GoJeVa
Member
- Sep 15, 2021
- 41
- 60
RIZIKI ANAPANGA MOLA? AU JITIHADA?.
Nitafafanua andiko langu hili kwa kuzingatia mitazamo miwili, yaani mtazamo wa kidhanifu (hapa nitajikita kidini zaidi) na mtazamo wa kiyakinifu (hapa nitajikita kisayansi zaidi). Hebu tuangalie ufafanuzi huo kama ifuatavyo;
*UFAFANUZI KWA MTAZAMO WA KIDHANIFU.
Huu ni mtazamo unaoangazia zaidi kuhusu dini yaani tunaamini Mungu ndiye muweza wa yote. Vivyo hivyo hata katika suala la kupata riziki inaaminika Mola ndiye anagawa, mtazamo huu unazidi kutuaminisha kuwa kama leo hujapata riziki yako ni vizuri kuwa mvumilivu kwani kila mmoja ana fungu lake. Hivyo kuhusu swali letu lisemalo, RIZIKI ANAPANGA MOLA? AU JITIHADA?, kupitia mtazamo huu tunapata jibu kuwa RIZIKI ANAPANGA MOLA. Mtazamo huu, una mapungufu yake na ubora wake. Hebu tuanze kuangalia mapungufu ya mtazamo huu;
*MAPUNGUFU YA MTAZAMO WA KIDHANIFU.
-Mtazamo huu ni vigumu kuuthibitisha kisayansi, kwa sababu upo kiimani zaidi.
*UBORA WA MTAZAMO WA KIDHANIFU.
-Mtazamo huu unasaidia watu wasikate tamaa kwenye maisha, kwani wanaamini siku ya kufanikiwa itafika kwa msaada wa Mola.
*UFAFANUZI KWA MTAZAMO WA KIYAKINIFU.
Katika mtazamo huu sayansi ndio inaaminika, yaani tunaamini kitu baada ya kuona uhalisia na uthibitisho. Kwa mfano katika maisha kupitia mtazamo huu tunaamini ili mtu afanikiwe inambidi afanye kazi kwa bidii, kwa ufasaha na kwa kujituma. Mtazamo huu unapingana na mtazamo wa kidhanifu, kwa sababu mtazamo huu hauamini katika mipango ya Mola bali unaamini katika jitihada na kujituma.
*MAPUNGUFU YA MTAZAMO WA KIYAKINIFU.
-Mtazamo huu haumini mchango wa Mungu katika ugawaji wa riziki, kwa kifupi mtazamo huu unawapinga wanaoamini Mola katika kupata riziki.
*UBORA WA MTAZAMO WA KIYAKINIFU.
-Mtazamo huu unahamasisha watu kujituma na kufanya kazi kwa bidii.
*MAONI YA MWANDISHI.
Ni vizuri tuchukue mazuri kutoka katika kila mtazamo hapo juu, yaani tufanye bidii katika kazi zetu na tujitume kama vile mtazamo wa kiyakinifu unavyoeleza. Pia katika kujituma kwenye kazi zetu tumtangulize Mungu, kwani ndiye mpaji kama usemavyo mtazamo wa kidhanifu, hivyo tusisahau kumtanguliza Mungu katika harakati zetu za maisha za kila siku, wazawa wa lugha ya kiingereza wana msemo usemao; “One day yes.” Wakimaanisha tukifanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mungu tutafikia malengo yetu (sio tafsiri rasmi, ni tafsiri ya kimaana). Pia vijana wa kisasa wana msemo wao, usemao; “Kila hatua dua.” AHSANTE.

Upvote
3