SI KWELI Roberto Carlos anatumia eneo la mazoezi ya klabu ya Real Madrid kama makazi baada ya kutaka kutalikiana na mkewe

SI KWELI Roberto Carlos anatumia eneo la mazoezi ya klabu ya Real Madrid kama makazi baada ya kutaka kutalikiana na mkewe

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nyota wa zamani wa Real Madrid, Roberto Carlos anadaiwa kuingia kwenye mgogoro na mkewe hali iliyopelea atumia majengo ya uwanja wa mazoezi wa Real Madrid kama makazi wakati akishughulikia suala lake la talaka na mkewe waliodumu kwa miaka 15

Wenzi hao, waliofunga ndoa mwaka 2009, sasa wanakabiliwa na vita vya kisheria kuhusu utajiri mkubwa wa Carlos, unaoripotiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 133 (Tsh410,091,550,000)

Carlos.jpg
 
Tunachokijua
Roberto Carlos jina lake kamili ni Roberto Carlos Da Silva Rocha mzaliwa wa Brazil mwaka 1973. Roberto alikuwa beki wa kushoto wa timu ya Taifa ya Brazil na Real Madrid ambapo katika soka alipata mafanikio mbalimbali ikiwemo kuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa na timu ya taifa ya Brazil iliyoshinda kombe la dunia mwaka 2002, lakini pia alifanikiwa kushinda ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Madai

Kumekuwapo kwa taarifa mbalimbali zilizosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nyingi zikiwa ni za terehe 07, Januari 2025 ikieleza kuwa gwiji huyo wa zamani wa soka analala katika uwanja wa Real Madrid mara baada ya kutalakiana na mkewe. Ripoti zilidai kwamba gwiji wa Brazil alihamia kwa muda katika kituo cha Valdebebas baada ya kutengana na mke wake, Mariana Luccon.

Wanandoa hao, waliofunga ndoa mnamo Juni 2009, wana binti wawili pamoja ambao ni Manuela na Mariana. Kulingana na ripoti hizo, Luccon anabaki katika makazi makuu ya familia, huku wazazi wake wakiripotiwa kuishi katika mojawapo ya mali nyingine za Carlos. Talaka hiyo inasemekana kuwa ngumu, hasa kutokana na utajiri mkubwa wa beki huyo wa kushoto, unaokadiriwa kuwa pauni milioni 133 ($166m)

Uhalisia upoje?

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa madai hayo na kubaini uwepo wa tovuti mbalimbali zilizochapisha taarifa hiyo mathalani tovuti ya dailymail ya nchini Uingereza ilichapisha taarifa kupitia tovuti yao tarehe 07, January ikiwa na kichwa kilichosomeka

"Gwiji wa Real Madrid, Roberto Carlos, mwenye umri wa miaka 51, 'analala katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wakati anapoachana na mke wake ambaye ni mama wa watoto wawili kati ya watoto wake KUMI NA MOJA, huku wakipambana vikali kuhusu utajiri wa pauni milioni 133.'"

Tazama hapa kuona tovuti nyingine zilizochapisha taarifa hiyo.

Roberto Carlos alichapisha taarifa kupitia mtandao wa X (Twitter) kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na kueleza kuwa zina lengo la kuwavutia watu lakini hazina uhalisia wowote.

“Katika siku za hivi karibuni, nimepata taarifa za uwongo na zenye madhara zinazozunguka kuhusu mimi na familia yangu.

Ingawa ninathamini faragha, najisikia kulazimika kushughulikia uvumi wa msingi usio na ukweli kuhusu hali yangu ya kuishi. Hadithi hizi zilizotungwa ni za uongo kabisa na zinaonekana kutengenezwa kwa lengo la kuvutia watu.

Ninaendelea kuishi katika makazi ya binafsi, nikiwa nimeungwa mkono na wanafamilia wangu. Timu yangu ya sheria inakagua madai haya na itachukua hatua zinazofaa.

Ninaomba faragha kuhusu masuala ya kibinafsi na kuwashukuru wale wanaoendelea kunipa msaada katika kipindi hiki”
Hatari sana.

Halafu ndio Kuna simps wanataka na sisi tu adapt sheria za ndoa za huko ulaya eti ndio zinawatendea haki wanawake ipasavyo?
 
Dah! Huwa yanasikitisha sana haya mambo saa ingine.
 
Back
Top Bottom