Bwana Bima
JF-Expert Member
- Jul 29, 2014
- 429
- 929
Ukijaribu kuangalia sajili za simba nadiriki kusema kwamba angalau wako vizuri japo nadhani walikua wanahitaji angalau wapate beki mmoja ambaye anaweza kumpa changamoto Inonga.
Nasema hivyo kwasababu, viongozi wa simba wamesajili kwa maelekezo ya kocha. Ukiangalia kikosi chao asilimia kubwa kuanzia kwenye kiungo, wote ni aina ya viungo ambao wanawaza kushambulia zaidi. Bila shaka huo ndo mfumo wa soka la brazil na soka analolipenda Robertinho.
Swali ni Je, ataweza kuwajenga wachezaji wake hasa wapya waingie kwenye mfumo? Je atafikia malengo ya klabu ya kubeba makombe? Huu ni mtihani mzito sana kwake na ninavyowajua mashabiki wa simba safari hii sijui kama wataweza kuvumilia. Mtihani mzito zaidi kwake ni ngao ya jamii.
Asipobeba hili au ikatokea simba akacheza na yanga then labda simba ikafungwa, naona kabisa jamaa akifurushwa virago.