Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mwanasheria wa kimataifa Robert Amsterdam apanga kufikisha madai kwenye Jumuiya ya Madola ya kuitaka jumuiya hiyo kuifuta uanachama Tanzania kutokana na mambo yanoendelea nchini hususan watu kutekwa, kuteswa na kuuliwa huku serikali inoongozwa na CCM ikikaa kimya bila kuchukua hatua yoyote.
Akihojiwa na Dr Nhigula katika mahojiano yaliyopo kwenye mtandao wa YouTube, bwana Amsterdam amesema pia kuwa watafikisha madai yao katika Umoja wa Afrika kuutaka umoja huo kuikumbusha serikali ya Tanzania iheshimu siasa za ushindani na utawala wa sheria.
Bwana Amsterdam ambae ana kampuni ya sheria ya Amsterdam and Parteners yenye makao yake nchini Uingereza kwa sasa afutilia kesi ya madai ya bwana Clifford dhidi ya Millicom ambayo ilikuwa ni kampuni mama ya Tigo, akitayarisha makabrasha kadhaa kuandaa keshi dhidi ya serikali ya Tanzania na kampuni ya simu ya Tigo.
Amsterdam atamwakilisha makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu katika kesi ambayo amepanga kuifungua dhidi ya serikali ya Tanzania akiishitaki kampuni ya Tigo kwa kutoa taarifa za mawasiliano na zile zinoonyesha mienendo yake kimtandao kwa serikali ya Tanzania ambako kulipelekea kufanyika kwa jaribio la kutaka kumuua huko Dodoma makao makuu ya serikali.
Jaribio hilo lilifanywa na kikosi cha watu wasojulikana mwaka 2017 mjini Dodoma na hivi karibuni Tundu Lissu amefunguka kwa kusema kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ambae wakati wa tukio hilo alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam alikuwa akiongoza kikosi hicho kufanya jaribio hilo la litaka kumuua.
Jumuiya ya Madola ni umoja unokutanisha mataifa 56 ambayo yalitawaliwa na Uingereza na mkuu wake ni Mfalme Charles III wa Uingereza. Afrika Kusini ilikuwa ni nchi ya kwanza kuondolewa katika umoja huo mwaka 1961 pale utawala wa makaburu kuweka sera za kibaguzi dhidi ya wazawa wa kiafrika. Afrika Kusini ilirejeshwa katika Umoja huo mwaka 1994 pale kwa mara ya kwanza kulipokuwepo na uchaguzi wa vyama vingi.
Fiji ni nchi ingine ilofukuzwa kutoka umoja huo baada ya kufanyika kwa mapinduzi na baadae kurejeshwa. Nchi zingine ambazo zilikufukwa na baadae kurejeshwa ni Zimbabwe, Pakistan, Nigeria na nchi ambayo hadi sasa ipo nje ya umoja huo ni Gabon ambayo iliondolewa mwaka jana baada ya kutokea kwa mapinduzi.