Roho ya kukataliwa: Chanzo/asili na madhila yake

Mkuu mshana jr hapa tusidanganyane kabisa. Leviticus 2:13(WALAWI) inasema hivi; "Tena kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la MUNGU w
Asante ila naona unataka tuitafsiri Biblia kama novel na si kitabu kitakatifu chenye tafsiri za kiroho.. Nimekuwekea vifungu hivyo kama njia ya kupanua ufahamu... Vipo vingi kama chumvi ilitumika kutengeneza vingine kwanini isitumike kwenye maji?
Bado naomba niseme kuwa inawezekana kabisa hujaelewa dhana nzima ya uchawi na jinsi unavyofanya kazi... Kuogea maji ya chumvi sio uchawi ndugu yangu
 
Mshana jr natamanii ungekuwa mzee wanguu...maana madini kama haya vijana ndani ya familia hatu ya pati.
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji781] [emoji779] [emoji770]
 
kuna mtu analalamika kaachwa na mpenzi wake natamani asome uzi huu
 
Mimi nataka uniambie ni wapi YESU aliagiza mtu akipatwa na matatizo achukue maji aweke chumvi na aoge kisha hayo matatizo yake yatakwisha au mikosi itakwisha. Au unioneshe ni wapi MITUME waliwaagiza watu hayo mambo ya kuoga na CHUMVI.

Ukiniambia sijui YESU alitumia tope, YESU hakutumia tope peke yake, alichanganya tope na mate yake. Je! leo hii wewe waweza changanya tope na mate yako na mtu akapona?? Tena YESU hakuwaagiza wanafunzi wake nao watumie tope na mate yao kuwaponya watu. Bali aliwaagiza watumie JINA LAKE (YESU KRISTO) kuponya. Soma Biblia yako vizuri, siyo PETRO, wala PAULO, wala mtume yeyote yule aliponya kwa kutumia tope na mate, hakuna! Waliwaponya watu kwa JINA LA YESU WA NAZARETI.

Kuhusu wine (mvinyo) hii inajulikana ni dawa ya tumbo. Waisraeli walikuwa wanaitumia kujitibu tumbo miaka yote kabla hata Paulo hajazaliwa duniani. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kumeza dawa kwa ajili ya ugonjwa na kuoga maji ya CHUMVI kwa ajili ya kuondoa eti "mikosi".

Mikosi ni matatizo yanayomwandama mtu. Matatizo mengi yanayotuandama sisi binadamu yanasababishwa na DHAMBI zetu. Mikosi ipo ndiyo, lakini sababu mikosi inasababishwa na dhambi, haiwezekani kuiondoa kwa kuoga maji ya CHUMVI. Mikosi inaondolewa kwa mtu kutubu dhambi zake, kumwamini YESU KRISTO, na kubatizwa kwenye maji kwa JINA LA YESU. Hiyo ndiyo njia pekee ya kusafisha dhambi, na dhambi ndiyo inayobeba mikosi ya kila aina na mabalaa ya kila namna.

Shetani ni mjanja sana, anawadanganya mtumie chumvi kuogea na ninyi bila ufahamu wa NENO la MUNGU mnapotea kwenye madanganyo ya ULIMWENGU huu. Njia pekee ya kukuondolea mikosi, na laana na mabalaa ni JINA LA YESU peke yake. Tena mikosi mingine haitoki hivi hivi tu pasipo KUVUNGA NA KUOMBA KWA DHATI.

Endeleeni kudanganyika na chumvi zenu.
 
Acha kabisa kuwadanganya watu ndugu yangu. Hizo ni imani za kishirikina kabisa. Mimi kamwe sikubaliani nazo. Lakini kila mtu yuko huru kuifuata njia aitakayo. Lakini pia njia ya "KWELI" ipo na anayetaka kuifuata na awe huru kuifuata.

Njia ya KWELI ni JINA LA YESU KRISTO na mafundisho yake basi. YESU alisema hivi; "Mimi ndiyo NJIA, KWELI na UZIMA."

Tafakari ndugu yangu.
 
Mtumishi naona upeo wako wa kuyafahamu na kuyatizama mambo n mdogo sana..
Na sabab ni kuwa umekariri biblia kama ulivyofundishwa. Biblia ni pana Sana kuliko umavyoifaham.
Si kwel kwamba kila anayepitia mateso/balaa/magonjwa fulan bas ni kwa sabab ya dhambi... No si kwel
Nakujibu kwa andiko toka kitabu cha Marko pale yesu alivoletewa yule kipofu na yule kilema kuwaponya, ndiposa wanafunz wake wakamwuliza Je? Ni kwasabab ya nn had wale wamepata upofu na kilema? Yesu akajibu si yeye (kipofu/kilema) wala wazaz wake wala ndugu zake aliyesababsha madhila hayo kwake, bali wamefanywa hvyo ili utukufu wa Mungu udhihirike.
****//÷**TAFAKARI HILI SANA **////****

Aidha, tambua kuwa bwaba yesu alimsamehe dhambi yule kahaba aliyemlilia kwa kutoa machoz miguun mwake na pia yesu alitumia ishara ya kupaka mafita kama alama ya kusamehewa na kupokea baraka. Nnachotaka kusema ni kuwa si kila kitu kinatoka kwa jina la Yesu, bali yapo mambo mengne ywtaondoka kwa njiq mbalimbal kama zilivyoelwzwa hapo awali.
 
Hakuna hoja yoyote ya msingi uliyoandika hapa. Ukweli utabakia pale pale kuwa dhambi ndiyo iliyoleta matatizo yote duniani na siyo vinginevyo. Kama dhambi isingekuwepo hata hiyo mikosi pia isingekuwepo. Huo ndiyo ukweli dhahiri. Biblia yenyewe imeandika wazi kabisa kuwa wanadamu wote wamefanya dhambi chini ya jua. Hakuna hata mmoja aliyemsafi. Wewe ukatae au ukubali lakini mikosi na mabalaa husababishwa na dhambi.

Na isitoshe hiyo chumvi mnayosema haiwezi kumfanya kipofu aone tena HAIWEZI kumfanya kilema atembee. Kutumia chumvi kwa imani ya kuondoa sijui mikosi au sijui kusafisha nyota, ni aina ya ushirikina, and its not Biblical. Hizo ni imani potofu za kishirikina na siyo maagizo ya Mitume. Hii mambo ya chumvi, ni tiba za waganga wa kienyeji, tiba za vigagula. Akili zenu zimejaa imani za kishirikina kuliko imani ya MUNGU. Mnaupenda uwongo kuliko KWELI ya MUNGU. Mmekulia katika familia zinazojishughulisha na uchawi na ushirikina ndiyo maana inawawia vigumu sana kuifahamu KWELI ya MUNGU. Matokeo yake mnaichanganya KWELI ya MUNGU na imani za KICHAWI.

Nimesema, na narudia tena kusema; nataka unioneshe ni wapi Mitume walifundisha kuwa, mtu akipata matatizo, achukue chumvi aweke kwenye maji na aoge kisha matatizo yake yatakwisha. Kama kweli hii ni tiba inayokubalika na MUNGU, basi hata Mitume wa MUNGU wangeifahamu na wangeifundisha kwa wanadamu kama tiba halali.

Narudia tena kusema, suluhisho la matatizo ya mwanadamu ni JINA LA YESU pekee. Hakuna suluhisho lingine lolote zaidi ya JINA LA YESU KRISTO.
 
Roho ya kukataliwa.....I do believe tutakataliwa na wengi ila Baba wa Mbinguni hawezi kutukataa...Live long JF, God bless you Kaka Mkubwa Mshana
 
Roho ya kukataliwa.....I do believe tutakataliwa na wengi ila Baba wa Mbinguni hawezi kutukataa...Live long JF, God bless you Kaka Mkubwa Mshana
Aaamen barikiwa zaidi [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Duuu....kama kuna ukweli fulani hivi mana kiwango kikubwa kwangu yana ukweli kabisa roho hiyoo ipo yani hata nikivaa smart kabisa bado na one kana nipo ovyo yani nipo nipo tuu hali ya kiuchumi sio haba sana a ila daa story ndefu mkuu ...

Mshana Jr. ..
 
Pole sana kama hutojali unaweza kufunguka hapa ama la njoo PM tuongee machache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…