Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Hata kama ningekuwa mimi ningekuuzia fake. Kinachokufanya usiitaje hiyo kampuni ni nini? Taja ili watu waijue kuliko kuwaficha.
 
Mtaani kwetu wote waliopaua na bati ya alaf na dragon hakuna iliyopauka, binafsi nimepaua na dragon.

Jambo la msingi nenda kiwandani bati ikatwe unaiona upewe na warranty, usichukue za bando.

Pia mtoa mada alichokosea ni kuchukua rangi ya blue, ikipauka inaonekana sana.
Mpaka sasa hiyo dragon ipoje?
 
Yaani nimefanikiwa kujenga nyumba tena kubwa ila sijahamia bado vitu vichache nihamie, lakini kinachoniuma kipindi napaua (kupiga bati)niliaminishwa kuwa bati za kampuni fulani (hapa siitaji jina) ni nzuri na nikaonyeshwa nyumba ya jirani yenye hizo bati kuwa hazipauki.

Nilikubali baada ya kukagua na nikajiridhisha kila kitu, nikaenda nunua hizo bati pale Tazara nikapaua nyumba vizuri tu, sasa ni miaka 4 tangu nipaue sijahamia lakini zile bati kwa kweli zinatia kinyaa zimepauka hadi sina hamu ya kuhamia tena huko.

Hapa kinachoniuma zaidi nyumba ya jirani zake rangi iko vile vile na ni yeye aliniagizia alikonunua hadi bei ni hiyo hiyo, na hata jirani na ofisini kuna bati kama hizo hizo zimezungushiwa kama fensi sehemu wanakojenga hazijapauka kila siku naona ni mpya na nashindwa elewa hapa kuna siri gani kwenye hiyo kampuni nyingine zipauke nyingine zisipauke!

Hapa nawaza je! Ninunue bati zingine au ninunue rangi ya bati nikapake upya kwa mkono?

Ushauri wenu naombeni.
Picha tofauti na hapo inakuwa kama story za minzan ya ushambegex
 
Back
Top Bottom