KIUFUPI KABISA KITABU CHA DANIELI
Kitabu hiki kinakadiriwa kuwakilinadikwa
mwaka 165 K.K. kipindi ambacho Waisraeli
kutoka ufalme wa Yuda walikuwa wakitawaliwa
na Wagiriki waliotawala kutoka 333-63 K.K.
Mwandishi akiwa mtu kutoka ufalme wa Yuda
aliandika kitabu chake hususani sura ya 7 kwa
kuzingatia historia ya utawala wa ufalme huo
wa Yuda.
Hivyo mwandishi anawafariji watu waliokuwa
katika enzi ya madhulumu yaliyofanywa na
__ Wababeli kutoka mwaka 587-539 K.K.
___ Wamedi 539 K.K. (Isa 13:17).
___ Waajemi 538-333 K.K.
___ Wagiriki 333-63 K.K.
SASA NAOMBA NIJARIBU KUKUELEZEA
BAADHI YA AYA AMBAZO HUTOLEWA TAFSIRI
POTOFO NA BAADHI YA WATU
Mwandishi katika sura ya 7:1-12 anatumia
wanyama wanne ili kuwasilisha ujumbe wake.
Ukweli huu tunapata tunaposoma Dan 7:1-12; “
Danieli akanena, akisema: naliona katika maono
yangu wakati wa usiku, na tazama, hizo pepo
nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya
bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne
wakatoka baharini, wote wanamna
mbalimbali.” (Dan 7:2-3).
Na ukisoma Dan 7:15-28 mwandishi anatoa
tafsiri ya maono aua ndoto inayosimuliwa
kutoka Dan 7:1-14.
Wanyama hao wanne ni wafalme wa falme nne
zilizotokea duniani. (rej. Dan 7:17). Mnyama wa
kwanza alikuwa kama simba (7:4); mnyama
huyu anasimama badala ya ufalme wababeli
ambao walikuwa wa kwanza kuwatawala
Waisraeli walioishi ufalme wa kusini – ufalme
waYuda – kutoka587- 539 K.K.
Mnyama wa pili alikuwa kama dubu (7:5).
Mwandishi alimtumia mnyama huyu (dubu)
kama jina bndia la ufalme wa Wamedi
waliotawala kwa muda mfupi sana – yaani 539
K.K.
Mnyama wa tatu ni chui (7:6). Chui anasimama
badala ya ufalme wa Waajemi lililokuwa taifa la
tatu kuwatawala Waisraeli walioishi katika
ufalme wa Yuda. Waajemi walitawala kutoka
ufalme 538-333 K.K.
Mnyama wa nne anayeelezwa katika Dan 7:7-8
na ambaye hatajwi jina lake ; na ambaye
anaonekana kuwa ni mwenye kutisha sana, ni
ufalme wa Wagiriki ambao ulikuwa ufalme
shupavu uliowatawala Waisraeli kutoka 333-63
K.K.
Katika kitabu cha Dan 7:7-8 tunasoma hivi: “…
mnyama wa nne mwenye kutisha, mwenye
nguvu, mwenye uwezo mwingi, nayw alikuwa na
mwno ya chuma, makubwa sana; alikula na
kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga
mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa
mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa
na pembe kumi, nikaziangalia sana pembe
zake, na tazama, pembe nyingine ikazika kati
yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbgele yake
pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa
kabisa; na tazam, katika pembe hiyo moikuwa
na macho kama macho ya mwanadamu, na
kinywa kilikuwa kikinena mneno makuu.” (rej
Dan 7:7-8).
Pembe 10 ni wafalme 10 ambao wataondoka
katika ufalme huo. (Dan 7:24a). na Dan 7:24b
panasomeka hivi; “na mwngine ataondoka
baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa
kwanza, naye atawashusha wafalme watatu.’
Mfalme anayedokezwa katika Dan 7:24b ni
mfalme Antioko Epifani ndiye anayesemwa
kuwa atawashusha wafalme watatu. Ni mfalme
aliyeziangamiza falme tatu zilizokuwepo nyakati
zake. Na wafalme wa falme hizo tatu
walioshushwa ni: mfalme Ptolemy VI
Philometor mnamo mwaka 169 K.K.; mfalme
Ptolemy VII Euergete mwaka 169 K.K.; na
mfalme Artakias wa Armenia katika mwaka
166 K.K.
Ukisoma Dan 7:25, naadokezwa mfalme
ambaye atanena maneno kinyume chake Aliye
juu,naye atawadhoofisha watakatifu wake Ailye
juu. Mfalme huyo pia ni Antioko Epifani
ambaye aliwalazimisha Wayahudi (walioishi
Palestina) kufuata utamaduni wa Kiyunani aua
Kigiriki kwa kuiacha dini yao katika Mungu wa
kweli na kufuata dini ya Kipagani kama
tusomavyo 1Macc 1:41-64. Ili kufanikisha
lengo lake la kukomesha dini ya Kiyahudi na
kueneza utamaduni wa Kigiriki aliamuru hekalu
la Zeus – mungu wa kipagani; pia alipiga
marufuki kwa Wayahudi kutahiriwa kama
Torati ilivyodiwa.
Kadiei ya Wayahudi kuiabudu miungu ya
kipagani ilikuwa ni kuvunja amri ya Mungu ya
kutoabudu miungu wengine. (Kut 20:3; 34:14
Kumb 5:7). Na kupiga marufuku kutahiri ilikuwa
ni kupingana na agizo la Mungu kuwa kila
mwanaume atahiriwe kma ishara ya agano
alilofanya Mungu na taifa