Ule wimbo utaishia miaka 1000 mbele, ni wimbo matata sana, hata asingekuwa Mwakyembe angeibuka mchawi yeyote tu angeupigia promo bila kujua.Ujue Mwakyembe kwa kutojua kaufanyia promo kubwa huo wimbo, wapo watanzania wengi hawakuwa wakiujua sasa wataanza kuutafuta na ndipo Roma atauza sasa, kuaupaishi wimbo kirahisi ndiyo maana tunasema wanaojiita wasomi huko CCM wengi si wasomi halisia kabsa
Mwakyembe katiba ya Tanzania anaijua?"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"
Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
Hata Yesu alipingwa.Roma aachane na siasa aimbe mambo mengine awamu hii inafanya vema sioni kwa nini kelele za kupinga ziwe nyingi hivyo bila shaka AMENUNULIWA huyo Roma
Pale mwenye Degree nne anaposhindwa hoja na mwenye std 7, ulienda kusoma kufuta ujinga au kupalilia ujinga?? Najua Mwakyembe ana akili lakini anaziacha nyumbani kutumikia tumbo lake. ndiyo maana kakurupuka kuujibu wimbo ambao haujataja jina mtu akajikuta anaupigia promo. Alitakiwa awe na subiri na atumie akili. Kutokana na anataka kuwa wa kwanza ili Jpm amsifie amejikuta kaharibu Hizo ndio akili za Degree Nne.Kusifiwa sawa sio ila mkikosolewa ndio mnaanza ooghh Nina degree NNE! What is degree NNE? What's kufundisha vyuo? Ndio unakua malaika? Go Roma
Nchi haiko salama. Iko kwenye mikono ya hovyo.Kama kweli kayasema hayo, basi hayo ndio tunaita matumizi mabaya ya akili.
Hua najiuliza kama hii ndo aina ya viongozi tunaowaamini kufanya maamuzi ya nchi. Je, nchi yetu iko salama kweli?
Natamani huu uzi uwe ni propaganda na isiwe kayasema hayo kweli .
Mmesahau Mwakyembe aliwahi kuwatishia wanamuziki eti marufuku kumtaja rais mnapotunga nyimbo zenu, watu wakauliza hata kama ni kumsifia tusimtaje ? Mwakyembe akawa kimya.Digree nne! Anajua kutengeneza Simu? anajua IC inavyotengenezwa? Hawa ndiyo wale wanaotoswa kwenye maji na Waendesha Ngalawa wanapovuka mito.
Mimi msomi...
Ogelea basi..
Kauli hiyo kama ni mwakyembe ametoa basi amekosea sana...angenyamaza tu tunahitaji busara na hakima zake kama mzee ...Nina mashaka sana kama nmeongea hivyo au mitandao imeamua kumchafua waziri .
Sabatho njema nawe mleta mada .
Kwani ametajwa? Mbona anajishuku!"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"
Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
Siku zote nasema CDM ina watu smart! Angalia alivyoandika kwa mantiki kubwa! Nani CCM anaweza kuandika hivi! Namlilia Ben Saanane he was another Albert Einstein in the making!Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.
Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.
Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.
Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.
Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?
So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.
Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.
Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.
Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?
Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI". Na kama hamna kinachobakia basi hilo bichwa halina tofauti na mtungi wa gesi.
#SinaAkili
#NinaDegree4
Malisa GJ
Roma mimbo yake inafundishwa kwenye Vyuo vikubwa duniani.
Fasihi jinsi inavyoweza kuchochea mijadala mikubwa ya kukosoa jamii.
Dr mwakyembe amejishusha kujibu jibu Kama la mtu asiye dokta.
Viva Roma Viva zimbabwe
Mwakyembe kachemsha sana sasa Roma ndiyo msomi zaidi yake kwani kukurupuka kutoa matamko pasipo kutafakari ndiyo madhara yake hayaPale mwenye Degree nne anaposhindwa hoja na mwenye std 7, ulienda kusoma kufuta ujinga au kupalilia ujinga?? Najua mwakyemba ana akili lakini anaziacha nyumbani kutumikia tumbo lake. ndoo maana kakurupuka kuujibu wimbo ambao haujataja jina mtu akajikuta anaupigia promo. Alitakiwa awe na subiri na atumie akili. Kutokana na anataka kuwa wa kwanza ili Jpm amsifie amejikuta kaharibu Hizo ndio akili za Degree Nne.