Roma Mkatoliki usiposema ukweli kesho, wakatoliki halisi tutausema Jumanne

Roma Mkatoliki usiposema ukweli kesho, wakatoliki halisi tutausema Jumanne

Status
Not open for further replies.
Kesho tunataka kusikia yafuatayo..wale watu wawili waliokuja kukuhoji kwanini walikuwa hawakujui je walielekezwa na nani kwako?..mlipoingia ndani ya ile Noah kwanini nyote mlifungwa vitambaa vichwani na mkaja kufunguliwa mlipoingizwa katika nyumba ya kwanza Mikocheni na siku mbili baadae mkahamishiwa katika nyumba iliyopo Oysterbay..

Kwanini kati yenu wote ni wewe tu ndiyo uliyepigwa sana na virungu magotini huku ukikanyagwa kila mara mbavuni mwako na kuna wakati ukawekewa bastola kichwani ndipo ukaanza kunywea...?

Ni kiongozi gani ambaye juzi usiku alikuja katika hiyo nyumba na kuzungumza nanyi kisha akawatishieni nyote?

Yule dada aliyekuwa akiongoza mateso yenu huku akiwa anawahoji na kuwarekodi anatoka katika taasisi gani?

Kiongozi gani aliomba kuongea na wewe jana asubuhi kabla hamjaondoshwa hapo Oysterbay na kupelekwa Polisi?

Ole wako usiseme huu ukweli kesho.
Smahani lakini labda kwa sababu simjui vizuri huyu jamaa lakini naona anaongea kama kadata data vile au?

Kwa mnao mjua hivi huyu jamaa yuko sawa kweli?
 
Watakuwa wamepuliziwa sumu na kuambiwa waseme hivi ili wapewe dawa ya kuwaponya laa sivo watakufa tu
Hilo nalo neno... Maskini Roma Mungu akutetee tuuu haya maswaibu si madogo [emoji17] [emoji17] [emoji17]
 
Malaana mengine ndo yanasababisha mtu unakuta unapata matatizo dunian bila kujua. Kama mtu kaish hv haf hajapata mtoto atamlaum nan na ni muuaj mkubwa. Nimewaza lkn
 
Mbona unapanic

Hajamchafua kiongozi yeyeto Bali viongozi ndio wanajichafua wenyewe

Unfortunately tumemuelewa vizuri sana tena kupita kiasi

Hata macho ya Nancy mke Wa Roma yalikuwa yanajieleza vizuri sana alivyokuwa akipata hasira kwa Roma kuongea uongo

Wewe ndio una wafuasi wawili tu

Next time waambie ma boss zako wachukue short course za utekaji ili uwe successful


Amini unavyotoka, niache na yangu.
 
naomba unisaidie hivi kumbe katika maelezo yangu yote ya kimaandishi humu nimemtaja huyo mkuu wako wa mkoa? halafu kama hutojali hebu tusaidie ni mkuu wa mkoa gani huyo unayemsemea wewe?
mkuu usikijibu hichi kipunguani kisicho na chembe ya akili kimekalia kila kitu oyeee oyee bila hoja ya msingi kama kizezeta, sijui kina umri gani hichi kitoto nahisi kibeki tatu cha bashite 0kama sikosei
 
Kwanza nianze tu kwa kuwapa pole kwa waliyowakuta ila nadhani Roma Mkatoliki akishapona hayo majeraha yake basi aachane tu rasmi na kazi yake ya muziki na aje huku hergeisa nchini somalia nilipo ili tuweze kuvua sote samaki kwani kitendo chake cha leo ni kama vile amejidhalilisha na amewatukana watanzania kwa kuuficha ukweli.

Kwanza niseme tu simlaumu kwa kusema kuwa hawakujua walipelekwa katika nyumba gani ila hayo maeneo niliyoyataja hapo juu ndipo ambapo walipelekwa ila kwakuwa muda wote hata wakati wanateswa walikuwa wamefunikwa ili wasiwajue watesaji wasingeweza kujua ni wapi walikuwepo.

Roma Mkatoliki kwani ungesema tu haya kwa waandishi wa habari hata kama ungekufa leo udhani kama ungebaki kuwa shujaa kwetu kama walivyo mashujaa wengine?

Roma umepigwa na kuteswa sana ila unajikaza tu ili kuwaficha watanzania. Roma umehojiwa mno kuhusu itikadi yako ya kisiasa na kipigo chako kikubwa kilitokana na hili. Je, umeogopa nini kuwaambia watanzania hapo mkutanoni?

Roma uliwekewa kitu sehemu ya haja kubwa na kuwa waya wa umeme ulitaka kuwekewa katika uume wako. Roma ulitishiwa sana kuuliwa mkeo na mwanao kama usingewaambia ukweli.

Roma uliposema kuwa unahisi hauko salama nakubaliana nawe kwani ile kemikali mliyopuliziwa imewamaliza na ndiyo maana wote mapafu yenu sasa yanawasumbueni na watanzania tufunge tu tuwaombee hawa wenzetu.

Roma ni kwanini ulipomwona Mwakyembe anasikiliza ile sauti ya yule kiongozi katika simu ya mwandishi ukainama ghafla na ukawa unafuta machozi huku ukiwa na maumivu na amani yako pale ilitoweka ghafla?

Roma kwanini umedanganya kuwa mlitupwa tu pale Ununio kisha wewe ndiyo ukapata nguvu na kuanza kuwafungua wenzako vile vitambaa wakati ukweli ni kwamba mlipotupwa ni wewe ndiyo uliyefunguliwa haraka kamba na aliyekufungua akakuambia kuwa usigeuke huku akikunyooshea silaha kisha akapanda gari upesi na wakaondoka kwa spidi ya hali ya juu?

Roma kwanini hujasema kuwa katika mahojiano yako hasa wewe kila mara ulikuwa ukiulizwa kuhusu mwanaharakati mwenzio msanii Ney wa Mitego?

Roma kwanini hujawaambia watanzania kuwa kuna maagizo ulipewa uwape wasanii wenzio akina Niki wa Pili na kaka yake Joh Makini kuwa watulie na wafanye kazi zingine?

Roma kwanini hukusema kwamba moja ya sababu inayomfanya mmoja wenu mpaka leo kuogopa na kukosa usingizi na kuwasumbueni usiku kucha kunatokana na zile sinema za vitisho na za mauaji ya kikatili mlizokuwa mkionyeshwa ili kuwamalizeni kisaikolojia?

Ni hayo tu ndiyo nilitaka nimkumbushe Roma Mkatoliki kuwa hakuyasema au kuyaweka wazi kwa waandishi wa habari pale mkutanoni kwa kuogopa kumaliziwa kabisa japo kwa taratibu za watekaji wote duniani huwa wakimteka mtu halafu wakaja kumuachia yule mtu huwa haishi muda mrefu kwani huwa wameshammaliza kwa vitu vyao wanavyovijua wao.

Sababu kubwa ya Mwakyembe kuwa hapo ni kumjengea uwoga Roma Mkatoliki kitu ambacho kweli kilifanikiwa kwani Roma alikuwa hajui kama angemkuta hapo hivyo alishtuka na hata saikolojia ya Mwakyembe ilikuwa ni ya kutishia zaidi na siyo ya kutafuta suluhu na ndiyo maana muda wote alikuwa na wasiwasi, mkali na anachukia maswali ya maana.

Sababu kubwa ya yule dada pale ukumbini kuwa vile ni kwamba alishapewa maelekezo kabla ya kuyafanya hayo aliyokuwa akiyafanya ili tu kuweza kutibua mtiririko mzima wa ule mkutano na katika hili aliweza kufanikiwa kwani hata waliompa maelekezo mmoja wao alikuwepo ndani mule akihakikisha kama anafanya alichoelekezwa huku wenzako wakiwa katika gari.

na huu ndiyo mwisho wangu wa niliyowaahidi kuwaambieni kama roma mkatoliki asingesema ukweli wote juu ya kile kilichomtokea na baada ya hili sihitaji tena swali lolote sana sana tu niwatake watanzania kuwa tayari kwa taarifa za kupikwa na kuficha ukweli kutoka kule ambako akina roma mkatoliki walienda kuripoti, na nimwambie tu roma kuwa kwa aina ile ya mateso yanayokaribia na kifo aliyoyapata hasa yeye leo asingekuwa na cha kupoteza hata kama angesema ukweli wote na kuja kuuwawa kwani ukweli wake wa leo ungeweza kuisaidia tanzania na watanzania wote na hata kama angekufa basi angegeuka kuwa shujaa wetu kama hayati edward moringe sokoine.
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji119]
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom