Robertinho bado hajui anatafuta nini

Robertinho bado hajui anatafuta nini

Mi sina neno maana yote mmeongea. Sina Imani na falsafa ya Robertinho kwenye mashindano makubwa tangia tutolewe kwa penalty robo fainali iliyopita kwa uzembe mdogo tu.
 
Mimi nasema ikitokea Simba akachukua Ngao siku hiyo, wote mnaolaumu na mnaolalamika kuhusu kocha mnatakiwa mkae kimya. Yaani msimpongeze kocha, msimpongeze mchezaji na msimpongeze kiongozi yeyote. Unafiki hautakiwi, kama umeona kikosi cha Simba ni kibovu, uendelee na msimamo huo huo hadi mwisho wa msimu watakaposajiliwa wachezaji wengine
Eti "....ikitokea Simba akachukua Ngao siku hiyo,..."

Kirahisi tu mbele ya timu iliyokamilika kila idara kama Yanga!! Ok, let us wait and see. Siyo mbali, ni kesho jioni.
 
Eti "....ikitokea Simba akachukua Ngao siku hiyo,..."
Kirahisi tu mbele ya timu iliyokamilika kila idara kama Yanga!! Ok, let us wait and see. Siyo mbali, ni kesho jioni.
Tena mbele ya washambuliaji hatari Ngushi na Mzinze!
 
Nina WASIWASI na uongozi WA Simba kwenye UFUNDI.

Ninawasiwasi na VIONGOZI WA Club ya Simba.

Pia Nina WASIWASI mkubwa sana NA Robertinho.

Simba wanachukulia poa SUPER CUP.
B5 WANAZICHEZEA HOVYO HOVYO.
Basi simba iwaachie yanga wakacheze super cup badala yao., huenda yanga akafika fainali kama alivyofanya kwenye kombe la losers. Simba na hili mkaliangalie
 
Naunga Mkono hoja ya Mkuu Capo Delgado!

Uongozi wa Simba, hasa Try Again na Magungu! Inawezekana sio watu wa Mpira kama inavyosemekana!

Haiwezekani timu msimu wa tatu huu wameshindwa kutatua tatizo la kiungo mkabaji wa uhakika!
Kwa Sasa tunaweza sema tuna Ngoma, lakini asipokuwepo tu ,tunarudi kwa kina Mzamiru na Kanuote ambao wana kasoro nyingi kiuchezaji!
Viongozi wameenda kuongeza tatizo lingine kwenye beki wa kati, beki wa kushoto na golikipa!
Asipokuwepo Inonga au Che- eti sub ni Kennedy!
Kwa Shabalala- sijui sub ni nani!
Umefanyika Uzembe wa kumuacha Kakolanya, Huku wakijua Aishi anaumwa!
Mwisho! Binafsi sikuona haja ya kumtoa kocha Mgunda!
Huyu Robetinho- naomba boli halitembei kabisa!
Butua butua na anao anao nyingi sana!
Ingawa ligi ndio inaanza- ila inatia mashaka kidogo!

Mwisho! - au ni kweli yule Marehemu Hans popu- ndio alikuwa bingwa wa ku- scout
Kimeo pale simbaa ni Try Again akifuata yule Mangungo then Kajura. Hawa ni wapigaji bin wapigaji
 
Kocha ni mzee atakua na shida ya kumbukumbu yule yani mpira ukianza anasahau kama kuna sub...
 
Back
Top Bottom