SIN 115
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Ehee Mungu wangu!!!”
Josephine alihamaki.
“Kuna nini?”
“Zime baki dakika ishirini kabla ya kile jambo kukamilika”
“Acha likamilieke tu, sisi si tupo mbali”
Levina alizungumza kana kwamba kitu kinacho kwenda kutokea ni cha kawaida kabisa.
“Levina kumbuka kuna watoto na wana wake ambao wana kwenda kufa pasipo hatia ya aina yoyote”
Josephine alizungumza kwa msisitizo huku machozi yakimlenge lenga usoni mwake. Magreth akashusha pumzi na kumuona jinsi rafiki yake anavyo pata maumivu ya moyo. Josephine akaanza kusali na kumuomba Mungu kama ikiwezekana basi kisasi hicho cha Al-Shabab aweze kukiepusha kwenye ardhi ya Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
ENDELEA
Gafla Josephine akaanza kuhisi kizungu zungu, akajaribu kusimama ila akastukia akiaanguka chini na akazimia. Magreth na Levina wakajikuta wakishangaa sana kwani hali kama hiyo hawajawahi kumuona nayo Josephine. Wakamnnyanyua kwa haraka na kumlaza kitandani, wakafungua vifungo vya shati lake pamoja na suruali ailiyo ivaa.
“Amezimia hiyu”
Levina alizungumza huku akiwa ana mpima Josephine mapigo yake ya moyo.
“Vipi tumpelekea hospitali?”
“Hapana ata kaa sawa tu”
Levina alizungumza kwa kujiamini kwa maana ana ujuzi kidogo kwenye maswala ya udaktari kwani marehemu mama yeke elikuwa ni dokta.
***
Omary hakucheza mbali sana na hoteli ambayo maharusi na familia zao wamekusanyika eneo hilo. Wapambe pamoja na waandishi wa habari nao pia wapo hotelini hapo kuhakikisha wana shuhudia kila kinacho endelea katika sherehe hiyo. Omary akaitazama saa yake ya mkononi na ima bakisha dakika tano kabla ya mambo waliyo tatege kwenye simu zaina za Nokia, kulipuka.
“Hii hoteli ni nzuri sana”
Julieth alizungumza huku akitazama tazama eneo la hoteli hiyo.
“Baba aliichagua hoteli hii kw amaana ni mpya na pia upo pazuri sana”
“Hei baby una jua ni watu wengi wapo nje wana tusubiria. Njoo uone”
Jery akasogea dirishani hapo na kutazama nje, akaona jinsi watu walivyo kusanyika wakiwa wana wasubiria japo wawaone tu kwa macho.
“Harusi yetu ime weka historia Tanzania”
“Ni kweli ime weka historia.”
“Mke wangu una weza kunipa kidogo?”
“No baby acha totoke ukumbini, nitakupa hadi uchoke mwenyewe. Tambua zime baki dakika mbili tu tuelekee eneo la kupiga picha”
Mlango wa chumba chao uka gongwa. Jery akatembea hadi mlangoni na kuufungua.
“Baba”
“Ahaa nina weza kuingia?”
“Ndio”
Raisi Mtenzi akaingia ndani hapo.
“Nina imani mume pumzika vya kutosha?”
“Ndio baba”
“Basi twendeni kuna viongozi nina hitaji kuwatambulisha kwao”
Jery akamshika mkono Julieth kisha wakatoka chumbani hapo. Wakaingia ndani ya lifti wakiwa na walinzi wao wawili. Galfa mtikisiko mkubwa ukatokea katika jengo hilo, umeme uka katika na kusababisha hofo kubwa kwa raisi Mtenzi pamoja watu wote.
Mlipuko mkubwa ulio tokea eneo alilo kuwa amesimama Omary na kumgawanyisha vipande vipande, ukawadhuru watu wote walipo eneo hilo. Magari na kila kitu kilichopo eneo hilo kiliweza kulipuka vibaya sana. Maeneo mbali mbali ndani ya jiji la Dar es Salaam ambapo zilitupwa simu na maeneo ambayo vijana hao wa Al-Shabab walisambaa maeneo yote yalilipuka kwa mabomu hayo ambayo ni makubwa sana. Vilio vilizidi kutanda na kutawala maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Majengo mengi yalivunjika mithili ya biskuti zinavyo vunjwa vunjwa. Hapakuwa na eneo la kukimbilia kwani milipuko hiyo ni mikubwa sana na ime dhuru eneo kubwa sana.
***
Mzee Mbogo na vijana wake wote macho yamewatoka. Kila mmoja alihisi kwamba habari za mashambulizo hizo ni propaganda tu katika mitandoa ya kijamii. Wengi wao machozi yalianza kuwamwagika, video inayo rekodiwa na satelati, ina onyesha milipuko mbalimbali jinsi inavyo tokea ndani ya jiji la Dar es Salaam.
“Mkuu”
John alimuuita Mzee Mbogo huku akimtazama usoni mwake.
“Mmmm”
“Hali ime tokea kama hivyo. Tuna fanyaje?”
“Hatuna la kufanya ila kusema katika hili”
Mzee Mbogo akaondoka ndani hapo na kuingia chumbani kwake. Kila akifumba macho ana ona jinsi milipuko hiyo ikiendelea kulipuka katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam. Mzee Mbogo akatoa simu yake, akaitafuta namba ya Evans, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akampigia. Simu ya Evans ikapokelewa.
“Kijana”
Mzee Mbogo alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyonge ndani yake.
“Ndio muheshimiwa”
“Wewe ni nani?”
“Kivipi mzee wangu mbona sija kuelewa?”
“Ulijuaje kama Al-Shabab wata shambulia leo?”
“Kama nilivyo kuambia nilipewa maono na Mungu ndio maana niliweza kukupa habari hiyo. Niliyo yazungumza yame timia”
“Malaki wa watu wame teketea na moto ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa nini hii habari hukuizungumza toka wiki iliyo pita ili hili janga lisiangamize watu wengi”
“Mzee wangu ilipaswa kutokaa hivi ili raisin aye aweze kujifunza. Kazi yangu mimi ni kutabiri tu na siwezi kuzia mambo kama hayo kutokea”
“Nahitaji kuonana na wewe. Niambie upo wapi?”
“Nita kufwata wewe ulipo ila usije nilipo.”
“Sawa nipo Morogoro”
“Natambua upo shambani kwako”
“Ume juaje?”
“Mungu akiwa na uwezo wa kumfunilia mtumishi wake basi ana uwezo wa kuona hata yaliyo jificha. Kama nina uwezo wa kuwaona mizimu, vibwengo ma majini basi nina weza kukuona hata wewe”
“Sawa nina kusubiria”
Mzee Mbogo akakata simu huku akiwa na huzuni kubwa sana. Kwenye maisha yake yote aliyo wahi kuishi duniani hajawahi kuona shambulizi kama hilo na baadhi ya mashambulizi ambayo kidogo yana endana na hilo, aliyashuhudia Iraq kipindi alipo kuwa chini ya jeshi la umoja wa mataifa, UN.
***
“Sasa ni wakati wa wewe jina lako kukua na huduma yako pia kukua”
Jini Maimuna alizungumza huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Nini nina paswa kufanya?”
“Una paswa kupona wagonjwa, una paswa kutoa misaada kwa watu na una paswa kuanzisha taasisi yako ambayo ita tambulika kitafita na uta wajengea watu wote nyumba zao zilizo bomoka. Ukifanya hivyo uta pata wafuasi wengi na wata kusujudia na hato kuwa Evans huyu wa sasa, bali uta kuwa ni Evans mwenye nguvu na mamlaka hata ndani ya serikali”
Jini Maimuna alizungumza msisitizo.
“Nina imani uta kuwa nami kwenye kila hatua?”
“Ndio sinto weza kukuacha”
“Sawa ina bidi leo hii niondoke na nielekee Morogoro nikaonane na mzee Mbogo.”
“Hakuna shaka tuta ondoka wote”
Mlango wa chumba cha Evans uka fungulia na akaingia mdogo wake.
“Kaka una zungumza na nani?”
“Kuna rafiki yangu nilikuwa nina zungumza naye kwenye simu”
“Ahha…..ume ona kilicho tokea leo Dar es Salaam?”
“Rafiki yangu ndio alikuwa ana nina taarifa hiyo”
Evans alizungumza huku akimtazama jina Maimuna ambaye mdogo wake hawezi kuomuona zaidi yake yeye pake yake.
“Daa yaani kuna ogopesha. Watu wame kufa hao, mabomu yame lipuka”
“Ndio hivyo mdogo wangu nina shukuru Mungu nilisha ondoka”
“Ni kweli?”
“Mama yupo wapi?”
“Mama yupo sebleni ana tazama habari hiyo”
“Sawa mimi nina hitaji kuondoka leo na kuelekea Morogoro”
“Mmmm kaka Morogoro na Dar si karibu, usije uka lipuka na wewe?”
“Hakuna kitu kama hicho siwezi kulipuka”
“Mmm sijui kama mama ana weza kukubalia”
“Usijali nita zungumza naye. Hakikisha una simamia mafundi wana maliza kujenga hiyo gorofa ya mwisho pamona na ukuta uta jengwa vizuri”
“Sawa, je hakuna fundi ambaye ana tudai?”
“Mafundi wote nilisha walipa hakuna anaye dai”
“Sawa kaka”
Mdogo wa Evans akatoka ndani hapo.
“Jiandae sasa tuondoke”
Evans akaingiza nguo kadhaa kwenye kibegi chake kisha akatoka ndani hapo. Akamueleza mama yake juu ya safari hiyo na hakuweza kupinga kwa lolote. Evans na jini Maimuna wakaingia kwenye gari jipya la Evans aina ya Toyoter Harrier new model na wakaianza safari ya kuelekea mkoani Morogoro
***
Magreth na Levina nao wakawa kama watu walio shikwa na bumbuwazi. Walihisi mlipuko una weza kuwa ni mmoja ila hawakuamini kuona jiji ambalo lilikuwa na magorofa makubwa na majumba ya kifahari kwa sasa lina teketea kwa moto huku magorofa hayo yakiwa yame katika katika. Levina akajaribu kuminya japo batani moja kwenye laptop yake hiyo ila akajikuta mikono yote ikimtetemeka kwa woga.
Hadi sasa rafiki yao Josephine bado jaja zinduka na wakaanza kuhisi kitu kilicho mfanya azimie ni hii hali wanayo iona hivi sasa.
“Levina”
“Mmmmm”
“Sa…sa…aa tuna fanya nini?”
“Sijui rafiki yangu. Nime amini Josephine ana tumiwa na Mungu. Piga picha na sisi tunge kuwepo eneo hilo”
“Ila hawa Al-Shabab wame wau watu wasio na hatia kwa nini wame fanya hivi?”
“Sijui”
“Nahitaji kukiteketeza kikosi chote cha Al-Shabab”
Magreth alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Una hisi ni jambo rahisi kama hivyo”
“Ita wezekana tu nilazima niwewe kufanya jambo”
“Mage usije uka sababishia watu balaa jengine.”
“Haijalishi ila nikiwa kama mtanzani ni lazima niwe na uchungu. Wale walio kufa pale sio panya au kuku, ni watu wale Levina. Kuna ndugu zetu pale, kuna rafiki zetu pale na pia kuna watoto na vichanga ambavyo havina hatia yoyote. Kwa nini wawaue, kwa nini wasinge lipiza kisasi kwa raisi Mtenzi mwenyewe na serikali yake”
Magreth alizungumza huku akilia kwa uchungu sana. Levina naye machozi yakaendelea kumwagi. Josephine akakurupuka na kuwakuta weake wakiwa katika haliya huzuni kubwa.
“Jose Jose ime tokea kweli”
Levina alizungumza huku naye akilia. Josephine kwa haraka akashuka kitandani na kusogea ilipo laptop ya Levina, akashika mdomo wake kwani dakika za mwisho hali hiyo ndio aliyo weza kuiona kwenye maombi yake na ilimstua sana hadi akazimia.
“Josephine muombe huyo Mungu wako na akuonyeshe ni wapi lilipo kundi la Al-Shabab nina taka kwenda kuwaua wote. Nina taka kwenda kuchinja kundi zima la Al-Shabab na kiongozi wao nina hitji kumleta hapa nchini Tanzania na kumkabidhisha kwa wananchi waweze kumtandika mawe hadi afe”
Magreth alizungumza huku akimshika Josephine mikono yake. Josephine hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kuendelea kuduwaa mithili ya mtu anaye anza kupandwa uwenda wazimu.
***
Gorofa ya hoteli waliyopo raisi Jery pamoja na familia yake, japo ime tengeneza kwa uimara wa hali ya juu, ila haikuweza kuhimili mlipuko huo wa bumo kubwa. Gorofa hilo likaanza kukatika vipande vipande huku rais, Jery, Julieth na walinzi wawil wakipigizw a pigizwa ndani ya lifti hiyo na kila mtu aliweza kumuomba Mungu wake aweze kumsaidia.
“Mungu wangu ni nini kimetokea ume usikia huo mtikisiko?”
Mrs Sanga ali hamaki huku wakiwa wamo ndani ya boti ya kifahari ambayo walikuwa wana ifanyia majaribio kabla ya kuinunua.
“Ndio, sijui hembu turudi”
Nabii Sanga alimuambia nahodha wa boti hiyo, kugeuza kwani hapo walio ni mbali na fukwe ya hoteli hiyo. Nahonda wa boti hiyo taratibu akaigeuka na wakaanza kurudi eneo lilipo hoteli.
“Mapigo yangu ya moyo yana nienda kasi mume wangu”
Mrs Sanga alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana.
“Usijali labda ita kuwa ni tetemeko la ardhi”
“Baharini?”
“Ndio”
Nabii Sanga alimtia matumaini mke wake, ila na yeye ame tawaliwa na wasiwasi mkubwa sana. Kila jinsi walivyo karibia nchi kavu ndivyo jinsi walivyo weza kushuhudia moshi mwingi mweusi ukiwa ume tanda kwenye anga la hoteli hiyo.
“Ohoo Mungu wangu”
Nahonda wa boti hiyo ambayo nabii Sanga walipanga kuinunua na kumpatia mtoto wao zawadi katika sherehe ya usiku, alizungumza huku akiwa ana tazama eneo la fukweni kwa kutumia darubini yake. Nabii Sanga kwa haraka akampokonya darubini hiyo na kuiweka machoni mwake. Nabii Sanga akajawa na mstuko mkubwa sana kwani hoteli ya gorofa hamsini, ime katika na zime baki gorofa tatu tuu huku kipande chote cha juu kikiwa kimetapakaa chini.
ITAENDELEA
Haya sasa, nabii Sanga na mke wake bahati ime kuwa upande wao. Wame salimika na hawakuwepo ndani ya hoteli hiyo je watoto wao watatu wata fanikiwa kuwa hai, ita kuwaje kwa upande wa raisi Mtenzi na familia yake? Usikose sehemu ya 116.