Roma Mkatoliki / Ibrahim Musa, rudi Tanzania haraka sana, ugombee Ubunge

Roma Mkatoliki / Ibrahim Musa, rudi Tanzania haraka sana, ugombee Ubunge

Zero Hours

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
12,942
Reaction score
18,669
CZ_L4845-566x600.jpg
Katika wasanii wenye Uwezo mkubwa wa kujenga hoja zenye maana katika Jamii hivi sasa hapa Tanzania, ni Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki.

Kwa Ujasiri na uwezo wako mkubwa kimaono kama kijana umeonesha unastahili kuwa bungeni na ninauhakika popote pale utakapogombea lazima uingie bungeni bila kujali utagombea kupitia chama gani cha siasa.

Kwa CV yako nilivyoiona kielimu, unawazidi wabunge wengi sana waliopo hivi sasa bungeni. Kwa kifupi unasifa zote za kuwa mjengoni na wapiga kura unao.

Binafsi Ningependekeza ungegombea kupitia Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili uwe huru utakapokuwa ukitoa Maoni/ hoja zako bungeni.

Nakuhakikishia hutajutia and you will thank me later.
 
Kama ulisikiliza Interview za Roma mwezi uliopita alipofanya na kituo cha Clouds Fm kupitia kipindi cha XXL na Wasafi Fm katika kipindi cha The Switch aliongea mengi moja wapo lilikuwa na hili alipoulizwa kwann asigombe Ubunge au kama atapewa angekataa kuwa mwana siasa alisema yeye anapenda kuwa kama RUGE na ndio alisema ndiye ROLE MODEL wake anapenda aishi kama yeye kwa kujitoa tu katika harakati za kijamii tu ndio anachokitaka ROMA.
 
...akiingia mjengoni aisee ile burudani tutakosa kabsa na anaweza akawa kwnye kundi la wanafiki...

"Najuaaa msemaa kweli hufa mapemaa mm sijali,Kama mlimuua Amina apa kwangu chuma cha reli.." moja ya verse yake.

Bungeni si sehemu salama kwa muongea ukweli.
 
Bongo ukipata fame kidogo unataka kuwa mbunge

Binafsi najiona ninazo sifa za kuwa mbunge kabisa namzidi msukuma,lusinde, na wengine wengi tu kielimu sema wao wananizidi idadi ya waganga

Kwa hio siwawezi[emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao uliowataja kwenye majimbo yao wanafanya vizuri na wanapendwa Sana labda utumie kigezo kingine especially Cha uwakilishi wa kitaifa bungeni.
 
Chadema imeshaozaga kabisa zamani niliwapenda kwa hoja zao nakujitolea ila sasa wanapresha na hawana sifa tena.
Yaani wao wadelete tu hicho chama au wakae kimya kama vyama vingine.

Eti naye tundu lissu anataka kugombea uongozi mwaka huu kwanini asisubirie tu 2025 ?
 
Back
Top Bottom