Me Ni Mfuatiliaji mzuri wa swahili Hip Hop. Na kwa kumbukumbu zangu hawa clouds kuna kipindi wali-vow kuiangusha swahili hip hop, kipindi kile cha wagosi wa kaya, mapacha na wengine wengi. Cha kushangaza sasa hivi hip hop imerudi tena na kwa nguvu tena kutokana na uwepo wa medias nyingine nyingi, na clouds wanakumbatia wanahip hop wachache sana. Ukiimba concious Hip hop hawakutaki.
Now Back to Roma, huyu jamaa hawamzoei wanamuogopa kwa sababu watanzania wengi wamemkubali na haogopi kusema lolote. Kwa mfano kwenye moja ya nyimbo zake iitwayo "Mathematics" kule ndani kampaka Ephraim Kibonde. Mstari unasema ".... Kibonde wewe ni member wa Loan Board au TCU???" Hii ni kutokana na Kibonde kuzngumzia mkopo kuwa wanafunzi wanautapanya.