SI KWELI Robert Amsterdam amesema huu ni wakati mwafaka kwa Tundu Lissu kuchuana na Freeman Mbowe katika kuwania nafasi ya Uenyekiti wa chama

SI KWELI Robert Amsterdam amesema huu ni wakati mwafaka kwa Tundu Lissu kuchuana na Freeman Mbowe katika kuwania nafasi ya Uenyekiti wa chama

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu Salaam

Nimekutana na Taarifa kuokea Akaunti ya Mtandao wa X ukiwa na Post inayppnekana kuwa ni ya Robert Amsteram (Mwanasheria wa Tundu Lissu) akitoa maoni kuwa kwa sasa CHADEMA inatakiwa imruhusu Lissu kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa chama:

je kuna kuna ukweli hapa?

IMG_20241210_214612_550.jpg
 
Tunachokijua
Robert Amsterdam ni wakili wa kimataifa, mwanzilishi mwenza wa kampuni ya sheria ya Amsterdam & Partners LLP yenye makao yake makuu London na Washington, DC. Amejulikana kwa kushughulikia kesi kubwa za sheria za kimataifa, haki za binadamu, na masuala ya kisiasa, mara nyingi akiwakilisha wateja katika mazingira magumu au yenye utata wa kisiasa.

Amsterdam amehusika katika kesi mbalimbali zinazoangazia ukandamizaji wa haki za binadamu, migogoro ya kiuchumi, na sheria za kimataifa, akiwakilisha wanasiasa, mashirika, na hata makundi ya kijamii. Pia ameandika machapisho na maoni mengi kuhusu siasa za kimataifa, haki za binadamu, na utawala wa sheria.

Uhusiano wa Lissu na Robert Amsterdam
Robert Amsterdam alikuwa wakili wa Tundu Lissu, mwanasiasa wa Tanzania na wakili wa haki za binadamu, wakati wa masuala kadhaa ya kisheria na kampeni za kimataifa. Amsterdam alimwakilisha Lissu katika juhudi za kushtaki na kuibua masuala ya haki za binadamu, hususan baada ya shambulio la risasi dhidi ya Lissu mnamo Septemba 2017.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020 ambapo Lissu aligombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia (CHADEMA) Robert Amsterdam aliendesha kampeni za kimataifa kwa niaba ya Lissu kupinga kile alichokiita ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa kisiasa Tanzania kwa kuandika barua maalumu (Barua hiyo imehifadhiwa hapa).

Mnamo Desemba 9, 2024 imeibuka taarifa (hii) ya Mandao wa X (zamani Twiter) ikionekana kutumia jina la Robert Amsterdam ikiwa Uthibitisho wa tiki ya bluu ikiwa na maoni yanayoonekana kama ni ya Wakili huyo yanayopendekeza Tundu Lissu kugombea nafasi na Uenyekiti ndani ya CHADEMA ili kukifanya chama kipate tija zaidi. Katika andiko hilo hapo juu lililoletwa na Mdau wetu katika uzi huu limeandika:

Hii inahusu siasa za ndani za CHADEMA nchini Tanzania. Ninachokiona ni kizuri, na nadhani huu ni wakati mwafaka kwa Tundu Lissu kumkabili Freeman Mbowe kwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama. Hii italeta tija kwa CHADEMA.

Upi uhalisia wa posti hiyo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Taarifa hiyo haijawahi kuchapishwa katika ukurasa rasmi wa X wa Wakili Robert Amsterdam kama inavyoonekana Posti hiyo. Mara ya mwisho Robert Amsterdam kuchapisha katika ukurasa wake ilikuwa Desemba 5, 2024 mpaka kufikia leo Desemba 10, 2024. Chapisho lililoibuka linaonekana kuwa ni la Desemba 9, 2024 siku ambayo Robert Amsterdam hakuchapisha taarifa yoyote.

Aidha, JamiiCheck imebaini kuwa Posti iliyoibuka na kutumia jina la Robert Amsterdam inaonekana imethibitihswa (ina tiki ya bluu) lakini akaunti rasmi ya Wakili huyo mpaka leo Desemba 10, 2024 haina tiki ya bluu, tazama katika picha hapa chini:

1733835126161-png.3173747

Akaunti rasmi ya Robert Amsterdam ikiwa haina tiki ya bluu
Zaidi ya hayo, JamiiCheck imebaini kuwa mara ya mwisho Robert Amsterdam kuchapisha taarifa kuhusu Tundu Lissu ilikuwa ni Oktoba 28, 2020 akiandika barua ya kulalamika namna ukosefu wa haki ulivyojitokeza wakati wa Uchaguzi huo mwaka 2020 nchini Tanzania, taarifa hiyo imehifadhiwa hapa
Wakuu Salaam

Nimekutana na Taarifa kuokea Akaunti ya Mtandao wa X ukiwa na Post inayppnekana kuwa ni ya Robert Amsteram (Mwanasheria wa Tundu Lissu) akitoa maoni kuwa kwa sasa CHADEMA inatakiwa imruhusu Lissu kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa chama:

je kuna kuna ukweli hapa?

View attachment 3173992
Kwa sasa CHADEMA inamuhitaji sana LISSU kuliko MBOWE a.k.a Museveni.

Quote
 
Ukiangalia hata english yenyewe ni ya st kayumba....
Eti productivity hata sijui inahusiana nini?
cc LIKUD
 
Back
Top Bottom