Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Asante mkuu nimeelewa
 
Coils zote huwa zinakuja zikiwa zina rangi kabisa ila kinachotofautisha ni Ile thickness ya coating. Kuna baadhi ya makampuni Yao hata ukichubua kwa mkono tu rangi inatoka.
asante nimeelewa
 
Karibu sana tukuuzie bati kiwandani kabisaaa na siyo madukani.[emoji28][emoji28][emoji28]
kiwanda gani maana kama ni ALAF nilimpeleka rafiki yangu kiwandani na zimekuwa kimeo. Kabla hata ya miaka 3 zimeanza kupauka. Kwa sasa inasikitisha hata kuzitazama
 
kiwanda gani maana kama ni ALAF nilimpeleka rafiki yangu kiwandani na zimekuwa kimeo kabla hata ya miaka in 3 kuisha zikaanza kupauka. Kwa sasa zinasikitisha hata kuzitazama
Kiwanda Cha Kinglion Mabati. Tuna mwaka na miezi mitatu tangu tuingie sokoni lakini bidhaa zetu zimekuwa kimbilio la wengi kwasababu ya ubora mkubwa lakini Bei ni nafuu.
Tumefungua viwanda Dar,Unguja,Dodoma,Arusha,Mbeya na Mwanza.
 
Mkuu kwa faida ya wengi ungeelezea jinsi ya kutambua which ni fake na which ni original
Kitu ambacho hawawez kuiga kwenye bati fake kutoka original ya ALAF n chapa yao ya moto kwenye bati
 
Ndugu yangu mmoja alipata shida kama hii Dom,alinunua kwa wachina wauza mabati..alifungua kesi,ikaunguruma kama miaka miwili hivi na akafanikiwa kulipwa fidia milioni 9 hivi. Uzuri alikuwa na nyaraka zote za mauziano na warrant....Mwishowe bati hakuzitoa wala kupiga rangi...yaani paa lipo kama suti ya vipande vitatu. Hela alifanyia ,mambo yake mengine ila aliwanyoosha....Ila piga rangi,walau yatakaa vzr
 
Kiwanda Cha Kinglion Mabati. Tuna mwaka na miezi mitatu tangu tuingie sokoni lakini bidhaa zetu zimekuwa kimbilio la wengi kwasababu ya ubora mkubwa lakini Bei ni nafuu.
Tumefungua viwanda Dar,Unguja,Dodoma,Arusha,Mbeya na Mwanza.

Vipi kuhusu ubora na kupauka kupoteza rangi kwa haraka
 
Vipi kuhusu ubora na kupauka kupoteza rangi kwa haraka
Mabati ya kampuni zote hupoteza rangi lakini yanatofautiana muda. Kwa sisi kinglion tumeweka matazamio ya kuanza kupoteza rangi ni miaka mitano(5 yrs warranty) lakini inaweza kuvuka zaidi ya miaka hiyo.
Lakini ukitaka kupata kitu Cha uhakika usinunue bati linalouzwa chini ya sh 27,000/=.
 
Kuna jamaa wa kiwandani kwenu mwanza kaniambia bei 26,000 ila 25,000 nachukua
 
Jirani yangu alipaua mwaka Jana mwezi Mei kwa mabati yenu kinglion rangi ya charcoal Grey. Hivi tunavyozungumza bati imekuwa nyeupeeee.

So kinglion ni hovyo tu ndugu yangu. Tena hovyo kabisa. Hii nimejionea mwenyewe kwa macho yangu. Hovyoooo!
 
Tupe picha haya maneno bila ushahidi hakuna kitu
 
Jirani yangu alipaua mwaka Jana mwezi Mei kwa mabati yenu kinglion rangi ya charcoal Grey. Hivi tunavyozungumza bati imekuwa nyeupeeee.

So kinglion ni hovyo tu ndugu yangu. Tena hovyo kabisa. Hii nimejionea mwenyewe kwa macho yangu. Hovyoooo!
Hizo zitakuwa siyo bati za kinglion mkuu.
 
Chukuwa risiti uliyonunulia hayo mabati na andika barua ya MALALAMIKO kwa aliyekuuzia hayo mabati. Ipo relief utakayoipata kutoka kwa mtengeneza mabati hayo.

Sijafahamu kifungu cha sheria kilichotumika maana jamaa yangu aliwasilisha malalamiko kama yako na wakamrejeshea 50% ya gharama aliyonunulia mabati yote.

Naomba wanasheria wa shade light katika hili.
 
Nijibu swali hili; ulinunua TAZARA (ALAF) au kwa wale wanauza bati reject? Maana wote wapo TAZARA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…