Roho ya kukataliwa: Chanzo/asili na madhila yake

chukua muda wa kuzipumzisha hisia
 
the moment of truth, mwambie waweza kwenda
 
Asante Jr. Umenifungua macho. Nimepata kitu hapa
 
Mkuu kuna wakati mwingine unaandika "point" na kuna nyakati unaandikaga "ugoro" mtupu. Hii thread ya leo kiasi fulani inafundisha kumtumainia MUUMBA, lakini umeharibu unaposema watu watumie "chumvi". Hapo unakuwa umeingiza ushirikina tayari.

Mkuu hakuna chemi chemi itoayo maji moto na maji baridi kwa wakati mmoja. Au chemi chemi itoayo maji "matamu" na maji "chumvi" kwa wakati mmoja. Wewe unatoa vyote kwa wakati mmoja, haiwezekani bhana. Kama umeamua kuwafundisha watu kumtegemea MUNGU, basi sisitiza hapo hapo kwenye MUNGU, na usiingize tena imani za kishirikina.
 
Mkuu, hapo kwenye kutumia chumvi hebu ongezea nyama tafadhali. Mada yako nzito sana aisee


Naomba kufahamu zaidi kuhusiana na hiyo tiba ya chumvi mkuu?

mshana Jr kaka vipi kuhusu kitunguu swaumu na matumizi yake kukwepa nguvu za giza na kiafya?
Tazama namna ambavyo wanadamu wanaacha kumtumainia MWOKOZI YESU KRISTO na kuitumainia "chumvi" iwasaidie. Mimi nimesoma Biblia yote, na siyo mara moja, sijaona mahali YESU KRISTO ameagiza tukipata matatizo hapa duniani tutumie chumvi.

Hii tiba ya kuogea chumvi ni imani ya kishirikina na ningewashauri Wakristo wenzangu tuache huu upuuzi na tumtumainie YESU KRISTO. Imeandikwa hivi; "Mjue sana MUNGU ili uwe na amani. Ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee tafadhali mafunzo yatokayo kinywani mwake, na maneno yake yaweke moyoni mwako. Ukimrudia MWENYEZI utajengwa; ukiuondoa udhalimu mbali na nyumba yako"........ "Naye MWENYEZI atakuwa hazina yako, atakuwa ni fedha ya thamani kwako.....Utamwomba yeye naye atakusikia, nawe utazitimiliza nadhiri zako. Nawe utakusudia neno nalo litathibitika kwako; na mwanga utaziangazia njia zako". AYUBU 22:21-30

Tena YAKOBO akaandika hivi; "Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe.....Mtu wa kwenu amekuwa hajiwezi, na awaite wazee wa Kanisa nao wamwombee na kumpaka MAFUTA kwa jina la BWANA. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule na BWANA atamwinua". WARAKA WA YAKOBO 5:13-15

Jamani, hakuna mahali imeandikwa tuitumainie "chumvi".
 
.... Naandika ugoro mtupu.... Naona huufahamu ulimwengu wa giza vizuri... Chumvi na mchawi ni vitu viwili tofauti kabisa na pia kumbuka Bwana Yesu alitumia chumvi hiyo hiyo kutakasa na hata maji ya baraka yanatengenezwa kwa kutumia chumvi ingia hapa kwa elimu zaidi.... jinsi ya kuchaji maji
 
...usimwache muumba wako hata nukta moja.. Hakuna binadamu aliyezaliwa na mwanamke anaweza kusafisha nyota yako ikasafishika milele.. HAKUNA.. hakuna mganga atakayeweza kukupa mafanikio yasiyo na maagano HAKUNA... hakuna Pete ya bahati isiyokosa mawaa HAKUNA... jaribu kuivua siku moja uone shughuli yake... Maudhui hii ni muhimu sana kuielewa!
 
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Naomba unioneshe kifungu kwenye Biblia kinachosema BWANA YESU, alitumia "chumvi" kutakasa.
 
Mkuu mi mwenyew naijua biblia vizur, ilaa nakushauri ukaisome vizuri.
Acha kupanik bro..

Ni hv Yesu mwenyew alimtibu yule kipofu kwa kutumia matope Refer. The book of Luke
Pia Paulo alimwambia Timotheo atumie kilevi kwa ajil ya uponyaji wa tumbo lake. Likewise Mfalme Naaman aliambiwa na Elisha akajichovye mtoni mara 7 na ukoma wake ukaisha.
Ipo mifano mingi tu, ukitaka nitaendelea kukutajia, ila cha muhmu faham kuwa Mungu kuna wakat anaponya kwa kutumia vtu mbalimbali ikiwemo chumvi hata tope, na kingine ukijuacho.

Mungu n mpana kulko tumzaniavyo mkuu
 
Mkuu MshanaJR hetithe avae,
Aisee leo nimeshangaa ulivoidadavua hii mada kama vile haya maswahbu yameshakupata.. Maana umenena vyema kabisa, haya mambo yapo na yanasumbua Watu sana.

Ngoja nikae vizur nikuongezee nyama kweny hii mada maana nayajua mengi sana kuhusu kukatalika au wenyewe wanasema kupewa USO WA STARA (USO WA KUKATALIKA) sio kwa wanadamu tu bali hata kwa Mungu

Hii ni roho mbaya sana. Mi nasemaga ni mbaya kulko zote, maana ina mateso sana na ndio mara nyng inapelekea wengi kujiua
 
Usijali nikiipata takuonyesha
Levictus 2:13, Exodus 30: 34-35
Mkuu mshana jr hapa tusidanganyane kabisa. Leviticus 2:13(WALAWI) inasema hivi; "Tena kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la MUNGU wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote".

Hapo tunaona chumvi ilitolewa pamoja na unga kama sadaka, tena siyo chumvi tu, ukiendelea kusoma mstari wa 14, utaona maelekezo yanaendelea kusema kwenye unga huo wa sadaka waweke na mafuta na ubani. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwenye moto kwa ajili ya MUNGU.

Ni kama vile wewe ukipika chakula chako unaweka na chumvi na mafuta, basi hivyo hivyo ukimtolea MUNGU sadaka ya unga, unapaswa pia kuweka chumvi na mafuta na harufu nzuri ya ubani. Kifungu hichi ni irrelevant kabisa na hoja yako ya KUOGEA CHUMVI, yaani ni vitu viwili tofauti kabisa wala haviendani. Hakuna mahali Waisraeli waliagizwa waoge maji kwa kuyatia chumvi. Hakuna!

Kifungu kingine ni hicho cha Exodus 30:34-35(KUTOKA), hapa tunaona MUNGU anampa Musa maelekezo namna ya kutengeneza manukato kwa ajili ya kuweka ndani ya HEMA LA BWANA. Tena BWANA MUNGU, aliwakataza kabisa Waisraeli, mtu asije akatengeneza manukato kama hiyo kwa kutumia viungo vya aina hiyo na kisha kuitumia yeye binafsi. Manukato hiyo ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya BWANA MUNGU, pekee. Ilikuwa ni manukato takatifu sana, na hakuna mwanadamu anaruhusiwa kuvuta harufu yake!

Hapa pia tunaona hakuna swala la chumvi, wala kuoga kwa maji yaliyotiwa CHUMVI! Hoja yako haiendani na hivyo vifungu vya Biblia ulivyonipa. Mimi nakataa kabisa, kuoga kwa maji yaliyotiwa chumvi kwa lengo la kuondoa "mikosi", ni kitendo cha "kishirikina" kabisa.

Narudia tena kusema, tukiwa kama Wakristo, na wewe mshana jr ukiwa kama MKRISTO pia, unapaswa kuweka imani yako na matumaini yako kwa YESU KRISTO, na siyo vinginevyo. YESU alisema hivi; "Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini, jipeni moyo; nimeushinda ulimwengu".
 
Mshana jr natamanii ungekuwa mzee wanguu...maana madini kama haya vijana ndani ya familia hatu ya pati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…