagiza ili tujue jinsi ya kukusaidia kwa maana huna hatia yoyote, aliyopo nyuma yako ndio mwenye makosa”
Magreth alizungumza kwa upole sana kiasi cha kumfanya Jackline moyo wake kumuua na kuamini kwa asilimia kadhaa kwamba nabii Sanga ame muuza kwenye dili hilo.
“Nipo tayari kumtaja aliye niagiza ila kwa sharti moja”
Magreth na kila mtu anaye fwatilia mahojiano hayo katika chumba cha pili chenye tv nne akastuka kwani ime kuwa rahisi sana kwa binti huyo kuzungumza ukweli tofauti na vile walivyo kuwa wame tarajia.
****************************************************************************************************************
***
ITAENDELEA
Haya sasa, Jacklinea ameingia mikononi mwa vyombo vya ulinzi. Amesema yupo tayari kumtaja yule aliye muagiza kwa sharti moja tu. Sasa sijui ni sharti gani hilo ambalo ana kwenda kulitaja ikiwa ame hisi kwamba nabii Sanga ame msaliti kwenye kazi hiyo? Usikose sehemu ya 160.