Roho Mtakatifu ndiye suluhisho la kudumu la matatizo ya mwanadamu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!

Kama kitu mwanadamu anapaswa kujuta akikosa basi ni Roho Mtakatifu.

Kitu cha thamani mno.

Mtu aliyejawa Roho Mtakatifu na akaishi kwa kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu hawezi kusumbuka kwa jambo lolote.

Natamani watu wote wapate kipawa hiki cha Roho Mtakatifu ili wapate suluhisho la kudumu la matatizo yao.
Wasitangetange na kutumia gharama kubwa kutafuta uponyaji na suluhu za matatizo yao.

Ingekuwa vizuri ule umati wa juzi kwa Mwamposa wangeombewa wajawe na Roho Mtakatifu wote ili wapate suluhisho la kudumu la matatizo yao, maana wale watu walienda pale kwasababu ya matatizo ya kifedha, ndoa, kesi, kazi na magonjwa.

Kwenye somo la Roho Mtakatifu kuna vipengele vingi. Kama nitapata watu angalau 10 walio tayari nitawafundisha hapa kwa siku 5-7 bure. Nitawafundisha vipengele vifuatavyo;

1. Roho Mtakatifu (maana na asili yake)

2.Umuhimu wa Roho Mtakatifu (kazi ya Roho Mtakatifu)

3. Namna mtu anapata Roho Mtakatifu

4. Utofauti wa Roho Mtakatifu na roho mchafu (kupambanua roho)

5. Ubatizo wa Roho Mtakatifu

6. Karama kuu 9 za Roho Mtakatifu (Nitachambua moja hadi moja)

7. Huduma na vipawa

8 Huduma ya kinabii na karama ya unabii (utofauti na uwiano wake).

9. Kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu ( kujua kutofautisha sauti ya ibilisi, ya Mungu na sauti yako binafsi. Hapa pia tagusia ndoto za kipepo, za Kimungu na za mwanadamu.

10. Nitajibu maswali.

Amina.
 
Baada ya kumpokea Yesu Kristo na kuzaliwa upya, yani kubatizwa, ulizaliwa katika familia mpya ya Kristo Yesu.

Awali tulikua chini ya Dhambi na hukumu ya damu asilia ya adamu lakini baada ya kumpokea Yesu, ulizaliwa upya, katika familia ya kiMungu. Roho Mtakatifu Yu nawe, unahitaji kuzungumza nae na kumuomba.

‭Yoeli 2:28 BHN‬
[28] “Kisha hapo baadaye nitaimimina roho yangu juu ya binadamu wote. Watoto wenu wa kike na wa kiume watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.

Haya ni maneno ya nabii Yoeli, Roho Mtakatifu ndie msaidizi wetu, Tena tuna neema sana kua nae tofauti na watu walioishi kabla ya Yesu, ilibidi wamtafute Kuhani. Lakini Kuhani wetu ni Yesu, na roho wake you nasi siku zote kutusikiliza, kutufundisha na kutuongoza namna ya kuishi maisha yanayompendeza Mungu.

Ingekuwa vyema ungeeleza namna gani yakumpata huyo Roho Mtakatifu
 
Hii kuhusu kipawa imekaaje mkuu

Funguka kidogo tupate Maarifa
Kuhusu Vipawa vya roho vimeeleza vyema katika 1 Korinto 12

‭1 Wakorintho 12:28 BHN‬
[28] Mungu ameweka katika kanisa: Kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.

Hivi ni Vipawa vya roho Mtakatifu, vinakuja baada ya kumpokea Yesu, na vinahitaji utumike Ili uweze kujua nguvu Yako iko kwenye kipawa Gani
 
Hadithi za roho mtakatifu ni sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.
FB_IMG_1715617688837.jpg
 
Hadithi za roho mtakatifu ni sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.
View attachment 3040662
roho Mtakatifu ni real na Mimi Binafsi nashuhudia matendo ya Mungu maishani mwangu. Hao samaki watu wanaelezewq kwenye biblia kwenye kitabu Cha Mwanzo 5, ni jamii ya Nephilims. Dinosaur walitengenezwa na Wazungu tu kupata story japo mifupa ni kasli ila muonekano wao ni nadharia.

Yesu, mwana wa Mungu Kila Imani Duniani inakiri ukweli kua alikua ni Mungu na kwamba aliishi. Hakuna jina kuu kuliko la Yesu
 
Thibitisha uwepo wa huyo Yesu na si imani na mawazo yako ya kufikirika tu.

Au hadithi uchwara za biblia zisizo na uthibitisho wowote ule wala uhalisia.
 
Hello!

Kama kitu mwanadamu anapaswa kujuta akikosa basi ni Roho Mtakatifu.

Kitu cha thamani mno.

Mtu aliyejawa Roho Mtakatifu na akaishi kwa kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu hawezi kusumbuka kwa jambo lolote.

Natamani watu wote wapate kipawa hiki cha Roho Mtakatifu ili wapate suluhisho la kudumu la matatizo yao.
Wasitangetange na kutumia gharama kubwa kutafuta uponyaji na suluhu za matatizo yao.

Ingekuwa vizuri ule umati wa juzi kwa Mwamposa wangeombewa wajawe na Roho Mtakatifu wote ili wapate suluhisho la kudumu la matatizo yao, maana wale watu walienda pale kwasababu ya matatizo ya kifedha, ndoa, kesi, kazi na magonjwa.

Kwenye somo la Roho Mtakatifu kuna vipengele vingi. Kama nitapata watu angalau 10 walio tayari nitawafundisha hapa kwa siku 5-7 bure. Nitawafundisha vipengele vifuatavyo;

1. Roho Mtakatifu (maana na asili yake)

2.Umuhimu wa Roho Mtakatifu (kazi ya Roho Mtakatifu)

3. Namna mtu anapata Roho Mtakatifu

4. Utofauti wa Roho Mtakatifu na roho mchafu (kupambanua roho)

5. Ubatizo wa Roho Mtakatifu

6. Karama kuu 9 za Roho Mtakatifu (Nitachambua moja hadi moja)

7. Huduma na vipawa

8 Huduma ya kinabii na karama ya unabii (utofauti na uwiano wake).

9. Kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu ( kujua kutofautisha sauti ya ibilisi, ya Mungu na sauti yako binafsi. Hapa pia tagusia ndoto za kipepo, za Kimungu na za mwanadamu.

10. Nitajibu maswali.

Amina.
Ubarikiwe Mtumishi.
Endelea na somo, hata kama mwezi mzima. Wewe fundisha tu

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom