Role of Indians in the Tanzanian Economy

Role of Indians in the Tanzanian Economy

Wao kama sio wabaguzi kwanini wasionyeshe ushirikiano na usawa katika maisha yao ya kila siku?mimi naishi nao jirani hawashiriki kabisa kwenye misiba na hata kwenye shughuli nyingine za kijamii.

Bado sitaki kuamini kuwa wahindi ndiyo mafisadi, kuna wahindi wazalendo damu hasa na pengine kupita hata baadhi yetu mfano Prof. Issa Shivji.

Tatizo la nchi yetu si wahindi, tatizo la nchi yetu ni "Viongozi corrupt", hawa ni watu ambao naweza kusema kwa uhakika si wazalendo hata kidogo na hawa ndiyo wa kuwashughulikia zaidi. 99.9999% ya Viongozi wa CCM (nawataja hawa kwa kuwa ni watawala) kuanzia ngazi ya kata mpaka taifa ni wabinafsi na waroho wa utajiri. Wengi ya viongozi hawa wanafikra finyu za kuona kuwa kushinda uchaguzi ndiyo kipimo cha ulaji wao. kuanzia "serikali za mitaa na kwenye matawi". Na majority wanawatumia wahindi kama ngazi either kuombaomba na kupitisha bakuli. Yaani kwa upande wa wahindi kodi hukusanywa na CCM kupitia michango. Kwenye mashina, kata,wilaya,mikoa na mpaka taifa target yao kwenye fundraising ni wahindi. kazi wanazofanya viongozi hawa ni

1. Kuorozesha maduka ya wahindi wote kwa kuwa hawa ni waoga sana na kuwaambia kila mwezi watoe kiasi kadhaa, wakiisha fanya hivyo wanaona mambo yao yanaenda vizuri tu, hata kama wakikwepa kodi hawaguswi, si wameshalipa via michango?

2. Wahindi hawa wakiishaambiwa kwa muda mrefu kuchangia wanaona suluhu ni wao pia kugombea uongozi CCM (Azim Premji, Rostam et al, hawa ni miongoni mwa wahindi wa mwanzo kugombea nafasi CCM). CCM baada ya kuwakubali kwa kisingizio kuwa nchi yetu haibagui kwa kushindwa kujua kuwa hawa ni wajasiliamali na si wanasiasa wala viongozi kwani hawana uchungu kabisa na maisha watanzania zaidi ya kufanya biashara (Mabwanyenye, wanyonyaji)

3. Wakiisha ingia kwenye system wanakuwa wachoraji wa michongo kibao ya kujinufaisha huku wakiwashirikisha wanasiasa wetu wa kibantu walioona nyota kupata uongozi na kuipora nchi kwa style tofauti kama ( miradi mbalimbali n.k) huku viongozi nao ni shareholders waliojificha na kupokea gawio lao kisirisiri (Corruption).

4. Hapo sasa ndipo mgongano wa maslahi unapokuja mtu ni mmoja ni mtoa maamuzi na wakati huo huo maamuzi yake yanaweza mnufaisha direct unatarajia afanye nini?

5. Kinachofuata sasa ni kukomba mpaka wanawashika mikono wananchi yaani kila kona ya system, hapo sasa kila mtu anaona kumbe dili ni kumake mbona mkuu yule anafanya hivi na yeye anaunga tera na ku-collude na kuua system nzima ya uongozi Tanzania.


Kama mnakumbuka Nyerere aliisha mramba mtuviboko kwa kutamka kawaweka viongozi mkononi kwa sababu ni aibu sana.

Cha kufanya CCM iwatoe wafanyabiashara wote katika uongozi na kuzirejea zile kanuni za TANU kuwa ni mwiko kwa kiongozi kuwa na "HISA katika kampuni binafsi"

Vinginevyo wahindi tunawaonea tu wabaya ni wenye ngozi nyeusi kama majority ya sisi watanzania. Sasa hivi nchi ipo uchi yaani ukiingia polisi, pesa, mahakamani pesa, ukienda jeshini pesa, ukiingia usalama wa taifa pesa yaani kila mtu anahitaji kuwa tajiri fasta fasta na wahindi kama wajasiliamali wameliona hilo na kuchukua kama opportunity ya kumake profit.


SULUHU PEKEE: Ni CCM kuwa nje ya utawala wa nchi hata kwa miaka mitano (Wapinzani wakiingia wao watakuwa hawa network ya kihalifu kwani hawaungwi mkono na hawa wanyonyaji wapora nchi,Mafisadi) tu ili kunguni wote waliokivamia chama wapukutike, hapo tutapata CCM mpya yenye nguvu, mwelekeo na mwanga wa matumaini kwa watanzania wote.
 
The Following 12 Users Say Thank You to Mwafrika wa Kike For This Useful Post:
BabaH (11th February 2008), Gembe (11th February 2008), jmushi1 (12th February 2008), macho_mdiliko (20th September 2008), Mkandara (11th February 2008), Mtanzania (11th February 2008), Mzee Mwanakijiji (11th February 2008), Nsaji Mpoki (20th September 2008), Nyambala (11th February 2008), Nyumbu (21st September 2008), Positive Thinker (11th February 2008), Rubabi (11th February 2008)

kAZI KWELI KWELI
 
tumeanza na wachagga.. lets keep going..! hadi tujue ni mtanzania gani, ni kabila gani, ni watu wenye asili ya wapi watatuokoa! keep breaking the principle.. the "principle will find a way of breaking you" (Mwalimu)!

Look who is talking...
 
Msipende kuleta ubaguzi, jambo la msingi wafanya biashara hao wenye asili ya kihindi wafanye biashara zao kwa mujibu wa sheria. Je hakuna wafanyabiashara wa kiafrika wasiofuata sheria? Katika kesi za EPA kuna mchanganyiko wa wahidi na waafrika.
 
Swali je
a)wahindi wanamhonga nani?
b) nani anayepokea rushwa?
c) anayepokea rushwa alilazimishwa?
Kwakuwa wanaopokea rushwa kwa hiara yao nia maofisa wakubwa serikali tatizo siyo wahindi tatizo ni wabongo wenyewe... kama "wa tachange altitude yao" mhindi atafanya biashara kwa haki au ataondoka akiona vipi??
 
Salaam wakuu,
kwani kuna shida gani siku moja mtu mmoja mwenye nguvu akatwaa inji hii na akatangaza kufuta mikataba yote mibovu na kuinetiate upya pia kutokomeza rushwa yoye ikiwa pamoja na kukamata wote waliokuwa wakinufaika nayo??? mi sioni shida yeyote!
Naona watu tunazungushana hapa tuuu!
Natoa Shilingi.
Kwa amani.
 
nahisi kuna mtu keshakula "nyama ya mtu".....damn.....maana kila akilala akiamka ni fikra za kibaguzi tu.....aina ya watu kama hawa ni wa kuogopwa kama ukoma........
 
Swali je
a)wahindi wanamhonga nani?
b) nani anayepokea rushwa?
c) anayepokea rushwa alilazimishwa?
Kwakuwa wanaopokea rushwa kwa hiara yao nia maofisa wakubwa serikali tatizo siyo wahindi tatizo ni wabongo wenyewe... kama "wa tachange altitude yao" mhindi atafanya biashara kwa haki au ataondoka akiona vipi??

Neno ni "attitude" na si "altitude". Anyway nakubaliana na unavyo sema hapa. Hao wahindi hawali na wahindi wenzao wala hawawahongi wahindi wenzao. Siki zote mwenye kutongoza ana tongoza na anaye tongozwa anaweza kukubali au kukataa. Tatizo watanzania wengi hawaoni kuwa tatizo ni kubwa kuliko wahindi. Tatizo ni wala rushwa.
 
Salaam wakuu,
kwani kuna shida gani siku moja mtu mmoja mwenye nguvu akatwaa inji hii na akatangaza kufuta mikataba yote mibovu na kuinetiate upya pia kutokomeza rushwa yoye ikiwa pamoja na kukamata wote waliokuwa wakinufaika nayo??? mi sioni shida yeyote!
Naona watu tunazungushana hapa tuuu!
Natoa Shilingi.
Kwa amani.

Your idea is a good thought but very impractical. What are the chances of that happening?
 
Neno ni "attitude" na si "altitude". Anyway nakubaliana na unavyo sema hapa. Hao wahindi hawali na wahindi wenzao wala hawawahongi wahindi wenzao. Siki zote mwenye kutongoza ana tongoza na anaye tongozwa anaweza kukubali au kukataa. Tatizo watanzania wengi hawaoni kuwa tatizo ni kubwa kuliko wahindi. Tatizo ni wala rushwa.

Miaka mitano ya hii coment na baadhi ya michango mengine ya wana JF tatizo ni kuchange kwenye hilo neno kuanzia shule utamaduni na rushwa yenyewe.
Hata baada ya PPRA kuanzishwa bado kwenye manunuzi tunanunua kuliko bei ya soko sijui tunapinga nn hapa
 
Back
Top Bottom