Roho mtakatifu ndani mwetu

Roho mtakatifu ndani mwetu

third eye chakra

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2023
Posts
713
Reaction score
1,745
KUNDALINI

"Ni Mfumo wa Mazoezi ya Asili na ya kiroho, mazoezi haya hujumuika kama njia ya kuongeza nishati iitwayo KUNDALINI
Wakati wa kufanya mazoezi haya unahitajika kufuata Mlolongo mkali uitwao KRIYA

Katika Nadharia na Mazoezi ya YOGA hili ni Jina la Nishati ambayo iko ndani ya Binadamu Mwanzoni mwa Mgongo wako, Ipo Usingizini na Inahitaji Kuinuliwa Hapo kwa Kupitia Chakras Saba Kuu Zinazopatikana Kando ya Safu za Mgongo Wako.

KUNDALINI KATIKA DHANA ZA MAANDIKO

Hufafanuliwa kwa Lugha Tofauti tofauti za Alama Baadhi ya Hadithi ya Kale ya Adamu na Hawa Imejifunua Katika Mtindo wa Lugha ya Alama Kama NYOKA, na Nyoka anae Zungumziwa Katika Kitabu Cha MWANZO SURA YA 3, si NYOKA Halisi, Nyoka ni Alama Inayo Wakilisha KUNDALINI Ambayo ipo Ndani yako Na TUNDA Ambalo Adamu na Hawa Walikula si TUNDA HALISI Bali ni Kiwakilishi cha ELIMU AU UJUZI WA AINA YOYOTE UNAO KUSUDIA WEWE KUAMSHA KUNDALINI.

Pia KUNDALINI Imefafanuliwa Kama Kitabu kilicho Jaa Maneno Ndani na Nje na Kimefungwa kwa Muhuri Saba, Sasa KITABU Kinachozungumziwa Sio Kitabu Halisi Cha Kimwili Bali ni Nishati Hii Ya KUNDALINI Iliyo Ndani ya Kila Mtu chini ya Mgongo Katika Mfupa wa SACRUM, na Kitabu Hicho kimefungwa kwa Mihuri Saba, MIHURI SABA sio Mihuri Halisi ya Kibinadamu Bali ni Alama ya KIROHO Kuwakilisha VITUO SABA vya Nishati Yaani CHAKRAS Ambapo Kundalini Inapo Amka Hupita Katika Chakra Hizo Ikizifungua Kutoka Root Chakra Mpaka Crown Chakra.

_ Mahala Pengine KUNDALINI Imefafanuliwa na KRISTO Kama ROHO MTAKATIFU Au Nguvu ya Roho Mtakatifu Ndani Yenu.

ROHO MTAKATIFU NDIO KUNDALINI YENYEWE, NGUVU YA ROHO MTAKATIFU NI KUNDALINI ENERGY ILIYO NDANI YAKO.

Nguvu hii ya KUNDALINI Haina Ubaguzi Mtu wa Aina Yoyote yule Awe Mtu wa Dini au Awe Mtu Asiye Amini Katika Dini (Kama Mimi Hapa) Inapo Funguliwa Inafunguka na Inatenda Kazi Pasipo Kipingamizi, Kama Itafunguliwa Vizuri kwa Kufuata Kanuni Rasimi za Kiroho Basi Itakuwa Na Faida Njema Kwako/Kwenu.
🙏🙏🙏🙏🙏
 

Attachments

  • IMG-20240331-WA0009.jpg
    IMG-20240331-WA0009.jpg
    220.8 KB · Views: 35
KUNDALINI
_ Mahala Pengine KUNDALINI Imefafanuliwa na KRISTO Kama ROHO MTAKATIFU Au Nguvu ya Roho Mtakatifu Ndani Yenu.

ROHO MTAKATIFU NDIO KUNDALINI YENYEWE, NGUVU YA ROHO MTAKATIFU NI KUNDALINI ENERGY ILIYO NDANI YAKO.
🙏🙏🙏🙏🙏
KUNDALINI ENERGY SIYO ROHO MTAKATIFU. Nitataja sababu
Kwa mara ya kwanza, hapa duniani Roho Mtakatifu alishuka kwa ajili ya watu wote siku ya PENTEKOSTE, wiki kadhaa baada ya Yesu kupaa mbinguni

Kabla ya hapo, RM alikuwa anashuka kwa watu maalumu tu kama vile MANABII, MAKUHANI, WAFALME, na pia kwa special annointee waliokuwa wanapewa kazi maalumu na Mungu, kama vile SAULI au SAMSON

Kufuatana na maelezo yako hapa, KUNDALINI energy inapatikana ndani ya mwili wa mtu na hivyo hguvu hii si sawa na nguvu ya RM kwa sababu inavyoonyesha, KUNDALINI energy ni MECHANICAL IN NATURE, wakati nguvu ya RM ni SPRITUAL

Mbali na hilo, KUNDALIN ENERGY HAIWEZI KUWA ROHO MTAKATIFU KWA SABABU imekuwepo tangu kuumbwa kwa mwanadamu wakati Roho Mtakatifu alishuka hivi kafribuni tu siku ya Pentekoste, takribani miaka 2000 tu iliyopita
 
Hapana bhana.. Ulichosema kuhusu Roho Mtakatifu ni vitu viwili tofauti.. Si semi kama nimekubali katika kumjua lakini kanuni namba moja ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani ya mtu ni lazima awe amezaliwa mara ya pili..
 
Hapana bhana.. Ulichosema kuhusu Roho Mtakatifu ni vitu viwili tofauti.. Si semi kama nimekubali katika kumjua lakini kanuni namba moja ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani ya mtu ni lazima awe amezaliwa mara ya pili..
Kuzaliwa mara ya pili kivipi? fafanua.
 
2 Wakorintho 5:17.
17. Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Hivyo..
Basi kama ndo hivi ili mtu ajae nguvu za Roho Mtakatifu halazimiki kuwa Mtristo kwanza. Anaweza kujaa roho akishakuwa anamuamini Munbu na Mungu akiwa na kusudi naye anamjaza tu kama ambavyo amekuwa akifanya tangu enzi za Mababu. Hata Sauli alikuwa anajazwa nguvu za Roho Mtakatifu na roho chafu pia.
 
Basi kama ndo hivi ili mtu ajae nguvu za Roho Mtakatifu halazimiki kuwa Mtristo kwanza. Anaweza kujaa roho akishakuwa anamuamini Munbu na Mungu akiwa na kusudi naye anamjaza tu kama ambavyo amekuwa akifanya tangu enzi za Mababu. Hata Sauli alikuwa anajazwa nguvu za Roho Mtakatifu na roho chafu pia.
Yohana 3:1.,2.,3.,4.,5.,6.,7.,8.
1. Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2. Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. 3. Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5. Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. 8. Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
 
Basi kama ndo hivi ili mtu ajae nguvu za Roho Mtakatifu halazimiki kuwa Mtristo kwanza. Anaweza kujaa roho akishakuwa anamuamini Munbu na Mungu akiwa na kusudi naye anamjaza tu kama ambavyo amekuwa akifanya tangu enzi za Mababu. Hata Sauli alikuwa anajazwa nguvu za Roho Mtakatifu na roho chafu pia.
Yakobo 3:11.,12.
11. Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu? 12. Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.


Mathayo 22:29.
29. Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.



Mungu ambaye ni mwema ambaye anatoa roho Mtakatifu ambaye ndio roho wake mwenyewe anaweza kutoa roho chafu? Inamaana anayo hiyo roho chafu pia???


Yoeli 2:28.
28. Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

Agano la Kale ndio walikuwa wanapewa roho kwa kazi maalum na ni kama portion lakini zama hizi ni kwa kila atakae muamini Yesu Kristo.


Ezekieli 36:26.,27.,28.,29.
26. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. 28. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. 29. Nami nitawaokoeni na uchafu wenu wote; nitaiita ngano, na kuiongeza, wala sitaweka njaa juu yenu tena.

Hii ndio kusudi la kupewa Roho Mtakatifu
 
Back
Top Bottom