Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Hata mimi sipendi kumwaga damu. Kwahiyo kama viongozi wanapaswa kuwasikiliza wa nchi
================
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Riziki Saidi Lulida, ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kulinda misingi ya amani na mshikamano iliyojengwa tangu kuasisiwa kwa Taifa, akisisitiza kuwa Tanzania imejengwa juu ya msingi wa uhuru wa kuabudu na kuheshimiana.
Lulida ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 26, 2025, wakati akihutubia katika Kongamano la Wanawake wa Dar es Salaam lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa DYCCC, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.
“Ndani ya nchi hii tuna uhuru wa kuabudu dini zetu. Hii ni misingi mizuri ambayo imejengwa katika Taifa letu la Tanzania. Wenzetu wanashangaa inakuwaje Tanzania hawamwagi damu wakati wa uchaguzi. Tusiruhusu damu kumwagika, ni jambo baya sana,” amesema Lulida.
“Amani ikipotea, hakuna mtu anayeinufaika. Mataifa yenye rasilimali nyingi bado yanakosa amani ya kudumu. Hivyo sisi Watanzania tuendelee kuilinda,” amesema.