Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Kufuatia mwanamuziki Roma Mkatoliki kutoa wimbo jana wenye maudhui ya kuikosoa serikali katika masuala ya kuongoza nchi, Waziri wa habari na utamaduni Harrison Mwakyembe amesema Roma hana elimu ya kuweza kuikosoa serikali, akitaka akajielimishe kwanza au aingie kwenye siasa ndio aanze kuikosoa serikali.

Swali kwa Waziri Mwakyembe, wanaosifu hawahitaji digrii nne? Ila wanaokosoa wanahitaji digrii nne? Hivi CCM siku hizi mmekosa kabisa watu wa kujibu hoja kwa kujenga hoja kinzani?

Hoja tu za mwanamuziki zimekushinda kuzijibu, vipi hoja za wapinzani? Au ndio maana mmezuia mikutano ya kisiasa?
 
Vipi kuhusu elimu ya Mtukufu Mbowe? Lema je? Sugu? Pro. Jay? Ahahahah! minyoo umenikumbusha msemo wa "nyani haoni ......."!
Wewe mbweha uwezo wako wa kufikiri umefika mwisho? Mbumbumbu vilaza punguani siku zote kipimo chao ni kuisengenya ID ya JF ambayo huwa haitokani na ubatizo kanisani wala msikitini, acha ufala wako Eilmu za wapinzani ni kubwa ndiyo maana nyie wajinga mnatumia mabilioni pesa za walipa kodi kuwahujumu kuwadhoofisha kuwapiga risasi, kuwabambikia kesi kuwapora ushindi kwenye chaguzi mbalimbali, kama wapinzani hawana Elimu iweje CCM itumie gharama kubwa kuibaka demokrasia si mngeacha wananchi wenyewe waamue? Wanaojiita wasomi huko CCM hawana fikra mpya zaidi ya udikiteta uchwara.
 
Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Vinakuwa wazi kama mzinga wa nyuki. Kitu pekee walichojaza kichwani ni yale waliyofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Manguli wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakakubaliana waanzishe utaratibu ambao utamuwezesha mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

Kwahiyo mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.

Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.

Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree, PhD au 'digrii 4' unazojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?

Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI". Na kama hamna kinachobakia basi hilo bichwa halina tofauti na mtungi wa gesi. #Akili #Elimu #NinaDegree4

Malisa
 
Eti ccm wanajidai wana wanaojiita wasomi lakini cha ajabu ccm ndiyo inahaha kuhujumu wapinzani, sasa usomi huko ccm hutumika kupanga njama haramu?
 
N
Unaweza kujindanganya kuwa wapinzani wana elimu kubwa, lakini kwa mitusi uliyotoa, jitathimini una elimu gani. Halafu, acha kupaniki, kila Mtanzania anajua kuwa elimu ya hao jamaa ni tia maji tia maji. Na ukweli unasemwa hadharani! Ahahahahahaha!
 
Katika hili 'mwakiboy' kachemka
Sema sasa kufuta kauli ndio inshu
 
Ndio maana 75% ya wasomi uwa wanafail maisha kwa kutaka ku apply elimu ya darasani mtaani.

Ndio maana mtu unakuta ni lecture wa commerce lakini hajawai fanya biashara ya aina yeyote.

ndio maana unaona wakina mwigulu wasomi wa uchumi lakini baada ya kuondolewa uwaziri wanalia njaa wanatamani warudi ni matokeo ya kusoma bila kuelimika kiukweli elimu dunia ndio muhimu kuliko elimu fake ya darasani.
 
Najiuliza hivi wimbo kuuza au kulipa ni kitu gani maana ninavyojua Mimi hata ujumbe tu kukukubalika ni mauzo ya wimbo.
 
Nchi hii ukisifia tu hata kama ni darasa la saba unatunukiwa ubunge kama alivyoambiwa Harmonize ana sifa kuwa mbunge ila kosoa sasa.
Meneja wa Hamonize amepewa Tenda nyingi uchaguzi wa sasa na hata uchaguzi wa 2020 kaahidiwa vingi
 
Kwa hiyo mbunge Msukuma anavyoongeaga mle bungeni huwa anaona ni upumbavu tupu? Maana Msukuma ni LY
 
Anataka sifa kama zile za diamond,
Mwaki baba lao
 
Najiuliza hivi wimbo kuuza au kulipa ni kitu gani maana ninavyojua Mimi hata ujumbe tu kukukubalika ni mauzo ya wimbo.
Ujue Mwakyembe kwa kutojua kaufanyia promo kubwa huo wimbo, wapo watanzania wengi hawakuwa wakiujua sasa wataanza kuutafuta na ndipo Roma atauza sasa, kuaupaishi wimbo kirahisi ndiyo maana tunasema wanaojiita wasomi huko CCM wengi si wasomi halisia kabsa
 
Wale wazee wa Iringa kama sijakosea, waliotumia akili na maarifa kuzalisha umeme na kuzisaidia jamii jirani mbona hawakua na vyeti hata vya darasa la 7 na wameiletea jamii manufaa kulikua hayo madigrii ya Mwakyembe, yeye jamii imefaidika nini na digrii zake, zaidi ya kulitia Taifa hasara ya kutibiwa alipobwia sumu? Akwende zake na tudigrii twake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…