Robert Amsterdam athibitisha kufungua mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa Tanzania ndani ya ICC jumatatu

Robert Amsterdam athibitisha kufungua mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa Tanzania ndani ya ICC jumatatu

Mzungu hajawahi kumpenda au kuipenda Africa kutoka moyoni. Lazima ujiulize mara mbili mbili. Strings attached hapo. Aids with conditions. Siyo bure, tena mbaya zaidi. History keeps repeating it self, kama Thomas Sankara
Mzungu ndiye aliye komesha biashara ya utumwa baada ya sisi kuuzans wenyewe kwa wenyewe.
 
CDM pelekeni majina ya viti maalum bungeni,, acheni ubinafsi. Halima Mdee,m/kiti BAWACHA (T) unakwama wapi mrembo..
 
Hahaha nitasubiri mpaka nione imekuwa kweli,kwa sasa ni blah blah tu.
 
Hakuna aliyekukataza kumtumia Muzungu au yoyote yule maadamu una fedha za kumlipa, huo ni uamuzi wenu, lkn fedha zetu za ruzuku sasa Mbowe, Tundu &Co. la kihalifu hawapati hata shilingi ngoja tuone wataende mbali kiasi gani na hizi drama bila ya hela, ...
Nadhani na wao walijua fika kwamba ruzuku hawatapewa na yamkini walijiandaa kukabiliana na hali
 
Watu wanaokufa Rwanda, Butundi, Congo DRC, Congo Brazavile, Sudan n.k ni wengi kuliko Tanzania na hakuna aliyefungwa na ICC
Huko watakuwa wameridhika na hayo mauaji.Na hakuna aliyepeleka malalamiko ICC.Kwa hapa kwetu huu mwaka naona kizungu-zungu tu kwa kweli.Sijawahi kuona nchi yetu ikishupaliwa hivi.
 
Umesahau taasisi inayotetea wanawake duniani pia imefungua kesi dhidi ya serikali ya CCM.
Jamaa wanabana kila upande, huku EU, Pompeo, Bunge la Ulaya, Amnesty, CCM kazi wanayo.
 
Baada ya gwiji la sheria la kimataifa ndugu Robert Amsterdam kufanikiwa kuishawishi idara ya mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya kuijadili Tanzania dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu na hatimaye kusubiri hatua rasmi za kinidhamu kuchukuliwa, sasa Robert amethibitisha rasmi kuwa jumatatu anaenda ICC kufungua mashitaka dhidi ya uhalifu wa binadamu nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa kanuni za ICC, endapo mashitaka yatafunguliwa basi Tanzania itahitajika kupeleka utetezi wake na kisha pande zote mbili kujadiliwa kwa kina.

Sasa mataifa mbalimbali yanaendelea kuchukua hatua dhidi ya Tanzania baada ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhuru kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Hakuna kinatakachotokea!!!Ni shahidi gani atajitolea kwenda huko,tumeona kilichotokea Kenya.La pili ni kuwa tunaonekana kufanya vibaya kwa kuwa haikuwa kawaida yetu kuvuruga kwa kiasi hiki lakini kuna nchi zimevuruga chaguzi mara kumi ya nchi yetu na bado zinadunda.

Rais ameshaapishwa,bunge limeshafunguliwa (tena ambalo halina najisi nyingi) na hakuna uchaguzi mwingine wala kuapishwa Raisi mwingine.Wote tulio (tulio) na maoni tofauti ni wakati wa kuvumilia na kukandamiza hisia zetu maisha yaendelee la sivyo ni kuumia kusiko na sababu (Prof J si mbunge lakini mwan FA ni mbunge).
 
CCM wana polisi, sisi wananchi tuna wazungu.
Ngoma droo!
Walitaka tuandamane watuue wanywe damu yetu. Wazungu wataandamana kwa niaba yetu, wanakata misaada, wanasitisha ARV za bure, ndipo Magufuli atapojifunza kuheshimu haki za binadamu kitu ambacho Marais wenzie waliopita walikifanya bila shuruti.
 
Wafuasi wa Chadema ni kama majuha flani hivi..

Lissu si alisema muingie barabarani na hakuna aliyeonekana. Hapa mnategemea sijui kesi ICC, vipi MIGA tulishashtakiwa??
 
CDM pelekeni majina ya viti maalum bungeni,, acheni ubinafsi. Halima Mdee,m/kiti BAWACHA (T) unakwama wapi mrembo..
Si mlimtamtafuta mbunge aliye ingia bungeni kwa hisani ya mtu wa Chato, Halima Mdee mlisema analysis vikao anachelewesha maendeleo. Sasa mnamtaja wa nini tena?
 
Back
Top Bottom