Kumkufuru Roho Mtakatifu ni dhambi pekee inayotajwa katika Biblia kuwa haina msamaha milele. Kulingana na mafundisho ya Yesu katika Mathayo 12:31-32 na Mariko 3:28-30, dhambi hii inahusisha kukataa kwa makusudi na kwa kudumu kazi ya Mungu na neema yake ya wokovu.
Matumizi mabaya kwa jina la RM na matokeo mabaya yanayowapata watu walioamini kwa UJINGA wao wenyewe hakuhalalishi mtu kukanusha uhalisia wa RM.
HUNA HOJA, umeelezea uzoefu ulioshuhudia kwa watu wasiokuwa na maarifa. lakina kwa upande mwingine wapo waliofanikiwa kwa jina la RM.
RM sio wa mchungaji, nabii wala mwalimu, kama hajakusemesha wewe ukimwamini aliyesemeshwa ukapata matokeo mabaya hilo halitoshi kujenga hoja ya kukanusha utendaji wa RM.
MFN. Mimi niliwahi kuambiwa niache shule niwe mchungaji, kwa kisingizio wanaona Roho wa Bwan anashuhudia mimi ni mchungaji wao na mafanikio ntapata kupitia UCHUNGAJI.
Sikukataa niliingia kwenye maombi ya siku 21, baada ya 21 days nikaja na jibu kuwa MM SIJASIKIA. walinilaumu sana kwamba mm nimkaidi lakini fact ni kwamba MM SIJASIKIA.
Leo nimepiga hatua kubwa halafu walewale walotaka niache kusoma niwachunge, kila mmoja ananipa kongole kwa adabu na utumishi unaendelea.
Ukweli ambao sipingi ni kwamba watuwanatapeliwa mjini kwa jina la RM lakini ila sio kweli kwamba RM ni utapeli kwenye maisha ya mwanadamu
KIPI KINATOKEA
1; Tamaa ndo zinawasukuma watu kuamini au kutenda kila kitu hata kila ambacho roho mtakatifu hajaongoza
Yakobo 1:14, "Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa yake mwenyewe."
(a) Tamaa ya heshima na madaraka kwa mtenda.
(b) Tamaa ya kufanikiwa kwa mtendwa
2; Kutokuwa na maarifa ya utendaji wa RM kwenye maisha ya mwanadamu.
Hosea 4:6, ambapo Mungu anasema: "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa."
Mwisho;
Sio kila mtumishi, nabii, mtume ni wa MUNGU, namna ya kuwatambua;