Robertinyo ni bonge la kocha! Nimependa anao uthubutu

PSEUDOPODIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2020
Posts
392
Reaction score
798
Sub ya Chama ni very technical, baada ya kuusoma mchezo na kuona ni ngumu kuwafunga Mbeya City kupitia katikati, akaona ni bora aimarishe Wings, Magoli yapatikane kupitia pembeni. Akaingiza watu wenye kasi pembeni, kisha akamtoa chama ambaye yeye saido kiuhalisia walikuwa wanafanya kazi inayofanana.

Technical sub kama ile Mgunda hawezi fanya kwa kuogopa mashabiki, Kocha mwenye mbinu huwa ana react mapema baada ya kumsoma mpinzani. Sio mikocha yetu dakika 60 wachezaji wanacheza style hiyohiyo na kocha wala ha react. Huyu mzungu angekwepo toka mwanzo tusingefungwa wala ku draw draw kizembe.

Kongole kwa Mzungu, wachezaji wakielewa mfumo wake Simba itakuwa moja ya timu tishio sana kwa wapinzani.
 
Sub ya Chama ni very technical, baada ya kuusoma mchezo na kuona ni ngumu kuwafunga Mbeya City kupitia katikati, akaona ni bora aimarishe Wings,...
Hakuna unachojua kuhusu mpira. Unachojua ni kuangalia matukio ya mpira sio uchambuzi.

Unajua Chama katoka kwasababu zipi kama sio majeraha.
 
Hakuna unachojua kuhusu mpira. Unachojua ni kuangalia matukio ya mpira sio uchambuzi.

Unajua Chama katoka kwasababu zipi kama sio majeraha.
Kwani wewe ni daktari wa Simba SC?

Mwenzako ametulia amekupa maneno ya busara, wewe unamuona hajui kwasababu akili yako imekomazwa na ufundi wa Mgunda...

Amka kijana, muda umebadilika.

Kocha mzungu anajielewa, akiachwa ataitengeneza ile Simba kila shabiki atamkubali, sio game yake ya kwanza tu mnaanza kelele zisizo na maana.
 
Achana nae hajielewi huyu!!
 
Tatizo atafukuzwa wiki ijayo
 
Maamuzi magumu yanayo igharimu timu ni upuuzi simba haina uwezo wa kumiliki mpila bila chama.

Tatizo sio chama kutoka tatizo ni anatoka chama anaingia nani?
Hivi kocha una akili kabisa unamtoa chama una muingiza kibu kabisa?kibu ni mchezaji ambayo hafai kwenye mfumo wowote ule pale simba.

Alafu unacho takiwa kujua ni kuwa Simba farsafa yake ni kutumia viungo kufanya mashambulizi na sio mawinga ni lazima kocha haendane na falsafa ya timu kama hawezi asepe.

Timu yenye farsafa ya kutumia mawinga kufanya mashambulizi ni utopolo na ndio maana huwa wanapenda kusajili mawinga wanakimbia kimbia hovyo kama vichaa.
 
Mna wenge sana.
 
Ishu hapa Simba wameshazoea kufungwa Kwa uhakika na kushinda Kwa uhakika mechi yajana haikua yakushinda tatu mbili
 
Duuh aisee.
 
Tuache upwapwapwa mwalimu apewe muda. Tunaamini tunajuaaaaa.
 
Ingekuwa vipi kama Simba jana ANGEFUNGWA..?? Je, ungekuja hapa na kumsifia kocha au ungekuja na uzi wa kumtukana kocha..??
 
Yani ile kuona tu ameanza na Bocco na Kiyombo up front nikaona hapa kuna shida kwangu mimi ameanza na kuni disappoint.

Kiyombo control yake sio nzuri kabisa so as Bocco which means mipira haiwezi kukaa mbele na ndo kilichotokea.

halafu akaanza na chama na Saidoo kwenye Flangs kitu ambacho hawa wote ni play makers hivyo hawewezi kutrack back kwa ufanisi ndiomaana uliona Kapombe alikua akipata tabu sana na zimbwe.

Binafsi alini disappoint.

Hawa akina kibu ni wazuri kwenye kusaidia kwenye ulinzi ila sasa inapokuja kwenye mambo ya matumizi mazuri ya akili na decision hua ni zero.
 
Tuache upwapwapwa mwalimu apewe muda. Tunaamini tunajuaaaaa.
Kwa farsafa ya kutumia mawinga hata akipewa muda hawezi kutoboa hivi kwanza kwa winga gani iliyo nayo au hawa akina kibu?
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…