Roho ya CCM inaning'nia kwenye uzi ulioshikiliwa na Jeshi la Polisi

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Usiporuhusu ushindani kwenye biashara yako huwezi kujua ubora wa bidhaa zako kwenye soko, vile vile usiporuhusu uchaguzi huru huwezi kujua kama wananchi bado wanakiunga mikono chama chako.

Imagine Simba aikimbie Yanga kwenye mechi na mwisho wa ligi Yanga atangazwe bingwa, au Azam TV aikimbie ITV mwisho wa siku atambe yeye ni Superbrand.

Kumuengua au kumkimbia mpinzani wako ni dalili za uoga na kuishiwa mbinu.

Siku jeshi litakapotambua majukumu yake kwa wananchi ndipo utakapokuwa mwisho wa CCM kwa sababu haitakuwa na base yeyote kwa wananchi.

CC. Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Siku jeshi litakapotambua majukumu yake kwa wananchi ndipo utakapokuwa mwisho wa CCM kwa sababu haitakuwa na base yeyote kwa wananchi.🙏🏾
Hiyo siku haitafika Leo kwa sababu Vyombo vya ulinzi vya TANU ndio vikageuka kuwa vya Serikali baada ya Nyerere kupewa Uhuru UN na Dola ya muingereza kuondoka

Nyerere hakuwaga Mjinga kukubali Upinzani wa 20% 😀😀
 
Vilikuwepo vyama vya, ZANU-PF, SWAPO, FRELIMO, ANC, MCP, UNIP, KANU, where are they, nchi zao hazikuwa na jeshi la polisi?

Utabaki na mawazo ya Nyerere kwa muda gani? Change is inevitable.
 
Vyama Vyote ulivyovitaja vilipigania Uhuru lakini Tanu Ilipewa Uhuru

Sidhani kama utaelewa 🐼😃
 
Ndio sababu nimesema Siyo " Leo"
Kasema "kila kitu kina mwisho wake", hata mimi sijasema leo, nimesema

"Siku jeshi litakapotambua majukumu yake kwa wananchi ndipo utakapokuwa mwisho wa CCM".
 
Sawa viko wapi?
Viko viliko

Nchi zenye wapiganaji madaraka huwa ya kupokezana

Nchi zenye Waongeaji madaraka huwa ya mwenye sauti

Nyerere alivyofuta uchifu Kimsingi aliwaondoa wapiganaji wakabaki Wazungumzaji 😂
 
Siku jeshi litakapotambua majukumu yake kwa wananchi ndipo utakapokuwa mwisho wa CCM kwa sababu haitakuwa na base yeyote kwa wananchi.🙏🏾
Ndio ukweli mkuu Mshana.
Na wanajua ukweli huu ndio maana wanafanya hadi ushetani ambao hata shetani hakuwahi kufanya kwenye uchaguzi huu.
 
Usiporuhusu ushindani kwenye biashara yako huwezi kujua ubora wa bidhaa zako kwenye soko, vile vile usiporuhusu uchaguzi huru huwezi kujua kama wananchi bado wanakiunga mikono chama chako.

Imagine Simba aikimbie Yanga kwenye mechi na mwisho wa ligi Yanga atangazwe bingwa, au Azam TV aikimbie ITV mwisho wa siku atambe yeye ni Superbrand.

Kumuengua au kumkimbia mpinzani wako ni dalili za uoga au kuishiwa mbinu.

Siku jeshi litakapotambua majukumu yake kwa wananchi ndipo utakapokuwa mwisho wa CCM kwa sababu haitakuwa na base yeyote kwa wananchi.

CC. Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.
Ubaya viongozi wa Jeshi ni makada wa CCM
 
Ndio ukweli mkuu Mshana.
Na wanajua ukweli huu ndio maana wanafanya hadi ushetani ambao hata shetani hakuwahi kufanya kwenye uchaguzi huu.
Ushawishi wa CCM kwa wananchi umepungua sana ni suala la muda tu kitasahaulika.
 
Hiyo siku haitafika Leo kwa sababu Vyombo vya ulinzi vya TANU ndio vikageuka kuwa vya Serikali baada ya Nyerere kupewa Uhuru UN na Dola ya muingereza kuondoka

Nyerere hakuwaga Mjinga kukubali Upinzani wa 20% 😀😀
Hiyo siku itafika watu watakalozaliana mpaka vijijini vijana wakakosa mashamba ya kulima; nchi yote itakapogeuka ya wapiga debe, machinga, wacheza kamari n.k; mbaya zaidi huko UVCCM n.k kutakuwa kumekorogeka, hakukaliki na kahuna fursa za uchawa na kubeba mikoba.
Ubaya ni kwamba kipindi hicho wengi wetu hatutakuwa hai, iwapo JF itakuwa hai vijana za wakati huo watafanya rejea
 
Vilikuwepo vyama vya, ZANU-PF, SWAPO, FRELIMO, ANC, MCP, UNIP, KANU, where are they, nchi zao hazikuwa na jeshi la polisi?

Utabaki na mawazo ya Nyerere kwa muda gani? Change is inevitable.
Kabla hujaandika kitu ni vyema kufanya utafiti japo kidogo tu ili kujiridhisha, Zimbabwe bado inaongozwa na ZANU PF, Namibia bado inaongozwa na SWAPO, Msumbiji bado yaongozwa na FRELIMO, Malawi inaongozwa na MCP, ANC bado imetoa raisi wa South Africa.
Watanzania sio tu kwamba wameichoka CCM, Wamechoka vyama vyote vya siasa, ndio maana hawajiandikishi kupiga kura, na kwenye maandamano pia hawatokei, suluhisho ni vyama vya upinzani kuacha undumilakuwili ili waTZ wapate chombo cha kuwasupport, kwa sasa CCM na Upinzani vyote havieleweki.
 
Back
Top Bottom