Robo Fainali ACL: Simba boresheni Safu ya Ulinzi.

Robo Fainali ACL: Simba boresheni Safu ya Ulinzi.

dudunyama

Member
Joined
Jan 25, 2017
Posts
36
Reaction score
37
Habari Wadau.

Kwanza nitoe pongezi nzito kwa Simba SC na Tanzania kwa ujumla kufuatia kufuzu hatua ya robo fainali Africa Champions League, maana hatua hii inaitangaza Club na Taifa.

Kumalizika kwa hatua ya Makundi kunaonesha kuwa Simba ndio yenye uwiano mdogo zaidi wa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa(-7) kati ya timu zote katika hatua hiyo(hata zile ambazo hazijafuzu).

Kuna haja ya kutathimini upande wa ulinzi hasa katika mechi za nje. Sawa takwimu zinaonesha timu nyingi zimepoteza mechi za nje lakini issue ni idadi ya magoli ambayo unafungwa.

Hili ni muhimu kulitazama kuelekea mechi za robo fainali maana kama unapigwa goli nyingi nje ile hali uwezo wa kushinda mechi za ndani ni mdogo hama kwa goli chache hiyo ni hatari katika hatua hii.Hivyo ni vyema kutafuta njia bora za ulinzi katika hatua hii.

Wadau mlio na chochote juu ya nini kifanyike karibuni sana kuchangia bila kujali itikadi za timu zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa namna au Nyingine kukosekana kwa E .Nyoni file mechi za ugenini zilipelekea kukosekana kwa utulivu pale Kati Nyoni Ana akili Sana ya mpira na anaficha magepu Sana ya P.wawa, kinachotakiwa kufanyika ni kumkomaza huyu Dogo paul Bukaba katika mechi za Away a cheze mbele ya Nyoni na Wawa ...mechi za ugenini tutumie Mkude,kotei na huyu Bukaba Chama awe anaingia Sub au Kama atakua anacheza basi tucheze na mshambuliaji mmoja fomesheni iwe 4-5-1 mechi za ugenini kagere na Bocco inabidi aanze mmoja.

Options ya pili ni kucheza na mabeki wakabaji watatu Bukaba/Murshid,Nyoni na Wawa Yani mfumo uwe 3-5-2 Tshabalala na Zana wacheze Kama viungo na beki maana Wana Kasi na Wana uwezo mzuri wa kushambulia huku eneo la nyuma tukiwa na mabeki watatu

NB
Mechi za ugenini Chama sio lazima kuanza na pia Tusianze na Forward mbili kwa pamoja maana hatuendi ugeninikutafuta ushindi Bali ni sare au kufungwa kwa goli zisizozidi 2...ila tukiwa nyumbani tucheze kawaida katika fomesheni yetu hiyo itamchanganya hata mpinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna kuongeza wachezaji...basi beki wa kati.. Kiungo mkabaji..na mshamuliaji hapo nadhani timu itakuwa imara kupambana.
 
Halafu hii si knock out stage? Ukipigwa umetoka ?
Hata kabla ya makundi kulikuwapo knock out home & away, na walikutana na timu ngumu kabisa ya Nkana, lakini walipenya. Simba haihitaji ushauri wenu
 
Simba haihitaji ushauri wenu. Ina uzoefu wa kucheza kadiri ya aina ya mashindano iliyopo. Mnatakiwa mzishauri timu zinazotolewa raundi ya kwanza
 
Habari Wadau.

Kwanza nitoe pongezi nzito kwa Simba SC na Tanzania kwa ujumla kufuatia kufuzu hatua ya robo fainali Africa Champions League, maana hatua hii inaitangaza Club na Taifa.

Kumalizika kwa hatua ya Makundi kunaonesha kuwa Simba ndio yenye uwiano mdogo zaidi wa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa(-7) kati ya timu zote katika hatua hiyo(hata zile ambazo hazijafuzu).

Kuna haja ya kutathimini upande wa ulinzi hasa katika mechi za nje. Sawa takwimu zinaonesha timu nyingi zimepoteza mechi za nje lakini issue ni idadi ya magoli ambayo unafungwa.

Hili ni muhimu kulitazama kuelekea mechi za robo fainali maana kama unapigwa goli nyingi nje ile hali uwezo wa kushinda mechi za ndani ni mdogo hama kwa goli chache hiyo ni hatari katika hatua hii.Hivyo ni vyema kutafuta njia bora za ulinzi katika hatua hii.

Wadau mlio na chochote juu ya nini kifanyike karibuni sana kuchangia bila kujali itikadi za timu zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Strategy tofauti kaka. Kwani hukuona na nkana na wale wajinga wengine tulioanza nao kabla ya nkana tuliowapiga nje ndani. Hili kombe la champions league linakuja simba mkuu usiwe na wasiwasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom