Robertinho asema “Tangu nimefika sipajata nafasi nzuri ya kuiandaa Simba, kila wakati ni mechi mechi tu, nipeni muda

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baada ya Simba kupoteza kwa magolo 3-0 dhidi ya Raja Casablanca, hivi ndivyo Kocha wa Simba, Roberto Oliveira Robertinho alivyosema:

“Nafikiri timu yangu imecheza vizuri lakini ilitakiw akucheza kwa umakini zaidi ya ilivyokuwa, ndivyo mchezo wa soka ulivyo, Raja wamekuwa wazuri kuliko sisi.

“Tunatakiwa kusahau kuhusu mchezo huu na kuelekeza mawazo yetu katika mchezo ujao.

“Nilipotea wachezaji kadhaa kutokana na kuwa majeruhi kama Saido na Baleke ambao wote walihtaji kuwa na utayari mzuri kabla ya mchezo wa leo.

“Nilipokuja hapa sikupata muda wa kuiandaa timu mwanzoni mwa msimu, nimekutana na mazingira ya mechi mechi kila muda, nahitaji muda wa kuwaandaa kifiziki na kimbinu.

“Tulipata nafasi kadhaa hatukutumia vizuri, wenzetu wamepata nafasi wametumia vizuri.”
 
Mechi zingine mnazitafta wenyewe, mlienda kufanya nini Dubai,? kulikua na haja gani ya kucheza na Al Hilal?
Mechi ya Al hilal ilikuwa ya kupanga full mkoko,tuwapime wachezaji wetu kimbinu kuelekea mechi za Kimataifa.Badala yake tukaweka wachezaji wa kawaida.
 
Raja ndio mabingwa wa Afrika, sioni sababu ya kulalamika sana, muhimu tukacheze na wale walio na uwezo wa kawaida tupate matokeo, robo fainali bado inawezekana kabisa.
 
Raja anaishia robo fainali
 
Yuko sahihi kabisa. Apewe muda, lakini pia apewe uhuru wa kusajili wachezaji anaowataka kwenye dirisha lijalo la usajili.
 
Raja ndio mabingwa wa Afrika, sioni sababu ya kulalamika sana, muhimu tukacheze na wale walio na uwezo wa kawaida tupate matokeo, robo fainali bado inawezekana kabisa.
Mabingwa sio Raja ni Wydad
 
Baada ya Simba kupoteza kwa magolo 3-0 dhidi ya Raja Casablanca, hivi ndivyo Kocha wa Simba, Roberto Oliveira Robertinho alivyosema:

“Nafikiri timu yangu imecheza vizuri lakini ilitakiw akucheza kwa umakini zaidi ya ilivyokuwa, ndivyo mchezo wa soka ulivyo, Raja wamekuwa wazuri kuliko sisi.

“Tunatakiwa kusahau kuhusu mchezo huu na kuelekeza mawazo yetu katika mchezo ujao.

“Nilipotea wachezaji kadhaa kutokana na kuwa majeruhi kama Saido na Baleke ambao wote walihtaji kuwa na utayari mzuri kabla ya mchezo wa leo.

“Nilipokuja hapa sikupata muda wa kuiandaa timu mwanzoni mwa msimu, nimekutana na mazingira ya mechi mechi kila muda, nahitaji muda wa kuwaandaa kifiziki na kimbinu.

“Tulipata nafasi kadhaa hatukutumia vizuri, wenzetu wamepata nafasi wametumia vizuri.”
OKW BOBAN SUNZU
 
Kibu
Bocco
Nyoni
Mkude
Akpan
Banda
Kenedi
Onyango
Manura
Chama
Beleke
Husein
Mwinuka
Outtara

Hawa sio wachezaji wa kutufikisha popote pale
 
Simba tutafukuza kila aina ya kocha kama hatutakubali kuweka fedha kupata quality players. Mashabiki maandazi ndio wanaofikiri pale kocha angekuwa Mgunda tungetoboa.

Tumeona hata vs kama ile ya Onyango intensity ilivyomzidi! Raja wastani wa umri mdogo, lakini wana experience na wamekamilika! Mchezaji kama Mkude labda ligi ya ndani ila ameshachoka!

Tuache kocha anunue wachezaji apewe muda hata miaka miwili tuone kama hatuonja matunda. Lakini tukiacha wale madalali waendelee kuleta wachezaji tutaingia aibu mfululizo tusiamini.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom