Robo Fainali Klabu Bingwa Africa: TP Mazembe 4 - 1 Simba SC

Robo Fainali Klabu Bingwa Africa: TP Mazembe 4 - 1 Simba SC

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Wadau Karibuni katika mechi hii ya marudiano (Second Leg- CAF CHAMPIONS LEAGUE) kati ya TP Mazembe ambao wako nyumbani wakiwakaribisha Simba SC ya Tanzania katika uwanja wa Stade TP Mazembe ulio katika viunga vya Jiji la Lubumbashi DRC


Yote yanayojiri katika mtanange huu wa kukata na shoka utayapata hapa kuanzia saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki

Kuwa nami kwa 'Live updates' kuanzia Dakika 0 hadi 90

TP Mazembe anahitaji ushindi wa aina yoyote ili aweze kufuzu hatua inayofuata huku Simba anahitaji sare ya magoli au ushindi ili apite kwa advantage ya away goal, ila wakimaliza 90 minutes bila kufungana, mpira utakwenda extra time,

Mechi ya raundi ya kwanza iliyochezwa Dar es salaam April 06/2019 timu hizi zilitoshana nguvu kwa kutoka sare tasa (0-0)

Je Simba itapindua Matokeo? au TP Mazembe itasonga mbele? Tusubiri dakika 90 za mtanange huu zitatoa majibu...

☆Vikosi vya timu zote vitakavyoanza vitawekwa hapa .

TP MAZEMBE XI:-

Starting 11 : GBOHOUO – ISSAMA, MONDEKO, CHONGO, OCHAYA – MIKA, SINKALA – MPUTU – ELIA, MULEKA, KALABA

Bench : MOUNKORO, MASENGO, KASUSULA, KOUAME, LIKONZA, SISSOKO, KABANGU


SIMBA STARTING XI:-
1. Manula A.
2. Coulibaly Z.
3. Mo Hussein
4. Nyoni E.
5. Juuko M.
6. Kotei J.
7. Mzamiru Y.
8. Mkude J.
9. Bocco J.
10. Niyonzima H.
11. Okwi E.


☆Kwa Wenye TV mnaweza kuangalia kupitia DSTV channel ya Supersport 9 na Azam TV kupitia channel ya ZBC 2..* Mwenye Link ya kustream live anaweza kuweka pia

☆ Rais wa DR Congo, Mhe. Felix Tshisekedi leo atakuwepo uwanjani (Stade TP Mazembe) kuangalia mchezo huu wa marudiano

☆ Updates

- Timu zimeshaingia uwanjani na wanasalimiana pale
- Uwanjani mashabiki wamejaa sana

Dk.0' Mpira umeshaanza hapa

Goooooal Dk 1 kwenda ya 2 Simba anapata goal kupitia Okwi

Dk 5 TP mazembe wanashambulia hapa lakin Aishi Manula anaokoa


Dk 8 bado mpira haujatulia..ni piga nikupige

kona kwa Tp mazembe

Dk 11 Mo Hussein anapata kadi ya njano

Dk 15 TP wanashambulia goli la Simba lakini wanazuiwa

Joseph Ochaya wa Mazembe anapiga shuti kali linaenda nje pale

Dakika ya 21 Mazembe wanapata Kona...James kotei anatolewa nje

Goooooaaal Tp Mazembe wanapata goli la kusawazisha kupitia kwa Chongo Kabase

Dk 24 TP mazembe wanachangamka hapa kuongeza goli lingine

DK 31 Rainford Kalaba anacheza faulo...inapigwa kuelekea Mazembe

Dk 35 TP mazembe wanafanya shambulizi hatari pale lakini Aishi manula na mabeki wanaokoa..

Dk 37 Goooooaal Tp mazembe wanapata la pili kupitia Meshack Elia

Dk 42 TP mazembe wanafanya shambulizi kali hapa linagonga mwamba inakuwa kona

Dk 44 TP Mazembe 2 Simba 1 mpira unatoka nje hapa TP mazembe wanautoa wakti huohuo dakika 1 imeongezwa kuelekea mapumziko

Mapumziko TP Mazembe 2 Simba 1

-----------------------------------------------------------------------------

Kipindi cha pili kimeanza

Kagere Medie ameingia ametoka Muzamiru Yasin

Dk 46 Timu zote zinashambuliana kwa kasi sana...

TP Mazembe wanapata kona inaokolewa

Dk 49 Simba wanazembea hapa TP mazembe wanaingia golini..namna gani pale bado...inapigwa kule Simba wanazubaaa...gooal lakin inakataliwa inakuwa offside

Chama Clotus anaingia Jurko Murshid nje

Dk 52 Rainford Kalaba anajaribu pale Aishi manula anaitoa nje inakuwa kona


Dk 55 TP mazembe Meshack Elia anawekwa chini baada ya faulo ya Kotei James

Dk 58 TP mazembe wanapata kona ( TPM 2 SSC 1)



Dk 62' Goooooooaaal TP mazembe wanapata goal la 3 kupitia Trezor Mputu

Dk 64 Simba wamefunguka nao TP Mazembe wamefunguka

Dk 67 Matokeo ni TPM 3 SSC 1

Dk 70 Simba wanapata kona...Niyonzima anapiga kona ndeeeeeeefu inatoka nje kule namna gani

Rashid Juma wa simba ndani, Okwi E. nje

Dk 71 Kadi ya njano kwa Erasto Nyoni.. Faulu kwenda Simba TP mazembe wanapata inapigwa inaenda nje

Dk 72 Gooooooooal TP MAZEMBE WANAPATA GOAL la 4 linalofungwa na Jackson Muleka

DK 74 KRISTIAN KOFI NDANI KALABA NJE

DK 78 TP mazembe wanashambulia lango la Simba ila wanakosa

Dk 79 John Bocco anamchezea faulu beki Kelvin Mundeko



Dk 84 TP MAZEMBE SUB TREZOR MPUTU GLODY LIKONZA NDANI

DK 88 Simba wanapanga mashambulizi hapa lakini yanazuiwa na TPM

Dk 89 Offside Simba wanazidi kwa TPM

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA KUMALIZA MCHEZO

Dk 90+1 TP mazembe wanacheza kwa kupoteza muda wakati huo Simba wanaonekana kuchangamka

Dk 90+3 Mpira inakuwa gooal kick Kipa wa Mazembe anapiga mbele wananziana pale kati na mpira umeishaaaaa

MPIRA UMEKWISHA KUTOKA DIMBA LA STADE TP MAZEMBE---- TP MAZEMBE 4 SIMBA 1

SIMBA ANAAGA MASHINDANO HAYA YA LIGI YA MABINGWA KATIKA HATUA HII YA ROBO FAINALI HUKU TP MAZEMBE AKITANGULIA NUSU FAINALI YA CAF CHAMPIONS LEAGUE



Ahsanteni kwa kuwa nami...Pamoja sana

IMG_20190413_153707.jpg
 
@Shaffih Dauda anasema....Mechi kadhaa za mwisho za TP Mazembe ndani ya uwanja wao wa Nyumbani.
::
Mazembe 2 - 0 CS Costantine
Mazembe 8 - 0 Club Africain
Mazembe 2 - 0 Ismaily
Mazembe 1 - 0 Zesco United
Mazembe 1 - 1 De Agosto
Mazembe 1 - 1 Difaa El Jadida
Mazembe 1 - 0 MC Alger
Mazembe 4 - 1 El Setif
Mazembe 4 - 0 US Dongo
::
Takwimu zinaonesha katika mechi 4 za mwisho hawajaruhusu goli lolote wakiwa nyumbani wakiwa wamefunga magoli 12.
::
Wakati upande wa pili wa karata Vigogo wa soka wa Tanzania Simba mechi zake 4 za mwisho ugenini wamefunga goli moja tu dhidi ya (Nkana FC) na kufungwa magoli 14.
::
Kikubwa tahadhari na kumheshimu mwenyeji. Magoli ni kitu cha muhimu.
 
Leo naona umeweka uyanga pembeni, na uhamie SSC 💪 mazima.
 
Wadau Karibuni katika mechi hii ya marudiano (Second Leg- CAF CHAMPIONS LEAGUE) kati ya TP Mazembe ambao wako nyumbani wakiwakaribisha Simba SC ya Tanzania katika uwanja wa Stade TP Mazembe ulio katika viunga vya Jiji la Lubumbashi DRC


Yote yanayojiri katika mtanange huu wa kukata na shoka utayapata hapa kuanzia saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki

Kuwa nami kwa 'Live updates' kuanzia Dakika 0 hadi 90

TP Mazembe anahitaji ushindi wa aina yoyote ili aweze kufuzu hatua inayofuata huku Simba anahitaji sare ya magoli ili apite kwa advantage ya away goal, ila wakimaliza 90 minutes bila kufungana, mpira utakwenda extra time,

Mechi ya raundi ya kwanza iliyochezwa Dar es salaam April 06/2019 timu hizi zilitoshana nguvu kwa kutoka sare tasa (0-0)

Je Simba itapindua Matokeo? au TP Mazembe itasonga mbele? Tusubiri dakika 90 za mtanange huu zitatoa majibu...

☆Vikosi vya timu zote vitakavyoanza vitawekwa hapa .

☆Kwa Wenye TV mnaweza kuangalia kupitia DSTV channel ya Supersport 9 na Azam TV kupitia channel ya ZBC 2

☆ Rais wa DR Congo, Mhe. Felix Tshisekedi leo atakuwepo uwanjani (Stade TP Mazembe) kuangalia mchezo huu wa marudiano

View attachment 1070355View attachment 1070356

Sent using Jamii Forums mobile app
Na tusio na TV ila tuna access na smartphone channel gan online itaonyesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom