Roberto Carlos ayatimba kwa mkewe, huenda akafirisika kisa kesi ya talaka

Roberto Carlos ayatimba kwa mkewe, huenda akafirisika kisa kesi ya talaka

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
31,913
Reaction score
65,514
Roberto Carlos, beki maarufu wa zamani Real Madrid, anaripotiwa kuishi katika uwanja wa mazoezi wa klabu ya, Real Madrid Sports City huko Valdebebas, huku akipitia talaka ya juu kutoka kwa mke wake wa miaka 15, Mariana Luccon.

Wawili hao, waliofunga ndoa mwaka 2009, kwa sasa wako kwenye vita vya kisheria kuhusu utajiri wa Carlos, ambao unakadiriwa kufikia pauni milioni 133, kulingana na ripoti kutoka Goal. Wakati nyota huyo wa Brazil amechukua makazi kwa muda kwenye uwanja wa mazoezi, mke wake wa zamani anasalia katika nyumba yao kuu, na wazazi wake wanakaa katika mali nyingine inayomilikiwa na Carlos. Wenzi hao wa zamani wana mabinti wawili, Manuela na Mariana.

Carlos, ambaye ali ichezea Real Madrid kwa zaidi ya muongo mmoja, anajivunia maisha mazuri, baada ya kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa na mataji manne ya La Liga. Zaidi ya soka, maisha yake ya kibinafsi pia yamevutia, kwani amekiri hadharani kuzaa watoto 11 na wanawake saba katika nchi tofauti.

Huku taratibu za kisheria kuhusu mgawanyo wa mali ukiendelea, bado haijulikani ni muda gani Carlos atakaa katika kituo cha mafunzo au matokeo ya mwisho ya kesi hiyo yatakuwaje. Mbali na mafanikio yake ya zamani uwanjani, sasa anatumika kama balozi wa Real Madrid.

Fununu zina sema "mwanamke ndie aliye msaliti r. Carlos" na alipo ulizwa kwanini kafanya hivyo .yeye kakimbilia talaka.

ushauri tu,
ikiwa wewe ni maarufu na umepata pesa, hakuna haja ya kuoa. Ndoa daima huisha kwa talaka. Kuwa kama Christiano Ronaldo.

KATAA NDOA LINDA UHURU WAKO, KATAA NDOA LINDA UCHUMI WAKO.
KATAA NDOA LINDA JUHUDI ZAKO.
NDOA NI MKATABA WA KITAPELI.
FB_IMG_17363630895374360.jpg
 
Wanawake wana tamaa sana.. Kuna mwingine nilisoma mahali aliomba talaka bahati nzuri akapewa. Walivyofika mahakamani mwanamke akashinda kesi na kukabidhiwa mali zenye thamani ya dollar milioni tatu kama sijakosea.. kufupisha story baada ya miaka mitatu yule mwanamke akaponda mali zote kwa sasa ni omba omba huko Marekani
 
Wanawake wana tamaa sana.. Kuna mwingine nilisoma mahali aliomba talaka bahati nzuri akapewa. Walivyofika mahakamani mwanamke akashinda kesi na kukabidhiwa mali zenye thamani ya dollar milioni tatu kama sijakosea.. kufupisha story baada ya miaka mitatu yule mwanamke akaponda mali zote kwa sasa ni omba omba huko Marekani
aisee halafu wajomba wana nikazania nioe🙄😃😃, KATAA NDOA LINDA UHURU WAKO .
 
Back
Top Bottom