Roma Mkatoliki: Sera za Maji na Umeme tulipaswa kumaliza mwaka wa 10 baada ya Uhuru!

Roma Mkatoliki: Sera za Maji na Umeme tulipaswa kumaliza mwaka wa 10 baada ya Uhuru!

Msanii wa muziki wa hip-hop Tanzania Ibrahim Mussa maarufu Roma Mkatoliki, ametoa maoni yake kuelekea Uchaguzi Mkuu na Serikali za Mitaa, kuhusu masuala ya uongozi na maendeleo ya nchi, akisisitiza kuwa changamoto za maji na umeme zilipaswa kutatuliwa tangu miaka ya mwanzo baada ya uhuru. Kupitia mtandao wake wa Instagram Roma amewataka wananchi kuangalia mbali zaidi ya ahadi za huduma za kimsingi kama maji, umeme, barabara, shule na madawati wakati wa kuchagua viongozi ifikapo 2025.
"Maoni yangu binafsi, 2025 tusimchague kiongozi kwa kutazama tu huyu atatuletea maji, umeme, barabara, shule na madawati. NO!!" amesema Roma.

Badala yake, amesisitiza umuhimu wa kuchagua kiongozi ambaye atavumilia kukosolewa ndani ya miaka mitano ya uongozi wake, kiongozi ambaye hatatishia raia kwa kutoa maoni yao, na ambaye atakuwa tayari kufariji na kutatua matatizo badala ya kutumia nguvu kuwatuliza.

"Hivi kwangu mimi ni bora kwanza kuliko hata hayo maSGR sijui mandege," amehitimisha Roma, akiweka msisitizo juu ya haki za raia na uhuru wa kujieleza kuwa ni kipaumbele kikubwa.
Yeye aje agombee uongozi umri unakwenda huko alipojificha. Isiwe kazi nyepesi kuwashauri wapiga kura ni muda wa yeye kutoa mchango wake wa kisiasa mbali na muziki anaaumba na kupata pesa.

Akili zile zile za Diaspora wakiwa huko US wanapinga kila kitu wakija bongo na kupewa nafasi wanafanya madudu kuliko yale waliyoyakosoa.
 
Anaweza akiwa na akili na mambo yakawa safi maana hawezi kuwa na akili kama hizi za hawa wa sasa za kuagiza gari moja ya 600milion kwa ajili ya kutembelea mkuu wa wilaya mmoja wakati kuna vijiji vina watu 300 havina maji ambapo mradi wa tsh 20milion tuu ungetosha kuwapa maji hao watu 3000
 
Kama hana akili hizo ndio sababu ya muhimu ya yeye kuja kuleta mabadiliko ya fikra.

Kuongea mitandaoni mbali, kutenda kile unachokiongea unapopewa nafasi ni mbali.
 
Back
Top Bottom