Robo Fainali UEFA: Liverpool na Barcelona kufanya 'Comeback' dhidi ya PSG na Atletico leo?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Liverpool na Barcelona usiku wa leo zinakabiliwa na kibarua kigumu cha kujaribu kufanya mapinduzi (comeback) katika michezo yao ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA). Timu zote mbili zinaingia uwanjani zikiwa na deni la mabao mawili, hali inayozilazimu kushinda kwa tofauti kubwa ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali.

1776152848283.png

Katika mchezo wa kwanza, Liverpool ilikubali kichapo cha 2-0 ugenini dhidi ya PSG, huku Barcelona ikipoteza kwa matokeo kama hayo mbele ya Atletico Madrid. Klabu hizi kongwe sasa zinahitaji nidhamu ya hali ya juu safu ya ulinzi na makali ya ziada katika ushambuliaji ili kupindua matokeo hayo dhidi ya wapinzani wao ambao wanaonekana kuwa na faida kubwa ya kisaikolojia.

1776152891149.png
Mechi hizi zinazotarajiwa kupigwa saa 4:00 usiku, zinatupiwa macho na mashabiki duniani kote kusubiri kama uzoefu wa Liverpool na Barcelona utatosha kuwatoa nishai PSG na Atletico. Wakati PSG na Atletico wakihitaji sare tu kusonga mbele, shinikizo kubwa liko kwa miamba hii miwili ambayo kihistoria imewahi kufanya maajabu makubwa ya 'comeback' katika michuano hii.
 
Yetu 👀 dakika n 90
 
Ngoja tuone lakini Kwa Liverpool Sidhani kama wataweza kutoboa, Kwa uchezaji ule watakufa vibaya kwenye counterattack, liver hawana cha kupoteza watafungulia busta zote na ndipo PSG wataua mtu, maana striking force Yao ni hatari Sana pasi mbili washafika golini,

Barca uko uwezekano wa kutoboa kama kweli wakiamua kucheza, shida Atletico wanaweza kupaki basi tuuu na kusubiri kaunta ambazo ni 50/50.
 
Salah akianza Liverpool wanashinda hii mechi
 
Comment ya mwisho kwenye huu uzi🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom